Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 369 | 370 | (Page 371) | 372 | 373 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Uzinduzi wa EP Album ya Msanii wa Mziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Swahili Pop/House & Techno. Itafanyika tarehe 9 March 2014 CLUB BILLICANAS. Atasindikizwa na wasanii wakali WAKAZI, NIKKI MBISHI, NIITE SONGA, GODZILLA, M-RAP, COUNTRY BOY, AZMA, OBI na wengine kibaoo. Ni siku ya Jumapili kuanzia saa nne usiku mpaka chweee kwa kiingilio cha buku 8 tuu. Pia EP Album ya JanB itapatikana pale kwa buku tano tuu.

  Venue: Club billicanas
  Date: 9th March 2014
  Price: T.sh 8,000
  Instagram@janbizo

  0 0

   Simon Osborne,the CEO of the Institute of Chartered Secretary and Administrators(ICSA) congratulating Advocate Saidi Yakubu after becoming an Associate Member of the Institute.The colourful Ceremony was held in Kampala,Uganda and was attended by graduands from Kenya,Uganda,Malawi,Zambia and Tanzania.ICSA is the membership and qualifying body for Company Secretaries and other professionals working in governance and compliance roles.
   A cross section of the 53 new qualified ICSA members.The new members hailed from 5 countries but only two were from Tanzania namely Advocate Yakubu from Parliament of Tanzania pictured far behind and Mrs Farzana Karimjee (4th from right,2nd row) who is a Manager at Deloitte.
  Advocate Saidi Yakubu chatting to the President of ICSA,David Venus on the possibility of forming an ICSA Branch in Tanzania.Becoming a Chartered Secretary is a pinnacle of achievement in Governance,Risk Management and Compliance roles.There are currently only 9 members and 8 students in Tanzania and hence the country is in dire need of ICSA members.More information on ICSA can be obtained from www.ICSA.org.uk
  Photo by  Suwedi Yunus Abdallah (Kampala).

  0 0
 • 02/26/14--14:05: FLAVANITE is BACK!

 • FLAVANITE is BACK ndani ya MzalenDo pUb, MiLLennium tOwers, JUMAMOSI  hii ni Rasmi na Kila SATURDAY chini ya dj BONILUV, dj MACKAY & dj OSCA wakiburudisha na OLDIES, NAIJA, SOUTH, AFRICAN na Zoote kaLi.


