Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

zawadi ya ushindi wa 5-1 kwa ankal

$
0
0
Mpenzi wa kufa wa Bwawa la Maini yupo Anfield hivi sasa na keshamwandalia Ankal zawadi nono kwa ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Arsenal jana. Asante mdau kwa zawadi bomba.
ANGALIZO: Hivi tunavyoongea Man U wameshikwa shati na Fulham baada ya kupigwa bao dakika ya 94 za majeruhi, na ngoma imemalizika kwa mabao 2-2.

USIKU WA DAYNA NYANGE TZ V/S CINDY SANYU WA UG NDANI YA LINAS NIGHT CLUB BUKOBA FEB 15,2014

$
0
0
FEB 15, 2014 Itakuwa ni usiku wa aina yake kwa wakazi wa mji wa Bukoba na maeneo ya jirani, Watakapo takiwa kujua nani mkali kati ya DAYNA NYANGE TZ V/S CINDY SANYU WA UGANDA.
Usiku huo hatuangalii Vivazi au  nani anamiliki nini,ama yupi ni hot zaidi ya mwenzake,tunaangalia kitu kimoja tu,Nani mkali wa kuimba na kucheza Jukwaani?

CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR CHAFANYA SHEREHE ZA MAHAFALI YA TANO

$
0
0
Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi. Zulekha Khamis Omar akitoa maelezo juu maendeleo ya Chuo katika Mahafali ya tano Chuoni hapo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Khamis Mussa Omar akieleza machache kuhusu muelekeo wa Chuo hicho na kumkaribisha Mgeni rasmin kutunuku vyeti kwa wahitimu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizunguza na wahitimu mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwatunuku vyeti na stashahada katika Mahafali ya tano Chuoni hapo, (kulia yake) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Khamis Mussa Omar na (kushoto) Kaimu Mwenyekiti Bi. Naila Jidawi.
Baadhi ya wahitimu wa Mapishi ya vyakula na Uokaji wakiwa wamesimama mara baada ya kutunukiwa vyeti na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk katika sherehe zilizofanyika Chuoni hapo.

vibweka vya bingwa wa masumbwi duniani, Muhammad Ali

TAI YATOA MAFUNZO KWA VITENDO JUU YA KUNAWA MIKONO NA KUSAFISHA KINYWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILIMANI JIJINI DAR

$
0
0
Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAI - Tanzania Aspiration Initiatives imefanya mafunzo ya kulinda afya kwa vitendo kwa wanafunzi Zaidi ya 200 wa Darasa la Kwanza, la pili na darasa la awali katika shule ya msingi Kilimani iliyopa Sinza Uzuri wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa miradi miwili inayojulikana kama Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi).

Miradi yote ina lengo kuu la kupambana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama Magonjwa ya tumbo na yale ya meno na kinywa yanayoathiri zaidi watoto. Mafunzo hayo pia yalishirikisha Vijana wengine kutoka nchini Denmark walio nchini katika ziara ya kimasomo chini ya Jukwaa la kimataifa la Global Platform.

Mikono Ming’avu (MiMi) ni mradi uliyojikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watoto wa shule za msingi kutatua tatizo la magonjwa yanayosababishwa na mikono michafu kama vile Pneumonia na homa ya Matumbo (Diarrhea). Mradi huu tayari umeshawafikia Zaidi ya watoto 1000 katika baadhi za shule za msingi jijini Dar es salaam huku malengo ni kufikia shule zote za msingi Tanzania nzima.

"Hatua hizi za TAI ni baada ya kuona Watanzaia wengi hawana tabia ya kunawa mikono na sabuni kwa ufasaha ambapo ni moja ya sababu inayochangia magonjwa yanayoweza kuzuilika, lakini pia yanaathiri ukuaji wa mtoto. Kila mwaka watoto Zaidi ya milioni 3.2 duniani walio chini ya miaka 5 wanakufa kwa sababu ya homa ya matumbo na pneumonia yakiwa ni magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto baada ya malaria hasa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania ikiwepo" alisema Bw. Gwamaka Mwaibuka, Katibu Mkuu wa TAI.

