Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 358 | 359 | (Page 360) | 361 | 362 | .... | 3348 | newer

  0 0

  URGENT MASJID  APPEAL
  MADRASATUL  AQSAA COVENTRY (Reg Charity No 1148412) 
  We humbly appeal to All Islamic Organisation and Muslims for kind and argent financial support to purchase building for Masjid and Madrasah.
  The purchase price of the building is £300,000. We have only six months to pay this sum
  You can donate by:
  1- Making a Standing Order will ensure you donate a regular amount to this noble cause.
  2- Sending us a cheque made payable to Madrasatul Aqsaa
  3- Making a refundable goodly LOAN (Qardhan Hassanah) to the Madrasah
  Bank detail  
  Hsbc , A/c #14062833, Sort Code 40-18-17, IBAN: GB75MIDL40181714062833
  Post your Cheque(Payable to Madrasatul Aqsaa) or postal order to Madrasatul Aqsaa, 188 Eagle Street, Coventry, CV1 4GQ.
  If you would like to speak to someone about the project, please telephone us (Sheikh Dawood: 07882442699/ ust Ali: 07767241499 / Ust Yakoub: 07800526992 and we will be please to discuss further over the phone.
  Jazaka Allahu Khayran for your Support.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akifanya mahojiano na Mwandishi wa Gazeti la The Independent la Nchini Uingereza kuhusiana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akimtambulisha Mshauri wa Masuala ya Vyombo vya Habari nchini Uingereza Bw. David Tarsh (kulia) kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe jijini London, Uingereza wanakohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Biashara Haramu ya Wanyamapori.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Daily Mail la Uingereza Bw. Guy Zitter (kati) na Mhariri wa Gazeti la Mail on Sunday Bw. Geordie Greig (kulia) alipotembelea Ofisi za Gazeti la Daily Mail jijini London, Uingereza kuelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akihojiwa na Mtangazaji wa Idhaa ya  BBC News Day Bola Mosuro katika Studio za BBC World Service jijini London, Uingereza anakohudhuria Mkutano wa Biashara Haramu ya Wanyamapori ambapo alipata fursa ya kuelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini. Picha zote na Pascal Shelutete, TANAPA. 
  Habari kamili soma hapo chini.

  0 0
 • 02/13/14--12:30: Article 0


 • 0 0
 • 02/13/14--07:16: ngoma mpya ya P-Square

 • 0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzamnia Bw.Marcel ESCURE alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
  / Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana   na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzamnia Bw.Marcel ESCURE alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo

  0 0

   
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Fadhili  Manongi  na  Mkurugenzi Msaidizi wa  Mamlaka ya Usafiri wa  Anga wa China (CAAC)Li Jian  wapili kutoka (kulia) wakisaini mkataba wa  ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo  Ndege zinazotengenezwa nchini China  zitaruhusiwa  kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha   Mamlaka hiyo hapa nchini  kuweza  kujenga  kwa wataalam kuweza kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China. Kutoka Kushoto ni Mwanashereia wa TCAA  Vallery Chamulungu na  Kulia ni  Executive Vice President of  Aviation Industry Corporation of China (AVIC)   Mr. Geng Runguang.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Fadhili  Manongi na   Mkurugenzi Msaidizi wa  Mamlaka ya Usafiri wa  Anga wa China (CAAC)Li Jian   (kulia) wakikabidhiana hati  za mkataba wa  ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo  Ndege zinazotengenezwa nchini China  zitaruhusiwa  kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa leo katika  katika Makao makuu ya ofisi hiyo  jijinia Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Fadhili  Manongi  akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (hawapo pichani) juu mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo  Ndege zinazotengenezwa nchini China  zitaruhusiwa  kutua katika Anga ya Tanzania. Pia Mkataba huo  utawawezesha   wataalam  wa TCAA uwezo wa  kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China. Kulia ni  Mkurugenzi Msaidizi wa  Mamlaka ya Usafiri wa  Anga wa China (CAAC)Li Jian. 
   Baadhi ya wajumbe Kutoka nchini China waliohudhuria  hafla ya utiliwaji  mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo  Ndege zinazotengenezwa nchini China  zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha wataalam wa TCAA kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China.
  Viongozi wa kuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  China (CAAC) wakiwa katika Picha ya Pomoja baada ya kusaini mkataba wa Ushirikiano wa maswala ya usafiri wa anga ambapo ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutuoa katika anga la Tanzania .

