Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 397 | 398 | (Page 399) | 400 | 401 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Chipukizi wa Mkoa wa Tanga wakimkaribisha kwa maua Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika tarafa ya Mkata, wilayani Handeni mkoa wa Tanga, Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi 
   -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Msomela wakatia  a lipokwenda kukabidhi madume bora ya ng’ombe kwa wafugaji leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madume bora ya ng’ombe na kasha kuwakabidhi baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Msomela wilayni Handeni leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mmoja wa wafugaji mwenye asili ya kimasai bwana Shayo Lahoda aliyegawiwa dume bora la ng’ombe katika kijiji cha Msomela wilayani handeni leo 
   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni leo
   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na ngoma za utamaduni baada ya kuzindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Bwawa la maji la Mkata muda mfupi baada ya kulizindua huko Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga leo asubuhi.Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

  0 0


  0 0

  The High Performance Leadership seminar by international leadership experts Brian Tracy and Azim Jamal is coming your way this June. Book now for early bird discounts and avoid last minute disappointments. Limited seats available. Call 0717 109 362 or 0784 636 169, or email info@mikono.biz


  0 0

  Russell Hobbs, today, launched its Tanzanian distribution outlet at Viva Towers Dar es salaam. Russell Hobbs, the number one small appliances brand in the United Kingdom, is a brand that is known for its quality and unique functional design. 
  It is strong in all the categories in which it operates, such as beverage, cooking, food preparation, house wares, personal care and others. It is therefore able to offer a quality, branded family of products which other competitors are not always able to. This will be the world’s first exclusive Russell Hobbs concept store. 
  “The move to open in Tanzania is driven by it’s fast growing economy which is quickly making investors realize it’s potential as a hub for East Africa. The port facilities are an added benefit and the road infrastructure gives ample access to neighbouring countries.” said Alan Coward, Chief Executive Officer of HOLB (Pty) Ltd .
  In addition, Marion Kearns, Marketing Executive of HOLB(Pty) Ltd said that, the Growth in the country’s infrastructure and government investment therein make Tanzania a strategic location for investment and business development.

  And further noted that “The work ethic and diligence of the Tanzanian people make it a natural target for future expansion for HOLB.”

   

  The relationship between JD Pharmacy, which is the leading provider of pharmaceuticals in Tanzania, and HOLB (Pty) Ltd will create major opportunities for all the stakeholders such employees, suppliers, government and consumers.

   “We perceive an exciting epoch with HOLB in bringing the Russell Hobbs brand to Tanzania. Our clientele are the lifeline of our business and we are committed to provide outstanding service to our customers.” commented Kiran Pattni, Chief Executive Officer of JD Pharmacy.

  Home of Living Brands (Pty) Ltd is an African Company with its head office based in Johannesburg, and is a wholly-owned subsidiary of the Bidvest Group Limited. HOLB is a consumer brands company which has leading world brands either under licence or with direct ownership, which it markets along with its chosen business partners to consumers in Africa, the JD Pharmacy in Tanzania


  Home of Living Brands Limited is a focused group specializing in the sales and marketing of branded household durables. Whereby their vast range of quality products consists of the best known local and international brands, so you always know that you're getting world-class products.

  Russell Hobbs which was Founded in Great Britain in 1952 by Bill Russell and Peter Hobbs, the brand led the way by introducing products which offer real consumer benefits and technological advancements to make life in the home easier and more enjoyable, also has presence in South Africa, Namibia, Botswana, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Tanzania, Kenya, Ghana, Nigeria, Ivory Coast and Angola.


  In attendance of the event from Home of Living Brands (Pty) Ltd (HOLB) was: Alan Coward -Chief Executive Officer; Murray Crow - Managing Director; Erwin Minnie - Africa Sales Manager; Marion Kearns - Marketing Executive; and Michele Snyders – Exports Operations Manager. Attending from JD Pharmacy, the official Tanzanian distributors for HOLB: Kiran Pattni - Chief Executive Officer; and Sanjay Patadia - Managing Director. Also in attendance were store owners and management from Tanzania Retailers, HOLB (Pty) Ltd distributors from various African countries, VIP Guests and select media. 


