Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 37 | 38 | (Page 39) | 40 | 41 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Kaimu mhifadhi katika hifadhi ya Mikumi Damian Saru akiteta jambo na mwandishi wa habari mwandamizi wa ITV  Kanda ya Kaskazini James Paul (mwenye shati jekundu) wakati wa kuangalia njia hiyo mpya.
  Moja ya wanyama  aina ya Duma ambao pia wanapatikana katika njia hiyo. 
  Ili kuweza kuendelea na safari kutizama njia hiyo wakati mwingine waandishi walilazamika kushika bereshi ili kuweka njia sawa kwa gari kupita. 
   Maeneo mengine ukarabati uliendelea katika njia hiyo mpya.
  Watalii katika hifadhi ya taifa ya Mikumi wakipita katika njia mpya ya utalii iliyofunguliwa hivi karibuni iliyopo upende wa kusini mwa hifadhi hiyo.
  Njia katika eneo hilo maarufu kama Vuma Circuit. 
  Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Kikosi cha timu ya Tanzania.
   Wachezaji wa Taifa Stars wakisalimiana na wenzao wa Cameroon.
   Kikosi cha timu ya Cameroon kikiwa katika picha ya pamoja.
   Beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Erasto Nyoni akijaribu kumzuia kiungo wa pembeni wa Cameroon, Bedimo Henri wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo.
  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samata akimtoka beki wa kushoto wa timu ya Cameroon, Benoitte Assou-Ekotto  wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Tanzania imeshinda 1-0.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza,akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Masoko Vodacom Tanzania wakiwa wameshikilia hundi yao yenye thamani ya $ 5,000 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Rene Meza (wa pili kulia)kwa kuibuka wafanyakazi bora kwa mwaka 2012/13.

   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo hayupo pichani akiongea nao wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza(kulia)akimkabidhi Abella Tarimo, Meneja biashara wa Vodacom Tanzania zawadi ya ngao na cheti kwa kuwa mfanyakazi bora katika kuunganisha idara zote kwa wakati na utendaji kazi kiufanisi. Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja Harrieth Lwakatare.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza wa saba toka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha Jasiliamali watu mara baada ya zawadi ya ngao na cheti wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.


  0 0


  Pichani katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania bi. Sadaka Gandi akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo, kulia Raisi wa tuzo hizo bi. Irene Kiwia na kushoto ni bi. Esther Shayo mratibu.
  Pichani kulia ni Raisi wa tuzo hizo Irene Kiwia akielezea jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tuzo hizo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013, zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.

  Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.

  "TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa si tu kibinafsi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na  michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufariji na kuridhisha sana.”


  Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi naTeknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.


  Bi SadakaGandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteuawa na wake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili watuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wamabadiliko katika jamii zao.


  Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "


  Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu yaMtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna waTume ya Hakiza Binadamu naUtawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga-Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi.Ludovicka Tarimo–Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlakaya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.


  Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwana Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, WatuwaMarekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.

  0 0

  Ngoma ya Lucille ya mzee mzima Kenny Rogers si ya kawaida

  0 0

  Piga ua lakini ngoma ya Koffi Olomide 'Mopaoa' na kundi lake la QUARTIER LATIN ya ULTIMATUM si mchezo

  0 0


  Ridhiwani Kikwete
  ---
  Habari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .

  Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe. lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

  Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata twitts juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack Obama kuja tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.

  kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

  Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

  Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa mliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

  Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na zoezi hili. lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao juu ya hili

  MIMI NDUGU YENU
  RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
  AKHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea mpira ukiwa ni miongoni mwa mipira kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Bi.Sharifa Khamis Salim,alipofika Ikulu kukabidhi mipira hiyo pamoja na kamati ya ugawaji mipira hiyo,kutoka mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA”,hafla hiyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kamati ya ugawaji Mipira kutoka mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA”,chini ya Mwenyekiti wake Bi.Sharifa Khamis Salim,pia akiwa  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo,hafla hiyo ilifanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
  Katibu wa Kamati ya Ugawaji wa Mipira ya Mradi wa “ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA”, Khamis Abdalla Said,akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati kamati hiyo ilipofika Ikulu Mjni Zanzibar kukabidhi Mipira kwa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar

  0 0
 • 02/06/13--22:50: Tuamke Dar

 • Tarehe 14, Februari, 2013, saa 10 jioni, Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati duniani kote kwa ajili ya ONE BILLION RISING, Siku Kubwa kabisa ya utekelezaji katika historia ya Siku ya Ukatili, harakati za wanaharakati za kimataifa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

