Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Balozi Seif Ali Iddi asaidia vifaa vya ujenzi kwa Ofisi ya CCM Tawi la Kazole, Kaskazini Unguja

$
0
0
Othman Khamis Ame, OMPR
Zaidi ya asilimia 95% imefikiwa katika ujenzi wa Matawi ya Kisasa ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Jimbo la Kitope liliomo katika Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Hali hiyo imekuja kufuatia hatua za ukamilishaji wa Linta katika Tawi la Chama cha Mapinduzi la Kazole likiwa miongoni mwa Matawi 19 ya Kisasa yaliyo kwishajengwa kati ya Matawi 20 yaliyomo ndani ya Jimbo hilo. 
Katika kuunga mkono harakati za Wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la Kazole za ukamilishaji wa ujenzi wa Tawi lao Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi vifaa mbali mbali kwa ajili ya ukamilishaji wa linta na baadaye kujiandaa kwa uwezekaji. 
Balozi Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wanachama hao wa Tawi la CCM Kazole wajitahidi kukamilisha kazi hiyo ili wao pamoja na Uongozi wa Jimbo hilo ujizatiti katika hatua ya uwezekaji. 
“ Ukweli nimefarajika sana kuona kwamba ile kiu yangu ya muda mrefu ya kuona Matawi yetu 20 yaliyomo ndani ya jimbo letu yanakamilika kujengwa katika mfumo wa kisasa kabla ya mwaka 2015 “. Alifafanua Balozi Seif. 
Alisema Chama cha Mapinduzi wakati wote kimekuwa kikisisitiza wanachama wake Nchini kote kuendelea kujenga Ofisi za kisasa zenye hadhi ya Chama chao zikienda sambamba pia na uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi kwenye Ofisi hizo. 
Balozi Seif aliwatahadharisha wanachama hao wa Chama cha Mapinduzi kujiepusha na tabia za fitna ambazo zikiendekezwa zinaweza kusababisha mpasuko miongoni mwa wanachama wenyewe kitendo ambacho kinaweza kupunguza nguvu za chama hicho kikongwe Nchini. 
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alielezea matumaini yake kwamba juhudi za ziada zitachukuliwa ili kuona Tawi la CCM la Kijiji cha Boma lililobakiika kati ya Matawi 20 yaliyomo kwenye Jimbo hilo nalo linakamilika kujengwa. 
Mbunge huyo wa Jimbo la KitopeBalozi Seif alikabidhi vifaa vya ujenzi kukamilisha hatua ya linta ya Tawi hilo la Kazote ambavyo ni pamoja na Nondo,Matofali, Saruji na Kokoto. Pia alikabidhi Shilingi Laki 200,000/- za Fundi pamoja na Fedha taslimu kwa Kikundi cha Ushirika cha kuweka na kukopa vyote hivyo vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 1,700,000/-. 
 Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo jipya la Tawi la Chama cha Mapinduzi la Kazole kabla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya hatua ya ukamilishaji wa Linta. Nyuma ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
 Balozi Seif Akimkabidhi Vifaa mbali mbali  vya ujenzi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kazole Nd. Sharif Makame Kundi ili kukamilisha hatua za linta.
 Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akimkabidhi fedha Taslim Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kazote Nd. Sharif Makame Kundi kwa ajili ya fundi wa ujenzi wa Tawi hilo katika hatua ya Linta.
 Balozi Seif akizungumza na Wanachama wa CCM Tawi la Kazole mara nbaada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya Tawi hilo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

