Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Wanafunzi wa Tanzania Thailand Waizungumzia sekta ya Madini

$
0
0
Kamishna Msaidizi wa Madini Mhandisi,Hamis Komba (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand. Wa kwanza kulia ni Agatha Mwinuka, anayefuata ni Emmanuel Minja na wa kwanza kushoto ni Doricas Moshi.
Wanafunzi wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea banda la Tanzania.
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.

Na Asteria Muhozya, Bangkok

Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na mchango wake kiuchumi.

Aidha, wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.


RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. PICHA NA IKULU

MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ADOLOTEA NJAVIGE

$
0
0
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
Mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.


Na Mbeya yetu

Hotuba ya Prof. Mwandosya katika uzinduzi wa Kanisa la Moravian - Kariakoo

DStv / SuperSport Key Live Events this weekend

Tamasha la Pasaka, CXC, NSSF wadhamini mkutano TASWA

$
0
0
KAMPUNI ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika kesho.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh milioni moja kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
 
“Tunashukuru Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam,  waandaaji wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
 
“Bajeti yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
 
Alisema mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa aina yake.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

MAISHA PLUS ‘REKEBISHA’ WASHIRIKI KAZI ZA JAMII

$
0
0
 Washiriki wa maisha Plus wakichimba shimo kwa ajili ya kujenga choo cha shule ya msingi Igula.

 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya kazi ya kuchumba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa wamepumzika baada ya kufanya kazi ya kuchimba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Moja ya nyumba za watu wasiojiweza ikiendelea kukarabatiwa na washiriki wa maisha plus 'Jirekebishe'
Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakigawana chakula.


MAISHA PLUS ‘REKEBISHA’  WASHIRIKI KAZI ZA JAMII

Na Denis Mlowe,Iringa

WASHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus walioko katika kijiji cha awali cha Igula kilichoko tarafa ya Ismani kata ya Kihorogota wameshiriki katika kazi za kijamii zikiwemo ujenzi wa choo katika shule ya Msingi Igula.

Washiriki hao 20 wakiongozwa na mwenyekiti Yasinta Hokororo wamefanikiwa kukarabati baadhi ya nyumba ambazo zinakaliwa na wazee wasiojiweza na kufanya shughuli za kilimo kwa walezi wanaoishi nao kijijini hapo.

Akizungumza,Hokororo alisema maisha wanayoishi kijijini hapo ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kijiji ikiwemo kuwasaidia wazee wasiojiweza kuwahudumia shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo.

Alisema changamoto wanazokutana nazo zimewafanya kuwa mahiri katika utendaji wa kazi tofauti na maisha yao ya nyumbani.

Hokororo alisema maisha wanayoishi katika kijiji cha awali lengo kuu ni kurekebisha changamoto wanazokumbanazo wananchi wa kijiji husika zikiwemo za kilimo kwa kuwapa mbinu mbalimbali za kujikwamua na kupata mazao bora.

“Moja ya Changamoto ambazo tumekutana nazo hapa ni masuala ya kilimo na wanafunzi wa shule ya msingi Igula kukosa choo bora hivyo sisi kama vijana tukaamua kuanza na ujenzi wa choo kwa wanafunzi hao na kisha kwenda mashambani kusaidia kazi za walezi wanaotulea.” Alisema Hokororo

Kwa upande wake mkuu wa usanifu wa Maisha Plus Kaka Bonda alisema shindano la mwaka huu limekuja na kauli mbiu ya ‘Maisha Plus 'Rekebisha’ likiwa na lengo la kuingia ndani ya jamii na kuibua na kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo na kuzitatua kwa njia mbadala.

Bonda alisema washiriki wa  shindano hilo watakuwa na jukumu la kufanya kazi za kijamii zaidi na kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha ya kijijini na kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine wanakumbana nazo.

