Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 384 | 385 | (Page 386) | 387 | 388 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu. 
   Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Naguamesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. 
  "Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi”, alisema.

  Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.

  “NMB itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.

  Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa  miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. 
  Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.


  Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%)  ya bei ya pikipiki ya miguu miwili  au mitatu  kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors. 
  Kwa maelezo zaidi temembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: 
  *Mwanza -Buzuruga na Kenyata Road,

  *Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport

  *Arusha-Clock Tower na Arusha Market

  *Manyara-Babati na Katesh

  *Dodoma

  *Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe

  *Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka

                                                          NMB BENKI YAKO

  Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.

  Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akimpongeza Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.

  Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza


  0 0
 • 03/12/14--13:11: Article 0


 • 0 0

  Wafanyakazi wanawake wa Airtel wakitoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wenzao wakati wa tafrija fupi waliyoiandaa kwa dhumuni la kukusanya fedha ili kuwachangia wagonjwa wa kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam. jana
  Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akichangia fedha kwa huduma ya Airtel Money kupitia simu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
  Mmoja kati ya wafanyakazi wa Airtel, Bw. Deodatus Hondo akichangia fedha wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.

  Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania unaofahamika kwa jina la Airtel Divas leo wameandaa halfa ya kuchangisha pesa kwa ajili yakina mama  wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa katika hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.

  Halfa hiyo ya kuchangisha pesa ilifanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania  na kushirikiksha wafanya kazi wa Airtel Tanzania kwa ujumla

  Akizungumza kwa niaba ya  Airtel Ofisa Mahusiano na matukio Dangio Kaniki alisema” Airtel Tanzania kupitia Umoja wa wanawake Airtel Divas” tumeamua kuchangisha pesa kwaajili ya kina mama wenzetu ambao ni wagonjwa mahospitalini,  ambapo leo tumeaandaa kifungua kinywa kwa wafanyakazi wote wa Airtel na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Saalam.

  Tunatambua jamii inayotuzunguka ina changamoto nyingi ikiwemo maradhi, na ndio sababu umoja wa wanawake wa Airtel tumeamua kuchangisha pesa kwa dhumuni la kuwasaidia wagonjwa hususani wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa kansa. Tunaamini zoezi hili tunalolifanya leo litatuwezesha kufanikisha lengo letu.  

  Mpango huu wa kusaidia jamii zinazotuzunguka ni endelevu, na tumejipanga kutoa misaada ili  kuchangia katika kutatua vikwazo mbalimbali vya maisha na kujenga jamii iliyo bora. alisema Kaniki.

  Kwa upande wa wafanyakazi Bi Doris Kibassa ambaye ni mmoja ya wanachama wa Airtel Diva alisema “ najisikia furaha kuwa sehemu ya kusaidia jamii,  mbali na kampuni yetu kuwa na shughuli za kijamii bado sisi  kama mfanyakazi tunanafasi ya kushiriki na kutoa msaada  kwa jamii. 

  Tunaamini mchango huu tunaoutoa leo utaweza kunusuru maisha ya baadhi ya watanzania na hivyo basi tunaziasa asasi nyingine kuiga mfano huu  na kushiriki katika kuokoa maisha ya watanzania walio wengi,”

  Airtel Tanzania imekuwa ikitoa michango kwa jamii kutupitia shughuli zake za huduma kwa jamii, Airtel kwa kushirikisha wafanyakazi wake pia inatoa huduma kwa jamii nchini.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Kipya cha Televisheni (TV 1 Tanzania),Marcus Adolfsson akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Southen Sun,jijini Dar es Salaam leo,wakati wa kutangaza Uzinduzi wa Kituo hicho cha Televisheni kitakachokuwa kikirusha matangazo yake kutokea Jijini Dar na kuonekana nchi nzima.
   Watangazaji wa Kipindi cha The One Show kinachorusha na Kituo hicho kipya cha Televisheni(TV 1 Tanzania),Jokate Mwegelo na Ezden Jumanne wakizungumzia namna walivyojipanga kwenye kipindi chao hicho. 
   Wanahabari wakiendelea kupata taswira za watangazaji hao.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Kipya cha Televisheni (TV 1 Tanzania),Marcus Adolfsson (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya watangazaji wa televisheni hiyo.toka kulia ni Ezden Jumanne,Jokate Mwegelo,Meshack Nzoha na Agness Kahonga,wakiangalia moja ya vipindi vyao wakati wa uzinduzi huo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.
   
  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza.

  “Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu.

  “Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake. 

  “Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama.

  Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

  Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na kwaya ya Kwetu Pazuri wote wa Tanzania.

