Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 385 | 386 | (Page 387) | 388 | 389 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.
  Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.


  0 0

  Chinese netizens have mocked reports that the Malaysian government invited a witch doctor to help hunt for the missing state carrier's plane amid increasing criticism of the search and rescue operation.

  Malaysian media reported that Ibrahim Mat Zin, a famous “bomoh” [shaman] also known as the Raja Bomoh Sedunia Nujum VIP, performed a prayer at Kuala Lumpur International Airport on Monday to help locate the missing MH370, allegedly at the invitation of one of the country’s top leaders.

  “I think the plane is still in the air or has crashed into the sea,” he was quoted by Free Malaysia Today as saying.

  Cynical Weibo users in China ridiculed the conclusion. “Wow, that is exactly what I think too,” many wrote.

  One user who claimed to be Malaysian wrote: “I feel so ashamed as a Malaysian for the first time, not because of any wrongdoing on Malaysia’s part but for having a brainless prime minister.


  0 0

   Taarifa ya Uhakika iliyotufikia hivi punde ndani ya Ofisi za Globu ya Jamii,inaeleza kuwa Kivuko cha Mv. Magogoni kinachovusha watu na mali zao kutoka Magogoni - Kigamboni jijini Dar es Salaam,kimepatwa na kwikwi jioni hii baada ya kukatika kwa sehemu ya mkono unaoshika mlango wa upande mmoja wa kuvushia magari na waenda kwa miguu.Utaratibu wa kutengeneza Kivuko hicho unafanywa hivi sasa na Mafundi wa Kivuko huku Abiria wakiwa wamesimama pembeni kusubiria utaratibu mwingine.
  Sehemu ya Abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho wakiwa wamesimama pembeni kusubiria Kivuko kingine.

  0 0

  Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 487 dhidi ya mpinzani wake, Mhe. Hashim Rungwe aliyepaya kura 69 kati ya kura 593 zilizopigwa, na saba kuharibika katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita Bungeni mjini Dodoma. Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu. Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.
   Wajumbe wakipiga kura 
   Upigaji kura ukiendelea
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo
  Hongera sana sana....anaambiwa mshindi
  Mikono ya pongezi yazidi kumiminika
  Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Katika ulimwengu wa leo neno blog siyo kitu kigeni, leo hii karibu kila mtumiaji wa internet anayo blog yake. Blogu hizi kuna zile zinazotembelewa na watu wengi na kuna zile zinazopata watembeleaji kwa mdondo.

  Je umewahi kujiuliza kwanini watu hawatembelei blog yako kama wanavofanya kwa blog fulanifulani? Ingawa kuna sababu nyingi kama umri wa blog, umarufu wa mmiliki wa blog nk lakini kuna kuna vitu ambavyo unaweza kuvifanya na vikakuongezea idadi ya watembeleaji.

  Hivyo kwenye makala ya leo tutaangalia ni vitu gani vya msingi kuzingatia ili blog yako ivutie wasomaji wengi zaidi.

   1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.

  Kama umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule.

   Ingawa ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi (blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi, ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.

  Siyo tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.


  0 0

  Na Mwandishi Maalum 

   Uingereza imeeleza kuwa , mkutano wa kimataifa uliofanyika mwezi uliopitia jijini London, Uingereza na kujadili namna ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyama pori duniani, haukulenga kumnyoshea kidole mtu yeyote.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Balozi Peter Wilson wakati wa mkutano wa kundi la nchi marafiki kuhusu ujangili na biashara haramu ya wanyamapori.

  Mkutano huo ulifanyika siku ya jumatano katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa, chini ya uenyekiti- weza wa Wawakilishi wa Kudumu wa Gabon na Ujeruman. Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Balozi Tuvako Manongi alikuwa mmoja wa washiriki wa kundi hilo la nchi marafiki.

  Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilisha mawazo miongoni mwa marafiki wa nchi hizo ambazo zimefika 20. kuangalia ni kwa namna gani juhudi hizi za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya wanyama pori zinaweza kuungwa mkono ndani ya Umoja wa Mataifa lengo likiwa ni kuzipa juhudi hizi msukumo wa kisiaza pamoja na ushiriki mpana zaidi.

