Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 404 | 405 | (Page 406) | 407 | 408 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,wakikata utepe  kuzindua barabara  5 za mradi zikiwa ni Kipangani-Kangani,Chwale –Likoni,Mzambrauni Takao-Pandani,Finya-Mzambarauni,Karimu-Finya-Mapofu na Bahanasa –Daya Mtambwe,Mkoa wa Kaskazini Pemba,ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,kwa pamoja wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bara bara 5 za Mradi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia wa Watu wa Marekani (MCC) hafla iliyofanyika leo katika uwanja wa Gombani wilaya ya Chake chake Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na   Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Changamoto za Milenia Tanzania Bw.Bernard S.Mchomvu,katika uzinduzi wa Mradi wa  Barabara 5 zilizojengwa na Mfuko huo wa Mcc Mkoa wa Kaskazini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,(kushoto) wakipata maelezo ya ramani ya michoro  ya ujenzi kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Usafirishaji (MCA-T) Eng Salum I.H.Sasillo,alipofika kuzindua Barabara 5 za Mradi Mkoa wa Kaskazini Pemba zilizojengwa kwa udhamini wa Mfuko wa Mcc.

  0 0

   Mchungaji Boniface Frank Mwenegoha akizungumza kuhusiana na sakata la ujenzi wa mji mpya Kigamboni

  Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi inayowakilisha malalamiko yao kuhusiana na ujenzi mpya wa mji wa Kigamboni,Bwa.Kassim Abdallah.

  0 0


  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Hondogo,Kata ya Mandera wakati wa muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,leo Machi 29,2014.

  Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,Suleiman Jaffo akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mandera Kibaoni wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo  Machi 29,2014.

  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kuruka sambamba na wakina Mama wa Kabila la Wamasai,wakati alipowasili kwenye Kitongoji cha Nameloki Chatanga,Kijiji cha Umasaini,Kata ya Mandera.

  Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Magole,Kata ya Mandera wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.

  Wananchi wa Kijiji cha Hondogo katika Kata ya Mandera ndani ya Jimbo la Chalinze,wakinyoosha mikono juu kuashiria kumpigia kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Mkutano wa Kampeni zake zilizofanyika Machi 29,2014.Picha na Othman Michuzi.


  0 0

  Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.
  Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, John Mwalisu, akitoa mada kwenye semina ya siku mbili, iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada.


  0 0
 • 03/29/14--17:49: bei ya madafu leo


 • 0 0

  Timu yaVijimambo inapenda kuwatangazia wadau wake kwa sasa imeanzisha VIJIMMBO RADIO ambayo ipo hewani sasa hivi kwa majaribio kwa hiyo kama utapata nafasi naomba uisikilize kupitia www.vijimamboradio.com 
  Toa maoni yako kumbuka tupo kwenye majaribio na bado tunaendelea kuboresha Radio hii na kama una maoni au ushauri unaweza toa maoni yako au tuandikie barua pepe djlukejoe@gmail.com au Vijimamboblog@gmail.com asante endelea kuburudika na 
  VIJIMAMBO RADIO

  0 0


   Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu.
  Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu.Kinana amewasili mkaoni humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi,mkoani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi na wanachama mbalimbali wa CCM waliofika uwanja ndege mjini Sumbawanga kumpokea mapema leo mchana.Kinana amewasili mkoani humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi leo,mkoani humo ikiwemo mkoa wa Katavi na Kigoma..
   Ni Chungu lakini kinatumika kama ngoma kikiwa kimebebwa baada ya kazi yake kuisha wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kina mapema leo mchana mjini Sumbawanga.
   Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi.
  PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0

  The Chief Secretary of the Government of Tanzania, Amb. Ombeni Sefue, will chair a roundtable dinner on ‘Local Content’, on Monday in Dar es Salaam, to promote dialogue on local content amongst relevant stakeholders by providing cross-country lessons on Local Content Policies. 

  In the months following the approval of the national “Natural Gas Policy of Tanzania”, a policy debate has emerged on the need for a Local Content Policy. Such a policy aims at fostering linkages within the gas industry and to maximise the benefits of natural resource extraction for the economy. Frequent media reports reported public and private sector leaders calling for immediate action by the Government to ensure local enterprise development and job opportunities.

  The roundtable event, which has been jointly organised by UONGOZI Institute, the Tanzania Private Sector Foundation, the Revenue Watch Institute/Natural Resource Charter and the World Bank, will gather representatives from the Government, private sector, academic sector, civil society and donor partners active in the local content agenda. 

