Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 353 | 354 | (Page 355) | 356 | 357 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Ubao wa Matokeo.
   Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza akiipachikia timu yake bao la nne kati ya saba yaliyotiwa kimiani mpaka sasa wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 7-0.
   Mshambuliaji wa Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakimsindikiza wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 7-0.
   Mrisho Ngassa bado yuko na mpiraaaaa.....
   Mrisho Ngassa anapachika bao paleeeee...... Gooooooooo ni goli la sita hili linaungwa hivi sasa na Mrisho Ngassa na kuwa mchezaji pekee aliefunga bao tatu peke yake.
  Wachezaji wa timu ya Komorozine wakilaumiana.

  0 0  0 0


  Jambazi kuu anayetuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji na unyanganyi wa kutumia silaha yaliyo tokea Wilayani Tarime kuanzia 26 hadi 28.01.2014 amekamatwa na jeshi la polisi jioni ya Tarehe 06.02.2014 mkoani Tanga. 

  Akisimulia kukamatwa kwa jambazi huyo Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jioni ya Tarehe 06.02.2014 majira ya saa 1.30 na katika mahojiano ya awali ya jeshi la polisi mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na matukio ya mauaji ya kuanzia tarehe 26 hadi 28 na unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na mengine. 

  Kamugisha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw. Chaerles Range Kichune, 38 maafuru kama Josephat Chacha ama Joseph Charles Chacha Msong'o mkazi wa Kenyamanyori kata ya Turwa Wilayani Tarime. 

  Aidha Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa alimtaja Marwa Keryoba Alex 30 - 38 mkazi wa Kijiji cha Kebeyo Sirari Wilayani kuwa wanashirikiana kufanya ujambazi na silaha amemtunzia nyumbani kwake huko Musoma. 

  '“Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifuatilia hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walimkuta na alipo waona maasikari polisi alijaribu kukimbia huku akiwa amebeba silaha aina ya (bunduki) SMG Askari walipiga risasi hewani wakimtaka kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kuwarushia risasi na ndipo asikari waliendelea kurushiana risasi na hatimaye kumpiga risasi, marehemu alifia njiani akiwa anapelekwa hospitalini kwa matibabu,” alisema Kamugisha. 

  Kamugisha ameendelea kusimlia kuwa marehemu alikutwa akiwa na Bunduki aina ya SMG moja  iliyo futwa namba na kukatwa kitako na mtutu,magazine moja na risasi kumi katika upekuzi nyumbani kwake polisi wamefanikiwa kupata vitu kadhaa vikiwemo simu mbili za mkononi CD 21 za picha mbalimbali deki moja,viatu pea mbili na tochi mbili na mpira wa baiskeli moja na bidha mbalimbali za dukani. 

  Pia Kamanda alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 1.45  Februari 7, 2014 katika Kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Mjini Musoma mkoani Mara ambapo marehemu ameuawa kutokana na taarifa zilizo tolewa na Bw Charles Chacha Kichune maafuru (kenonke) amemtaja marehemu kuwa ni mshirika wake. 

  Kamugisha ameshukuru jeshi la polisi Mkoa wa Tanga kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi Tarime/Rorya kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa pia amewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea kufanya shuguli zao kama kawaida wakati hatua zingine zinachukuliwa aidha alimewataka wananchi kutoa ushirikiano na yeyote atakaye toa taarifa ya jambazi kukamatwa atapewa zawadi ya Tsh milioni moja papo hapo.

  0 0


  0 0
 • 02/08/14--12:41: Research Assistants Needed
 •  Experienced Research Assistants conversant in 
  topics such as theories of:
  1. Political Economy
  2. International Economic Relations
  3. Regional Integrated Economic Schemes
  4. Research Methodology
       4.1 Research Philosophy
       4.2 Research Design and Data Collection

  Please email your contact details to 
  Thank you 

  0 0

  Bondia Rudia Mashala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ratifa Khalidi wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Champion Ship yaliyo malizika katika viwanja vya Kawe Dar es salaam Ratifa alishinda kwa point.

  Bondia Ezira Paur wa Kigoma akipambana na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open CHampionship yaliyomalizika kawe Dar es salaam Paur alishinda kwa point.