  Naibu Muwakilishi Balozi Wilson aliombwa kutoa muhtasari wa matokeo ya mkutano huo wa kimataifa uliofanyika mwezi wa februari. Ambapo alianza kwa kusema, “ kwanza ningependa kulieleza hili, mkutano ule hakuwa wakunyosheana vidole, tuliuitisha kwa lengo la kujadiliana ni kwa namna gani tutashirikiana katika kuikabili biashara hii haramu ya wanyamapori pamoja na ujangili”.

  Kwa ujumla Balozi Peter Wilson, aliwaambia wajumbe wa nchi hizo marafiki dhidi ya ujangili na biashara haramu ya wanyamapori kwamba mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa kuliko walivyokuwa wametarajia.

  Akaeleza kuwa mwitikio wa ushiriki ulikuwa mkubwa sana, zaidi ya nchi 50 zilishiriki wakiwamo marais watatu, akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mashirika ya Kimataifa.

  Akasema kuwa mkutano huo ulitoka na tamko lenye nguvu ambalo linazungumzia mambo mengi yakiwamo uimarishiji na uboreshaji wa sheria na sheria za makosa ya jinai, uwezeshwaji wa jamii zinazoishi katika maeneo ya wanyamapori kama sehemu ya kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu.

  Akaongeza kuwa tamko hilo pia linazungumza udhibiti wa hitajio na soko la pembe za tembo na raslimali nyingine zitokanazo na wanyamapori na akazitaka nchi nyingine ambazo hazikuhushuria mkutano huo kuunga mkono tamko hilo.

  Akabainisha kwamba viongozi kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, walionyesha ushirikiano mkubwa na pia wao wenyewe walitoka na mpngo mkakati wao wa kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya wanayapori ikiwamo mikakati ya kuwalinda tembo Naibu Muwakilishi huyo wa Uingereza pia ameeleza kwamba viongozi wakuu wa serikali yake pamoja na Mwanamfalme wote wameonyesha utayari mkubwa katika kukabiliana na changamoto hii. Aidha nchi kadhaa zikiwamo Marekani, Canada na Jumuiya ya Ulaya zimetoa ahadi za kuchangia raslimali fedha kusaidia juhudi hizo.

  Wazungumzaji wengine katika mkutano huo walikuwa ni watendaji kutoka CITES, UNODC na UNEP ambapo katika ujumla wao, walieleza kwamba ili juhudi za kuukabili ujangili na biashara haramu ya wanyapori ziweze kufanikiwa lazima pawepo juhudi na ushirikiano wa kimataifa.

  Walieleza kwamba, ni kujidanganya kwamba nchi moja moja inaweza yenye peke yake kukabiliana na hatimaye kuumaliza ujangili na biashara haramu ya wanyamapori kutokana na ukweli kwamba, ujangili na biashara hiyo haramu mtandao wake ni mkubwa wenye sura ya uharifu wa kimataifa.

  Baadhi ya wajumbe akiwamo Balozi Manongi, waliunga mkono umuhimu wa kundi hilo la marafiki kutakafari mbinu na mikakati ya kupata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka ndani ya Umoja wa Mataifa. Na pia akasisitiza hoja ya udhibiti wa soko na hitajio la raslimali zitokanazo na wanyamapori.

  Balozi Manongi akaeleza kwamba taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zimeonyesha utayari mkubwa wa kushiriki katika juhudi hizi za kuthibiti ujangili na biashara haramu ya wanyamapori na kwamba itakuwa vema kwamba utashi na utayari huu kutoka kwa wadau mbalimbali ukaenziwa na wahusika wote.

  0 0

  Leaders of the Harvard Club of Washington DC, Ms. Caren Pauley (right) and Mr. Flavian Marwa (center) meet with Tanzania Ambassador to US H.E. Liberata Mulamula (left). The Harvard Club of Washington DC is made up of those who graduated from all schools of Harvard University and are working & living in the Washington DC metropolitan area, and are mostly influential private sector, multi-lateral institutions officials as well as society and public leaders.