Kinywa Kisafi (KiKi) ni ni moja kati ya mradi ya TAI ukiwa na lengo la kupunguza tatizo la magonjwa ya Kinywa na meno kwa watoto ambapo taasisi hiyo hufanya mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalam kuwafundisha watoto njia sahihi za kufanya usafi wa meno na kinywa na kuhimiza tabia ya kusafisha kinywa kuanza tangu utotoni.

TAI ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha maisha ya kila mmoja katika jamii hasa watu wanaoushi katika mazingira magumu na umasikini kupitia sekta tano za Elimu, Afya, Ujasiriamali, Teknolojia ya Habari na Mazingira. Kwa taarifa Zaidi ingia www.tai.or.tz au Tufuate katika ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/tai2012.
Katibu Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration Initiatives - TAI Bw. Gwamaka Mwabuka akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Kilimani Juma Abdul jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi ili kuipeka magonjwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanafunzi toka Denmark waliopata mualiko na TAI kupitia taasisi ya Global Platform.
Wanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kilimani wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kusafishwa kinywa na kuepukana na magonjwa yanayotokana na kutosafisha kinywa.

Baadhi ya wanafunzi w shule ya awali ya Kilimani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waliowatembelea kuwafundisha swala zima la usafi shuleni hapo kupitia miradi ya Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi) chini ya Taasisi isiyo ya kiserekali ya Tanzania Aspiration Initiatives – TAI.

bongo dar es salaam tambarare....

profesa mwandosya atembelea rwanda

$
0
0
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe.Prof.Mark J.Mwandosya akizungumza na Mawaziri wa Rwanda.Kutoka kulia ni waziri ofisi ya Rais Mhe.Venantie Tugireyezo, Waziri wa mambo ya nje Mhe.Louise Mushikiwabo pamoja na kaimu balozi wa Tanzania nchini Rwanda Bw. Francis Mwaipaja.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe.Prof. Mark J.Mwandosya na ujumbe wake akizungumza na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda. Kutoka kushoto ni Kanali Ramadhan Mrangira(mwambata wa ulinzi), Bw.Francis Mwaipaja(kaimu balozi),Charles Masayanyika(mshauri wa siasa) na Felix Ngamlagoso(mkurugenzi wa uchumi -EWURA)

CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR CHAFANYA SHEREHE ZA MAHAFALI YA TANO

$
0
0
  Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi. Zulekha Khamis Omar akitoa maelezo juu maendeleo ya Chuo katika Mahafali ya tano Chuoni hapo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Khamis Mussa Omar akieleza machache kuhusu muelekeo wa Chuo hicho na kumkaribisha Mgeni rasmin kutunuku vyeti kwa wahitimu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizunguza na wahitimu mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwatunuku vyeti na stashahada katika Mahafali ya tano Chuoni hapo, (kulia yake) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Khamis Mussa Omar na (kushoto) Kaimu Mwenyekiti Bi. Naila Jidawi.
 Baadhi ya wahitimu wa Mapishi ya vyakula na Uokaji wakiwa wamesimama mara baada ya kutunukiwa vyeti na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk katika sherehe zilizofanyika Chuoni hapo. 
 Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika sherehe ya Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii  Maruhubi Zanzibar. 
 Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (hayupo pichani) ambae ni mgeni rasmin wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi Zanzibar. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akimpa zawadi ya mlango kwa niaba ya wanafunzi wa ICT & ACCOUNT, Maalim. Hassan Mrisho Haji katika sherehe ya Mahafali iliyofanyika Chuoni hapo.
Wapiga Picha nao wakiuza picha zao mara baada ya kumaliza kwa Mahafali chuoni hapo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

TASWIRA YA SHEREHE YA KUZALIWA CCM TAWI LA NEW YORK

$
0
0
Tawi la CCM New York walivyoshereheka miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho, Kulikuwa na  hotuba ya viongozi wa tawi na mgeni rasmi kutoka Tanzania UN Mission Mama Maura Mwingira. Historia ya chama  iliyosomwa na mwenyekiti wa tawi bwana Maftah na mambo mengi kama kula chakula  kucheza ngoma na muziki kutoka kwa Dj Paul Masoud wa Boston.
Mgeni rasmi  akiingia ukumbini hapa akisindikizwa na viongozi wa tawi la CCM New York. 
Viongozi wakijiweka sawa kwenye meza kuu

