Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

NHC kujenga Satelite City Jijini Arusha

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.

Eneo hilo la Tengeru ambalo zamani lilikuwa likimilikiwa na Hortculture Tanzania Ltd linatazamiwa kujengwa mji wa kisasa utakaojulikana kama Satelite City.

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa NHC Nehemea Mchechu aliwaambia wajumbe wa kamati ya ardhi ,amaliasili na mazingira kuwa tayari NHC imenunua ekari 600 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 5.

Nyumba 300 zinatarajiwa kujengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo kadharika kutajengwa maduka makubwa ,shule pamoja na vituo kwa ajili ya huduma kwa jamii na kwamba ujenzi wa nyumba nyingine 300 utafuati.

Mchechu alisema ujenzi huo hauta athili kwa namna yoyete ile uoto wa asili ikiwemo miti katika eneo hilo na kwamba wanataegemea kuacha sehemu ya Mikahawa iliyopo hapo kama kumbukumbu.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akisalimiana na mbunge wa jimbo la Arumeru Joshua Nassar wakati kamati ya bunge ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la hifadhi la taifa(TANAPA)Allan Kijazi alipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI WA HABARI AFUNGUA KONGAMANO LA 9 LA CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF) ARUSHA LEO

$
0
0
 
 Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akifuatilia hotuba mbalimbali katika ufunguzi wa Kongamano la 9 la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali Afrika  2014 (DBSF)ulioanza leo jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano kwa nchi za Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkomwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkomwa akizungumza.

BALOZI KAMALA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA ACP ANAYESIMAMIA UTAWALA NA FEDHA

$
0
0
Balozi wa Tanzania BELUX, Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific(ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa ACP anayesimamia Utawala na Fedha Bi. Nthisana Phillips ofisini kwake Brussels. Balozi Kamala anaendelea na ziara ya kukutana na watendaji wakuu wa ACP kwa nia ya kubainisha masuala ya kupewa kipaumbele na ACP katika kipindi cha miezi sita ijayo.

KAMATI KUU YATEUA MGOMBEA WA CCM KALENGA

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha kwa waandishi wa habari, mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa (kushoto), leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Nape amemtambulisha Godfrey ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. William Mgimwa, baada ya Kamati Kuu ya CCM kumpitisha, leo kuwania nafasi hiyo ya Ubunge. (Picha na Bashir Nkoromo).

MDAU KIZITO ASHINDA MILIONI 10 ZA 'CHAMPIONI MAHELA' AKIWA KWENYE DALADALA

$
0
0
BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye, mshindi wa milioni 10 amepatikana kupitia droo ya Shinda Mahela na Championi ambaye ni Kizito George Chuka.

Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao kwenye Viwanja vya Mbagala- Zakhem jana Jumanne.

Akizungumza Kizito ambaye ni makazi wa Kawe jijini Dar alipopigiwa simu na muendeshaji wa shughuli hiyo MC Chaku, mshindi huyo alikuwa ndani ya daladala hivyo hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kushukuru kwa kujinyakulia kitita hicho.

Kizito, 43 alionekana kufurahia kutokana na sauti yake kusikika akichekelea na haijafahamika kama aliwasilimulia abiria wenzake aliokuwa nao ndani ya daladala hiyo.

Hata hivyo keshokutwa Alhamisi anatakiwa kuja Ofisi za Global Publishers kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuchukua mkwanja wake huo.

“Nimefurahi sana lakini sasa hivi nipo ndani ya daladala naomba muda nikifika nitakupigia,” alisema Kizito.
Washindi wengine ambao walipatikana siku hiyo ni Athuman Yusuph, 40, mkazi wa Mwanza aliyejinyakulia shuka za kisasa na Amiri Kinguaba, 60 aliondoka na simu kali aina ya Samsung Galaxy.
MC Chaku (kushoto) akiwa na mmoja ya wakazi wa Mbagala tayari kwa kuchagua mshindi wa Championi Shinda Mahela.
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) na kulia ni Ofisa Masoko wa Shinyanga Emporium, Herman Bernard wakiendelea kufuatilia droo.

Maalim Seif atembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Afisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Ali Ussi, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu, Mkokotoni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea skuli ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya. (picha na Salmin Said, OMKR).

Mh. Lowassa na Mh. Warioba washiriki Ibada ya Kuaga Mwili wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro jijini dar leo

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsalimia Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (mstaafu), Jaji Joseph Warioba wakati walipokutana katika msiba wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro,Nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ada Estate,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Mzee Joseph Butiku wakati wakiwa kwenye msiba wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro,Nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ada Estate,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro,Nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ada Estate,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akibadilishana mawazi na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (mstaafu), Jaji Joseph Warioba wakati walipokuwa wakiondoka msibani,mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kuaga Mwili wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro,Nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ada Estate,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Prof. Issa Shivji wakati walipokutana kwenye msiba wa Mbunge wa Zamani wa Karatu,Marehemu Patrick Qorro,Nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ada Estate,Jijini Dar es salaam leo.

