Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 402 | 403 | (Page 404) | 405 | 406 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 03/27/14--15:05: SINDA ISLAND TOUR


 • 0 0

  Gari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Meck Sadicky likinasuliwa kwenye tope baada ya kukwama katika kijiji cha Mataya-Ruvu Chini,yote hiyo ikiwa ni sehemu ya changamoto ya Miundo mbinu hasa barabara,Wakati wakiongoza msafara wa Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anakwenda kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni;wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
  Utaratibu wa kulinasua ukiendelea.
  OOppss..haya twendeeeee....!
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh.Mecky Sadicky akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukumbana na changamoto ya miundombinu,wakati wakielekea  kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea hali halisi na kazi kubwa inayofanyika ya upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
   Wakitafakari namna ya kupita mara baada ya kukutana na changamoto ya miundombinu,hasa barabara kama uonavyo pichani Lori likiwa limeziba njia kutokana na hali ya mvua kunyesha eneo hilo.  
  PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

  0 0

  Mhe. Mwigulu Nchemba alivyochangia katika mjadala wa kupigwa  kura za siri ama kura za wazi katika Bunge Maalum la katiba mjini Dodoma leo, na kuleta mtafaruku mkubwa miongoni mwa wajumbe. Hatimaye iibidi aombe radhi na kufuta usemi wake baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe Samia Suluhu Hassan.

  0 0
 • 03/27/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya "Bolingo ya Telephone" ikipigwa na  Viva Mosukusuku

  0 0

   
  KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount Tanzania,Bwana William Christian kuhusianana namna maji yanavyokusanywa na kusambazwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar,kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar,Mh.Mecky Sadicky akisikiliza.
   KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaongoza viongozi wa CCM Wilaya ya Kinondoni kutembelea mitambo mipya baada ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, kufanyika. Ujenzi wa mitambo hiyo umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Kinana amemaliza ziara yake jijini Dar,wilayani Kinondoni pia kwa kutembelea kituo cha mabasi ya mjini kilichopo sinza na kufungua tawi jipya la vijana wakereketwa Kawe.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiendelea kupata Maelezo kutoka kwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount Tanzania,Bwana William Christian,juu ya mitambo hiyo mipya ya kuchujia maji.Ndugu Kinana alieleza kuwa ameridhishwa na namna ya kazi ya upanuzi wa mitambo mipya ya maji Ruvu chini inavyoendelea,ameeleza kuwa kazi hiyo ya upanuzi ikikamilika basi jiji la Dar na maeneo mengine mbalimbali tatizo la maji litapungua kwa asilimia kubwa. 
  Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiangalia sehemu ya kuchanganyia dawa za maji kabla ya kusambazwa kwa matumizi mbalimbali.
   upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, ukiendelea.

    KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na  viongozi wa CCM Wilaya ya Kinondoni wakipata maelezo mafupi kuhusiana na usambazaji wa maji maeneo mbalimbali sambamba na namna ya upanuzi wa mitambo mipya ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, a Ujenzi wa mitambo hiyo umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.


  0 0

  Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Bw. Andrii Deshchytsia akiwasilisha mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Azimio ambalo pamoja na mambo mengine limeitaka Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika ya Kimataifa, kutoitambua kura ya maoni iliyopigwa March 16 ya kujitenga kwa Crimea kutoka Ukraine na hatimaye kujiunga na Urusi, Ukraine inasema kura hiyo ya maoni si halali na ni njama za kumega mipaka halali ya nchi yake. Azimio hilo lilipitishwa siku ya Alhamis kwa kura 100 za ndiyo, 11 za hapana na 58 hazikuegemea upande wowote.
  Muwakilishi wa Kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Balozi Vitaly I. Churkin akitoa maelezo kuhusiana na Azimio hilo lilowasilishwa na Ukraine na kuungwa mkono na nchi nyingi za Magharibi na zile za Ulaya, kwamba, kujitenga kwa Crimea kulikuwa halali na Urusi haikuwa na namna nyingine bali kuitambua kura hiyo na kusisitiza kwamba kihistoria Crimea ni sehemu ya Urusi.

