Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 394 | 395 | (Page 396) | 397 | 398 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fatma Abubakar Mwassa akikata utepe kuzindua rasmi tawi la AccessBank Tabora mnamo tarehe 15th March 2014. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa benki hiyo Ndugu Muganyizi Bisheko akifatiwa na muwakilishi wa uongozi wa AccessBank Ndugu Emmanuel Venance. Waliosimama kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tabora mh. Suleiman Kumchaya akifatiwa na Meneja wa Tawi hilo ndugu Enosy Ndobeji.
  Meneja wa Tawi la AccessBank Tabora ndugu Enosy Ndobeji akitoa neon la shukrani kwa walioudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi hilo. Kushoto kwake ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa Benki hiyo ndugu Muganyizi Bisheko na aliekaa kulia ni Mwakilishi wa uongozi wa Benki hiyo ndugu Emmanuel Venance.
  Wafanyakazi wa AccessBank tawi la Tabora wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hili iliyofanyika tarehe 15th March 2014.

  0 0  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi Bw. Mrtin Ntemo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu maendeleo yaliyofikwa katika ujenzi wa barabara hapa nchini tangu Serikali ya  awamu ya nne ilipoingia madarakani . Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.

  0 0

  MADADI MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi.

  Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

  Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.

  Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.

  Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo.

  Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi.

  Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

  YANGA, SIMBA ZAPIGWA FAINI MIL 25.

  Klabu za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu hizo.Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

  Tunatoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na tutachukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.

  RAMBIRAMBI KIFO CHA MSHABIKI.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mshabiki Deodatus Mwakyangula kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Msiba huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea wakati akiwa uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

  RWIZA, LIUNDA KUSIMAMIA MECHI ZA CAF.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua Watanzania Alfred Rwiza na Leslie Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii na mwezi ujao.

  Liunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) kati ya How Mine ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka huu) jijini Bulawayo.

  Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael na Luelseghed Ghebremichael.

  Naye Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Maseru.

  Mechi hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan Lengani, Innocent Kaundula, Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka nchini Malawi.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer
  Tanzania Football Federation (TFF)

  0 0  0 0

   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akiongea kwa njia na mmoja wa washindi wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid wakati wa  kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo aeleza jambo kwa wana habari(hawapo pichani)  wakati wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid(kushoto), Maafisa waandamizi kutoka PWC(wa pili kulia) na push mobile(wa kwanza kulia) mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akitangaza washindi wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha  mhe Mwigulu Nchemba amehutubia kikao cha pamoja cha bunge la ACP na EU katika mji wa Strasbourg nchini Ufaransa.
  Katika hotuba yake, mhe Mwigulu alianza kwa kukishukuru chombo hicho kwa ajili ya msimamo wake usioyumba kwenye maswala ya amani akitolea mfano wa kazi nzuri waliofanya kwenye swala la Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudani  Kusini. Mhe Mwigulu aliitaka Jumuiya ya Kimataifa imsaidie Rais wa muda Mama Carthrine Samba Panza ili kuwezesha kipindi cha mpito na maridhiano kuwezesha zoezi la uchaguzi huru na wa haki. 
  Kuhusu maswala ya kiuchumi mhe Mwigulu aliwakumbusha wajumbe wa bunge hilo  kuwa umebaki mwaka mmoja tu kumalizia mpango wa malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s). Mhe Mwigulu aliitaka  Jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa mpango wa maendeleo baada ya 2015 unalenga nguzo  tatu mhimu akizitaja kuwa  kijamii, kiuchumi na Mazingira.  
  Kuhusu kiuchumi na Kijamii mhe Mwigulu alisema kuna umhimu sasa wa kuhakikisha malengo yanalenga sector zinazogusa na kubadilisha maisha ya watu wachini na masikini. ‘Tumekuwa na kipindi cha kutosha kushughulikia uchumi mkubwa , tumefanikiwa sana, ila maeneo mengi sekta zilizokuwa hazigusi maisha ya mtu masikini na hazitengenezi ajira kwa watu masikini’  hivyo malengo yamekuza uchumi na kuongeza pengo kati ya watu masikini na watu matajiri.
  Ni kiu yangu kuona agenda ya baada ya 2015 inalenga kuwainua masikini kwa kulenga sekta zinazogusa maisha ya watu masikini na kutengeneza na kubooresha fursa kwenye sekta zinazogusa watu wengi. Umhimu huo pia utolewe kwenye swala la mazingira kwani mazingira yanaathiri zaidi shughuli za mtu wa hali ya chini.
  Mhe Mwigulu alisisitiza kuwa kuna uhitaji mkubwa zaidi wa kuendeleza sekta binfsi kwa kutengeneza sekta binfsi inayolenga ujasiliamali zaidi na kutengeneza elimu ya kujiajri. Kwa sasa misaada mingi inalenga elimu ya siasa na haki za binadam. “Elimu nzuri zaidi ni ya kujiajiri na haki  mhimu zaidi ni ya kuishitena maisha bora” kama tunasaidia kuelimisha uraiani tusaidie kulimisha ujasiliamali, ubunifu wa miradi, uendelezaji miradi, biashara na kutambua fursa. Misaada ilenge kutambua fursa za uzalishaji, kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji na kutambua masoko. Mhe Mwigulu alisema, soko la Ulaya limekuwa likiathiri sana mazao ya Afrika kwa bei kutokutabirika na bei kuyumba sana. Mafia makubwa yanalinda wakulima wao na yanazuia mataifa madogo kulinda wakulima wao. 
  Mataifa makubwa yanalinda mazao ya wakulima wao kwa kuwahakikishia masoko lakini yanawapambanisha na  wakulima wa mataifa madogo wasiokuwa na ruzuku ya kutosha na wanaopangiwa bei za chini kwa mazao yao. Tukiamua kuinua maisha ya mkulima masikini wa Afrika, tufute wimbo wa kushuka kwa bei za mazao yake ktk soko la Dunia huku wakulima  wa mataifa makubwa wakiwa wamepata hifadhi.
  Katika hatua nyingine Mwigulu aliitaka Jumuiya ya kimataifa kufikia mwisho kwenye Economic Partnership Agreements kwa kanda ambazo hazijakamilisha kwani limekuwa jambo la muda mrefu. Wanajua kinachokwamisha, wafike mahali wayasikilize na matakwa ya mataifa madogo kama kweli lengo la makubaliano na nia ni kuyanufaisha mataifa madogo ili yaendelee. 

