Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 367 | 368 | (Page 369) | 370 | 371 | .... | 3284 | newer

  0 0

  The EACJ First Instance Division today dismissed a case filed by an Advocate from the Republic of Kenya, Mr. Mbugua Mureith, an accomplished lawyer and human rights defender, against the Republics of Kenya and Uganda.

  Mr. Mbugua’s claim his alleged arrest and detention in Uganda and his subsequent deportation by the security agents of Uganda in complicity with the security agents of Kenya without lawful or justifiable cause and in violation of Uganda’s and Kenya’s obligation under Articles 6(d), 7 (2), 104 (1) of the Treaty for the Establishment of the East African Community as well as Principles 16, 17, 18 and 21 of the United Nations Basic Principles on the Role of Lawyers and Article 7 of the EAC Common Market Protocol.

  The Court held that it had jurisdiction to entertain the matter as the cause of action in the case was based on the alleged infringement of the Partner States’ Treaty obligations which lies outside the Territory of Human Rights and therefore the case fell under its jurisdiction. However, the Court in its decision said that the matter was filed out time as provided under Article 30 (2) of the Treaty for the Establishment of the East African Community, which provides a two month time limit of the enactment or action complained of came to the knowledge of the Complainant. 

  The Court added that the Applicant took exactly one year, three months and twelve days to file the case instead of two months prescribed by the Treaty. The Applicant was arrested and detained in Uganda on 15th September 2010 and was later released and sent back to Kenya on 18th September 2010. He then filed his case on 30th December 2011. 

  The Court further added that the Treaty does not provide any power to the Court to extend, condone, waive or modify the prescribed time limit for any reason and that it is bound by the law (Treaty) and to the above reason it took cognizance of the fact of limitation.

  The Court therefore dismissed the case and ordered each party to bear its costs. Lawyers present to receive the Judgment were Mr. Selemani Kimunyu Counsel for the Applicant, Counsels for the Republic of Uganda (1st Respondent); Mr. Denis Bireje Director Prosecution, Phil Mwaka Principal State Attorney; Mr. Elisha Bafirawala Senior State Attorney and Mr. Richard Adrole State Attorney. 

  The Republic of Kenya represented by Ms. Stella Mwinyi Chief Litigation, and Antony Mulekyo. The Amicus Curiae was represented by Mr. Opiyo all appearing before Hon. Justices Jean Bosco Butasi Principal Judge, Justice John Mkwawa and Dr. Faustin Ntezilyayo.

  0 0

  Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla akielezea jinsi watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwawezesha vijana kuleta maendeleo katika jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi.
  Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi akichangia wakati wa majadiliano ya awali jinsi ya kuendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla.
  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akielezea kuhusu moja ya kituo cha vijana kinachojishughulisha na ufundi makanika kilichopo Ilonga Morogoro, kulia ni Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla wakati wa majadiliano ya awali ya kuendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd kujadili jinsi watakavyoweza kushirikiana kuanzisha program ya kuwaendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii. Kushoto ni Bw. Prashant Shukla Mkuu ya kampuni hiyo na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Genofeva Matemu - MAELEZO

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MFUKO WA PENSHENI WA
  PSPF


  TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU
   Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam.

  Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
  “PSPF - TULIZO LA WASTAAFU”

  Mkurugenzi Mkuu
  Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
  Makao Makuu,Golden Jubilee Towers,  S.L.P 4843. Dar-es-Salaam.
  Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
   Nukushi: +255222120930
   Barua pepe:pspf@pspf.tz.org

  0 0
 • 02/25/14--03:00: Article 7

 • Institute of Management and
  Entrepreneurship Development  RETIREMENT PLANNING COURSE

  A unique opportunity for employees to develop Entrepreneurship, Financial Literacy and Retirement Planning Skills. The longer prior to retirement you take this course, the more you will benefit.

  Approach and Contents
  The course is delivered by highly experienced facilitators using experiential methods. Participants are guided to recognize opportunities and challenges of retirement; their talents and other tangible and intangible assets and liabilities; alternative  post-retirement “careers”;  to choose when to retire; and to continuously build their asset base, streams of income and fulfilling lives after retirement. 

  They are exposed to good practices in starting and running a business, personal finance and health management; expected pension benefits and investment schemes tailored to retirees. They leave with self awareness, a Retirement Vision and look forward to their exit from employment.

  Dates, Fee and Registration
  24th - 27th March, 2014, Morogoro. Tuition is Tshs 500,000/= per person. Apply: info@imedtz.org or 0718-942314 (Ulrich) and
  0754-548248 (Hellen) or visit us at Mwalimu House, 7th Floor, Uhuru Road, Ilala, Dar es Salaam or www.imedtz.org to pick the Registration Form.

