Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live

CHADEMA WAZINDUA RASMI KAMPENI ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

0
0

makumbusho_a0aac.jpg
Viongozi na wanachama wa CHADEMA wakielekea kwenye makumbusho ya Chifu mkwawa kabla ya kuanza kampeni hizo
mvua_6aa63.jpg
Hapa wakitoka kwenye Makumbusho ya Chifu Mkwawa huku hali ya hewa ikiwa ni ya ubishi kutokana na mvua kubwa kunyesha
kumnadii_f8eb3.jpg
Mgombea wa Ubunge kupitia chama cha CHADEMA akinadiwa na Katibu mkuu wa chama hicho Dr. W. Slaa wakati wa kampeni hizo zilizoanza hii leo katika jimbo la Kalenga.

MASIBA DMV NA TANZANIA: Balozi Fulgence Kazaura afariki dunia

0
0
Balozi Fulgence Kazaura enzi ya uhani wake

Sima Kazaura anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi Balozi Fulgence Kazaura kilichotokea leo nchini India. Kama ilivyo ada kupeana mkondo wa pole na kufarijiana ndio ustaarabu wetu wakatio wa msiba hapa DMV 
Msiba upo 
21, Featherwood Court Apt. 14
Silver Spring MD 20904
Tutazidi kuwajuza mambo yanavyoendelea katika msiba huu hapa DMV na nyumbani Tanzania.  Chini hapo ni namba ya mfiwa
Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Sima Kazaura 202 413 9184 

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake na lihimidiwe.
Amina

TTCL yaahidi makubwa mradi wa mawasiliano vijijini

0
0
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeahidi kutekeleza kwa ufanisi na kwa wakati zabuni iliyoshinda ya mradi wa kutoa huduma za mawasiliano vijijini. Ahadi hiyo imetolewa na Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kampuni hiyo kutiliana saini na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. 
TTCL inatekeleza mradi huo wenye thamani ya Tshs 9.8 bilioni baada ya kushinda zabuni hiyo. Ushindi huo unamaanisha kuwa baada ya kukamilisha mradi huo, TTCL itakuwa na uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano katika kata 33 zenye jumla ya vijiji 202 vyenye jumla ya wakazi zaidi ya 300,000 katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 
“Tutafanya kwa ubora zaidi katika awamu hii kwa maana tuna uzoefu wa kina kwani kwa sasa tunao wataalamu wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha kusimamia miradi ya aina hii,” alisema Bw. Ngota aliyekuwa akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura. Bw. Ngota alisema kampuni hiyo ni muhimili wa mawasiliano Tanzania kwa zaidi ya miaka hamsini sasa katika kutoa huduma za mawasiliano hivyo hawana shaka yoyote katika kutekeleza mradi huo. Katika awamu ya kwanza yenye kata 20 kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine za simu hapa nchini ilishinda zabuni yenye thamani ya Tshs 3.4 bilioni ambayo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. 
Bw. Ngota aliiomba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na UCSAF na wadau wengine kuendelea kushirikiana katika kuleta mapinduzi ya mawasiliano bora kwa wananchi wengi ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 
Awali, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa alisema serikali inatambua umuhimu wa watoa huduma za mawasiliano katika kupeleka mawasiliano sehemu zenye mawasiliano hafifu. 
“Upelekwaji wa mawasiliano umeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi wa kijamii katika maeneo hayo,” alisema. 
Alisema ni shauku ya serikali kuona kuwa huduma zote wanazofurahia watu wa mijini kutokana na matumizi ya TEHAMA zinawafikia pia watu wa vijijini ifikapo mwaka 2015. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Injinia Peter Ulanga alisema mfuko wake umedhamiria kuona maeneo mengi zaidi vijijini yanafikiwa na huduma za mawasiliano. 
“Hii ni kwa mujibu wa dira ya maendeleo ya serikali na mkakati huu utasaidia kufikia maendeleo endelevu hapa nchini,” alisema. 
Vijiji husika vya mradi huu viko katika mikoa 16 ambayo ni Arusha, Tabora, Iringa, Kagera, Manyara, Dodoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tanga. 
Mradi huu ulifadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia UCSAF ambao upo chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia umepangwa kumalizika ndani ya kipindi cha miezi nane kuanzia Februari 20 mwaka huu. 
 TTCL pia itagharamia kiasi cha pesa katika mradi huo. Kwa kuanzia, huduma zitakazotolewa ni zile za msingi kama huduma za ujumbe mfupi, mtandao wa intanenti kupitia simu za mkononi na za mezani zisizotumia waya.
 Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bw. Peter Ulanga wakitia saini mkataba wa mradi wa kutoa huduma za mawasiliano vijijini wenye thamani ya Tshs 9.8 bilioni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma (kushoto), Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dr. John Mngodo.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bw. Peter Ulanga na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (katikati) wakifurahia kusainiwa kwa mktabara huo