  0 0


  0 0


  Mdau Ernest Makulilo ambaye huandika kuhusu masuala ya Scolarship HAPA na pia kutoa video za suala hili HAPA
  UNATAKA SCOLARSHIP? Unajua pa kuzipata? Unajua namna ya kuzipata? Masharti yake je? Makosa yanayofanywa na wengi? Tofauti ya Scholarships za Undergraduate na Graduates wazijua? Yapi ya kuchunga wakati wa kutafuta scholarships? Boniface Makulilo ambaye amenufaika na scholarship hizi na kuandika kuzihusu kwa miaka ipatayo sita anaungana na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kujadili hili. Kuna mengi mema ya kujifunza. KARIBU NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

  0 0
 • 03/23/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • George Michael  na "Careless Whisper"

  0 0

  KUNA njia nyingi ya kumtukuza, kumuabudu na kupata Neema ya Mungu ambayo ni kwenda kanisani na kusali na njia ya nyimbo ambayo mtu unaweza kupata Baraka kubwa kutokana na nyimbo za injili zinazoimbwa na waimbaji mbalimbali wa muziki huo; amesema Mama Tunu Pinda.

  Mama Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda, ameyasema hayo alipozungumza na Hekaheka kuhusu Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 20 mwaka huu ambayo itakuwa  ni Sikukuu ya Pasaka inayoadhimishwa na Wakristo Duniani kote kwa Kufufuka Yesu Kristo mwana wa Mungu.

  Akielezea faida za kwenda kwenye Tamasha la Pasaka, Mama Pinda anasema ni kwa ajili ya kwenda kusikiliza nyimbo mbalimbali zitakazokuwa zikiimbwa na waimbaji wa nyimbo za injili ambako unaweza kupata Baraka na kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu na hatimaye kutenda dhambi.Tamasha hilo ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kwa siku hiyo ya Pasaka na hatimaye katika Mikoa mingine saba ya Tanzania Bara.

   “...Mwaka juzi nilipokuja kwenye Tamasha la Pasaka kulikuwa kuna watu wengi wa kila rika wazee, vijana na hata watoto wadogo hali hiyo ilidhihirisha ni kwa namna gani Watanzania wanapenda nyimbo za injili ambazo ninaamini wanapata Neema ya Mungu, alisema Mama Pinda.Akaongeza, “Utamaduni huu wa kusherehekea Sikukuu za kidini kama vile Pasaka kwa kwenda katika matamasha ya nyimbo za injili ni mzuri kwa sababu unawaondoa watu katika vishawishi na kuwafanya kuwa karibu zaidi na uwepo wa Mungu,…”

  Amesema ili kupata Neema ya Mungu ni vyema watu wengi zaidi wakajitokeza siku hiyo ya Tamasha la Pasaka kwa Dar es salaam na mikoa mingine ambayo Tamasha litafika ili kuweza kujizolea baraka za Mungu kupitia nyimbo za injili ambazo zitaimbwa na waimbaji wa ndani na nje ya nchi; huku akisisitiza kuwa endapo atapata nafasi kwa mwaka huu atahudhuria tamasha hilo. Hata hivyo alisema nyimbo za injili ni burudani lakini kwa upande mwingine ni sehemu ya ibada ambayo msikilizaji anapokea Baraka na mafundisho ya biblia kupitia nyimbo hizo; lakini pia zinasaidia kutokutenda dhambi kwa kwenda katika starehe ambazo hazimpendezi Mungu.

  “…Sikuku ya Pasaka inaadhimishwa kwa Kufufuka kwa Yesu Kristu ambayo ni alama ya ushindi kwa wanadamu, hivyo ni busara kwa Wakristo wote kuhakikisha tunaacha dhambi na kuyashika yale yote aliyotuachia Yesu Kristo, ambayo ni Upendo na Amani bila kusahau kuiombea nchi yetu. 

  Tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kuwashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi, lengo kuu ni kuweza kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima, akinamama wajane na wengine wenye uhitaji maalum.