  0 0

   Egypt3138710-7
   Cape Verde Islands3527-884
   South Africa5464108-10
   Mali4059195-19
   Zimbabwe105100-552
   Cameroon5046-440
   Tunisia444514-1
   Botswana9794-330
   Chad165162-330
   Sierra Leone7673-33-1
   Uganda8784-33-1
   Benin9997-220
   Central African Republic107105-22-1
   Gambia139137-22-8
   Liberia9896-220
   Malawi117115-220
   Rwanda13113432-3
   Senegal6866-22-2
   Tanzania118116-222

  KUONA CHANZO NA JEDWALI LOTE LA NCHI ZA AFRIKA BOFYA HAPA

  0 0

  Siku za karibuni nimekua nikipita Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Mlandizi. Huu ni umbali wa kama 50Km hivi. Ajabu katika umbali huu kuna polisi wa usalama barabarani wengi sana kiasi cha kufanya barabara hii ionekane kama ni ya kuogofya au kuna ukaguzi maalum au operation tokomeza madereva wabovu. Hata hivyo, sijasikia kabisa uwepo wa operation hii, labda kama inafanyika kiintelejensia zaidi na kwa mwaka mzima.
  Katika kushangaa wingi wa askari hawa, nilimekua nikihesabu makundi ya askari wa usalama barabarani ambayo yanafika zaidi ya nane (hii ni kutoa walioko mizani Kibaha). Kuna sehemu ya kipande cha umbali wa kama 5km unapotokea Kongowe kwenda Mlandizi, kunakua na polisi makundi hadi manne walioko umbali wa chini ya 2km kutoka kundi moja hadi jingine.

  Vituo hivi wanaposimama polisi, kuna askari zaidi ya wawili na kuna kundi  linakua na askari hadi sita. Kwa hali hii unaweza kujikuta unasimamishwa kila baada ya 2km au 5km na kila unaposimamishwa wote wanauliza mambo yaleyale; wanakutaka uoneshe leseni yako, kadi ya gari, fire extinguisher, kukagua bima na road license. Kibaya zaidi ni kuwa hakuna uratibu au mawasiliano yanayoweza kukufanya ukikaguliwa kituo hiki usikaguliwe kinachofuata. Hivyo unaweza kunajikuta unasimamishwa na kuulizwa mambo yaleyale na kukaguliwa vitu vilevile kila baada ya umbali mdogo sana.

  Mazingira ya barabara hii na wingi wa magari haviruhusu sana dereva kukimbiza gari kwa mwendo wa kutisha. Lakini kuna makundi kadhaa ya askari hawa wenye tochi za kupima mwendokasi na wanafanya hivi kwa kujificha au kuvizia.

  Kwa mtazamo wangu, huu mpangilio au matumizi ya askari unahitaji kutizamwa upya kwa sababu zifuatazo:

  1.    Moja; ninaona kama haya ni matumizi mabaya ya nguvu kazi na rasilimali watu. Kuweka kundi kubwa namna hili la askari wa usalama katika umbali mdogo kiasi hiki ni kutumia rasilimali watu vibaya. Ni gharama kubwa sana kuajiri watu na kisha kukawa hakuna kazi ya kutosha kufanya na kufanya kazi ya mtu mmoja kuwa ya watu kumi.

