Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 387 | 388 | (Page 389) | 390 | 391 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini Iringa kuhusiana na ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.

  "Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa kadi ya kupigia kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.

  Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
   Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitoa ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuvu amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu na naibu katibu wa Bunge Maalum la katiba katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Dodoma leo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Katibu wa Bunge Maalum Mhe Yahya Khamis Hamad. Wa pili kushoto akishuhudia  ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu
   Dkt. Thomas Kashililah akila kiapo kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Wa pili kushoto akishuhudia kiapo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho. Picha na Freddy Maro.  0 0


  Vodacom Tanzania’s internet users today experienced slow internet speeds which were caused by a cut on the Eassy Submarine Fibre cable which carries the company’s data traffic through South Africa.
  Speaking in Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Managing Director, Rene Meza said his company had no option but to route all its internet traffic through the Seacom Submarine Cable in the Indian Ocean in order to ensure that customers had continued access to the internet.
  “As a result of this, customers will have experienced low internet and delays in the execution of other services which rely on the internet. We understand the inconvenience that this outage has caused them and would like to apologize to them and to ask for their patience and support while we work to restore our services,” said Meza.
   He went on to say that due to its location on the Southern tip of Africa, the Eassy submarine cable is designed to carry Vodacom’s internet traffic via the Atlantic Ocean whereas the Seacom one routes traffic via   the Indian Ocean adding that…” the two cables are also able to support each other in times of failure and that is why we are now carrying all our internet traffic through the former. This increased traffic load on the Seacom cable is slowing down our internet speeds as it is now carrying a far heavier load than it was originally designed to.”
  With regards to what was being done to rectify the situation, Meza said, the Eassy technical team was working hard to assess the magnitude of the damage caused by the fibre cut at Mtunzini Bay which lies  29.5 kilometres off the shore of the Atlantic Ocean and to repair it.    
  “We would kindly like to request our esteemed customers to please bear with us as we continue to work to restore all our services. I would like to assure our esteemed customers that we at Vodacom remain committed to continue providing them with world-class services and our aim is to restore services as soon as possible,” says Meza


  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni Meneja Masoko wa Airtel , Upendo Nkini.
   Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (kushoto) akikabidhi hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni kushoto ni rafiki wa mshindi huyo Antidius Diocresi. 
   Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto) akiongea kushukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kuanzisha promosheni hiyo ambayo imeweza kumfanya akawa bingwa. Pembeni ni  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
  ============  =========  =========
  Airtel yakabidhi milioni 50 kwa mshindi wa promosheni ya MIMI ni Bingwa leo 
   
  ·         Washindi wengine 14 kwenda OLD-TRAFFPORD Uingereza kesho -Ijumaa
   
  Kampuni ya simu za mkononi ya kupitia promosheni yake ya mimi ni bingwa  iliyomalizika hivi karibuni imemkabidhi mshindi wake BW, Rashidi Kagombora mkazi wa Bukoba hundi ya shilingi milioni 50 leo katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam 
   
  Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tunawashukuru wateja wote walioshiriki kikamilifu katika promosheni yetu ya MIMI NI BINGWA, leo tunamkabidhi bw, Kagombola kitita chake kupitia hundi hii ya mfano na baada ya siku chache pesa zake zitaingia katika akaunti yake ya benki moja kwa moja”
   
  Vilevile tunafuraha kuwatangazia kuwa jumla ya wateja 14 wa Airtel walioshiriki katika promosheni ya MIMI BINGWA wataondoka kesho kwenda nchini Uingereza jiji la Manchester CITY na watapata nafasi ya kushuhudia soka LIVE kati ya Manchester United na Liverpool siku ya jumapili tarehe 16/03/2014 soka litakalochezwa saa 9 na nusu alasiri. 
   