  Alitambua kuwa Afrika Magharibi wamepiga hatua, lakini kwa EAC na SADC mnatambua mahitaji yetu, tusikilizeni. “there can be no celebration in reaching a deal for the sake of it and thereafter, encounter problems with its implementation”. Serikali zitapoteza mapato kutokana na kupungua au kuondolewa kwa tarrifs kuathiri   sana utoaji wa huduma kwa jamii, hivyo nivyema tukajua hizi  Economic Partnership Agreements zinachangia vipi kuyafikia Malengo ya Milenia.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akiongea katika mkutano a Mazungumzo ya usuluhishi wa mgogoro wa mpaka baina ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa yameanza leo Jijini Maputo, Msumbiji kwa kuzikutanisha pande zote mbili za mgogoro huo. 
  Mazungumzo hayo yaliyopo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chissano akisaidiwa na Mhe. Thabo Mbeki Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini na Mhe. Festus Mogae Rais Mstaafu wa Botswana yaliwapa nafasi pande zote mbili kutoa tamko rasmi kabla ya usuluhishi kuanza. 
  Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo hayo yanoyotarajia kuchukua siku mbili umeongozwa na Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Anna K. Tibaijuka, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Frederick M. Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dr. David S. Mayunga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na wataalamu wengine kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
  Aidha ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo haya umejumuisha Wabunge wawili kutoka Kanda ya Ziwa ambao ni Mhe. Kapt. John Komba na Mhe. Deo Filikunjombe.
  Hapa chini ni tamko rasmi la Tanzania Kama lilivyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe.

  0 0

  Mkurugenzi wa Heineken Tanzania Bw. Uche Unigwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mchezo wa foosball katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia kwake wamesimama washindi kutoka michuano ya mwaka jana waliopata nafasi ya kwenda Amsterdam.