  2.    Mbili; Askari hawa wanatumika kwa wingi hivi sehemu moja wakati ni kweli kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa ulinzi na usalama kwenye maeneo mengi wanayoishi raia. Ninadhani ndugu zetu hawa wangeweza kutusaidia usalama maeneo mengi mengine na tukawa na jamii ambayo iko salama na amani zaidi ya ilivyo sasa

  3.    Tatu: Ninaona kama huku ni kutesa raia na waendesha magari pale ambapo gari linasimamishwa kila baada ya muda na umbali mfupi na kuulizwa maswali yaleyale na kukaguliwa vitu vilevile. Katika kupita njia hii na kusimamishwa kwenye umbali usiozidi 2km, niilimuuliza askari mmoja ni kwa nini wana utaratibu mbaya hivyo; naye akakiri kuwa ni mfumo mbaya na anaomba tushauri njia mbadala.

  4.    Nne, kwa mtazamo wangu, hali hii inachelewesha sana maendeleo na kuongeza umaskini kwa nchi yetu. Tayari tuna tatizo kubwa la matumizi ya muda ambalo linachangia sana umaskini katika nchi yetu. Kulazimishwa kupoteza muda zaidi bararabara kwa mambo yasiyo na tija  ni kushindwa kuthamini matumizi sahihi ya muda kama kiungo muhim sana cha maendeleo binafsi, familia, jamii na taifa

  5.    Tano; Askari wengi hawana haraka na hawaogopi kukupotezea muda wapendavyo. Unaweza kusimamishwa ukiwa na kila kinachotakiwa na bado ukajikuta unapotezewa muda tu na mara nyingine kuambiwa unapelekwa kituoni kwa jambo ambalo halina ulazima huo. Wengi wa askari hawa wanashikwa na hasira wanapokukuta huna kosa.


  Ushauri kwa Jeshi la Polisi:

  1.    Jeshi la polisi na seriakli kwa ujumla, liwekeze zaidi katika kutoa elimu sahihi ya usalama  barabarani ikiwa ni pamoja na kudhibiti upatikanaji wa leseni bila mafunzo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa barabara wana elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu matumizi ya barabara na hivyo kuondoa ulazima wa kutumia nguvu kubwa kusimamia sheria


  2.    Jeshi la polisi wajisikie vibaya kujenga kizazi na jamii inayotii sheria kwa woga na shuruti na badala yake ifurahie kuwa na jamii inayotii sheria kw akupenda. Kwa minajili hiyo, isiwekeze sana katika kutoa adhabu na kuvizia makosa ya kuadhibu, bali wawekeze katika kuelimisha, kuelekeza na kuongoza.


  3.    Kuna haja ya ungozi wa jeshi la polisi kushirikiana na wataalamu wa fani zingine kama ICT kuangalia namna nzuri, rahisi, ya kisasa na yenye gharama nafuu katika kufanya ukaguzi wa kawaida wa magari barabarani. Kwa mfano, kwa magari yanayokwenda mikoani (hasa madogo) kunaweza kuwekwa utaratibu kuwa, likashakaguliwa mambo ya msingi katika kituo cha kwanza (mfano kikawa baada ya mbezi mwisho), kunakua na alama inayoonesha gari na dereva wana vigezo vya kutembea njia kuu bila ukaguzi hadi mwisho wa safari; isipokua tu iwapo atatenda kosa. Hili linawezekana kabisa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha askari wa vituo vingine kuhakiki (validate) ukaguzi husika.


  4.    Pamoja na unyeti wa kazi za walinzi hawa wa usalama wetu, ni vema wakatambua umuhimu na unyeti wa muda katika kulitoa taifa letu hapa lilipo. Ni shida kidogo unapokwenda umbali wa 50km na kutumia masaa kadhaa kwa sababu tu ya ukaguzi wa kila hatua chache au kwa sababu askari fulani alijisikia vizuri kukuonesha mamalaka yake kwa kukuweka barabarani muda mrefu au kukupeleka kituoni bila kosa