  Washindi wa MIMI NI BINGWA wanaotarajiwa  kuondoka kesho siku ya ijumaa ni GEOFREY DAVID MSITU, JOSEPH STEVEN MAMBO,SEVERA MORIS MATHIAS, HARRSON WILSON, RAFAEL WAIRES KABENGA, EDMUND HENRY KAGIMBO, AMINIYEU NLILIE NATAI, MAULID BARAKA KITENGE, JOSEPH MOSES NDOSSI, CHARLES JOSEPH BUCHWA, GOODLUCK RICHARD KIMARO, RAHABA EUSEBIUS MVUONI, RAJAB SAID MANGARA, na watasindikizwa na  Meneja Masoko wa Airtel Bi UPENDO GILLIARD NKINITunatoa  pongezi kwa washindi wote walioibuka na zawadi mbalimbali  kupitia promosheni hii iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Pia tunawapongeza wateja wengine wote walioshiriki katika promosheni lakini hawakushinda ikumbukwe kuwa hii ni bahati nasibu hivyo kila mtu anajishindia kwa bahati yake 
   
  Nae  mshindi wa Promosheni hiyo Bw, Rashidi Kagombola alisema “ninafurahi sana kuwa mshindi wa mamilioni haya, kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kubadili maisha kwa haraka hivi, leo hii natoa ahadi kwa Airtel na watanzania wenzangu kuwa nitahakikisha nazitumia kwa uangalifu pesa hizi ili kukuza biashara yamgu ya samaki”
   
   
  Promosheni MIMI BINGWA imekwisha huku jumla ya pesa taslim milioni mia tatu ishirini na nne 324 zikiwa zimekwenda kwa wateja toka mikoa na sehemu mbalimbali, vile vile jumla ya washindi wengine 35 wamepata zawadi ya nafasi yakusafiri na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester na watalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za malazi, usafiri, pamoja na gharama zote za kuandaa safari hadi kupatikana kwa hati ya kusafiria na VISA ya kwenda Uingereza na kushuhudia SOKA katika kiwanja cha OLD Traford cha Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Prof. Ali Seif Mshimba akitoa nasaha kwa wajumbe wa Kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar pamoja na kumkaribisha mgeni rasmin.
   Katibu Mkuu Wizara Biashara, Viwanda na Masoko Julian B. Raphael akizindua kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar katika hafla iliyofanyika Grand Palace Hotel Mjini Zanzibar (kulia) Prof. Ali Seif Mshimba na (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salu.
  Mkufunzi kutoka (TBS) Bw. Nickonia Mwabuka aliesimama akitoa elimu juu muundo upatikanaji wa viwango kwa tasisi kusika katika hafla iliyofanyika Grand Palace Hotel Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) wakimskiliza Mkufunzi kutoka (TBS) Bw. Nickonia Mwabuka hayupo pichani alipokua akitoa maelezo kuhusu muundo upatikanaji wa viwango kwa tasisi kusika.

  0 0

  Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma.
  Muungano wa Tanzania kwa miaka 50  umekuwa ni  undugu hivyo kuufuta ni sawa na kufuta  utaifa wetu na kukaribisha ukabila.

  Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma, na Kapteni John Chiligati ambaye ni mjumbe aw Bunge Maalum la Katiba wakati wa mahojiano na kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC One.

  Aliendelea kusema kwamba muundo wa kimaisha  wa Muungano wetu ni wa serikali  mbili, hivyo tusivunje kabisa Muungano huo.

  "Kuvunja Muungano ni kukaribisha ukabila na kuchanganya wananchi maana watajitenga kwamba wengine ni Wazanzibar, wengine ni Watanganyika, hivyo ni kurudi nyuma badala ya kusonga mbele" aliongeza Mhesh Chiligati.

  Akizungumzia madhara ya serikali tatu Mhesh Chiligati alisema kwamba Serikali tatu italeta utata maana kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Kwa muundo huo Serikali tatu, serikali ya Muungano haitakuwa na watu, madaraka,utaifa na hata pesa zake.

  Akichangia ya kuwa na serikali mbili, Mzee maarufu Mjini Dodoma Jumanne Gombashi alisema kwamba suala la zaidi ya Serikali mbili si tatizo la Watanzania, hivyo tusiwasingizie kwamba wanahitaji serikali tatu , kwani badala ya kutatua matatizo tutaongeza matatizona tutakuwa tunaicha chana nchi yetu.

  " Tumekuwa na Serikali mbili kwa miaka 50, kama kuna makosa hatuna budi kujitathmini, na kujisahihisha na kujikosoa ili tutatue matatizo hayo na tuendelee na Serikali mbili.." alisema mzee Gombashi.

