Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 376 | 377 | (Page 378) | 379 | 380 | .... | 3282 | newer

  0 0

  ................................................................................................
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.Mangula amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini.Kiongozi huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya kata hiyo. 

    Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda. 

    Samson alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika. 

    “CHADEMA hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanatakakuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa. 

    Kwa mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo. 

    Betha alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha, alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla. 

    Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wake atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa kufariki dunia Januari mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

  0 0
 • 03/05/14--05:43: Article 12


 • 0 0

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, na wadau mbalimbali wa afya leo walizungumzia madhara ya ugonjwa hatari wa homa ya ini kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana Jijini Dar. 
  Miongoni mwa wadau waliokuwa kwenye mkutano huyo ni madaktari mbalimbali, Sanofa ambao huhusika na vipimo vya ugonjwa huo, Damu Salama ambao huhusika na upimaji wa damu na SD Tanzania.
  Shigongo akizungumza kwa masikitiko jinsi watu wengi walivyo kwenye hatari ya kufa kwa ugonjwa wa ini.
  …Akiwa na jopo la madaktari. Kushoto ni Dk. Mtebe Majigo, Mganga Mkuu wa Amana, Meshack Shing'wela (wa pili kulia) na Daktari Kiongozi Andrew Method.
  Ndeonasio Towo kutoka Damu Salama akielezea umuhimu wa wananchi kupima damu kubaini maradhi mbalimbali bila kusahau virusi vya homa ya ini.
  Mwakilishi kutoka SD Tanzania ambao ni wadau wa ugonjwa huo, Phillip Sawe, akielezea umuhimu wa kupima mapema ugonjwa huo kabla mwili haujashambuliwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Of recent there has been information circulating in the social media originating from the story that was written in the Daily News Online (http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/27935-mt-k-njaro-overwhelmed-by-climbers) which is a Tanzanian online newspaper. 
  Briefly the article was trying to quote some of the officials from Tanzania National Parks saying that Mount Kilimanjaro is currently overwhelmed by thousand of people and thus threatening the natural feature’s ecological balance.
  Tanzania National Parks would like to 
  clarify on this incorrect information as follows:

  0 0

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya akiwa amebeba watoto watatu mapacha Catherine, Caroline na Cathrine ambao walizaliwa mwanzoni mwa wiki hii katika Hospitali ya AICC Jjiini Arusha. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Hospitali ya AICC Prof. Sendui Ole Nguyaine (kushoto), mama mzazi wa watoto hao, Janeth Kimario (katikati) pamoja na wauguzi wa Hospitali hiyo. (Picha kwa hisani ya AICC). Mama huyo alijifungua kwa njia ya oparesheni wakiwa na afya njema. (Picha na AICC).

  0 0  0 0

  Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro amefanya ziara katika Kisiwa cha Anjouan. Akiwa Anjouan Mhe. Balozi Kilumanga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe. Aniss Chamsudine kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kisiwa cha Anjouan na baadhi ya Mikoa ya Tanzania, hususan katika nyanja za elimu na uwekezaji. 
  Baadaye, Mhe. Balozi alitembelea maeneo mbalimbali ya kisiwa hicho na kujionea vivutio vya utalii pamoja na mazingira ya uwekezaji. Kisiwa cha Anjouan chenye wakazi laki tatu, ni sehemu ya Muungano wa Visiwa vya Comoro. 
  Kisiwa hiki kimepambwa na mandhari nzuri ya mito ya maji baridi inayotiririka kwenye milima kutoka kwenye bwawa la asili lililopo kileleni mwa kisiwa hicho. Takriban kisiwa chote kimekolezwa na rangi ya kijani kutokana miti aina mbalimbali inayositawi vyema, kama vile minazi na mikarafuu jambo ambalo linachangiwa na hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutuba. Itakumbukwa kwamba mwaka 2008 Tanzania iliongoza vikosi vya Umoja wa Africa kumaliza uasi wa Kanali Mohamed Bacar aliyejaribu kukitenga Kisiwa cha Anjouan kutoka kwenye Muungano wa Visiwa vya Comoro. 
  Tangu wakati huo hadi sasa, viongozi na wananchi wa Anjouan pamoja na Wacomoro kwa ujumla wanayo kumbukumbu ya mchango wa Tanzania katika kukikomboa kisiwa hicho.
  Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga na ujumbe wake wakitembelea maporomoko ya maji  wakati  wa ziara ya kisiwa cha Anjouan, katika Muungano wa Visiwa vya Comoro.