  A joint statement by the organizers stated that “the event is the first in a series of planned monthly roundtable dinners which will provide a space for key stakeholders to gain and share knowledge on the design and implementation of local content policies and ultimately inform the local content policy making process".

  The monthly roundtable dinners will continue to be chaired by the Chief Secretary and feature selected countries with relevant LCP experience that Tanzania could benefit from.

  This month, the roundtable dinner will feature the experience of Trinidad and Tobago, with a keynote presentation from Anthony E. Paul, an oil and gas strategy consultant and Managing Director of the Association of Caribbean Energy Specialists Ltd.

  “These dialogues are a crucial step in the development of the Local Content Policy,” said Prof. Semboja, "the presence of the Ambassador Sefue further demonstrates the commitment of the government to ensure that opportunities from natural gas extraction translate into increased opportunities for Tanzanian society as a whole”. 

  0 0

  Kampuni ya EMOC imetoa msaada Kwa watoto yatima katika kituo cha New Life Orphanage Home kilichopo kigogo ambacho ni makao makuu ya kituo cha watoto yatima. New Life Orphanage Home ni kituo ambacho kimejitolea kulea watoto yatima wasiojiweza tangu mwaka 1998.

  New Life Orphanage Home kilianzishwa Magomeni mwaka 1998 Kwa lengo la kusaidia watoto yatima, na kilianza na watoto 18 tu. New Life Orphanage Home kimefanikiwa kufungua kituo kikubwa zaidi Kigogo iliopo wilaya ya Kinondoni na kuwa na idadi ya watoto 101 kuanzia watoto wachanga wa miezi hadi watoto wanapopata kazi.

  “Kipindi hiki Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhudumia watoto wasiojiweza wakiwemo yatima ambao wazazi wao walifariki wengine kwa magonjwa. Kuna namba kubwa ya watoto yatima wasiojiweza na wengina kuwa mitaani bila msaada wowote.

  Kuna vituo vichache sana ambavyo vilianzishwa na watu binafsi katika kusaidia watoto wasiojiweza. Kimoja wapo ni kituo cha New Life Orphanage Home ambacho kimejitolea kulea watoto kuanzia miezi mpaka wanapoolewa kwa wasichana na kupata kazi kwa wavulana.
  Kutokana na matatizo yanayowakabili watoto yatima, Excel Management and Outsourcing (T) Limited imeamua kutoa msaada kwa watoto yatima katika kituo cha New Life Orphanage Home kila baada ya miezi mitatu. Kampuni ya EMOC imeona ichukue nafasi hii ndogo kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha New Life Orphanage Home kwa kila baada ya kipindi cha miezi mitatu ikianza leo hii tarehe 28.03.2014”.

    “Japo msaada sio mkubwa sana kukidhi mahitaji ya watoto yatima,bali itasaidia kidogo kufanya watoto wajisike wapo kama watoto wengine wenye wazazi, wanapendwa na watu wote wanaowazunguka na pia kupata haki zao za msingi za kulelewa kama watoto wengine kwa wazazi wao” Excel management and Outsourcing (T) Limited Ni Kampuni ambayo imejikita kutoa huduma East Africa Yote ikiwa na malengo ya kufungua matawi katika mikoa ya Arusha na Mwanza. Kwa hapa Dar es Salaam imetanua mabawa yake Kwa makapuni zaidi ya 50.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifungua Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   : Mgeni rasmi katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akitoa hotuba fupi wakati wa tamasha hilo, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel.
   }: Mshereheshaji kutoka kikundi cha Temeke akionyesha umahiri wake kwa kula moto wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi lililofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Viongozi wa makundi ya muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi kipya na Utenzi waliooshiriki katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi wakiwa katika picha ya pamoja ambapo katika mziki wa dansi kundi la Msondo ngoma liliibuka kidedea huku upande wa taharabu Jahazi Modern Taharabu walishika nafasi ya kwanza huku muziki wa kizazi kipya msanii Kelvini Nyoni kuwabwaga wenzake na katika fani ya Utenzi Bi. Mariam Mponda kushika nafasi ya kwanza.
   Kundi la muziki wa dansi lijulikanalo kwa jina la Mashujaa wakitumbuiza wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

  0 0


  Katika gazeti la Jamhuri Toleo Namba 129 Machi 25-31, 2014 kulikuwa na habari iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari “Nyalandu ‘auza’ Hifadhi” ambapo maelezo ya habari hiyo yaliitaja Hifadhi ya 
  Taifa ya Katavi kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.

  Shirika la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Hifadhi nyingine 15 nchi nzima linapenda kukanusha habari hiyo iliyoandikwa kwa lengo la kupotosha umma kama ifuatavyo.