  Na Mwandishi Maalum

  Wakati hali ya sintofahamu ikiendelea kuwa tete kufuatia Crimea kuamua kupiga kura ya maoni na hivyo kujitenga kutoka Ukraine na kasha kujiunga na Urusi.Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jana alhamisi, limepiga kura kupitisha na kuunga mkono azimio ambalo pamoja na mambo mengine, linaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuto tambua kwa namna yoyote iile kura hiyo na kujitenga kwa Crimea kutoka Ukraine.

  Kabla ya tukio la upigaji kura kufanyika, baadhi ya wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao, walitoa maelezo ya kwa nini nchi zao zilikuwa zimeamua kupiga kura ya ama kuunga mkono azimio , kutoliunga mkono au kutoegemea upande wowote. Baada ya maelezo hayo, matokeo ya kura yalikuwa ifuatavyo, Nchi 100 zilipiga kura ya ndiyo, nchi 11 zikipiga kura ya kulikataa azimio wakati nchi 58 zenyewe ziliamua kupiga kura ya kutoegemea upande wowote.

  Azimio hilo liliwasilishwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na Bw. Andrii Deschcytsia, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine ambaye katika uwasilishaji wake alijenga hoja zilizowataka wajumbe kuliunga mkono azimio hilo.

  Naye Muwakilishi wa Kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Balozi Vitaly I.

  Churkin yeye pamoja na kutetea uamuzi wa serikali yake wa siyo tu kutambua kura hiyo ya maoni lakini pia kujitenga kwa Crimea, alitoa hoja ya kutaka upigaji wa kura hiyo uwe ni wa kura zilizohesabiwa ( recorded vote).

  Balozi Churkin alisititiza kwamba, kura ya maoni iliyopigwa na wananchi wa Crimea na hatimaye kuamua kujitenga na kisha kujiunga na Urusi ilikuwa ni ni kura halali na kwamba Urusi haikuwa na namna nyingine zaidi ya kuitambua kura hiyo.

  Aidha kupitia azimio hilo ambalo limepitishwa baada ya Baraza Kuu la Usalama kushindwa kupitisha azimio kama hilo mnamo March 15 siku moja kabla ya kura ya maoni kufanyika baada ya Urusi kulipinga, linayataka pia Mashirika ya Kimataifa kuto tambua kujitenga kwa Crimea na jiji la Sevastopol kwa mujibu wa kura ya maoni ya March 16.

  Ingawa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limepitisha azimio hilo, azimio linakosa nguvu kama ambavyo lingepitishwa na Baraza Kuu la Usalama.

  Wengi wa wazungumzaji waliounga mkono azimio hilo, au hata wale ambao hawakuegemea upande wowote,wamesisitiza haja na umuhimu wa kuheshimu Katiba ya Umoja wa Mataifa pamoja na Misingi ya sheria za kimataifa, ambazo pamoja na mambo mengine zinasisitiza kuheshimiwa kwa mipaka ya nchi na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyigine, pamoja na kuimarisha umoja na mshikamano.

  Baadhi ya wazungumzaji, wameleezea wasiwasi wao kuhusu kupitishwa wa azimio hilo ambalo limeungwa mkono karibu na nchi zote za Magharibi na zile za Ulaya kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa na kuchochea zaidi mgogoro huo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money kulia pichani ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imeanzisha mapinduzi ya malipo ya kielectoniki kwa kuwawezesha watumiaji wa huduma ya Airtel Money kulipia mikopo ya elimu ya juu  kupitia huduma ya Airtel money

  Ushirikiano huo kati ya Airtel na HESLB unawawezesha wahitimu wa masomo ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kuweza kulipia mikopo yao kwa urahisi kupitia huduma ya Airtel Money na hivyo kuongeza ufanisi katika  ukusanyaji wa mikopo hiyo

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” tumewawezesha kupitia huduma yetu ya Airtel money wateja wetu kuweza kulipia mikopo yao ya elimu ya juu inayotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu kirahisi wakiwa majumbani mwao. Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora, salama, ya uhakika yenye viwango vya gharama nafuu  na inayopatikana mahali pote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 35,000 walionea nchini.