  Baadhi ya watu waliofulika kuangalia michuano hiyo

  Mstahiki Meya wa Kinondoni  Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo

  Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis katikati akiwa na mabondia wa kike waliopigana na kunyakuwa zawadi mbalimbali

  Meya wa Manspaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda akimkabizi  Mwenyekiti wa timu ya Mkoa wa Kigoma  Eddie Kikwesha  baada ya kuibuka timu yenye Nidhamu katika mchezo wa masumbwi katikati ni Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis

  Katika picha ya pamoja
  Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimzawadia kocha wa timu ya kawe baada ya kuibuka washindi wa tatu katika mashindano hayo. Picha zote na Super D

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mkutano wa viongozi wa matawi, majimbo na Wilaya kwa Wilaya za Wete na Micheweni uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
  Na Khamis Haji , OMKR
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho wasivunjike moyo na matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki na badala yake waendelee na juhudi za kukiimarisha chama, ili kiweze kukamata dola katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
  Akifungua mkutano wa viongozi wa matawi, majimbo na Wilaya kwa Wilaya za Wete na Micheweni uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Maalim Seif amesema kilichotangazwa Kiembesamaki si matakwa ya wananchi, kwa vile  kimsingi wananchi wa jimbo hilo walisusia uchaguzi huo.
  Maalim Seif amesema idadi kubwa ya wapiga kura walioshiriki katika uchaguzi huo si wakaazi wa eneo hilo, ambao walichukuliwa katika maeneo mbali mbali, baada ya kubainika wananchi wenyewe hawatashiriki kwa sababu hawakuridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa hadi kufanyika uchaguzi huo.
  “Kama kuna wananchi wa Kiembesamaki waliokwenda kupiga kura basi hawazidi 1000, wengi walichukuliwa katika maeneo tafauti, kama vile Makunduchi, Mtende, Kitope na Bumbwini na wakapelekwa kupiga kura huku wakilindwa na vikosi vya Serikali”, alisema Maalim Seif.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Jamaica ya Mtaa wa Keko Molemo, Paulo Peter zawadi ya sh. 300,000 baada ya kuifunga timu ya DotmondMtaa wa Jamaica  ya Mtaa wa Keko Magurumbasi katika mechi ya kuchagua wachezaji wa kuunda timu ya kombaini ya Kata ya Keko jana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Elimu (DUCE), Chang,ombe Dar es Salaam . Jamaica lishinda mabao 3-1. Pia timu ya Dotmond ilizawadiwa sh. 200,000.
  Abbas Mtemvu  akimkabidhi Nahodha wa timu ya Dotmond ya Maa wa Keko Magurumbasi zawadi ya sh. 200,000 baada ya kuwa washndi wa pili katika mchezo huo.
  Bakari Hemed wa timu ya Dotmond akka mca Mbegu  
  Wapenzi wa soka wakiangalia mechi hiyo

  0 0

  Bw. Aidan Pugili
  WAKALA wa magazeti mjini Iringa Aidan Pugili (34),  amejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Uchaguzi mdogo wa kujaza kiti hicho kilichoachwa wazi na Dk William Mgimwa aliyefariki Januari 1, mwaka huu, utafanyika Machi 16, mwaka huu.

  Akitumia umaarufu wake wa kuuza magazeti mjini hapa, Pugili aliyesindikizwa na baadhi ya wauza magazeti wenzake alichukua fomu za Chadema kwa staili ya aina yake huku akisindikizwa na magari madogo manne ya kukodi.

  Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchukua fomu hizo anazotarajia kuzirudisha Jumanne, alisema amejipima na ameona anatosha kuiwakilisha Chadema katika uchaguzi huo.

  Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka katika chama hicho kura za maoni kwa wagombea watakaojitokeza zitapigwa Jumatano ya Februari 12.

  Pugili ambaye pia ni mjasiriamali aliyewekeza biashara ndogondogo mjini Iringa na Mbeya alisema tangu Chifu Mkwawa afariki dunia kwa kujiua mwenyewe wananchi wa Kalenga iliyokuwa ngome kuu ya chifu huyo hawajawahi kupata mwakilishi mwenye nguvu.
  “Nina uwezo wa kuwa mwakilishi wao. Ni mzoefu katika siasa za upinzani na nimekuwepo ndani ya Chadema kwa muda mrefu,” alisema.

  Alisema ajenda yake ya kwanza endapo atapewa ridhaa ya chama chake na wananchi wa jimbo la Kalenga itakuwa ni kupambana na ufisadi ndani ya halmashauri ya wilaya ya Iringa.

  Ajenda yake ya pili alisema itakuwa ni kuleta mapinduzi katika kilimo kwa kuwashawishi wagiriki wenye mashamba makubwa ya tumbaku katika jimbo hilo kugawa ardhi wasiyoitumia kwa wananchi.

  “Lakini ili kilimo kiwe na tija Chadema tunataka kuondokana na biashara ya kuwatumia mawakala kusambaza pembejeo,” alisema.

