Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

kikombe cha chai

$
0
0
Hiki ni kikombe cha chai ambacho kwa Tanzania bara kilichomo hutwa chai ya rangi ama chai ya mkandaa. Kwa Zanzibar ni Chai kavu... Yaani ukiagiza chai ya rangi uwapo visiwani unaletewa ya maziwa. Upo hapo?

Article 5

utii wa sheria bila shuruti

Kutoka maktaba: Mzee Ruksa na kamati ya saidia taifa stars ishinde mwaka 1994 na wanahabari Ikulu

$
0
0
Mwaka 1994: Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa na wajumbe wa kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde Ikulu jijini Dar es salaam baada ya timu hiyo kunyakua ubingwa wa Chalenji. Kutoka kulia mstari wa mbele ni Ankal, Brigedia Moses Nnauye (RiP), Mwenyekiti wa FAT Alhaj Muhidin Ndolanga, Rais Mwinyi, Waziri wa Elimu na Utamaduni Profesa Philemon Sarungi, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi, Mbunge wa Dodoma Kuwayawaya S. Kuwayawaya na Kamanda Richard Mwaikenda. Toka wakati huo Taifa Stars haijashinda kombe lingine lolote... Kulikoni?

RAIS KIKWETE AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa jana, Jumamosi, Februari 22, 2014, aliongoza harambee ya kupatikana kwa zaidi ya sh milioni 600 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya matibabu kwa ajili ya Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam. 
Katika halfa hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam, Rais Kikwete pia ameahidi kuendeleza kuongoza jitihada za kupatikana kwa kiasi cha sh milioni 328 ambazo zinahitaji kukamilisha hesabu ya sh. 929, 915,000 ambazo ndizo zilikuwa lengo la halfa ya jana. Halfa hiyo pia iliwakutanisha viongozi wakuu wa awamu tatu za uongozi wa juu wa Tanzania ambako Rais wa Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Tatu za Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa walikuwa wenyeji wa halfa hiyo kwa nyadhifa zao kama walezi wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT). 
Uchangiaji katika halfa hiyo ulikuwa wa aina tatu – kuna fedha taslimu milioni 55.4 zilizochangwa moja kwa moja, kuna ahadi za uchangiaji na kuna wachangiaji walioamua kuwa watatoa fedha za kununua vifaa mbali mbali vinavyohitajika katika Wodi hiyo ambayo gharama yake inakadiriwa kufikia dola za Marekani 570,500. 
Katika halfa hiyo, Ikulu ya Rais Kikwete imetoa mchango wa kununua mashine iitwayo Infant Radiant Warmer yenye thamani ya dola za Marekani 15,300 wakati Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mama Salma Kikwete imechangia ununuzi wa mashine iitwayo Compressor Nebulizer ambayo gharama yake ni dola za Marekani 12,000. 
Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, 
DAR ES SALAAM. 23 Februari, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa UNICEF nchini kwa mchango wa dola za kimarekani 100,000 huku Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa wakishuhudia katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa NSSF Bw. Juma Kintu kwa mchango wa mfuko huo katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA BALOZI FULGENCE KAZAURA

Kansiime Anne enjoys a good beating

DTBi & Silicon Valley Entreprenuer Seminar


nyalandu BBC HARD TALK interview to be aired tonight

$
0
0
Minister for Tourism and Natural Resources Hon. Lazaro Nyalandu's BBC HARD TALK Interview to be aired today Tuesday 25th February, 2014 at 12:30 pm; 19:30 pm and 00:30 am local times through BBC World News.

GODFREY MGIMWA AANZA KUPANGUA MAKOMBORA YA CHADEMA ADAI YEYE NI RAIA MZALENDO WA TANZANIA

$
0
0
Mgimwa wa pili kulia, akifurahi pamoja na wana CCM wenzake, siku ya kwanza ya kampeni zake kuwania ubunge jimbo la Kalenga iliyofanyika katika kijiji cha Mseke
 --------------------------------
Na Francis Godwin
MGOMBEA ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa amesema hana chembechembe yoyote ya uzungu na amekishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kumtuhumu kwamba sio mtanzania..

