Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 370 | 371 | (Page 372) | 373 | 374 | .... | 3270 | newer

  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao alipokutana nae kwa mazungumzo kwenye Jumba la Mikutano la Kitaifa la China maarufu kama People's Great Hall mjini Beijing, China. Mhe. Membe yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014.
  Mhe. Membe na Mhe. Yuanchao wakiendelea na mazungumzo.
  Mhe. Membe akiagana na Mhe. Yuanchao mara baada ya mazungumzo yao.


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Wang Hanning, Makamu Waziri wa Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China alipokutana nae mjini Beijing wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Membe nchini China tarehe 26 Februari, 2014.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Li Jinzao, Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China kabla ya kufanya mazungumzo rasmi na Waziri huyo wakati wa ziara yake nchini China.
  Mhe. Membe (kulia) na Ujumbe wake wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na Mhe. Jinzao (kushoto) na ujumbe wake.

  0 0

   WABUNGE WAKIPITIA RASIMU YA MAPENDEKEZO YATAKAYO TUMIWA NA KIKAO CHA BUNGE LA  KUJADILI  RASIMU YA KATIBA MARA BAADA YA KUWASILISHA NA MWENYEKITI WA KAMATI ILIYO ANDAA RASIMU HIYO PROF.OSCAR MAHALU.PICHA NA DEUSDEDIT MOSHI WA GLOBU YA JAMII, DODOMA
   MJUMBE AKICHANGIA. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 02/27/14--11:49: Article 21
 • Kila ijumaa na jumamosi karibu isumba lounge (zamani Jollies club) tule oldies, old scul, chacha,charanga, soka rumba na nyingine kibao, doors open from 9pm entry 10,000/-  tu. 

  0 0


  *       Initiative to generate US$1.2 billion revenue
  *       2 million people will be lifted out of poverty
  *       10,000 small-scale growers will be commercialised

  By Our Reporter
  GROWERS associations have signed a Memorandum of Understanding (MoU)
  to strengthen farmers participation in the design and implementation
  of the Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

  The associations which have signed the MoU include; Agriculture
  Council of Tanzania (ACT), Agricultural Non-State Actors Forum
  (ANSAF), the SAGCOT Centre Ltd,   and Tanzania Horticulture
  Association (TAHA).

  The actors will jointly facilitate the engagement of civil society and
  farmers in SAGCOT initiatives.  Their concerted efforts aim to
  mobilize and monitor inclusive investments in agriculture and improve
  policy reforms that promote and encourage growth in the agriculture
  sector.

  The first phase of implementation of the agreement is funded through a
    grant provided by BEST-AC. The MoU is one of the outcomes of a
  Non-State Actor consultation session, facilitated by UNDP, where
  non-state actors called for a more structured engagement in SAGCOT.

  According to SAGCOT Centre Ltd, CEO Geoffrey Kirenga, this agreement
  symbolizes the partnership approach that is required to ensure that
  investments in the Corridor are inclusive, engage and benefit farmers.

  The MoU is considered a landmark for the farmers lobby by Mrs Janet
  Bitegeko, Executive Director of ACT. "The coalition underpins what we
  have all along advocated for; working in partnership. Through the
  Tanzania Agriculture Partnership program (TAP), ACT has long
  championed the multi-stakeholder partnership approach in agriculture.
  I can assure you that ACT is ready for action."

  Mr. Audax Rukonge, Executive Director of ANSAF stated that the MoU
  aims at providing a platform to the smallholder farmers to raise their
  voices and marks the start of deeper involvement of smallholder
  farming communities in SAGCOT. "We look forward to contribute to the
  promised outcomes from the SAGCOT initiative"

  Ms Jackie Mkindi, the CEO of TAHA, said that the most viable way to
  sustainably address the numerous challenges faced by farmers is
  through transformational partnerships. "This MoU will define our roles
  and responsibilities as partners in catalyzing actions and commitments
  to strengthen farmers' involvement in agriculture value chains as
  business partners."

  SAGCOT which was launched in 2010 is a multi-stakeholder partnership
  that seeks to transform the agriculture sector of Tanzania by building
  inclusive agribusinesses in the country's southern region.

  Its innovative model brings together various partners - including food
  companies, processors, service providers, and farmers' associations -
  to develop viable agricultural value chains and enhance the
  profitability of farmers, especially those which are small-scale.

  SAGCOT's ambitious goals include bringing 350,000 hectares into
  profitable production; transitioning 10,000 small-scale farmers into
  commercial farming; creating 420,000 new employment opportunities;
  lifting 2 million people out of poverty; and generating $1.2 billion
  in annual farming revenue by 2030.

  0 0


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe saidi Meck Sadick.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Kwa Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama. 


