Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 375 | 376 | (Page 377) | 378 | 379 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kesho (Jumatano Machi 5, 2014) anaongoza hafla inayowakutanisha wanawake zaidi ya 250 kutoka kada mbalimbali wakiwemo wasomi, wake wa viongozi, wajasiriamali, wanasiasa kuangalia mafanikio ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii wa mwanamke hapa nchini.

   Wanawake hao wanakutana chini ya kile kinachoitwa “Connected Women” ya Kampuni ya Vodafone ambapo kupitia hafla hiyo wanawake hao watajadali mchango wa teknolojia ya simu za mkononi na jinsi ilivyobadili maisha ya wanawake hapa Tanzania kupitia miradi inayofadhiliwa na Vodacom Foundation.

  “Shabaha ni kujenga daraja kwa wanawake wenye mafanikio kwa umoja wao kujenga hamasa na kuwawezesha wenzao wasio na mafanikio kufikia mafanikio ili kuondoa pengo la utofauti wa jinsia lililopo ndani ya jamii hususani sekta ya elimu, afya, uchumi na uongozi.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Georgia Mutagahywa. 

   Usawa wa kijinsia imekuwa ni ajenda ya muda mrefu katika mataifa mbali mbali duniani ambapo mengi yao wanawake wamekuwa wakinyimwa fursa za msingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuleta mafanikio ya kasi kwa jamii husika.

   Mama Salma Kikwete anatarajiwa kuwakutanisha wanawake hawa ambao wamefanikiwa kwa kuwezeshwa kupata fursa za kielimu, kiafya, kiuchumi na uongozi mpaka kuwa watu muhimu na wanaotambulika ndani ya jamii ya watanzania.

   Hafla hiyo inayofadhiliwa na Vodacom ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake dunaini inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

   Mutagahywa aliongeza kuwa “Wapo wanawake wenye nyadhifa kubwa serikalini, katika sekta binafsi pamoja na mafanikio ya kiuchumi ambapo  kwa umoja wao wakiamua kutumia nafasi walizonazo wanaweza kumkomboa mwanamke mwenzao kutoka katika tanuri la usawa wa kijinsia.”

   Utofuati huu wa kijinsia pamoja na sababu nyengine unachangiwa pia na mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo siku zote zinamkandamiza mwanamke na kumfanya abaki nyuma katika shughuli zote za kimaendeleo huku zikimpa nafasi zaidi mwaname”. Alisema.

  Miongoni mwa mafanikio ambayo teknolojia ya simu za mkononi katika kubadili maisha mpango wa M-pesa wa kuwawezesha wanawake mikopo nafuu isiyo na riba – MWEI, mradi wa fistula katika hospitali ya CCBRT

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.

  Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.

  Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.

  TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza.

  Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer

  Tanzania Football Federation (TFF)

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid akifungua mafunzo kwa wanahabari na waratibu wa NHIF/CHF wa mkoa wa Lindi,Kushoto ni Meneja Nhif Lindi,Bi Fortunata Kullaya na kutoka kulia ni Bw Faustine Nzota,Mshauri wa Mfuko wa Afya na anaefuata ni Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Wilaya ya Nachingwea,Christopher Lilai.
  Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi akitoa taarifa fupi kuhusiana na mfuko huo katika mafunzo ya wanahabari na waratibu wa Mifuko ya CHF na NHIF Lindi.
  Mratibu wa CHF wilaya ya Liwale akichangia kuboresha mfuko huo katika mkutano wa mafunzo kwa wanahabari na waratibu.
  Washiriki wa Mkutano huo.

  Na Abdulaziz Video,LINDI

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) mkoani Lindi,imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa Habari na waratibu wa Mifuko hiyo,ili kuboresha utendaji kazi ili kutatua changamoto za Afya kwa jamii ya wakazi wa mkoa huo.

  Akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo,Meneja wa (NHIF) mkoani hapa, Fortunata Raymond Kullaya ameeleza kuwa mafunzo hayo yaliyojumuisha waandishi wa habari na waratibu kutoka Halmashauri zote sita za mkoa huo yamelenga katika kuboresha utendaji wa kazi na kubaini changamoto mbalimbali zinazokwamisha jamii kujiunga na mifuko hiyo ukiwemo wa Afya ya Jamii(CHF).

  Aidha alibainisha kuwa wanahabari wanashiriki vizuri katika kuhamasisha na kuwapa wananchi taarifa muhimu, zikiwemo za kujiunga na Mifuko hiyo ya (NHIF na CHF) ili kuwaondolea usumbufu pale wanapokwenda kupata huduma za matatibabu pale wanapougua.

  Kullaya pia alisema kuwa Ofisi yake imeona upo umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo ili wanahabari waweze kuielimisha jamii iweze kubaini fursa zitakazowezesha utatuzi wa Changamoto hasi na chanya za huduma sanjari na kubadilishana uwezo wa kiutendaji baina yao na watumishi wa mifuko hiyo.

  Kullaya akataja sababu nyingine ni pamoja na kuwapa elimu ya mabadiliko yaliyotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya pamoja na maboresho yaliyokwishatekelezwa hivi karibuni na kuwa na kauli moja. "Kama mjuavyo ugonjwa unapokwenda kwa mwanadamu haupigi hodi,hivyo muda unapokujia huna pesa za kujitibia,Bima yako itakusaidia kukuwezesha kupata matibabu sehemu yeyote hapa nchini kwetu"Alisema Kullaya.

  Akifungua Mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid aliwataka Waratibu wa Mifuko hiyo kuhakikisha dawa zinapatikana na Wahudumu wa Afya wanakuwa na Lugha Mzuri kwa wagonjwa wanaowahudumia ambapo pia aliitaka ofisi ya NHIF Pia kutumia viongozi mbalimbali wa Serikali katika kuhamasisha kutokana na Idadi ndogo ya Jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii ambapo kwa mkoa wa lindi ni asilimia 6.6 tu ndio iliyojiunga na mfuko huo.

  Katika kupunguza makali ya Tiba katika hospital za Binafsi licha ya kuwa na gharama ndogo za Uchangiaji kwa kaya ambapo unalipa mara moja kupata huduma za Tiba kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  Nae Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid ameahidi kushirikiana na ofisi hiyo ili wanahabari watumie kalamu zao katika kuhakikisha Jamii inapata huduma stahiki ikiwemo kushauri pale ambapo kuna changamoto zinazochangiwa na watoa huduma sambamba na kutoa wito kwa Wanahabari kujiunga na mifuko hiyo badala ya wao kuhamasisha tu.

  Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoratibiwa na Ofisi ya Mkoa ya NHIF pia wito umetolewa kwa zahanati,Vituo vya Afya vilivyopo mkoani humo kutumia fursa ya kukopa Vifaa tiba kwa mikopo na nafuu Kupitia katika mfuko huo ambapo malipo yake yatakatwa kupitia madai mbalimbali wanapowahudumia wagonjwa wa Mfuko wa NHIF

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akisalimiana na Mhe. Tanja Rasmusson, Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden alipofika Wizarani leo. Mhe. Rasmusson yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, uwekezaji, elimu, haki za binadamu na vita dhidi ya rushwa.
  Mhe. Rasmusson akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Wizarani.
  Wajumbe waliofuatana na Mhe. Rasmusson wakifuatilia mazungumzo kati ya Bw. Haule na Mhe. Rasmusson (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Washiriki wa warsha ya miradi ya ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa miradi TASAF Amadeus Kamagenge mara baada ya kufungua warsha hiyo.
  Mkurugenzi wa miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge akifungua warsha ya miradi ya ujenzi kwa wataalam wa halmashauri ya manispaa ya kibaha ikiwa ni moja ya mikakati ya kufanikisha mpango wa kunusuru kaya masikini unao
  Washiriki wa warsha ya miradi ya ujenzi wakimsikilza kwa makini mkurugenzi wa miradi TASAF Amadeus Kamagenge (hayupo picha) wakati wa warsha hiyo.
  TASAF yaanza kuwajengea uwezo wataalaam watakaosimamia miradi ya ujenzi kufanikisha mpango wa kunusuru kaya masikini (PSSN).
  Mkurugenzi wa Miradi (DCS) wa TASAF Amadeus Kamagenge akilakiwa na baadhi wa washiriki, kufungua warsha ya miradi ya ujenzi katika halmashari ya manispaa ya Kibaha