"Kama kila mtanzania anayekwenda nje ya nchi kusoma anapoteza uraia wake, basi nchi hii itakuwa na wanasiasa na watanzania wengi wanaokosa sifa ya kuendelea kuwa raia wa Tanzania," alisema.

Akiongea kwenye mkutano wa kwanza wa kampeni za kinyang'anyiro hicho zilizofanyika katika kijiji cha Mseke, jimboni humo juzi, Mgimwa alisema "mimi ni Mhehe, mtoto wa familia ya marehemu Dk William Mgimwa, nimezaliwa Iringa, nimesoma Iringa na baadaye nikabahatika kwenda Uingereza nilikopata shahada yangu ya kwanza na ya pili."

Alisema kwa mara ya mwisho kuitumia passport yake ya Tanzania ilikuwa Desemba mwaka jana alipokuwa anakwenda Afrika Kusini kumuuguza marehemu baba yake Dk Mgimwa.

Kabla mauti hayajamkuta Januari 1, mwaka huu, Dk Mgimwa alikuwa mbunge wa jimbo hilo la Kalenga na Waziri wa Fedha.

Uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo utafanyika Machi 16, mwaka huu katika kinyang'anyiro kinachoshirikisha vyama vitatu vya siasa.

Mbali na CCM chama kingine kilichosimamisha mgombea ni Chadema ambacho mgombea wake ni Grace Tendega na Chausta kilichomsimamisha Richard Minja.

Mgimwa alisema Chadema hawana sera na katika shughuli zao za siasa za kila siku wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuzungumza habari binafsi za watu badala ya kuongelea jinsi wanavyoweza kuyakabili matatizo ya watanzania.

"Jimbo la Kalenga limepiga hatua kubwa ya kimaendeleo lakini pia lina changamoto zake; waseme kabla ya kuja Kalenga wao na mgombea wao wamechangia shughuli ipi ya maendeleo katika jimbo letu hili?" alisema.

Alisema akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kazi yake itakuwa kumalizia utekelezaji wa Ilani ya CCM kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 na ahadi mbalimbali zilizoahidiwa na marehemu baba yake.

"Kipaumbele changu cha kwanza ni elimu, cha pili kilimo, cha tatu miundombinu na mawasiliano; hizo ni baadhi ya kazi nitakazofanya ili kuwaletea watu wangu maendeleo," alisema.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu alisema katika kampeni hizo kwamba wananchi wa jimbo la Kalenga walikwishafanya uamuzi kwa kuichagua CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

"Yapo mengi tumefanya kwa miaka mitatu iliyopita, tunatakiwa kupewa fursa ya kumalizia kazi tuliyoanza. Mpeni Godfrey Mgimwa kura zenu za ndio ili amalizie ahadi za CCM za 2010 na zile za Dk Mgimwa," alisema.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu alisema wanaoituhumu Chadema wakiihusisha na ubaguzi hawakosei na ndio maana kwa ubaguzi ule ule wamemkataa mtanzania mwenzao kwamba sio raia.


"Chadema wanakuja Iringa wakisema kwamba mtoto mliyemzaa nyie wahehe sio mtanzania; hivi angekuwa mweupe si wangesema ni mjerumani?" alisema.


Alisema njia pekee ya kumaliza ubaguzi wa Chadema dhidi ya watanzania wenzao ni kwa kuinyima kura katika uchaguzi huo mdogo  na Uchaguzi Mkuu ujao.

LEO NI HEPI BESDEI YA KUZALIWA DIXON BUSAGAGA WA GLOBU YA JAMII MOSHI.

$
0
0
Leo ni Hepi Besdei ya kuzaliwa mpiganaji Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii mjini Moshi. Uongozi wa Michuzi Media Group unamtakia afya tele itayomuwezesha kuendeleza Libeneke kama afanyavyo kila kukicha huko mkoani Kilimanjaro. Vile vile anaaswa asisahau kumuweka Mungu mbele kwa kila jambo alipangalo na alifanyalo maana yeye ndiye mjuaji na mgawaji wa vyote. Hongera sana Dixon - Uongozi MMG

WAZIRI NYALANDU AWANG'OA VIGOGO IDARA YA WANYAMAPORI

$
0
0


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo ametangaza kuwang'oa viongogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao. 


Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu,  kama alivyolisoma leo:


Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo: 

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  

Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  
Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza. 
Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa. 

Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo. 

Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori. 

Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti. 

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) na kukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  

Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu. 

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. 

 Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
 Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
 Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014

zungu la unga ladakwa na kilo 5 za 'sembe' uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere dar es salaam

$
0
0
Raia wa  Ugiriki, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.
 Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini  Zurich, Uswisi. 
Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo  akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.

SALMA MSANGI: KULIKO UNAVYOMJUA NA ULIVYOWAHI KUMSIKIA [INTERVIEW]

$
0
0
Maisha ni safari ya aina yake. Ndani ya safari moja, zipo nyingine nyingi. Pengine ukweli huo ndio chanzo cha ule usemi kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kilicho muhimu ni kwanza kuianza safari yenyewe[moja].

Ninachokiongelea hapo juu kina ukweli zaidi katika maisha ya Salma Msangi ambaye leo kwa wengi ni mtangazaji wa luninga na radio mwenye tabasamu zito, wepesi wa kuelewa mazingira na mwenye kuipenda kazi yake na kuwapenda mashabiki,watazamaji wa vipindi vyake vya kwenye luninga na wasikilizaji wa vipindi vyake radioni.

Mara ya kwanza nilimuona Salma akiwa binti mdogo tu aliposhiriki shindano la kumtafuta mrembo wa Wilaya ya Ilala[ Miss Ilala]. Ilikuwa mwaka 2003. Ukumbi ulikuwa ni Diamond Jubilee. Endapo kungekuwa na mizani ya kupima nani angefika mbali sio tu katika shindano lile bali maishani kwa ujumla, bila shaka Salma angekuwemo. Kilichomtofautisha yeye na wengine si urembo. Ni kujiamini. Bado ninakumbuka jinsi alivyojibu swali. Jibu lake halikuwa jibu sahihi kupita yote. Lakini jinsi alivyolijibu, ilitosha kumuweka katika ukurasa mwingine.

Ndivyo safari yake ilivyoanza. Safari ile ikaanzisha safari nyingine na nyingine mpaka kufikia hapa alipo. Leo hii Salma Msangi ni mtangazaji anayefahamika na mwenye wafuasi wake lukuki ilhali akiendelea kujifunza mambo mengi zaidi na hivyo kuongeza maarifa kila kukicha.

Hivi karibuni nilipata bahati ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Endapo uliwahi kutamani kujua amefikaje hapo alipo,fursa ndio hii. Endapo unataka kujua Salma ana mtizamo gani kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wanawake, mitandao ya kijamii, wasanii nk, fursa ndio hii. Kikubwa zaidi, Salma ana ushauri ambao naamini kila mtu anapaswa kuusoma hususani vijana.Uuze “sembe” au ufanyeje? Ungana nami….

BC: Salma, karibu sana ndani ya BC na shukrani nyingi kwa kukubali kufanya nami mahojiano haya. Mambo yanakwendaje?

Salma: Mambo sio mabaya tunashukuru tunasonga. Ahsante sana Jeff, Kaka hahaa.. kwetu kumoja weweee  au sio? Nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kutaka kufahamu kidogo kuhusu mimi. Mara nyingi huwa sipendi interview na nimekuwa nazikwepa kweli. Huwa naogopa maswali lakini nitajaribu.

BC: Naam, kweli kabisa mimi na wewe njia moja.Salma Msangi ni nani? Alianzia wapi mpaka kufikia hapa alipo?

Salma: Salma Msangi ni msichana aliyezaliwa miaka 29 iliyopita katika wilaya ya Same Mjini mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Masandare hapo hapo Same kabla ya kuhamia jijini Dar Es Salaam kuungana na mama yake mzazi kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Kabla  ya hapo Salma alilelewa na Mama yake mkubwa ambaye alikua ameolewa na Mjerumani. Hii ni baada ya mama yake mkubwa kuamua kumchukua kwasababu wakati anazaliwa mama yake alikua na umri mdogo kama wa miaka 18 hivi kwa hiyo ndugu na jamaa wakashauriana na kukubaliana kwamba kutokana na umri huo mdogo asingeweza kumpa mtoto matunzo mazuri au yanayostahili. Alikuwa bado mdogo na kwa ujumla angehitaji kuendelea zaidi na jitihada zake katika maisha.