KATIBU WA MKUU WA CCM,KINANA AFUNGA KAMPENI KWA KISHINDO JIMBO LA KALENGA JIONI YA LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia Wananchi wakati wa kufunga Kampeni za Uchaguzi wa jimbo la Kalenga jioni ya leo,katika kijiji cha Kidamali,kata ya Nzihi Iringa vijijini.
 Mkutano wa kufunga kampeni ukiendelea kwenye kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi jioni ya leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama hicho,Ndugu Godfery Mgimwa,wakati wa mkutano wa kufunga kampeni katika jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mkoani Iringa.Uchaguzi wa jimbo la Kalenga unafanyika kesho siku ya jumapili,Machi 16,kuziba pengo la aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,Waziri wa Fedha na Uchumi,Marehemu Dk.William Mgimwa.
  Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke wake,Bi.Robby Mgimwa kwa wananchi wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,ambako kumefanyika mkutano wa kumfunga kampeni jioni ya leo.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini  na Mtangazaji wa Radio One na ITV,Godfrey Gondwe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa wakiwapungia mikono wananchi jioni ya leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho.
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa akiwa amebebwa juu juu na Wafuasi wa chama hicho,mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kufunga kampeni za cha hicho,zilizofanyika katika kijiji cha Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa vijijini.

modern operating theatre to save lives of women, children in inaugurated in Rukwa region

$
0
0
Minister of Health and Social Welfare, Dr. Seif Rashid, inaugurated a building to accommodate state-of-the art operating theatre at the Mtowisa Health Centre in Sumbawanga district, Rukwa region at the climax of the national White Ribbon Day celebrations. 
 The theatre has been constructed by the Wazazi na Mwana programme which is being jointly implemented by Plan International, Africare and Jhpiego in both Rukwa and Mwanza regions with financial support from the Government of Canada and Plan International. 
The programme is being implemented through an integrated approach involving community and facility-based Maternal, Newborn and Child Health-MNCH programming, supporting the Government of Tanzania to implement multiple strategies addressing MDGs 4 and 5-the main objective being to reduce maternal, neonatal and child mortality amongst underserved populations in Tanzania. 
 The operating theater has cost a total of USD 317,500 to construct, for the building, provision of electricity and water supply for the operating theater. To supplement the equipment and supplies already present at Mtowisa, Wazazi na Mwana will be providing additional items including patient stretcher, aenesthesia stool, heavy duty suction machine, cesarean section sets, theater gowns and surgeon boots, baby weighing scale, and resuscitator masks for adults and children, among other necessary accompanying items. 
As part of support to the facility, staff from the Mtowisa Health Centre will also be provided with training on Comprehensive Emergency Obstetric and Newborn Care(CEmONC) in order to equip them with skills to perform cesarean sections for safe delivery of babies. 
Minister of Health and Social Welfare, Dr. Seif Rashid,  cuts the ribbon to inaugurate th e building to accommodate state-of-the art operating theatre at the Mtowisa Health Centre in Sumbawanga district, Rukwa region.
Minister of Health and Social Welfare, Dr. Seif Rashid,  unveils a plaque to inaugurate th e building to accommodate state-of-the art operating theatre at the Mtowisa Health Centre in Sumbawanga district, Rukwa region.

MKUU WA MKOA WA DODOMA AONGOZA MATEMBEZI KWAAJILI YAKUAMASISHA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI MKOANI DODOMA LEO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), akikata utepe kufungua matembezi kwa ajili ya maji, yaliolenga kuihamasisha jamii kuhusu utunzaji wa miundombinu ya maji nchini.yaliofanyika katika kata ya Chibelela wilayani Bahi  Machi 15, 2014 (katikati), ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, na kulia Mwenyekiti wa Kijiji cha Chibelela, Dorice Mkwawa.  KWA PICHA ZAIDI NA PHILEMON SOLOMON WA  DODOMA BOFYA HAPA

introducing 'Show Me Love' by BQ & KIMO

$
0
0
Dear all, 
 Introducing to you Bongo Fleva artists called BQ & Kimo. These are two artists who work together as a team. BQ & Kimo belong to a group called Sababisha Empire. T
he artists are residing in Tegeta Chanika (behind Kibo Complex). BQ & Kimo have been in the game for quite sometime now (since 2008), although they have never been able to successfully penetrate it all these years. 
This time, however, they are determined to make it to the top. Among the songs they have released over the years include Check Nyuma, Acha Choyo, Unataka hiki unataka kile, Bongo fleva time, and many more.  Artists: BQ & Kimo 
Title: Show Me Love 
Studio: Mj Records 
Video: Kallage Pics

RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA HARAKATI ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

$
0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014, wakati akiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa wakazi wa Kijiji cha Miono,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano ya Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi (kulia) akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kabla ya kumpatia kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wanakijiji wa Kimange.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKUTANO WA MASWALA YA ULINZI MTANDAO WAKAMILIKA KWA KUPIGILIA MSUMARI KAULI MBIU “MWAKA 2014 NI MWAKA WA VITENDO”

$
0
0
Akizungumzia mkutano huo bwana Yusuph Kileo ambaye aliongoza timu ya maandalizi ya mkutano huo alibainisha hayo na kueleza mkutano huo umekamilika salama ambapo mambo mbalimbali yalipata kujadiliwa yahusuyo ulinzi mtandao “Cyber security” na kupigilia msumari kauli mbiu ya mwaka 2014 kua ni mwaka wa vitendo. 
Mwanzo wa mkutano bwana Craig Rosewarne (Mwenyekiti wa kundi linalojiuhisisha na maswala ya ulinzi mtandao (ISG) katika nchi za afrika ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni Wolfpack inayo jihusisha na maswala ya ulinzi mtandao na mkurugenzi wa SANS ukanda wan nchi za Afrika na mashariki ya kati) alianisha hali ilivyo sasa na kusema kumekua na wimbi kubwa la makosa mtandao ambapo kila mwaka yanaongezeka kasi huku akitolea mifano mbali mbali ya matukio ya hivi karibuni. 
Aidha alipata kuanisha ukuaji wa teknologia ambapo inaendelea kukua kwa kasi na inavyo ongeza uwezekano wa kasi ya uhalifu mtandao kukua endapo jitihada za dhati hazitowekwa tayari ili kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma vita dhidi ya ulinzi mtandao. Akitolea mifano changamoto mbali mbalizinazopelekea ugumu katika ulinzi mtandao alianisha changamoto hizo ikiwa ni pamoja na:- 
1. Uhaba wa programu za kompyuta salama kimtandao huku akitolea mifano baadhi ya program za komputa zinavyo tengenezwa kutoa mwanya kwa wahalifu kupa urahisi kuingilia komputa za watumiaji wa program hizo 
2. Kutokuwepo na makubaliano ya pamoja ya kisheria katika mapambano dhidi ya makosa mtandao. 
3. Kutokuwa na ushirikiano wa kuunganisha nguvu kati ya serikali mbali mbali na sekta binafsi kutokomeza uhalifu huu ambao unaendelea kukua kwa kasi. 
4. Kutokua na elimu kwa jamii juu ya makosa mtandao na jinsi ya kukabiliana nayo katika ngazi ya ya mtu mmoja mmoja. 
5. Kutokuwepo na utayari kwa kuunda timu katka nchi mbali mbali zenye uwezo wa kukabiliana na uhalifu mtandao.
Kwa upande mwingine Bwana Martin Euchner kutoka ITU (International telecommunication union) wakala wa umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya mawasiliano alianisha hatua mbali mbali mbali ambazo hadi sasa ITU imekua ikizichukua ili kujaribu kuunganisha nchi zote za umoja wa mataifa ili kwapamoja ziweze kupambana kupunguza uhalifu mtandao. 
Pia alipata kuzungumzia jitihada za dhati na mafanikio yaliyo patikana kupitia mpango wa COP (Child Online Protection) ambao umejikita kuhakiki watoto wanabaki salama mtandaoni, kauli iliyo ibua hoja nzito ya mchezo unao patikana kwenye simu hivi sasa ujulikanao kama “Talking angela” ambao umekua unachezwa na watoto wengi wadogo mtandaoni chezo ambao ume ukitiliwa shaka unaweza kuwa unatumika vibaya na wahalifu mtandao ili kukusanya sauti za watoto na picha zao zinazoweza kutumiwa vibaya baadae. 
Aidha bwana Eucner, aliweza kuzungumzia mpango kabambe ambapo mapitio na kuangalia kwa karibu changamoto mtandao katika nchi mbali mbali katika mwaka huu wa 2014 zinategemewa kufanyika katika nchi takriban 16 Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zitakazo weza kufaidika na mpongo huo.
 Kwa upande wa bwana Kileo, Aliweza kufafanua kwa kina uhaba mkubwa wa wataalam wa maswala mtandao katika ngazi ya kidunia kwa sasa na mahitajio ya wataalam imekua ni kubwa huku akitolea mfano katika nchi zilizo endelea kuwa na mikakati kabambe ya kuunda jeshi Mtandao ili kukabiliana na vita mtandao maarufu kama “Cyber war”. 
Bw. Kileo aliasa washiriki kuendelea kufahamu yakua swala la mitandao ni swala lisilo na mipaka ya kijografia na linaweza kufanywa na mhalifu kutokea maeneo yoyote bila kujali anadhuru nchi gani hivyo nguvu ya pamoja ni muhimu sana ili kuweza kukabiliana na hali mbaya iliyo sasa.
 Picha Ya pamoja ya waandalizi wa mkutano wa maswala ya ulinzi mtandao wakiwa katika mapunziko ya chakula cha mchana kabla ya kuendelea katika sehemu ya pili ya mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano huo ambapo ulipigilia msumari kauli mbiu iliyoainisha Mwaka 2014 uwe ni mwaka wa vitendo.
Yusuph kileo (kati) akiwa pamoja na Bwana Craig Rosewarne (kushoto) na Martin Euchner kabla ya kuelekea ukumbi wa mkutano