  0 0

  Gari likiwa limebeba matenga ya nyanya kutoka shambani,katika kijiji cha Magubike,Iringa Vijijini mapema leo,tayari kwa kusafirishwa kupelekwa mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuuzwa,Mmoja wa wakulima wa zao hilo la Nyanya aliyejitambulisha kwa jina moja la Ezekiel alieleza kuwa wakulima wengi wa zao hilo kwa sasa wako kwenye mavuno,akaongeza kuwa changamoto kubwa walionayo ni suala la barabara kwa ajili ya kusafirisha mazao yao,si ya za uhakika sana kutokana na jinsi zilivyo,"hapa mvua ikinyesha tu ni shida sehemu kubwa ya barabara magari yanashindwa kupita kwa sasa miundombinu yenyewe ni mibovu,hivyo tunaiomba serikali iangalie pia suala la miundombinu kwa wananchi wa kijiji hiki,angalau basi barabara iwe ya uhakika na inapitika.ili mazao yetu yasituharibikie/ozea nyumbani ama mashambani" alisema Ezekiel.

  0 0


  0 0


  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Jenista Mhagama (Kushoto) ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bi. Christowaja Mtinda wakiwasili katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimwelekeza jambo Mtangazaji wa TBC ONE Bw. Shaaban Kissu wakati akiwasili katika katika ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa bunge maalum la Katiba Jumanne Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Maji akiwa na Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira( Kulia). Leo Mjini Dodoma. Chini yao ni wajumbe wa Bunge Hilo Seif Khatibu( Kushoto) na Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo Wajumbe wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma

  (PICHA NA HASSAN SILAYO)

  0 0
 • 03/04/14--12:30: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0
 • 03/05/14--02:34: Article 24
 • Guardian Angels Children's Home  we are happy to welcome visitors/volunteers from all over the world to our home.

   You will have chance to meet beautiful children  and spend time with them, playing games,help them with their studies etc.

  Conctact us on our website: www.angelstz.org, email mirium2000@gmail.com or info@angelstz.org .
   Call us on +255 757 855858.
  We are at Mbezi Temboni, near Sinon College.

   If you will be in Dar es Salaam ,please consider to visit us!

  0 0

  Gavana wa Klabu za Lions kanda ya Tanzania na Uganda, Wilson Ndesanjo ( katikati) akimkabidhi tuzo ya juu iliyotolewa na klabu za kimataifa za lions kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi, kwenye hafla ya kukabidhi tuzo hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Gavana Ndesanjo amekabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa klabu hizo, Barry Palmer ambaye ametambua mchango mkubwa unaotolewa na Dk Mengi kwa jamii. Kushoto ni Gavana wa zamani wa kanda hiyo, Abdul Majjid Khan. 

  0 0


  0 0
 • 03/05/14--03:47: YALE YALEEEEEE.......
 • Ankal salamaaaa? 

  Leo katika pita pita zangu,nilibahatika kupita Barabara ya Nyerere mbele ya Mataa ya Tazara,nililikuta Gari hili lililazimishwa kugeuzwa katika sehemu ambayo si salama na wala hairuhusu kufanyika hivyo,kwani pia gari hilo lilikuwa linakanyaga sehemu ya baraza la kati lilalotenganisha upande mmoja na mwingine wa barabara.

  Nilimshangazwa sana na yule Jamaa ambaye inaonekana dhahiri kuwa aliona uvivu au ugumu wa kwenda kwenye kona inayomhusu ili akate kulia na ageuze Lori lake hilo.

