Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 359 | 360 | (Page 361) | 362 | 363 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Hili ni gari...Chukulia hili gari kama usafiri wako katika kuendesha mahusiano yako na yule mweza umpendae. Humu ndani ya gari kuna familia yako yote na wewe ndiye dereva...Njia utakayochagua kulipitisha hili gari,ndio njia watakayopita familia yako
  Gari hili lina matairi yanayokaribia kugusa ardhi...ni kama unaendesha Lamboghini vile...Very delicate! Endesha gari lako katika Njia iliyonyooka,utakutana na mabonde na milima,lakini usipokwepa hivi na kuingia njia za uchochoroni usikojua kuna matope kiasi gani,basi hii milima na mabonde itapita na njia itaendelea kunyooka. 

  Baki Njia Kuu, Michepuko Sio Dili

  Epuka Ukimwi. 

  0 0


  Jumuiya ya Waislamu wa DMV (TAMCO) inapenda kuwakaribisha  wote kwenye  sherehe za MAULID .
   Sherehe za Maulid zitafanyika siku ya Jumapili 
  Hii tarehe 16 Februari 2014. 
  Claridge Local Park
   11901 Claridge Rd, Wheaton-Glenmont, MD 20902. 
  3:00 PM - 8:00PM
  WOTE MNAKARIBISHWA

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki wakati alipotembelea Banda la Kituo hicho kwenye Maonyesho ya Kongamano la Uwekezaji yaliyoanza jana kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (katikati) akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akibadilishana Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki mara baada ya kusainiana na wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,jijini Mwanza jana.Shughuli hii imefanyika wakati wa Muendelezo wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akizungumza wakati alipokutana na baadhi ya wawekezaji wenye leseni za TIC (hawapo picnani) ,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Jijini Mwanza jana.
  Mmoja wa Wawekezaji waliopo ndani ya Kanda ya Ziwa,akiwasilisha jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki. Picha Zote na Othman Michuzi, Mwanza.

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akiongea kuhusu mbinu za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, ambapo katika mkutano maalumu wa tatizo hilo leo huko Lancaster House jijini London, Uingereza leo, mependekeza kupigwa marufuku kwa biashara hiyo ulimwenguni kote ili kuua biashara hiyo.

  0 0

  Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43. 
   Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe  wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida. 
   Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria. 
   Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.
  "Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.
  Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.
  Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza.
  Katika mkutano huo amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.

  0 0

  Video kwa hisani ya CNN

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Jumbe Mangu akisisitiza jambo kwenye mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Chuo cha Taluma ya Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mkutano huo umebebwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Weledi katika Kutoa Huduma Bora Kwa Jamii”.
  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Paul Chagonja akisisitiza kwa Makamanda wa mikoa na Vikosi wa Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu hususani katika kushughulikia migogoro, kwenye mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  0 0

  Na Anna Nkinda – Maelezo

  Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)  umempongeza Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza leo Mjini Dodoma.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi ilisema uteuzi wa Rais umezingatia umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.

  Mwingizi alisema uteuzi huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201 hii ikiwa ni wanawake 100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.

  Aidha katibu Mkuu huyo alilitakia heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuzingatia maoni ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania yenye kulinda, kutetea  na kusimamia maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

  0 0

  Mwelimishaji wa masuala ya lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe,Bi. Sara Luzangi akiongea na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Babati mkoani Manyara juu ya umuhimu wa matumizi ya vyakula vilivyowekwa virutubishi katika kampeni za kutoa elimu hiyo zinazoendelea katika wilaya mbalimbali za hapa nchini.
  Waendeshaji wa kampeni ya kuongeza virutubishi katika chakula kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Chakula wakiendesha kampeni ya umuhimu wa virutubishi kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani humo leo.
  Waendesha kampeni wakitoa elimu ya wanafunzi wa njia ya kutoa burudani katika kampeni zinazoendelea mkoani Manyara.

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi (Kushoto) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi Mramba wakati wa Halfa ya kupokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 itakayokwenda kufungwa Kinyerezi ambapo mitambo hiyo itaanza kufanya kazi mwezi wa kumi mwaka huu.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi akishuka kutoka juu ya meli wakati wa Hafla ya kupokea mitambo miwili ya kuzalishia umeme thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 kutoka kwenye Kampuni ya General Electronics ya Marekani inayokwenda kufungwa Kinyerezi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Moja ya mitambo ya kuzalishia umeme ikipakiwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda Kinyerezi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa Tatu na kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) ambapo mitambo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi. (Picha zote na Benjamin Sawe wa Maelezo).

  0 0

  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Serikali zipatazo 851 zilizopo katika eneo la Mabwepande, Kinondoni,jijini Dar es Salaam zinazosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Huu ni muendelezo na mikakati ya Wizara ya Ujenzi ya kuwajengea na kuwauzia watumishi wa Serikali nyumba kwa bei nafuu.
  Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka Bw. Mwakalinga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania.
  Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi huo.
  Sehemu ya nyumba hizo.

