Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 386 | 387 | (Page 388) | 389 | 390 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa  bidhaa  mpya kwa wateja wao ya NBC Direct, inayowapa wateja nafasi ya kupata huduma zote za kibenki ndani ya bidhaa hiyo.. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Hduma Rejareja za Kibenki, Mussa Jallow akizungumza na wateja na waalikwa wengine katika uzinduzi huo akieleza faida mbalimbali zinazopatikana katika bidhaa ya NBC Direct.
   Baadhi ya maofisa wa NBC na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi  jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia) akisamiliama na baadhi ya wagenzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa NBC Direct  jijini jana. 


  0 0

  Balozi in VOA 027Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Mwamoyo Hamza akiwa na Mh.balozi wa Tanzania Washington Dc na Mexico Liberata Mula mula alipotembelea idhaa hiyo Jumatano Machi 12, 2014. Balozi in VOA 001Kushoto Mkamiti Kibayasi, akiwa na Mh.balozi Liberata Mula mula na Khadija Riyami katika ofisi za idhaa ya Kiswahili ya VOA. Balozi in VOA 007Mh.balozi Liberata Mula mula akijibu maswali katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya VOA. Balozi in VOA 008Khadija Riyami akimhoji balozi Mula mula. Balozi in VOA 003Sunday Shomari na Mh.balozi Mula mula na Khadija Riyami. Balozi in VOA 021Mh.balozi Mula mula na Prodyuza wa VOA Duane Collins. Balozi in VOA 032Mtangazaji maarufu wa "Straight Talk Afrika" VOA-TV Shaka Ssali akiagana na Mh.balozi baada ya mahojiano yake aliyofanya kwa upande wa radio na TV huku akisindikizwa na Khadija Riyami,Mwamoyo Hamza na Mkamiti Kibayasi.Picha na Mdau Sunday Shomari

  0 0

  The Secretary General of the East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera continued with his engagement in Brussels and today met H.E. Didier Reynders, the Deputy Prime Minister and Minister of Foreign Affairs, External Trade and European Affairs of the Kingdom of Belgium. Amb. Sezibera also met H.E. Jean-Pascal Labille, the Kingdom’s Minister for Public Enterprises and Development Cooperation.

  Amb. Sezibera, who is in Brussels at the invitation of the European Commission and European External Action Service, discussed with the two Ministers how to enhance further the bilateral cooperation between the Kingdom of Belgium and the EAC.

  The Secretary General lauded the recent decision by the Belgium Government to further support the EAC in areas of Peace and Security and Infrastructure development including Energy and Natural resources.

  Amb. Sezibera will be taking part today in the Eastern Africa, Southern Africa, and Indian Ocean’s 11th European Development Fund (EDF) regional programming scheduled for 13-14 March 2014 in Brussels.

  He is expected to join CEOs of other RECs in the Eastern Africa, Southern Africa, and Indian Ocean Union region to finalize the Rules of Procedures, Memorandum of Understanding on the governance of the Regional Indicative Programme; and a list of actions to be financed under the cross-regional envelope.
  EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera with Deputy Prime Minister and Minister of Foreign Affairs, External Trade and European Affairs of the Kingdom of Belgium, H.E. Didier Reynders.
  EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera with the Minister for Public Enterprises and Development Cooperation of the Kingdom of Belgium, H.E. Jean-Pascal Labille.

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na wanahaabari (hawapo pichani) kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka hiyo.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
  Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza, akionesha moja ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamalaka hiyo kinachotumiwa na wanawake kukuza makalio.
  Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
  Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza (hawapo pichani). Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

  Frank Mvungi-Maelezo

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imeteketeza vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya binadamu vyenye thamani ya takribani Shilingi Milioni 188 katika kipindi cha mwaka 2012/2013.

  Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza wakati akizunguza na wanahabari kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Alisema TFDA imeweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia mbalimbali ambazo ni pamoja na usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya biashara ya bidhaa husika na ukaguzi wa majengo ya vipodozi.

  Simwanza aliongeza kuwa hatua nyingine ni ufuatiliaji wa vipodozi katika soko ili kujiridhisha kuwa vina ubora na usalama unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

  Alibainisha kuwa vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu vina madhara kama vile kusababisha kupata mzio wa ngozi, kusababisha ugonjwa wa ngozi kwa mtumiaji.

  “Matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya zebaki (mercury) kwa mama wajawazito huathiri mtoto tumboni hali inayoweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto atakayezaliwa.