  Mhe. Aniss Chamsidine, Gavana wa Kisiwa cha Anjouan (mwenye suti) akiwa na  Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga na Mke wake, Mama Irene Kilumanga na afisa wa ubalozi Ali Jabir Mwadini wakati  wa ziara ya kisiwa cha Anjouan, katika Muungano wa Visiwa vya Comoro.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro (kushoto) akimkabidhi bati Bi. Ami Mahenge, ambaye ni mmoja kati ya waathirika wa kimbunga katika kijiji cha Ndulamo, Makete. 
   Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro akiwa na waathirika hao muda mchache kabla ya kuwakabidhi.
   Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na waathirika wa kimbunga katika ofisi za kijiji cha Ndulamo.
   Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo akizungumza na waathirika wa kimbunga (hawapo pichani) wakati wa kuwakabidhi bati kama walivyoahidiwa na serikali.
   Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kabla ya kukabidhi bati kwa waathirika wa kimbunga katika kijiji cha Ndulamo.
   Bati zenyewe.Picha zote na habari na Edwin Moshi.
  =====
  Kufuatia maafa yaliyokikumba kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoa wa Njombe ya nyumba 10 kuezuliwa na kimbunga mwishoni mwa mwezi februari mwaka huu, halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kushirikiana na mfuko wa jimbo, hii leo wamekabidhi bati 180 kwa waathirika wa maafa hayo.
  Akizungumza na waathirika wa tukio hilo wakati wa kukabidhi bati hizo zenye thamani ya tsh. milioni 2.5, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema kufuatia mkutano uliofanyika baina ya serikali na wananchi wa kijiji hicho, waligawana majukumu ambapo serikali iliahidi kutoa bati kwa wananchi hao, na hii leo imetekelezwa.
  Mh. Matiro amesema ingawa msaada huo haukuwa asilimia 100 kwa waathirika wote lakini wamepatiwa zaidi ya robo tatu hivyo kiasi kilichobakia ni kidogo na kuwaomba wananchi hao kumalizia gharama zilizobaki.
  "Mfano mtu alikuwa ameharibikiwa nyumba yenye bati 24, hapa serikali inampa bati 20 na hizo nne anatakiwa azigharamie yeye mwenyewe, na hii ni kutokana na msaada huo kuhitajika katika vijiji vingine viwili vya makete ambavyo vilikumbwa na maafa tena ili kila mmoja apate kidogo kidogo" amesema Matiro.

  Amesema kwa hivi sasa hawana budi pia kumshukuru mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni waziri wa mazingira Dkt. Binilith Mahenge kwa jitihada zake na uongozi wa wilaya kwa ujumla kuhakikisha wananchi hao wanapata bati hizo na kuwaomba wananchi hao kuzitumia kwa makusudi yaliyopangwa na si kuziuza.
  Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya, kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo amesema ilifanyika tahmini ya kina na wataalamu wa halmashauri mara baada ya maafa hayo kuwakumba wananchi hao, na hivyo kila mwananchi atapewa bati kulingana na ukubwa wa tatizo lake.
  "Kwa mfano wapo waliopata maafa kidogo wanahitaji bati chache, wengine bati mbili hao watapata zote mbili, lakini wale waliopata maafa makubwa watapata bati nyingi ila kila mmoja atagharamia kiasi kidogo pale palipopelea" alisema kaimu mkurugenzi.
  Naye mmoja wa waathirika hao akizungumza na mwandishi wetu baada ya kukabidhiwa bati zake Bi. Ami Mahenge amesema anaishukuru serikali kwa msaada huo aliopewa na kuongeza kuwa kutokana na maafa hayo yaliyomkumba hakujua hatima ya maisha yake, ukizingatia yeye kukosa uwezo wa kifedha lakini msaada huo umekuwa mkombozi wa maisha yake.
  Bi. Mahenge ametoa wito kwa waathirika wenzake kuhakikisha wanatumia ipasavyo msaada huo, kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya kutumia vibaya misaada na baadaye wanaishia kulalamika.

  0 0
 • 03/05/14--07:11: Kali TV this week
 • This week, Kali TV sits down with young Nigerian designer Maryam Elisha who showcased her designs at the DC fashion week.

  0 0

   Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa (kulia) akiwa  na bibi yake, Consolata Semgovano wakipungia mikono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji alichozaliwa cha Magunga, Iringa Vijijini leo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0  0 0

   HOTEL VICTORIA, ILIYO CHINI YA UONGOZI WA MDAU WA DIASPORA CHEF ISSA, IPO SHANGANI WEST MJINI MTWARA.  ILIFUNGULIWA RASMI TAREHE 14 FEB 2014 SIKU YA WAPENDANAO NA KUALIKA WATU ZAIDI YA 200. UNAWEZA KUPATA MAELEZO ZAIDI KWA http://www.hotelvictoria.me/ (JAPO BADO MATENGENEZONI)
   VYUMBA SAFI CHAKULA SAFI NA UKARIMU WA HALI YA JUU. HOTEL NAMBA MOJA MTWARA KWA BEI YA KAWAIDA.

