Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 372 | 373 | (Page 374) | 375 | 376 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 02/28/14--23:25: BAJAJ IKIWA IMEKULA NYOMI
 • Kamera ya Globu ya Jamii,imeinasa Bajaj hii maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam ikiwa imesheheni abiria kupiga uwezo wake,huku suka wa Bajaj hiyo pia akiwa amekaa kiti kimoja na abiria huku akiwa hana noma wala nini.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo jana.

   Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
   Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.
  Mgombea  wa CHADEMA akipokelwa Lumuli.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID,Bi. Rebecca Savoie katikati,akitoa paketi ya unga wa uji uliochanganywa na virutubishi kwa mmoja wa wakazi wa kata ya Mpunguzi aliyehudhuria uhamasishaji wa lishe kwenye kata hiyo.
  Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,na maofisa wenzake kutoka mradi huo wakifurahi na wananchi wa Mpunguzi kwa kupiga makofi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe kwenye kata hiyo leo.
  Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Bwana Lephy Gembe akiwasili katika kata ya Mpunguzi katika shughuli za uhamasishaji wa kutumia vyakula vyenye virutubushi ambao unafanywa na USAID kupitia mradi wake wa Tuboreshe Chakula.
  Mkurugenzi Mkaazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,akitoa hutuba kwa lugha ya Kiswahili katika sherehe za uhamasishaji juu ya faida na umuhimu wa Virutubishi kwa watoto,umri miezi 6-miaka 5.Sherehe hizo zilizofanyika kata ya mpunguzi wilaya ya Dodoma mjini..Kushoto ni Bwana Lephy Gembe aliyekuwa mgeni rasmi,na kulia ni Dr Generose mtaalamu wa lishe.
  Mmoja wa wahamasishaji wa umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto wenye umri wenye miezi 6 mpaka miaka 5,Tom David,akiwagawia uji uliopikwa ukaongezwa virutubishi,wamama wa kata ya mpunguzi,wenye watoto umri wa miezi 6-miaka 5.Ikiwa sehemu ya uhamasishaji na uelimishaji kwa vitendo.Kampeni hizi zinadhaminiwa na mradi wa USAID Tuboreshe chakula.

  0 0

   MBUNGE WA MTERA,LIVINGSTONE  LUSINDE NA MBUNGE WA MOSHI MJINI MHE PHILEMON NDESAMBURO AMBAO PIA NI WABUNGE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA WAKIAGANA MARA BAADA YA KUAHIRISHWA KWA SEMINA YA KUANDAA KANUNI ZITAKAZO TUMIWA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA MJINI DODOMA.
  MWENYEKITI WA CHAMA CHA UDP MHE. JOHN MOMOSE CHEYO NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA NCCR;MAGEUZI MHE. JAMES MBATIA AMBAO PIA NI WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA WAKIJADILIANA WAKATI WAKITOKA KATIKA SEMINA YA KUJADILI RASIMU YA KANUNI ZA KUONGOZA BUNGE HILO. 
   
  MHE.OLE SENDEKA AKICHANGIA MSWADA WA KANUNI ZITAKAZO TUMIKA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA JANA JIONI. 
  MHE.JAMES MAPALALA AKIWELEKEZA JAMBO MJUMBE MWENZAKE KWA KIDOLE WAKATI WA SEMINA YA  KUJADILI RASIMU YA KANUNI ZITAKAZO TUMIKA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA. PICHA NA DEUSDEDIT MOSHI WA GLOBU YA JAMII, KANDA YA KATI

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Bwana Lephy Gembe akiwasili  katika kata ya Mpunguzi katika shughuli za uhamasishaji wa  kutumia vyakula vyenye virutubushi ambao unafanywa na USAID kupitia mradi wake wa Tuboreshe Chakula.
   Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,akitoa paketi ya unga wa uji uliochanganywa na virutubishi kwa mmoja wa wakazi wa kata ya Mpunguzi aliyehudhuria uhamasishaji wa lishe kwenye kata hiyo.


  Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,na maofisa wenzake kutoka mradi huo wakifurahi  na wananchi wa Mpunguzi kwa kupiga makofi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe kwenye kata hiyo leo.

