Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

LUDEWA WAMPONGEZA RAIS DKT JAKAYA KIKWETE

$
0
0

Na  Francis Godwin Blog 
WANANCHI  wa Ludewa  mkoani  Njombe  wamempongeza  Rais Dr Jakaya Kikwete kwa  hatua  yake ya  kuwashirikisha  wananchi wa maeneo husika katika suala la utatuzi wa mgogoro wa mpaka  kati ya Tanzania na Malawi

Hatua  ya  wananchi  hao  kumpongeza  Rais  Dr Kikwete  imekuja  huku  ikiwa ni  siku  tatu zimepita  toka  mbunge wao  wa jimbo  la Ludewa Deo Filikunjombe ,mbunge wa jimbo la Kyela Dk. Harrison Mwakyembe na mbunge wa   jimbo la Mbinga  Magharibi John Komba  kurejea nchini  kutoka Malawi  katika  kikao  cha usuluhishi  wa mgogoro  wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania

Wakizungumza na  mwandishi  wa habari hizi wananchi hao  akiwemo Yohana  Haule  walisema  kuwa  hatua  ya  Rais Kikwete  kutumia  wananchi  wenye  kushughulikia  suala  hilo  ni hatua ya  kupongezwa  kwani wabunge hao  ni wawakilishi wa  wananchi hivyo kila kinachoendelea kitawafikia mapema  wananchi  wa maeneo ya mpakani Malawi na Tanzania.

Haule  alisema  kuwa  imani na matumani  ya  wana Ludewa ni kuona mbunge  wao amewawakilisha  katika  suala hilo na  kuwa  hawana  shaka na uwakilishi  wake na wanaamini  watapewa mrejesho  wa  kila kinachoendelea  katika  suala  hilo.

Hivyo  alisema  kwa  sasa hofu  ambayo awali  wananchi wa kando ya  ziwa Nyasa  walikuwa nayo  juu ya mgogoro  huo wa mpaka kati ya  Tanzania na Malawi  imeanza  kutoweka  kutokana na mbunge  wao Filikunjombe kuzunguka maeneo  yote ya Mwambao na  kufanya  mikutano na  kuwaondoa hofu  juu ya  hilo.

Huku Sarah Haule  mbali  ya  kumpongeza  Rais  Kikwete kwa  hatua  hiyo  pia  alimpongeza mbunge  Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali  za  kuwaletea  maendeleo  wananchi  wa Ludewa  huku  akimtaka  mbunge   huyo kuendelea  na msimamo  wake  katika kuwawakilishi  wana  Ludewa bungeni .

Red Cross yapigwa jeki kuwasaidia wahanga wa mafuriko Kilosa

$
0
0
 Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akifurahia jambo wakati akipokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii" Vodacom Foundation" Yessaya Mwakifulefule. Fedha hizo zimetolewa kwa chama hicho kwa ajili ya kuimarisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro na kuacha mamia ya kaya bila makazi. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Julius Kejo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu.
 Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kupokea msaada wa fedha, kiasi cha Shilingi milioni kumi kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii"Vodacom Foundation" kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nae katika picha kutoka Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
 Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale na Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzanaia"Vodacom Foundation" Yessaya Mwakifulefule, wakimsikiliza mmoja wa Maafisa wa Tanzania Red Cross punde baada ya kupokea msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo hicho  kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro
 Mkuu wa Kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania" Vodacom Foundation" Yessaya Mwakifulefule akizungumza na  waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kutoa msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na kitengo hicho"Vodacom Foundation"kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nao katika picha ni Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale (katikati)Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.

NEWZZ ALERT:STENDI KUU YA MABASI MOSHI,WAMILIKI WA MABASI MADOGO WAGOMA KUTOA HUDUMA

$
0
0
Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma.
Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta.