  0 0

  Picha na Habari, John Nditi, Morogoro 
   LICHA ya madereva wa daladala wa Manispaa ya Morogoro kusitisha mgomo uliodumu saa 10 siku ya Jumatano , Machi 19, mwaka huu na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro , Faustine Shilogile, kusisitiza kuwa Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wataendelea kuzikamata daladala zitakazovunja sheria , baadhi ya madereva na makonda wao wamekuwa ni vichwa sugu kwa ukiukwaji wa sheria hizo. 
   Dereva na konda wa daladala lenye namba za usajili T 870 AED linalofanya kazi za kusafirisha abiria Kihonda- Mjini kwa makusudi na kiburi cha hali ya juu wamemua kuweka kituo cha kupakia abiria barabarani kabisa karibu na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwenye kona ya barabara ya zamani ya Dar es Salaam eneo lisiloruhusiwa na ni hatari kwa kuweza kusababisha ajali kwa watumiaji wengine kama inavyoonekana pichani. 
  Na huyu ni mmoja tu ya mifano hai ya ujeuri wa watu hawa. Kila mahali hali ni kama hii, na wakichukuliwa hatua huja juu na hata kugoma kutoa huduma.
   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogole , akizungumza na waandishi wa habari jana tu, mjini hapa kuhusiana na mgomo huo alisema kuwa  askari wa kikosi cha usalama barabarani wanafanya kazi zao za kukamata magari yanayokiuka sheria kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani. 
  Kamanda huyo alisisitiza kuwa askari wa Usalama Barabarani hawapo kumwonea mtu , kazi yao ni kukamata magari mabovu na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kupingwa faini kuligana na makosa yaliyojitokeza.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki akichukua Keki maalumu iliyoandaliwa katika kuukaribisha mwaka mpya 2014
   Wafanyakazi wakishiriki mchezo wa kuigiza katika sherehe hizo.Kutoka kushoto ni Bw. Renatus Sona, Bw. Prosper Mwendi na Bw. Liberatus Chonya mwenye kipasa sauti aliyekuwa MC katika shughuli hiyoa
     Mwenyekiti wa sherehe hiyo Bw. Renatus Sona akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi katika sherehe hiyo Bi. Yuster Ng’owo
   Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bw. Renatus Sona akikabidhi zawadi kwa Bw. Werrick Mushi
   Picha ya pamoja ya washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali katika Sherehe hiyo

  0 0

    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani,Mwishehe Shaban Mlawa akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.Picha zote na Othman Michuzi.
    Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akitambulishwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwidu,Mzee Mohamed Said kwa Bw. Chomiki kutoka jamii ya Wafugaji mwenye makazi katika kijiji hicho,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mzee Ally Mohamed Meta mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kampeni kwenye Kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Sam wa Ukweli akitoa burudani kwa wananchi wakazi wa kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.

  BOFYA HAPA KUONA TASWIRA MBALI MBALI

  0 0

  Two Tanzanian Doctors, Dr. Rehema Laiti and Dr Shakilu Kayungo will be the first Doctors in Tanzania to study for a newly developed Masters in Paediatric Haematology/Oncology at “MUHAS” Muhimbili University for Health and Allied Sciences.
  They have received scholarships from the Karimjee Jivanjee Foundation to fund their two years of  study including a 3 month international work experience in hospitals in Ireland. The cost of the scholarships provided by Karimjee Jivanjee Foundation is Tshs 70 million.
  Tanzania has pledged through the National Cancer Plan to make cancer care free for all patients. The Rotary Paediatric Oncology (Cancer) Ward at Muhimbili National Hospital is the only dedicated children’s cancer ward in Tanzania and all treatment is provided free of charge. The ward treats between 400-500 new cases annually. Children in Crossfire is an Irish NGO that has worked on children with cancer since 2008. 
  A new ward was completed under their supervision in 2013 and funded by Six Rotary Clubs in Dar es Salaam at a cost of US $700,000. Children in Crossfire have made significant improvements in cancer treatment by supplying drugs and training nurses. 
  An Irish children’s cancer specialist, Dr Trish Scanlan has managed the Paediatric Oncology services since 2007 and with the dedicated team of Tanzanian doctors and nurses, is responsible for increasing the long term survival rates of children with cancer from approximately 5% to 40-50%.
  Mr Hatim Karimjee, Chairman of Karimjee Jivanjee Foundation, said “It is now time for us to train Tanzanian doctors in this specialised field of Paediatric Oncology, and that is why we have agreed to provide scholarships to two Doctors”. Dr Trish Scanlan said that “The foundation for long term sustainability in clinical services is the establishment of local capacity in treating children with cancer. This requires qualified Tanzanian doctors working in hospitals around the country”.
  Currently Tanzania does not have a single qualified Paediatric Oncologist apart from Dr Trish Scanlan. Doctors Dr Rehema Laiti and Dr Shakilu Kayungo are expected to be the first Tanzanian Paediatric Oncologists. 