  Mosi, hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliokwisha kufanywa wa kuingia Mkataba wa Uendeshaji wa aina yoyote ile baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa na Mwekezaji yeyote kutoka nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni pamoja na African Parks Network waliotajwa katika habari
  husika.

  Pili, Sheria inayosimamia uanzishwaji wa maeneo ya Hifadhi za Taifa ikiwemo Katavi imelipa dhamana hii pekee shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya Watanzania na ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya usimamizi kama ilivyobainishwa katika habari hiyo.

  Tatu, Shirika la Hifadhi za Taifa bado linao uwezo thabiti wa kusimamia uendeshaji wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa ikifanya tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1974.

  Aidha, kama ambavyo shirika limekuwa likipanga katika mipango yake ya maendeleo mwaka hadi mwaka, katika mwaka mpya wa fedha ujao shirika limepanga kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi Saadani, Mikumi na Ruaha. Mkakati huu utahusisha kuongeza ubora wa utoaji huduma ikiwa ni pamoja na malazi ili kukuza utalii wa ndani. 

  Shirika litafungua ofisi Jijini Dar es Salaam na kuimarisha ofisi za Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za Hifadhi na kuweza kufanya
  ‘bookings’ kwa urahisi. Aidha, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa masoko ya nje, Shirika sasa litaanzisha ‘Road shows’ mbalimbali kwa soko la ndani na nchi za jirani. Vilevile, Shirika litaongeza kujitangaza kupitia Mitandao ya Jamii, TV, majarida na tovuti ya Shirika itaboreshwa katika kuarifu wadau masuala mbalimbali yanayojiri kwenye Hifadhi zetu.

  Tayari Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya kutekeleza mkakati huu wa kuzifanya hifadhi za ukanda wa kusini kuvutia watalii wengi zaidi.

  Imetolewa  na Idara ya Mawasiliano
  Hifadhi za Taifa Tanzania
  30.03.2014

  0 0

   Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Halamshauri ya mji mdogo wa Namanyere Wialayani Nkasi jioni ya leo,kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa Ofisi za chama hicho.Kinana alieleza kuwa kufuatia na taarifa mbalimbali alizokabidhiwa na Viongozi wa chama wilayani humo,alieleza kuwa wilaya ya Nkasi ina kero kadhaaa ikiwemo suala la Maji,Umeme,Uhaba wa walimu,Barabara pamoja na tatizo la soko la kuuza mazao ya wakulima,Kinana ameahidi yote hayao kuyafannyia kazi kwa kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa namna moja ama nyingine.
  Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakisikiliza kwa makini huku na wao wakiandika mambo kadhaa yaliyokuwa yakizungumza na Kinana kwa ajli ya kuweka kumbukumbu.
   Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Rukwa,Ndugu Hypolitus Matete akimtambulisha Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa,kutoka Zanzibar,Balozi Ali Abeid karume kwa wananchi halmashauri ya mji mdogo Namanyere,wilayani Nkasi mkoani Rukwa,kwenye mkutano wa hadhara.
   Wanachama mbalimbali wa CCM na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa hadhara,wakishangilia jambo.Ambapo katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa halmashauri ya mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi  mkoani Rukwa jioni ya leo.
   Baadhi ya wananchi wakishangilia jambo.


  0 0
 • 03/30/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Orchestre Fauvette wanakuja tena na "Jacqueline"

  0 0

  Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.
   Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam
   Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer International Tanzania umedhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda Foundation.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Bongo Movie akitoa maneno kwa wageni waalikwa pamoja na wasanii wa bongo movie na muziki nchini waliohudhuria sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa East 24.
   Keki ikikatwa kama ishara ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bongo Movie ikiwa imetimiza miaka 3
   Rich Rich akilishwa keki na Mwenyekiti.
  Mwenyekiti wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies, Bw Johnson Lukaza akipokea cheti cha kuthaminiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu nchini  iitwayo Proin Promotions Limited.
   Mtitu akipokea Cheti kutoka Kwa Mwenyekiti.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa East 24 uliopo Mikocheni katika jengo la Arcade.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, leo Machi 28, 2014. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). 
   Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
   Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
  Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
  **************************************************
  Na Sufianimafoto Reporter, Kibaha 
  Serikali imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

  Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu.

  Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.  

  Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia. 

  Alisema huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha  viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki. 

  Aidha, viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana. Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka. 

  Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16;

  0 0

  EALA
  According to East African Legislative Assembly rules and understandings, the speakership is rotational. As it is, the current Speaker is from Uganda. Her name is Margaret Nantongo Zziwa [in the photo above]. But before her term expires or come to an end, as the document below indicates, her speakership is in danger. Her removal seems to be eminent although she seems to be determined to hold on her seat. Zziwa, was elected in June 2012 for a five year term.