TAARIFA YA POLISI KUTOKA MKOA WA MBEYA LEO

NAIBU WAZIRI JANETH MBENE AFUNGUA MAFUNZO YA WADADISI WA ZOEZI LA SENSA YA VIWANDA

$
0
0
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene akiwahutubia wadadisi na wasimamizi kabla ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wadadisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.
======  ======  ======

NAIBU WAZIRI JANETH MBENE AFUNGUA MAFUNZO YA WADADISI WA ZOEZI LA SENSA YA VIWANDA
Na Veronica Kazimoto
Morogoro.

Wamiliki wa viwanda nchini wameagizwa kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha wakati wadadisi watakapofika katika ofisi zao kuwahoji kwa ajili ya kupata takwimu za viwanda vyao. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi na wasimamisi wa zoezi la Sensa ya Viwanda iliyofanyika leo mkoani Mororgoro, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (Mb) amesema ni muhimu wamiliki wa viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi kwa kuwa takwimu zitakazopatikana kutokana na Sensa hiyo zitatumika katika kupanga shughuli mbalimbali za maendeleo.  

“Nichukue Fursa hii kuwaagiza wenye viwanda wote nchini kuona kuwa zoezi hili ni lao na ni jukumu lao kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na pia waone kuwa zoezi hili ni kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.” Amesema Naibu Waziri Mbene.

Naibu Waziri Mbene amefafanua kuwa, zoezi hili la Sensa ya Viwanda lisichukuliwe kama njia ya Serikali kutaka kujua mapato au faida wanayopata wenye viwanda kwa lengo la kukusanya kodi bali ni kuisaidia Serikali kubaini mabadiliko ya muundo wa sekta ya viwanda, mchango wake kwenye pato la taifa na hatimaye kufanya maamuzi sahihi ya kisera.

Aidha ametoa wito kwa wadadisi wote wanaoshiriki katika mafunzo ya Sensa ya Viwanda kufuatilia na kuzingatia kwa makini mafunzo yote yatakayotolewa na wakufunzi ili lengo la kupata takwimu sahihi za viwanda liweze kufanikiwa. Awali akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa  amesema takwimu zitakazokusanywa katika Sensa hiyo zitahusu viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Dkt. Chuwa amefafanua kuwa katika sensa hiyo baadhi ya taarifa zitakazokusanywa ni pamoja na anuani na mahali viwanda vilipo, aina ya umiliki, utaifa wa mmiliki, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa na idadi ya wafanyakazi.

Taarifa nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaji, gharama za uzalishaji na mapato mangineyo. Mafunzo ya zoezi la Sensa ya Viwanda yamelenga vijana wapatao 175 ambao watafanya kazi ya kukusanya takwimu zinazohusu sekta ya viwanda hapa nchini kwa muda wa miezi miwili kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2014.  

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, SAAZ SULULA, AKAGUA MIRADI YA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA

$
0
0
Safari ya msafara wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula mwishoni mwa juma katika kukagua miradi inayofadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wahisani wengine katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa haikuwa rahisi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya barabara kutokana na mvua kubwa kunyesha na hivyo kupelekea magari ya mizigo inayokwenda nchi jirani za Burundi na DRC kupitia bandari ya kasanga kukwama na kuziba njia. Juhudi za ziada kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mkandarasi anaejenga barabara hiyo ya Sumbawanga - Kasanga kwa kiwango cha lami zilisaidia katika kuhakikisha magari yote yaliyokwama pamoja na msafara wa katibu Mkuu yanavuka salama.   
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake wakikagua vitanda kwa ajili ya wanafunzi pamoja na daharia katika shule ya  Sekondari Kasanga  Mkoani Rukwa. Mradi huo wa daharia (bweni) ni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake katika kukagua ujenzi wa miundombinu inayoendelea kujengwa katika soko la samaki la Kirando Wilayani Nkasi Mkaoni Rukwa mwishoni mwa juma.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com).