  0 0

  Watanzania Wameshauriwa Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwa Lengo la Kuwekeza kwaajili ya Maisha mara Baada ya Kusataafu.

  Wito Huo Umetolewa  na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania Bwana Daudi Mbaga Wakati Akitoa Mada Kwenye Semina ya wafanyakazi Wanaokaribia Kustafu Inayoendelea Mkoani Morogoro.

  Alisema Kwamba Watanzania Wengi huwa hawajui Nini Cha Kufanya Pindi Wanapostaafu Hali Inayosababisha Watanzania Wanapostaafu wakishapokea Mafao Yao wanajaribu Kufanya Kila Shuguli Mbalimbali Lakini Kutokana na kutokuwa na Uzoefu wa Shuguli Hizo shuguli  nyingi hazidumu.

  Bw Mbaga Amewashauri Watanzania  hasa Wale wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Kuwekeza  Mifuko iliyopo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kama MFUKO WA JIKIMU Wenye "Kauli Mbiu Ishi Vizuri Unastahili". Kwa Lengo la Kuwasaidia Wastaafu Ili Kuondokana na Kupata Hasara na Kufurahia Maisha Zaidi Mara Baada ya Kustaafu.

  Ameongeza Ni vizuri kwa watanzania kuwekeza katika Mfuko Huo kwa kuwa Upo Chini ya taasisi ya Serikali  na uwekezaji wao ni wa Uhakika.Pia Kuwekeza Katika Mfuko Huu watanzania watapata Faida Nyingi kwani Mfuko Huu Unaendeshwa Kitaalamu na Wataalamu Waliobobea Katika Msawala ya Uwekezaji ,Urahisi wa  wawekezaji wanaweza kufuatilia Maendeleo ya Masoko ya FedhaKwa Kufuatilia Mandeleo ya Mifuko.

  Mkurugenzi alisema Uwekezaji katika Mfuko Huo ni wa Uhakika kwasababu Unampa Mwekezaji Unafu wa Gharama za Uwekezaji, Uwazi ,Faida Nzuri,Urahisi wa Kujiunga katika Mfuko Huu.
  Mkurugenzi wa Masoko Na Mahusiano Kutoka  Dhamana ya Uwekezaji  Tanzania Bwana Daudi Mbaga Akitoa Mada Kuhusu Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwajili ya Maisha Mara Baada ya Kustaafu kwenye Semina ya Wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Iliyoandaliwa na TAGLA Mkoani Morogoro.
  Washiriki wa Semina ya Wanaokaribia Kustaafu Wakifuatilia Kwa Makini Mada Iliyokuwa Ikitolewa Kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikimu Iliyokuwa Inatolewa Na Mkurugenzi wa Masoko  Ndugu Daudi mBAGA (hayupo Pichani)Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Inayoendelea Mkoani Morogoro
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bi Martha Mashiku Akieleza Faida za Kuwekeza Katika Mifuko iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.Bi Martha Liwashauri Watanzania Kjiunga katiaka Mifuko Umoja Fund,Wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto,Mfuko wa Jikimu,Na Ukwasi.


  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (wa tatu kushoto), akiwaelekeza jambo wadau kutoka  Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu kiwandani hapo juzi, kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa na kuzalisha na kulinda mazingira (wa nne kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi, Bw. Hussein Kamote mkuu wa msafara na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama (wa sita). 
   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (aliyesimama), akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI), Bi Lilian Manga, baada ya wadau kutoka shirikisho hilo kufanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi TBL ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji bora bila kuharibu mazingira.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (kulia), akizungumza na wadau kutoka  Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu juzi kiwandani hapo kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji na kulinda mazingira. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Lilian Manga, Mkurugenzi wa Machapisho na Habari, Bw. Thomas Kimbunga, Bw. Jesper Friis na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama. 
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (kulia), akizungumza na wadau kutoka  Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu juzi kiwandani hapo kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji na kulinda mazingira. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Lilian Manga, Mkurugenzi wa Machapisho na Habari, Bw. Thomas Kimbunga, Bw. Jesper Friis na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama. (Na Mpigapicha Wetu)

  0 0

  Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
  Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
  Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.
  Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.


