Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

Article 13


NMB YAFUNGUA RASMI TAWI LA HIMO, MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe.Dkt. Ibrahimu Msengi (kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Himo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo akifuatiwa na  Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo,Mhe.Augustino Mrema wakishuhudia uzinduzi huo. Hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la NMB Himo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya tawi hilo mkoani Kilimanjaro.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa tawi jipya la NMB Himo

mambo ya gado

CCM YATOA SHUKRANI KWA WANANCHI KUIMWAGA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI ULIOFANYIKA JANA

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23. 


Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.

Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).

Apartments for sale at Mbezi Beach, Dar es Salaam.

$
0
0
Apartments at Mbezi Beach, Kinondoni, in  Dar es Salaam. 
Price per house : $300,000.00
 Each House has : 4 Self Contained Bedrooms
 First Floor: Living Room, Kitchen with Cabinets, Self Contained Guest Room 
Second Floor: One Big Self Contained Master Bed room and Two Self contained Rooms
Contacts: +255 784 782578, +255 652 386706 Email:range_charles@yahoo.com 
Name: Charles Isaroche Range


in everlasting memory

$
0
0
Mzee John Harrison Simtaji


Today it is exactly 24-years since we said goodbye to our dearest Father, we shed lots of tears and we were confused. We thank God for wonderful years we spent with our dad; we laughed and joked together… what a wonderful father...

Our father worked so hard and today we remember him and appreciate everything he did for us.

You will always be in our hearts and you are remembered by your children Anna, Bahati, Kotto and Baraka. Grandchildren Emmanuel, Irene, Loveness P, Joshua, Kotto Jnr, Edward, John, Jairus and Jabar. Your Brothers and sisters, friends and other members of the family.

‘’...the Lord gave and the Lord has taken away may the name of the Lord be praised’’


Job 1:21

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE PATRICK QORRO LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.

Marehemu Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na hitilafu ya figo.Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa  aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu

Second bust by Australian navy in a week of a vessel with drugs off Tanzania coast

$
0
0
Crew members of HMAS Melbourne with seized drugs prior to
them being destroyed. Photo: ABIS JAYSON TUFREY

The Australian Associated Press reports that on Friday, Australian warship HMAS Melbourne made another multimillion dollar drug bust on the high seas off Tanzania, the second in a week following the seizure and destruction of 385 kilogrammes of heroin from a vessel in the same area on February 5th, 2014.


The two big drug hauls are estimated to be worth more than A$1 billion in a street value.


In October, the ship disrupted a pirate gang off Somalia and then made three amphetamine busts, totalling 23.8 kilograms.


After testing, seized drugs are usually destroyed by dumping them overboard.


KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA

$
0
0
 Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo  Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi.
 Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akikagua paredi maalum lililoandaliwa kwa heshima yake katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es salaam.
 Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato.

TFF yatangaza ukaguzi wa katiba za wanachama wake

EAC Directors give evidence in Court over a former employee case

SERIKALI INA NIA NA BWAWA LA KIDUNDA - NAIBU WAZIRI WA MAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, amesema Serikali ina nia na bwawa la Kidunda na watahakikisha wanautekeleza mradi huo kama ilivyopanga.

Mhe. Makalla amezungumza hayo jana wakati alipotembelea kijiji cha Bwira Chini ambacho pamoja na Bwira Juu ni moja ya vijiji vitakavyopisha ujenzi wa bwawa hilo kubwa, kuongea na wananchi ambao wamekua katika hali ya sintofahamu kuhusu utaratibu wa kuhama katika makazi yao kwa ajili ya kupisha ujenzi huo.

“Serikali ina nia na bwawa la Kidunda, ila yapo mapungufu katika kutekeleza mradi huu na kama Serikali tunazipokea changamoto hizi na tutazifanyia kazi. Nitahakikisha hatua sahihi zinachukuliwa ili utekelezaji wa kazi hii uanze”, alisema Naibu Waziri.

“Naagiza DAWASA na Halmashauri ya Wilaya walitafutie ufumbuzi suala hili na watoe tamko baada ya siku kumi na nne na ninaomba wananchi waelewe Wizara ya Maji ina taasisi kama DAWASA inazozielekeza kufanya kazi kwa niaba yake, hivyo naomba msivilaumu wala kutokubaliana na maamuzi yake, bali mviheshimu na kuvipa ushirikaiano wa kutosha ili vitekeleze majukumu yake vyema”, aliongeza Mhe. Makalla.

Pia, Naibu Waziri alisema atazungumza na Rais, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili Serikali itafute fedha za dharura ili kufanikisha mradi huo kama moja ya kutimiza sera na mipango yake iliyojiwekea.