Maboresho bandari ya Dar es Salaam yaanza kuzaa matunda

0
0
Maboresho yanayofanywa na serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) katika kuboresha huduma zinazotolewa na bandari ya Dar es Salaam sasa zimeanza kuzaa matunda. 
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa bandari imeanza kupata mafanikio katika kuwahudumia wateja wake na maeneo mengine kutokana maboresho yanayo endelea kufanywa. 
Katika miaka ya hivi karibuni pamekuwepo na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, TPA pamoja na wadau wengine kuhakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inatoa huduma bora kwa wateja wa hapa nchini pamoja na wale wan chi jirani. 
“Takwimu zinaonyesha kuwa maboresho haya yanasaidia sana kuimarisha huduma zetu,” alisema Bi. Ruzangi. 
Alitaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la shehena, tija katika kuhudumia shehena na meli zinazotumia bandari hiyo, na kupungua kwa msongamano wa meli. 
Pia kumekuwepo na punguzo kubwa la mrundikano wa mizigo na kufanikiwa kukomesha vitendo vya upotevu wa mizigo na wizi kwa kiasi kikubwa. 
Akitoa mfano alisema idadi ya meli zinazotumia bandari hiyo imeongezeka kutoka 1,236 mwaka 2011/12 hadi kufikia meli 1,301 mwaka 2012/13. 
Kwa upande wa shehena mwaka 2012/13 bandari ilihudumia jumla ya tani milioni 12.5 ikilinganishwa na tani milioni 10.9 mwaka 2011/12, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 15. Alisema mwaka wa 2012/13 bandari ilizihudumia nchi zinazotumia bandari hiyo shehena ya tani milioni nne ambayo ni sawa na asilimia 32 ya shehena yote. 
“Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2013 tulihudumia tani milioni 7.50 ukilinganisha na tani milioni 6.38 zilizohudumiwa kipindi cha Julai hadi Desemba, 2012, ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 17.6,” alisema Bi. Ruzangi. 
Mafanikio mengine ni kupungua kwa siku meli kukaa bandarini kutoka siku 6.9 mwaka 2008/09 hadi siku 4.9 mwaka 2013, ambapo Julai hadi Disemba 2013 zilipungua hadi kufikia siku 5.6 ukilinganisha na siku 5.9 kipindi cha Julai hadi Disemba 2012, ikiwa sawa na punguzo la asilimia 5.1 
Aidha alisema maboresho hayo yamesaidia pia kuongeza mapato. Mwaka 2012/13 wastani wa Tshs bilioni 371.7 zilikusanywa, sawa na ongezeko la asilimia 14.3 ukilinganisha na Tsh. bilioni 325.3 mwaka 2011/12 
Katika mapato hayo, bandari bila ya makusanyo ya TICTS, ilikusanya Tsh.bilioni 324.5 mwaka 2012/13, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.9, ikilinganishwa na mapato ya Tsh.bilioni 272.9 mwaka 2011/12. 
Kwa mujibu wa meneja huyo, matukio ya uhalifu na wizi yamepungua sana kutoka matukio 21 mwaka 2011 hadi matukio 7 mwaka 2012, na kufikia matukio 3 mwaka 2013. 
Alisema hali hiyo imetokana na mikakati mbalimbali inayochukuliwa na mamlaka ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya kisasa katika udhibiti wa uingiaji bandarini, uboreshaji wa miundombinu, mafunzo kwa askari na dhana ya ulinzi shirikishi kwa wafanyakazi na wateja.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bi. Janeth Ruzangi akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu matunda ya maboresho ya bandari ya Dar es Salaam yanayofanywa na serikali kupitia Mamlaka hiyo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO TAREHE 23.02.2014.