  Aidha aliendelea kusema kwamba tunapozungumzia serikali tatu tuangalie pia upande wa gharama za uendeshaji wa Serikali hizi. Kila upande yaani Zanzibar na Tanzania Bara utatakiwa kuchangangia uendeshaji wa serikali ya Muungano, na pia tutalazimika kuwa na viongozi watatu, mabaraza ya mawaziri matatu na mabunge matatu.

  "Kwa  kuwa na serikali tatu hawa watu wote wanahitaji huduma  kwa hiyo kwa kufanya hivyo tutapanua matumizi kwa nchi changa kiuchumi kama hii yetu" alisema mzee Gombashi.

  Mhesh. Chiligati alitoa ushauri wa kudumisha Muungano,na kuepuka muundo utakaodhoofisha  Muungano bali tuhakikishe  Muungano unaimarishwa na pande sote mbili.

  Naye mzee Gombashi  alimalizia kwa kuwahimiza Watanzania kutotetereka na kuburuzwa na watu wasiopenda Muungano, na kwamba iko siku tutafika kwenye serikali moja na tuwe wamoja zaidi.

  0 0


  KISHAKILENA Reality TV Show
  LikeBrothaz Production.

  KISHAKILENA Reality TV Show is geared towards exploring the complexity of life particularly when beautiful girls referred to as ‘Kishakilena’ come under one roof. Though they share cultural heritage they have different personalities that set out serious life dramas. Episode‐#1 establishes the show’s characters by zeroing in on; Jestina, CoCo Diva, Kim, Nusrat and Linda the four complex personalities.

  JESTINA, an educated and iron lady, cannot stand crazy ideas of her mates particularly on men of their dreams. She gets wild when CoCo DIVA, the crazy party girl, tries to insinuate evil minds to the youngest girl LINDA.

  CoCo Diva is highly threatened by the natural beauty of sexy KIM. She Cannot also stand NUSRAT, the eldest among them all who has brilliant ideas but fails to execute them. The serious back rash between CoCo Diva and Nusrat steers up the mood of the house.

  Can the youngest, funny, sexy, music lover and model‐dreamer Linda stand the peer pressure? 
  Enjoy first episode below:  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.

  Kinana amewataka wakazi wa Kalenga kumpigia kura za kutosha na hatimae kuibuka mshindi kwa maendeleo ya jimbo hilo,hapo siku ya jumapili ambapo uchaguzi utanfanyika.Uchaguzi unafanyika ndani ya jimbo hilo kuziba nafasi ya aliyekuwaMbunge wajimbo hilo kwa tiketi ya  CCM,Marehemu William Mgimwa.
   Katibu Mkuu wa CCm,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Magulilwa mapema leo jioni wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama,alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho,Ndugu Godfreya Mgimwa kwa wananchi.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa akijinadi kwa wakazi wa kijiji cha Magulilwa,kata ya Magulilwa Iringa Vijijini wakati wa mkutano wa kampeni  za lala salama,amapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16,siku ya jumapili.

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.
   Wananchi wa kijiji cha Magulilwa wakishangilia jambo.
   Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Magulilwa akisoma moja ya gazeti la kila siku wakati mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi,ukiendelea jioni ya leo.
  Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe akiagana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kumlaiza mkutano wa hadhara wa Kampeni,kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika jioni ya leo kwenye kijiji cha Magulilwa,Iringa vijijini,pichani kati ni Mbunge wa jimbo la Mwibala,Mh Kangi Lugora akisikiliza.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR BLOG

  0 0

  Pursuant to our call for the right of dual citizenship for all Tanzanians, the Tanzanian Communities in the United States of America and the Diaspora Council of Tanzanians in America (DICOTA) have agreed to file a petition for this cause to the Constitutional Review Parliament that is now taking place in Dodoma, Tanzania through our Representative Honorable Kadari Singo, who is also a member of the our Diaspora Community and who resides in California. With the highest honor, we invite you to support this petition.

  Honorable Kadari Singo is now attending the Constitutional Review Parliament in Dodoma.  After consultation with other members of the Parliament and in seeking their support, and after thorough deliberations on how to bring the issue of dual citizenship to the attention of all members of the above-mentioned Parliament, it was decided that a workshop, training or conference should be arranged to lobby to the members of the Parliament and inform them of the necessity and urgency of their supportive votes when the motion of dual citizenship will be tabled.