  0 0
 • 03/01/14--01:00: ukishangaa ya mussa....
 • Awali mabunda haya yalivyokutwa katika jumba la Zungu la Unga  lililovamiwa na vikosi maalumu huko Mexico yalikadiriwa kuwa ni dola bilioni 18 za Kimarekani. Baada ya kuhesabiwa ikakutwa ni zaidi ya dola bilioni  22. Hii inadhihirisha jinsi biashara ya 'Sembe' ilivyo na changamoto kubwa kwani kwa kiasi hicho mwenyewe anaweza kununua chochote ama mtu yeyote na kufanya atakalo. Lakini pamoja na hayo vikosi vya kupiga vita biashara hii haramu vinaendelea na jitihada zao kupambana nao usiku na mchana, kwa mafanikio kama haya...  0 0

  Hili ni eneo la Ubungo ambalo limekuwa na wimbi kubwa la wafanya bishara wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila aina pembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

  Licha ya usumbufu na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na kufanya wizi.

  Wakizungumza watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wa kutowazuia nao wameamua kuendelea kuleta kero

  "Eneo hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la kuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayo mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni aibu" 

  Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.  
   Hii ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge? Je Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara hizi?

   Hawa nao wanauza Viatu pande hizi kwa bei nafuu...
   Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya sio sahihi.


  0 0

   Katika hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia Mashabini wenzao wa Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.lakini kwa hali ilivyo hivi sasa Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.

   Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
   Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.  
   Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
   Askari Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa Mashabiki wa Simba. 
   Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.


  0 0

   Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wananchi/Wanakijiji wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mapema leo jioni,alipokwenda kuzungumza nao na kuomba ridhaa yao ya kuwaongoza kama Mbunge.
   Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akizungumza na Wananchi/Wanakijiji wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mapema leo jioni,akiomba kura na ridhaa yao ya kuwaongoza kama Mbunge. Ndugu Mgimwa alisema kuwa Wananchi Wamuamini kwani anafahamu changamoto zilizopo na majibu ya kuzitatua anayo "Nimefanya utafiti  wa kutosha hivyo najua changamoto zinazotukabili,nipeni nafasi ili niweze kuzitatua kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010" alisema Mgimwa.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa,Mh.Gervas Ndaki akiwa amepiga magoti ikiashiria kutoa heshima kwa wananchi kwa ajili ya kuwaomba kura kwa ajili ya Mgombea wa CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika kijiji cha Ilala Simba kata ya Nzihi mkoani humo.
   Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Inzihi,Iringa Vijijini,wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mapema leo jioni.
   Wanachama wa chama cha CCM na wananchi wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na CCM mapema leo jioni,ambapo mgombea wa chama hicho,Godfrey Mgimwa alifika na kujinadi kuomba kura na ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.
   Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akipokelewa kwa shangwe mapema leo jioni katika kijiji cha Magubike,kabla ya kuzungumza nao kwenye mkutano wake wa hadhara,katika safari nzima ya kuomba kura na ridhaa ya kuwaongoza kwa nafasi ya Ubunge.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mapema leo jioni katika kijiji cha Magubike,ikiwa ni sehemu ya kumnadi mgombea wa chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa ambaye anagombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kalenga.

  0 0

   Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wasanii Februari 28,2014 katika ukumbi vijana kinondoni jijini Dar es Salaam, kuhusu viongozi mbalimbali wa Sanaa hapa nchini kwenda mkoani Dodoma Bungeni kupeleka ujumbe wa matakwa ya wasanii kuingizwa katiba Katiba mpya. Kutoka kulia ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili, Addo November, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (Tamunet), John Kitime.
   Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza akibonyeza kitufe kuzindua rasmi CD yenye wimbo wa kuhamasisha wabunge la katiba kuweka kipengele cha kulinda haki bunifu za wasanii nchini wimbo huo umetungwa na wasanii mbalimbali.uzinduzi huo lifanyika Februari 28,2014 katika ukumbi vijana kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Wasanii mbalimbali pamoja na waandishi wa habari wakishuudia uzinduzi huo.PICHA NA PHILEMON SOLOMON

  0 0

   Lately, I have followed the diaspora dialog taking place among members of the Tanzania diaspora living in the US.  I have read with great curiosity all that is being brought to light regarding our participation in the effort to support and uplift our homeland’s economy, thanks to those who have gone the extra mile to obtain data that proves the validity of the initiative.  
  I would also like to address alongside this noble subject, the passionately celebrated issue of Direct Foreign Investment in Tanzania both of which subjects are for the good intentions of supporting the country’s economy.  In either case, I agree albeit with some reservations:
  Before discussing the participation of diaspora in a homeland economy, let me first begin with the definition of the term diaspora which in recent years seems to magnetically draw interests of African countries to connect with compatriots leaving abroad and enlist them in the effort to help develop national economies.  
  The term diaspora originates with the Jewish communities dating as far back as 587 BC that had been forced out of their homeland in the Middle East by warring invaders, the Babylonians who conquered their land. But because of the strong love they had for their motherland, they kept their traditions and religion intact and always tried to find ways to connect with their loved ones at home and especially the religious community.