KAMISHNA WA SENSA YA WATU NA MAKAZI ASISITIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI

$
0
0
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (katikati) akizungumza na Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Kulia kwake ni Opio Mamu Msimamizi wa mafunzo katika kanda hiyo na kushoto kwake ni Juma Shaban Meneja Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Manyara.
Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara wakimsikiliza kwa makini Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (hayupo pichani) katika mafunzo ya utafiti huo yanayotarajia kumalizika kesho jijini Tanga.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Mafunzo ya utafiti huo yanayotarajia kumalizika kesho jijini Tanga. (Picha zote na Veronica Kazimoto - Tanga).

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH. MATHIAS CHIKAWE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekaa kutoka kushoto  Mh, Mathias Chikawe akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Idara ya Wakimbizi kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Tanzania  Joyce Mends-Cole aliyekaa kati kati. Mwakilishi huyo alimtembelea Waziri Chikawe leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kujitambulisha kwa Waziri huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Kikwete  kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe akimsikiliza kwa Makini Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania UNHCR Joyce Mends-Cole aliyekaa kati kati  wakati mwakilishi huyo alipomtembelea leo Waziri Chikawe kwa ajili ya kujitambulisha ikiwa ni Siku chache baada ya Waziri Chikawe kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Article 22

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 10.02. 2014.

$
0
0
MTU MMOJA ANAYESADIKIWA KUWA 
JAMBAZI SUGU AMEUAWA NA WANANCHI WILAYANI MOMBA.


MNAMO TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:20HRS JIONI MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HEZRON MWAISANILA (22) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE. 
CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU HUYO AKIWA NA WENZAKE WAWILI WALIOKIMBIA  WALIPORA FEDHA TASLIMU TSHS. MILIONI 1,200,000/=, ZAMBIA KWACHA MILIONI 1,200,000/=, DOLA ZA KIMAREKANI 60 NA SIMU YA KIGANJANI MALI YA DENIS ODAS (22)MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAPOROMOKO – TUNDUMA MAJIRA YA SAA 16:45HRS JIONI AKIWA ANATOKA DUKANI. MAREHEMU ALIKUWA NI JAMBAZI SUGU NA ALIKUWA ANATAFUTWA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU LIKIWEMO TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA BAADA YA KUPORA PESA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA TOYOTA KLUGER MNAMO TAREHE 25.01.2014MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA AKITUMIA SILAHA AINA YA SMG NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA AITWAYE OBADIA JANAS (41)MKAZI WA ISYESYE KWA KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WA UHALIFU WANAOWAKAMA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


WATU 7 WASHIKILIWA NA JESHI 
LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI MBUNGE.


MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI – CCM MHE. JACKSON MWANJALI (55) ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RUNGU NA FIMBO KICHWANI NA KUNDI LA VIJANA WANAODAIWA KUWA NI WAFUASI WA CHADEMA. 
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SHIPONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MBUNGE HUYO AKIWA NA SHADRACK MWATUNGUJA - KATIBU WA UCHUMI NA MIPANGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA BAADHI YA VIONGOZI WA CCM WA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKIWA WANATEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA KATIKA KATA YA SANTILYA AMBAVYO VIPO KATIKA JIMBO LAKE. 
MTUHUMIWA PAUL WUMBULA (32) MKAZI WA MBALIZI NA WENZAKE SITA WALIKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. WAHANGA WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA, HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA VURUGU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MTU YEYOTE YULE ATAKAYEJIHUSISHA NA KITENDO CHOCHOTE CHA UVUNJIFU WA AMANI. 
Signed by:

[AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TAARIFA YA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUHUSU WAFUNGWA WA KITANZANIA NCHINI CHINA

