Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 403 | 404 | (Page 405) | 406 | 407 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Kampuni kadhaa kutoka nchi ya Uturuki zimeanza kuingia Tanzania ili kushiriki katika kazi za ujenzi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. Kukua kwa sekta ya ujenzi kumekua ndiyo kivutio kikuu kilichozifanya kampuni hizo kuonyesha nia ya kufungua ofisi zao hapa nchini.

  Wakizungumzi katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walipomtembelea ofisini kwake, wawakilishi kutoka Kampuni Kampuni tatu tofauti wamempongeza Waziri huyo kwa jinsi anavyosimamia sekta hiyo ya ujenzi kiasi cha kuanza kuvutia makampuni makubwa kutoka nje.

  “Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa kadhaa barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo” alibainisha Bw. Orhan Babaoglu ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki.

  Mwakilishi mwingine kutoka Kampuni ya CEYTUN ya huko huko Uturuki Bw. Kursat Durak amebainisha kuwa, utendaji wa kampuni za Kituruki unafahamika duniani kote, hivyo ujio wao unalengo la kuamsha ushidani wa ubora lakini pia kuona kuwa gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinathibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti.

  Mhe. Magufuli kwa upande wake wakati akiwakaribisha amewataka kuzingatia sheria na taratibu zinaoongoza shughuli za kandarasi hapa nchini. Waziri Magufuli aliwajulisha kuwa, mbali na kazi za kawaida za kandarasi kwa hivi sasa kuna miradi kadhaa mikubwa inayokusudiwa kuendeshwa kwa kushirikisha sekta binafsi hivyo hiyo pia ni fursa wanayoweza kujishughulisha nayo hapa nchni.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu (kushoto) akiwasilisha kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, utambulisho wa makampuni ya Uturuki ambayo yamefungua ofisi hapa nchini kwa lengo la kushiriki katika kazi za kandarasi za ujenzi hapa nchini.
  Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipitia baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa na makampuni ya kandarasi kutoka Uturuki. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Alhaj Mussa Iyombe na kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu.
  Bw. Kursat Durak (aliyenyoosha mkoni) kutoka Kampuni ya CEYTUN ya Uturuki akifafanua jambo. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu, Bw. Hassan Tunk Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya CEYTUN na kushoto kabisa ni Bw Remzi Demircan Mbia wa Kampuni ya KAYA.

  0 0

  Mwananchi wa Kata Pera waahidi kumpigia kura Ridhiwani Kikwete tarehe 6 mwezi wa nne baada ya kuridhishwa na Hotuba zake zinazogusa changamoto zao kama elimu, maji, zahanati, barabara na namna atakavyoboresha miundo mbinu ya jimbo la Chalinze na kuwasaidia wafugaji katika suala zima la kuongeza majosho ya mifugo.

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete  akihutubia wakazi wa kijiji cha Pera wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani aliwaambia wananchi hao kura yao ya tarehe 6 mwezi wa Nne itakuwa ndio jibu la changamoto zote kwa wananchi wa jimbo la Chalinze kwani anatambua Changamoto zote za jimbo hilo.
   Imani Madega akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Pera na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuhakikisha Ridhiwani Kikwete anashinda kwa kura nyingi ilikufanikisha azma ya kusaidia jimbo la Chalinze kukua kimaendeleo inakua.
   Msanii Sam wa Ukweli akiruka juu na Morani wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM uliofanyika Mbala Kijiweni, kitongoji cha Mbala kwenye kijiji cha Chamakweza kata ya Pera .

   Meneja wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Steven Kazidi akizungumza na viongozi wa wafugaji wa kijiji cha  Chamakweza kata ya Pera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbala Kijiweni.
   Mgombea Ubunge wa CCM Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafugaji wa kijiji cha Chamakweza ,Ridhiwani alihutubia wafugaji hao ambao walimueleza kuwa wanatatizo kubwa la majosho ya mifugo yao na wanaamini yeye akiwa Mbunge atawasaidia katika kuboresha miundo mbinu itakayowasaidia kufuga kwa kisasa zaidi.
  Wananchi wa Bwawani Pingo wakielekea kwenye uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la CCM lililokuwa likizinduliwa na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

  0 0
 • 03/28/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Orchestre Fauvettte wanakupa "Francisca"

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akifunga mafunzo ya siku tatu kwa washiriki juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
  Mwakilishi wa TradeMark Afrika Mashariki kupitia Tanzania Asaac Mtwale akiwashukuru washiriki wa mafunzo juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru bara maada ya kufungwa kwa mafunzo hayo katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum (hayupo pichan) alipokua akifunga mafunzo hayo.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum (wakatikati waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru yaliyofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar. (PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR).