kagera sugar yaichapa Tanzania prisons 2-1 leo bukoba

$
0
0
Kikosi cha Kagera Sugar

Na Faustine Ruta, 
Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea leo na hapa Mjini Bukoba tukishuhudia Timu ya Maafande kutoka Jijini Mbeya ikinyukwa bao 2-1 na  wenyeji Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba. 
Kipindi cha kwanza Tanzania Prisons ndio walipata bao kupitia kwa mchezaji wao Peter Michael katika dakika ya 37 baada ya kuwachambua kama karanga mabeki wa Kagera Sugar na kuachia shuti kali na kumfunga kipa wa Kagera Sugar. 
Mpaka dakika za mapumziko Tanzania Prisons ndio wameenda kupumzika wakiwa mbele ya Bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.Kipindi cha pili dakika ya 55 Kagera Sugar walipata penati na mkwaju huo ulipigwa na Salum Kanoni na kupata bao la kusawazisha. 
Katika dakika za lala salama dakika ya 88 Kagera Sugar walipata bao la ushindi lililofungwa na Benjamini Asukire kwa shuti kali ndani ya eneo hatari la penati nakufanikisha Timu yao kuibuka na ushindi wa bao hizo mbili.
Kikosi Cha Timu ya Tanzania Prisons kilichoanzaWaamuzi wa Mtanange huu wa Kagera Sugar na Tanzania Prisons ya jijini Mbeya
Kipute kimeanza kipindi cha kwanza...

YANGA YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 na MTIBWA SUGAR LEO MJI KASORO BAHARI

$
0
0

Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Iliyoanza Leo Dhidi Ya  Yanga.
Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema 
Kikosi cha Timu ya  Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja. 









Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi  Yanga ya Dar es Salaam . 
Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.
Timu ya   Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini walishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan  na Kuingia Said Dilunga, na Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia  Husein Javu. Lakini haikiusaidia kitu...
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji wao Abdalah Juma  alipooneshwa Kadi Nyekundu kwa kuchezea rafu mbaya.