  The Karimjee Jivanjee Foundation is a charitable foundation established by the Karimjee family. It provides funding for enhancing Education in Tanzania. This is achieved by providing scholarships to Tanzanians to study at graduate and post graduate level in Tanzania. 
  The Karimjee Foundation currently has 50 scholars studying in Tanzania.  

  0 0

  Na Fakih Mapondela wa Tabora Police Press
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan S. Kaganda Alhamisi  tarehe 20/03/2014 alifanya ziara katika manispaa ya Tabora na kukutana na kikundi shirikishi (Sungusungu) na kukipatia mafunzo mbalimbali ya ulinzi shirikishi na ukamataji salama wa watuhumiwa pamoja na kukipa somo la dhana ya Polisi jamii.
  Kamanda Kaganda akiwa katikati ya Sungusungu kuonesha mbinu bora za ukamataji salama wa watuhumiwa
  Kamanda Kaganda akiwa katika harakati za kutoa somo la dhana ya polisi jamii
  Hapa Kamanda Kaganda anajumuika kucheza ngoma na Sungusungu hao
  Baada ya shamrashamra Sungusungu wote na wananchi wanakaa chini kumsikiliza Kamanda Kaganda
  Wake kwa waume wakimsikiliza Kamanda Kaganda ambaye ameleta muamko mkubwa wa ulinzi shirikishi kwa wananchi wa mkoa wa Tabora
  Juu na chini Kamanda Kaganda akihutubia wananchi wa mkoa wa Tabora ikiwa ni pamoja na mafunzo mbalimbali ya ulinzi shirikishi na ukamataji salama wa watuhumiwa pamoja na kukipa somo la dhana ya Polisi jamii.
  0 0
 • 03/20/14--15:11: Camera zinauzwa
 • Zimewasili juzi kutoka Ujerumani  kwa mahitajio yako ya NIKON D40X,D40, D60, D70 , na D3000 na Nikkor AF-S 18-55G

  Kwa mahitajio ya aina yeyote yale ya camera hizi za NIKON, tafadhali sana wasiliana na mimi DULLA, kwa simu kwa namba hii   065 331 21 86
  Dar er salaam.

  0 0
 • 03/20/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Malika anakupa 'Vidonge'

  0 0

  Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa  ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma  huku  akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, leo Ijumaa, Machi 21, 2014.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la  ya Kanuni za Bunge Maalum. PICHA NA IKULU.

  0 0

   Pichani ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Deos Mndeme akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar mapema leo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania.
  Pichani Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara,Bwa.Fortunatus Kapinga akifafanua jambo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.Amesema kuwa Shirika la Posta limeanza utekelezaji mpango kabambe wa miaka kumi (2014-2023) ikiwa ni dira na mwelekeo wa kuliongoza shirika hilo liweze kujiendesha kibiashara,kubuni na kutoa huduma mbadala,kutumia teknolojia maridhawa na kukidhi mahitaji ya soko la huduma za mawasiliano jumuishi.Kushoto kwake ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Deos Mndeme.
   Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Elias Madule akifuatilia mkutano huo akiwa sambamba na mdau mwingine wa shirika hilo la Posta.
   Waandishi wa Habari wakisikiliza taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Viongozi wakuu wa Shirika hilo,katika mkutano uliofanyika mapema leo,ndani ya Makao makuu ya Ofisi hizo.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa Fortis Insurance Brokers Ltd , Bi Maryam Shamo.( wa pili Kulia) akimkabidhi Mshindi wa mwanamakuka 2014‎, nyaraka zake za Bima. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hio.
  Mshindi wa Mwanamakuka 2014, Bi Leyla Mwambungu, baada ya kujinyakulia Tuzo ya Million Tatu, kweye Tuzo za Mwanamakuka Awards, ambazo zinaandaliwa na Unity Of Women Friends. Fortis Insurance Brokers Ltd, Imeamua kulinda Biashara yake Kuwa kwa kumkatia Bima ya Moto Na Wizi, Ili Biashara yake isije ikatetereka atakapopata majanga hayo.

  0 0

  Bw. Sultan A. Sultan akitoa mada wakati wa kongamano la viongozi lililojadili mada kuu isemayo ‘Rasilimali za Taifa kwa amani na Maendeleo, Bagamoyo , Pwani  tarehe 20 Machi,2014.
  =====  ====== =====
  Zipo fursa nyingi kwenye uchumi wa gesi- Sultan
  Na Malik Munisi, Bagamoyo.

