Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 393 | 394 | (Page 395) | 396 | 397 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ilipopambana na Azam  FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. 

  Heka heka: Golikipa wa timu ya Azam FC, Aishi Salum akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
  Mfungaji wa bao la Yanga, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Azam FC.
  Beki wa Azam FC, Gadiel Michael akimiliki mpira (kushoto) akiwania mpira huo ni mshambuliaji wa yanga, Hamis Kiiza. 
  Mashabiki wa Yanga, wakishuhudia pambano hilo.
  Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Azam FC, Bolou Michael. Picha na Francis Dande

  0 0

  NAIBU Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Abdurahman Kaniki, ameipa changamoto bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kuhakikisha majengo yanayojengwa nchini yanakuwa bora na salama kwa makazi ya watu na kuepusha majanga ya majengo kuporomoka kama ilivyowahi kutokea. 
  Naibu IGP Alitoa changamoto hiyo jana jijini Mbeya wakati akifungua mkutano wa mashauriano baina ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu (DPP) na maofisa wa AQRB, kuhusu masuala mbali yanayohusu ujenzi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kitaaluma lengo ikiwa ni kuboresha huduma. 
  “Tumeshuhudia majengo yakiporomoka hivi karibuni na tunajiuliza je ni kweli wataalamu wa kutosha hakuna ? lakini jibu ni kwamba wapo, sasa kinachotakiwa ni usimamizi wa karibu kuhakikisha tunawapa watanzania makazi bora na salama,” alisema. 
  Alisema utaratibu wa AQRB kukutana na wadau na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya ujenzi na sheria ya ujenzi namba 4 ya mwaka 2010 imekuja wakati mwafaka lakini alishauri wapanue fursa hiyo ili kuwafikia wadau wengi zaidi. 
  “Nyie ni wadau muhimu sana kupendezesha miji yetu ambayo kwa kweli mingine imejengwa holela holela …..hii changamoto naileta kwenu mhakikishe mambo yanafanyika kisasa, hata sisi polisi milango iko wazi kwa chochote mnachohitaji kwa ajili ya kuboresha kazi zenu,” alisema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Ambwene Mwakyusa, alisema bodi hiyo ilianza shughuli zake mwaka 1998 na imeshakagua miradi ipatayo 14,000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini. 
  Alisema katika shughuli za ukaguzi ambazo bodi huzifanya kwenye kanda zake mbalimbali wamekuwa wakilishirikisha Jeshi la Polisi ili wanapopata tatizo wakiwa kazini wasaidiwe. 
  Mwenyekiti huyo wa bodi alimwomba Naibu IGP kusaidia kuhakikisha wabunifu na wakadiriaji majenzi walioko ndani ya jeshi hilo wanasajiliwa na bodi yake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria. 
  Msajili wa bodi hiyo, Jehad Ahmed Jehad, alisema kupitia sheria ya AQRB wamekuwa wakibuni mikakati mbalimbali ya kuhakikisha shughuli za ubunifu na ukadiriaji zinafanyika kwa weredi wa hali ya juu. 
  Alisema bodi yake imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali za serikali kama ya wakandarasi, wahandisi na wakala wa majengo ili kuwezesha majengo yanayojengwa yanakuwa bora na salama kwa wananchi.
   Washiriki wa semina wakimsikiliza Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Abdurahman Kaniki akihutubia mkutano wa mashauriano baina ya maofisa wa polisi, maofisa wa ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu (DPP) na wataalamu wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) uliofanyika jijini Mbeya 

   Mwenyekiti wa bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Ambwene Mwakyusa akizungumza kwenye mkutano baina ya viongozi wa Jeshi la Polisi, Maofisa kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu (DPP) na maofisa wa bodi hiyo uliofanyika Mbeya jana, pembeni yake kulia ni Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Abdalah Jehad na kushoto  ni Naibu IGP, Abdurahman Kaniki.
  3: Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Abdurahman Kaniki akizungumza kwenye mkutano wa mashauriano baina ya viongozi wa Jeshi la Polisi, maofisa kutoka ofisi ya DPP  na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB),jijini Mbeya. Kulia wa kwanza ni Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Abdalah Jehad na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.
  Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Abdurahman Kaniki akizungumza kwenye mkutano wa mashauriano baina ya viongozi wa polisi na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB),jijini Mbeya. Kulia wa kwanza ni Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Abdalah Jehad na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.