  0 0
 • 02/27/14--17:30: Article 16


 • 0 0
 • 02/27/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Kipande Cha Papa cha Jamhuri Jazz Band

  0 0

  Aleyekuwa Rais wa mwanzo wa Zambia mkongwe wa siasa Dr.Kenneth Kaunda amelazwa katika Hosptali ya Lusaka Trust Hospital kuanzia Ijumaa wiki ya jana, Mzee Kaunda haijulikani ugonjwa gani uliokuwa unamsumbua lakini kwa sasa hali yake inaendelea vema mapema pia Rais wa sasa wa nchi Bw.Michael Sata na mkewe Bi.Dr.Christine Kaseba walenda kumjulia hali Mzee Kenneth Kaunda aka KK(pichani kama kawaida na kitambaa cheupe)

  0 0

  Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC
  Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII.
  Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.

  Mzee Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30 katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia mitandao ya kiJamii

  Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada
  Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine.
  Karibu sana

  NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

  0 0

  Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi sign MOU copy

  Bw.Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.

  Na Mwandishi Wetu

  KAMPUNI tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa wajasiriamali.

  Mkataba huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano kwenye sekta zote za kiuchumi.
  Mkataba huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.
  Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi shake hands after signing MOU copy
  Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.

  Mkataba huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Injinia. George Mulamula amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa ya Silicon Valley ya ujasiriamali.

  Amesema hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.
  Mr Mulamula explains the partnership to the press copy
  Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.

  Baada ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.

  Mr Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.
  Mr Carl Davis Jr, gives a talk to Tanzanian entreprenuers at DTBi copy
  Bw. Carl Davis Jr, akitoa majadiliano DTBi kwa wajasiriamali wa Tanzania juu ya jinsi ya kuwa mwekezaji mwenye mafanikio.
  Attendee contributing to the discussion copy
  Mshiriki akichangia mjadala.

  0 0

   Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
   Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
    Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.


  0 0

  Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.

  Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.

  Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.

  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.

  Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine.

  ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.
  Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia).
  Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi.


  0 0

  Mgeni rasmi, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Prof. Sospeter Muhongo akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa za AWANGO uliofanyika ndani ya hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, usiku wa jana. Waziri Muhongo aliwapongeza TOTAL kwa juhudi wanazozifanya kusaidia jamii ya Watanzania kupata chanzo cha nishati kitakachowaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Pembeni ni baadhi ya bidhaa hizo zinazotumia nishati ya jua.
  Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo (kulia), mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa zinazotumia nishati ya jua kuzalisha umeme zinazojulikana kama AWANGO, wa kwanza kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mh. Marcel Escure pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TOTAL nchini Tanzania Bw. Stephane Gay wakishuhudia tukio mojawapo katika hafla hiyo.
  Kikundi cha burudani kikionyesha umahiri wa kutoa burudani kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kuashiria uzinduzi rasmi wa AWANGO. AWANGO ni bidhaa zilizo chini ya Mradi wa ‘Total Access to Solar’ ulioanzishwa na kampuni ya TOTAL mwaka 2010 kusaidia kutatua tatizo la upungufu wa nishati kwa nchi zinazoendelea ukiwalenga watu wa kipato cha chini hasa wa vijijini na pembezoni mwa miji.
  Meneja wa Maswala ya Kisheria na Ushirika wa kampuni ya TOTAL Tanzania Bi. Marsha Msuya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa bidhaa za AWANGO zilizo chini ya mradi wa TOTAL unaojulikana kama ‘Total Access to Solar’ (TATS) wenye lengo la kutatua tatizo la ukosefu wa umeme nchini Tanzania kwa jamii ya watu wa kipato cha chini. Bi. Marsha alisema kuwa bidhaa hizo zitafika katika mikoa yote nchi nzima.
  wafanyakazi wa TOTAL kwenye picha ya pamoja

  0 0
 • 02/28/14--00:00: Article 8


 • 0 0

   The 2014 Martin Luther King Drum Major for Justice Award will be given to the Executive Director of Equality for Growth (EfG), Mrs. Jane Magigita Milyango, in recognition of her tireless efforts advocating for women’s rights. 
  According to a media advisory released today, the United States Chargé d’Affaires, a.i. Virginia Blaser will present the award to Mrs  Milyango on Tuesday, March 4, 2014 at the U.S. Embassy  at Msasani, along Old Bagamoyo  Road in Dar es Salaam.


  Officials  from the Government of the United Republic of Tanzania, Former MLK Drum Major for Justice Award recipients and their families as well as members of the Press have been invited.