Vodacom yaendelea kupanua wigo wa huduma kwa wateja Dar es Salaam

0
0
Wateja wa Vodacom wameendelea kukumbushwa kupata huduma katika maduka mapya yanayoendelea kufunguliwa maeneo mbalimbai karibu na makazi ili kuepuka gharama na usumbufu usio wa lazima wa kufuata huduma kwenye maduka yalyozoeleka yaliyopo mjini na yaliyo kwenye maeneo ya kibiashara. 
 Vodacom kwa sasa imekuwa ikifungua maduka sehemu mbalimbali ili kuwapunguzia gharama na muda wateja wake ikiwemo lilifunguliwa jana Tabata Magengeni jijini dar es salaam duka ambalo litatoa huduma kwa wakazi wa maeneo ya Tabata. 
 Mkuu wa idara ya Mauzo ya Rejareja wa kampuni hiyo, Upendo Richard amewataka wateja hao kutumia ipasavyo duka hilo na kuachana na kuepuka adha kusafiri kwenda mbali kutafuta huduma za Vodacom kwani duka hilo litakuwa likitoa huduma zote wanazo hitaji wateja wa kampuni hiyo. “Huduma katika maduka yetu yote bila kujali eneo lililopo yanatoa huduma zenye ubora sawa na za kiwango cha juu."lengo letu ni kuwasogezea wateja huduma karibu na walipo hivyo tunawaomba wayatumie kwa kujiamini na watapatapa suluhusho la mahitaji yao yote"aliongeza Upendo. 
 Kwa Upande wao wakazi wa Tabata Bwana, Saimon Edward Rugenga na Bi. Arafa Hamza ambao ni wateja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo wamesema kusogezwa kwa huduma kwa wateja katika maeneo hayo ni jambo jema kwani sasa wateja wa matandao huo hawatopata tena tabu ya kusafiri kutoka Tabata kwenda maeneo mengine ya mji kufuata huduma hiyo. 
 “Eneo hili la tabata Magengeni ni eneo la makazi ya watu, tumezoea kuona maduka kma haya yakijengwa sehemu zenye maofisi au biashara, sasa kwa hatua hii ya kutuletea huduma hasa watu tulioko maeneo ya pembezoni mwa mji ni jambo jema ninaamini duka hili litatusaidia wakazi wengi na ninawasihi Vodacom wasiishie hapa Tabata waendelee katika maeneo mengine ya Mikoani,” alisema Bwana, Saimon Rugenga. 
 Nae Bi Arafa Hamza alisema “Kwa kipindi kirefu wateja wa Vodacom walioko tabata na maeneo ya karibu walilazimika kwenda Buguruni, Posta au Mlimani city ili kufuata huduma sasa jambo hili halitokuwepo tena, na yeye kama mfanyabiashara atakamilisha mahitaji yake yote ya kimawasiliano katika duka hilo, alisema.
Alihitimisha kuwa” Hatua hii ni yakupongezwa na watoa huduma za mawasiliano wengine waige mfano huu ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma hizi za mawasiliano kwa Watanzania.” 
Duka hilo ambalo ni la 77 kufunguliwa nchini litakuwa likitoa huduma mbalimbali zikiwemo ununuzi wa modem, kusajili laini, kuunganishwa na intaneti, kufanya manunuzi ya simu, huduma mbalimbali za M-Pesa pamoja na ushauri wa huduma za kimawasiliano.
 Muonekano wa duka jipya la Vodacom lililopo Tabata Magengeni.Duka hilo linatarajiwa kuwarahishia wateja kupata huduma kwa karibu na kuwapunguzia usumbufu na gharama za kufuata huduma umbali mrefu.
 Mkuu wa idara ya mauzo ya rejareja wa kampuni ya vodacom Upendo Richard akifungua mlango wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Tabata tayari kuanza rasmi kazi ya kutoa huduma. Kushoto ni meneja mauzo wa vodacom Tabata Michael Bigambo na kulia ni meneja wa duka hilo Simon Rugenge.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) akimsikiliza  Saimon Rugenga ambae ni mteja wa pili kufika katika duka la Vodacom Tabata Magengeni mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Liganga alipongeza mkakati wa kampuni hiyo wa kufungua maduka kwenye maeneo ya makazi hatua itakayowapunguzia usumbufu na gharama wateja za kufuata huduma maeneo ya mijini na ya kibiashara. Katikati ni Meneja wa idara ya mauzo ya rejareja Elihuruma Ngowi. 
 Wafanyakazi wa Vodacom wakijumuika kutakiana heri na Saimon Liganga (wa tatu kushoto) na Arafa Hamza (wa nne kushoto)ambao ni wateja wawili wa kwanza kupata huduma kwenye duka jipya la kampuni hiyo lililopo Tabata Magengeni muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi jana. Vodacom inaendelea na mkakati wake wa kuwasogezea wateja huduma maeneo ya karibu na makazi yao.