  Nilikasirishwa sana na kitendo hicho na ilinitia uchungu sana kuona kodi zetu zinaharibiwa kizembe hivi,nikasisimama na kuanza kumueleza Dereva huyo ambaye alianza kupayuka kwa nguvu na kama kawaida mimi ndie nilieonekana mjinga kwa wapita njia maana wao hawakujali.

  Naomba Wahusika wamsake muharibifu huyu wa miondombinu yetu ili kina Dkt Magufuli na Tanroads wamshughulikie. 

  Mdau Mpenda Maendeleo ya Nchi.
  Sehemu ya Uharibifu uliofanywa na Dereva huyo.

  0 0

  Mchungaji kiongozi wa kanisa la Kinondoni Reviral Church ambao ndio waandaaji wa mkutano wa Injili unaoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni, Dkt. Rogate Swai akihubiri neno la mungu katika mkutano huo.
  Waambaji wa kwaya wa Kanisa la Kinondoni Reviral Church wakipamba jukwaa katika mkutano mkubwa wa injili unaoendelea kufanyika katika viwanja vya Biafra,Kinondini jijini Dar es salaam.
  Mamia ya watu wakifuatilia kwa karibu mkutano huo mkubwa na waaina yake, katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dare s salaam.

  0 0

  Baadhi ya wateja wakubwa wa benki ya NMB na wafanyabiashara jijini Mwanza wakimsikiliza meneja wa mahusiano wa biashara,Wogofya Mfalamagoha wakati wa mkutano elekezi kwa wateja wa benki hiyo uliofanyika katika Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza leo.


  0 0

   Naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.
   Fredrick Mwakalebela akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.
   kulia ni mratibu wa mafunzo hayo Anzawe Chaula akiwa na baadhi ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.

  =======  ======  ==============
  WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

  Na Denis Mlowe,Iringa

  KAMPUNI ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA wametoa msaada wa kielimu kwa wajasiriamali zaidi ya 200 walioko mkoani Iringa kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

  Mratibu wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare, Anzawe Chaula alisema baada ya kubaini wajasiriamali mkoani Iringa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu ya biashara ndogondogo na kusababisha wengi wao kushindwa kuendeleza biashara zao wanazozianzisha.

  Alisema mafunzo hayo yatawasaidia wajasiriamali kutambua fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa na kuwataka kuyafanyia kazi mafunzo hayo waliyopatiwa katika kujikomboa kiuchumi.

  Kwa upande wake mgeni rasmi wa mafunzo hayo Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa Gervas Ndaki akizungumzia kuhusu mafunzo hayo alisema kuwa ni muhimu kwa wajasiriamali kwani ni kati ya fursa za kielimu ambazo zinaweza kuwakwamua na kuondokana na umaskini wakizingatia kwa umakini.

  Alisema wajasiriamali hao watanufaika na mafunzo hayo na uwezekano wa kupata mabadiliko makubwa kiuchumi upo kwa sehemu kubwa na hivyo hali ya utegemezi kwa baadhi ya wanawake itapungua.

  Ndani alisema pamoja na mafanikio hayo kuna tatizo ambalo kama halitatatuliwa kwa wajasiriamali hao kupatiwa mafunzo kwa ujumla yatakuwa hayana manufaa na kuishia kuwa na kumbukumbu za kwenye daftari na kuwataka waifanyie kazi elimu hiyo waliyopata bure na kuwashukuru wafadhili hao.

  “Ni kweli mafunzo haya yamewapa mwelekeo wa maisha wengi hatukuwa na chochote katika ujuzi, lakini mafunzo haya yanahitaji mali ghafi na mitaji lakini kutokana na mafunzo haya utajua ni sehemu gani ya kuanzia na kuweza kujinufaisha katika maisha yako na kuongeza uchumi wa nchi yako na wewe mwenyewe kwa ujumla na itakuwezesha  kuendesha miradi inayoibuliwa ”alisema Ndaki.

  Ndaki aliwataka wajasiriamali hao kuwa wabunifu katika kuzitumia fursa za elimu na kusikitika kwa kiasi kubwa kwa wajasiriamali wa Iringa kushindwa kujitokeza kwa wingi kama ilivyokuwa malengo ya wafadhili wa mafunzo hayo kukadilia zaidi ya wajasiliamali 1000 kujitokeza.

