Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Bodi ya Filamu yatathmini maendeleo ya tasnia ya Filamu

0
0
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana Bodi ya Filamu kuanzia miaka ya 1930 hadi sasa, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Consilia Niyibitanga.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo akionyesha moja ya picha zinazotolewa na wadau wa filamu kama matangazo ya kutambulisha filamu zao sokoni, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Consilia Niyibitanga. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalilini, WHVUM

WAZIRI WA MAJI JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA KWADELO WILAYA YA KONDOA

0
0
 Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi kisma cha bomba la maji katika kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa Machi 20, 2014 sambamba na maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji dunia ambapo kitaifa yana fanyikia Mkoani Dodoma (kulia kwake), Mbunge wa Jimbo la Kaskazini Kondoa Mhe: Zabeini Mhita. kauli mbiu ni uhakika wa maji na nishati.
 Profesa.Jumanne Maghembe akipanda mti baada ya kuzindua mradi wa maji.
 Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Kwadelo Bi.Hawa Athuman baada ya kuzindua rasmi kisima cha bomba la maji.
 Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Enjinia Bashir Mrindoko wakihutubia wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa sambamba na maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji dunia ambapo kitaifa yana fanyikia Mkoani Dodoma
 wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa mji.
 wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa mji.

KIFUA KIKUU NI UGONJWA WA TATU UNAOSABABISHA VIFO VYA WATU WENGI HAPA NCHINI.

0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa  wa kifua kikuu   kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsilikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu   kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo 
  Meneja Mpango  wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma, Dk. Beatrice Mutayoba wa kwanza kulia , katikati ni Naibu Meneja wa  mpango  huo, kushoto ni Afisa wa mpango huo Dk.Deus Kamara wote  kutoka Dodoma.Picha na Magreth Kinabo -Maelezo
========  ======  =======
Na Magreth Kinabo-
 
Imeelezwa kuwa ugonjwa wa kifua kikuu  ni ugonjwa wa tatu ambao unasababisha vifo vya watu wengi hapa nchini  baada ya Malaria na Ukimwi.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa huo kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma, ambayo itaandhimishwa Machi 24, mwaka 2014 hapa nchini na nchi nyingine  duniani .

Aidha  kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo zinaonesha kuwa  idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo imeongezeka kutoka 11,000 mwaka 1980  hadi kufikia 63,892 mwaka 2012. “ Utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu vya watu walioathirika na ukimwi vinatokana na kiifua kikuu.

“Tangu kuzuka kwa ukimwi hapa nchini ,inakadriwa kuwa  asilimia10 ya waathirika wa ukimwi wana ugonjwa wa kifua kikuu na takribani asilimia 40 ya wagonjwa wa kifua kikuu wana maambukizo ya VVU. Hali hii inafanya kifua kikuu kuwa miongoni mwa changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ukimwi na katika vita vya kutokomeza umasikini hapa nchini,” alisema Dk. Rashid.

 Dk. Rashid   aliongeza kuwa  miongoni mwa sababu nyingine zinazochangia kuongezeka kwa idadi ni msongamano wa watu mijini, makazi duni  ya watu na wagonjwa kuchelewa kupata matibabu.Aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu “ Fikia  kila mtu Gundua .Tibu na Ponya mgonjwa wa TB” .

 Aliongeza kuwa sasa  takribani zaidi ya watu milioni mbili  hufariki kwa ugonjwa huo kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo hutokwa Barani Afrika hususa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hivyo Tanzania ni nchi ya 14 kati ya nchi 22 zenye idadi kubwa  ya wagonjwa wa  ugonjwa huo duniani.

 Alisema  miongoni mwa mikoa inayoongoza kuwa na  wagonjwa wapya  wengi  kwa takwimu za mwaka 2012  kati ya mikoa iliyoathirika kwa tatizo hilo ni Dares Salaam 13,983,Mwanza 5,946 na Shinyanga 4,074.
 

MAADHIMISHO YA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI KUFANYIKA MACHI 23, 2014.