  Watanzania wameaswa kutambua fursa zitokanazo na rasilimali zinazogunduliwa nchini ili waweze kunufaika kutokana na uwepo wa rasilimali hizo.

  Hayo yamebainishwa na Bwana Sultan Sultani mkazi wa kilwa alipokuwa akitoa mada juu ya ‘‘Ushiriki wa wenyeji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia’’, katika Kongamano la Viongozi lililojadili mada kuhusu  “Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania” lililofanyika Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

  Bw. Sultani alieleza kuwa, wananchi wanatakiwa kuelewa fursa mbadala zipatikanazo kutokana na uwepo wa rasilimali za gesi na mafuta nchini zikiwemo ununuzi wa hisa  kwa makampuni makubwa ili kuwawezesha kuongeza  mtaji yao  ambapo faida yake itapatikana mara tu baada ya gesi kuanza kuuzwa.

  Aidha, alitaja fursa nyingine kuwa ni uwezekano wa uhitaji mkubwa wa majengo na maghala yatakayohitajika kwa ajili ya kutunza vifaa na pembejeo muhimu kwa ajili ya utafutaji na uzalishaji wa gesi katika maeneo yaliyoko baharini.

  Alizitaja fursa nyingine kuwa ni pamoja na makampuni ya ulinzi, kampuni za usafirishaji, maabara, vyuo maalumu vya kuelimisha umma katika tasnia ya petroli na nyanja zake, makampuni ya kutunza mazingira, usalama na afya, na kuongeza kuwa  hizo ni baadhi tu ya fursa zitokanazo na uwepo wa rasilimali gesi na mafuta nchini.
    
  Pamoja na hayo, alieleza uwekezaji katika mafuta na gesi si bahati nasibu ya kutoa moja ukapata milioni moja bali ni ile ya kutoa mamilioni kama sio mabilioni na kisha ukaambulia patupu. Hivyo, alisisitiza kuwa, mifano ipo ya watu walionunua leseni za utafiti kwa kuwekeza mabilioni wakaishaia kukosa na matokeo yake wakapoteza maisha kwa maradhi ya moyo au msongo wa mawazo.

  “Pamoja na kuwa sayansi ya hali ya juu kutumika katika utafiti wa mafuta na gesi, bado kwa kiasi kikubwa ugunduzi wa rasilimali hizi ni wa pata potea huku uwekezaji wake ukiwa ni wa ghali sana” aliongeza Sultan.

  Alisisitiza kuwa, yapo makampuni mbalimbali yaliyofika nchini ili kuwekeza katika maeneo ya Songosongo (Lindi) na Msimbati (Mtwara) ambapo mengi yaliingia kwa kifua mbele lakini yakatokea kwa mlango wa nyuma kutokana na ugumu wa kazi hiyo na kufanya utafiti bila ya mafanikio.

  Mwisho Sultan alihimiza umuhimu wa wananchi kuelezwa mapema ugumu na pata potea iliyopo katika sekta ya mafuta na gesi  ili wananchi waweze kuzitambua fursa na  kujihusisha katika kuanzisha biashara katika maeneo mbalimbali ili waweze kutoa huduma kwa wawekezaji wanaofanya utafiti na wale wanaoendelea na shughuli za uchimbaji wa gesi asilia, ikiwemo  elimu ya soko la hisa ili iweze kuwasaidia wananchi kuwekeza katika makampuni ya mafuta katika namna ambayo itawanufaisha.

  0 0

  KIKOSI KAZI KUSHUGHULIKIA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB zimeunda kikosi kazi (task force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi za elektroniki ambayo yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza.

  TFF na CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya uboreshaji matumizi ya mfumo huo.

  Kikosi kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.

  Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao akiongoza timu yake.

  Malinzi amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.

  YANGA, RHINO KUCHEZA TABORA VPL
  Yanga inaumana na Rhino Rangers katika moja kati ya mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa wikiendi hii katika miji miwili tofauti.

  Mechi hiyo itafanyika kesho (Machi 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora ambapo kiingilio kitakuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 3,000 mzunguko.

  Nayo JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika mechi itakayochezwa kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

  Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Jumapili) kwa mechi nne ambapo Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mechi hizo mbili zitakuwa ‘live’ kupitia Azam Tv.

  Mechi nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer
  Tanzania Football Federation (TFF)

older | 1 | .... | 394 | 395 | (Page 396) | 397 | 398 | .... | 3272 | newer