  5.    Polisi wetu watambue kuwa karne ya watu kujazana Dar es Salaam imepitwa na wakati. Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa baadhi ya watu wanaweza kufanya kazi au shughuli zao za kipato DSM na wakaishi nje ya mji kama vile Kibaha, Mlandizi, Ruvu, Bagamoyo, Msata Chalinze na hata Morogoro. Hii inasaidia kupunguza msongamano ndani ya mji na kuwawezesha watu kufanya shughuli zingine za uzalishaji hasa kilimo ambacho ni ngumu kufanya hapa mjini. Kwa mfumo wa kupotezeana muda barabarani ulioko sasa, hili haliwezekani; sio kwa vile maeneo haya ni mbali sana au kuna foleni; bali ni kwa sababu ya ukaguzi wa polisi ambao ungeweza kuboreshwa na kuokoa muda.


  6.    Jeshi la polisi lishirikiane na wataalamu wengine nje ya jeshi lao kuona namna ambavyo watasimamia sheria na taratibu za barabarani kwa rasilimali watu ndogo (askari wachache) na bado wakafanikisha majukumu yao kwa ufanisi mkubwa. Hii haitaondoa tu usumbufu na matumizi mabaya ya rasilimali watu na muda, bali itapunguza hata shutuma na rushwa zinazohusishwa sana na askari hawa (bila kujali ni za kweli au uongo)


  Mwalimu MM

  UDSM

  0 0

  The Love & Dine Valentine Dinner by Mikono Speakers at Peacock Hotel is nothing like your average Valentine dinner. This event goes beyond just providing you with a sumptuous dinner and live entertainment. 
  You will get food for the soul from renowned relationship counsellors who will unveil a wonderful surprise for empowering your relationships. Plus, a grand raffle draw where you can win a special Valentine present for you and your  other half.
  Get your ticket today. Call 0717 109 362 or 0784 636 169.


  0 0

   Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
   Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo ambaye ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,akizungumza na washiriki wa Kongamano hilo (hawapo pichani) wakati ufunguzi wake uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
  Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kuzungumza na Washiriki wa Kongamano hilo,jijini Mwanza leo.
  Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Mh. Thamduycse Chilliza (katikati) akifuatilia Kongamano hilo sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Julieth Kairuki (kushoto).Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Afrika Kusini,Terry Govender.


  0 0  0 0

  Shirikisho la Soka Dunia (FIFA), limemruhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi kuichezea Yanga. Barua ya Fifa iliyotua ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilisema kuwa suala la malipo ya Simba kwa Etoile du Sahel hayausiani na Emmanuel Okwi kucheza mpira. 
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kuwa taarifa hiyo ya Fifa imemruhusu mshambuliaji huyo acheze mpira iwapo ametimiza vigezo vyote vya usajili ikiwemo ITC. 
  "FIFA  wametuletea taarifa leo saa nne asubuhi na wametaka Okwi aruhusiwe kucheza mpira kama anakidhi vigezo vyote, sasa vigezo ni pamoja na ITC na ITC Okwi anayo, hivyo ni ruksa kucheza mpira."alisema 
  Simba ilimuwekea pingamizi FIFA  mshambuliaji huyo raia wa Uganda asicheze Yanga, kwa kuwasilisha pingamizi hilo mwaka jana ikiwa imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo Fifa iliirudisha kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuomba itafsiriwe kwa lugha ya Kingereza ili waweze kuielewa kwa ufasaha. 
  "Sisi tulimzuia kwa sababu Simba wamemuwekea pingamizi Okwi asicheze Yanga, ndio maana tulimsimamisha. Usajili wake CAF upo cleared kabisa hauna matatizo yoyote, CAF haijatoa leseni yake kwa vile wanasubiri Fifa itoe hukumu, imehofia isije ikatoa leseni alafu ikajikuta inaingia kwenye mkanganyiko na FIFA." alisema 
   Hata hivyo hukumu hiyo ya Fifa ni njia nyeupe kwa Okwi kuichezea Yanga kwenye michuano ya kimataifa ikiwemo mchezo wao dhidi ya Ahl Haly ya Misri. Awali, Okwi aliyekuwa mchezaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia, aligoma kuwachezea Waarabu hao baada ya kushindwa kuheshimu makubaliano ya kimkataba, na baada ya mgomo uliochukua miezi kadhaa SC Villa ambayo ndiyo iliyomkuza Okwi kabla ya kumuuza Simba, iliomba Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumruhusu arudi Uganda ili asipoteze kiwango chake. 
  Licha ya Fifa kutoa hati ya uhamisho (ITC) kuiruhusu SC Villa kumtumia, baadaye majogoo hao wa Uganda walimuuza kwa Yanga jambo ambalo limezua kesi. 
  Baada ya kusajiliwa kwa Okwi Yanga, Simba kupitia mwenyekiti wake Ismail Aden Rage, walipinga usajili huo wakidai haujafuata sheria kutokana na nyota huyo kuwa katika kesi dhidi ya Etoile. 
  TFF ilibaini utata katika usajili wa Okwi, na baada ya kupitia makubaliano ya Fifa na Villa iliona hakuna jibu la moja kwa moja kutoka Fifa ambalo lingewaruhusu Villa kumuuza Okwi katika klabu nyingine yoyote kwavile aliruhusiwa kwenda SC Villa kwa kibali maalumu.