“Kama unavyoona vijana wameanza kutengeneza choo cha shule ya msingi Igula, na wanaendelea na ukarabati wa nyumba ya mzee asiyejiweza baada ya kuanguka na mvua ndio kazi ambazo kwa mwaka huu wa maisha plus rekebisha watahusika nazo washiriki.” Alisema Bonda

Alisema shindano la mwaka huu litakuwa la kimataifa zaidi kwa kushirikisha washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Tanzania.

Alisema maisha plus kipindi cha televisheni kinachoonyesha maisha halisia ya Vijana na Wakulima Wanawake ambao ni mama shujaa wa chakula hivyo washiriki wanaohitajika kuingia katika fainali ni 9 kati ya 19 walioko katika kijiji na kisha wataelekea kijiji cha awali cha Zanzibar.

MWIGULU NCHEMBA AUNGURUMA KALENGA, AMNADI MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO HILO GODFREY MGIMWA MKOANI IRINGA

MWIGULU NCHEMBA ,MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA WASHIRIKI MAZISHI YA WANANCHI WATATU KIJIJI CHA KIDAMALI MKOANI IRINGA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba na akishiriki mazishi ya wananchi watatu waliofarika kwa ajali ya gari,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani humo.
 Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga,mkoani Iringa,Ndugu Godfrey Mgimwa akishiriki mazishi ya wananchi watatu waliofarika kwa ajali ya gari,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani humo.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kidamali wakishiriki kwenye mazishi ya wananchi watatu waliofariki kwa ajali ya gari,iliotokea jana,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo ambapo.Katika mazishi hayo  wanachama wa Chama cha CHADEMA na CCM walishiriki na kutoa ubani wao kwa wafiwa,ambapo CCM walitoa kiasi cha shilingi Miloni moja na CHADEMA shilingi Elfu Hamsini.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga,mkoani Iringa,Ndugu Godfrey Mgimwa wakiteta jambo kabla ya kwenda kutoa pole na kushiriki mazishi ya Wananchi watatu wa kijiji cha Kidamali,waliofariki kwa ajali ya gari hapo jana mkoani humo.

BODI YA VYAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAKUBALIANA NA MFANYA BIASHARA KUREJESHWA MCHELE MBOVU PAKISTAN.

$
0
0
DSC_1374
Mmiliki wa Mchele uliodhibitishwa kuwa mbovu na kutofaa kwa chakula na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar Bw. Mohamed Mauly akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la kurejeshwa kwao Mchele huo wenye wingi wa tani 26 sawa na kg 2,600 katika Godauni lake Mwanakwerekwe Zanzibar. DSC_1378
Mchele mbovu uliodhibitishwa na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar ukiwa kweye Godauni Mwanakwerekwe ukisubiri kurejeshwa Pakistan ulipo nunuliwa.
 

Mmiliki wa Mchele huo Bw. Mohamed Mauly akionyesha Mchele mbovu ulithibitishwa na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar na mwenyewe kuridhika na majibu hayo, nakusema sio aliouagizia hivyo ameshapeleka madai na kutakiwa aurudishe ili kupewa haki zake na Kampuni ya Bilal Rice Mills ya Pakistan. Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar.

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI NEW YEAR OFFERS!

$
0
0
SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,250 
40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,750 
SALOON CARS TO DAR NOW £700
SALOON CARS TO MOMBASA £680
4 X 4 CARS TO DAR  NOW £780
4X4 CARS TO MOMBASA NOW £760
AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
KAMA UNA MZIGO WA MSAADA TUNASAFIRISHA BURE
FREE STORAGE IN OUR OFFICE
FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
£50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
COLLECTION POINT IS
ILALA MTAA WA BUKOBA
CONTACT; TORNADO+255713607116
SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
WE WILL GET IT INSPECTED AND DELIVERED TO PORT FOR YOU!
BEI ZETU HAZINA WASHINDANI NDIO MAANA TUMEZIANIKA WATU WAJUE
THE DIFFERENCE IS CLEAR!
WE ARE NOW OPEN ON SATURDAYS

Tanzania at the 20th African Mining Indaba held at the Cape Town International Convention Centre

$
0
0
 Hon. Stephen J. Masele ( MP ), Deputy Minister for Energy and Minerals of the United Republic of Tanzania at the 20th African Mining Indaba held at the Cape Town International Convention Centre ( CTICC )
 The Deputy Minister has had different bilateral meetings with the mining companies as well as counterparts from different countries such as the Republic of the Sudan , the Republic of Kenya etc. He also did a presentation that  highlighted among others, conducive investment environment in the mineral sector, geological infrastructure, mineral licencing, future of the mineral sector etc.