  Aidha alizitaka taasisi za kibenki kupunguza masharti ya mikopo kwa wajasiriamali na kuiomba serikali kutoa hamasa kwa asasi za kifedha za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kuangalia uwezekano wa kuwapa mikopo wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji na kukuza pato la Taifa.

  0 0

   Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akiwasili katika ofisi za bunge mjini Dodoma Leo
   Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akisalimiana na Mhe.James Lembeli
   Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akisalimiana na Mhe. Muhammad Seif Khatibu.
  Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, akijadiliana na Mhe.Seif  Khatib (kushoto)  na Mhe.Simbachawene. Pamoja na mambo mengine Jaji Mutungi ameelezea kuridhishwa na mwenendo wa mjadala wa Bunge maalumu  la katiba hasa mjadala wa semina yakujadili kanuni. Wabunge wanaendelea na semina ya kujadili rasimu ya kanuni za bunge maalum jioni hii. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma

  0 0


  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mizengo Pinda amechomoza kwenye zoezi la upigaji kura kuchagua mgeni rasmi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa Tanzania.

  Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era sambamba na Waziri Mkuu, wengine wanaofuatia katika zoezi hilo ni Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi  na Askofu Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International, Sylvester Gamanywa,  mchungaji wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ pia wanamfuatia Waziri Mkuu katika zoezi la upigaji kura linaloendelea.

  Mang’era anaendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika pasaka acha nafsi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.

  Pia kwa mgeni rasmi  andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda ili tamasha lifanyike.

  Aidha Mang’era mbali ya viongozi hao wa dini na serikali, pia waimbaji Jescar BM  na Bahati Bukuku ni mojawapo ya waimbaji wanaoonekana kuelekea kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa kuwa na kura nyingi.

  Mang’era alisema mikoa ambayo inaongoza kupigiwa kura nyingi ni pamoja na Mwanza, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam inapigiwa kura nyingi kwa ajili ya kufanyika kwa tamasha hilo.

  Makamu Mwenyekiti huyo alisema kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo wanazingatia na kutekeleza yale ambayo yanayotakiwa na wadau ambao wanachagua wanachopenda.

  0 0


  -Katika kusherehekea siku ya Wanawake Jumamosi hii tarehe 08-03-2014 Bendi yako PENDWA ya Twanga Pepeta ikishirikiana na Mdau wake mkubwa Christer Bella Mwingira na Rukia Saloon, kwa pamoja wameandaa bonge la Pati kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hii.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka (pichani), mnuso huo unataraji kufanyika ndani ya Twanga City Mango Garden ambapo muonekano wake utakuwa tofauti na siku za kawaida kwa kuwa ukumbi utapambwa vilivyo.

  Amesema Mavazi rasmi yatakuwa ni ya ya rangi NYEKUNDU, NYEUPE na NYEUSI, na kwamba -Zawadi kedekede zitatolewa na Rukia Saloon na Christer Bella Mwingira kama vitenge na Khanga ambayo ni mavazi rasmi ya mwanamke.

  Ameongezea pia kutakuwa na ofa maalum kwa ajili ya akina mama toka kwa Mkurugenzi wetu Asha Baraka kwa kila atakayefika katika onyesho atalipia Tshs 5,000. kuanzia saa mbili mpaka saa nne usiku.

  -Kiingilio kitakuwa ni Tshs 10,000. kwa VIP 
  pamoja na kinywaji na kawaida ni Tshs 7,000/=

  0 0

  Serikali ya China imekubali kuendesha mafunzo kwa wana michezo 30 wa Tanzania wanaotegemewa kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Nchi za Jumuiya ya Madola  Julai 2014. Vilevile Tanzania na China zimekubaliana kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia unaoendelea kuimarika kila mwaka hususan kwa sasa nchi hizo zinaposherehekea miaka 50 ya ushirikiano. 