  0 0

  Na Dixon Busagaga 
  wa Globu ya Jamii, Moshi. 
   Waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon wametangaza njia mpya zitakazotumika kwa mbio za mwaka huu ikiwa ni hatua nyingine muhimu katika mafanikio ya mbio hizo ambazo sasa zinaingia mwaka wa 12 tangu kuanzishwa. 
  Njia mpya zimelenga kuboresha mwendo wa washiriki barabarani na kuwafanya wafurahie zaidi mbio hizo zilizopangwa kufanyika tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi. 
   Akitangaza njia hizo mpya jana, John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema alisema: 
  "Tumeanzisha njia mpya ili kuzuia msongamano wa watu wakati wa mbio kutokana na kuongezeka idadi ya washiriki kila mwaka. Washiriki wa mbio ndefu za marathon ya km 42, nusu marathon km 21, mbio ya walemavu na mbio ya kujifurahisha ya Vodacom 5km Fun Run sasa hawatapishana tena barabarani bali kila njia itatiririka katika muelekeo mmoja. 
   "Pia kutokana na mabadiliko haya washiriki watakuwa wameepuka kilomita 3 za mwinuko mkali kuelekea Chuo cha Mweka ambapo awali ndio palikuwa mahali pa kugeuzia washiriki wa mbio za full marathon na nusu marathon". 
  Mbio ya walemavu za Gapco ambazo zitakuwa na makundi mawili tu mwaka huu ya kiti cha magurudumu (wheelchair) na baisikeli ya mikono (handcycle) imefupishwa kutoka nusu marathon na kuwa kilomita 10 ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki na njia sasa itapita eneo tambarare na lenye kivuli. 
   Mbio ndefu za Kilimanjaro Premium Lager 42km Marathon zitaanza saa 12.30 asubuhi kutokea uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) na kuelekea barabara iendayo Dar es salaam kwa kilomita kumi na kurudia geti la ushirika halafu zitaenda kilomita 8 kuelekea hospitali ya KCMC na kukata kushoto hadi Barabara ya Lema (Lema Road). 
  Wanariadha watatelemka na Lema Road wakitelemka kupitia shule ya ISM halafu watamalizia na kipande tambarare cha Barabara ya Kilimanjaro na kipande cha mita chache za barabara ya Sokoine kuelekea uwanjani. 
   Mbio za Nusu Marathon zitaanza saa moja kamili asubuhi kutokea MUCCoBS na kupandisha kaskazini kuelekea hospitali ya KCMC kwa kilomita 8 ambazo ni sawa na ongezeko la mwinuko wa futi 250 kutoka usawa wa bahari. 
  Halafu mbio hizo pia zitapita njia ya Lema Road na kurudi uwanjani. Addison alisema kuwa mbio za full marathon na nusu marathon zinapita kwenye maeneo mbalimbali yenye vivutio na mandhari nzuri ya mji wa Moshi na sehemu zenye mandhari ya mashamba ya kahawa na migomba jambo ambalo pia litawavutia wananchi wengi kujitokeza kuwashangilia wanariadha.
  "Njia zote zitakuwa na vituo vya maji vya kutosha ili kuwafanya wanariadha wafurahie mbio bila kushikwa na kiu muda wote wa mbio. Vilevile, njia nzima itakuwa na madaktari na wauguzi wa kutoa huduma ya kwanza pamoja na magari ya kutosha ya wagonjwa huku mamlaka husika zikidhibiti usalama wa wanariadha barabarani. Madaktari wengine na wauguzi wataukuwa uwanjani ambapo kutakuwa na zahanati ya dharula kwa ajili ya huduma ya kwanza na kuchua misuli", alisema.
   Mbio ya walemavu ya Gapco Disabled 10km Marathon itaanzia uwanja wa MUCCoBS na kufata barabara ya Kilimanjaro halafu mpaka Lema Road na kugeuza. 
   Addison alisema mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanzia kwenye mzunguko wa YMCA upande wa barabara ya Arusha na zitaenda hadi kwenye mnara wa saa halafu kupita Boma Road kuelekea mzunguko (roundabout) wa barabara ya Arusha na mzunguko wa YMCA tena na watapita Uru Road na kuingia uwanjani kupitia geti la mashariki. 
   Executive Solutions ni waratibu wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2014 wakishirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, and KK Security among others, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.
   Ramani ya njia itakayotumika kwa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Vodacom fun run.
   Mkurugenzi wa mbio za Kilimanjaro marathoni 2014, John Bayo akizungumzia njia mpya ambazo wakimbiaji watazitumia mwaka huu.
   Mabango mbalimbali ya wadhamini wa mbio za Kimatafa za Kilimanjaro marathoni tayari yameanza kuupamba mji wa Moshi.
  Ramani ya njia itakayotumika kwa wakimbiaji wa mbio za Full marathon,half marathoni pamoja na mbio za walemavu.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini.
   Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM.
   Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
  Sebastian Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu  Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini tarehe 26 Februari 2014.

  0 0
 • 02/26/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • DDC Mlimani Park wanakuambia 'Bubu'

  0 0
 • 02/26/14--19:53: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU DR. CLEOPHAS KENTE RUTABINGWA 
  KUZALIWA 18/1/ 1952  –  KIFO  17/1/2014

  Leo tarehe 27/02/2014 zimetimia siku Arobaini (40) tangu Mwenyezi Mungu akuite nyumbani, tarehe 17/1/2014.

  Ilikuwa siku ya majonzi makuu katika familia yetu kifo kilitokea katika Hospitali ya Mbweni Dar es Salaam, ulipoumwa na tumbo.