RAIS KIKWETE AKILIHUTUBIA LIVE BUNGE MAALUM LA KATIBA HIVI SASA MJINI DODOMA

TASWIRAZZZ JIONI YA LEO MAENEO YA KIWANGWA,BAGAMOYO

0
0
 Kamera ya Globu ya Jamii,imefanikiwa kuzinasa taswirazz hizi jioni ya leo katika mji wa Kiwangwa,Bagamoyo Mkoani Pwani.

MKUU WA WILAYA YA NKASI AFUNGUA RASMI KAMPENI YA TOHARA KWA WANAUME MKOANI RUKWA LEO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014 Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000 wameshafanyiwa tohara.  

Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583 wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.

Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi  pamoja na kusaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa wanaume husaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%. 
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha (watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya (wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

Binti Mfalme wa Sweden aendelea na ziara yake nchini

0
0
Binti Mfalme wa Sweden, Mtukufu Victoria Lugrid Alice Desiree akisalimiana na mmoja wa Maafisa waliompokea alipotembelea Mradi wa Maji wa WaterAid unaofadhiliwa na nchi yake uliopo Kigamboni eneo la Tungi, Wilayani Temeke, Dar es Salaam. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Bi. Sofia Mjema. Mtukufu Victoria alitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 19 hadi 21 Machi, 2014.
Mmoja wa Vijana wa skauti akimvisha skafu Mtukufu Victoria alipowasili katika eneo hilo.
Mtukufu Victoria akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika eneo laTungi- Kigamboni Wilayani Temeke kwa ajili ya kuangalia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Sweden.
Mtukufu Victoria akifurahia mapokezi kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungi huko Kigamboni.
Mtukufu Victoria katika matukio ya uzinduzi wa miradi huko Kigamboni eneo la Tungi
Mtukufu Victoria akizindua huduma ya maji  safi ya bomba katika eneo la Tungi
Mtukufu Victoria akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungi (hawapo pichani) alipotembelea shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungi wakimsikiliza Mtukufu Victoria (hayupo pichani)

 ...Binti Mfalme akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa kuondoka nchini

Binti Mfalme wa Sweden, Mtukufu Victoria Lugrid Alice Desiree akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege huku Mkurugenzi wa Idara hiyo Balozi Dora Msechu akisikiliza wakati Binti Mfalme huyo  akijiandaa kuondoka Tanzania baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu.
Picha ya pamoja
Mtukufu Victoria akiagana na Balozi Msechu mara baada ya kuhitimisha ziara yake nchini tarehe 21 Machi, 2014.
Balozi Msechu kwa pamoja na Bibi Mwakasege na Bi. Tunsume Mwangolombe (wa kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje na Afisa kutoka Ubalozi wa Sweden wakisubiri ndege iliyombeba Mtukufu Victoria (haipo pichani) kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Picha na Reginald Philip

MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI NA ZINAZOISHI MAZINGIRA HATARISHI UNAORATIBIWA NA TASAF WAHAMASISHA AKINA MAMA WAJAWAZITO KUHUDHURIA KLINIKI

0
0
 Baadhi ya akinamama na watoto ambao kaya zao ziko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakisubiri huduma ya kliniki katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
 Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika mpango wa knusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika msitari wa kusubiri kuonana na Daktari katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
 Mratibu wa TASAF wilayani Bunda Nyasegwa Piloty akizungumza na akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini kwenye zahanati ya Mcharo katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Muuguzi wa hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda akitoa mafunzo kwa akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF waliohudhuria kliniki 
Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratbiwa na TASAF wakiwa katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda kuhudhuria kliniki ambalo ni moja ya masharti ya Mpango huo

=====  =====  ======
Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umewahamasisha akinamama wajawazito na wale wenye watoto wa chini ya miaka MITANO kuhudhuria kiliniki ili kulinda afya ya mama na mtoto.