  0 0

  Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi. Anna T. Maembe akisisita haja na umuhimu wa wazazi kuwawezesha watoto wao wa kike kuyapenda masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu ( STEM) badala ya kuliachia jukumu hilo serikali au walimu. Alikuwa akizungumza katika mkutano wa pembezoni ulioandaliwa kwa pamoja kati ya Tanzania, Uingereza na Kampuni ya Kimataifa ya GlaxoSmithkline ili kujadili fursa na changamoto za mwanafunzi wa kike katika masomo hayo, kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bibi. Irina Bokova ambaye alikuwa modereta wa majadiliano hayo na pia alielezea nafasi na Mchango wa UNESCO katika kumsaidia mtoto wa kike. Kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi , Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
  Waziri wa Wizara ya Wanawake na Usawa wa Uingereza, Bibi, Maria Miller ( Mb) akielezea uzoefu wa nchi yake katika kuwahamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya STEM, kulia kwake ni Bibi Nicola Yates, Makamu wa Rais wa UK and Ireland Phamarceuticals na Meneja Mkuu wa GlaxoSmithkline. Nyuma ya Waziri Miller na anayefuatilia kwa makini majadiliano hayo ni Mwanamitindo Bi. Flaviana Matata ambaye pamoja na kujikita fani ya mitindo na ambayo imemjengea heshima kubwa, lakini pia kupitia Taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation ameonyesha mapenzi makubwa ya kuwasaidia wanafunzi kuipenda shule na kudumu shuleni.
  Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi. Asha Ali Abdullah ( Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto) na Bibi. Mwanaidi Salehe Abdulla ( Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amari) wakifuatilia majadiliano hayo kuhusu fursa na uwezeshaji wa wanafunzi wa kike kujiunga na masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.

  sehemu wa washiriki wa Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake, walioshiriki majadiliano hayo ambapo pia walipata fursa ya kuchangia kwa kuuliza maswali meza kuu iliyowahusisha Katibu Mkuu, Anna Maembe, Mkurugenzi Mkuu UNESCO, Irina Bokova, Waziri Maria Miller ( Mb) na Nicola Yates Meneja Mkuu GlaxoSmithkline ambao ndio waliokuwa wazungumzaji wakuu.


  0 0
 • 03/13/14--01:40: Article 18


 • 0 0

  Mkufunzi wa Chuo Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar Bw Haji Nyange Makame, kwa faida ya wanafunzi wake akiuliza swali Linalo husu Uhifadhi wa Historia ya Wahasisi wote wa Muungano walio shirikiana na Hayati Baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume.
  Muhifadhi mwanadamizi wa Historia, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni nchini Bi Flower Manase akiwafafanulia wanachuo cha UCEZ Historia ya Muungano.
  Mkufunzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Bedda Athanas akiwasilisha Mada ya Historia ya Tanzania mbele ya wanachuo wa UCEZ.
  Wanachuo cha UCEZ wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam juu ya biasha ya watumwa hapa Nchini.
  Wanachuo na Wakufunzi wa UCEZ wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

  Na Mdau Sixmund Begashe wa Makumbusho ya Taifa

  Taasisi za Elimu nchini zimeshauriwa kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Nchini ilikuwapatia nafasi walimu na Wanafunzi nchini kujifunza kwa Matendo mambo mbali mbali ya Historia ya nchi yao hususani ya nayo husu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Rai hiyo imetolewa na Muhifadhi mwanadamizi wa Historia, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni nchini Bi Flower Manase baada ya kutoa semina fupi ya Historia ya Muungano na Faida zake  iliyo andaliwa maalum kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar  na kutolewa na Bw Bedda Athanas katika Makumbusho hiyo.

  Bi Manase aliongeza kuwa vijana wengi wa Taifa hili wamejiingiza kwenye mijadala mingi inayo husu Muungano kwa kufuata maneno ya watu wengine bila wao kuijua historia ya kweli ya Mungano wa Tanzania na kusababisha malumbano ya siyo na msingi. 