  Unakumbukwa sana na familia yako, Mama yako mzazi Magreth Kente , Mke wako Praxeda Rutabingwa, watoto wako Andrew, Antidius, na Magreth, ndugu jamaa, majirani, marafiki, wanachama wenzako MAJIRANI SOCIAL CLUB, UJIRANI MWEMA TANGIBOVU- MBEZI BEACH,  JUMUIYA YA KRISTO MFALME, KIGANGO CHA MT. THOMAS MORE, PAROKIA YA MT. GASPAR DEL BUFALO MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM, CHUO CHA MT. AUGUSTINE, CHUO CHA MZUMBE,  na wengine wote, wanakukumbuka kila mmoja kwa namna ya pekee.

  Misa ya kumuombea Marehemu itafanyika tarehe 1/3/2014 siku ya Jumamosi asubuhi saa 12.45 katika Kigango cha Mt. Thomas More Mbezi Beach.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, kwa watakatifu wake. Bwana alitoa na ametwaa jina lake lihimidiwe milele.

  Amen.

  0 0

  Tunamtafuta Bibi Husna ambaye asili ya kimalaysia, aliolewa na Mtanzania Baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni Bw. Said Abdullah Belwal.

  Kwa taarifa Husna ni Muuguzi (Nurse) ila haifahamiki hospitali gani na mji gani.

  Mume wake ni Mwanajeshi na ndoa yao ilifungwa kijeshi.  Tafadhali atapopata tangazo hili au yeyote mwenye taarifa zake awasiliane na namba hizi
  Mob: +60102987357
  Tel: +60342517603
  Kuala Lumpur, Malaysia


  0 0

  Benki ya NMB imezindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam.  Vilevile imetoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Amana.
  Hili ni tawi la ishirini kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 150 yaliyosambaa nchi nzima. 
  Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali. 
  Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili. 
  Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. 
  Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road .Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam ,Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni  Mkuu  wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa  NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
   Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay akimwelezea  Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam (kwanza kushoto , Mhe Said  Meck Sadick huduma mbali mbali zitolewazo na tawi jipya la NMB Mandela Road
   Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Said Meck Sadick akiwa katika  picha ya pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road.

   Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Meck Sadick (kwanza Kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.


  0 0


  0 0

  Maisha ni safari ya aina yake. Ndani ya safari moja, zipo nyingine nyingi. Pengine ukweli huo ndio chanzo cha ule usemi kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kilicho muhimu ni kwanza kuianza safari yenyewe[moja].

  Ninachokiongelea hapo juu kina ukweli zaidi katika maisha ya Salma Msangi ambaye leo kwa wengi ni mtangazaji wa luninga na radio mwenye tabasamu zito, wepesi wa kuelewa mazingira na mwenye kuipenda kazi yake na kuwapenda mashabiki,watazamaji wa vipindi vyake vya kwenye luninga na wasikilizaji wa vipindi vyake radioni.

  Mara ya kwanza nilimuona Salma akiwa binti mdogo tu aliposhiriki shindano la kumtafuta mrembo wa Wilaya ya Ilala[ Miss Ilala]. Ilikuwa mwaka 2003. Ukumbi ulikuwa ni Diamond Jubilee. Endapo kungekuwa na mizani ya kupima nani angefika mbali sio tu katika shindano lile bali maishani kwa ujumla, bila shaka Salma angekuwemo. Kilichomtofautisha yeye na wengine si urembo. Ni kujiamini. Bado ninakumbuka jinsi alivyojibu swali. Jibu lake halikuwa jibu sahihi kupita yote. Lakini jinsi alivyolijibu, ilitosha kumuweka katika ukurasa mwingine.

  Ndivyo safari yake ilivyoanza. Safari ile ikaanzisha safari nyingine na nyingine mpaka kufikia hapa alipo. Leo hii Salma Msangi ni mtangazaji anayefahamika na mwenye wafuasi wake lukuki ilhali akiendelea kujifunza mambo mengi zaidi na hivyo kuongeza maarifa kila kukicha.