 Mashabiki wa Timu ya  Yanga waliojitokeza kwa Wingi katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani morogoro
Benchi la Timu ya Soka ya Mtibwa ya Morogoro  Likiongzwa na Kocha wa Timu Hiyo  Meky Mexime wa kwanza Kushoto..
Makocha wa  Yanga 
Mashabiki waliojitokeza kwa Wingi Katika Uwanja w Jamhuri Mkaoni Morogoro Leo Katika Mcheza Kati ya Yanga Dhidi ya Mtibwa Sugar 
Mshambuliaji wa Timu ya  Yanga Emanuel Okwi akitafuta Mbinu za Kufunga katika Lango la Timu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro.
Moja ya Purukushani katika Lango la Timu ya  Yanga Katika Mchezo Uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro  
Mchezaji wa  Yanga Simon Msuva Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Timu ya Mtibwa Sugar Paul Ngalema 
Patashika kwenye lango la Yanga wakati wa kona.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mkipuuza kanuni, tusilaumiane,' Sitta alionya Bunge la Katiba

$
0
0
Courtesy of Mwananchi Communications Limited (MCL)

ujumbe

BREAKING NEWZZZZZZZ:MBUNGE WA CHADEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI IRINGA AKITUHUMIWA KUGAWA FEDHA KWA WANANCHI

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili, ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini kwa tuhuma za kugawa Fedha kwa wanakijiji hao, akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria. PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-IRINGA.

MANNY CHUGA AJIANDAA KUMKABILI SELEMANI MOTTO MARCH 23

$
0
0


Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kushoto  akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga' jinsi ya kupiga ngumi kwa shabaha wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam 


Kocha wa mchezo wa ngumi Waziri Chara (kushoto ) akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga'  jinsi ya kupiga begi wakati wa mazoezi yake makali yanayofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam 
Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kushoto  akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga' jinsi ya kupiga ngumi kwa shabaha wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam. Picha na Super D

uzee mwisho wake ....?

$
0
0
Mlioko huku wote ma-Bebi...tehe tehe tehe....Inasemekana wazee wa Chalinze wamekata rufaa kutaka mpaka uwe Morogoro....

Article 24


Mkandarasi wa mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka aruhusu maeneo ya kugeuzia magari

$
0
0
 MSHAURI Mkuu wa Ufundi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Bwana Dieter Schelling (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (ambao hawapo pichani) eneo la Kimara kuwa Kampuni ya STRABAG kuruhusu vituo tano vitumike kugeuzia magari (U-turns) mpaka vituo vya kudumu vitakapokamilika ndani ya miezi sita. Kushoto ni Mhandisi wa DART, Mhandisi John Shauri.   
Sehemu ya barabara ya Morogoro 
road maeneo ya Kimara

KAMPUNI ya ujenzi wa barabara ya STRABAG  inayoendelea na ujenzi kwa ajili  ya mradi wa mabasi yaendayo haraka umeruhusu upande mmoja wa barabara uliokamilika kutumika ili kupunguza foleni  ya magari yanayoka Kimara kuelekea katikati ya jiji au sehemu nyingine kupitia  barabara ya Morogoro.  


Mhandisi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART),Mhandisi John Shauri aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwamba mbali ya kuruhusu upande mmoja wa barabara, kampuni ya STRABAG imeruhusu pia vituo vitano vitumike kwa kugeuzia magari kwa muda wa miezi sita (provisional U-turns) mpaka maeneo matatu ya kudumu yatakapo kamilika katika kipindi hicho.

“Kuruhusu upande mmoja kutumika na pia maeneo ya kugeukia magari kumesaidia sana kupunguza foleni kwa magari yanayotoka kimara kwenda Ubungo nay ale yanayotoka Ubungo kwenda Kimara,”alisema Mhandisi Shauri.

Mhandisi huyo amewataka madereva kuwa waangalifu na mwendo kwani wastani wa mwendo unaotakiwa ni spidi 50 tu na si vinginevyo kwani mwendo kasi utasababisha ajali zisizo za lazima.

“Mwendo wa kawaida utasaidia sana maeneo ambayo yameruhusiwa magari kugeuka na na kuelekea sehemu husika bila kusababisha ajali,” alisema na kuongeza kuwa mradi utakapokamilika utapunguza kabisa foleni na msongamano wa magari.

Mhandisi Shauri ambaye aliambatana na Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi huo, Bwana Dieter Schelling, alivitaja vituo hivyo vitano vya kugeuzia kuwa ni Kimara Corner,Kimara Baruti, katikati ya Kimara Butcher na Kimara kwa Thomas, Kimara Resort na Kimara mwisho.