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha taarifa za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari kuwa kuna Watanzania wapatao 160 wamenyongwa nchini China kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Wizara inapenda kuujulisha Umma kuwa hakuna Mtanzania yeyote aliyenyongwa kama inavyodaiwa kwenye mitandao na vyombo vya habari.
Aidha, taarifa hiyo ya uvumi imedai kuwa ndugu wa mmoja wa Watanzania hao ambaye kwa jina anajulikana kama Bw. Rajab Mohamed Ismail Mapusa wamekaa matanga kuomboleza kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Serikali ya China, Bw. Mapusa yupo hai gerezani akitumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kuingiza madawa ya kulevya nchini humo, na hivi karibuni alishiriki kuandaa maonyesho ya utamaduni wa Kiafrika wakati wa kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya wa China.
Wizara inapenda kuwakumbusha Wanahabari kuandika taarifa ambazo ni sahihi zisizopotosha Umma kwa kuzingatia weledi, maadili na ukweli kutoka mamlaka zote husika.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
10 Februari, 2014

Eric Ng'imaryo mwenyekiti mpya Tanzania Horticultural Association (TAHA)

$
0
0
 Mwenyekiti mpya wa TAHA, Bw. Eric Ng'imaryo, akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo. 
  Na Mwandishi Wetu TAASISI inayoshughulika na kilimo cha maua na mboga mboga nchini (Tanzania Horticultural Association -TAHA) imemteua Bw. Eric Ng'imaryo kama Mwenyekiti wake mpya kuchukua nafasi iliyoaachwa wazi na Bw. Colman Ngalo, ambaye ameiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio kwa takribani miaka kumi ya utawala wake. Sambamba na uteuzi huo pia Bw. Ng'imaryo.
Pia taasisi hiyo imepata Makamu Mwenyekiti mpya pamoja na wajumbe wanane wa Bodi ya TAHA pia walichaguliwa katika Mkutano Mkuu uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.
 Miongoni mwa wanaounda Bodi mpya ya taasisi ya TAHA ni pamoja na: Bi. Fatma Riyami, Bw. Ravi Bhalerao, Bw. Herald Peeters , Bw. Juma Lossini, Bw. Robert Daniel, Bw. Tjerk Scheltema na Bw. Adrian Moss. 
Bw. Eric kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAHA na ni mategemeo yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi pamoja naye katika miaka ijayo. Mchanganyiko wa ujuzi wake katika sekta ya maua na mboga mboga na uzoefu mkubwa sambamba na utaalamu unafanya kuwa mtu bora kuchukua nafasi ya Uenyekiti wa TAHA na sekta yenye maendeleo endelevu.
 "Napenda pia kuishukuru Sekretarieti ya TAHA na wanachama wake kwa ushirikiano wao bora katika muongo uliopita. Kwa ushirikiano tumepata mafanikio mkubwa. Mimi ninajisikia fahari kubwa kukabidhi taasisi hii yenye mafanikio ambayo bado ina fursa kubwa kwa ukuaji zaidi katika TAHA na sekta nzima kwa ujumla." 
 TAHA ni taasisi ambayo ni mwanachama wa sekta binafsi ambapo imekuwa ikishiriki kwa ufanisi katika kubadilisha kilimo cha sekta ya maua na mboga mboga toka kuanzishwa kwake mwaka 2004. 
 Kutokana wa hatua za uwepo wa TAHA , sekta ya maua na mboga mboga nchini na kufanikiwa kuvutia washirika mbali mbali kutoa misaada mikubwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania na Washirika kama vile USAID, BEST- AC, Ubalozi wa Uholanzi , ITC, na Serikali Finland. TAHA inatoa sapoti mbali mbali kwa wadau wa sekta ya maua na mboga mboga ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye majukwaa, kulinda na kukuza maslahi ya watendaji katika sekta hiyo ya maua yaani wazalishaji, wauzaji, wasindikaji, na watoa huduma ya maua, matunda , mboga, viungo, mimea na mbegu za maua

news alert: watano wapanda kizimbani kwa mashtaka ya usambazaji wa Dawa feki za kurefusha maisha kwa waathirika wa Ukimwi