  Below is an excerpt of the removal document!;
  On 26th March 2014, a notice of motion for a resolution to remove the East African Legislative Assembly (EALA) Speaker from office was served on the EALA Clerk.

  This notice was seconded by Hon. Peter Mathuki from Kenya, Hon. Shyrose Bhanji from Tanzania, Hon. Dr. Odette Nyiramilimo from Rwanda, Hon. Hafsa Mossi from Burundi and supported by 33 signatures which is more than two thirds of the Assembly. These signatures were composed of all 9 Members of Burundi; all 9 Members of Rwanda; 5 Members of Tanzania; 5 Members of Kenya; and 5 Members of Uganda.

  On 27th march, a motion for a resolution to remove the speaker of EALA from office was served on the Clerk of the Assembly according to the Rules of Procedure. This motion cited the reasons for the bid to remove her from office as:
  -Poor governance and leadership skills;
  -Abuse of office; and
  -disrespect and intimidation of Members and Staff.
  In line with the Assembly Rules of procedure, the Motion requests the Assembly to remove the current speaker; she cannot continue to preside over proceedings of the Assembly since proceedings for her removal have commenced.

  In addition to this, the Motion Assembly urged the Assembly to elect a Member to preside at the next sittings of the Assembly.
  Immediately after the motion was served, Hon. Zziwa went to Kampala to attend a meeting with President which she had solicited for. She wanted to use female Members of EALA to persuade him to intervene in the matter. Out of 17 women members of EALA only 3 attended. The majority refused to attend the meeting. The women feel that the fact that she is the first woman speaker should not be used as an excuse, because she is incompetent and failed to deliver.

  The fact that she knew that the process of her removal was in accordance with the Assembly Rules of Procedure and she still proceeded to seek audience with the President demonstrates her disrespect for the Assembly and desperate attempts to hold onto to her office despite the fact that more than two third of the members have expressed their desire to remove from office. The process to remove Zziwa is now irreversible, the only option left for her is to resign or face the Legal Rules and Privileges Committee, which will interrogate her in public on the issues raised in the Motion.
  The next steps to be taken by the Assembly according to the Rules of Procedure are :

  • The clerk will put the motion on the order paper;
  • Procedure does not allow the Speaker to preside over the proceedings of the Assembly since proceedings for her removal commenced;
  • The Assembly may thereafter adjourn for say 30 minutes in order for the Members to confer on the person to chair the House.
  • The Clerk will then preside over the election of the person who will chair the sitting.
  • The motion will be tabled in the House and seconded in a sitting presided over by the person elected to chair the meeting.
  • The Assembly will then elect an elected member to preside over the sittings of the assembly;
  • the elected chairperson will then refer to motion for the removal of the Speaker to the Legal, Rules and Privileges Committee.
  • The Committee will then interrogate the issues raised in the motion.
  • when appearing before the Committee, the Speaker is entitled to appear in person or can be represented by a lawyer or any other person then the Committee is investing his or her removal.
  • The Committee will then compile a report, which report will be tabled before the House for debate.
  • the Assembly has to pass the motion for removal of the Speaker by not less than two-thirds majority of elected members of the Assembly, after which the Speaker shall cease to hold office.

  0 0

  DSC_0243
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi. Mwanaidi Salehe (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji, Bi. Fatma Gharib Bilal wakati wa sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious uliofanyika mwishoni mwa juma ndani ya Zanzibar Ocean View.(Picha na Zainul Mzige).
  DSC_0058
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-kulthum Ansel (kulia) akipozi na MC wa shughuli Bi. Fauziat Abood (katikati) pamoja na mjumbe mmoja wa wajumbe Mariam Yusuph Otembo.
  DSC_0063
  Pichani juu na chini ni wageni waalikwa wakipata Ukodak kabla ya shughuli kuanza kwenye Red carpet.
  DSC_0064DSC_0181
  Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Jana Machi 30,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini Mzee Hussein Mwindadi ambaye ni Baba wa Diwani wa Kata ya Mkange.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika jana Machi 30,2014.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akionyeshwa maendeleo ua ujenzi wa Msikiti (haupo pichani) na Sheikh Yahya Abdullah Imam wa Msikiti huo.
  Wananchi wa Kijiji cha Manda Mazinga wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika jana Machi 30,2014.


  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
  Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
  Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela, Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.

older | 1 | .... | 404 | 405 | (Page 406) | 407 | 408 | .... | 3284 | newer