  Alifafanua zaidi kuwa viambato kama Zirconium na Vinyl Chloride husababisha kansa ya ngozi na mapafu kwa mtumiaji wa vipodozi vyenye kemikali.

  Simwanza alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha matumizi ya vipodozi vyenye viambata vyenye sumu na kemikali.

  TFDA imekuwa ikifanya operesheni na ukaguzi wa vipodizi katika maduka mbalimbali yanayouza bidhaa hizo na kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu na kuziteketeza kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani Prof. Kwaku Aning (mwenye tai ya bluu) akiwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu (wa kwanza kushoto) wakijadiliana kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Shirika hilo kwa ajili ya matumizi salama ya mionzi na ujenzi wa Kituo Mahiri cha Tiba ya Ugonjwa wa Saratani nchini.
  Prof. Kwaku Aning, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (International Atomiki Energy Agency-IAEA) akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Patrick Makungu (hayupo pichani) ofisini kwake, Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa Kituo Mahiri cha Tiba ya Saratani nchini Tanzania ambacho kinaweza kuhudumia Kanda ya Afrika Masharii na nchi za jirani.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Patrick Makungu (mwenye tai nyekundu) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya Prof. Kwaku Aning, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani na ujenzi wa Kituo Mahiri cha Tiba ya Saratani nchini Tanzania ambacho kinaweza kuhudumia Kanda ya Afrika Mashariki na nchi za jirani.

  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani Prof. Kwaku Aning yupo ziarani nchini Tanzania kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 13 hadi 15 Machi, 2015 kwa lengo la kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Shirika lake kuhusu matumizi salama ya mionzi kwa ajili ya tiba ya ugonjwa wa saratani.

  Pia aliongeza kuwa Tanzania ni mahali panapofaa kujenga Kituo Mahiri cha Tiba ya Ugonjwa wa Saratani ambacho kitaweza kuhudumia wagonjwa wa kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na nchi jirani.

  Katika maelezo yake alisema kuwa ugonjwa wa saratani umekuwa ni tishio kwa wananchi wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea kama vile Tanzania na ni ugonjwa ambao unasababisha vifo kwa watu wengi kwa mwaka ukilinganisha na magonjwa mwengine ya UKIMWI na Malaria.

  Alizidi kuongeza kuwa hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, (WHO) lilitoa taarifa kuwa inakadiriwa kiasi cha wananchi wapatao 4.6 milioni wanakufa kutokana na ugonjwa wa saratani kwa mwaka kwenye nchi zinazoendelea kama vile Tanzania ikilinganishwa na wagonjwa wapatao 2.1 milioni wanaokufa kwa ksababu ya UKIMWI na takribani milioni moja kwa sababu ya malaria.

  Nchi nyingi zimetoa kipaumbele kwenye magonjwa ya UKIMWI na Malaria ambapo ni tofauti ikilinganishwa na ugonjwa wa saratani ambao unasababisha maumivu makali na hatimaye vifo kwa wananchi walio wengi. Hii inajidhihirisha pia kwa namna ambavyo nchi husika zinatoa msukumo na kipaumbele kwa magonjwa mengine ikiwa ni pamoja na kupata misaada kutoka nchi mbalimbali za nje.

  Pamoja na juhudi za kuwepo na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road ya Dar es Salaam na ile ya Bugando, Mwanza Prof. Aning ametoa wito kwa Tanzania kuendelea na jitihada za kuweka kipaumbele kwenye kudhibiti na kutibu ugonjwa wa saratani kwa wananchi wake.

  Aidha, aliongeza kuwa Shirika lake liko tayari kushirikiana na Tanzania kujenga Kituo Mahiri cha Tiba ya Ugonjwa wa Saratani. Alisisitiza kuwa wanachi waelimishwe kuhusu dalili za ugonjwa wa saratani na kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kuchukua hatua mapema.Prof. Aning alisema kuwa kuna zaidi ya aina 178 za ugonjwa wa saratani.

  Hivyo alitoa rai kwa wananchi kuacha kutumia sigara na kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa kuwa kwa namna moja au nyingine zinaweza kusababisha ugonjwa wa saratani.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu alimueleza Prof. Aning kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Shirika lake kwa kuwa tayari nchi imekuwa ikifanya hivyo na wananchi wa Tanzania wamenufaika na misaada ya Shirika hilo kwa kuleta vifaa tiba, wataalamu na kutoa mafunzo kwa watanzania kwenye masuala mbalimbali yanayohusu matumizi salama ya mionzi na nguvu za atomiki ikiwa ni pamoja na kusaidia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. 