  0 0

  Uzinduzi wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2014 utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi 2014 saa 5.00 kamili asubuhi katika hotel ya JB Belmont ukumbi wa Savannah jijini Dar es salaam.

  Awali uzinduzi huu ulikuwa ufanyike sambamba na semina ya mawakala, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, imebidi semina isogezwe mbele hadi tarehe 25 Machi 2014. 

   Mawakala waliopo jijini Dar es salaam  na wale wenye nafasi mnakaribishwa kuhudhuria uzinduzi huu. 

  Natanguliza shukrani. 
   HIDAN .O. RICCO. 
  PRO Redds Miss Tanzania

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza wakati akifungua warsha kwa wataalamu wa kilimo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo. 
  Mwezeshaji kutoka shirika ka TAHA Bw. Isaac Ndamanhyilu akizungumza kwenye warsha hiyo. 
  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wataalamu wa kilimo wa kata na vijiji vya wilaya ya Makete. 
  Wataalamu wakifuatilia mafunzo hayo. 
   Mwezeshaji Manfred Bitala akiwawezesha washiriki wa warsha hiyo.
  Na Edwin Moshi, Globu ya jamii Makete
  Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imedhamiria kuinua kilimo cha matofaa maarufu kama apples, ili kiweze kuinua uchumi wa wakulima pamoja na wilaya kwa ujumla

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema wilaya imeanza kutekeleza agizo la rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara wilayani hapo kuwa ni lazima kilimo cha apple kiwe cha biashara wilayani Makete

  Mh. Matiro amesema mafunzo watakayopatiwa maafisa hao wa kilimo, wanatakiwa kuyafuata na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kata na vijiji vyao ili mabadiliko yaanze kuonekana na ndiyo maana halmashauri imeshirikiana na shirika la TAHA kuwapatia mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo hicho katika maeneo wanayotoka

  Amesema kwa kuwa jambo hili halihitaji masihara anatarajia kuona mabadiliko mara moja pindi mafunzo hayo yatakapo malizika kwa kwenda kuwaelekeza wakulima kitu cha kufanya ili apples zizalishwe kwa wingi na kwa ubora unaohitajika kwani hilo linawezekana kwa mujibu wa utafiti ambao umefanyika wilayani hapo

  Mh. Matiro amesisitiza pia badala ya wananchi kupanda miti mingi ya mbao kwa sasa wanatakiwa wabadilike na wapande miti ya matunda hasa apples kwa kufuata elimu ya wataalamu hao wa kilimo ambayo wamepatiwa katika mafunzo hayo 

  Kwa upande wake Bw. Isaac Ndamanhyilu kutoka shirika la Tanzania Hoticultural Association maarufu kama TAHA ambao ni watoaji wa mafunzo hayo, amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza uzalishaji wa apples pamoja na uuzaji wa matunda hayo

  Amesema kwa wilaya ya Makete imekuwa ikizalisha matunda hayo kwa wingi lakini hakuna kumbukumbu zinazoonesha kama uzalishaji huo upo Makete, na pia hakuna taarifa zinazoonesha kama wilaya hii ni miongoni mwa maeneo ndani ya Tanzania yanayozalisha apples

  Bw. Ndamanhyilu amesema kufuatia kukosekana kwa kumbukumbu hizo, ndiyo maana wameamua kushirikiana na halmashauri kuhakikisha elimu inatolewa kwa mabwana shamba na mabibi shamba na wao wawaongoze wakulima kulima kilimo cha kisasa ili matunda hayo yazalishwe kwa wingi na yenye ubora unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa

  "Kulikuwa kuna maonesho fulani jijini Arusha, na mgeni rasmi alikuwa Rais Kikwete na alibahatika kuona apples pale, na alipoambiwa kuwa zinazalishwa Makete kwa kweli alishangaa, na ndiyo maana alisema atafika Makete kujionea, na kweli alifika na amesisitiza kilimo hiki kiwe cha biashara na ndio maana tunatoa hii elimu kwenu" alisema

  Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amewaasa mabwana na mabibi shamba hao kubadilika kwani wapo baadhi ya wataalamu hao wamekuwa wakihubiri elimu bila kufanya kwa vitendo jambo linalowakatisha tamaa wakulima

  "Yaani wakati mwingine ukiliangalia shamba la mabwana na mabibi shamba nia aibu, yaani unakuta shamba la mkulima linaubora kuliko la ninyi wataalam, sasa hii inakatisha tamaa, lazima ninyi muwe mfano wa kuigwa" alisema Bitala

  Amesema wao wananafasi kubwa ya kuibadilisha hii nchi kutoka hapa ilipo na kuonekana mabadiliko makubwa na yenye tija katika sekta ya kilimo kama kila mmoja ataamua kufanya kazi yake ipasavyo

  Katika mafunzo hayo wamefundishwa mambo mengi ikiwemo dalili na aina za magonjwa yanayoshambulia matunda, na namna ya kulima na kupata mazao mazuri zaidi ya ilivyo sasa

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Sweden HRH Crown Princess Victoria Lugrid Alice Desiree alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Mach 19, 2014
  Princess Victoria, ambaye ameambatana na Waziri wa Biashara wa Sweden. Bi Ewa Björling, yuko nchini kwa ziara ya siku tatu.

  0 0

  Watu wawili wamefariki dunia leo baada ya bodaboda yenye usajili namba T 293 ARM kugongwa na basi la abiria la kampuni ya Maning Nice lenye usajili namba T624 CQD ambalo nalo lilipinduka baada ya ajali hiyo katika kijiji cha Ngongo mkoani Lindi  na abiria saba walijeruhiwa. Majina ya marehemu na ya majeruhi hayakuweza kupatikana mara moja. Picha na Abdulaziz Video.