  “Wakati sasa umefika wa Tanzania Bara nao waige mfano wa Chuo kikuu cha Zanzibar wa kujifunza historia ya kweli ya Nchi yetu kupitia machapisho, picha na Video zinazo husu Muungano zinazo patikana hapa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam na kuachana na habari za kishabiki zinazo patikana vijiweni’’ aliongeza Bi Manase.

  Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu wa Chuo Kikuu hicho, Bi Hawa M. Saidiq alisema kuwa amepata nafasi adimu iliyo mpatia mafunzo adhimu ya kimatendo zaidi na kufanya aelewe zaidi yale aliyo kuwa akijifunza darasani juu ya historia ya Muungano wa Tanzania.

  Nae Mkufunzi wa Chuo Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar Bw Haji Nyange Makame alie ongozana na wanafunzi hao, alikishukuru uongozi wa Idara ya Program cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo amesema yamezidisha ufahamu zaidi kwa wanafunzi wa Chuo hicho juu ya Historia ya Tanzania hususani ya namna zilivyo ungana.

  “Nawashauri wanafuzi na walimu wa Tanzania Bara na Hata Visiwani, kwa kupitia Makumbusho ya Taifa waisome vyema historia ya Tanzania ili wapate ufahamu wa kweli zaidi juu ya Muungano kwani kwa kufanya hivyo itasaidia sana kuulinda Kuueshimu na Kuudumisha Muungano huu tulio nao sasa’’ Alisema Bw Makame.

  Wanafunzi na Walimu wa Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar (UCEZ) wamekuwa wakiitembelea Makumbusho na sehemu mbali mbali za kihistoria hapa nchini ili kujitanua zaidi katika ufahamu juu ya Historia ya Tanzania na Mambo mengine ya nayo husu Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani.

  0 0

  Mr. Enoch Osei-Safo Managing Director Ecobank Tanzania adressing invited guests at the China Direct initiative launch
  Mr. Bertrand Jandoh,Regional Account Manager & Acting Head of Corporate Banking at Ecobank Tanzania adressing guests at the China Direct initiative launch.
  Deputy Managing Director Bank of China-Zambia giving a speech at the China Direct initiative launch by Ecobank-Tanzania.
  Mr.Enoch Osei-Safo introducing Ms.Wenzai Dai the Chinese liaison officer at the Ecobank Tanzania China Desk.
  Deputy Managing Director Bank of China-Zambia (right),Assistant Manager of Banking BOC-Zambia,Ms.Wang Hao interacting with members of the Chinese business community in Tanzania.


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) akisaini mkataba wa msaada ambao serikali ya Ubelgiji imetoa Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 za Kitanzania kuisaidia Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors akimwakilisha Waziri wa Ushirikiano kwa niaba ya Serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) kwa niaba ya serikali ya Tanzania akikabidhiana hati walizosainiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors (kushoto) kwa niaba ya serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa serikali ya Ubelgiji kuisadia Tanzania Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa serikali ya Ubelgiji kuisadia Tanzania Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 hivi karibuni jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi - MAELEZO)

  0 0

  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Dodoma

  Jeshi la Polisi nchini limebuni mikakati itakayosaidia kukomesha ajali za barabarani kwa kuvishirikisha vikosikazi vya Polisi Jamii vilivyotawanywa katika kila kata na tarafa nchini kote.

  Mikakati hiyo imetangazwa na Kamishna wa Polisi Jamii CP Mussa Ali Mussa, wakati wa mafunzo ya maadili awamu ya pili yanayotolewa kwa Askari Polisi wa ngazi ya kati yanayoendelea Mjini Dodoma.

  Kamishna Mussa amesema kuwa mpango huo utasaidia kuwanasa madereva wazembe wasiozingatia taratibu na sheria za usalama barabarani na hivyo kupunguza ajali ziletazo vifo na majeruhi kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

  Amesema vikosikazi hivyo vinaundwa na askari Polisi kutoka katika vitengo tofauti na kikubwa vikizingatia kazi ya msingi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia na kukamata makosa mblimbali yakiwemo ya usalama barabarani.