TANZANIA YASISITIZA NYONGEZA YA POSHO KWA WALINZI WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza mwanzoni mwa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Wajumbe wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, (C-34). Katika baadhi ya mambo aliyosititiza ni pamoja na kuangaliwa upya kwa posho ya kila siku wanayolipwa walinzi wa amani ambayo ni dola 1.28, posho ambayo imedumu kwa miaka 20 bila ya kufanyiwa mabadiliko. Mkutano huo unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Aliyeketi nyuma kwa Balozi, ni Lt. Kanali Wilbert Ibuge Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu.
Baadhi ya Waambata wa Kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao Katika Umoja wa Mataifa, wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Kulinda Amani. Katika Mkutano huu wajumbe ambazo ni kutoka nchi ambazo zinachangia walinzi wa amani watajadili sera zote zinazohusu ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Mdau Yakubu becomes a Chartered Secretary!

$
0
0
Simon Osborne,the CEO of the Institute of Chartered Secretary and Administrators(ICSA) congratulating Advocate Saidi Yakubu after becoming an Associate Member of the Institute.The colourful Ceremony was held in Kampala,Uganda and was attended by graduands from Kenya,Uganda,Malawi,Zambia and Tanzania.ICSA is the membership and qualifying body for Company Secretaries and other professionals working in governance and compliance roles.
A cross section of the 53 new qualified ICSA members.The new members hailed from 5 countries but only two were from Tanzania namely Advocate Yakubu from Parliament of Tanzania pictured far behind and Mrs Farzana Karimjee (4th from right,2nd row) who is a Manager at Deloitte.
Advocate Yakubu chatting to the President of ICSA,David Venus on the possibility of forming an ICSA Branch in Tanzania.Becoming a Chartered Secretary is a pinnacle of achievement in Governance,Risk Management and Compliance roles.There are currently only 9 members and 8 students in Tanzania and hence the country is in dire need of ICSA members.More information on ICSA can be obtained from www.ICSA.org.uk Photo by Mr Suwedi Yunus Abdallah (Kampala).

SAFARI LAGER YATANGAZA RASMI BAA 10 ZILIZOINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA MKOA WA MBEYA KWA MWAKA 2014

$
0
0
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi majina ya Bar 10 yaliyofanikiwa kuingia fainali katika  shindano la uchomaji nyama kwa mwaka 2014 lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2014”.

Shindano hili linalofanyika kila mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar Es Salaam. Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo. Kwa mwaka huu baa 10 zilizopigiwa kura kwa wingi(Top 10 Bars) ni New City Pub  kura 2519, Kalembo Bar kura 2161, Bonanza Bar kura 455, Blue House kura 353, Rombo Deluxe kura 319, Nebana Bar kura 275, Tarakea Bar kura 247, Savoy Bar kura 139, Mbeya City Pub kura 122 na Iwawa Bar kura 107.Jumla ya Bar 45 zilipigiwa kura kwa Mkoa wa Mbeya.

Baa tano zilizopata kura nyingi zaidi zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakalofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba zikikisindikizwa na burudani ya muziki wa Bendi ya hapahapa  Mkoani ya TOT. Baa hizo ni New City Pub yenye kura 2519, Karembo Bar yenye kura 2161, Bonanza Bar yenye kura 455, Blue House Bar yenye kura 353 na Rombo Deluxe yenye kura 319.                          

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Nyanda za juu Kusini, Cloud Chawene, , “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.

Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 2, Mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe  ama CCM Ilomba kuanzia saa nne asubuhi ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili

Bwana Cloud Chawene  alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma pale wanapoihitaji. Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu. Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”. Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Bila Safari Lager, Nyama Choma haijakamilika!.

Balozi Ami Mpungwe ateuliwa kuwa mwenyekiti wa (Chemba ya Madini na Nishati Tanzania)

$
0
0
Chemba ya Madini na Nishati Tanzania (TCME) imemteua Balozi mstaafu, Bwana Ami Mpungwe kuwa mwenyekiti wake. Uteuzi huu wa Bwana Mpungwe kwa mara nyingine, unalenga kujizatiti kikamilifu kwa kuwaleta pamoja washikadau na umma  kushirikiana katika masuala ya sekta ya madini. 