  Prof. Aning atakutana na viongozi na watendaji wa Wizara ya Afya, Taasisi ya Chakula na Dawa, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road na ile ya Bugando, Mwanza.

  0 0  0 0


  0 0

  Hatimaye leo Bunge maalum la Katiba limemchagua Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wake mjini Dodoma. 
   Hii inakuja baada ya jana kumchagua Mhe.Samweli Sitta kuwa Mwenyekiti. Mhe Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour. Kura 7 ziliharibika - kama jana. 
   Katibu wa Bunge hilo Maalum ambaye atajulikana wakati wowote kuanzia sasa ataapishwa na Rais Jakaya Kikwete kesho asubuhi Ikulu ndogo Dodoma. 
   Katibu wa Bunge ndiye atakayemwapisha Mwenyekiti na Makamu wake, na Mwenyekiti atawaapisha wajumbe wote, ndipo shughuli itapoanza rasmi ya kuandika katiba mpya. 
  Globu ya Jamii inawatakia heri na fanaka katika zoezi hili la kihistoria
  Mhe.Samia Suluhu  Hassan (anaye angalia kamera)akipongezwa na aliyekuwa mshindani wake Mhe Amina Abdalla Amour  mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
  Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Bunge 
  la Maalum la Katiba mteule Dodoma, akishukuru wajumbe kwa kumchagua  

  Wajumbe kinamama wakishangilia mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kumpata Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma leo
  Hoi hoi na nderemo 
  Chereko chereko...
  Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma

  0 0

  Mhe. Yahya Khamis Hamad Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.

                         Dkt. Thomas Didimu Kashililah, 
                         Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.


  0 0

   MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega. 
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo. 
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.
   Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.

  ===========  ======== ======
  MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,  Ndugu Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

  Akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ndugu Ramadhan Maneno, pamoja na Ndugu Imani Madega, Ridhiwani aliwashukuru wana CCM na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa kumuunga mkono.

  Ridhiwani pia ameahidi kushirikiana na wana-Chalinze katika kutekeleza yote yaliyofanywa na wabunge waliotangulia lakini pia amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa Chadema inayodhihaki kuwa yeye sio mkazi wa Chalinze. 

  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo hilo.

  Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa wagombea kutangaza sera zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa Chalinze.


  Alisema kuwa hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kurumbana na kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa. 

  Alisema hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa tangia mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia wananchi.

  Alisema kuwa kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji ya uhakika, kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi wa maji ya uhakika. 

  Aliongeza kuwa pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya za uhakika za afya kwa wakazi wa eneo la Chalinze. "Najua awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo yanaongezeka"alisema Ridhwani.

  Aliongeza kuwa ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma mbalimbali kama hizo za za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo.

  "Watu wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa. Hapana! Yaani tena hata sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura huku sio! Ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa hapa Chalinze"alisema Ridhiwani.

  Kuhusiana na tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo jukumu kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu imekuwa ikifanya hivyo. Alisema kuwa atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu baina ya wafugaji na wakulima.

  Ndugu Ridhwani anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Said Bwamdogo.


  0 0
 • 03/13/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Mzee mzima Harry Belafonte anakuimbia 'Banana Boat Song'

  0 0
 • 03/13/14--20:08: Article 16


 • 0 0

   Wananchi wa kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama,Iringa Vijijini wakinyanyua mikono yao juu kumuunga mkono Mgombea Ubunge jimbo la kalenga,Ndugu. Godfrey Mgimwa.Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16 siku ya jumapili.
   Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili kuzisikiliza sera za mgombea Ubunge wa Jimbo la kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika kwenye kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama Iringa Vijijini
   Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama Iringa vijijini, akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani yao na kumpa kura za ndiyo siku ya Machi 16,Jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo katika jimbo hilo.
   Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis Lupala akipiga magoti kumuombea kura kwa wananchi mgombea Ubunge wa CCM Bw. Godfrey Mgimwa.
   Baadhi ya Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