  The U.S. Embassy Dar es Salaam annually presents the Dr. Martin Luther King, Jr. Drum Major for Justice Award in commemoration of the life and achievements of Dr. King, and to honor a Tanzanian whose life embodies the life and legacy of Dr. King. 
  Other Dr. Martin Luther King Jr. Drum Major for Justice award recipients have included:  Hon Joseph Sinde Warioba – 1999, Mwalimu Julius Nyerere (posthumously) – 2000, Hon. Francis Nyalali – 2002, Prof. Geoffrey R.V. Mmari – 2003, Mama Justa Mwaituka – 2004, Ambassador Gertrude Mongella - 2005, Dr. Salim A. Salim – 2006, Mr. Rashid M. Kawawa – 2007, Mr. Reginald Mengi – 2008, The People of the Albinism Community of Tanzania – 2009, Dr. Marina Alois Njelekela – 2010, the Zanzibar's Committee of Six - 2011, Retired Chief Justice Augustino Ramadhani – 2012 and Dr. Esther Daniel Mwaikambo - 2013. 
  In a sermon on February 4, 1968, Dr. King said, “Yes, if you want to say that I was a drum major, say that I was a drum major for justice, and say that I was a drum major for peace.  I was a drum major for righteousness.  And all of the other shallow things will not matter.” 
  Dr. King was ordained in 1948 at the age of 19 and received his PhD in Systematic Theology from Boston University in 1955.  Upon completion of his studies at Boston University, he accepted the call from the Dexter Avenue Baptist Church in Montgomery, Alabama, where he served as pastor from September 1954 through November 1959.  He resigned to move to Atlanta, Georgia to direct the activities of the Southern Christian Leadership Conference and serve as co-pastor with his father at Ebenezer Baptist Church.

  0 0

  Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyafikia malengo ya Milenia ya kuhakikisha utoaji wa elimu ya msingi kwa watoto wote ifikapo mwaka 2015 ambapo kwa sasa, uandikishaji wa watoto wote katika elimu ya msingi umefikia asilimia 96.2. 
   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa wakati akifungua warsha ya uwasilishaji wa ripoti ya upimaji wa kitaifa wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu maarufu KKK kwa darasa la pili uliofanyika mwezi Oktoba 2013. 
   Hata hivyo Waziri Dkt Kawambwa amesema matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la UWEZO mwaka 2010 yanaonesha kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi katika madarasa ya chini hawazimudu stadi za Kuandika, Kusoma na Kuhesabu kwa kiwango kinachotakiwa. 
   "Ni hakika kwamba, ufundishaji wa stadi za Kuandika, Kuhesabu na Kusoma unatakiwa ufanyike kwa makini hata hivyo upo ushahidi kwamba ufundishaji huo haufanyiki kama ilivyotarajiwa."Alisema Dkt Kawambwa 
   Amesema hali hiyo ya ufundishaji hafifu inajidhihirisha zaidi kwa matokeo ya ufaulu wa chini katika madarasa ya juu darasa la nne la saba. 
   Waziri Dkt Kawambwa amesema Ili kutatua changamoto hiyo na kuwezesha kuinua kiwango cha ubora wa elimu itolewayo,, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kiushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imeanza kutekeleza mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa, (Big Results Now ) 
   Amesema chini ya utekelezaji wa Makkati wa Matokeo Makubwa sasa katika sekta ya elimu upimaji wa kitaifa wa stadi za KKK na mafunzo kazini kwa walimu wa darasa la I & II kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi hizo ni miongoni mwa mikakati 9 iliyoibuliwa. 
   Aidha Waziri huyo wa Elimu nchini ameishukuru serikali ya Marekani ambayo kupitia shirika la USAID, imewezesha kufanya upimaji wa kitaifa wa stadi za KKK ulioongozwa na taasisi ya "Research Triangle Institute"(RTI). 
   "Ni matarajio yangu kwamba matokeo ya upimaji huu uliofanyika kwa kutumia Zana za "Early Grade Reading Assessment (EGRA)", the "Early Grade Mathematics Assessment (EGMA)" na "Snapshot of School Management Effectiveness (SSME)" utaisaidia serikali kupata taarifa kuhusu hali halisi ya kumudu stadi za KKK kwa wanafunzi wa Darasa la Pili."Alisema 
   "Matokeo ya utafiti huu pia yatasaidia katika kulinganisha na matokeo ya upimaji wa darasa la pili unaotarajiwa kufanyika mwaka 2014 na 2015 pamoja na kusaidia serikali katika kuandaa programmu mbalimbali ili kufikia malengo tarajiwa ya kuinua ubora wa elimu na ufaulu"Aliongeza . Ushiriki wa Jamii na Wazazi katika masuala ya elimu ni muhimu ili kuinua upatikanaji wa elimu bora, upatikanaji wa rasilimali na kuongeza uwajibikaji. 
   Tanzania ina rekodi nzuri ya ushirikishaji wa jamii kupitia kamati za shule na taasisi za kiraia na hivyo Waziri Dkt Kawambwa ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau mbalimbali wa elimu kuwasaidia watoto kwa kuwawezesha kupata na kutumia stadi mbalimbali za lugha kupitia usomaji wa vitabu na kuzungumza nao wakiwa nyumbani ili hatimaye kuwawezesha kufanya vizuri wakiwa shule.
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa akimpongeza  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la USAID Tanzania Bi, Sharon Croner wakati wa uzinduzi wa Warsha ya uwasilishaji wa ripoti ya  upimaji  wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana na shirika la maendeleo la Marekani la  USAID  Tanzania ,jana   katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Tamisemi Kassim Majaliwa .Warsha hiyo iliwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu hapa nchini.