KATIBU MKUU WA CCM AMNADI RIDHIWANI KIKWETE KATIKA KATA ZA UBENA ZOMOZI LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa amemuinua mkono Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete ikiwa ni ishara ya kumnadi kwa wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ubena Zomozi huku akishangilia kwa shangwe,leo Machi 24,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akimwaga sera zake kwa Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa amesimama kusikiliza kwa makini sera za  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alizokuwa akitoa kwa Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakifatilia kwa makini sera za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete huku wakiwa wamejikinga kwa mvua kwa kutumia viti,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakiwa wamejikinga kwa mvua chini ya paa la moja ya Nyumba zilizopo kwenye Kata hiyo wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.Picha zote na Othman Michuzi.

KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta (kushoto) akimwapisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda (kulia) kuwa mjumbe wa Bunge hilo, Bungeni Mjini Dodoma Machi 24, 2014.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda baada ya kumwapisha kuwa mjumbe wa Bunge hilo, Bungeni Mjini Dodoma Machi 24, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, January Makamba (kushoto) na Ismail Jusa Ladhu wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Machi 24, 2014 baada ya Bunge kuahirishwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanachuo wa Chuo cha Nyuki cha Tabora waliotembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma Machi 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

"BACK to 90's "every Jumamosi with dj BONILUV ndani ya mzaLendo pUb, millennium tOwers

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA TANZANIA (TFF)

$
0
0
KORTI YAAGIZA TFF IKAMATE MIL 106/- KULIPA WACHEZAJI YANGA.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tumepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.

Tayari tumeanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.

Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.

Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.

Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo.

AZAM, YANGA VIWANJANI DAR, TANGA VPL
Timu za Azam na Yanga ambazo zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania pointi tatu.

Azam yenye pointi 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 19.

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina pointi 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).

KAMATI YA SHERIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa agizo la wanachama kurekebisha katiba zao.

TFF tulitoa agizo kwa wanachama wetu kufanyia marekebisho katiba ikiwemo kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa Machi 20 mwaka huu.

Hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa hatua inayofuata.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YAENDA BRAZIL
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo (Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani.

John Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania.

Michuano hiyo ya siku 10 inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana) inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.

Mwaka 2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.

MABINGWA WA MIKOA WATAKIWA MACHI 30
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwa vinatakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu.

Majina ya mabingwa yanatakiwa kuwasilishwa pamoja na usajili wa wachezaji waliotumika kwenye ligi ya mkoa. Kila klabu inaruhusiwa kuongeza wachezaji watano kutoka ndani ya mkoa husika, ambapo unatakiwa uthibitisho wa usajili huo.

Mpaka sasa ni vyama viwili tu ndivyo vimeshawasilisha mabingwa wao. Vyama hivyo ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) ambapo bingwa wake ni Kiluvya United, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi (LIREFA) ambapo bingwa ni Kariakoo SC.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

BANDARI MTWARA YAJIDHATITI KUONGEZA UWEZO WA KUHUDUMIA MIZIGO

$
0
0
 Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella (Kuliai) akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake kukagua kukagua mirdai ya maendeleo Bandari hapo. Kutoka kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus Rutasitara (Wakwanza Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Katikati).
 Afisa Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Kushoto) akitoa maelezo ya uendelezaji wa maeneo ya Bandari hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara Bandarini hapo. 
 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea eneo la Bandari ya Mtwara ambapo panapotarajiwa kuongezwa magati.

TCRA yapongeza Ushirikiano wa Vodacom na UmojaSwitch

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Prof. John Nkoma akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa mtandao wa ATM za Umoja na M-pesa unaowawezesha wateja wa M-pesa kutoa fedha kupitia ATM za mtandao huo nchi nzima. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Tiwssa na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Switch Danstan Mbilinyi. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es salaam. Huo ni ushirikiano wa kwanza unaohuisha mtandao wa ATM za benki zaidi ya 20 na huduma za kifedha za simu ya mkononi.