 The Deputy Minister also met with the leaders of the Tanzanian Association in Cape Town (TAC) and discussed issues pertaining to life and potential contribution of the Tanzanians living in the diaspora. In this context, the Deputy Minister put an emphasis on the importance of observing laws of the land in the pursuit of good life in the dispora.


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Karubandika by Kasaloo Kyanga & Orch.Maquis Original

MAMBO 6 YANAYOMFANYA MTU AWE KIONGOZI BORA NA SIO BORA KIONGOZI

$
0
0
Tukiacha mbali picha ambayo mara nyingi au kwa miaka mingi imekuwa ikijengwa  vichwani mwa wengi wanapoona na kudhani kwamba fulani ni kiongozi bora [pengine kwa muonekano tu], au kwa sababu anashuka kutoka kwenye gari kwa mbwembwe, tabasamu baada ya kufunguliwa mlango na mkanda na kisha kupokelewa briefcase yake, yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora na sio bora kiongozi. Na kadri siku zinavyokwenda, taswira ya kiongozi kwa muonekano tu inazidi kupotea. Vitendo,maadili,mafanikio, uvumbuzi na maendeleo vinachukua mstari wa mbele.

Tofauti na miaka ile ambayo picha ya kiongozi bora ilikuwa kama hiyo hapo juu, siku hizi viongozi bora wapo na wanajitokeza katika hali tofauti tofauti kabisa. Anaweza kuwa asiyevaa suti kama Dalai Lama na akawa kiongozi bora. Au asiyevaa suti bali t-shirt na jeans tu kama alivyokuwa Steve Jobs wa Apple au Mark Zuckerberg boss wa Facebook. Mifano ya viongozi hawa ipo mingi.

Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinasema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti, briefcase, tabasamu[ hususani lile la uongo] bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.


WENYE BUCHA MOSHI WAGOMA KUUZA NYAMA KWA SIKU MBILI

$
0
0

Baadhi ya mabucha yaliyofungwa.
Wauzaji wa Nyama wakiwa nje ya mabucha yao baada ya kugoma kuuza nyama.
Baadhi ya mabucha yaliyofungwa.
Na Dixon Busagaga wa 
Globu ya Jamii, Moshi

WAKAZI wa mji Manispaa ya Moshi, wametaabika kwa siku mbili sasa wakiwa hawapati kitoweo cha Nyama baada ya halmashauri ya manispaa hiyo na mamlaka ya udhibiti wa Chakula na dawa TFDA kuyafunga maduka ya nyama ambayo hayakidhi vigezo vya afya.

Katika hali inayoonesha kuwapo kwa mgomo wa wauza nyama,pamoja na manispaa kuyafunga maduka sita tu ambayo yalibainika kutokidhi vigezo, katika manispaa hiyo yenye maduka zaidi ya 50, lakini hakuna hata moja linaloendelea na biashara hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake, Damian Temba alisema pamoja na kwamba manispaa ilitoa muda wa wafanyabiashara kuyafanyia marekebisho maduka yao lakini bado masharti waliyoweka hayatekelezeki.

"Tulipewa notisi yenye masharti 16, ikiwamo bucha kuwa na kiyoyozi, msumeno maalum wa kukata nyama, kuwapo kwa vioo na leseni ya TFDA.......hii misumeno haipatikani na iliyopo haina ubora na bei yake ni Zaidi ya Mil 1 ambayo ni vigumu kuinunua"alisema.