   Baadhi ya wadau wa Elimu kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini wakifuatilia uzinduzi wa Warsha ya uwasilishaji wa ripoti ya Upimaji wa Kitaifa wa Stadi za Kusoma,Kuandika na Kuhesabu kwa Darasa la Pili  uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Utafiti huo ulifanywa na Shirika la Misaada la Marekani la USAID kwa ufadhili wa Marekani.
   01.  Mkurugenzi wa Idara ya Elimu wa Shirika la USAID  Tanzania Bw, David Bruns  akielezea jijini Dar es salaam matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lake kuhusu upimaji  wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika nchini Oktoba mwaka jana kwa ufadhili wa serikali ya Marekani na taarifa yake kuzinduliwa rasmi jijini Dra es salaam.

   Mkurugenzi wa  Shirikala la USAID Tanzania Sharon Croner, akiongelea jijini Dar es salaam matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lake wakati wa uzinduzi wa Warsha ya uwasilishaji waripoti ya  upimaji  wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana. Taarifa ya utafiti huo ilizinduliwa jana jijini Dar es salaam.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa  akiongea wakati wa uzinduzi wa Warsha ya uwasilishaji waripoti ya  upimaji wa wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana na serikali ya Marekani kupitia shirika lake la Maendeleo la USAID  Tanzania ,jana   katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
  0 0

      Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akifungua mafunzo hayo rasmi jana, katika maneno yake ya ufunguzi Kattanga amewaasa Makarani kutokufanya kazi kwa mazoea bali kufanya kulingana na misingi ya maadili ya Mahakama iliyopo lengo likiwa ni kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi, (kushoto) ni Msajili wa Mahakama ya Ardhi, Mhe. Lameck Mlacha, kulia ni Naibu Mkurugenzi Mafunzo, Bi. Rehema Vyas.

   Mmoja wa Makarani kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipendekeza jambo mbele ya Mtendaji Mkuu kuhusiana na maboresho ya huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

  Baadhi ya Makarani wa Mahakama wakiwa katika Mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Learnit kilichopo jijini Dar es Salaam.

   1.      Mhe. Hussein Kattanga akiwa darasani kushuhudia baadhi ya wanafunzi hao wakipewa somo kuhusiana na mfumo wa kuingiza taarifa za mashauri/kesi kwa kutumia kompyuta, aliye pembeni na Mtendaji huyo ni Bw. Machumu Essaba, Mkuu wa Kitengo cha ICT, Mahakama ya Tanzania, na wengine waliosimama kwa nyuma ni baadhi wa wakufunzi wa Mafunzo hayo ambao pia ni Watumishi wa Mahakama, Kitengo cha ICT. 
   Mtendaji akiendelea kushudia wanafunzi wakiwa katika mafunzo hayo. Lengo la Mahakama ni kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki nchini inapatikana kwa urahisi kwa kutumia njia za teknolojia hususani katika kuingiza taarifa muhimu za kesi kwa kutumia kompyuta. Mafunzo hayo ambayo yatachukua jumla ya siku 21 yanajumuisha jumla ya Makarani 30 kwa kila wiki, ambapo kundi la kwanza litamaliza mafunzo yake siku ya Jumapili 02.03.2014.         
    Mgeni rasmi aliyefungua mafunzo hayo ya Makarani, Mhe. Hussein A. Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (katikati), Mhe. Lameck Mlacha, Msajili wa Mahakama ya Ardhi (kushoto), pamoja na Bi. Rehema Vyas, Naibu Mkurugunzi Mafunzo, Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi (Makarani) wanaohudhuria katika mafunzo hayo na baadhi ya Wakufunzi wa mafunzo hayo. 

  Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania.

older | 1 | .... | 370 | 371 | (Page 372) | 373 | 374 | .... | 3270 | newer