  We also offer Certificate and Diploma courses in Entrepreneurship and Business Management registered by NACTE

  0 0

  Kijiwe cha Ughaibuni kinamtakiwa mwenzao Eric Bahunde (shati la njano) afya njema na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka Eric Bahunde amelazwa University of Maryland Medical Center kwa matibabu baada ya kupata ajali ya kukatika kwa miguu yote na mkono wa kulia. Kruu nzima ya Kijiwe cha ughaibuni inawaomba Watanzania wote wajitahidi kufika Hospitali kumjulia hali yupo ghorofa ya 6 chumba namba 8 na muulizie kwa jina la Elisha Bahunde Eric anapenda vyakula vya Kitanzania kama unaweza kumpekelekea maandazi, vitumbua na vinginevyo atashukuru sana.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa iringa DK CHRISTIN ISHENGOMA amewataka wananchi mkoani  Iringa,kutokuwa na hofu katika kipindi hiki cha kuelekea kampeni za uchaguzi wa jimbo la kalenga.

  Akizungumza leo  kwenye moja ya kituo cha redio mjini humo,Nuru FM ,kupitia kipindi cha sunrisepower, amesema kuwa tayari ameshakaa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama akiwemo Kamanda wa Jeshi la Polisi,aidha ameongeza kuwa wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi, hivyo wananchi wanapaswa kutokuwa na hofu.

  Amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa jimbo hilo wageni wengi watakuwa wanaingia hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na vishawishi vya makundi mabalimbali katika kipindi hiki cha uchaguzi.

  Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwa yeye yupo katika vikao vya bunge maalum la katiba atakuwa anakuja kushiriki na wananchi katika mkoa wake katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kampeni zinazoendelea.

  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kuhusu suala la posho kwa upande wake yupo tayari kupokea kiwango chochote atakachopewa ambacho kitakuwa kinatolewa katika kikao cha bunge maalum la katiba.

  0 0

   Mratibu wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Omar Abdallah Ali akitoa muhtasari wa majukumu ya Jumuiya yao kwa Wandishi wa habari hawapo pichani katika Ofisi yao Mpendae Mjini Zanzibar.
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Ali Mansour Vuai akielezea matayarisho ya Uzinduzi wa Jumuiya yao utakaofanyika Machi 1 katika Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
   Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA)  Ali Mansour Vuai (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia matayarisho ya Uzinduzi wa Jumuiya yao utakaofanyika Machi 1 katika Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar .

  0 0

  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Paul Makonda akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzie,Mh. Godbress Lema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

  Mimi ni Kijana, ninayoyazungumza,ninayoyafanya yana reflect uhalisia huo. Hivyo kwa wito wa Ujana najikuta nashawishika sana kuongeza umakini katika masuala yahusuyo vijana hasa kwenye Katiba.

  Ni ajabu lakini kweli kuwa sehemu inayotaja juu ya Haki na Wajibu wa Vijana katika Rasimu yote ni Ibara ya 44 tu, tena inataja kwa ujumla wake bila hata kuweka ibara ndogo ama vipengele vya ufafanuzi.

  Ibara hiyo inasema;

  "..kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali za nchi washirika na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa "Raia Wema" na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni..."

  Sikuwa nategemea huu unaweza ukawa ndio mwisho wa maelezo ya Rasimu kuhusu Vijana. Nilitegemea nitakuta vipengele vinavyobainisha namna vijana watakavyonufaika na rasilimali, namna ambavyo sheria ndogo na taratibu baguzi ktk upatikanaji wa ajira na fursa zitakavyobainishwa kikatiba ili kumaliza kabisa matatizo ya Vijana.

  Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana.

  Nikitumia fursa na nafasi yangu kama mbunge wa bunge maalum la Katiba zipo hoja hizo kuu (3) tatu ambazo nitazisimamia ziingie kwenye Katiba kwa manufaa na mustakabal mwema wa Vijana bila kujali tofauti ya itikadi, dini ama kabila.

  Na nakaribisha mawazo na michango ya fikra ktk hoja zihusuzo Vijana.

  IMETOLEWA NA:
  PAUL MAKONDA.
  MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


  TAARIFA KWA UMMA
  RATIBA YA UZIMAJI  WA MITAMBO YA UTANGAZAJI YA ANALOJIA AWAMU YA PILI

  Ndugu wananchi, napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza rasmi mwezi Machi mwaka huu. Awamu hii ya Uzimaji inaanza baada ya Serikali kujiridhisha na matokeo ya tathmini ya uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia awamu ya kwanza kwenye miji saba ya Dar e salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Moshi na Arusha. Tathmini hiyo imeonyesha kuwa asilimia 89% ya watanzania kwenye miji hiyo wamehamia kwenye mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali. 