  0 0


  0 0

  On 31th March, 2014, the Government of Japan and the Government of the United Republic of Tanzania will sign Exchange of Notes for the Japanese Grant Project “The food security project for underprivileged farmers”.

  The grant which will be provided from the Government of Japan, amounts to three hundred and eighty million Japanese Yen (\380,000,000), approximately six billion ninety million Tanzanian Shillings (Tsh 6,061,000,000).

  This project aims to improve food production, especially for underprivileged farmers, and its ultimate goal is to enhance food security in Tanzania. The grant is provided to the Government of Tanzania for procurement of fertilizer. After the procurement, the fertilizer will be supplied to farmers through private companies.

  The income derived from the sale of the fertilizer can make it possible for the Government of Tanzania to support agricultural development and poverty alleviation by providing infrastructure or access to financial opportunities for underprivileged farmers.

  H. E. Mr. Masaki Okada, Ambassador of Japan, and Dr. Servacius B. Likwelile, Permanent Secretary of the Ministry of Finance of the United Republic of Tanzania, will sign the Exchange of Notes, and Mr. Yasunori Onishi, Chief Representative of JICA Tanzania Office, and Dr. Servacius B. Likwelile, Permanent Secretary of the Ministry of Finance, will sign the Grant Agreement.

  0 0
 • 03/28/14--22:24: KATIBA MPYA NA WANAWAKE!
 • "Ikipatikana Katiba yenye usawa wa kijinsia, tatizo la wanawake wanaojiuza litakwisha!" Hayo ni maneno ya mwanamke mpiganaji Bi Sophia Jonas alipozungumza na Super Woman Joyce Kiria kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV kila Jumanne saa tatu kamili usiku. 

   Fuatilia kwa makini mjadala huu kwa kutazama video hii hapa

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
  Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.

  0 0
 • 03/28/14--22:32: GADO LEO


 • 0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi walionyakua tuzo mbalimbali wakati wa hafla ya kutunuku Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora wa mwaka 2013 iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana ijumaa.(picha na Freddy Maro)


  0 0
 • 03/29/14--09:30: IN LOVING MEMORY'


 • Dada Grace Simtaji Ngowi.

  Our  beautiful Sister, our beautiful Mother, it is hard to believe that  today 29.03.2014 it is exactly two years since you passed away and left us with sorrows, tears and confusion. We praise God’s name for the time we spent together the joy, laughter and words of encouragement from our sister and mother.  

  Our sister our mother will always be in our hearts, and will be remembered by son Emmanuel and his family, your husband Joseph, your sister Anna, your brothers Bahati, Kotto & Baraka, other members of the family and friends.

    ‘’...the Lord gave and the Lord has taken away may the name of the Lord be praised’’
  Job 1:21

  0 0

  Watanzania Wisconsin wamezuia kuchomwa moto kwa mpendwa wetu Michael Lukindo aliyefariki Jumapili ya March 16, 2014 wameomba msaada kwa Watanzania wengine waishio Marekani na kokote pale Duniani kujitahidi kadri tuwezavyo tuweze kumstiri Mtanzania mwenzetu ghrama za mazishi ni $6,000 
  jina la AC ni Memorial for late Mike Lukindo 
  Benki ni Madison Chase Bank AC ni 579362299 
  Route ni 075000019 
  Tafadhali ndugu zangu, Watanzania wenzangu msiba huu ni wetu sote chochote utakachokua nacho kitasaidia kumzika ndungu yetu asante