 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiokota kikaratasi cha mshindi wa zawadi ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililopo Tabata Magengeni. Droo hiyo ya kushtukiza ilihusisha wateja na wadau waliokuwepo wakati wa hafla ya uzinduzi.Mshindi alipatiwa moderm ya kisasa.
Mteja wa Vodacom Arafa Hamza akiagana kwa furaha na Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja Upendo( kushoto) kwa  kubahatika kuwa mteja wa kwanza kupata huduma kwenye duka jipya lililopo Tabata Magengeni baada ya kuzinduliwa rasmi jana.

ajali mbaya eneo la Mikese, Morogoro, leo Asubuhi

0
0
 Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund

 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA TFF LEO Februari 23, 2014


RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MISRI IKULU, DAR ES SALAAM

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy alipomtembelea Jumamosi Februari 22, 2013 jioni Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Fahmy amefanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipookea ujumbe toka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy alipomtembelea Jumamosi Februari 22, 2013 jioni Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Fahmy amefanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy na ujumbe wake walipomtembelea Jumamosi Februari 22, 2013 jioni Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Fahmy amefanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.Picha na IKULU.

Washindi wawili wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti wakabidhiwa zawadi zao

0
0
Washindi wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti Godbles Sehaba (kulia)na  Karushe Mathias  (kushoto) wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao za king’amuzi cha azam walizoshinda baada ya kuchezeshwa droo hiyo siku ya jumatano.
  mshindi wa king’amuzi cha azam katika promosheni ya winda safari ya Brazili na Serengeti Bw Godbles Sehaba katikati akikabidhiwa zawadi yake  na meneja mauzo eneo la mabibo Bi Anna Gassembe (kushoto) na afisa mauzo Bi Anna Msonga (kulia).

Washindi wawili wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti wamekabidhiwa zawadi zao jumamosi katika bar ya muleba iliyopo maeneo ya Mabibo Dar es Salaam, washindi hao Bw Godbles Sehaba na Karushe Mathias wakiwa na furaha walipokea zawadi hizo na kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwapa zawadi hiyo, wakiwa kama mashabiki wakubwa wa soka la nyumbani washindi hao wamefurahia kupata zawadi itakayowawezesha kuangalia ligi za mpira wa miguu ya nyumbani bila matatizo.


Meneja mauzo eneo la mabibo hilo Bi Anna Gassembe ambaye alikabidhi zawadi kwa washindi amehimiza watu kuendelea kunya bia ya Serengeti kistaarabu ili wajishindie zawadi. "zawadi bado ni nyingi na zawadi kubwa ya safari ya Serengeti bado haijatolewa kwa hiyo muendelee kushiriki zaidi ili mjipatie zawadi mbalimbali" alisema Anna.



promosheni ya winda safari ya Brazili na Serengeti inaendelea na washindi wanaweza kujishindia zawadi za simu aina ya samsung galaxy tab, king'amuzi cha azam, pesa taslimu shilingi 5000 na 10000, bia za bure pamoja na zawadi kubwa ya safri ya kwenda Brazili.


WADAU WA SOKA WAMUENZI MAREHEMU OMARY CHANGA KWA BONANZA LA SOKA

0
0
Wadau mbali mbali wa mchezi wa Soka jijini Dar es Salaam,leo wamekutana pamoja kwenye viwanja vya Tabata Shule katika Bonanza la kumuenzi Marehemu Omary Changa (pichani) aliyewahi kuwa Mchezaji katika timu za Yanga,JKT Ruvu,Kagera Suger pamoja na Moro United aliefariki dunia mwezi uliopita.Bonanza hilo limefanyika maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuisaidia familia ya Marehemu Changa ikiwa ni pamoja na kuweza kufanikisha kisomo cha Arobaini yake.
 Mshambuliaji wa Pembeni wa timu ya Kijitonyama Veterans,Majuto Omary akichanja mbuga katika lango la wapinzani wao ambao ni Tabata Veterans,wakati wa Bonanza la kumuenzi Marehemu Omary Changa (pichani) aliyewahi kuwa Mchezaji katika timu za Yanga,JKT Ruvu,Kagera Suger pamoja na Moro United aliefariki dunia mwezi uliopita,lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Tabata Shule,jijini Dar es Salaam.
 hapiti mtu hapa.......
Beki wa Kati wa timu ya Kijitonyama Veterans akiondoka na mpira huku mpinzani wake akimsindikiza.