  Ninaamini kuwa asilimia kumi na moja ya watanzania waliobaki kwenye miji hiyo watakuwa wameingia katika mfumo wa dijitali hadi hivi sasa.
  Ndugu wananchi, Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza mwezi Machi mwaka huu katika miji tisa na kukamilika mwezi Oktoba 2014. Miji hiyo ni Singida, Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma, Morogoro, Kahama, Iringa na Songea. 

  Natoa wito kwa wadau na wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kutekeleza vema zoezi hili la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia kwa manufaa ya Taifa letu na wananchi wote kwa ujumla.
  Asanteni sana.

  Imetolewa na:
  Prof. Makame M. Mbarawa (MB.)
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
  DAR ES SALAAM
  21/02/2014

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mh. Kaika Saning’o Telele akizungumza wakati akifungua warsha ya kimataifa inayojadili maswala ya Maendeleo, Miundombinu na Vituo vya maji,katika hoteli ya Bahari Beach,jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo ya kimataifa ambayo inawakutanisha wanataaluma mbalimbali itafanyika kwa siku mbili huku mada nyingi zikitegemewa kuwasilishwa.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Bashir Mrindoko, anayefuatia aliyevaa miwani ni Katibu Mkuu Msaidizi Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji nchini Malawi,Mama Erica Maganga, anayefuatia ni Mhandisi Mkuu Wizara ya Maji nchini Zimbabwe,Bi. Tatenda Mawokomatanda,na kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Taaluma kutoka UN yenye ofisi zake nchini Ujerumani,Dkt. Mathew Kurian.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Eng. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa mapumziko katika warsha ya kimataifa kuhusu maendeleo, miundo mbinu na vituo vya maji.kulia kwake anayesikiliza ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mh. Kaika Saning’o Telele, anayefuatia kwa Naibu Waziri ni Mhandisi Mkuu Wizara ya Maji nchini Zimbabwe Bi. Tatenda Mawokomatanda, na Kushoto kwa Mrindoko ni Katibu Mkuu Msaidizi Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji nchini Malawi,Mama Erica Maganga.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya kimataifa iliyofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach, Nchini Tanzania.Picha na Chris Mfinanga.

  0 0

  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.

  Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
  Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
  -----------------------
  Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
  Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
  Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
  Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
   Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
  Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 
  Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
  Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
  Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
  Nasi tutafikisha ubani wako. 
  Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
  kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
  Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.

  0 0

  Vijana wakifurahia simu zao za mkononi huko Unguja, Shamba. 
  Picha na Sabry Juma

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya Noah katibu Mkuu wa Saccos ya Tujikwamue ya Chang'ombe, Dar es Salaam, Itika  Mwankenja katika hafla ya Taasisi ya PFT ya kukabidhi mikopo ya magari, bajaji, pikipiki na fedha kwa vicoba mbalimbali, Temeke, Dar es Salaam juzi. Mtemvu ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Itika akiangalia wakati Mtemvu akiliwasha gari hilo.
   Mtemvu akikabidhi mkopo wa bajaji kwa moja ya wana vicoba
   Mwenyekiti wa Mpakani B Vicoba, Mwaimuna Ali akikabidhiwa funguo wa bajaji kwa niaba ya wenzie
   Ni furaha iliyoje kwa kikundi hicho kupata mkopo wa bajaji
   Moja ya Vicdoba ikipatiwa mkopo wa pikipiki
  Viongozi wa VICOBA ya VAMAU wakipatiwa funguo za pikipiki baada ya kukopeshwa na PFT

  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Madini ,Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Hamis Komba akiongea jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand Mhe. Srirat Rastapana mara baada ya kufungua maonesho ya 53 ya “Bangkok Gems & Jewelry Fair” mapema leo. Nyuma ya Kamishna ni Bw. Edward Rweymamu ni Mthamini wa Madini ya Almas Wizara ya Nishati na Madini. Kushoto Mhe. Dora Mushi mfanyabiashara wa madini kutoka Arusha.
  Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak akiangalia madini ya Almas katika banda la Tanzania. Anamwelekeza jambo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki maonesho hayo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sam Mollel wa pili kulia akionesha Hati ya Maridhiano ya kuendeleza ushirikiano wa tasnia ya madini ya vito na usonara baada ya kusaini kati yake na Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak. Wanaoshuhudia ni Kamishna msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba (Wa kwanza kulia) na Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
  Ujumbe wa Tanzania katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok katika picha ya pamoja na Rais Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak (aliyeshika kinyago cha mamba kilichochongwa kutokana na mawe ya madini yanayopatikana nchini Tanzania. Kinyago hicho kimechongwa na Kituo cha 'Tanzania Geomological Center' kilichopo Arusha.) Wa tatu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
  Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Thailand Mhe. Ruby Marks (katikati) katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ya madini( wa kwanza kushoto, Bw. Sam Mollel mwakilishi kutoka Tanzania Geomological Center (wa tatu kulia) Bw. Musa Shanyangi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi.(nne kulia).