Pamoja na kuwa Balozi mstaafu na kiongozi mzoefu wa sekta ya madini, Balozi Mpungwe, yupo katika nafasi nzuri ya kuiongoza Chemba kukua kiuongozi katika nafasi yake kama kioo cha sekta ya madini na kuwa kiunganishi cha washikadau wa sekta serikalini, wawekezaji, katika jamii na hata zaidi.

Balozi Mpungwe amesema; “Kwa unyenyekevu mkubwa, ninapokea kazi hii kwa mara nyingine.
Sekta ya madini imeleta faida nyingi sana Tanzania kupitia uingizaji wa Kigeni (Foreign Direct Investment, FDI),  teknolojia ya kisasa, ujuzi wa hali ya juu katika uongozi na utendaji wa uchimbaji wa madini, mabilioni ya shilingi kwa serikali kupitia kodi na fedha za kigeni kila mwaka na kutengeneza ajira nyingi zitokanazo na mchakato mzima wa uzalishaji madini. 

Kwa kwenda mbele, sisi kama sekta, tumejizatiti katika kutafuta njia bora zaidi za kuwasilisha mafanikio yetu, na pia kusikiliza mawazo ya washikadau wetu katika masuala yanayohusu Taifa letu kwa ujumla. Hii ndiyo dhumuni kuu ya Chemba na mimi nina dhamiria kutoa uongozi wa kina katika kutekeleza lengo hili.

TCME imeongeza nguvu katika jitihada zake za kuuelewesha umma kuhusiana na sekta ya madini na kazi zake  tokea mwaka 2011, kwa mfano, kuanzishwa kwa tovuti mpya ya TCME (www.tcme.or.tz) , uandaaji wa makala yanayohusu sekta ya Madini Tanzania yenye vipengele vinne iliyorushwa kwenye televisheni na pia inayopatikana  katika mtandao wa youtube (www.youtube.com) . 

 Katika kuboresha zaidi suala la mawasiliano, Chemba hivi karibuni, imemteua Bwana Nyanda Shuli  kuwa  Meneja wa Mawasiliano na Uenezi. Nyanda ni mwenye sifa kubwa ya uendeshaji wa Mawasiliano na Uenezi katika asasi za kijamii. 

Uteuzi wa Balozi Mpungwe kuwa Mwenyekiti wa Chemba ya TCME imeleta uzoefu na utaalumu katika nafasi ya uongozi. Balozi Mpungwe ni mwenyekiti wa bodi katika makampuni kadhaa, na ametumikia Taifa kama Mwanadiplomasia kwa zaidi ya miaka 25, na aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania wa kwanza nchini Afrika Kusini.

Hujafa hujaumbika:Mtanzania mwenzetu,elisha bahunde apata ajali na kuvunjika miguu yote miwili (back by popular demand)

$
0
0
Mtanzania Elisha Bahunde jina maarufu Eric ambaye siku ya Jumamosi Feb 15, 2014 alipata ajali Jimbo la Indiana iliyopelekea kukatika kwa miguu yote miwili na mkono wa kulia na baadae kuhamishiwa Jimbo la Maryland kwa matibabu zaidi kwa sasa yupo University Of Maryland Medical Center iliyopo 22 S Greene St, Baltimore, MD Ghorofa ya 6 chumba # 8 na anatumia jina la Elisha Bahunde.ama kweli hujafa hujaumbika na Mwenyezi Mungu ndiye mueza wa kila jambo,Mdau huyu wiki iliyopita alishiriki kwenye Kijiwe cha Ughaibuni (muangalie kwenye video hapo chini) ameva shati la njano na amekaa karibu na Ally Bambino