 Kutoka kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Switch Dunstan Mbilinyi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kelvin Twissa (wa kwanza kulia) wakifurahia Mkuu wa  Masoko wa M-pesa Isaac Nchunda kufanikiwa kutoa fedha kwenye M-pesa kupitia ATM ya Umoja ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma inayowawezesha wateja wa M-pesa kutoa fedha kupitia ATM hizo nchi nzima. Huo ni ushirikiano wa kwanza unaohusisha mtandao wa ATM za benki zaidi ya 20 na huduma za kifedha za simu ya mkononi.

 Mkuu wa Masoko wa M-pesa Isaac Nchunda (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi huduma mpya ya utoaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya M-pesa kupitia ATM za Umoja inavyofanyakazi muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo. Wanaoonekana pichani ni  Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma (wa pili kushoto), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa(wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Switch Danstan Mbilinyi.
  Mkuu wa Masoko wa M-pesa Isaac Nchunda (wa pili kulia) akifanya muamala wa kutoa fedha kutoka M-pesa kupitia ATM ya Umoja muda mfupi baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo la kihistoria ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof.John Nkoma (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Switch Danstan Mbilinyi (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa.Huo ni ushirikiano wa kwanza unaohuisha mtandao wa ATM za benki zaidi ya 20 na huduma za kifedha za simu ya mkononi
=======  ======  ======

TCRA yapongeza Ushirikiano wa Vodacom na UmojaSwitch
*        Ni baada ya Kuunganishwa kwa huduma ya M pesa na ATM za UmojaSwitch.

*      Wateja wa M pesa sasa kutoa fedha katika ATM za UmojaSwitch
Dar es Salaam, Machi 19, 2014 ... Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,(TCRA) imesema inafurahishwa na ukuaji na maendeleo ya kasi ya teknolojia ya simu za mkononi katika kuboresha maisha ya watu na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Prof. John Nkoma wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ushrikiano kati ya Kampuni ya Umoja Switch na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-pesa  utakao wawezesha wateja wa Mpesa kutoa fedha kupitia ATM za mtandao wa Umoja nchi nzima.

M-pesa ndio huduma inayoongoza miongoni mwa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi ikiwa na mtandao mpana zaidi wa mawakala zaidi ya 65,000 walioenea nchi nzima na hivyo kuiwezesha huduma hiyo kuwa rahisi zaidi kupatikana.

Prof. John Nkoma amepongeza ushirikiano huo katika kile alichokiita kuwa kitaendeleza mafanikio ya ukuaji wa tekonolojia ya simu za mkononi ikiwemo M-pesa huku akitanabaisha kuwa mamlaka yake imekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinarahisisha maisha ya Watanzania kwa kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku iwe katika kilimo na ufugaji, biashara na hata katika masuala ya kifamilia.

"Sisi kama Mamlaka ya Mawasiliano tumefurahishwa sana kwa ushirikiano huu, katika utoaji wa Leseni tunazo za aina nne moja ya miundombinu, huduma, matumizi na utangazaji. Katika Leseni ya Miundombinu huu ni mfano vizuri wa kutumia teknolojia ambapo sekta ya fedha zinaungana na sekta ya Mawasiliano katika kutoa huduma kwa Watanzania." Alisema Prof. Nkoma na kuongeza.

"Uwepo wa huduma hii utawawezesha Watanzania wengi kupata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi, haya ni maendeleo mazuri sana katika sekta ya Mawasiliano na sekta ya fedha, sasa hizi wananchi wanaweza kuchukua huduma nyingi sana, hili sio jambo dogo hivyo kwa namna ya upekee kabisa ningependa kuwapongeza Vodacom na Umoja Switch kwa kuwezesha Ushirikiano huu."

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alibainisha kwamba wateja sasa wanaweza wakatumia mashine za ATM za Umoja Switch sehemu yoyote ya nchi kufanya miamala yao ya kifedha.