Alisema maduka mengi yamefanyiwa ukarabati uliohitajika lakini baadhi yao walilipa fedha ili kupata kibali cha TFDA lakini bado hawajaletewa jambo ambalo limeendelea kukwamisha jitihada zao za kutimiza masharti yaliyowekwa.

Hata hivyo wafanyabiashara hao walisema wakati manispaa ikifunga maduka yao, hali ni tofauti katika machinjio yanayomilikiwa na manispaa hiyo ambayo walidai ni machafu na hayakidhi vigezo vilivyowekwa na TFDA.

"Manispaa haitutendei haki hata kidogo, machinjio ni machafu mno, yanahatarisha afya za walaji,lakini hawaangalii hilo,wanatubana na maduka yetu ambayo tayari yamekamilika na kilichokosekana ni misumeno ambayo hata hivyo nayo haina ubora"alisema.

Alisema waliagizwa kwenda kujifunza maduka ya mfano mkoani Dodoma lakini pamoja na kuyaona hayatofautiani na waliyonayo jambo linalowatia shaka kama haki inatendeka au la.

Kwa mujibu wa notisi ya manispaa hiyo ya Novemba 20, 2013 yenye kumbukumbu namba MMC HO/7012/Vol III/132 na kusainiwa na afisa afya wa manispaa hiyo V.M Makundi lilitaja wahudumu kuvaa sare,kupimwa afya kila miezi 6 na yapigwe rangi nyeupe ndani.

Masharti mengine ni pamoja na chumba cha duka kiwe na ukubwa wa Mita tatu kwa mita mbili, sinki la maji, kutokutumia magogo kucharanga nyama na kutoruhusu wateja kugusa nyama wakati wa ununuzi.

Hata hivyo mwendesha mashtaka katika idara ya afya ya manispaa hiyo, Godfrey Meela alisema tayari manispaa hiyo imewaburuza mahakamani wafanyabiashara wanne ambao wameshindwa kutekeleza maagizo ya TFDA na manispaa hiyo kwa kutokidhi vigezo vya afya.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara katika soko kuu mjini Moshi wanaoza vyakula, Halina Abdala na Zuleha Kasimu walisema wamekosa wateja kutokana kukosa kitoweo hicho.

UANDIKISHAJI KWA WAKIMBIAJI WA MBIZO ZA KILIMANJARO MARATHONI UNAENDELEA KEYS HOTEL, MOSHI

$
0
0
Uandikishaji kwa wakimbiaji wa mbio za Km 5 Fun Run ukiendelea katika hoteli ya Keys mjini Moshi. Mbio hizi hufanyika kila mwaka katika Jumapili ya mwisho ya mwezi Juni
Katika banda la Vodacom shughuli za uandikishaji kwa wakimbiaji wa mbio za Km 5 Fun Run zikienndelea.
Kampuni ya GAPCO pia wapo kuhakikisha mbio za walemavu zinafana mwaka huu

Kwa wale wanaokimbia wakitizama muda hawa jamaa pia wamepiga kambi Keys Hotel.

Upande wa wadhamini wakuu mbio hizo Kilimanjaro Premium Lager shughuli za uandikishaji ziliendelea.
Shirika linalopambana na masuala ya Ukeketaji NAFGEM pia wanahkikisha watoto wa jamii ya kimaasai wanashiriki mbio hizo.
Mazingira ya mji wa Moshi tayari yamebadilika ikiwa ni shamrashamra ya mbio hizo. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi


Shirikisho la Madini Thailand kuisaidia Tanzania kuwa kitivo cha Madini Afrika

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Bangkok, 
 Kutokana na kuwa na hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali hususani madini ya vito na usonara tofauti na nchi nyingi za Kiafrika, yakiwemo madini ya Tanzanite, Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand, limehaidi kuisaidia Tanzania kuikuza sekta hiyo, katika nyanja za kibiashara na kiuchumi ili kuifanya Tanzania kuwa, kitivo kikubwa cha madini barani Afrika, huku ikianzia na kuboresha maonesho ya kimataifa ya madini ya vito na usonara ya Arusha yanayofanyika kila mwaka. 
 Aidha, nia ya shirikikisho hilo imetokana na uwepo wa makampuni mengi ya wafanyabiashara wa Thailand kupenda madini yanayotoka Tanzania ikiwa pia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Thailand.
  Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Shirikisho la madini ya vito na usonara Thailand na kiongozi kutoka Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand. 
 “Tunataka kuisaidia Tanzania kutengeneza fursa nyingi zaidi za kibiashara katika tasnia hii. Tanzania ina kila sababu ya kufanikiwa katika hili, kuna madini mengi na bora ya kuifanya kuwa kituo kikubwa cha madini Afrika”. Amesema Tom Broke, Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini ya Vito na usonara Thailand. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, ambaye amelitembelea banda la Tanzania na kufurahishwa na aina za madini zilizowasilishwa, amehaidi kuboresha maonesho hayo ili kuziwezesha nchi zenye hazina kubwa kama Tanzania kuweza kushiriki maonesho hayo kwa kiwango kikubwa. 
 “Tanzania inashiriki katika maonesho haya kwa mara ya kwanza, tunataka kuwasaidia katika hili, ili muweze kujenga mtandao mkubwa zaidi wa kibiashara kwasababu mna kila sababu ya kufanikiwa kutokana na umuhimu wenu katika sekta hii. Sisi sote tunawahitaji ninyi.” Amesema Bibi. Sakuntanaga. 
 Hivyo, amewataka wafanyabiashara wa Kitanzania kujenga mtandao wa kibiashara na wadau wengine duniani kutokana na ubora wa madini yanayopatikana nchini. 
 Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania, (TAMIDA) Bw. Sam Mollel, amewaomba viongozi wa Shirikisho hilo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya kibiashara kati ya Tanzania na Thailand ili kuwawezesha wafanyabiashara wa madini kushiriki kwa wingi na kuleta bidhaa nyingi zaidi katika maonesho mengine nchini humo ikiwemo kufanya biashara na Thailand. 
 Kwa upande wake kamishna Msaidizi Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza kuwa, jambo hilo ni fursa kubwa kwa Tanzania na wadau wa madini nchini ambayo wanahitaji kuitumia kikamilifu kutokana na nafasi kubwa ambayo Tanzania imepewa katika maonesho hayo na utayari wa nchi ya Thailand kutaka kushirikiana na Serikali na wafanyabiashara wa madini wa Tanzania. 
 Ameongeza kuwa, maonesho ya madini ya Arusha ni fursa nyingine kwa Tanzania kutokana kuwa nchi pekee katika ukanda wa Afrika, ambayo inafanya maonesho ya vito vya madini na usonara, Afrika. 
 “Tumejidhatiti kujifunza kutoka kwao na tumefarijika kuona namna wafanyabiashara mbalimbali wanavyothamini madini yetu na maonesho yetu ya Arusha. Hiyo ni hatua ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini”. Amesema Kamishna Komba.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, akiangalia madini aina ya Tanzanite, alipotembelea banda la Tanzania. Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba,  wa tatu kulia ni Makam wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara, Thailand Bw. Tom Broke, wengine wanaoshuhudia ni wawakilishi wa Tanzania katika maonesho hayo.

 Mkurugenzi Mtendaji Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania katika maonesho ya 53 ya ‘Bangkok Gems and Jewelry Fair’’.

Wafanyabiashara wa madini kutoka nchi mbalimbali wakiangalia madini ya almasi katika banda la Tanzania. Wanaohushudia ni Bib.Teddy Goliama kutoka idara ya uthamini madini ya almas wizara ya nishati na madini na wa pili ni Bw. Gregory Kibusi mchimbaji wa madini.

introducing 'Inzaara' ya Msanii Nana Flow wa Morogoro

MDAU JOHN KITIME NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO "KUTAKAPOKUCHA"

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images