Aidha, Mbunge wa Morogoro Kusini na Bwira Chini ikiwa ni moja ya kijiji kilichopo katika jimbo hilo, Innocent Kalogeris, aliyeambatana na Mhe. Makalla katika ziara hiyo alimshukuru Naibu Waziri wa Maji kufika na kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu.

“Nashukuru Mhe. Makalla kwa kufika na kuzungumza na wananchi wa Bwira Chini ili kupata suluhisho la ujenzi wa mradi huu wa Bwawa la Kidunda. Maombi yangu ni kuomba tathmini ya fidia kwa wananchi ifanyike kama ulivyoagaiza, ili wananchi wajue stahiki zao sahihi ili waweze kwenda kwenye maeneo mengine waliyopangiwa na kupisha mradi huu mkubwa na wenye manufaa mengi kwa nchi yetu kuanza”, alisema Mhe. Kalogeris.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji, pia alifuatana na Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki, Lucy Nkya, ambaye alikuwa akiwawakilisha wananchi wa Bwira Juu ambao nao pia wanatarajiwa kuhama kupisha ujenzi huo. Ujenzi wa Bwawa la Kidunda ni mradi mkubwa uliopangwa kujengwa mkoani Morogoro ili kuweza kutoa maji ya kutosha kuhudumia mkoa wa Dar es Salaam na kumaliza changamoto za maji zinazikumba jiji hilo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akisikiliza ripoti ya maji ya Wilaya ya Morogoro katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, kushoto ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris.
Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki, Lucy Nkya akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wilayani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji katika ziara yake wilayani hapo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Bwira Chini katika ziara yake kijijini hapo, kushoto ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Wakazi wa kijiji cha Bwira Chini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (hayupo pichani), wakati wa alipotembelea kijiji hicho katika ziara yake wilayani hapo.
Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bwira Chini katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika jimbo lake, wilayani Morogoro.

salma msangi's MusicXpress Interview With Shilole

MAANDALIZI YA BUNGE LA KATIBA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 11.02.2014.


The Most Special Valentine Dinner is just round the corner.

$
0
0
Great food, live entertainment, inspirational talk 
from relationship experts and so much more! 
 Grab your ticket NOW. 
Call 0717 109 362 or 0784 636 169 today

Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, Ikulu jijini dar leo

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

TIC Congratulates Regional Commissioners on their Efforts to Attract Investments into the Lake Zone

$
0
0
Tanzania Investment Centre (TIC) Executive Director, Juliet Kairuki, extended her congratulations to Regional Commissioners belonging to the lake zone for their efforts to convene the first lake zone investment forum.

Speaking from Mwanza, she advised that The Regional Commissioners have created their own dedicated Secretariat to convene the investment forum which will occur from 13-15th February 2014.

The regions covered in the lake zone are Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Kagera, and Mara. The forum will bring will bring together Government and investors to appreciate the investment opportunities that are available in the zone as well as the measures being taken by the regional authorities and related agencies to facilitate investments into the region.

Central to TIC's participation in the forum is its determination to work closely with Regional Commissioners officers to enable more efficient investor servicing in the regions. 

TIC and the Regional Commissioners have agreed to work together to fast track and streamline the process of identifying land for investment that can be placed in the TIC land back as well as to deliver education to communities and laws, rules, and procedures to be followed when engaging investors on land and other investment related matters.

TIC will also work with Regional Administrative Secretaries offices to build their capacity to facilitate investors more effectively. For more information on the investment forum and investment opportunities visit www.lakezoneinvestmentforum.go.tz

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI AKUTANA NA WADAU WA PSPF

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwakaribisha Maafisa kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) katika Mkutano na Watumishi wa Wizara hiyo kuhusu Mpango wa Uchangiaji wa Hiari uliofanyika leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kushoto akisalimiana Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi. Matilda Nyallu katika Mkutano wa Watumishi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi. Matilda Nyallu akitoa mada kwa Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu ya kujiunga na Mpango wa Uchangiaji kwa Hiara .Picha zote na Benjamin Sawe wa Wizara ya Habari.

SAFARI LAGER YATOA SOMO KWA WACHOMA NYAMA JIJINI MBEYA

$
0
0
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Uchomaji Nyama Bora ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Nyama Choma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Uchomaji Nyama Bora ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Uchomaji Nyama Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza jaji Mkuu ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama choma. Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Picha ya pamoja ya wachoma nyama mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo ya kuchoma nyama yaliyofanyika Airport Pub mkoani Mbeya jana.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images