  0 0

  )

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova, ( kati kati) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu Teknolojia ya habari na mawasiliano na mchango wa vyombo huru vya habari katika kuwawezesha wanawake na watoto wa kike, katika majadiliano hayo, wazungumzaji waliokaa meza kuu ambao ni kutoka kushoto, Bi. Elisa Munoz, Mkurugenzi Mtendaji wa IWMF, Muwakilishi wa Kudumu wa Austria Balozi Martin Sjdik, Bw. Peter Launsky-Tieffenthal Katibu Mkuu Msaidizi na mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa , Anne Bennett, Mkurugenzi Mtendaji wa Hirondelle ( USA) na Pamela S. Fall, anayeripoti katika kituo cha CBS na Rais wa chama cha Waadishi wa habari Umoja wa Mataifa walijadili kwa kina umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kama nyezo muhimu ya uwezeshaji wa wanawake na watoto wa kike, lakini pia kama nyezo muhimu katika kuwapatia habari na taarifa mbalimbali, habari zinazoandaliwa na vyombo huru na ambavyo waandishi wake wenyewe na weledi wa matumizi ya ICT.
  sehemu ya washiri wa majadiliano kuhusu ICT ambayo yaliandaliwa kwa pamoja na UNESCO na Uwakilishi wa Kudumu wa Austria na kufanyika sambamba na mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake. katika majadiliano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya International Women's Media Foundation, (IWMF mwenye suti nyekundu, alitoa taarifa kuhusu uzinduzi utakaofanywa wa ripoti ya utafiti kuhusu mazingira hatarishi wanayofanyia kazi waandishi wa habari wanawake. Ripoti hiyo yenye kurasa 40 inahusu utafiti uliofanywa kwa kuwashirikisha waandishi wa habari wanawake 1,000 kutoka duniani kote.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi. Anna T. Maembe, akifutilia majadiliano ambayo yameingia siku ya pili ya ajenda kuu ya Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake, ajenda hiyo ni mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, ( MDGs) kwa wanawake na watoto wa kike. Mkutano wa 58 wa CSW ulifunguliwa siku ya jumatatu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.


  0 0

  Kundi la washiriki kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakielekezana jinsi ya kutumia vifaa rafiki ya kuhudumia Majokofu na Viyoyozi siku ya pili ya mafunzo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wakufunzi kutoka vyuo vya ufundi Mbeya, Mwanza na Mkunazini – Zanzibar wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kutumia njia rafiki ya kuhudumia majokofu na viyoyozi bila ya kuharibu tabaka la Ozoni. Picha na Rashda Swedi.

  0 0

  HE President Jakaya Kikwete receiving a key from the Director of FZS in Africa Robert Muir as a symbol of handing over the vehicles to Tanzanian Government.
  A cross section of the 11 Land Rovers donated by FZS to Serengeti National Park, Selous and Maswa Game Reserves.
  Some of the key official from the Ministry of Natural Resources and Tourism, Tanzania National Parks, Frankfurt Zoological Society, Selous Game Reserve and Germany Embassy pose for a group photo with HE President Jakaya Kikwete during the handing over event.

  As rhino and elephant poaching numbers reach unprecedented levels, Frankfurt Zoological Society (FZS) has donated five new Land Rover vehicles to Tanzania National Parks (TANAPA) as a commitment to anti poaching efforts in the Serengeti National Park.

  The vehicles were presented to His Excellency President of the United Republic of Tanzania Dr. Jakaya Kikwete by the Africa Director of FZS Robert Muir and will be used to expand surveillance and security activities in the Serengeti National Park.

  The donation of the vehicles lies under the framework of the Germany Development Cooperation project implemented by KfW and GIZ which symbolizes the fruitful partnership between Frankfurt Zoological Society and the Ministry of Natural Resources and Tourism.

  In acknowledging the support from FZS, Director General of Tanzania National Parks Allan Kijazi commended the support saying that the vehicles will help support anti-poaching efforts in the Serengeti National Park which is also a World Heritage Site.

  FZS also donated other six vehicles to the Ministry of Natural Resources and Tourism whereby five were for Selous Game Reserve and one for Maswa Game Reserve.

  Issued by Corporate Communications Department
  Tanzania National Parks
  11th March, 2014

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Na Kibada Kibada –Katavi

  Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wamepewa changamoto kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi  mazingira  kwani kuharibu mazingira kunapelekea kuchangia ukame na kukosekana na maji ambayo  ndiyo uhai wa viumbe na tegemeo la maisha ya wanadamu na wanyama.

  Changamoto hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Kibiriti Yasini wakati akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Milala Kata ya Kabungu kwenye  maandalizi ya wiki ya maji inayotarajiwa kufanyika kilelele cha machi 22 mwaka huu.