  0 0

  Habari na picha na John Nditi, Morogoro
  Kuanzia aljafiri leo, madereva wa daladala wanaoendesha magari yao ya abiria katika njiaa mbalimbali za Manispaa ya Morogoro waligoma kutoka huduma hiyo kwa muda wa saa 10 wakishinikisha kutendewa haki ya Kikosi cha Usalama Barabarani. 
   Madereva hao kwa umoja wao Machi 18, mwaka huu walipomaliza kazi yao usiku , walikubaliana kutoamsha magari yao siku inayofuatia kutoa madai ya kuyanyaswa na Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kwa kutozwa faini kubwa pasipo kuwa na makosa ya msingi. 
    Kufuatia mgomo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amewataka madereva wa daladala waliogoma kusafirisha abiria katika Manispaa ya Morogoro kusitisha mara moja mgomo wao na kurejea kazini. 
   “ Leo asubuhi kumekuwa na mgomo wa daladala za mjini Morogoro , wao wanawalalamikia askari wa Usalama Barabarani kwa kuwa wanawapiga faini kubwa kutokana na makosa ya magari barabarani” alisema Kamanda Shilogile.
  Akielezea kiini cha mgomo huo. Hata hivyo alisema haikuwa sahihi kwa wao kufikia hatua ya kugoma kuwa vile jambo hilo lilikuwa linazungumzika kwa kukutana kwa pamoja kupitia uongozi wao , uongozi wa Polisi na wa wilaya ili kujadili kile ambacho wanaona kinakwenda tofauti na utaratibu wa kisheria za usalama barabarani. 
   Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Polisi wa Kikiso cha Uslama Barabarani wapo kwa ajili ya kudhibiti ajari za baranarani na kuhakikisha magari ya nayofanya kazi za usairishaji ni mazima na si mabovu. 
   “ Askari wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo za usalama barabarani...hawapo kumwonea mtu , kazi yao ni kukamata magari mabovu na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kupingwa faini kuligana na makosa yaliyojitokeza” alisema Kamanda Shilogile. 
  Hivyo alisema magari mazima ambayo yamekidhi vigezo vya usafirishaji ndiyo yanatakiwa kuwepo barabarani, hivyo Jeshi hilo halitasita kuyakamata yale ambavyo hayajakidhi vigezo hivyo kwa kusingizio cha kuonewa. 
   Kamanda huyo aliwataka madereva ambao wanaona magari yao ni mazima na wanaonewa na Askari wa Usalama Barabarani wanao wajibu wa kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi wa Jeshi hilo ili yafanyiwe kazi . 
   Hivyo alisema , pale watakapobani kuna ukiukwaji wa utaritu na sheria kwa upande wa Askari hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa askari kulingana na kanuni za jeshi la Polisi nchini. Hivi alisistiza kuwa , kama magari yao ni mabovu na yanafanya kazi za kusafirisha abiria , ni wajibu wa Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kuyakamata na kuyapiga faini bila ya kumwonea mtu. Kutokana na mgomo huo wa muda ,viongozi wa chama cha madereva wa daladala, Uongozi wa Serikali ya Wilaya , Sumatra pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro walikuwa na kikao cha pamoja kwenye Ofisi y Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kulipatia ufumbuzi wa suala hilo. 
   Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiwemo na wanafunzi walilazimika kutumia usafiri wa magari madogo ya wazi ‘ Suzuki’ na wengine kupanda Pikipiki’ Bodaboda’ na kila aina ya usafiri ili kuwahi kwenye shughuli zao. 
  Mbali na kundi hilo kutumia usafiri wa aina hiyo, wananchi wengine waliamua kutembea kwa miguu wakiwemo wanafunzi , ambapo wenye magari madogo walionekana kufurahia hali hiyo wakisema wamejipatia kipato kizuri za kuendesha maisha yao kwa siku hiyo. 
   Hata hivyo baada ya mazungumzo ya pande hizo , madereva hao walirejea barabarani kuanzia saa kumi jioni ya Machi 19, mwaka huu kuendelea na kazi ya usafirishaji wa abiria
  Kufa kufaana. Magari madogo yakisanya baada ya daladala kutokewa barabari kufuatia mgomo huo

  Kila aina ya usafiri ulitumika
  Wengi waliamua kutembea
  Wanafunzi katika lori
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana akimuinua Mkono Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakiwapungia mkono wananchi wa Jimbo la Chalinze na WanaCCM waliofika kwa wingi kwenye Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani.


  0 0
 • 03/19/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • 'Sabah al kheir mpenzi'

  0 0

  Mlioko huku wote ma-Bebi...tehe tehe tehe....Inasemekana wazee wa Chalinze wamekata rufaa kutaka mpaka uwe Morogoro....

  0 0

  Meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd,s Miss Tanzania 2014kulia ni   mkurugenzi wa kamåuni ya LINO International Hashi Lundenga ambao ni waandaaji wa mashindano hayo na kushoto ni  Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
   Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
   Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.
   Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.

  0 0

   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo.
   Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa fulana nyeusi) akihoji uimara wa sehemu ya kutulia ndege wakati walipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
   Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mhandisi Mugasa Mlondo akitoa maelezo juu uimara na ubora wa uwanja wake wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo. Picha na Saidi Mkabakuli.

  ========  =========  ======
  UWANJA WA NDEGE MTWARA KUIMARISHWA ZAIDI

  Na Saidi Mkabakuli.

  Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani humo, hali inayochochea mahitaji makubwa ya kuutumia uwanja huo.

  Hayo yamebainishwa mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja wa huo.

  Bibi Mwanri alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini na mikakati mbalimbali itakayopelekea kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara ili kuweza kuhudumia uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi mkoani humo. Aliongeza: “Tathmini ya awali inaonesha kuwa miradi mingi ipo mkoani Mtwara kufuatia kugundulika kwa gesi hivyo kuna haja ya dhati ya kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara kwa lengo la kutoa huduma za uhakika wakati huu wa mfumuko wa kiuchumi mkoani Mtwara,” alisema Bibi Mwanri.