  Makubaliano hayo yalifanyika wakati Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na China walipokutana mjini Beijing wiki iliyopita kuzungumzia masuala yanayohusu maeneo ya ushirikiano wa nchi hizi. Mhe. Wang Yi alisema ushirikiano baina ya nchi hizi ni wa kidugu na hivyo Serikali ya China itaendelea kusaidia kwa hali na mali miradi waliyoahidi kwa maendeleo ya Tanzania na watu wake. 


  Mhe. Membe ambaye alikuwa nchini China kwenye ziara ya siku tano, aliahidi kuratibu Wizara na Taasisi za Serikali  zinahusika na miradi ya ushirikiano ili kuhakikisha matunda ya miradi hiyo yanaonekana. Mhe. Membe alisema China ni marafiki wa Afrika lakini ni marafiki wa karibu wa Tanzania hivyo sherehe za miaka 50 ya uhusiano huo zidhihirishwe na miradi ya mafanikio ambayo nchi zote mbili zimekubaliana kwa maendeleo ya watu wake.


  Mbali na misaada ya vifaa mbalimbali vya ujenzi na huduma za maji na afya, hadi sasa Serikali ya China imekamilisha miradi mikubwa ya ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, ukarabati wa Uwanja wa Amaan Zanzibar, ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ifakara na ujenzi wa shule mbalimbali. Miradi mingine kadhaa inaendelea sasa ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Miradi mingine mingi iko kwenye majadiliano kama vile ujenzi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje, awamu ya pili ya Mkongo wa Taifa, Nishati ya Umeme wa Upepo Singida, Bandari ya Mbegani Bagamoyo na ukarabati wa Reli ya TAZARA. 


  Akiwa kwenye ziara hiyo, Mhe. Membe pia alikutana na Makamu wa Rais wa China Mhe. Li Yuanchao ambaye alielezea China inaitazama Tanzania kama mshirika mwenza kwenye maendeleo, hivyo uhusiano wa nchi hizo una manufaa sawa kwa pande zote mbili. Alisema ukuaji wa uchumi wa nchi nyingi za Kiafrika umesababisha Serikali yake kushawishi wawekezaji wengi kuwekeza Afrika, lakini hali ya usalama na utulivu nchini Tanzania inawavutia wengi kuwekeza zaidi huko.


  Mhe. Membe na ujumbe wake pia walikutana na kufanya mzungumzo na Makamu Waziri wa Biashara Mhe. Li Jinzao ambapo aliainisha miradi mbalimbali inayotekelezwa na China kwa sasa. Mhe. Jinzao alisema mbali na miradi mingi inayoendelea kwa sasa mradi wa kukarabati Reli ya TAZARA unapewa kipaumbele na Serikali ya China kwani ndio mradi wa kwanza baina ya nchi hizi mbili.


  Katika mazungumzo yake na Makamu Waziri wa Usalama wa Raia Mhe. Wang Hanning, Waziri Membe alipendekeza kuanzisha ushirikiano wa karibu baina ya Wizara ya Usalama wa Raia China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania ili kusaidiana katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuhalifu duniani. Mhe. Hanning alikubali pendekezo hilo na kueleza kuwa kwa sasa uhusiano wa wananchi wa nchi mbili umeimarika, kuna raia wengi wa China nchini Tanzania na kinyume chake. Hivyo ni wakati muafaka kwa Wizara hizo mbili kuanza ushirikiano wa karibu kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili. 


  Mhe. Membe na ujumbe wake pia walifanya mikutano na Makamu Meya wa Jiji la Shenzhen Bw. Chen Biao na Makamu Gavana wa Jimbo la Guangdong Bibi Zhao Yufang na ujumbe wa Serikali ya Guangdong. 


  Waziri Membe alimalizia ziara yake kwa kukutana na viongozi mbalimbali wa biashata na makampuni ya sekta binafsi ambao wengi wao ndio wahusika wa miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ushirikiano na China. 


  Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,

  DAR ES SALAAM

                        5 MACHI, 2014

older | 1 | .... | 375 | 376 | (Page 377) | 378 | 379 | .... | 3285 | newer