CONCEPT NOTE: Extending Social Security to the Excluded


TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR (ZBS) NA TASISI YA VIWANGO TANZANIA (TBS) ZAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya mashirikiano kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na la Zanzibar (ZBS) Bwa. Suleiman Masoud Makame akiitambulisha kamati ya watalamu yenye wajumbe nane wanne kutoka Bara na wane Zanzibar kwa Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika Mkutano uliofanyika Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akimkabidhi ripoti ya Kamati ya pamoja ya mashirikiano Mhe. Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika Mkutano uliofanyika Amani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi (alie simama) akizungumza katika Mkutano wa uzinduzi wa kamati ya mashirikiano ya (TBS) na (ZBS) kulia ni Mkurugenzi Mkuu ZBS Bwa. Khatib Mwalim na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Viwango TBS Bwa. Leandr Kinabo.
Baadhi ya watendaji wakuu wa tasisi mbili wakiskiliza nasaha za Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi (hayupo pichani) mara baada ya kuizindua Kamati yawatalamu katika Mkutano uliofanyika ofisi ya Viwango Amani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika picha ya pamoja na watenandaji wa Tasisi mbili zinazoshuhulikia ubora wa viwango Tanzania. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar).

Washindi Kilimanjaro Marathon 2014 kujipatia zaidi ya shilingi milioni 40

$
0
0
Zawadi za fedha taslimu kwa washindi wa Kilimanjaro Marathon 2014 zimeongezwa hadi zaidi ya shilingi milioni 40 na kuifanya mbio hii kuwa kati ya m io kubwa zaidi barani Afrika.

Waandaaji wa mbio hizo wametangaza kuwa washindi wa wa Kilimanjaro Marathon 2014 watajipatia zaidi ya shilingi milioni 40 fedha taslimu kama zawadi.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbali na washindi kujinyakulia zaidi ya shilingi milioni 40 pia watapata fursa ya kujishindia zawadi nyingine kabambe za kuvutia kutoka wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini shirikishi

Alisema washindi wa mbio ndefu za marathon ya kilomita 42 watajishindia jumla ya shilingi milioni 20, na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio za walemavu maarufu kama GAPCO 10km Marathon wakijishindia kiasi cha shilingi milioni 6. Washiriki wote watakaomaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run wataweza kujishindia zawadi mbalimbali.

Addison alisema kuwa mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.

Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.  Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.

Ili kuwapa hamasa wanariadha wa Tanzania kufanya vizuri katika mbio hizi, Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 2 bama bonsai kwa wanariadha Watanzania watakaovunja rekodi katika mbio hizi.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA OMAN KUHUSU ELIMU YA JUU

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi , Mhe, Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na Balozi wa OMan ndugu H.E. Saoud Ali Ruqqishi kuhusu ushirikiano baina ya Oman na Tanzania katika Elimu ya juu.

THREE DAY WEATHER FORECAST: WARNING OF LIKELIHOOD OF HEAVY RAINFALL, STRONG WINDS AND LARGE WAVES

Tahadhari ya hali ya hewa mbaya kuanzia leo hadi Alhamisi

PRESS STATEMENT ON CLAIMS BY THE SUNDAY MAIL NEWSPAPER

LOVE IS GONNA BE IN THE AIR @ Isumba Lounge on Valentine's day

$
0
0
JD's Entertainment inakwambia kama una mume au mke na unampenda sana, kama una girlfriend au boyfriend na mnapendana kweli na kama una rafiki na uko tayari kwa chochote juu yake na hata kama uko single lakini moyo wako umejaa mapenzi lakini hujui wapi pakuyapeleka. Basi karibu sana isumba lounge (jollies club). Wapendanao watazungumza, hadithi na safari za maisha yetu ya kimapenzi zitasikika;ni valentine hii ya tarehe 14/02/2014 pale pale isumba lounge zamani jollies. Kiingilio ni 10000, karibu tusherehekee mapenzi kwanii ....
LOVE IS GONNA BE IN THE AIR


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' aipiga jeki Uhuru Gym

$
0
0
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo kutoka kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago ,Mussa Sindano Vifaa na kocha wa GYM hiyo Mohamed Chipota 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo kwa Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Mohamed Chipota kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi katika eneo ilo na kuwapa moyo wa kuendelea na mazoezi wanaoshudia wengine wa pili kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago na Mussa Sindano Vifaa hivyo pamoja na Dvd vina thamani ya shilingi laki mbili 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika 
GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo baada ya kuwakabidhi vifaa vya mchezo huo kutoka kushoto ni Atanasi kibwe,Raymond Mbwago,kocha wa GYM hiyo 
Mohamed Chipota,Mussa Sindano na Omari Bai
-------------------------------
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ameipiga tafu 
GYM ya mchezo wa ngumi ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Dar es salaam kwa kuwapati vifaa vya mchezo huo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Super D alisema amevutiwa na uanzishwaji wa GYM hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kuwatoa mabondia wazuri kipindi kijacho. Aliongeza  kusema kuwa unajua hizi GYM za mtaani zipo chache sana na wana uhaba wa vifaa vya kufundishia hivyo "Mimi nimeamua kujitolea gloves mikono mitatu kwa kuanzia ili wapate moyo wa kuendelea na mazoezi pamoja na DVD za mafunzo maana ndio timu ambazo tunazitegemea kwa siku za usoni kutuletea mabondia wakali watakaoweza kutuletea medali na kutupa sifa nchi hii".