  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye alikuwa kiongozi mwenza wa ukaguzi, alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika uwanja huo ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia wawekezaji wengi kuendelea kumiminika na kuwekeza mkoani humo.

  “Uwanja wa ndege wa Mtwara una fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hakika ni lango la biashara hasa kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara, hivyo uendelezaji wa uwanja huu ni jambo lisilo epukika,” alisema Prof. Rutasitara.
  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.
  Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
  Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  0 0


  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
   Bi Severa joseph akitoa maelezo ya aina ya dawa zinazotumika kwa akina mama wajawazito katika kituo cha afya Kaloleni cha jijini arusha kwa baadhi ya washiriki wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani.
  Dr Anna Kimaro mganga wa zamu wa kituo cha afya Kaloleni aliyebeba faili kwapani akiwa na wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani YWCA walipo tembelea katika kituo hicho jijini arusha.
   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha wakipata maelezo ya kina kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa kituo hicho.

  0 0

  • CCM bado inaamini katika Muundo wa Serikali mbili
  • CCM ina amini Muungano huu muhimu unadumishwa na kuimarishwa
  • Muundo tulionao uboreshwe
  • Tutangulize mbele Uzalendo na maslahi ya kweli ya nchi yetu.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti CCM Makao Makuu Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo alizungumzia imani ya CCM katika muundo wa serikali mbili.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza  baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Lumumba jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Machi 2014.
  ========  ======  =======
  Juzi tarehe 18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba rasimu ya pili ya katiba.

  Toka awasilishe rasimu ile bungeni , kumekuwa na maombi mengi sana ya kutaka kujua kama msimamo wa CCM juu ya baadhi ya mambo hasa muundo wa muungano bado ni uleule.

  Kwasababu ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara nyingine tena msimamo na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na muundo wake.

  Kimsingi CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

  Bado CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano tulionao wa serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora kwasasa utakao dumisha muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.

  Kwakuwa kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa kazi yao ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume sio mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu nyingine ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa mapungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa.

  Mwanzo wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli yaliyomo kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana akisi maoni ya Watanzania walio wengi.

  CCM   ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa zinahusisha wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na hatimaye itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao, zitatumika vizuri kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo na sio maoni au matakwa ya wachache.

  Wakati haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia pekee kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili ujibu vizuri zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi mazingira ya sasa.

  Tunawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hiki. Ni vizuri Watanzania tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza mbele uzalendo na masilahi ya kweli ya nchi yetu.
  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

  Imetolewa na;-
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa Itikadi na Uenezi

  0 0  0 0

   Hili ni ghorofa la chuo kikuu UDOM alipojirusha mwanafunzi huyo toka ghorofa ya pili.
  Muonekano wa ghorofa hilo alipojirusha mwanafunzi huyo.
  ======  ====  ====
  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.

  Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.

  Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote  kujibu shitaka la kujaribu kujiua.

  0 0


  Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Pamoja nae ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima. 
   *********
   1.0     UTANGULIZI

   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu makuu mawili; kwanza ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa ajili ya masomo ya Shahada au Stashahada ya juu. 
  Jukumu la pili ni kukusanya marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994.

  2.0        UTOAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
   Tangu kuanzishwa kwake, Bodi imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa. Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa mikopo kwa Wanafunzi 42,729 wa elimu ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni 56.1.

  Idadi ya Wanafunzi wa elimu ya juu wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka kutoka  wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi Wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013. Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4% kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.

  Kwa mwaka wa masomo 2013/2014, jumla ya wanafunzi 95,178 wamenufaika na mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi cha TZS 223,977,042,853.00 imekwishalipwa.
  Mwaka
  Idadi ya Wanafunzi Waliokopeshwa
  Ongezeko
  (%)
  Kiasi kilichoko-peshwa
  (Tshs Bilioni)
  Ongezeko
  (%)
  2004/05 (Na Wizara)

  16,345

  -

  9.9

  -
  2005/2006
  42,729
  161.4
  56.1
  467
  2006/2007
  47,554
  11.3
  76.1
  35.7
  2007/2008 
  55,687
  17.1
  110.8
  45.6
  2008/2009
  58,798
  5.6
  139.0