  0 0


   Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
   Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
   Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
   Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
  Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.

  Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. 
  Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
   Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali.
  Ambao hawakufika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiashiria jambo wakati wa akiufunga mkutano wa Tafakuri na maridhiano  katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania katika ukumbi wa White sand jijini  Dar es Salaam,uliowashirikisha wanasiasa,Mashirika ya Kijamii na Viongozi wa Dini mbali mbali nchini
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili  kuhusu tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiufunga mkutano  uliowashirikisha watu mbali mbali wakiwemo  Wanasiasa,Viongozi wa Dini na Mashirika  ya Kijamii Nchini
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi  katika Hoteli ya Whitesand Jijini Dar es Salaam,kuufunga mkutano wa siku mbili wa  Tafakuri na maridhiano katika  kuelekea Katiba mpya ya Tanzania leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia  Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Mbatia  baada ya kuufunga mkutano wa siku mbili wa Tafakuri na Maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania,Ukumbi wa Whitesand Jijini Dar es Salaam leo jioni. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.

  0 0

   Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakiwa na wenyeji wao mara baada ya kuwasili katika  Bunge la India (Lokh Sabha) wajumbe wa kamati hiyo wametembelea leo huko New Delhi, India
   Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe Anna Abdallah akisaini katika kitabu cha wageni wa Bunge la India (Lokh Sabha) ambalo yeye na wajumbe wa kamati hiyo wametembelea leo huko New Delhi, India
   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa ziarani India
   Kikao cha pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Lokh Sabha

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe Anna Abdallah  na Naibu Mwenyekiti nMhe. Dkt Muhammad Seif Khatib na mwenyeji wao Mhe. Rasheed

  Kikao kikiendelea

  0 0


   Taswira mbalimbali za watu wa mataifa mbalimbali walioandamana kuashiria uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara mwaka huu Ngome Kongwe, Zanzibar. Kwa muda wa wiki nzima tamasha hilo litarindima ambapo watu na makundi ya muziki toka kila pembe ya dunia yatatumbuiza

  0 0

  Joseph Msami katika mahojiano na Balozi Manongi
  ''Bila kujumuisha wanawake hakuna maendeleo na radio inawezesha jukumu hilo"amesema Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa balozi Tuvako Manongi wakati wa mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii kuhusu umuhimu wa siku ya radio duniani February 13 kila mwaka.
  Balozi Manongi ambaye nchi yake itaongoza mjadala hapa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku hiyo yenye kauli mbiu ya uwezeshaji wa kijinsia anaanza kwa kueleza kwanini Tanzania imeteuliwa kuwa kinara katika mjadala huo ambao utafanyika katika atarehe ya baadaye.
  (MAHOJIANO)
  Kusikiliza bofya hapa