Mratibu wa TASAF katika wilaya ya BUNDA  bwana Nyasegwa Piloty amwaambia Waandishi wa habari waliotembelea zahanati ya Mcharo na Hospitali ya Manyamanyama kuwa mahudhurio ya akinamama wajawazito na watoto katika huduma za kliniki yameongezeka tangu kuanza kwa mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani humo.

Naye Muuguzi katika hospitali ya Manyamanyama Beatrice Ludala amesema kuwa mwitikio wa akinamama wajawazito na watoto walioko kwenye kaya zilizoko kwenye mpango wa kunuru kaya masikini chini ya TASAF ni wa kuridhisha ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mahudhurio ya mama mojamzito na watoto wenye umri wa chini ya miaka Mitano ni moja ya masharti muhimu ya kaya zilizoingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini ili ziweze kuhudumiwa na mpango huo ulioanzishwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF ambao unatakelezwa kwa awamu nchini kote.

Picha zifuatazo zinaonyesha akinamama na watoto wao wakiwa katika zahanati ya Mcharo na hosipitali ya Manyamanyama katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.

NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WANACHUO WA CBE

0
0
 Mkurugenzi wa Wanafunzi wanaochukua Mafunzo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Esther Mbise akimkaribisha mgeni rasmi, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), Eunice Chiume (katikati),wakati wa Semina kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika katika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko chuoni hapo, Felix Chale. Jumla ya wanachuo 180 walihudhuria semina hiyo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada wakati wa semina ya kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu kuwa na uelewa kuhusu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), pindi watakapomaliza elimu yao.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini, Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati akitoa mada katika semina hiyo.
 Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF.
Tunasikiliza kwa makini.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF wakigawa vipeperushi vyenye maelezo ya muhimu kuhusu NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa vipeperushi kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina hiyo.
 Tunajifunza hifadhi ya jamii.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha CBE wakisikiliza kwa makini kazi za mfuko wa hifadhi ya jamii na faida zake
 Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akijibu maswali ya wanafunzi wa CBE kuhusiana na mfuko wa Taifa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.
 Jonas Pera akiuliza swali.
 Mwanachuo wa CBE, Hadson Mwakilima akiuliza swali kuhusu mafao ya NSSF.
Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed akiuliza swali.
Wanafunzi wakipewa zawadi za fulana za NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa zawadi ya Kalenda za NSSF kwa wanafunzi wa CBE.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Said Mohamed akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wameaswa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili wanufaike na mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi yanayotolewa.

Hayo yalisemwa na Meneja Kiongozi wa NSSF, Eunice Chiume, kwenye semina na wanafunzi wa chuo hicho.
Aidha, katika semina hiyo, Eunice alianisha aina za mafao yanayotolewa na Mfuko huo, ambayo ni ya miuda mrefu  na mfupi.

Mafao ya muda mrefu alisema ni pamoja na pensheni ya uzeeni, kuumia kazini na fao la mazishi, ambapo alisisitiza kuwa fao la pensheni ya uzeeni ni muhimu zaidi kwa wanafunzi hao kwa kuwa watanufaika na fao hilo watakapostaafu kazi.

 Aidha, Eunice aliendelea kufafanua kwa fao la pensheni ya ulemavu mfanyakazi hulipwa  kiinua mgongo endapo ataumia akiwa kazini na pensheni ya urithi endapo kama unachangia mfuko wa NSSF ni vema akawajuza wanafamilia ili akifariki dunia warithi wa marehemu wanufaike na penshen ya urithi.

Kwa upande wa mafao ya muda mfupi, Meneja Kiongozi huyo aliyataja kuwa ni pamoja na matibabu, kuumia kazini na msaada wa mazishi.

 Kwa upande wa matibabu alisema NSSF hutoa matibabu bure kwa  mke/mume na watoto wanne kama wana miaka 18 na miaka 21 kama bado wanasoma, ambapo alifafanua kuwa watapata matibabu bure bila gharama za ziada kwa wanachama wake.