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Mohamed Chipota amesema vifaa hivi pamoja na DVD za mafunzo ya ngumi zimekuja wakati muhafaka kwa kuwa walikuwa na uhaba wa vifaa kama hivi.

"Hivyo tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutupa sapoti kama alivyofanya Super D yeye ni kocha wa Mkoa wa Kimichezo Ilala sasa hapa kama amewekeza mabondia wa ilala sasa watatokea hapa kwa siku za usoni.

"Tumeanza hivi karibuni lakini mategemeo yangu ni kuibua vipaji vyipya kabisa vya mchezo wa masumbwi nchini",alisema Chipota .

introducing 'Unanichora' first official record from Ben Pol in 2014.

Wash out at Mbuta along main trunk road Arusha-Dar es Salaam

$
0
0
Dear Issa, 
These are are photos taken at Mbuta (approximately  40kms after Same)following heavy rains yesterday which caused a heavy traffic jam. The road contractors, Dott Services, are now trying to repair the section. Small Saloon cars should proceed with caution. 
 Regards - mdau N Virji




BREAKING NEWS: Moto wazuka katika Stoo ya kuhifadhia vifaa ya chuo cha POLISI MOSHI

$
0
0
Wanafunzi wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo. Chanzo cha  moto huo bado kujulikana na hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye. 
Askari wanafunzi wakipambana na moto kwa kila jinsi
Mapambano na moto yanaendelea.
Kwa picha zaidi na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii

NMB AND TIGO PESA LAUNCH CASH DEPOSIT AND WITHDRAWAL SERVICE THROUGH MOBILE PHONE

$
0
0
Tigo and NMB, two leading Tanzanian commercial firms in telecoms and banking industries respectively, have today February 2, 2014 launched an innovative service that enables customers of both NMB bank and Tigo Pesa services to deposit and transfer funds from their Tigo Pesa wallet to their bank account and from their bank account to Tigo Pesa through mobile phone.
NMBAg. CEO and Chief Risk Officer, Tom Borghols(center) and Tigo Pesa Commercial Manager, Ruan Swanepoelsign a partnership contract which will enable NMB and Tigo customers to make any transaction from their NMB accounts to Tigo Pesa services and from their Tigo Pesa wallet to their bank account through a mobile phoneconveniently. Witnessing is NMB Head of Personal Banking, Abdulmajid Nsekela


The launch ceremony was held at a hotel in Dar es Salaam where the executives from both companies, Mr Ruan Swanepoel - Tigo Pesa Commercial Manager and Mr Tom Borghols- NMB Ag. CEO and Chief Risk Officer described the new service which integrates banking and mobile financial services as an innovation designed to improve the lives of customers of the two companies.



Mr. Tom Borghols said “This extended cash deposit and transfer channel will enable around 1,000,000 customers registered with NMB Mobile to utilise Tigo Pesa agents to deposit or transfer directly into their bank accounts wherever they are.”

NMBAg. CEO and Chief Risk Officer, Tom Borghols(left) and Tigo Pesa Commercial Manager, Ruan Swanepoelexchange contracts as a sign of partnership which will enable NMB customers to make any transaction from their NMB accounts to Tigo Pesa services and from their Tigo Pesa wallet to their bank account through a mobile phone conveniently.


There are more than 20,000 active Tigo Pesa agents countrywide according to the company Commercial Manager found in all parts of the country, Pemba and Zanzibar included.



Borghols said the new service represents “a partnership of strength” between Tigo and NMB noting that the art to do mobile money deposit and transfer service will significantly contribute to the social and economic wellbeing of Tanzanians in both urban and rural areas.

NMBAg. CEO and Chief Risk Officer, Tom Borghols (left)and Tigo Pesa Commercial Manager, Ruan Swanepoelshake hands afterthe official launch of NMB Tigo Pesa cash deposit and withdrawal service through a mobile phone. Looking on is NMB Head of Personal Banking, Abdulmajid Nsekela


On his part, the Tigo Pesa Commercial Manager said integration of mobile financial services with NMB banking services is part of the company’s goal “to provide access to banking and mobile financial services to as many Tanzanians as possible.”



Our plan is to integrate our mobile financial services with other sectors of the economy in the country so that at end the of day bank account holders will no longer need to go to a branch to deposit or withdraw funds, but do it directly from their Tigo Pesa wallet ,” Mr. Swanepoel said.

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images