“Kwa sasa magari katika barabara hii ya Morogoro magari yanapita pasipo msongamano mkubwa kama ilivyokuwa awali na kurahisisha watu kutoka Mbezi,Kibamba kuwahi kwa wakati katika shughuli zao,” alisisitiza mhandisi Shauri.

Amesema wakati ujenzi ukiwa unaendelea vyema daladala zingeendelea kupita/kutumia barabara za pembeni (access roads) badala ya kutumia barabara kubwa kwani itapunguza sana msongamano.

“Katika kipindi hiki usimamiaji wa zoezi hili linahitaji kuungwa mkono na askari wa barabarani ilikuwadhibiti madereva wote wanaotembea kwa mwendo kasi ilikupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Kwa mujibu wa mhandisi Shauri, vituo vya kudumu vya kugeuzia (permanent U-turns) vitajengwa Kimara Baruti, Kimara Butcher na Kimara Mwisho.

Mradi huo mkubwa wa ujenzi unasimamiwa na Wakala wa Usimamizi wa Barabara nchini (TANROADS). DART ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


Hivi karibu waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya  mradi wa mabasi yaendayo haraka ambapo aliridhishwa na maendeleo ya ujenzi unaofanywa na kampuni ya STRABAG kutoka ujerumani.

wajumbe wa bunge maalum wahitimisha zoezi la kuapa kwa muda uliopangwa

$
0
0
 Mwenyekiti wa i wa Bunge maalum, Mhe.Samwel Sitt akiahirisha bunge hadi Jumatatu mara baada ya zoezi la kuwaapisha wabunge. Wajumbe ambao hawajaapishwa ni wale waliopo nje ya mkoa wa Dodoma kwa udhuru, na wataapishwa wiki ijayo.
 Wajumbe wa Bunge maalum Mhe,Anne Kilango Malecela (shoto) akijadiliana jambo na Mhe.Beatrice Shelukindo wakati wa zoezi la kuapisha wabunge.
 
 Waheshimiwa, Zakhia Meghji, Zarina Shamte Madabida na Zaynabu Matitu Vullu wakisubiri zamu yao ya kuapishwa wakiwa ni wajumbe wa mwishoni kuapa  kwa kufuata utaratibu wa alfabeti za majina yao ya kwanza yanayoanza na "Z".
 
 Wajumbe wa Bunge maalum la katiba wakishuhudia wenzao wakiapa

  Wajumbe wa Bunge maalum la katiba wakishuhudia wenzao wakiapa
 Wajumbe wa Bunge maalum la katiba wakishuhudia wenzao wakila kiapo. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma

zoezi la upigaji kura kuchagua mbunge wa jimbo la kalenga laendelea kwa utulivu

$
0
0
Wananchi  wa Nyamihuu wakiwa wamepakizana katika  boda boda  kwenda  kupiga kura
Wananchi  wa Kidamali  wakiwa katika foleni ya kwenda  kupiga  kura
mmoja kati ya  wazee  eneo la Nzihi akitoka  kupiga kura  kumchagua mgombea anayemtaka
Wananchi  wa Nzihi  wakiwa katika  foleni wakisubiri kupiga  kura

BONDIA FADHILI AWADH AFARIKI

$
0
0
Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya Mwananyamala jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa siku kadhaa. 
Marehemu Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza  mpambano wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka Tanga Alan Kamote, na  alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo. 
Sababu ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa Mwananyamala kwa kiongozi wa ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya  mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. 
Fadhili awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali. 
Shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.
Sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi,
Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “Tiger” peponi 
 AMINA

VODACOM TANZANIA YATOA MSAADA YA MIAVULI 20 KWA JESHI LA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akifungua mmoja ya miamvuli(20)kabla ya kuikabidhi rasmi kwa Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa(kulia) msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa  akipokea msaada wa miamvuli(20)kutoka kwa Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,wanaoshuhudia wa pili kutoka kulia ni Tumaini  Kimaro, Simoni Lugangila na Emmanuel David. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images