Meneja kiungozi huyo pia aliwaambia sasa shirika limekuja na huduma mpya tatu ambazo zinalenga kuwanufaisha wanachama wengi zaidi  na mafao hayo ya NSSF. Huduma hizo ni Hiyari , Mikopo ya riba nafuu na Westadi, ambapo zote alizitolea ufafanuzi.

Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi wa wanafunzi wanaochukua shahada ya kwanza, Dk. Esther Mbise,  alisema kuwa  semina hiyo ni nzuri kwa vijana wengi  kujua  kuhusu huduma na kazi za mifuko ya jamii.

Semina hiyo iliudhriwa na wanafunzi 180 wa  CBE , wa mwaka wa tatu na wa pili,  ikilenga kutoa elimu kwao ili wajue umuhimu wa mifuko mara tu watakapoanza kujitegemea.

TANGAZO KWA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

0
0
 Ubalozi wa Tanzania London - Uingereza, unafuraha ya kuwatangazia Watanzania wote waishio Uingereza kuwa Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakutana na Watanzania siku ya Jumapili tarehe 30 Machi 2014.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Forty Avenue, Wembley Park, London, Middx, HA9 9BE, kuanzia saa 10 jioni (16:00).


Katika Mkutano huo, Mhe.Rais Kikwete atazungumzia maendeleo ya nchi yetu na pia kutumia fursa hiyo kusikia masuala yanayogusa maslai ya

wanadiaspora.

Mhe. Rais atakuwa nchini Uingereza kuanzia tarehe 30 Machi hadi 2 April 2014 kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko rasmi wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. David Cameron.


Ubalozi unapenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wa maeneo ya Uingereza na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kumkaribisha Rais kwenye Mkutano huu adimu.


Kwa Taarifa zaidi:

Simu: 0207 569 1470

Email: balozi@tanzania-online.gov.uk

 Ahsanteni sana
Ubalozi wa Tanzania, London.

RIDHIWANI AITEKA KIWANGWA

0
0
 Ridhiwani afanya mikutano mitano ya hadhara na miwili zaidi maalum kwa Wazee na Vijana wa Kiwangwa,maeneo ambayo mgombea wa ubunge kupitia CCM alifanya mikutano ya hadhara ni Kijiji cha Msuguru,Mwetemo,Msinune,Bago na Kiwangwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mratibu wa shughuli za kampeni za ubunge wa jimbo la Chalinze akihutubia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa kata ya Kiwangwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwa wananchi wa Kijiji cha Kiwangwa katika jimbo la Chalinze.
Mratibu wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakicheza muziki kidogo pamoja na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM wakati wa kumtambulisha na kumnadi mgombea huyo kwa wapiga kura wa Kiwangwa.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akihutubia mamia ya watu waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM na kusisitiza tashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo.
 Umati wa wakazi wa Kiwangwa wakimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa amedhamiria kuinua wananchi wa jimbo hilo kielimu,afya,maji na namna ya kutatua tatizo la wakulima na wafugaji kuwasaidia vijana na kusisitiza kuna umuhimu wa kudumisha michezo kwa jimbo la Chalinze.
 Msanii Maarufu 'Dokii' akicheza na madansa wake wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge  za CCM jimbo la Chalinze .
 Vijana wa Boda Boda wakiongoza msafara wa mgombea wa ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.

 Mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akizungumza na Bibi Tanazina Mrisho Mfaume wa kijiji cha Msinune ambapo pamoja na mengi waliyoongea pia Bibi alielezea furaha yake na kuzungumzia CCM inavyoleta maendeleo kwa wananchi wake.