Malinzi akabidhi kombe bingwa Michuano shule za Sekondari Dar

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa a(BMT) Dionizi Malinzi (wapili kulia)akikabidhi kombe kwa kapteni wa timu ya sekondari ya Mugabe Laurian Didas baada yakuibuka mabingwa katika michuano maalumu ya Community Sports Cup ambapo walishinda jumla ya bao 1-0 dhidi ya shule ya sekondari ya Kawe,( wa pili kutoka kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo, Katibu Mkuu wa BMT Henri Lihaya (wakwanza kutoka kulia). Michuano hiyo imemalizika rasmi kwa udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mashabiki wa timu ya sekondari ya Mugabe wakishangilia baada yakuibuka mabingwa wa michuano maaalum ya Communnity Sports Cup baada ya kuichapa timu ya sekondari ya Kawe bao 1-0 katika fainali zilizopigwa kiwanja cha Turiani Sekondari. Michuano hiyo imemalizika rasmi kwa udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Meneja wa Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (aliyevaa flana nyekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Sekondari ya Mugabe kabla ya fainali hiyo ya mashindano maalum ya Community Sports Cup kuanza katika kiwanja cha Turiani Sekondari. Mashindano hayo yamewezeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.
Meneja wa Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (aliyevaa flana nyekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Sekondari ya Kawe kabla ya fainali hiyo ya mashindano maalum ya Community Sports Cup kuanza katika kiwanja cha Turiani Sekondari. Mashindano hayo yamewezeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.

Dkt Shein awaandalia chakula kwa watototo wa Halaiki Zanzibar

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi,(kulia) katika  hafla ya Chakula cha mchana alichowaandalia Watoto waliocheza  halaiki katika sherehe za  miaka 50 ya Mapinduzi  ya Zanzibar katika kilele kilichofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja tarehe 12 jan 2014.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi,(wa tatu kushoto) akiwa na katika picha ya pamoja na Watoto  waliocheza halaiki baada ya kuwanao pamoja katika  hafla ya Chakula cha mchana alichowaandalia Watoto hao waliofanikisha sherehe za  miaka 50 ya Mapinduzi  ya Zanzibar katika kilele kilichofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja tarehe 12 jan 2014, wakiwepo viongozi wengine.
 Baadhi ya Watoto waliocheza halaiki wakichukua chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Sheinkatika viwanja vya Beit El Ras leo mchana kwa kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kilele kilichofanyika Uwanja wa Amaani Mjini Unguja tarehe 12 jan 2014
 Watoto waliocheza halaiki wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Sheinkatika viwanja vya Beit el Ras leo,watoto zaidi ya Elfu mbili walihudhuria katika hafla hiyo  iliyofanyika baada kufanikisha kwao kwa umahiri kabisa katika sherehe za kilele cha miaka 5o ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja tarehe 12 jan 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi,Mwanaidi Abdalla,wakati alipowasili katika viwanja vya Beit el Rasi  katika hafla ya Chakula cha mchana alichowaandalia Watoto waliocheza  halaiki katika sherehe za  miaka 50 ya Mapinduzi  ya Zanzibar katika kilele kilichofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja tarehe 12 jan 2014. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKANUSHA KUZIBANA WIZARA

0
0
Na Veronica Kazimoto 
wa MAELEZO

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa wito kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wanasiasa wote  nchini kutumia taakwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi hiyo ili ziweze kutumika katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam, Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza (pichani) amesema Ofisi ya Takwimu imerahisisha upatikanaji wa takwimu hizo kupitia Kanzidata inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED).
 
“Lengo la kanzidata hii sio kuzibana Wizara wala kuwashurutisha wanasiasa kutumia takwimu  bali ni kuwarahisishia watumiaji wote wa takwimu kupata taarifa kwa wakati pindi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku,” amesema Bi. Mahiza.
 