  25.5
  2009/2010
  72,035
  18.4
  237.8
  28.7
  2010/2011
  92,791
  28.8
  230.0
  24.5
  2011/2012
  94,533
  2.0
  311
  35.0
  2012/2013
  97,348
  2.9
  335.2
  7.2

  0 0

  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule, (aliyeshika vitabu) akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo tofauti tofauti kutoka kampuni ya  simu ya Airtel jana. katikati ni Ofisa Masoko wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Mbeya Priscus Kimario.  
   Ofisa Masoko wa kampuni ya simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga, akionesha vitabu kabla ya kumkabidhi mkuu wa shule ya Sekondari ya  Mbeya, Magreth Haule (kushoto) wakati walipofika shuleni hapo kutoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
   Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa shule hiyo  kwa maofisa wa kampuni ya Simu ya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu zaidi ya 200 vya masomo tofauti tofauti kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne jana. (katikati) ni Ofisa Masoko wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Mbeya Priscus Kimario.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule (kushoto) akikabidhiwa msaada wa Vitabu vya masomo tofauti tofauti jana kutoka kwa Ofisa Masoko wa kampuni ya simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga, (katikati) vitabu hivyo vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo.
   ========  ======  =======
  AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI MBEYA

  Kampuni ya simu ya Airtel chini ya mradi wa shule yetu imetoa msaada wa vitabu  vyenye thamani ya takriban shilingi milioni 2 kwa shule ya sekondari ya Mbeya.

  Makadhiano ya vitabu yameshuhudiwa na jumuiya nzima ya Shule yenye zaidi ya watu takribani 1365 wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine waliokusanyika kwa shauku ya kupokea vitabu hivyo ikichagizwa na kauli mbiu ya Airtel Baba lao.

  Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Jonas Mmbaga amesema “lengo la kutoa msaada huo ni kutekeleza azma ya kuendeleza ushirikiano na jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kukuza taaluma mashuleni. Chini ya mpango wa shule yetu tumeweza kuzifikia shule mbalimbali nchini na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari mbeya.

  Mbaga alisema Vitabu hivi ni vya masomo ya sayansi vikiwemo vya Hisabati, Kemia, Fizikia, na Biolojia, kwa ajili ya  kidato cha kwanza hadi cha nne. Na tumeichagua shule ya Sekondari Mbeya ili kuwakilisha shule nyingine zilizopo mkoani Mbeya.

  “Tunaahidi kuendelea kuzifikia shule nyingi zaidi mkoani hapa na mikoa ya jirani kupitia mpango wetu maalum wa shule yetu ambao ni endelevu uliodumu zaidi ya miaka 7 mpaka sasa.  Tuaamini kwa kujikita kwenye sekta ya elimu tunaendeleza ushirikaino wetu na serikali chini ya wizara ya elimu kusaidia kutatua changamoto zilizopo husasani ya vitabu mashuleni na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini”.aliongoza Mmbaga

  Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbeya Bi Magreth Haule alisema” Nawashukuru sana Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa shuleni hapa huu ni uthibitisho kuwa Airtel wapo karibu na jamii hasa katika kuendeleza sekta ya elimu. Msaada huu ni mchango mkubwa na ni changamoto kwa wanafunzi na walimu kuongeza juhudi katika kuhakikisha tunakuza kiwango cha elimu shuleni hapa. Tunaahidi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa manufaa ya wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla

  Nao Wanafunzi  Revina Florence, Denis Michael na Happy Mwaisengela kwa nyakati tofauti na kwa niaba ya wenzao wameipomgeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na kwamba vitabu hivyo vitachochea hamasa za wanafunzi kuongeza bidii katika masomo ili kufikia lengo lililokusudiwa.

  Vitabu hivyo ni mwendelezo wa shughuli za huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya ada na kiada, mpaka sasa shule zaidi ya 900 zimeshafaidika na mpango huu.

older | 1 | .... | 393 | 394 | (Page 395) | 396 | 397 | .... | 3284 | newer