  0 0


  THEME: 'SOLVING THE CYBER SECURITY PUZZLE'
  ON: 27TH AND 28TH MARCH 2014
  AT: MLIMANI CITY CONFERENCE CENTER
  FROM: 8.00AM – 5.00PM
  SPEAKERS:
  1. Mr. Luther Martin – Msc. Data Comms, Bsc. ICTM, ADIT, DIT, C|HFI, Data Security Consultant

  2.Prof. Samuel Liles – Consulting Lecturer – University of California
  3. Dr. Peter Obadare (Nigeria) - Forensics Expert

  Chief Guest of Honor: Eng. Prof. Patrick J. Makhungu (PHD) - Permanent Secretary, Ministry of  Communications, Science and Technology

  Conference Goals:
  • To educate the community about protecting information
  • To increase awareness about cyber security threats and risks
  • To sharpen technical skills
  • To present cutting edge information to broaden cyber security professionals' knowledge
  • To present useful sessions that examine an issue, problem, or threat and offer solutions, best practices and lessons learned
  • To ensure participants leave the event with practical information that can be applied to their cyber security environment
  Cost to Attend Conference:
  Tsh: 500,000/participant
  Tsh: 250,000/participant for NGOs
   *Group discount of 20% for 5 or more employees from the same organization
  For more information:

  0 0
 • 03/13/14--21:32: shukurani toka tano ladies
 • TANO Ladies wanatoa shukrani za dhati kwa watu mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhadhimisha sherehe  ya siku ya Wanawake Duniani 2014. Shukrani za pekee kwa Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na wanawake Wajasiriamali walioshiriki kwenye maonyesho:Mitindo Nite, NASHONA,Taste of Tanzania, Farida Cartering, Little Ladies of Diaspora, SHINA INC, IskaJoJo Studios, Computer Repair Services, Nesi Wangu, Bahari Deco. Crafts, Marbella Events Inc, Lucy Nombo, Erica Lulwakwa Glenn na Design by Salha Saleh.  Mwisho ni akina baba na akina mama wote mliokuja kujumuhika nasi siku ya Jumamosi ,Machi 08. Hatuna cha kuwalipa,lakini wema wenu haujaenda bure! Ahsanteni sana kwa kuwa sisi pekee hatutaweza lakini kwa ushirikiano nanyi, tunaweza! Ahsanteni sana.
  Kwa taswira zaidi ilivyokuwa mtembelee IskaJoJo Studios


  0 0

  20140306_152406Joseph Muya captured  with the acting African Development Bank Vice President on the subject of green energy and development in Africa. 20140306_161117Joseph Muya, Alvin Wanyama, pose with Dr, Raymonde Aggousus, the head of HR and Youth Division after candid discussions in her office about the challenges unique to the African Youth and the opportunities that the AU has for the African youth, on her left is Sia Marupa, the TUNZA regional Ambassador. 20140306_161131Glory Blasio and Joseph Muya poses for a light moment in the office of the Head of Youth and HR in the AU on 10th floor in the AU hq. 20140308_085242Youth delegates having fun during the African Village Night event at the Monarch hotel in Addis Abbaba, it was during this event that they shared about their different cultures and exchanged gifts from their respective cultures. 20140308_132422Tuwakuze founder Joseph Muya and TUNZA regional Ambassadors outside Dr, Raymonde Aggousus office. DSC_0038Youth delegates having fun during the African Village Night event at the Monarch hotel in Addis Abbaba, it was during this event that they shared about their different cultures and exchanged gifts from their respective cultures.For more pictures join sundayshomari.com

  0 0
 • 03/13/14--22:21: WAKITETA JAMBO
 • Naibu Katibu mteule wa Bunge Maalum la Katiba,Dkt. Thomas Kashilila (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba aliye maliza muda wake,Mhe. Pandu Kificho. Picha na Deusdedit Moshi.

  0 0

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa akisalimiana na vijana na wananchi kwa jumla baada ya kuwasili leo katika kijiji cha Elandutwa, katika jimbo hilo, Iringa Vijijini kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akimnadi Mgimwa katika Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini, leo.
  Wananchi wa Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini wakionyoosha mikono kuahidi kumpa kura zote Mgomwa katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo.
  Mgimwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kijiji cha wafugaji cha Elandutwa, Iringa Vijijini leo.
  Kinamama wa Elandutwa wakimshangilia mgombea wa CCM katika mkutano wa kampeni.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Ramadhani Mungi akizungumza na Waandishi wa Habari  kutoka vyombo mbalimbali,mapema leo asubuhi kwenye Ofisi zake,kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyohusu kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Kalenga,mkoani Iringa.
  ========   ======  ===========
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI
  JESHI LA POLISI TANZANIA

                                Ndugu waandishi wa habari , kwa niaba ya askari Polisi wa Mkoa wa Iringa, nitumie fursa hii kuwakaribisha hapa ofisini kwetu.