  0 0

  Bwa.Marco Hingi akifurahia mara baada ya kujishindia gari hilo aina ya Noah kutoka kampuni ya Be Forward
  Meneja  Masoko wa Be forward Tanzania,Bwa Kohei Shibata (kulia) na  Meneja Mkuu wa kampuni hiyo  Isaac  Mbinile  wakimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa gari  aina ya Noah  Marco Hingi (katikati) ambaye ni mwanafunzi wa kutoka  hosipitali ya  bungando, jijini mwanza.
   Meneja Mkuu wa kampuni ya uagizaji na usambazaji  magari  ya Be forward Tanzania Issac Mbinile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari  wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi gari aina ya noah mshindi (kulia). hafla hiyo ilifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo   katika bustani za Palm Resdency , mkabala na hospitali ya  saratani 'ocean road' jijini dar es salaam.
  Kampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka JAPAN ya BEFORWARD imeendesha shindano la kuwapata washindi 25 duniani kote waliojielezea jinsi wanavyoweza kuitumia kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo mtanzania MARCO HINGI ameibuka mshindi na kujishindia gari.

  Akizungumza jijini DSM Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA amesema shindano hilo liliendeshwa wakati wa sikukuu ya CHRISMASS ambapo wateja waliotembelea ukurasa wa facebook wa befoward walipata nafasi ya kuulizwa maswali na kujibu mambo kadha wa kadha  
  Kati ya washindi hao Tanzania imepata nafasi mbili ambapo mwanafunzi wa chuo cha afya cha BUGANDO MWANZA bwana MARCO HINGI ameibuka mshindi

  Makabidhiano ya zawadi ya gari aina ya NOAH yenye thamani ya shilingi milioni 11.8 yamefanyika leo jijini DSM kati ya Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA na Mshindi MARCO HINGI ambapo SHIBATA amesema hiyo ni moja ya mikakati yao ya kuongeza mauzo kwa kuwafanya wateja kuwa na imani nao kama anavyoeleza meneja mkuu ISAAC MBINILE  
  Kwa upande wake MARCO HINGI ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha  afya BUGANDO mwanza amesema aliwaomba BEFORWARD kumpatia gari la kubebea wagonjwa kutokana na mradi wake alioubuni wa kusaidia mama wajawazito vijijini.

  Aidha HINGI ameongeza kuwa baada ya kujibu swali la BEFORWARD walijitokeza watu wengi waliolipenda wazo lake kwa kuandika ‘like’ na hatimaye kuibuka mshindi.HINGI amesema atalitumia gari hilo kubebeea wagonjwa katika mradi huo waliouanzisha mkoani MWANZA

  0 0
   Waombolezaji wakisukuma jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), marehemu Balozi Fulgence Kazaura ulipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)


   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akwafariji ndugu wa marehemu


   Ndugu wakifunua jeneza kuutengeneza mwili wa marehemu Kazaura.   Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni  0 0


  0 0

  Na Hellen kwavava

  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya wadau wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 21 mwaka huu ambayo ni viwango vya ufaulu, alama ya chini ya ufaulu na ufaulu wa jumla wa mtahiniwa.

  Akitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza hilo Dakta CHARLES MSONDE amesema viwango vya ufaulu ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na wale walio katika kundi jingine.

  Amesema mkanganyiko uliojitokeza katika mitihani hiyo ni kutokana na baraza kuanza kutumia utaratibu wa makundi 7 ambayo ni A ikiwa ni 75-100,B+ ikiwa ni 60- 74, B ikiwa ni 50-59, C ikiwa ni 40-49, D ni 30-39, E ni 20-29 na F ni 0-19 lengo likiwa ni kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja.

  Ameongeza kuwa madaraja hayo yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)6 cha kanuni za mitihani ambacho kinaeleza kuwa ufaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama na ufaulu katika daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili.

  Kuhusu kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja MSONDE amesema ufafanuzi utatolewa na Kamishna wa elimu.

  0 0
 • 02/25/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ni Wewe Pekee by Nguza Viking "Big Sound" Zembwela

  0 0


older | 1 | .... | 367 | 368 | (Page 369) | 370 | 371 | .... | 3284 | newer