  0 0

  Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti ya sh.bilioni 121 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.


  Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Yusuph Mwenda alisema fedha hizo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya mapato , pesa kutoka ruzuku serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo ya ndani ya Halmashauri .Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa kujiendesha kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa ikijiendesha kwa asilimia 20 tu.

  Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo la kutekeleza mipango ya maendeleo na kuwaondolea umaskini wakazi wa kinondoni na kuboresha maisha yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Chief Promotion Amoni Mkoga (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam 18 Februari-214 kuhusina na maandalizi ya semina ya hatimilki kwa wasanii wa bongo movi itakayofanyika katika ukumbi wa Vijana kinonondoni 21-Februari 2014 (katikati), Mwenyekiti wa Bongo Movi, Steven Mengeze (kushoto), Meneja Msaidizi Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Matilda Nyallu.
  Mwenyekiti wa Bongo Movi, Steven Mengeze akifafanua jambo kwenye mkutano huo.

  0 0

  TMEA Tanzania Country Director, Paulina Elago shaking hands with TANGO Executive Director Mr. Ngunga Tepani during signing of Tshs 153 Million grant agreement.

  TradeMark East Africa (TMEA) has today signed a 153 million Tanzanian Shillings grant agreement with the Tanzania Association of Non-Governmental Organizations (TANGO) to scale up the participation of citizens in EAC integration processes. The project seeks to empower civil society actors in Tanzania with knowledge/evidence and skills to be able to engage and gain the benefits of regional integration. 

  TANGO is the focal point for the Tanzanian civil society organizations in the EAC processes. This support will strengthen the organisation’s capacity by empowering organized civil society in Tanzania in their work of advocating for policy changes.


  0 0

  NIC Bank Tanzania will benefit from Tzs 8.5 Billion of additional capital from the Bank’s shareholders. The funds will be disseminated in two tranches of Tzs 5.8B with the injection of additional capital from NIC Bank Kenya already done in December 2013, with the Tzs 2.7B balance from the other local shareholders of NIC Bank Tanzania expected within a period of 6 months but no later than June 2014.


  “A growing financial need in this market has required that NIC Bank Tanzania further grow its’ competitive position. The capital will be used to fund the Bank’s business plan in the coming year with the aim of growing our market share with a focus on Corporate and SME lending, “said Mr. Pankaj Kansara – NIC Bank Tanzania MD.

  NIC Tanzania is banking on the emerging opportunities inasset finance, trade finance and infrastructure project financing to increase its’ market share, driven by  an improved business framework that has helped attract foreign direct investments and spur SME growth.

  “The capital-injection scheme is an appropriate, necessary and proportionate means of stabilizing the institution and will also enable us increase lending to the Tanzanian market across the Corporate and SME segments” added Mr. Kansara.

  “This additional capital will partly finance the growth of theanticipated loan book for 2014 and is expected to cushion the bank’s undertaking in respect to its Non-Performing Loan book” explained Mr. Kansara.

  NIC Bank Tanzania has grown its balance sheet from Tzs 30 Billion in 2009 to Tzs 180 Billion in 2013, representing an annualized growth of 43 %.

  “Looking at the success of our parent company, we hope to leverage on these strengths and replicate the product offering in the Tanzania market where applicable, while  exploiting the available resources at the Group level to develop even more targeted products to grow our presence,”said Mr. Kansara.

  “We are pleased by the demonstration of confidence by the Bank’s shareholders through their decision to inject additional capital,” added Mr. Kansara.

  “The shareholders remain committed to the bank’s operations in Tanzania and see growth opportunities arising from the integration of the East African Community. This capital injection will support our operations, taking into provision the bank’s Non-Performing Loan book,” concluded Mr. Kansara.

  In 2013, NIC Bank Tanzania undertook a very successful rights issue of Tzs8.5 billion with the parent company increasing its shareholding to68.97%.

  The Bank operates on a fully integrated system, offering a seamless cross border platform and in support of Corporates operating within the East Africa Community lock.


  NIC Bank Tanzania currently has branches in Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and Kahama.

  In November last year, NIC Bank Tanzania moved its headquarters to Ohio Street and opened an additional branch at the same location.

  NIC Bank Tanzania is a subsidiary of Nairobi Securities Exchange (NSE) listed NIC Bank holding which owns majority stake following the acquisition of the Savings & Finance Commercial Bank Limited in 2009.


  NIC Bank’s acquisition of majority interest in Savings & Finance Commercial Bank (S&F) was the Bank’s first cross-border acquisition, underlining the bank’s growth and expansion strategy in the region.


  0 0

  Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Jimbo la Flanders la Ubelgiji Mhe. Kris Peeters akisalimiana na Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala. Balozi Kamala amemtembelea Mhe. Kris Peeters leo ofisini kwake Brussels.

  0 0older | 1 | .... | 359 | 360 | (Page 361) | 362 | 363 | .... | 3353 | newer