  ,Kibiriti mewataka kutoa ushirikiano wa karibu kila mtu kwa nafsi yake kuhakikisha anatimiza wajibu wake katika kulinda,kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

  Katika hotuba yake hiyo alisisitiza wananchi watoe ushirikianao wa thati  kutunza vyanzo vya maji na kuilinda miradi ya maji iliyopo katika katika kijiji hicho na kuiona kuwa ni mali yao  na itawasaidia kwa manufaa ya wote hivyo ni wajibu wao kuitunza na kulinda. Kwa kuwa  mradi wa ,maji uliopo hapo kijijini utawaondolea kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwabaili hasa wanawake na watoto ndio wanaotabika kwa kukosa maji sehemu yeyote ile.

  Akizungumzia  maandalizi ya wiki ya  maji kila mwaka  alisema kila mwaka  huambatana na utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira,na uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala,kwa kutambua  umuhimu serikali imefanya juhudi za kuhakikisha inwaondolea wananchi wake kero ya upatikana wa maji na kuwasogezea karibu wananchi maji.

  Alieleza kuwa Katika kijiji cha milala vituo kumi vya kuchotea maji vimejengwa na wananchi watapata maji hivyo kuwaondolea kero iliyokuwa ikiwakabili wakazi hao na Halmashauri yake kwa kushirikiana na Serikali kuu kwa kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa Big Results Now  (BRN).

  Hata hivyo amemwagiza Kaimu Mhandisi wa maji katika Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wa kijiji cha Milala kero ya ukosekanaji wa maji inakwisha kwa kuwa halmashauri imejipanga kutekeleza na kuwaondolea kero hizo.

  Kwa upande wa upatikanaji wa maji katika halimashauri ya wilaya ya Mpanda  ni wastani wa asilimia 48 tu ambapo hali hiyo ni kiasi kidogo lengo ni kuhakikisha asilimia hiyo inaongezeka angalau kila kijiji kiwe na maji ya uhakika.

  Aidha aliwaeleza wananchi hao kuwa ifikapo juni 2014 miradi ya maji ya katika vijiji vya Isenga Kata ya MIshamo,Ikola Kabungu na Karema itakuwa imekamilika kwa karibu asilimia 75,na kwasisistiza kuwa miradi hiyo ni mali yao waitunze na kuienzi pia wanachangia mifuko ya maji ili kuimarisha mifuko kwa kuwa na mifuko wa maji utasaidia katika matatizo madogo madogo yanayojitokeza katika maradi kama ukarabti kwa kununua vifaa vidogovidogo vya matengenezo ili maji yaendelee kuwanufaisha wananchi.

  Awali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Milala Rosemary Omera akisoma taarifa ya kijiji alieleza kuwa kijiji kilikuwa kinakabiliwa na matatizo ya maji lakini kupatikana kwa mradi wa maji katika kijiji hicho kumesaidia kwaondolea kero iliyokuwa ikiwakabili.

  Ingawa wakazi wa kijiji hicho wanakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira unaoambatana na uingiaji wa mifugo kiholela hali inayochangia uharibifu wa mazingira na hasa vyanzo vya maji katika maeneo mengi hapa kijijini.

  Akawataka wananchi wajenge utamaduni wa kutunza na kuhifadhi mazingira ili kusaidia kuhifadhi vyanzo vya maji pia aliomba serikali iendelee kuwaletea miradi mingine ya maji na has katika shule ya Sekondari y  ufundi ya Milala amabayo inakabiliwa na tatizo la maji safi na salama.
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yasini Kibiriti akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Milala  Kata ya Kabungu Wilayani Mpanda wakati wa maandalizi ya maazimisho ya  wiki ya Maji sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa mikutano  Kijiji cha  Milala.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Milala waliofika kujumuika na wazazi wao katika sherehe za maandalizi ya wiki ya Maji, kama ilivyo kwa wanafunzi kujenga tabia ya kusoma alikuwa alikuwa  akisoma gazeti la Mpandaleo linalotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, mwanafunzi huyo alikuwa  akisubiri mchakato wa mzima wa sherehe za maandalizi akiwa na  wananfunzi wenzake waliofika kushuhudia maandalizi hayo .
  Wakazi wa kijiji cha milala wakichuana kunywa pombe ya kienyeji aina ya Komoni katika kusherehesha maandalizi ya wiki ya maji katika halmashauri ya Mpanda mshindi katika mpambano huo alijinyakulia kitita cha shilingi elfu kumi.

  0 0

  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akiongea na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum Ofisi kwake leo. Picha na Owen wa Bunge.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uwekezaji Mhandisi Decklan Mhaiki (katikati) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) pamoja na Waandishi wa habari moja ya mashine za kufua Umeme zitakazofungwa katika eneo la Kinyerezi I jijini, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi huo, Bw. Shaun Moore.
  Mmoja wa mitambo ya kufua umeme ambao utafungwa katika eneo la Kinyerezi I mara baada ya ujenzi kukamilika. Mitambo hiyo, inatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati za umeme 150 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya Taifa.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wa kampuni inayojenga kituo hicho ya Jacobsen Elektro.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I, Bw. Shaun Moore, wakati akimweleza maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.