"M Pesa imepiga hatua nyingine ya juu zaidi. Wateja wetu sasa hawana wasi wasi tena kwani wanaweza kutoa fedha kutoka katika Akaunti zao za M pesa kupitia ATM za UmojaSwitch mahali popote."

"Hii ni hatua kubwa tumepiga kwetu sisi wote na tutaendelea kuwaletea huduma na bidhaa nyingi zaidi sokoni," alisema Twissa na kuongezea kwamba, "M Pesa inaendelea kubadilika kulingana na maendeleo ya kiteknolojia ambayo yamelenga kuihudumia wateja wetu vizuri zaidi."

Mtandao wa Umojaswitch umeanzishwa mwaka 2006 ukiunganisha benki zaidi ya 24 nchini na ATM takribani 200.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UmojaSwitch Bw.Danford Mbilinyi   amesema kuwa anashukuru sana ushirikiano huu na Vodacom na kubainisha kwamba hii itasaidia katika kuwahudumia wateja ipasavyo mahali popote walipo.

"Hii ni siku kubwa sio tu kwetu sisi bali hata kwa wateja wetu pia. Ushirikiano huu ni wa aina yake kwetu sisi, na tunawashukuru sana Vodacom kwa kuamua kuja kwetu sisi." Alisema Mbilinyi.

Mpaka sasa huduma ya M Pesa inayotolewa na Vodacom inajivunia kuwa na mawakala takribani 65,000 waliosambaa nchi nzima, ambao siku zote wapo tayari kuwahudumia wateja wetu.

Huduma hii pia imekuwa ikiingia katika ushirikiano na mabenki na makampuni mengine nchini, wateja wetu sasa wana uwezo wa kununua bidhaa na huduma mbali mbali na kufanya malipo kupitia M Pesa.

WIZARA YA MABO YA NJE NA UBALOZI WA CHINA WAFANYA MKUTANO WA PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. 

Lu Youqing wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo siku ya Jumanne tarehe 25 Machi, 2014. Mkutano huo ulizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia  kati ya Tanzania na China na mafanikio ya ziara ya Rais wa China aliyoifanya nchini ambayo imetimiza mwaka mmoja.
Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mkutano wa waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Bw. Assah Mwambene wakati wa Mkutano wa Pamoja na waandishi wa habari kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi wa China.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga akisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa. wengine ni maafisa wa Ubalozi China.
Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mkutano huo. 
Picha ya pamoja, kutoka kulia ni Balozi wa China, Mhe. Lu Youqing; Katibu Mkuu, Bw. John M. Haule; Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nathaniel D. Kaaya; Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga na Afisa kutoka Ubalozi wa China.

KUSOMA HOTUBA YA  KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA BOFYA HAPA

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AKAMILISHA ZIARA YAKE WILAYA YA ILALA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mradi wa ujenzi wa tanki la maji katika eneo la Tabata Kimanga, akiwa katika ziara ya siku moja katika wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadik.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kina ameanza ziara ya siku nne mkoani Dar Es Salaam,akiwa ameanzia wilaya ya Ilala leo.lengo ya Ziara hiyo ikiwa ni Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni utejelezaji wa chama hicho.
 Kinana akishuka baada ya kukagua tanki hilo litakalohudumia wakazi wa Tabata,zaidi ya Elfu 20 lenye ujazo wa lita 200,000.
Kinana akikagua soko la Tabata Kisiwani wakati wa ziara hiyo.
Mbune wa Ilala Mussa Zungu akizungumzia mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo kwenye eneo la Kidongo chekundu, wilayani Ilala
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akizungumzia mradi huo mbele ya Kinana.