  For that conference, we will need experts on this issue from other parts of Tanzania and abroad (including International Office for Migration - IOM) to attend at a very short notice. We will also need an excellent venue and some refreshments. Moreover, the experts on this issue will need to be paid. Hence, we are looking for at least $25,000 dollars to cover expenses for this event. The plan is to run a workshop/seminar for 3 days targeting different groups of MPs for each day.

  We are certain that if the members of the parliament are made to understand our motion, it will be easier for them to vote for dual citizenship. Dual citizenship is an important right that has been denied to Tanzanians since 1964. Thus, we hope that the workshop or conference will provide the members of the Parliament with an opportunity to understand the overall benefits of dual citizenship and why their votes for this cause are imperative. Moreover, we invite you to think about your interests, family and opportunities offered by dual citizenship.

  For these reasons, we ask you to support this cause by giving any donations to the following account:


  Or, you deposit to our Account below:
  Account Name: ATC- DMV
  Bank Name: PNC- BANK
  Routing Transit Number:  054000030
  Account Number:  5313293767
   
  The funds obtained will be used to arrange the above-mentioned workshop or conference inDodomaTanzania. We need at least $ 25,000 so you may contribute any amount you can afford. If every Tanzanian in the United Statescontributes at least $10, we will reach or surpass the amount of $ 25,000.

  We are grateful that you are supporting dual citizenship for Tanzanians outside their country and we hope through your support, we will be able to achieve this goal.
  Sikiliza Audio ya mwakilishi wetu Kadari Singo akiongea toka Dodoma
  Iddi Sandaly
  President

  Association of Tanzanian Community in Washington DCMaryland and Virginia

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa amepokea zawadi yenye heshima kwa asili ya watu wa korea kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Jamhuri ya Korea Mr. AHN Hong  Joon (kushoto) kiongozi huyo na ujumbe kutoka Bunge la Korea na shirika la kimataifa la misaada la Korea-KOICA katikati ya wiki  walimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ofisini kwake kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akielezea fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma kwa ujumbe wa bunge la korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge hilo Mr. AHN Hong Joon (wa pili kulia), ujumbe huo wa bunge la korea katikati ya wiki ulimtembelea Mkuu wa Mkoa Dodoma kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa na ujumbe kutoka Bunge la Jamhuri ya Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Korea Mr. AHN Hong Joon (mwenye tai nyekundu waliokaa), ujumbe huo kutoka Korea ulimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katikati ya wiki na kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo. PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA WA OFISI YA MKUU WA MKOA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadiki akitoa maelezo machache kuhusu suala la upatikanaji wa maji Mkoani mwake, katika warsha iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro.
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Mhe. Mwantumu Mahiza , akitoa salamu pamoja na umuhimu wa ushirikishwaji wadau mbalimbali katika kulinda mazingira na vyanzo vya maji. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mhe. Modest J. Mero, Balozi wa kudumu, Ubalozi wa Tanzania, Geneva alipokutana na Bi. Jan Beagle, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na UKIMWI (UNAIDS), katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania. Bi. Jan pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
  Bi. Jan alimtembelea Balozi kwa lengo la kumtaarifu juu ya majukumu ya bodi ya UNAIDS. Hii pia ni muendelezo wa mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi.

  Tanzania itakuwa moja wa wajumbe 22 wa bodi ya UNAIDS kwa mwaka huu 2014 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2016. Katika mazungumzo, umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumble mikakati ya kuzuia maambukizo mapya ya UKIMWI yalijadiliwa. 
  Msimamo wa Tanzania katika kupambana na janga hili la UKIMWI uliwekwa bayana. Bi Jan alisifu juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania katika kukabiliana na janga hili, ikiwa ni pamoja na juhudi za serikali inazo fanya kuchangia gharama  kwa kuwa na mpango wa kuanzisha mfuko wa fedha wa kupambana na UKIMWI- AIDS  Trust Fund(ATF).  Mhe Balozi alimhakikishia Bi. Jan kwamba, Tanzania itatoa ushirikiano  wa kutosha katika ushiriki wake kwenye  bodi ya UNAIDS.  

  0 0

   Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni ya Raia Mwema, Mpiganaji Anthony Siame akikabidhiwa tuzo ya Umahairi wa Uandishi wa Habari na Bw. Aggrey Mareale  baada ya kuibuka mshindi wa picha bora kwa mwaka 2013 wakati wa Sherehe zilizofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Hongera mpiganaji!