MSHINDI WA TUZO YA MWANAMAKUKA AKATIWA BIMA YA KULINDA BIASHARA YAKE

0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa Fortis Insurance Brokers Ltd , Bi Maryam Shamo.( wa pili Kulia) akimkabidhi Mshindi wa mwanamakuka 2014, nyaraka zake za Bima. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hio.
Mshindi wa Mwanamakuka 2014, Bi Leyla Mwambungu, baada ya kujinyakulia Tuzo ya Million Tatu, kweye Tuzo za Mwanamakuka Awards, ambazo zinaandaliwa na Unity Of Women Friends. Fortis Insurance Brokers Ltd, Imeamua kulinda Biashara yake Kuwa kwa kumkatia Bima ya Moto Na Wizi, Ili Biashara yake isije ikatetereka atakapopata majanga hayo

introducing Director Shaibu Changamka(Produced By Tiddy Hotter)

ujumbe maridhawa

0
0
Ujumbe huu umeletwa kwenu na mdau Suleiman Mungiya

Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani Tarehe 23 Machi, 2014

0
0
 Kila mwaka tarehe 23 Machi nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani hujiunga na kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika hilo lililoanzishwa tarehe 23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu. 
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’- ”(Weather and Climate: Engaging Youth)”. Katika kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMO), Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana ulimwenguni kote kujihusisha na masuala ya hali ya hewa, ili kupata maarifa na uelewa wa hatua za kuchukua katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Hatua hii ya WMO ni muhimu kwa ustawi wa kizazi hiki na kijacho ili kujenga jamii imara hapo baadae. 
 Siku ya Hali ya Hewa Duniani ni siku ya kutafakari Juhudi zinazofanywa na Wanasayansi Duniani katika kufahamisha Dunia kuchukua tahadhari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani na athari zake. 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa wito kwa vijana wote kubadilika na kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika kizazi hiki na kuchukua tahadhari ili kizazi kinachokuja waweze kufaidi dunia yenye mazingira bora zaidi. 
Vijana wote walioko mashuleni vyuoni na wajasiriamali washiriki katika kuokoa dunia kutoka kwenye majanga yaletwayo na mabadiliko ya hali ya hewa. 
Aidha chachu kubwa ni kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini. Kama ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania inaungana nao kuadhimisha siku hii inayofikia kilele tarehe 23 Machi, 2014 kwa kuwakaribisha wananchi wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona shughuli zitolewazo na Mamlaka kuanzia tarehe 21-23 Machi 2014. 
Aidha, Mamlaka itatembelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali mbali kupitia ofisi zake zilizopo nchini kuanzia tarehe 19-20 Machi 2014. 
Kutoa statements/makala za siku hiyo kwenye magazeti, vipindi kwenye radio, na televisheni kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya hali ya hewa. Mamlaka inawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani ’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’ (Weather and Climate: Engaging Youth)
 IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

JK ALIPOHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIKA MJINI DODOMA LEO

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassa Mwinyi na wajumbe wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete leo
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Makungu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume na wajumbe wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete leo 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Tundu Lissu akigonga meza kuashiria kukunwa na hotuba ya Rais Kikwete
 Mjumbe wa Bunge Maalum Mhe Freeman Mbowe akishangilia hotunba ya Rais Kikwete

 Rais Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum
 Rais Kikwete akisisitiza jambo katika hotuba yake
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, na Mhe Mohamed Seif Khatib na wajumbe wengine. PICHA NA IKULU

Mkuu wa wilaya ya Makete afunga warsha ya maafisa kilimo

0
0
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (katikati) akisisitiza jambo wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa maafisa ugani wilaya hapo yaliyotolewa na TAHA hii leo, kushoto ni mwakilishi wa shirika la TAHA Bw. Manfred Bitala na kulia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Iddi Nganya.
 Miongoni mwa bwana shamba akizungumzia atakayoyafanya pindi akirudi kwenye eneo lake la kazi mara baada ya mafunzo hayo kumalizika.
 Afisa Mifugo wilaya ya Makete Dr. Nuru Issae akizungumza watakavyopambana na magonjwa ya matunda ya apples.
 Bibi Shamba akichangia hoja.
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete

Mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji wilayani Makete mkoani Njombe walioshiriki warsha ya siku 3 ya namna ya kuboresha kilimo cha matofaa maarufu kama apples iliyotolewa na shirika la TAHA, wametakiwa kutekeleza kwa vitendo mikakati waliyojiwekea ya namna ya kuboresha zao hilo

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa wagani kazi hao, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro, amerudia kauli yake kuwa suala hilo ni mkakati wa kitaifa ambao umeagizwa na rais Dk. Jakaya Kikwete, hivyo mafunzo hayo waliyopatiwa yanatakiwa kutendeka kwa kuwa yana manufaa kwa wakulima na wananchi wa Makete kwa ujumla

Mh. Matiro amesema ndani ya muda mfupi anatarajia sifa ya Makete kuwa inaongoza kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi sasa itabadilika mara moja na kuonekana kuwa inaongoza kwa kuzalisha matunda ya apples

"Nadhani mtu ukienda pale Dar es Salaam ama sehemu nyingine ukasema unatoka Makete tayari wanaelewa kuwa kuna Ukimwi, sasa hilo tunaweza kulibadilisha, kwa kwenda kuwasaidia wakulima huko mnakotoka, wazalishe apples kwa wingi kwa kufuata utaalam mliopatiwa na TAHA ili tuone mabadililo" Alisema Mh. Matiro

Amesema mikakati waliyojiwekea baada ya mafunzo hayo ni njia nzuri ya kuifikisha wilaya kule inakotaka kuhusu kilimo cha apples, ambacho kinatarajiwa kuwa kilimo cha biashara kwa lengo la kuinua uchumi wa wakulima na wilaya kwa ujumla

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Iddi Nganya amesema wagani kazi hao ndio watekelezaji wakubwa wa mikakati hiyo na ndiyo maana wakapatiwa mafunzo hayo, hivyo kila mmoja ana jukumu la kwenda kuitumia ipasavyo kwa wakulima wake

Amesema tathmini itaonekana hivi karibuni, kwani kipimo cha hayo yote ni kuona wamebadilishaje kilimo cha wakulima wao huko wanakotoka, kama ikionekana kuna utofauti itaonekana kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia, hivyo waone jitihada zinazofanywa kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa

Naye Mwakilishi kutoka shirika la TAHA ambaye alikuwa miongoni mwa mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amesema ili kufanikisha malengo hayo kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kukubali kubadilika na kuwajibika ipasavyo kwa nafasi yake

Amesema wao kama TAHA wanawajibu wao ikiwemo kutoa elimu ambayo tayari wameshaitoa, na maafisa kilimo hao nao wana nafasi yao na hali kadhalika na wakulima, hivyo jitihada za vitendo zikifanywa anaimani lengo la kilimo cha apples kuzaliwa kwa wingi na kwa ubora wa hali ya juu litafanikiwa

Dk. Nuru Issae ni Afisa mifugo wilaya ya Makete ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo ambapo amesema jambo watakaloanza kulifanyia kazi mara moja ni kutambua magonjwa yanayoshambulia apples na kuyatokomeza kwa kuwa wameelezwa aina mbalimbali za magonjwa yanayoshambulia matunda hayo

Dk. Issae amesema kabla ya mafunzo haya hawakuwa na wazo kuwa magonjwa yanaweza kuzorotesha jitihada za mkakati wa kuboresha kilimo cha apple wilayani hapo, na kwa kuwa wametambua kuwa magonjwa ni kikwazo kimojawapo, watapambana nayo mara moja

Miongoni mwa mikakati iliyopangwa baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ni pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na kampeni ya pamoja ya kuyatokomeza magonjwa yanayoshambulia apples, kushirikiana na taasisi mbalimbali na wadau binafsi wanaolima matunda hayo, kukaa na wakulima na kupanga nao namna nzuri ya kulima apples kwa manufaa kama walivyoelekezwa na mengine mengi

ngoma azipendazo ankal

0
0
GATHO BEEVENS anakupa "Azalaki awa"

AUDIO YA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA MARCH 21, 2014

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images