  0 0

  DSCF2699Kaimu kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya mapato Tanzania Rished Bade akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha kuhusu mgomo wa wafanyabiashara hapa Nchini
  DSCF2695Waandishi wa habari wakiwa kazini
  DSCF2697Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo
  DSCF2713Mr.Jangala ambaye ni Ajenti wa usafirishaji wa magari ya mikoani akilalamikia hali ya wafanyabiashara kugoma ambapo anadai kuwa imemuathiri kwa kiasi kikubwa kukosa abiria wanaokuja kununua bidhaa za jumla
  DSCF2700
  DSCF2706Shughuli mbalimbali zilidorora hata zile za M-pesa
  DSCF2711Hapa maduka yakiwa yamefungwa kama inavyoonekana katika picha eneo la maduka ya stendi mabasi yaendayo Moshi
  DSCF2712
  DSCF2708Muonekano katika stendi kubwa ya mabasi baada ya mgomo wa wafanyabiashara

  Na Pamela Mollel,Arusha
  Wafanyabiashara hapa nchi wametakiwa kutoendeleza mgomo  wa mashine za kieletroniki za EFD’S na badala yake wafungue maduka na kuendelea na biashara zao kwa kutumia mashine  kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza masharti ya kufanyabiashara.

  Rai hiyo aliitoa jana Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania Rished Bade wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha ambapo alisema kuwa kitendo cha kutumia mashine kwa wafanyabiashara itawawezesha kuweka  kumbukumbu sahihi.

  Alisema kuwa kodi ya ongezeko la dhamani ilikuwa kwenye awamu ya kwanza hivyo  awamu ya pili wafanyabiashara hawatahusika kulipa kodi kama wengine wanavyodai
  “siyo kweli kwamba wakitumia mashine watafilisika bali watakuwa na kumbukumbu sahihi…na kuna watu wachache wanapotosha wafanyabiashara kwa hili” alisema Bade.

  Aidha aliwataka wafanyabiashara kutokubali kutumika na wasiowafanyabiashara ambao wamekuwa  wakiwashawishi kufunga maduka ili kushinikiza serikali bali wawaripoti katika mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (wa pili kushoto) akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh. Aggrey Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akibadilishana Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki mara baada ya kusainiana na wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,jijini Mwanza leo.Shughuli hii imefanyika wakati wa Muendelezo wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kwa siku tatu mfululizo jijini humo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akizungumza na baadhi ya wawekezaji wenye leseni za TIC (hawapo pichani),wakati wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Jijini Mwanza leo.
  Mmoja wa Wawekezaji waliopo ndani ya Kanda ya Ziwa,akiwasilisha jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (aliesimama mbele).

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi na Mkurugenzi Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China (CAAC)Li Jian wapili kutoka (kulia) wakisaini mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha Mamlaka hiyo hapa nchini kuweza kujenga kwa wataalam kuweza kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China. Kutoka Kushoto ni Mwanashereia wa TCAA Vallery Chamulungu na Kulia ni Executive Vice President of Aviation Industry Corporation of China (AVIC) Mr. Geng Runguang.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi na Mkurugenzi Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China (CAAC)Li Jian (kulia) wakikabidhiana hati za mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa leo katika katika Makao makuu ya ofisi hiyo jijinia Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe Kutoka nchini China waliohudhuria hafla ya utiliwaji mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha wataalam wa TCAA kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China.
  Viongozi wa kuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga China (CAAC) wakiwa katika Picha ya Pomoja baada ya kusaini mkataba wa Ushirikiano wa maswala ya usafiri wa anga ambapo ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutuoa katika anga la Tanzania.

older | 1 | .... | 358 | 359 | (Page 360) | 361 | 362 | .... | 3348 | newer