  ONE BILLION RISING ilianza kama wito wa kuchukua hatua kwa takwimu ya kustua kwamba mwanamke 1 kati ya 3 duniani atapigwa au kubakwa wakati wa uhai wake. Pamoja na idadi ya watu duniani kuwa bilioni 7, hii inafikia zaidi ya WANAWAKE NA WASICHANA BILIONI MOJA. Tarehe 14 Februari, 2013, ni siku ya maadhimisho ya miaka 15 ya Siku ya Ukatili. Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati, waandishi, wanafalsafa, watu mashuhuri, na wanawake na wanaume kote duniani tutakapoeleza hasira zao, mabadiliko ya mahitaji, mgomo, ngoma, na ONGEZEKO la kupuuzia mateso ya uonevu wayapatayo wanawake, hatimaye wakidai mwisho wa ukatili dhidi ya wanawake.

  0 0
 • 02/06/13--22:57: DR WILBROAD SLAA AUNGURUMA
 • Video Kutoka Chadema:Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Amesema:''CHADEMA kimechoshwa na uonevu na ukiukwaji mkubwa wa Kanuni unaofanywa na kiti cha Spika.Amesema hakuna Mbunge yoyote wa CHADEMA atakayeenda kuhojiwa na Kamati ya Bunge mpaka hapo rufaa zote 10 za Wabunge wa CHADEMA dhidi ya kiti cha Spika zitakapojibiwa..'

  0 0
 • 02/06/13--23:01: Article 13


 • 0 0

   Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya (Mwenye suti)  akikagua mafunzo kwa vitendo ya vijana wanaomaliza mafunzo ya kujitolewa ya JKT katika kambi ya JKT Kanembwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma
  Baadhi ya vijana wanaomaliza mafunzo ya kujitolea katika kambi ya JKT Kanembwa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo

  0 0

  Na Abdulaziz Video,Lindi 
  Wazazi mkoani Lindi wametakiwa kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa wanaenda shule ili kusaidia kuondokana na tatizo la watumishi na wataalamu katika mkoa huo ulio na rasilimali nyingi 


  Wito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri kuu wilaya ya Lindi ambae pia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kimkoa katika kata ya Chiponda -Rondo wilaya ya Lindi vijijini.   Mama Kikwete Lindi alieleza kuwa kutokana mikoa hiyo kuwa nyuma kimaendeleo sasa ifike wakati Wazazi na walezi kusaidia na kuakikisha watoto wao wanapata elimu kufuatia matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha pili hivyo basi kina baba washirikiane na wake zao kuhakikisha kuwa watoto wanahudhuria shule na kufanya vizuri katika masomo yao.   Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM taifa aliwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kutosubiri nafasi za upendeleo(viti maalum)   ‘Wanawake wenzangu mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje chama ili muingie katika ngazi ya maamuzi na kuachana na mawazo kuwa hamuwezi kuingia katika chaguzi za wananchi'alisema.  Sambamba na sherehe hizo Mama Kikwete aliwataka Wananchi wa Mkoa huo kuendelea kudumisha amani, upendo na utulivu, kufanya kazi kwa bidiii, maarifa na kujituma, wakulima walime kilimo cha kisasa ambacho kitawafanya wavune mazao mengi.  Awali Mama Kikwete pia alifungua jengo la ofisi ya CCM lenye thamani ya shilingi milioni 35 ambalo limejengwa na Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe.   Waziri Membe alisema kuwa jengo hilo lina vyumba sita ambavyo ni ofisi za jumuia zote za chama hicho ambazo ni Vijana, Wanawake, Wazazi, pia kuna ofisi za Mbunge, Mjumbe wa NEC na chumba cha mikutano.   Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Ally Mtupa aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na mahusiano mazuri baina yao na viongozi wanaowaongoza. Wakisikia jambo wasiwe na papara ya kukimbilia kuandamana bali wafanye upelelezi kwanza na wakishabaini ukweli ndipo wachukue hatua.   Mtupa alisema, “Hivi sasa kuna watu wanapita mitaani na kupotosha ukweli kuwa Serikaliyetu haijaleta maendeleo, wamesahau kuwa wanatembea katika barabara na kutibiwa katika Hospitali zilizojenga na CCM, tunawaomba watu hawa wawaheshimu viongozi wanaotawala kwani hata vitabu vya dini vinasisitiza umuhimu wa kuwatii viongozi waliopewa mamlaka ya kutawala”.   Sherehe hizo zilienda sambamba na mchango wa matembezi ya mshikamono ambapo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana, ufunguzi wa ofisi za CCM Kata ya Chiponda, ufanyaji wa usafi wa mazingira , kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, utoaji wa kadi kwa wanachama wapya ambapo wanachama wapya wa CCM 286 walijiunga,Jumuia ya wazazi 63 na kutoka vyama vya upinzani 23 walipewa kadi katika sherehe hizo.