  Hivi karibuni nilipata bahati ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Endapo uliwahi kutamani kujua amefikaje hapo alipo,fursa ndio hii. Endapo unataka kujua Salma ana mtizamo gani kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wanawake, mitandao ya kijamii, wasanii nk, fursa ndio hii. Kikubwa zaidi, Salma ana ushauri ambao naamini kila mtu anapaswa kuusoma hususani vijana.Uuze “sembe” au ufanyeje? Ungana nami….

  BC: Salma, karibu sana ndani ya BC na shukrani nyingi kwa kukubali kufanya nami mahojiano haya. Mambo yanakwendaje?

  Salma: Mambo sio mabaya tunashukuru tunasonga. Ahsante sana Jeff, Kaka hahaa.. kwetu kumoja weweee  au sio? Nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kutaka kufahamu kidogo kuhusu mimi. Mara nyingi huwa sipendi interview na nimekuwa nazikwepa kweli. Huwa naogopa maswali lakini nitajaribu.

  BC: Naam, kweli kabisa mimi na wewe njia moja.Salma Msangi ni nani? Alianzia wapi mpaka kufikia hapa alipo?

  Salma: Salma Msangi ni msichana aliyezaliwa miaka 29 iliyopita katika wilaya ya Same Mjini mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Masandare hapo hapo Same kabla ya kuhamia jijini Dar Es Salaam kuungana na mama yake mzazi kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari.

  Kabla  ya hapo Salma alilelewa na Mama yake mkubwa ambaye alikua ameolewa na Mjerumani. Hii ni baada ya mama yake mkubwa kuamua kumchukua kwasababu wakati anazaliwa mama yake alikua na umri mdogo kama wa miaka 18 hivi kwa hiyo ndugu na jamaa wakashauriana na kukubaliana kwamba kutokana na umri huo mdogo asingeweza kumpa mtoto matunzo mazuri au yanayostahili. Alikuwa bado mdogo na kwa ujumla angehitaji kuendelea zaidi na jitihada zake katika maisha.


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara katika siku ya pili ya kongamano la viongozi hao kuhusiana na rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania. Kongamano ambalo lilifanyika leo katika ukumbi wa VETA, Mtwara.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagani akitoa mada juu ya Mipango ya Matumizi ya gesi asilia Lindi na Mtwara katika siku ya pili ya semina ya siku mbli ambapo leo ndio kilele cha kongamano hilo lililowahusisha viongozi wa dini katika mikoa hiyo.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris Mtwara Padre Dkt. Aidan Msafiri akitoa mada ya Tunu na maadili katika rasilimali za gesi, mafuta na madini leo katika ukumbi wa VETA Mtwara kwa viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo alisisitiza kuwa mwanadamu amepewa jukumu la kuwa meneja wa rasilimali ikiwemo gesi. Kongamano ambalo lilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa VETA, Mtwara na kuwashikisha viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
  Baadhi ya wanakongamano wakimsikliza Padre Dkt. Aidan Msafiri katika siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya matumizi bora ya tunu za kimaadili, kiroho, akili, utashi, imani, haki na elimu adilifu ambapo mwanadamu amepewa jukumu la kuwa meneja wa rasilimali vitu ikiwemo gesi asilia, mafuta na madini.
  Makam wa Askofu wa Kanisa la Kanisa la Anglikana Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Newalaa Oscar Mnung’a (wa kwanza kushoto) akifuatilia kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara lililofanyika katika ukumbi wa VETA Mtwara. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura likiwa ndani ya Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam tayari kwa Ibada maalum ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika mchana wa leo kanisani hapo.Picha zote na Othman Michuzi.
  Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.


  0 0


  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(Centre seated) in a group picture with senior government officials and members of the Private sector organizations shortly after he launched Improving Business Environment Lab at Kunduchi Beach Hotel in Dar es Salaam this evening. Others in the picture seated from left is the Vice President Dr.Mohamed Gharib Bilal, The CEO of the Presidential Delivery Bureau Mr.Omar Issa(second left), Malaysian Cabinet Minister and Expert in Development Affairs Prof. Idris Jala(Fourth left) and extreme right is the Chairman of Tanzania Private Sector Foundation Dr. Reginald Mengi. Photo by Freddy Maro.