  Hata hivyo Mama Pinda aliwataka Watanzania kuwa na Moyo wa kujitoa kwa watu wahitaji ambao wanahitaji misaada mbalimbali na hawana mtu wa kuwasaidia. “…Unaweza kukuta familia moja mtoto anakula chakula mpaka anazasa na kutupwa, lakini familia nyingine mtoto hana chakula na analala njaa; hivyo ni jukumu letu sote kusaidiana kama binadamu, tusiiachie serikali kila kitu ifanye,” alisema Mama Pinda.

  Akaongeza kuwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, ni mfano mzuri wa kuigwa na  watu wenye uwezo kuwasaidia wahitaji, kwa kufanya hivyo watapata Baraka na kuongezewa zaidi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya  Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL.
  Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

  Kituo cha Afya Tunduma

  Kampuni ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.

  Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

  Malulu amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza  tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .

  Aidha Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo  mbinu  ya maji. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.


  0 0

   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kifuleta,Kata ya Mbwewe jana Machi 23,2013 
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini,Mzee Rajab Seif Kabeilwa ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mzee Mrisho Kikwete ambaye ni Babu yake,wakati alipokwenda kumsalimia kijijini kwake,Pongwe Kiona jana Machi 23,2013.
  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akizindua shina CCM la vijana wa boda boda katika kijiji cha Pongwe Kiona, jana Machi 23,2013.

  0 0

  Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
  Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
  Mkuu wa Kijiji... Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe.

  0 0
 • 03/24/14--01:15: Article 17


 • 0 0

  DSC_0043
  Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya.

  Na. mwandishi wetu, Pangani.
  Mawakala wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .

  Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.

  Mmoja wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,” alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.
  DSC_0105
  Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.
  Katika kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa na vipindi vya redio.

  “Sisi baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone” tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.
  DSC_0281
  Sospeter Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.
  Sabina Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kabla ya mafunzo haya kuanza. 

  Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki kituo cha Sengerema FM redio.

  “Mimi nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo, bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali ya vijijini hususan ya maendeleo”.


  0 0
 • 03/24/14--01:22: BMW X5 For sale.
 •  Manufactured in 2003, Imported 2013, Convertible, Milage 176K, Engine Capacity 3000cc...Excellent condition. Serious buyers only call 0754 978 6440787 6099990685102222
  0 0
 • 03/24/14--01:31: Article 14


 • 0 0  Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
  Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
  Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam

  mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi

  Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu

  mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu

  katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia  Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne

  Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa
   

  0 0


   picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.
   Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm

  Na Woinde Shizza,Arusha  Jumla ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti  wilayani Arumeru  kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani  wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa   vijana wa  CHADEMA wa kata hiyo .

  tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.  Akiongea wakati wa kurudisha  kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa   ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.  Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani CHADEMA  ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli  ambayo inatakiwa iwenacho kama chama  Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi  na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama  .  Aidha alibainisha kuwa katika kata yao  tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi  bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa.Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi  ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.  Kwa upande wake  katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa  wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi  kufuatilia swala hili.  Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka  na kata yao haitapata viongozi wazuri.  Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto wao wakilala njaa.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 03/24/14--02:30: Article 11


 • 0 0

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye koti jeusi katikati) akiwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani Tanga.
   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyenyoosha mkono) akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anayempongeza kiongozi wa kikundi cha ngoma ya Selo baada ya kutumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mkata – Handeni - Korogwe. Anayeangalia (kulia) ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Handeni Dkt. Abdallah Kigoda.
   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kukata utepe kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani Tanga.
  Sehemu ya barabara ya Handeni – Mkata.


  RAIS KIKWETE AZIFUNGUA BARABARA ZA MKATA – HANDENI NA KOROGWE – HANDENI MKOANI TANGA.
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wakazi wa Handeni na maeneo inakopita barabara ya Mkata – Handeni na Korogwe – Handeni kutumia ipasavyo fursa ya kupatikana kwa barabara hizo za lami kuyaboresha maisha yao.
   
  Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara  inayoinganisha Makao Makuu ya Wilaya ya Handeni na barabara kuu ya Tanga - Dar es Salaam kupitia Mkata na upande mwingine kuunganisha na barabara kuu ya Tanga – Moshi – Arusha kwa upande wa Korogwe.
   
  Mhe. Rais ameelezea kuwa lengo la Serikali ni kuona kwamba, barabara ya Mkata hadi Handeni inaendelezwa hadi Kondoa kupitia Kiberashi kwani kufunguka kwa ukanda huu kutakuwa ni chachu kubwa ya kuinua shughuli nyingi za kiuchumi hasa kwa sekta ya kilimo katika maeneo hayo inakopita barabara hiyo.
   
  Akiwasilisha tarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa barabara ya Mkata - Handeni ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ina urefu wa kilometa 53.2 ikiwa imejengwa na Mkandarasi Sinohydro Corporation Ltd kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya Shilingi bilioni 57.3.  Eng. Mfugale alibainisha kuwa mkataba wa mradi huu ulisainiwa mwezi June 2009 na kazi zikakammilika mwezi Novemba 2012 baada kutatua changamoto ambazo zilikuwa zinakwamisha kukamilika kwa muradi huo mapema zaidi kama ilivyokuwa imepangwa kimkataba.
   
  Ufunguzi wa barabara hiyo umeenda sambamba na ufunguzi wa barabara ya Korogwe hadi Handeni ambayo vile vile imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
   
  Akitoa tarifa kuhusu miradi huo wa Korogwe – Handeni, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa Mkandarasi Sinohydro Corporation Ltd ndiye pia iliyeijenga barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilometa 65. Mkataba wa Mradi huu ulisainiwa mwezi June 2009 na kazi zikakamilika mwezi June 2013 na imejengwa kwa ghrama ya Shilingi bilioni 63.2. Kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 kimelipwa kama fidia kwa wale waliofuatwa na barabara hiyo katika baadhi ya maeneo.
   
  Naye Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielezea baadhi ya faida zitakazopatikana kutokana na kujengwa kwa barabara hizo alibainisha kuwa barabara ya kutokea Korogwe hadi Handeni ndiyo barabara itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari katika barabara  kuu ya TANZAM hasa kwa wasafiri na wasafirishaji wanaotokea maeneo ya Iringa, Mikumi na mengineyo katika ukanda huo.

  Waziri Magufuli alifafanua kwa kwa kupitia Mikumi, Kilosa, Turiani, Mziha hadi Handeni na kuelekea Korogwe au Mkata mkoani Tanga kunapunguza zaidi ya kilometa 120 tofauti na kuzungukia Morogoro na Chalenze.

  “Hivi sasa mtu anayetokea Iringa analazimika kupitia Mikumi na Morogoro mjini hadi Chalinze ndipo aelekee Tanga, mzunguko ambao ni mrefu kulinganisha na barabara hii ya kupitia Mikumi, Kilosa Magole, Mziha hadi Handeni” alisistiza Waziri Magufuli.

  Kwa upande mwingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliwafahamisha wananchi waliohudhuria kwa wingi katika sherehe hizo kuwa, tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika kwa barabara inayoanzia Handeni kuelekea Kiberashi hadi Kwamtoro mkoani Dodoma.

  Rais Kiwete aliabinisha kuwa hatua hiyo pia imefikiwa kwa barabara ya Handeni, Mziha, Dumila, Kilosa hadi Mikumi. “Hatua inayofuata ni kutafuta fedha za kujenga maeneo katika sehemu hizo ambayo bado hayajapata makandarasi” alifafanua zaidi Rais Kikwete.  

  Hata hivyo Mhe. Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaasa wasafirishaji kuzingatia masuala ya usalama barabarani kwa kupakia mizigo kulingana na viwango vilivyowekwa kisheria. Alielezea kuwa moja ya adui wakuu waharibifu wa barabara ni uzidishaji wa mizigo kupita viwango vilivyowekwa kisheria.

  Mheshimiwa Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo pia ataweka jiwela msingi kuzindua ujenzi wa barabara ya Korogwe – Mkumbara.