   Viongozi wa CCM Wakiongozwa na Mama Salma Kikwete  wakikata keki kuashiria kuzaliwa kwa chama hicho
   .Wanachama wa ccm wakisikiliza hotuba ya Mjumbe wa Nec,Mama salma kikwete
  Mjumbe wa Nec,Mama Salma Kikwete akifurahia burdan iliyokuwa inatolewa na Wasanii katika sherehe za ccm.

  0 0
 • 02/06/13--23:36: lakeland africa THIS WEEKEND

 • HELLO DAR ES SALAAM RESIDENTS
  LAKELAND AFRICA NOW BRINGS YOU AFFORDABLE WEEKEND TOURS THAT STARTS EVERY SATURDAY AND RETURN ON SUNDAY.

  OUR DESTINATIONS ARE: MIKUMI NATIONAL PARK, SAADANI NATIONAL PARK, KILWA HISTORICAL SITES, BAGAMOYO, PANGANI AND LUSHOTO.
  YOU WILL TRAVEL IN AN OVERLAND TOURIST TRUCK, CAMP IN OPEN AFRICAN SKIES AND EAT FOOD PREPARED BY THE CHEF ONBOARD.
  AT NIGHT YOU SIT BY THE CAMPFIRE AND CHAT ABOUT THE HAPPENINGS OF THE DAY.

  COME MEET FELLOW EAST AFRICANS AND OTHER CITIZENS OF THE WORLD AND MAKE FRIENDS ALONG THE WAY.

  CALL LAKELAND AFRICA TODAY ON +255 222 761811 
  OR VISIT WWW.LAKELANDAFRICA.COM FOR DETAILS
  GOOD TIMES NEVER LAST BUT GOOD MEMORIES DO!

  UPCOMING TRIPS: 09-10 FEB 2013 MIKUMI NATIONAL PARK
  16-17 FEB 2013 KILWA HISTORICAL TOUR
  23-24 FEB, 2013 SELOUS GAME RESERVE 

  0 0

  Ramadhani Shauri na Mkanda wa Ubingwa wa IBF Afrika

  Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight) Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.

  IBF imeamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,

  Mabondia wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.

  Kama Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King, Bob Arum na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya kujitangaza kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati ya nchi zinazotoa mabingwa wa dunia.

  Kama Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia ya ngumi nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na WBA.

  Shiriksiho la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu ya kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.

  IBF/Africa inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na makampuni mbalimbali bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri ufadhili wa kuweza kuligombea taji hili.

  Mungu mbariki bondia Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amen.

  Imetolewa na:

  UTAWALA
  Shiriklisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa)
  Dar-Es-Salaam, Tanzania

  0 0
 • 02/07/13--00:01: DStv’s BIG SURPRISE
 • Most people agree…winning a cash prize is always great. You can buy what you want, go where you want and do what you want…it’s your money and your choice. So the news that the continent’s leading pay TV operator MultiChoice Africa is giving away cash prizes to simply say thank you to its subscribers is very good news!

  From February 5 until April 10, DStv subscribers in Tanzania stand the chance of winning 5,000,000Tshs in cash for simply staying connected to DStv’s exciting world of sport, movies, music, news, kids, documentary and lifestyle entertainment. MultiChoice Africa has also announced that all its DStv subscribers in Tanzania are eligible to win cash prizes, regardless of the bouquet they subscribe to.

  MultiChoice Africa CEO Nico Meyer says that DStv was particularly pleased by the support it has received and wished to express its gratitude that consumers continue to choose DStv for its diverse range of bouquets and channels.

  “We’re always searching for new ways to add extra value to our subscribers’ lives. Whether through innovative programming, embracing new technology or expanding our operations network, we aim to be the best. This year we’re consolidating all our subscriber loyalty competitions and initiatives into one portfolio called DStv Rewards.”