  0 0  Mwana Diaspora Benja ambaye pia ni nyota katika kipindi cha kila wiki katika mtandao wa Vijimambo cha IJIWE CHA UGHAIBUNI ametua Dar es salaam wiki hii akiwa katika harakati za kusaka fursa ya uwekezani na kutoa ajira kwa ndugu, jamaa na marafiki. Hapa ni katika kiota cha Break Point ya mjini ambako leo ameandaa dina la mchana kwa wadau kadhaa akiwamo Ankal

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (katikati) akiwa na Balozi wa Ubelgiji Tanzania, Koen Adam (kulia) na Mkurugenzi wa Maendeleo na Ushirikiano Wizara ya Mambo ya Nje Ubelgiji, Peter Moors (kushoto) wakizunguka kuangalia mradi wa maji Mbagala Kuu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (katikati) akiwa na Balozi wa Ubelgiji Tanzania, Koen Adam (kulia) na Mkurugenzi wa Maendeleo na Ushirikiano Wizara ya Mambo ya Nje Ubelgiji, Peter Moors (kushoto) wakikata utepe katika uzinduzi wa mradi wa maji Mbagala Kuu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko akiinua ndoo kwa ajili ya kumtwisha mmoja wa wakazi wa Mbagala Kuu baada ya kuzindua mradi huo.


  0 0

  MKURUGENZI wa Mashitaka Nchini (DPP), amemfutia mashitaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime (61) na kisha kumuunganisha na wenzake 11 na kuwasomea upya mashtaka 27 ya mauji katika mtaa wa Indira Gandh, yaliyotokana na kuporomoka jengo la ghorofa 16.

  Mbali na Fuime washtakiwa wengine ni, Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki, Raza Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad Mugyabuso,Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare, Zonazea Oushoudada, Vedasto Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph Ringo.

  Washtakiwa hao walisomewa hati mpya ya mashitaka baada ya kuondolewa hati ya zamani ya mauaji ya bila kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao kufikia 12, mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka.

  Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na Wakili wa Serikali Joseph Maugo.

  Kongola alidai kuwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha 294 kidogo cha (1) upande wa Jamhuri unaomba ridhaa ya mahakama ya kumuongeza mshtakiwa Fuime katika hati mpya ya mshitaka.
  Hakimu Kisoka alisema mahakama haina pingamizi na maombi ya Jamhuri ya kubadilisha hati ya mashitaka dhidi ya washtakiwa.

  Jamhuri ilidai kuwa katika shtaka la kwanza, Machi 29, mwaka 2013 mtaa wa Indira Gandh, Wilaya ya Ilala washtakiwa kwa pamoja walimuua kwa makusudi  Yusuph Khari.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Muungano wa Jamhuri ya Korea, Ahn Hong Joon (kulia kwake) na msafara wake baada ya mazungumzo, kwenye makazi ya Waziri Mkuumjini Dodoma Machi 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Muungano waJjamhuri ya Korea, Ahn Hong Joon baada ya mazungumzo kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjni Dodoma Machi, 12, 2014.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Uchukuzi , Ujenzi na Vifaa wa Burundi, Mhandisi Virginie Ciza na mwenyeji wake Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma Machi 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkabidhi  Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi Hati zinazomwezesha kufanya kazi kama Mwakilishi wa Heshima wa Mauritius nchini Tanzania. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu tarehe 12 Machi, 2014. 
  Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kupokea kibali cha kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Mauritius hapa nchini
  Katibu Mkuu,  Bw.  Haule akizungumza na  Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akiagana na Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.Picha na Reginald Philip

  0 0

  A group photo of British High Commissioner with students, teachers and coordinators of Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School after her visits.
  British High Commissioner Dianna Melrose listens to a beneficiary student of Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School.
  British High Commissioner Dianna Melrose listens to Prof Eustella Bhalalusesa, Commissioner of Education from the Ministry of Education and Vocational Training during the visits at Kisutu Secondary School.


  0 0

  Andrew Mahaiga akiwa na rafiki yake Arther Samuel katika tamasha la Nyama Choma hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa Bongo Fleva, Cpwaa akiwa ndani la tamasha la Nyama Choma hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Mpenzi wa burudani akifurahia kuwa ndani ya banda la Heineken ndani ya Nyama Choma festival hivi karibuni.
  Millard Ayo akitangaza mshindi wa shindano la Heineken ya kwenda Amsterdam nchini Hollanzi, kulia kwake Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Bw. Uche Unigwe.
  Wapenzi wa Heineken wakiburudika ndani ya Nyama Choma festival.

older | 1 | .... | 384 | 385 | (Page 386) | 387 | 388 | .... | 3270 | newer