  0 0

  Tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji ya uhakika linalowakabili wakaazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mengine inayohudumiwa na mitambo ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini sasa litakuwa historia...
   Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa  mitambo ya Ruvu Chini.

  0 0

  Baada ya kusimamishwa kwa takriban wiki moja, vipindi vya Televisheni vya shindano la Maisha Plus, vinatarajiwa kurudi tena hewani leo saa tatu usiku, kupitia kituo cha televisheni kile kile, TBC1.


  Akizungumza mapema asubuhi hii katika mkutano na wanahabari, Mratibu wa shindano hilo ambalo mwaka huu limepewa jina la Maisha Plus Rekebisha, Ally Masoud `Kipanya', amesema baada ya kukaa chini na uongozi wa televisheni hiyo, wamekubaliana kimsingi kutangaza ratiba itakayokuwa rasmi ambayo haitabadilika kama ilivyokuwa awali.


  Kipanya amesema ratiba ya vipindi itaanza upya na ratiba itakuwa kwamba, siku za ijumaa na jumamosi, vipindi vitaoneshwa kuanzia saa tatu usiku lakini siku zote za wiki zilizobaki, kipindi kitakuwa kinaruka saa nne na dakika tano usiku.


  Alisema vipindi hivyo vitaonyesha hatua za awali ambazo ni usaili na mpaka kupatikana kwa washiriki 30 waliobahatika kuingia kijijini.  “Tutaanza kuwaonyesha kipindi chetu kuanzia leo hii saa tatu usiku, kipindi kitaanza kwa kuonyesha hatua za mwanzo kabisa za mashindano haya,” alisema Kipanya.  Alifafanua akisema kuwa vipindi 10 vya mwanzo vitaonyesha mchakato mzima wa upatikanaji wa vijana 18 kutoka Tanzania watakao ungana na vijana wengine 12 kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi zitakazotoa washiriki watatu kwa kila nchi.  Usaili wa mwaka huu ulikuwa tofauti na miaka mingine ambapo orodha ya washiriki 40 ilitengenezwa na ikagawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lilikwenda mkoani iringa kuishi kwenye vijiji vya huko na kushiriki shughuli za kijamii.  Kundi la Pili litaenda visiwani Zanzibar ambalo pia litashiriki utamaduni wa kila siku wa kimaisha wa visiwani humo ambapo ni washiriki tisa tu katika kila kundi watachukuliwa na watachujwa kutokana na jinsi walivyoyamudu maisha ya huko.

  “Vijana wakiwa huko katika vijiji vya kweli watakuwa wakishiriki shughuli za kilimo, usafi, za kiafya na nyinginezo kabla hawajaingia katika kijiji cha Maisha Plus”, alifafanua Kipanya.


  Baada ya kundi la kwanza na la pili kutoa washiriki tisa kila kundi, washiriki 18 watakuwa wameshapatikana, na sasa nchi za zikishapata washiriki wake 12, idadi ya washiriki 30 itaingia kijijini cha Maisha Plus katikati ya mwezi huu.

  0 0

  Wawakilishi kutoka Rotary Club Dar es Salaam wakizindua mabomba ya maji safi na salama ya kunywa katika Shule ya msingi ya Kijitonyama kupitia mradi wa Rotary wa “Maji kwa Maisha”. Kutoka kushoto ni Rais wa klabu ya Rotary ya Mikocheni John Gitonga akiwa na Naibu Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Sharmila Bhatt, mratibu wa Elimu kutoka manispaa ya Kinondoni Alexandrina Kahandoma na kulia ni Jane Pesha kutoka klabu Rotary ya Mikocheni. Mradi huo uligharimu kiasi cha Sh 15 milioni.