                                Ndugu zangu tumeitana hapa asubuhi hii ili niweze kuwapa taarifa ya usalama katika Mkoa wetu wa Iringa hususani katika Jimbo la Kalenga katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na usalama wa siku ya uchaguzi wenyewe.Ili iwe rahisi kueleweka taarifa hii nitaitoa kwa kifupi sana kwa kuigawa katika maeneo matatu. 

  Eneo la kwanza ni juu ya wapi tunataka tupafikie  ( Where we want to go ), eneo la pili ni lile la wapi tulipo ( Where are we? ) na eneo la tatu ni jinsi gani tutafika huko ( How do we get there ). Tuanze    na  wapi   tunataka   tupafikie. Sisi  Polisi  Mkoa  wa  Iringa  tunataka  wananchi  wa  Kalenga  wapinge  kura  kwa  amani  na  utulivu  mkubwa   siku  ya   jumapili  tarehe  16/3/2014. Hii   ndio  dila  yetu  na  tutahakikisha  tunafika  hapo.

  Kuhusu  wapi  tulipo  sasa, naomba   niwaelezeni  kwa  ufupi  sana  matukio  ya  kijinai  kuanzia  tarehe  19/02/14  mpaka   leo. Ndugu  zangu, kuanzia   tarehe  hiyo  mpaka  tarehe  2/03/2014  takribani  wiki  mbili  hakukuwa  na tukio  lolote  la  uvunjifu  wa  amani   lililokuwa  limepokelewa  katika  vituo  vyetu  vya  Polisi. 

  Hali  ilianza  kubadilika  tarehe  3/3/2014  ambapo  baadhi  ya  waandishi  walifika  ofisi  kwangu  na  kunieleza  kuwa  kumetoka  kwenye  mkutano  wa  CHADEMA  ambapo  wameelezwa  na  chama  hicho  kuwa   usiku  wa  siku  hiyo   walimkamata  mtu  mmoja  kwa  kosa  la   kujaribu  kuchoma  moto  nyumba  waliokuwa  wakiishi  wafuasi   wao  katika  kijiji cha  WASA. 

  Waandishi  hao  walinitaka  nithibitishe  kutendeka   kwa  kosa  hilo  na  walieleza  kuwa  wameelezwa  kuwa  bado  halijaripotiwa  kituoni. Mimi  nilikataa  kusema  lolote  kuhusu   hilo  kwani   lilikuwa  bado  halijaripotiwa  Polisi.  

  Tarehe  4/03/2014  nilifuatwa   tena  na  baadhi  ya  waandishi  na  kunieleza  kuwa  siku  hiyo  waliitwa  na  CCM   na  kuelezwa  kuwa  siku  ya  tarehe  27/2/2014  walitegewa  misumari  katika  kijiji  cha  WASA  ili  mabasi   yaliyokuwa  yamebeba   wafuasi  wao  yaweze  kutobolewa  magurudumu  yake, pia  nao  walisema  tukio  hilo  halijaripotiwa  Polisi. Mimi  nilikataa  kulizungumzia   swala  hilo.

  Ndugu wanahabari,  vitendo   vilivyofanywa  na  vyama  hivyo  vililenga  kuanzisha  propaganda  za   kisiasa   kwa   kutumia  uhalifu  kwa   kupitia  vyombo  vya   habari. Sisi   Polisi  tulibaini   hali  hiyo  na  ndiyo  sababu  tuliamua   kuwa  kimya  na  nyinyi  wenzetu  kwa  kuzingatia  maadili  ya  kazi  zenu  pia   mlikaa  kimya.     Kuanzia  hapo  vyama   vilianzisha   mashindano  ya   kuripoti  kesi  zao  Polisi. Leo  hii  vyama  hivyo  vimeripoti  kesi  ishirini  na  moja   ambazo  zilisababisha kukamatwa kwa wafuasi (19) wa vyama hivyo viwili.

