Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM MKOANI KIGOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia siku ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mkoani Kigoma.


Tigo kufanya tamasha kubwa la Muziki kuzindua msimu wa Tabasamu!

$
0
0

 Baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja,mapema leo asubuhi mara baada ya kumaliza mkutano wao na Wanahabari ndani ya ukumbi wa hoteli ya Bell Monte,jijini Dar.
Mmoja wa wasanii mahiri,Mr Blue,ambaye pia  atashiriki kutumbuiza kwenye tamasha hilo akitoa vionjo kwa Wanahabari (hawapo pichani). 
 Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Lumuliko Mengele a.k.a Dj Mully B akifafanua kuhsiana na maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika kwenye ufukwe wa Coco beach,februari 10 jijini Dar Es salaama,Shoto kwake ni baadhi ya wasanii watakaoshiriki tamasha hilo.
Pichani shoto ni Meneja wa chapa ya Tigo Bwana William Mpinga akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi huo akisema "Tigo ina fahari kubwa kwa jinsi ambavyo inawajali na kuwapa thamani wateja wake kupitia bidhaa zake mbalimbali za mawasiliano.

MAELEZO YA SPIKA KUHUSU UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA BUNGE WAKATI WA KUPITISHA HOJA BINAFSI ZA WABUNGE

MKURUGENZI WA UNESCO AZUNGUMZA NA MAWAZIRI WA ZANZIBAR

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova akizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huko katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova wakwanza kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari mbalimbali hapo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kushoto akipokeya Zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova walipomaliza Mazungumzo hapo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na Viongozi mbalimbali baada ya kumaliza kwa Mazungumzo yao katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar. PICHA NA -MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR.

SEBENE LIMEKOLEAAA.....

michango ya ushirikishi ni lazima shuleni?

$
0
0

habari za leo,

naomba uniwekee mada yangu kwenye mtandao wako.

Naomba kuuliza wizara ya elimu watueleweshe kuhusu maana ya michango ya ushirikishi shuleni kila siku. maana katika shule ya msingi Boko wilaya ya kinondoni imekuwa ni kero kwa watoto na wazazi watoto wanapigwa kwa ajili hilo mfano darasa la saba kila siku asubuhi ni lazima waende na sh. 300 na wanaambiwa ni lazima vinginevyo wanapigwa sasa nimepiga mahesabu kama watoto ni 300 kila siku kila kipindi kinakusanya sh. 300 x 300 = 90,000/= hizo hela zinaenda wapi. ukiuliza wazazi wanasema kwenye kikao cha shule walisema sio lazima  kwa hiyo aina maana mzazi asipompa mtoto hela lazima apigwe. Nawaomba Wizara ya Elimu watueleweshe kama ni kitega uchumi cha walimu? au inakuwaje?
Mdau 

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa ufafanuzi hali iliyotokea Bungeni leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Stella Manyanya (Viti maalumu) kuhusu yaliojiri Bungeni leo.
Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo (kushoto)pamoja na Said Arfi (Mpanda Mjini)wakifuatilia hoja mbalimbali Bungeni leo Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalla Kigoda (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazri wa afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid katika viwanja vya Bunge leo baada ya kuahirishwa mkutano wa kumi, kikao cha sita.

Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiongea na John Mnyika (Ubungo) katika viwanja vya Bunge leo, baada ya hoja yake binafsi kukataliwa Bungeni.
Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela (kushoto) akiongea na William Ngeleja (Sengerema)katika viwanja vya Bunge baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda (hayupo pichani) kuahirisha kikao hadi kesho.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

ndugu wawili wauwawa kinyama jijini arusha

$
0
0

Joseph Ngilisho,Arusha

WANAWAKE wawili wanandugu wameuawa kinyama katika nyumba waliokuwa wakiishi na watu wasiojulikana na miili yao kukutwa baada ya siku tatu ikiwa imelaliana huku ikiwa imeharibika vibaya.

Kugundulika kwa miili hiyo kumetokea leo majira ya saa 3.15 katika eneo la daraja mbili manipsaa ya jiji ya Arusha baada ya majirani kuhisi harufu kali iliyokuwa ikitokea ndani ya chumba hicho walichokuwa wamepanga katika nyumba inayomilikiwa na merehemu Samson Kivuyo.