  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu wa Nigeria na Mwenyekiti wa Kamati ya Watu Mashuhuri ya ACP Mhe Olusegun Obasanjo akiongoza kikao cha Kamati ya Watu Mashuhuri wa ACP. Kikao kinafanyika Addis Ababa Ethiopia leo. Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Dr. Leone Reyna, Mhe. Kaliate Tavola, Prof. Sebastio Izata, Prof Ibrahima Fall, Bi. Patricia Francis, Balozi Nureldin Satti, Dr Daoussa Cheriff, Mhe. Kolone Vaai, Mhe Peter Gakunu, Balozi Teshome Toga na Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala. Balozi Kamala amehudhuria kikao hicho kuwakilisha Kamati ya Mabalozi wa ACP.
  Kamati ya Watu Mashuhuri wa Afrika, Karibiani na Pacific (EPG-ACP) ambao wanakutana leo Addis Ababa Ethiopia wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Olesugun Obasanjo Rais Mstaafu wa Nigeria. Kamati hiyo inatafakari changamoto, muundo na majukumu mapya ya ACP na mfumo mpya wa ushirikiano wa nchi za ACP, nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya na nchi za ACP na wadau wengine wa maendeleo ifikapo mwaka 2020. Mkataba wa Cotonou ulioweka mfumo wa ushirikiano wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya utakoma ifikapo mwaka 2020.

  0 0

   Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe wa Shinyanga mjini ambapo aliwasaidia kufungua SACCOS na kuwaongezea mtaji wa biashara yao.
   Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia jambo wakati wa hotuba ya Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
   Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia baada ya kuwezeshwa pesa kwenye mitaji ya biashara yao Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
  Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakipeana mikono na  Mbunge wao Ndugu Stephen Masele baada ya kuwawezesha kuwa na SACCOSS pia kuwasaidia mtaji wa zaidi ya shilingi milioni nane,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.

  0 0

  EALA has today met with Parliamentarians from the Kenya National Assembly and the Senate to push for the integration agenda.

  In the meeting, EALA Members called on their counterparts to use every available opportunity to popularize the integration process in Kenya.  With devolution now in place in Kenya, legislators are optimistic that the counties and locations can fully embrace the integration message.  

  Members were emphatic that integration was non-reversible but maintained that sensitization was key to maintain its tempo.  The Speaker of EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa remarked that East Africans were looking forward to more achievements in the integration dispensation. She remarked that the Assembly was keen to reach out to the populace.

  “As legislators, we have to continuously play our part as engines of mobilization. We shall continue to re-double our efforts by reaching out to various groups including university students, the Faith Based Community, women groups and the Diaspora”, the Speaker remarked.

  The Chairperson of the Regional Integration Committee at the Kenya National Assembly, Hon Florence Kajuju, urged the Partner States to take integration a notch higher by ensuring the full implementation of the Common Market Protocol.

  She cited the cross border legal practice which is necessary to enable the legal fraternity to practice as a priority. 

  “I acknowledge that EALA is considering the EAC Cross border legal Practice Bill, 2014 and many are waiting to take advantage of the space”, Hon Kajuju stated.

  The Chairperson told the EALA Members to re-double their efforts in civic awareness as the integration process becomes stronger.  “As we move towards political federation, we must create awareness”, she remarked.

  0 0


  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akifurahia jambo wakati akifungua mkutano wa Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB) na wadau wa manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam. Kulia ni Msajili wa Bodi ya CRB, Boniface Muhegi na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Joseph Tango.

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akibadilishana mawazo na Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB), Boniface Muhegi na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Joseph Tango, mara baada ya kufungua mkutano baina ya bodi hiyo na watendaji wa manispaa za Jiji la Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 369 | 370 | (Page 371) | 372 | 373 | .... | 3270 | newer