  0 0

   Meneja wa Sido mkoa wa Lindi,Mwita Kasisi akieleza
  jinsi shirika lake linavyowezesha wajasilamali wa mkoa huo kwa kuwapa
  mikopo na elimu ya wajasiliamali katika hafla Fupi ya kukabidhi hundi
  za mikopo kwa wajasiliamali 21,kutoka kushoto ni Bw Dickson
  Kindole,Mhandisi Sido,Bi Salma Ally,Afisa mikopo na Mkuu wa Wilaya ya
  Lindi Dr Nassor Hamid

   Baadhi ya wajasiliamali waliokabidhiwa hundi za mikopo
  wakimsikiliza Mkuu wa wilaya( hayupo pichani)Katika Hafla hiyo
  iliyofanyika jana mjini Lindi

   Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dr Nassor Hamid akikabidhi Hundi kwa
  Bi Fatuma Hamis katika hafla ya kukabidhi hundi kwa wajasiliamali wa
  mkoa wa Lindi

   Bw Abdallah Mbinga akipokea Hundi ya mkopo toka kwa mkuu wa
  wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid


   Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi na Watumishi
  wa sido wakiwa na wajasiliamali waliowezeshwa na shirika hilo kwa
  kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kibiashara
  ========   ========  =======
  Na Abdulaziz ,Lindi
  Jumla ya Tshs Milioni 42.5 zimetolewa kwa Wajasiliamali  21 wa Mkoa wa
  Lindi katika Kuimarisha Biashara  ikiwa ni nyongeza ya Mikopo
  inayotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO)Chini ya Mpango
  unaowezeshwa  katika kusaidia Jamii kujitegemea ikiwemo kuchangia
  maendeleo.

  Akisoma taarifa ya Shirika hilo wakati wa kukabidhiwa Hundi kwa
  Wajasiliamali hao  Meneja wa Mkoa,Mwita Kasisi  ameeleza kuwa mkopo
  huo ni mfululizo wa mikopo iliyoyotolewa kwa wajasiliamali 1328
  kuanzia  mwaka 1994.

  Kasisi alibainisha kuwa  lengo kuu la kutoa mikopo ni kukuza na
  kuendeleza viwanda vidogovidogo pamoja na kuboresha masoko ya Bidhaa
  zinazozalishwa na wajasiliamali wadogo kwa kupandisha thamani ya mazao
  ikiwemo zao la Ufuta na korosho.

  Aidha Kasisi alisema kwa sasa Shirika linaendelea kujikita katika
  kuhakikisha wajasiliamali wanapata ushauri na mafunzo ya aina
  mbalimbali, ili kujiweka tayari kwenye ukuzaji wa viwanda vidogovidogo
  .
  Akiongea na wajasiliamali hao kabla ya kukabidhi Hundi kwa
  wajasiliamali hao 21,Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dr.Nassoro Ally Hamidi
  amewataka wajasiliamali hao kuitumia mikopo hiyo kwa malengo
  yaliyokusudiwa ili  kuendeleza na kukuza mitaji yao kufuatana na
  mifumo ya Ubora ili kupata soko zuri la Bidhaa zao

  Aidha Dr Hamid alisema kuwa Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sasa
  inaimarika kibiashara kutokana na ugunduzi wa Nishati ya Gesi hivyo ni
  lazima wafanyabiashara wajipange kuimarisha ubora wa bidhaa zao ili
  kupata soko na kuondoa ulazima wa kuagiza bidhaa toka katika mikoa
  mingine na nje ya Nchi

  Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali wameiomba Serikali kuendeleza
  elimu ya Kibiashara kwa wajasiliamali ikiwemo kuwawezesha kwa mikopo
  yenye riba nafuu ili kumkomboa mlaji mwenye kipato kidogo huku
  wakiitaka Mamlaka ya Mapato kuangalia viwango vya kodi kulingana na
  ukubwa wa biashara za wajasiliamali wadogo

  Hafla hiyo ya kukabidhi hundi hizo imefanyika katika ofisi za shirika
  hilo mkoani Lindi

older | 1 | .... | 397 | 398 | (Page 399) | 400 | 401 | .... | 3285 | newer