Taarifa zimeeleza kuwa majirani hao walijikusanya na kutoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo ambao kwa pamoja walikubaliana kutoa taarifa polisi ambapo ,polisi walifika eneo la tukio na kuvunja mlango ,ndipo walipokuta miili ya marehemu hao ikiwa imeharibika vibaya.

Miiili ya marehemu hao ilikutwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili, huku ndani ya chumba hicho kukiwa kimevurugika na baadhi ya vitu kuvunjika hali ambayo inaaminika kwamba kabla ya mauaji hayo kulikuwa na mvutano wa kutoelewana.

Akizungumza na vyombo vya habari msimamizi wa nyumba hiyo,Fatina Mringo aliwataja marehemu hao kuwa ni,Zainabu Iddy(Zai) mwenye umri wa miaka 19 na Zena Sadick Shengwatu mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa mfanyabiashara wa nguo na mmiliki wa chumba hicho.

Alieleza kuwa siku ya jumamosi marehemu hao walionekana majira ya mchana wakiwa nyumbani, na marehemu Zena alikabidhiwa fedha na wapangaji wenzake na kwenda kulipia bili ya umeme Tanesco na baadae alirudi na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Hata hivyo habari zimedai kwamba marehemu hao kwa pamoja hawakuweza kuonekana tena hadi miili yao ilipokutwa chumbani ikiwa imeharibika vibaya na kutoa harufu kali.

Hata hivyo baadhi ya majirani wakielezea tukio hilo wamebainisha kwamba marehemu hao mara nyingi walionekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume tofauti na kwamba siku ya tukio Zena alionekana akichukuliwa na gari dogo aina ya teksi huku gari jingine lilionekana likingia nyumbani kwake.

Majirani hao wamedai kwamba marehemu hao ambao ni wakazi wa Lushoto mkoani Tanga waliishi katika nyumba hiyo katika mazingira ya kutokuwa na waume .

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi unaendelea na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru kwa uchunguzi wa daktari.

SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA KWA BAR MBALIMBALI NCHINI KWA MWAKA 2013

$
0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Nyama Choma 2013 kwa Bar mbalimbali lijlikanalo kama ‘’Safari Lager Nyama Choma Competition 2013” liliofanyika TBL jijini Dar es Salaam .Kulia ni Jaji Mkuu wa shindano hilo, Douglass Sakibu na mratibu wa Shindano hilo, Peter Zacharia.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia) akikata nyama kuashilia uzinduzi wa shindano la Safari Lager Nyama Choma linalotammbulika kwa jina la “Safari Lager Nyama Choma Competition 2013”lililozinduliwa TBL jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji Mkuu wa shindano hilo, Douglass Sakibu.

Kikao kazi cha maafisa habari wa serikali mjini dodoma chaingia siku ya pili , changamoto mbalimbali zaibuliwa

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa Mawasiliano wakati wa Kikao kazi cha maafisa habari wa serikali kinachoendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya maafisa habari wa serikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Bw. Peter Millanzi mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Midradji Maez, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Bw. Abel Ngapemba, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Shiririka la Maendeleo la Taifa (NDC).
Maafisa Habari kutoka wizara mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya vikundi kuhusu mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi wakiongozwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Luteni Kanali Juma Sipe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Wizara ya Ulinzi.
Maafisa Habari kutoka wilaya na Mikoa mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya pamoja kuhusu mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Maandalizi ya Chumvi katika kiwanda cha Sea Salt kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani

$
0
0
Hii ni sehemu ya Viroba vya Chumvi vilivyopangwa kando kando ya bahari ya Hindi,eneo la Bagamoyo mkoani Pwani.mali ya kampuni ya Sea Salt iliopo Bagamoyo,vikiwa tayari tayari kwa kusafirishwa.

Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO,pia Amjulia Hali Mzee Msuya

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO Bibi Irina Bukova ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu,Mzee David Cleopa Msuya aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo(picha Rashid Ngurungu-Ikulu)

American People's Support for Anti-Poaching Initiatives

$
0
0
On Tuesday, February 5, United States Department of the Interior Deputy Secretary David J. Hayes handed over control of the Burunge Wildlife Management Area Visitor Center, Babati District, Manyara Region to the Ministry of Natural Resources and Tourism. The Burunge Wildlife Management Area is sponsored by the American People through the United States Agency for International Development (USAID). Wildlife Management Areas are community-owned and managed conservation areas that empower local communities to be decision makers over their natural resources. At the hand-over ceremony to the left of the plaque, from left to right: Director of the African Wildlife Foundation Tanzania (AFW TZ Country Director) John Salehe; USAID TZ Mission Director Sharon Cromer; Chairman of Burunge Wildlife Management Areas (WMA) Authorized Association Ramadhani Ismail; Deputy Secretary of the United States Department of the Interior David J. Hayes; to the right of plaque, from left to right is United States Ambassador Alfonso E. Lenhardt; Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Hamis Kagasheki; Parliamentarian and Chair of the Parliamentary Committee on Environment Hon. James Lembeli, and Regional Executive Secretary for Manyara region Claudio Bitegeko.

Rais Obama wa Marekani amewatakia wakenya Uchaguzi mwema

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAKAMATA VIROBA 20 VYA BANGI

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani) madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa kwenye moja ya viroba kati ya 20 vilivyokamatwa na Polisi,mkoa Arusha.

MNAMO TAREHE 31/01/2013 MUDA WA SAA 7:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LOSOITI KIJIJI CHA KIMOKUWA WILAYANI LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI MGAMBO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE MANDEGE S/O PAKASI (54) MFUGAJI NA NI MKAZI WA KITONGOJI CHA LOSOITI AKIWA NA MAGUNIA 20 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI YANAYOKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 50 KILA MOJA.

TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAAADA YA ASKARI HAO KUPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA, AMBAPO INAELEZWA KWAMBA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA WENZAKE WAWILI WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA HAYO KWA KUTUMIA WANYAMA AINA YA PUNDA AMBAO WALIKUWA KUMI AMBAPO KILA MMOJA ALIKUWA AMEBEBESHWA MAGUNIA MAWILI.

MARA BAADA YA WATU HAO KUWAONA ASKARI HAO WATUHUMIWA WAWILI WALIKIMBIA NA WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA MMOJA.

JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO HUKU WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA WANAENDELEA KUTAFUTWA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS

Article 3

Kali TV Online this week

$
0
0
This week, Kali TV attended Washington DC's African Affairs offices conferences which focuses on the 400,000 dollars grant that DC Mayor offered to struggling Africans and African-Americans small business in the nations capital. 
Kali TV also attended celebration of Barrack Obama as 44th president of United States and 100 years of African National Congress at Howard University.

Article 1

CAMEROON WATUA DAR, WAONGEA NA WANAHABARI

$
0
0

 Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu pambano lao na timu ya Taifa ya Cameroon utakaopigwa tarehe 6.2.2013. (Picha na Dande Junior wa Habari Mseto Blog)
 Nahodha wa Stars, Juma Kaseja akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Kocha wa timu ya Taifa ya Cameroon, Jean Paul akifafanua jambo. Kushoto ni Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song na Nahodha wa timu hiyo, Wome Pierre.
  Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. Katikati ni kocha Mkuu wa timu hiyo, Jean Paul na Nahodha, Wome Pierre.
 Meneja wa timu ya Cameroon, Rigobert Song (katikati) akiingia katika Ofisi za TFF wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
  Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. Katikati ni kocha Mkuu wa timu hiyo, Jean Paul na Nahodha, Wome Pierr

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI CONTAINER PRICE CUT!

$
0
0


40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950
20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
THIS IS MORE THAN £200 DISCOUNT!
THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE

RATIBA YA MELI MPYA FEBRUARY 2013
 
FROM TILBURY 21/02/2013
VESSEL CUT OF IS 19/02/2013
FROM SHEERNESS 22/02/2013
VESSEL CUT OF IS 20/02/2013
TUNATOA HUDUMA ZA UKAGUZI WA MAGARIMOT/VOSA OFISINI KWETU
VEHICLE INSPECTION FOR KENYA A NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES
JUST DROP YOUR  CAR IN OUR OFFICE AND WE WILL INSPECT IT AND DELIVER IT TO THE PORT FOR YOU

kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;
2 X FEMALE OFFICE CLERKS WANTED
CALL CHRIS FOR MORE INFO

CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
HASSAN (RICHARD) +44 07405159255


Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images