UHURU KENYATA AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI JIJINI ARUSHA,ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Pichani ni Rais wa Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mmashariki,Uhuru Kenyata akiwa anapanda mti nje ya jengo la ofisi ya makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mapema leo jijini Arusha wakati alipokuwa na ziara ya sikumbili  ya kutembelea makao makuu ya jumuiya hiyo.
Pichani ni  Spika wa bunge la Jmuiya ya Afrika Mashariki,Magrethi Ziwa  akiwa na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Uhuru Kenyata mara baada ya kutoka katika uwanja kupanda miti(picha zote na woinde  shizza,Arusha)

BUNGE LA KATIBA, PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA BARRICK GOLD TANZANIA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Africana  Barrick Gold Tanzania, kwenye makazi yake mjini Dodoma  Machi 25,2014. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Serikali (Director of Government Relations)), Balozi Emmanuel  Ole Naiko, Makamu wa Rais, Deo Mwanyika na Ofisa Mtendaji Mkuu (Chief  Executive Officer ), Brand Gordon. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masere  (kushoto kwake) wakizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Africana  Barrick Gold Tanzania, kwenye makazi yake mjini Dodoma  Machi 25,2014. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Serikali (Director of Government Relations)), Balozi Emmanuel Ole Naiko, Makamu wa Rais, Deo Mwanyika na Ofisa Mtendaji Mkuu (Chief  Executive Officer ), Brand Gordon. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiteta na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale-Mwiru, Bungeni Mjini  Dodoma Machi 25, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA MKUU WA MKOA WA MARA

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mhe. Hawa A. Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa, aliyefariki leo tarehe 25 Machi, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Pokea rambirambi zangu za dhati na  masikitiko makubwa kufuatia   kifo cha Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa kwa Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi.    Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki leo tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Rais pia amemwomba Mhe. Ghasia amfikishie salamu za pole kwa Mke  wa Marehemu,Watoto na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao. Rais amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu kwani wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.

“Hakika tumempoteza kiongozi mchapakazi ambaye amekuwa akijituma  na kuwatumikia Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake.  Pengo aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi kuzibika kamwe lakini hatuna budi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho ya Marehemu mahali pema peponi” Amina.

Taratibu na maandalizi ya mazishi zinafanywa kwa ushirikiano wa Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.

Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za  Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto watano.
 
Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Machi,2014

GLOBAL WOMAN OF THE YEAR 2013

KUTOKA BUNGE LA KATIBA DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Maalumla Katiba,Mh. Samweli Sitta (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na wajumbe wa Bunge hilo,mjini Dodoma mara baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge hilo. Wengine ni Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia),Captain Mstaafu John Komba , Erasto Zambi na Diana Chilolo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na Lazaro Nyalandu (kushoto) wakiwahi kuhududhuria mkutano wa Bunge Maalum unaoendelea mjini Dodoma leo. Picha na Tiganya Vincent-Dodoma

CHUO CHA VETA CHATAMBULISHA MRADI WA USHIRIKIANO KATI YAKE NA UJERUMANI UJULIKANAO KAMA "GERMAN DUAL SYSTEM APPRENTICESHIP" LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akizungumzia juu ya mradi ambao German wameshirikiana na Chuo cha VETA nchini katika kuhakikisha wanaboresha maswala ya elimu ya vitendo Tanzania. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru.
 Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutambulisha mradi wa ushirikiano kati ya Vyuo vya Ujerumani na VETA kwa wanafunzi wa Tanzania.
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiongea na waandishi wa habari wakati alipowatembeza kwenye moja ya karakana ambayo inatoa masomo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" iliyopo katika Chuo Cha VETA kilichopo Chang'ombe jijini Dar Es Salaam.
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiwaonyesha moja ya magari yaliyotolewa na Kampuni ya Noble Motors kwaajili ya Mafunzo ya Vitendo yaliyo chini ya Mradi wa "German Dual System Apprenticeship" kwa wanafunzi wa Chuo Cha VETA.
 Wanafunzi wa Chuo Cha VETA wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ambayo yapo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na kuunganishwa na makampuni ambao wanafunzi hao hupelekwa kwaajili ya mafunzo zaidi.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>