  Ndugu waandishi, kati ya kesi hizo ishirini na moja, kesi kumi na tisa (19) zile ambazo hazina madhara ya moja kwa moja kwa binadamu ama mali, kesi hizo ni  zile ndogondogo sana, kama vile kuchana mabango, kuteremsha bendera, kuchana vipeperushi, kutukanana n.k. kesi tatu zilikuwa zile zenye madhara kwa binadamu na mali ambazo ni kupigana hadharani, kujeruhi na kuharibu mali. Kati ya kesi ishirini na moja (21), kesi kumi upelelezi wake umekamilika na majalada yake yamefikishwa kwa mwanasheria wa serikali.
                                
  Ndugu waandishi, katika kesi hizo Polisi tumeibaini mengi mfano CHADEMA kilikuwa kikitoa malamiko kuwa tumeacha kumkamata ndugu hassan mtenga mtuhumiwa wa kesi moja iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake. Shutuma hizo hazina msingi kwani kesi iliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo haikuwa ya jinai bali ya madai na tuliwajulisha hivyo. Nia ya kufanya hivyo ilikuwa kuifanya jamii iamini kuwa Polisi ni dhaifu na wenye kuonyesha upendeleo katika kushughulikia kesi za uchaguzi. Nashukuru Polisi tulikuwa watulivu, hatukujibu na jamii imetuelewa sana.

  Ndugu waandishi, sijui mlijulishwa na nani kwamba Padri mmoja alifungwa kamba na alipingwa na kuburuzwa. Nanyi bila ya kuthibitisha kwetu mkaandika habari hiyo. Tuwaeleze kuwa mtu huyo ni miongoni mwa watuhumiwa tuliowakamata katika moja ya makosa yaliyotendeka, tulimhoji, aliandikwa maelezo yake na alipewa dhamana. Hata siku moja hajawahi kutoa taarifa Polisi juu ya matukio aliyotendewa. Nia ya kutangaza taarifa hiyo ni kuzua hofu kwa wananchi na kutaka kuchochea chuki kwa wafuasi wa dhehebu lake na wale wa dini yake.

  Ndugu waandishi, pamoja na matukio hayo polisi tumekuwa tukipokea taarifa za vitisho vya kuwepo kwa watu mbalimbali kutoka kwa vyama vyote walioingizwa mkoani humu kwa nia ya kutenda vitendo vya uvunjifu wa amani. Aidha, tumewasikia viongozi wa vyama wakitamba kuingiza maelfu ya watu mkoani mwetu. Kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Mbeya kwa visingizio vya kulinda kura.

  Sasa nataka niwaeleze kuwa sheria iko wazi kabisa, kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na wakala wa chama kinachoshiriki katika uchaguzi huo na hao ndio wawakilishi wa chama hicho na walinzi halali wa uchaguzi ni askari wa Jeshi la Polisi. 

  Kufuatia hali hiyo mambo yafuatayo yanasisistizwa sana.
  1.   Hatutaki kuona walinzi wa chama  chochote  katika Jimbo la Kalenga. Jukumu la kulinda uchaguzi, maisha na mali ya wana Kalenga ni la JESHI LA POLISI.
  2.   Hatutaki kuona watu wasiokuwa na shughuli maalumu wanapitapita katika maeneo ya kupigia kura.
  3.   Siku ya uchaguzi si siku ya kampeni. Hatutaki kuona helikopita za  vyama  vyote  zenye kuashiria kufanya kampeni.

  Nawaasa watu wote hasa wale waliotoka nje ya Iringa, sisi huku Iringa tunapenda sana amani kuliko kitu chochote kile hivyo ikiwa wameletwa kama MAJESHI YA KUKODIWA ili kuharibu amani ya Kalenga kama walivyozoea kufanya huko walikotoka, Sisi Polisi na wana Kalenga tupo imara, tumejipanga vizuri kukabiliana nao.

  Aidha, napenda kuwatoa hofu wana kalenga, wasiwe na wasiwasi kabisa, sisi Polisi Iringa tupo imara na tumejipanga vizuri katika kuwalinda kikamilifu. Nawaomba wajitokeze kwa wingi sana siku ya kupiga kura na wapige kura zao kwa uhuru kabisa.

  Ndugu waandishi, nawashukuru sana kwa jinsi mlivyofanya kazi zenu kwa ueledi mkubwa. Hata siku moja hatujawahi kusikia ama kusoma habari za uchochezi kwa kushabikia chama chochote kile.


  AHSANTENI SANA.

older | 1 | .... | 386 | 387 | (Page 388) | 389 | 390 | .... | 3270 | newer