  0 0

   Mhe. Mchungaji Christopher Mtikila, akiapa kuwa mbunge wa Bunge Maalum la kuandika katiba mpya mjini Dodoma leo katika zoezi linaloendelea vyema .
  Mhe. Emmanueli Makaidi akiapa kuwa mbunge wa Bunge Maalum la kuandika katiba mpya
   Mhe Tundu Lisu akiapa kuwa mbunge wa Bunge Maalum la kuandika katiba mpya
  Mhe Mkosamali  akiapa kuwa mbunge wa Bunge Maalum la kuandika katiba mpya.
  Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma

  0 0

  Na Fakih Abdul wa Police Press Tabora
  Kamanda wa Polisi Mkowa wa Tabora  Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzana S. Kaganda  amefanya ziara katika wilaya ya Sikonge na kukutana na vikundi mbalimbali vya ulinzi shirikishi. Kwanza alikutana na kikundi cha Pathfinder (maarufu kama Maisha Plus ya Tabora) kilichopo katika kijiji cha Tumbili kata ya Tutuo wilaya ya Sikonge na kuwafundisha mbinu mbalimbali za ulinzi shirikishi na dhana ya Polisi jamii kwa ujumla wake, pamoja na kuwapatia mazoezi ya ukakamavu 
  Kamanda wa Polisi Mkowa wa Tabora  Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzana S. Kaganda akiongea na mojawapo ya vikundi vya ulinzi shirikishi mkoani humo
  Vijana wakifundishwa  mbinu mbalimbali za ulinzi shirikishi na dhana ya Polisi jamii kwa ujumla wake
  Kamanda wa Polisi Mkowa wa Tabora  Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzana S. Kaganda akitoa maelekezo kwa vijana hao
  Kamanda wa Polisi Mkowa wa Tabora  Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzana S. Kaganda akisimamia zoezi la ukakamavu
  Kamanda wa Polisi Mkowa wa Tabora  Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzana S. Kaganda. Picha na Fakih Abdul wa Police Press Tabora

  0 0

  Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la Sabato wameendesha zoezi la kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
  Mikoa hiyo ni Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Mara, Morogoro, Mbeya na Iringa, lengo likiwa  ni kukusanya chupa 3000 katika mikoa hiyo.
  Akiongea na waumini waliofika katika kituo cha Damu salama ilala mchikichini Askofu wa Jimbo la Mashariki ambalo linajumuisha mikoa ya Dar-es-salaam, pwani, Dodoma, Morogoro, Lindi, Mtwara na Zanzibar Askofu Mark Walwa Malekana aliwashukuru waumini kwa moyo wa upendo wa kuja kuchangia damu.
  Amewaomba waendelee na moyo huo ili wawe wachangia damu k wakujirudia kwani amesema mwanaume anaweza kuchangia mpaka mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka . 
  Askofu Mark Walwa Malekana pia alikemea tabia ya baadhi ya watumishi wa hospitali ambao wanajihusisha na tabia ya kuuza damu kuwa waache tabia hiyo kwani ni dhambi.
  "Watu wanajitolea kwa hiari na upendo kuchangia damu bila malipo yoyote hivyo wanapaswa kupata huduma hiyo bure", aliasa Askofu Malekana.
   Askofu Mark Walwa Malekana akiongea na waandishi wa habari ambao walifika ilala mchikichini kushuhudia waumini wakichangia damu.
   Afisa mwendeshaji Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dr. Abdu Juma akimshukuru Askofu Mark walwa Malekana kwa kuhamasisha waumini wa makanisa ya sabato kujitolea damu kwa hiari kuokoa maisha ya wagonjwa
   Meneja wa Damu salama  kanda ya Mashariki Dr. Avelina Mgasa akimkaribisha askofu kuongea na waumini
  Zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es salaaam

  0 0

  Joseph Msami na Falviana Matata katika mahojiano

  Wakati mikutano mbalimbali kuhusu hali ya ya wanwake ikiendelea mjini New York Marekani, mwanamitindo nguli wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata ambaye pia anamiliki taasisi iitwayo Flaviana Matata inayotoa misaada ya kielimu, amesema ikiwa wanawake watainuana na kupeana nafasi watapiga hatua kwani kufanya hivyo kunatoa fursa zaidi kwa kundihilo.

  Katika mahiojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhudhuria kikao kilichoangazia ushiriki wa wasichana katika masomo ya sayansi, amesema inahuzunisha kuona wanawake wakiwekeana fitina katika kusonga mbele. Hapa anaanza kwa kueleza nafasi ya wanawake katika sayansi.
  (SAUTI MAHOJIANO)
  KUSIKILIZA BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 387 | 388 | (Page 389) | 390 | 391 | .... | 3283 | newer