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam pia ni Mkurugenzi Mkuu Kiwanda cha Kutengeza Dawa (TPI Ltd) Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka matano ya usambazaji wa Dawa feki za kurefusha maisha kwa waathirika wa Ukimwi na kuisababishia Bohari Kuu ya Dawa (MSD)hasara ya zaidi ya Sh.milioni 148.3. 
 Mbali na Madabida washtakiwa wengine ni, Meneja Uendeshaji Seif Shamte, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam na Meneja Masoko, Simon Msoffe, Mhasibu Msaidizi Fatma Shango, Sadiki Materu na Evans Mwemezi. 
 Walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
 Kesi hiyo ya Uhujumu uchumi namba 5 ya mwaka 2014, ilifikishwa jana katika viunga vya mahakama hiyo saa 3:13 asubuhi huku washtakiwa wakiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu wa jeshi la polisi na kuhifadhiwa kwenye chumba cha mahabusu ya mahakama kabla ya kupandishwa kizimbani. 
 Kimaro aliudai kuwa shitaka la kwanza linamkabili mshitakiwa Madabida, Shamte, Msoffe, na Shango, wanadaiwa kwamba Aprili 5 ,2011 jijini Dar es Salaam waliuza na kuisambazia Idara ya Bohari Kuu ya Madawa makopo 7776 ya dawa bandia aina ya Antiretroviral ambazo zinajumuisha gramu 30 za Stavudine,gramu 200 za Verirapine na Batch namba OC 01.85 zikionesha zimezalishwa Machi 2011 na kuisha muda wake Februari 2013 kwa lengo la kuonesha ni dawa halisi aina ya Antiretroviral wakati wakijua si kweli. 
 Shitaka la pili pia la usambazaji wa dawa hizo ambalo linawakabili washtakiwa hao wane ambapo wanadaiwa kwamba,wakiwa na nyadhifa zao hizo,waliisambazia Bohari kuu ya madawa kopo 4476 za dawa aina ya Antiretroviral ambazo zinajumuisha gramu 30 za Stavudide,gramu 200 za Nevirapine na gramu 150 za Lamivudine zenye batch namba OC 01.85 zikionesha zimezalishwa Machi 2011 na kuisha muda wake Februari 2013 kwa lengo la kuonesha ni dawa halisi aina ya Antiretroviral wakati wakijua si kweli. Katika shitaka la tatu washitakiwa hao pia wanadaiwa kwamba Kati ya Aprili 12 hadi 29 ,2011 jijini Dar es Salaam wakiwa na nia ya kudanganya kwa pamoja walijipatia Sh.148,350,156.48 kutoka Kitengo cha Bohari Kuu ya Madawa baada ya kudanganya kwamba fedha hizo ni malipo ya dawa halisi aina ya Antiretroviral wakati wakijua si kweli. 
 Kimaro aliendelea kudai katika shitaka la nne linamkabili Sadick na Evans ambao wanadaiwa kwamba,katika tarehe tofauti kati ya Aprili n5 na 13 mwaka 2011,jijini Dar es Salaam wakiwa kama waajiriwa wa Idara ya Bohari Kuu ya Madawa kama Meneja udhiditi Ubora na Ofisa udhibiti ubora ,huku wakijua nia ya kutendeka kwa kosa ambalo ni kusambaza dawa bandia,walishindwa kutumia nyadhifa zao kudhibiti kosa hilo lisitendeke. 
 Shitaka la tano,linawakabili washitakiwa wote ambao wanadaiwa kwamba kati ya Aprili 5 hadi 30,2011, kwa nafasi zao na kutotekeleza majukumu yao ipasavyo waliisababishia bohari Kuu ya Madawa kusambaziwa dawa hizo bandia na hivyo Bohari kupata hasara ya Sh. 148,350,156.48 . Baada ya kusomewa mashitaka hayo,washtakiwa wote walikana tuhuma hizo na upande wa Jamhuri ulidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
 Pia, upande wa Jamhuri ulidai kwamba hauna pingamizi na dhamana kwa washtakiwa wote. Hakimu Mwaseba alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kama watakuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakatoa fedha taslimu Sh.12,365,513 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha kwa kila mshitakiwa. 
 Hata hivyo, ni washtakiwa wawili tu -wa kwanza na wa tano Madabida na Materu - walitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana huku wengine walipelekwa mahabusu hadi Februari 24, mwaka huu kesi yao itakapotajwa.

news alert: wawili wahukumiwa faini shilingi milioni 15 ama jela miaka 15 kwa ujenzi wa jengo la ghorofa 18 jijini dar es salaam