  Chef Issa (shati la draught) akiwa na wafanyakazi wake pamoja na wageni hotelini hapo. Yeye ni mmoja wa wadau wa Diaspora waliorejea nyumbani na kuwekeza. Globu ya Jamii inampa hongera Chef Issa kwa uamuzi huo, hasa wa kuchagua eneo nje ya Dar es salaam, na kukusudia kuleta huduma za kimataifa pamoja na kutoa ajira kwa wananchi. Hongera sana Chef Issa. Wewe ni M-Diaspora wa kuigwa!

  0 0


  0 0

  Mr. Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President for Africa and Mr. Ammish Owusu-Amoah, Managing Director of BANK OF AFRICA - TANZANIA signing of MOU between the two parties to unlock Euros 7 M in Tanzania.
   Mr. Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President for Africa and Mr. Ammish Owusu-Amoah, Managing Director of BANK OF AFRICA - TANZANIA exchange documents after signing of MOU between the two parties to unlock Euros 7 M in Tanzania.
  ------------------------------------

  New lending programme to benefit small businesses across Tanzania

   The European Investment Bank, Europe’s long-term lending institution, has agreed a new lending programme with Bank of Africa Tanzania that will support investment by small companies across the country. 
  The European Investment Bank will provide EUR 7 million (over 15 billion Tanzanian shillings) that will be matched by Bank of Africa.
  The new initiative was formally agreed in Dar es Salaam by Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President for Africa, and Ammish Owusu-Amoah, Managing Director of Bank of Africa Tanzania. 
  The signature was witnessed by Ambassador Filiberto Ceriani, Head of the European Union Delegation to Tanzania.
  “Investment by small and medium sized companies is essential to create new jobs and unlock business opportunities. We are pleased to have signed a new partnership today with Bank of Africa Tanzania. 
  The European Investment Bank is committed to supporting private sector investment across Africa and today’s new initiative demonstrates our continued commitment to Tanzania.” said Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President. 

  0 0
 • 03/05/14--23:38: ankal akiwa bungeni dodoma
 • Ankal akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Riziki Said Lulida bungeni mjini Dodoma. Mjadala wa rasimu ya kanuni za bunge hilo bado unaendelea, ambapo kinachofuata ni uchaguzi wa Katibu wa Bunge hilo na naibu wake ambao wataapishwa na Rais. Kisha Katibu huyo wa Bunge maalum atamwapisha Mwenyekiti wa Bunge atayechaguliwa ambaye naye atawaapisha Wajumbe wote. Baada ya hapo Rais atazindua Bunge na kazi rasmi ya kupata katiba mpya itaanza. 

  0 0

   Balozi Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu akikaribishwa na  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dubai.
  Balozi Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga katika mazungumzo. 

  Katika mazungumzo yao wanadiplomasia hao  walipata fursa ya kuzungumzia njia muafaka na mbali mbali za kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha wanavutia utalii na uwekezaji katika nchi zao hasa kwa kuwavutia wawekezaji kutoka wakubwa waliopo Dubai.

  Mhe. Mjenga alimuomba Mhe. Yibeltal kubadilishana uzoefu wa Ethiopia katika kuvutia wawekezaji kutoka Dubai katika sekta ya kilimo. Alimuomba kuwa Maafisa wa Biashara kutoka Balozi zote mbili wakutane ili kubadilishana uzoefu huo ili Tanzania nayo iweze kuchukua mkondo huo kuwavutia wawejezaji kwenye kilimo.

  0 0

  Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha leo imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani hapo. 

  Magari hayo ni baadhi ya yale yaliyokuwa yakitumika kwa shughuli za usalama kubebea watuhumiwa au watu nyeti,na mahakama hiyo inatarajiwa kumaliza shughuli zake mwakani. 

  Magari hayo ni yale yaliyoimarishwa kiusalama ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake. 

  Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Lebratus Sbas.
  Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR), Bw. Robert Foot akikabidhi funguo za magari hayo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Lebratus Sabas.
  Kamanda Sabas akitoa shukrani zake kwa uongozi wa UN-ICTR kwa msaada huo. Katikati ni Afisa Habari wa Mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa

  0 0  0 0


older | 1 | .... | 376 | 377 | (Page 378) | 379 | 380 | .... | 3282 | newer