   Huduma hii ni ya haraka na nirahisi kutumia, sasa wateja hawana haja ya kusubiri kwenye mistari muda mrefu kufanya malipo, wanachotakiwa ni kufanya muamala rahisi kwa kupitia simu zao  kulipa na kupata uthibithisho wa malipo ndani ya sekunde chache

  Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60#  na kuunganishwa na orodha ya Airtel Money kasha kuchagua namba 5 kufanya malipo, alafu chagua namba 8  kupata huduma zinginezo kisha kuandika neno HESLB , ingiza kiasi cha pesa, kumbukumbu namba na namba ya siri kufanya malipo  aliongeza mmbando

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja alisema”hii imekuja wakati muafaka ambapo baadhi ya waliofaidika na mikopo hii muda wao wa kurejesha malipo ya mikopo yao umekwisha,  kwa kupitia huduma hii ya kulipia kwa Airtel Money hakutakuwa na haja ya watu kutembea umbali mrefu na kupanga foleni katika mabenki ili kulipia, tunaleta kwa wateja wetu urahisi wa malipo na njia mbadala ya kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo hiyo.

  Chagonja aliongeza kwa kusema kwa kupitia huduma hii ya Airtel Money sasa wateja wetu wataweza kulipa mikopo yao kirahisi wakati wowote mahali popote masaa  24 siku 7 kwa wiki.

  0 0


  0 0

  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Freddy Liundi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bandari ya Mwambani kwa kiongozi wa timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy.
  Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo, kutoka Tume ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Maduka Kessy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya mwambani ambapo upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga akionesha eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
  Picha ikionesha eneo la mwambani ambako ndipo miundombinu ya bandari itajengwa.
  Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi (wa pili kulia) ufukweni mwa bahari, eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa. Picha na Joyce Mkinga

  0 0


  0 0

  Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu wa Bunge),Mh. William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.


  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Ripoti ya Mwaka kutoka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza muhtasari toka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh kabla ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam leo. 
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh baada ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Picha kwa hisani ya mdau Bilal Ahmed

  0 0

  Mahakama ya Rufani imewaachia huru wafungwa wawili raia China (pichani)  waliokuwa wakitumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la uvuvi haramu katika katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania (Exclusive Economic Zone- EEZ)
  Wafungwa hao , Hsu Chin Tai ambaye alikuwa nahodha wa meli ya Tawaliq 1 waliyokamatwa nayo wakifanya uvuvi huo haramu na aliyekuwa wakala wa meli hiyo, pamoja na baharia Zhao Hanquing. 
   Walitiwa hatiani na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Februari 23, 2012, na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela, au kulipa faini ya Sh20 bilioni, kila mmoja, faini ambayo walishindwa kuilipa na hivyo kutumikia kifungo, huku meli yao ikitaifishwa. 
  Hata hivyo Mahakama ya Rufani leo imewaachia huru baada ya kushinda rufaa yao waliyoikata mahakamani hapo, kupitia kwa mawakili wao Kapteni Ibrahimu Bendera na John Mapinduzi.  Mahakama ya Rufani, katika hukumu yake, ilisema kuwa kulikuwa na dosari za kisheria katika taratibu za kuwafungulia mashtaka Mahakama Kuu na kwamba walifunguliwa mashtaka hayo bila kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). 
   Kutokana na kasoro hizo za kisheria mahakama hiyo iliamua waachiwe huru mara moja isipokuwa kama wataendelea kushikiliwa kwa kosa lingine. 
  Hukumu hiyo iliandaliwa na Jopo la majaji watatu waliosikiliza rufaa yao - Salum Massati, Semistocles Kaijage na Bethuel Mmila. 
   Hata hivyo licha ya mahakama hiyo kuwaachia huru jana, lakini Wachina hao walirudishwa tena gerezani kwa ajili ya kukamilisha taratibu za Magereza, ambako wamekuwa wakiishi kwa muda wote huo tangu walipotiwa hatiani. 
   Katika rufaa yao, Wachina hao kupitia kwa mawakili wao hao walikuwa wakipinga hukumu na adhabu hiyo ya Mahakama Kuu, iliyotolewa na Jaji Agustine Mwarija.
  Katika kesi ya msingi walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili. La kwanza lilikuwa kufanya shughuli za uvuvi katika ukanda huo wa Tanzania bila kuwa na kibali na la pili  ni kuchafua mazingira ya bahari kwa kumwaga baharini mafuta machafu na uchafu wa samaki. 
  Katika kosa la kwanza washtakiwa wote walihukumiwa adhabu ya kulipa faini ya Sh1bilioni kila mmoja au kifungo cha miaka 20 kila mmoja, na katika kosa la pili mshtakiwa wa kwanza aliadhibiwa adhabu ya kulipa faini ya Sh20bilioni au kifungo cha miaka 10 jela. 
  Washtakiwa hao na wenzao 35, walikamatwa Machi 8, 2009 wakiwa samaki tani 293 aina ya Jodari na samaki wengineo, waliodaiwa kuwavua katika eneo la Bahari Kuu la Tanzania. 
   Washtakiwa 35 kati yao walikuwa ni raia wa mataifa tofautitofauti ya Bara la Asia, ikiwemo China Ufilipino Vietnam na wawili walikuwa raia wa Kenya. 
  Mshtakiwa mmoja raia wa Kenya alifariki dunia akiwa mahabusu kabla ya kesi yao kuisha. Hata hivyo washtakiwa wengine 31 waliachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawana kesi ya kujibu, na kubakia washtakiwa watano, ambapo wawili kati yao ndio waliopatikana na hatia na watatu wakaachiwa huru, baada ya mahakama kuridhika kuwa hawana hatia.