$
0
0
Watu  wawili wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 15 au kwenda jela miaka miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ya ujenzi wa jengo la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu lililopo mtaa wa Chimala Kitalu cha 45 na 46, kinyume cha sheria. 
 Washtakiwa hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na aliyekuwa Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga (55) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam. 
 Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya washtakiwa, mahakama imeona wana hatia kwa makosa yote matano. 
 Alisema hati ya mashitaka inaonyesha mshtakiwa wa kwanza anakabiliwa na mashitaka watatu na upande wa mashitaka umethibitisha kweli alitenda makosa hayo na mahakama inamhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kila kosa au kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kila kosa. 
 Kwa upande wa mshtakiwa wa pili, hakimu alisema hakuna ubishi bila kuacha shaka mshtakiwa, alitenda makosa hayo na kwamba atalipa faini ya Sh. Milioni 3 kila kosa au kulipa fani ya Sh. Milioni 3 kila kosa. Hata hivyo, walilipa faini hiyo na kuachiwa huru.
 Katika kesi ya msingi, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.
 Ilidaiwa kuwa Kimweri alikuwa na wadhifa huo TBA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010 na Maliyaga aliajiriwa mwaka 2002 akiwa msanifu mkuu.
 Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai alidai kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na TBA, ambako hadi mwaka 2006 kilikuwa hakijaendelezwa. 
 Aidha TBA, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma iliwaalika wanaotaka kuwekeza kuwasilisha andiko la awali kwa ajili ya uendelezaji.
Wote wamelipa faini na kuachiwa huru

in loving memory

$
0
0
 Geraldina is fondly missed by her children, family and friends. 
What moves through us is a silence, a quiet sadness, a longing for one more day, one more word, one more touch, we may not understand why you left this earth so soon, or why you left before we were ready to say good-bye, but little by little, we begin to remember not just that you died, but that you lived. 
And that your life gave us memories too beautiful to forget. 

There will be a Memorial Mass Service (all masses) at St Joseph Catholic Cathedral on 09th Sunday and 11th Tuesday February 

KONGAMANO LA 9 LA CTO CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF) KUANZA KESHO ARUSHA

$
0
0

 Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbie Gunze (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya Kongamano la  9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania. Katikati ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin, akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mahsriki (EACO) Hodge Semakula.

 Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Kongamano la  9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania. Kulia ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin.
 Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze akifafanua zaidi juu ya Kongamano hilo 9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF)
 Katibu Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO) Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.Kushoto ni Habbib Gunze, Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula.
 Katibu Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO) Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.
 Viongozi TCRA, CTO na EACO wakizungumza na wanahabari
 Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
 Wanahabari na maofisa wa TCRA wakiwa katika mkutano huo.
 Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula akielezea zoezi la uhamaji kutoka mfumo wa Analojia kwenda Dijitali kwa nchi za Afrika Mashariki hasa Tanzania ulivyofanikiwa. 
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

Katibu Mkuu Elimu afungua Mafunzo Kazini kwa Walimu, atembelea shule na vyuo mkoani Mwanza

$
0
0
Matukio mbalimbali katika ziara ya siku moja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome mkoani Mwanza. Na hotuba yake katika ufunguzi wa Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Sayansi, Hisabati na TEHAMA wanaofundisha katika shule za sekondari katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Kagera na Mara.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome katika maabara ya TEHAMA katika shule ya sekondari Pamba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.
 Baadhi ya Wawezeshaji na Washiriki wa Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Sayansi, Hisabati na TEHAMA wanaofundisha katika shule za sekondari katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Kagera na Mara. Mafunzo yanafanyika jijini Mwanza katika shule ya sekondari Pamba
 Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Sayansi, Hisabati na TEHAMA wanaofundisha katika shule za sekondari katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Kagera na Mara. Mafunzo yanafanyika jijini Mwanza katika shule ya sekondari Pamba.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na mmoja wa wanafunzi katika shule ya sekondari Nganza.
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akifungua Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Sayansi, Hisabati na TEHAMA wanaofundisha katika shule za sekondari katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Kagera na Mara. Mafunzo hayo yanafanyika jijini Mwanza katika shule ya sekondari Pamba.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na mmoja wa wanafunzi katika shule ya sekondari Nganza.
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images