  He continues, “With the exciting game show THE MONEY DROP currently on AfricaMagic, we decided that the time was right for a significant cash give-away. So you can watch people win on TV and you can win at home! We definitely intend for DStv Rewards to become a major part of our brand’s overall identity in future. DStv Rewards may include cash prizes, trip give-aways, luxury gifting, channel promotions and more. And we will move between markets so while a country may not be included in one promotion, it will be included in others.”

  But that’s not all… winners walking away with cash prizes will be filmed for inserts that will be screened during the hit game show THE MONEY DROP on AfricaMagic and AfricaMagic Entertainment. So not only could you win, but you could also be on TV!

  And the exciting news continues…

  In addition, DStv audiences can win a full year’s subscription to their current bouquet, just by watching their favourite shows. Tune in and when you see a blue DStv Rewards Box pop up on screen, make sure you SMS/TEXT the competition hotline (details onscreen and at www.dstv.com) with your name. It’s that easy to win!

  DStv has also confirmed that there will definitely be winners from Tanzania because it will be drawing winners from all its key markets. One word of advice – make sure your contact details are updated on your DStv account so that if you win, you will get the good news quickly.

  The latest initiatives come just a few short months after DStv launched its attention-grabbing 10% discount campaign, also part of the DStv Rewards initiative, which knocks 10% off the subscription price for those consumers who pay on time and who enjoy unbroken service. So make sure you pay before you are disconnected and you will earn this discount. With 2013 getting off to a fantastic start for DStv subscribers, the question is…what would you do with your cash winnings?

  0 0
 • 02/07/13--01:51: kutoka bungeni mjini dodoma
 • Baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wakielekea katika mkutano wa kumi kikao cha saba leo mjini Dodoma.
  Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo (kulia) na Christowaja Mtinda (Viti Maalumu) wakielekea katika ukunbi wa Bunge – Dododma leo.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia ya Watoto Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za Wizara yake Bungeni leo.
  wanafunzi wa Shule ya Independence kutoka Dar es Salaam wakitambulishwa Bungeni leo.
  Mjumbe wa Timu ya watu sita Bernardetha Mushashu (Viti Maalumu (kushoto) akipokea vitabu vya mtaala wa Elimu ya Awali (2005), Mtaala wa Elimu ya Msingi (2005) na Mtaala wa Elimu ya Sekondari (2005) kutoka kwa Mfanyakazi wa Bunge Modesta Kipiko ,kwaajili ya kwenda kuchunguzwa vitabu vya mitaala vilivyowakilishwa mezani leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa Bungeni ili kujiridhisha. (hayupo pichani).
  Salehe Pamba (kulia) amkisikiliza Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya sola ya Rex Energy Francis Kibhisa jinsi ya matumizi mbalimbali ya umeme wa Sola. Maonyesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (kushoto) January Makamba wakibadilishana mawazo na Ahmed Shabiby(Gairo) katika viwanja vya Bunge .
  Waziri wa Fedha William Mgimwa akijibu hoja ya Amina Mwindau (Viti Malumu-hayupo pichani) kuhusu Deni la taifa limekuwa likiongezeka kwa kasi kubwa mwaka hadi mwani, na kutaka kujua Je, serikali ina mikakati gani wa kukabiliana na deni hilo.(Picha na MAELEZO).

  0 0

  By. Geofrey Tengeneza

  Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

  Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.

  Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.

  0 0

  Mrs. Leticia Daudi Lusala

  Mungu wetu ni Mwema, ametuliza mioyo yetu katika mwaka huu mzima wa ukiwa na majonzi mengi kwa kumkosa mpendwa wetu Leticia. Ndio maana tunajumuika tarehe 8 na ( ili kushukuru mungu na kumwomba amweke mahali pema peponi amina.

  Familia ya Mr. Lusala inapenda kuwakaribisha katika misa ya kutimia kwa mwaka mmoja tokea tulivyompoteza mama yetu mpendwa marehemu Leticia Lusala, itakayofanyika siku ya jumamosi tarehe 9 feb nyumbani sinza na misa tarehe 9 katika kanisa katoliki la sinza,halafu safari ya kwenda makaburini kinondoni kwa sala fupi, tunaomba wote tujumuike kumsalia na kumsindikiza mama yetu mpendwa.

  Kwa habari zaidi wasiliana na Seraphin 0786303038 na Edward 0754091883

  0 0
 • 02/07/13--02:26: taatifa toka TFF leo

older | 1 | .... | 37 | 38 | (Page 39) | 40 | 41 | .... | 3284 | newer