  0 0

  Mnamo tarehe 27.03.2014 majira ya saa 02:10 usiku huko Gulwe katika Wilaya ya Mpwapwa kulitokea ajali ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma baada ya kusombwa na mkondo wa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha. Kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo ilifanya kichwa cha treni hiyo kutumbukia kwenye mto Mimo.

                  VIFO:
  Ajali hiyo hadi hivi sasa imesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefahamika kwa majina yafuatayo:-
  1.  Felix s/o Kalonga
  2.  Ismail @ Suma

                MAJERUHI:
          Waliojeruhiwa ni kama ifuatavyo:-
  1.   Hassan s/o Kitambo, Miaka 89, Mkazi wa Kidete – Amelazwa katika Hospitali ya Mpwapwa.

  2.   Reuben Ngasongwa, Miaka 43 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Wilaya Mpwapwa kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

  3.   Michael Lupatu, Miaka 52 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Mpwapwa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
    
  4.   Ramadhan Kanenda, Miaka 34,  – Amelazwa Mpwapwa Hospitali.

  5.   Mohamed Salum, Miaka 25,  - Alitibiwa na kuruhusiwa

  6.   E.2699 CPL Mfaume – Ametibiwa na kuruhusiwa.

  7.   E.3295 CPL Respis – Bado amelazwa Mpwapwa Hospitali.

  Bado jitihada za kuwatafuta watu wengine wanne ambao hawajulikani walipo zinaendela.

  Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.


  0 0

  WAZIRI Mkuu Mhe.  Mizengo Pinda kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013-14, itakayowakutanisha wanawake wanne itakayofanyika kesho katika Ukumbi wa The African Dream mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye 
  atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, ambayo ndiyo iliyoratibu zoezi hilo, Eric Shigongo, amesema leo  kwamba shughuli hiyo itakuwa ni hitimisho la kazi kubwa ya kupokea na kuchuja kura zilizotumwa na wasomaji kumtafuta mwanamke bora ambaye ni nembo kwa taifa.