  0 0

  Stori: Ojuku AbrahamWAZIRI Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda leo atakutana na ‘surprise’ ya aina yake, wakati atakapokabidhi tuzo kwa mwanamke bora wa mwaka, ambaye hadi sasa bado hajafahamika ni nani kati ya wanawake wanne mahiri nchini, itakayofanyika katika Ukumbi wa The African Dream, Dodoma.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.
  Wanawake hao ambao mmoja wao ataibuka kinara na kuondoka na Tuzo na zawadi maalum ni pamoja na Dk. Maria Kam, Dk. Asha Rose Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na Mheshimiwa Anna Kilango Malecela ambao wamefikia hatua hiyo ya mwisho baada ya kuwashinda wenzao 150 walioanza kupigiwa nao kura.
  Dk. Asha Rose Migiro.
  Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Global Publishers iliyoratibu zoezi hilo, Abdallah Mrisho, waliamua kutoa tuzo hizo hasa baada ya kupata msukumo uliotokana na kuthamini michango ya wanawake nchini.

  Alisema wadau hao walituma majina zaidi ya 30,000, lakini kamati iliyachuja kulingana na sifa za kila mmoja na kupata wanawake 150 ambao walianza kupigiwa kura kwa awamu. Awamu ya kwanza iliyochukua miezi miwili, iliwapata wanawake 20, iliyofuata iliwapata watano na ya mwisho iliwapata washindi hao wanne.
  Prof. Anna Tibaijuka.
  Mrisho alisema hafla hiyo itawahusisha waalikwa pekee ambao aliwataja kuwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge wa bunge maalum la Katiba, wanaharakati na wawakilishi wa taasisi mbalimbali walioko mjini Dodoma kwa sasa.
  Dk. Maria Kamm.
  “Ikumbukwe kwamba washiriki hawa wote ni washindi, kila mmoja atapata tuzo, isipokuwa ile ya mshindi kidogo itakuwa tofauti na nyingine na zaidi, yeye atapata na zawadi nyingine,” alisema
  Mh. Anne Kilango Malechela.
  Mrisho alisema baada ya kutolewa kwa tuzo hizo mwaka huu, mara moja wataanza mchakato wa kumpata mwanamke mwingine kwa mwaka ujao.Aidha, katika upande wa burudani, Mrisho alisema atakuwepo msanii anayepiga nyimbo za Kiafrika, Zaid na wasanii wengine wa Bongo Fleva.

  0 0

  Kufuatia mpango kabambe wa kuelimisha jamii dhidi ya makosa mtandao tayari kumekua na video za katuni, Mchezo wa komputa “Computer gane”, majarida ya katuni pamoja na machapisho mengine yote yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya jinsi ya kujilinda dhidi ya makosa mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi kufikia ngazi ya kitaifa.
  Picha: Mfano wa Vijarida vinavyo toa elimu dhidi ya usalama mtandao.
  Aidha, Bwana. Yusuph Kileo ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuangalia kwa karibu namna itakavyo unganisha nguvu kuhakiki jamii ya watanzania inatambua kwa kina maswala ya husuyo uhalifu mtandao pamoja ulinzi mtandao. Kileo aeleza ni vyema maswala yaha ya uhalifu mtandao yanayoshika kasi sana kwa sasa yanatazamwa kwa karibu ili kuhakiki jamii ya watanzania inabaki salama kimtandao.
  Link: Mfano wa Video za Katuni zinazotoa elimu ya usalama mtandao.
  Athari za makosa ya kimtandao ni kubwa sana endapo hatua za msingi za kudhibiti uhalifu mtandao hazitochukuliwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla. Mataifa makubwa tayari wamesha yaona haya na sasa kumekua na jitihada mbali mbali zenye malengo ya kukabiliana na uhalifu mtandao.

  Kwa upande mwingine bwana Yusuph kileo ameasa vijana kuwa na juhudi ya kusomea maswala ya ulinzi mtandao kutokana na uhaba mkubwa ulioko wa wataalamu wa maswala ya ulinzi mtandao katika ngazi za dunia huku akitolea mfano mataifa makubwa kuanza kutengeneza majeshi mahususi yatakayokuwa yakikabiliana na vita mtandao “Cyber war”

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kombe la ushindi mwakilishi wa kampuni ya Jambo plastics Bi.Rupa Suchak baada ya kampuni yake kuibuka mshindi katika shindano la kuwania tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora wa mwaka 2013 katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. 

  Kongamano hili la Vijana kuhusu Muungano linafanyika Jumapili Machi 30, 2014  kuanzia Saa  5:00 Asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC Taifa.