  0 0

  Ujenzi wa mabanda mbalimbali ndani ya uwanja wa Ushirika ukiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0


  0 0

  1069410_488216681262565_60269170_n
  Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  ----------------------------------
  Nimerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara, wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.
  Ziara hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi (people Centred Integration).
  Kama nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni kubwa.
  Hata hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
  Ni imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa.
  Lengo kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au kutokufikiwa kabisa.

  0 0

  DSC_0549

  Embassy of the Federal Republic of Germany  Charge d’Affaires in Tanzania, Mr Hans Koeppel speaks to Hyatt Regency the Kilimanjaro Hotel, General Manager, Trevor Saldanha during the cocktail party organized by the Germany Embassy in Dar es salaam to honour  tour operators who are going to Berlin to attend International Travel show
  --------------------------------------
  By Damas Makangale and Caroline Alexandra, MOblog Tanzania
  Despite news of wildlife poaching in Tanzania the current statistics show that the country is generating nearly 4 billion USD in the tourism sector; equal to 13% of the GDP MOblog can report.
  Speaking to invited dignitaries at the cocktail party organized by the Embassy of the Federal Republic of Germany in Dar es Salaam, Chargé d’affaires Mr. Hans Koeppel said that after gold, tourism is the largest source of foreign exchange bringing 1.7 billion USD.
  He said that for nearly 50 years the ITB has been the driving force in the worldwide travel industry with more than 170,000 visitors. Among these 113,000 trade visitors and 11,000 represented companies from 180 countries.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia)akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya  Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo ,(wa pili kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,akifuatiwa na Waziri ayeshuhulikia Muungano Samia Suluhu Hassan
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia)akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia)akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo
   Baadhi ya wananchi na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wakiwa katika sherehe za Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo,zilizozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein
  Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi walijumuika na wananchi katika Uzinduzi wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo,zilizozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0  Ladies and Gentlemen,Exhibitors,

  It's an honour for me to inform you about the 1st African Tourism tradefair in Germany "Soul and Spirit of Africa " with focused on AFRICA ONLY! This tradefair is  initiated and organized by AfrikAktiv org. in cooperation with chamber of commerce and Industry , International African Festival Tübingen and supported by  African Ambassadors in Germany, Lord major and city of Tübingen / Reutlingen
  1st African Tourism Exhibition tradefair  "Soul and Spirit of Africa " will take place from Thursday17th July - Sunday 20th July 2014 at the African Village (Festplatz –Tubingen) near Stuttgart -South Germany (located in Baden-Württemberg and occupied by Swabian locals – Germany´s treasure of SME enterprizes, technocrats, Inventors, Global players in Automobile.. and Business Tycoons)
  Please, be informed- Exhibitors dealing in Tourism goods and services to register and participate, so that together we can establish a stable plattform for Tradefair Exhibition with focus only on Africa in Germany. As experts in Intern Business Adm- Marketing, Founder & CEO -Intern. African Festival Tübingen, the biggest and fastest growing in south Germany, there´s no doubt that The 1st AFRICAN TOURISM EXHIBITION will attract thousands of professional and public visitors this year.
  Join me,  let us make African Tourism accessible for global travelers – this is a golden opportunity and sustainable development for our continent and it´s people. Apart from Exhibitors, I look forward to partner with African trade & investment chambers, Trade fair organizations in and out of Africa.
  Any country that wishes to gain more exposure, attract more visibility, to be seen as FOCUS COUNTRY 2014,  PARTNER, SPONSOR and SUPPORTER  should contact us for more VALUABLE INFORMATION. JOIN ME, lets´s make African Tourism accessible for Eurozone & global travelers.
  SUSAN TATAH  
  (Chief Executive Officer - AFRIKAKTIV)  

       0 0

   Kikosi cha Yanga 
   Kikosi cha Al Ahly
   Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri akitafuta namna ya kumzuia katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
   Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Al Ahly ya Misri katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
   Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akizuiwa na Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri,Ramy Abdel Aziz katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
  Kipa wa timu ya Al Ahly ya Misri,Sherif Ekramy Ahmed akida moja ya hatari iliyokuwa ikielekeshwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

  0 0
 • 03/01/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • FM ACADEMIA "Dunia Kigeugeu"

older | 1 | .... | 372 | 373 | (Page 374) | 375 | 376 | .... | 3284 | newer