  “Zoezi hili lilifanyika kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu. Awali kabisa watu walitakiwa kutuma majina ya wanawake wanaowaona ni bora ili wapigiwe kura, watu waliitikia vizuri sana, kwani jumla ya majina 150 yalitumwa katika kipindi cha miezi miwili.
  “Baada ya hapo majina hayo yakaandikwa katika magazeti na watu wakatakiwa kupiga kura ili kuwatoa wanawake ambao wanadhani hawakustahili tuzo hizo,” alisema Shigongo, ambaye kampuni yake inatoa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi.
  Alisema katika awamu ya kwanza ya miezi hiyo miwili, majina ya wanawake 20 yaling’ara na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya kupigiwa kura, ambapo baada ya muda kama huo pia, wanawake kumi walipata alama nyingi na hivyo kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho.
  Alisema kwenye hatua hiyo ya mwisho, wanawake watano walipita ambao ni Ananilea Nkya, Anna Tibaijuka, Anna Kilango Malecela, Asha Rose Migiro na mama Maria Kham. Katika zoezi hilo, wanawake hao wenye mvuto katika jamii walichuana na mmoja wao, Nkya, kuondolewa baada ya kura zake kutotosha kwa ajili ya fainali,” alisema Shigongo.

  Kwa upande wake, mratibu wa Tuzo hizo, Luqman Maloto, alisema tukio hilo la kihistoria ambalo pia litashuhudiwa na wabunge wa Bunge la Katiba walio mjini Dodoma, litaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, akiwemo Linah,” alisema Maloto.

  0 0

  Kampuni kadhaa kutoka nchi ya Uturuki zimeanza kuingia Tanzania ili kushiriki katika kazi za ujenzi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. 
  Kukua kwa sekta ya ujenzi kumekua ndiyo kivutio kikuu kilichozifanya kampuni hizo kuonyesha nia ya kufungua ofisi zao hapa nchini. 
   Wakizungumzi katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walipomtembelea ofisini kwake, wawakilishi kutoka Kampuni Kampuni tatu tofauti wamempongeza Waziri huyo kwa jinsi anavyosimamia sekta hiyo ya ujenzi kiasi cha kuanza kuvutia makampuni makubwa kutoka nje. 
   “Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa kadhaa barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo” alibainisha Bw. Orhan Babaoglu ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki. 
   Mwakilishi mwingine kutoka Kampuni ya CEYTUN ya huko huko Uturuki Bw. Kursat Durak amebainisha kuwa, utendaji wa kampuni za Kituruki unafahamika duniani kote, hivyo ujio wao unalengo la kuamsha ushidani wa ubora lakini pia kuona kuwa gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinathibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti. 
   Mhe. Magufuli kwa upande wake wakati akiwakaribisha amewataka kuzingatia sheria na taratibu zinaoongoza shughuli za kandarasi hapa nchini. 
  Waziri Magufuli aliwajulisha kuwa, mbali na kazi za kawaida za kandarasi kwa hivi sasa kuna miradi kadhaa mikubwa inayokusudiwa kuendeshwa kwa kushirikisha sekta binafsi hivyo hiyo pia ni fursa wanayoweza kujishughulisha nayo hapa nchni.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu (kushoto) akiwasilisha kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, utambulisho wa makampuni ya Uturuki ambayo yamefungua ofisi hapa nchini kwa lengo la kushiriki katika kazi za kandarasi za ujenzi hapa nchini.

  Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipitia baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa na makampuni ya kandarasi kutoka Uturuki. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Alhaj Mussa Iyombe na kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu

  Bw. Kursat Durak (aliyenyoosha mkoni) kutoka Kampuni ya CEYTUN ya Uturuki akifafanua jambo. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu, Bw. Hassan Tunk Ma


  0 0

  Unajua kwamba unene wa kupindukia (overweight) unakuweka katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa mengi yakiwemo ya moyo,kisukari  presha n.k. ? 
  Kukabiliana na tatizo la unene ni chaguo lako na sisi tutakusaidia kutimiza lengo lako kupungua kilo unazotaka kwa kutumia programu yetu (Natural and healthy program) . Inakufikia popote ulipo.
  CLEAN 9. Ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusafisha mwili,kuondoa sumu mwilini,kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula. 
  Matumizi yake ni rahisi sana. 
  Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku. 
  Inatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 9 kisha kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15. Rahisi eeh?? 

  Nitafute kwa maelezo zaidi call 0752 36 13 05

  0 0
 • 03/28/14--10:00: Article 3

 • 0 0

  Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
  Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.
  Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali nchini.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani Mpwampwa.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)

older | 1 | .... | 402 | 403 | (Page 404) | 405 | 406 | .... | 3272 | newer