  “Kulinda usalama wa wananchi na mali zao ndiyo kazi kubwa ya Jeshi la Polisi na kwamba kwa yeyote atakayepatikana akienda kinyume na taratibu za usalama barabarani atatiwa mbaroni na hakutakua na huruma kwa mkosaji”. Alisema Kamishna Mussa na kuvitaka pia vikosikazi hivyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya Afisa wa Polisi.

  Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Kamisheni ya Intelijensia nchini, ACP Andrew Mwang’onda, alisema kamisheni hiyo imepanga kuwatumia Mainspekta wakiwemo Wakuu wa Polisi wa Tarafa na Majimbo hapa nchini katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia kwa lengo la kubaini viashilia vya kihalifu na wahalifu.

  Naye Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Andrew Makungu, ambaye amekokotoa idadi ya Watanzania, vitongoji, vijiji, kata, shehia, tarafa, majimbo, wilaya na mikoa iliyopo hapa nchini ikiwemo ya kipolisi, amewataka Mainspekta hao kuhakikisha kuwa wanashirikiana kwa karibu na wananchi katika kuwabaini wahalifu na maficho yao ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

  Awali Mkuu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna Mpinga Gyumi, alisema Jeshi hilo limejipanga kuboresha mifumo ya utoaji huduma bora kwa wananchi na kujenga maadili mema ili kuepukana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa.

  Zaidi ya Mainspekta wa Polisi 300 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanashiriki katika mafunzo hayo ya wiki mbili mjini Dodoma ambayo yanafanyika kwa awamu tatu tofauti kwa lengo la kukuza maadili kwa askari Polisi wa ngazi ya kati.
  Mratibu wa mafunzo SACP Patrick Byatao, akitoa mada kwa Mainspekta washiriki katika mafunzo ya kujenga maadili mjini Dodoma.
  CP Mussa Ali Mussa, akitoa mada ya utekelezaji wa miradi ya utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii wakati wa mafunzo ya Maadili kwa Mainspekta wa Polisi ambao ni Wakuu wa Majimbo n Tarafa.
  Mainspekta wanaoshiriki katika mafunzo ya maadili na rushwa wakiimba wimbo wa maadili kabla ya kuanza kwa mafunzo hao mjini Dodoma.
  Mainspekta wa Polisi ambao ni Wakuu wa Mmajimbo na Tarafa wanaoshiriki katika mafunzo ya maadili mjini Dodoma wakimsikiliza Kamishna Mussa Ali Mussa, akitoa mada ya Utekelezaji wa Miradi ya Polisi jamii.
  picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa, katikati waliokaa pamoja na baadhi ya Mainspekta wa Polisi ambao ni washiriki wa mafunzo ya maadili mjini Dodoma.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga (watatu kushoto) akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Gudluck Kway
    Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga (watatu kushoto) akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini  wa Kampuni ya  Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Edmund Rrutaraka, kwaajili ya kusaidia waathirika wa kipunga katika Kijiji cha Kwatito. Katikati yao ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Trade, Gudluck Kway na wafanyakazi wengine.


  0 0

  Chargé d’Affaires, a.i. Sharon Cromer (2nd from right), in the picture with Pan-Africa Youth Leadership Program participants from Dar es Salaam, left to right Victoria Mzamilu (from Tegeta Secondary School), Gideon Ntele (from Kisarawe Lutheran Junior Secondary School) and Almas Emelius (from Kambangwa Secondary School), when they visited her at the United States Embassy Dar es Salaam on March 12th

  The Pan-Africa Youth Leadership Program funded by the U.S. Department of State offers high school students and educators from 38 countries the opportunity to explore civic education, leadership development, respect for diversity, and community activism through U.S.-based exchange projects. 

  The program will employ a highly interactive approach both in workshops and in a range of public and community settings.  Through engagement in the activities of U.S. high schools, community organizations, youth groups, and government leaders in each location, the students and adult participants will better understand civic participation and the rights and responsibilities of citizens. 

  The program, which started in 2009, supports the Department’s goals of fostering regional cooperation on the continent in addition to nurturing young leaders.  It will take place in Washington, D.C., Chicago, Illinois, and Portland, Oregon.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma Machi 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

older | 1 | .... | 385 | 386 | (Page 387) | 388 | 389 | .... | 3272 | newer