Meneja huyo amefafanua kuwa TSED inasaidia kuondoa mlolongo wa upatikanaji wa taarifa uliopo kwenye baadhi ya ofisi nyingi ambapo wakati mwingine mteja huambiwa aandike barua au arudi baada ya siku kadhaa. 
Aidha, amesisita kuwa ni muhimu kutumia Kanzidata hiyo kwa kuwa ndani yake kuna takwimu rasmi ambazo zinatoka katika vyanzo sahihi vyenye mamlaka ya kutoa takwimu hizo hapa nchini. 
Bi. Mwanaidi Mahiza ameyasema hayo wakati akikanusha habari iliyoandikwa na moja ya gazeti la kila siku lililoripoti kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia marekebisho ya sheria ya takwimu ya mwaka 2002 ambayo yako bungeni kutumika kuzibana wizara ili zitoe takwimu sahihi katika ripoti zao kitu ambacho hakikuzungumzwa. 
Hivi karibuni baadhi ya wahariri na waandishi wa habari walipewa mafunzo na Ofisi ya Taifa ya Takwimu juu ya Kanzidata inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED) ambapo baadae moja ya gazeti la kila siku liliandika habari yenye kichwa cha habari Ofisi ya Takwimu kuzibana wizara. 
Kanzidata inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii ilizinduliwa rasmi mwaka 2001 ikiwa na viashiria 75 ambapo hivi sasa ina viashiria 940 na inapatikana katika mfumo wa DVD, CD ROMs na tovuti ya www.tsed.org.

Membe (Mb.) kufanya ziara ya kikazi ya siku tano katika Jamhuri ya Watu wa China

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atafanya ziara ya kikazi ya siku tano katika Jamhuri ya Watu wa China kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014. Ziara ya Mhe. Membe inakuja kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi.
Mhe. Membe anafanya ziara hiyo nchini China kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya Tanzania na China. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Membe atafuatana na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Ziara hii pia ni muendelezo wa maeneo ya utekelezaji baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini tarehe 24 na 25 Machi, 2013 na baadaye ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda nchini China mwezi Oktoba, 2013.

Akiwa nchini China, Mhe. Membe atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China tarehe 25 Februari 2014. Siku hiyo hiyo Mhe. Membe atamtembelea Makamu wa Rais wa China, Mhe. Li Yuanchao kwa lengo la kumsalimia na baadaye atafanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Gao Hucheng.

Aidha, tarehe 26 Februari, 2014 Mhe. Membe atatembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Poly Technologies yaliyopo katika mji wa Shenzhen na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa  na Kampuni hiyo kabla ya kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya China Merchant Holdings International ambako atapokea taarifa ya maandalizi ya kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Bandari katika eneo la Mbegani huko Bagamoyo.

Mhe. Membe pia atapata fursa ya kutembelea Kampuni ya HUAWEI ili kujionea shughuli mbalimbali. Kampuni ya HUAWEI ina Mkataba na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya hapa nchini kuhusu Elimu kwa Njia ya Mtandao (e-Education) kwa Shule za Sekondari.

Vile vile tarehe 27 Februari, 2014, Mhe. Membe atautembelea Mji maarufu wa biashara wa Guangzhou na kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi mjini hapo. Mhe. Membe atatoa taarifa kuhusu hali ya uchumi, siasa na masuala ya jamii yalivyo hapa nchini kwa sasa pamoja na  kutoa taarifa ya maendeleo ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Waziri Membe pia atatembelea Eneo la Viwanda la Huadu tarehe 28 Februari, 2014 kabla ya kurejea nchini tarehe 1 Machi, 2014.


IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

24 FEBRUARI, 2014


Simba yashindwa kufua dafu kwa maafande wa JKT Ruvu leo,yatandikwa bao 3 - 2

0
0
Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta akimpeleka markiti Golikipa wa timu ya Simba, Yaw Berko kwa mkwaju mkali wa Penati na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa mchezo Simba wamelala kwa Bao 3 - 2.Picha na Othman Michuzi.