Video streaming by Ustream
 Elisha Bahunde akiwa chumba # 8 ghorofa ya 6 alipolazwa tangia siku ya Jumatano Feb 19, 2014 alipoletwa Maryland kwa matibabu zaidi
 Elisha Bahunde au Eric akiwa hana miguu wa mkono kama picha inavyoonyesha.
 Rais wa Jumuiya DMV, Bwn. Idd Sandaly akiwa Hospitalini hapo kumjulia hali mgojwa
 Abdi Makeo amkimjulia hali Elisha Bahunde
 Said Mwamende akimjulia hali Bwn. Eric huku akilengwa na machozi
 Wanajumuiya waliofika kumjulia hali wakiwa hawaamini walichokiona.
Kutoka kushoto ni Abdi Makeo, Saidi Mwamende, Rais wa DMV Idd Sandaly na Jabir Jongo wakiwa chamba cha mapumziko baada ya kumaliza kumjulia hali Elisha Bahunde kwa jina lingine Eric

hoja ya haja na Dakta Anicetus Temba juu ya uraia pacha

$
0
0

Nimetumia muda mwingi kusoma vipeperushi vya kitaalamu kuhusiana na suala linalojadiliwa sasa la uraia pacha katika Tanzania na Afrika kwa ujumla. Wakati nchi nyingi za Kiafrka zikionekana kuelekea katika mfumo wa uraia pacha Tanzania bado tuna kazi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa sulala hili. Inawezekana kabisa suala hili linaweza lisipewe kipaumbele katika Bunge Maaumu la Katiba. Maombi yetu ni kuliomba Bunge hilo lijadili mada hii kwa undani na kwa mapana yake. Watanzania wengi wanaoishi kwenye diasopora husema “Mimi ni Mtanzania” kila mara wakiulizwa wao ni nani.
Rasimu ya pili ya katiba inazungumzia kuhusu masuala ya uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na rasimu hiyo inaelezea uraia wa Tanzania unapatikanaje. Lakini rasimu hiyo haizungumzii uraia wa Watanzania wanaoishi kwenye Diaspora. Suala ambalo Watanzania wa ughaibuni tunalipendekeza ni suala lifuatalo, kuwepo na muda kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambao utatumika kujadili uraia wa Watanzania wanaoishi kwenye Diaspora. Hii ni katika kuhakikisha kuwa haki ya uraia wa Watanzania waishio kwenye Diaspora inatambulika na Watanzania wote.
Wote tunafahamu manufaa ya kiuchumi na kijamii yatakayoletwa na uwepo wa uraia pacha kwa taifa la Tanzania. Kama suala la uraia pacha halitaingizwa kwenye katiba hii mpya itachukua miaka mingi sana kwa katiba hii mpya kubadirishwa. Hivyo wakati ni huu wa kulijadili na kuhakikisha Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba wanaliingiza suala la uraia pacha kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bado hatujachelewa na ndio tunaweza (“Yes we can”).
Kwa kumaliza nakuomba usome sehemu hii rasimu ya katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2013 sehemu ya 38 inayosema:
“Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa mathumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakawezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila upendeleo na ubaguzi wa aina yeyote, na pale panapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.”
 Sehemu hii inaposema “kitambulisho cha uraia wake”- kitambulisho hicho hakijasemwa kama kitawahusisha vile vile Watanzania tunaoishi ughaibuni. Tunaomba sehemu iweke bayana kuwa ruksa kwa Watanzania wa ughaibuni kupewa kitambulisho hiko kwa maana na wao ni Watanzania. Kwa maana nyingine tunaomba kutokupoteza haki ya kuzaliwa Tanzania ambayo inatupa uraia wa Tanzania moja kwa moja. Angalia: http://www.katiba.go.tz/attachments/article/185/RASIMU%20(Final).pdf
Wakati huo huo, sheria ya uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 kwenye sehemu ya 14 inasema:
“The Minister may by order deprive any person, other than a person who is a citizen by birth, of his citizenship of the United Republic if the Minister is satisfied that person has at any time while a citizen of the United Republic and of full age and capacity voluntarily claimed and exercised, in a foreign country, any right available to him under the law of that country, being a right accorded exclusively to its own citizens, and that it is not conducive to the public good that he should continue to be a citizen of the United Republic.” Angalia: http://www.refworld.org/docid/3ae6b5734.html
Katika katiba mpya suala hili litarekebishwa vipi?
Imeandaliwa na Dakta Anicetus Temba katika jitihada za Watanzania wanaoishi kwenye Diaspora kuelimisha umma wa Watanzania wenzao kuhusu suala la uraia pacha. Na imetafsiriwa na Deogratius Mhella, Katibu wa Vikao vya Jumuiya za Watanzania na DICOTA.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images