  Kongamano hili ni sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.

  Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.

  Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi  ujao unafikisha miaka 50.

  Washiriki wa Kongamano hili  ni vijana  300 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.

  Washiriki wa Kongamano hili watapata fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha mada kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu Mapendekezo ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.

  Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini wanakaribishwa kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu kongamano hili.

  Imetolewa na Idara ya Habari -  MAELEZO
  29 Machi 2014

  0 0
 • 03/29/14--10:10: Article 7


 • 0 0

  mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya 
  Viongozi  wa Halmashauri ya Nyasa  mkoani  Ruvuma  wakiwa katika  mafunzo 
  Viongozi  wa  Halmashauri ya  Nyasa mkoani Ruvuma  wakiwa  katika  picha ya  pamoja na  watumishi wa mfuko  wa Taifa wa  bima ya Afya  (CHIF) ambao  walitembelea  Halmashauri  hiyo  kutoa mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya


   mkuu wa mkoa wa Ruvuma  Said Mwambungu

  Na  Francis Godwin Blog Nyasa ..
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit  Mwambungu  amewataka  viongozi  wa Halmashauri  ya Nyasa  mkoani humo  kuendelea  kutoa  elimu  kwa  wananchi  ili  kujiunga na mfuko   wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya  


  Mkuu  huyo  wa  mkoa  alitoa  rai  hiyo  wakati  wa  warsha  ya  Viongozi  wa  Halmashauri ya  Nyasa mkoani Ruvuma    pamoja na  watumishi wa mfuko  wa Taifa wa  bima ya Afya  (CHIF) ambao  walitembelea  Halmashauri  hiyo  kutoa mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya .

  Alisema  kuwa CHF ni Mfuko wa Afya ya Jamii, ulioanzishwa kisheria kupitia Sheria Na 1 ya mwaka 2001 (SURA 409 ya Sheria za Tanzania) ili kutoa huduma za matibabu kwa jamii iliyopo katika sekta isiyo rasmi mijini na hasa vijijini katika ngazi ya halmashauri, tarafa kata na kijiji hivyo iwapo  viongozi  hao  watahamasisha  jamii kujiunga ni wazi  jamii  hiyo  itanufaika na huduma  hiyo.

  Hata  hivyo  alisema  kuwa kujiunga na huduma  hiyo ni utaratibu wa hiari unaoiwezesha kaya kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia mara tu kiasi cha shilingi 5,000/= au 10,000/= kwa kadiri jamii yenyewe katika Halmashauri husika itakavyoamua hivyo ni jambo zuri  ambalo wananchi  watanufaika nalo   iwapo  watajiunga .

  Mwambungu  alisema  kuwa Serikali kwa upande wake inachangia kwa kiwango ambacho kaya inachangia hivyo kuufanya Mfuko huu kujulikana pia kwa jina la Tele kwa Tele.  

  "Mfuko huu ulianza kwa majaribio wilayani Igunga mwaka 1996 na baadaye kuenea katika Halmashauri mbalimbali nchini ijapokuwa kasi yake imekuwa sio ya kuridhisha. ....Mwaka 2007 Serikali iliamua kuwa Shughuli za Mfuko huu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ziwianishwe.....hatua hii ilisababisha Serikali kuu mwezi Juni 2009 kukasimu mamlaka yake kitaifa ya kusimamia na kuendesha CHF  kuwa chini ya NHIF wakati Halmashauri zikiendelea na majukumu yake ya awali"


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa, baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa, baada ya mazishi leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani yake yaliyofanyika Morogoro.
   Makamu wa Rais akiweka udongo kwenye kaburi.
  (Picha na OMR)
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpa pole mjane wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa Mama Katherine Msamati baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpa pole Baba mzazi wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa Mzee Gabriel Tupa, baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa,  kwenye mazishi yaliyofanyika  nyumbani kwa marehemu, Kilosa Machi 29, 2014.
   Waziri Mkuu Mizengo  Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu, Kilosa, Machi 29, 2014.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimfariji  Mzee Gabriel Tupa baba mzazi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa  katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu  Kilosa achi 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 403 | 404 | (Page 405) | 406 | 407 | .... | 3278 | newer