Wachezaji wa timu ya JKT Ruvu wakishangilia mara baada ya kuitandika Simba bao la pili.
 Golikipa wa Timu ya Simba,Yaw Berko akiruka bila mafanikio ya kudaka shuti kali lililopigwa na Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta na kuingia kimiani moja kwa moja na kuiandikia timu yake bao la tatu dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imefungwa bao 3 - 2.
 Nahodha wa timu ya JKT Ruvu,Amos Mgisa akiangalia namna ya kumtoka beki wa Simba,William Lucian wakati wa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara,uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.katika mchezo huo Timu ya Simba ililala kwa Bao 3 - 2.
 Beki wa Timu ya Simba,Donald Mosoti (kulia) akichuana vikali na mshambuliani wa timu ya JKT Ruvu,Iddi Mbaga.
 Salum Machaku wa JKT Ruvu (kulia) akionyesha uwezo wake mbele ya Beki wa Simba.
Kufungwa kubaya jamaniiiii...... Pichani ni Beki wa Timu ya Simba William Lucian  akiwa amekaa chini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.
Madaktari wa timu ya JKT Ruvu wakitoka uwanjani kutoa huduma ya kwanza. 

DKT. MAGUFULI ATEMBELEA LA MAGARI YALIYOTEKETEA KWA MOTO MIKESE, MOROGORO LEO

0
0
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli amesafiri akitokea Mkoani Dodoma anakohudhuria Vikao vya Bunge la Katiba na kwenda moja kwa moja Morogoro maeneo ya Mikese (Kilomita kumi kutoka Mzani wa Mikese kuelekea Dar), ambapo magari mawili yaligongana na kuteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja alietambulika kwa jina la Moud Amin.

Ajali hiyo ambayo imetokea mapema leo ilifunga barabara yote ya Dar - Morogoro, takribani kwa masaa zaidi ya mawili na kusababisha foleni kubwa ya takribani kilomita 30. Malori hayo, lori moja lilikuwa likitokea Bukoba, mkoani Kagera likielekea Dar na lori lingine likielekea Sumbawanga, mkoani Rukwa. Chanzo cha ajali bado hakijafahamina na uchunguzi bado unaendelea.

Aidha, Dkt. Magufuli kwa mamlaka aliyopewa, ameruhusu malori yaliyokuwa yamesongamana kupita mzani wa Mikese bila kupimwa ili kuondoa usumbufu mwingine katika mzani wa Mikese.

Dkt. Magufuli kwa pamoja na mhandisi wa mkoa wa Morogoro Mhandisi Tenga walisimamia ukwamuaji wa malori hayo.
Dkt. Magufuli akiangalia hali ya lori hilo mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio, Mikese Morogoro.
Dkt. Magufuli akiongea na baadhi ya wahanga wa ajali hiyo.

ziwa la ajabu nigeria lavutia maelfu kama kilivyokuwa kikombe cha babu wa loliondo...

NGUMI ZAPIGWA MBAGALA

0
0
BONDIA Mussa Shuza kushoto akioneshana umwamba na Dackson Kawiani wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub mbagala rangi tatu Kawiani alishinda kwa point.

Mabondia Ibrahimu Ahmed kushoto na Mohamed Kashinde wakioneshana ubabe wakati wa mpambano wao uliofanyika mbagala Dar es salaam Kashinde alishinda kwa point 

Bondia Hassani Kidebe kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na Shabani Mtengela wakati wa mpambano wao Mtengela alishinda kwa point mpambano huo. Picha na Super D

Malinzi Ajitambulisha Rasmi Kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou Jijini Cairo,Misri Akisindikizwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF Leodegar Tenga

0
0
 Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akimkabidhi zawadi Rais wa CAF, Issa Hayatou Makao Makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga Makao Makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.
---
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemwahidi ushirikiano Rais waShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Ahadi hiyo imetolewa juzi (Februari 21 mwaka huu) makao makuu ya CAF jijini Cairo na Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou alipokutana na Rais Malinzi aliyekwenda kujitambulisha huko.
Utambulisho wa Rais Malinzi kwa Rais Hayatou uliongozwa na mtangulizi wake Leodegar Tenga ambaye aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia 2004 hadi 2013.
Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), alimweleza Rais Hayatou kuwa uchaguzi wa TFF ulikuwa mzuri.
Aliongeza kuwa alimkabidhi kijiti Rais Malinzi kwa maridhiano na ana imani na uongozi wake. 
Rais Hayatou alimpokea Rais Malinzi na kuahidi kuendelea kuipa Tanzania ushirikiano hasa katika maeneo ya utawala, ufundi na kuboresha miundombinu ya kuendeleza mpira wa miguu.
Kwa upande wake, Rais Malinzi alisema TFF itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa CAF ili kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania kinakuwa.

Baadaye mchana, Rais Malinzi alipata chakula cha mchana pamoja na wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live




Latest Images