  Alisema watapigania uanzishwaji wa Mamlaka ya Kilimo Tanzania itakayosimamiwa na serikali ili kuratibu kwa uhakika ukopaji na usambazaji wa pembejeo.

  “Nataka wananchi wa jimbo la Kalenga ambao asilimia 80 ni wakulima wanufaike na kilimo ili waweze kupeleka watoto wao shule,” alisema.

  Alisema afya na utalii zitakuwa ajenda zake zingine muhimu katika kinyang’anyiro hicho.

  “Afya ni majisafi, matibabu na lishebor, nitapiga kuhakikisha wananchi wa Kalenga wanapata huduma hizo muhimu,” alisema.

  Alisema  serikali ya CCM imeyatelekeza makumbusho ya Mkwawa yaliyopo Kalenga na kufanya jimbo hilo na watu wake wakose mapato mengi kutoka kwa watalii.

  “Nitahamasisha utalii wa makumbusho hayo. Nataka dunia isisahau historia ya chifu Mkwawa na katika hilo nitakuwa naenzi ushujaa wake,” alisema.

  0 0

   
   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana akimkaribisha Mama yake mzazi Regina Mlowe kuzungumza machache katika sherehe za kumkaribisha zilizofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Rudewa
   Mama mzazi akiwashukuru wananchi wa Rudewa katika sherehe za kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana.
   baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa katika sherehe za kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana.
   Mkuu wa Wilaya ya Rudewa Juma Solomon Madaha akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana. (Picha zote na Denis Mlowe).
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana akicheza muziki na baadhi ya viongozi wa ccm wilaya ya Rudewa

  0 0


   KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka na Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions imewaomba wadau wenye nia ya kufanikisha maendeleo ya matamasha hayo kuwasaidia katika muendelezo wa matamasha yanayoandaliwa na kampuni hiyo, Aprili  mwaka huu kampuni hiyo iko mbioni kuandaa Tamasha la Pasaka.  

  Kutokana na hali hiyo, wadau mbalimbali ambao wamepata kutoa ahadi za namba mbalimbali katika matamasha hayo wameombwa kutekeleza ahadi zao ili zitumike katika malengo yaliyokusudiwa. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema wadau mbalimbali wa muziki wa Injili, wakiwemo baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo utekelezaji wake umekuwa mgumu.
  “Wapo baadhi ya watu wanakuja katika matamasha yetu, wanatoa ahadi nzito hasa za fedha, lakini tamasha likishamalizika wanashindwa kutekeleza ahadi zao na ndiyo huwaoni tena, tunashukuru wapo wengine huwa wepesi kutimiza walichoahidi.“Huwa haya matamasha tunayaandaa kwa malengo maalum, ukitaja ahadi yako huwa tunaipa thamani kubwa na ukishindwa kuitimiza unatuangusha na hilo ndilo linatuharibia sana mipango yetu,” alisema Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi.

  Aliwaomba baadhi ya viongozi na wadau wengine ambao wamepata kutoa ahadi mbalimbali kwenye Tamasha la Pasaka kuhakikisha wanatekeleza ahadi zao kama walivyozitoa na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kuwataja majina kwani wenyewe wanajitambua.
  “Tunaamini pengine wana mambo mengine ndiyo sababu tumeandika barua kuwakumbusha wakati huu tukielekea katika maandalizi ya Tamasha la Pasaka,” alisema.

  0 0

  Honourable  Hawa Ghasia - Minister of State in the Prime Minister's Office for Regional Admin and Local Government during a demonstration in a mobile laboratory donated by BG Tanzania in Mtwara.
  BG Tanzania has donated 13 mobile laboratories to the Mtwara District Council to a tune of USD 50,000. The laboratories have the capacity to positively impact 910 secondary school students in the Mtwara rural district council.  
  Speaking at the donation event, Honourable  Hawa Ghasia - Minister of State in the Prime Minister's Office for Regional Admin and Local Government who was a Guest of honour at the event commended efforts of BG Tanzania to boost science education in secondary schools. 
  ''This support comes at an opportune time, given that our  schools have been doing poorly in science related subjects not because students don't have the capacity to understand science subjects, but because they have not been exposed to science related practicals due to unavailability of equipment. I ask the District Education officer and District executive Director to ensure that, those mobile laboratories are properly maintained all the time”, said honorable Ghasia. 
  BG Tanzania Head of Policy and Corporate Affairs Fred Kibodya said, "BG Tanzania is committed to improving education and hence facilitating capacity building initiatives in the southern coastal regions. These mobile laboratories will enable students to increase their capacity to learn by performing practical scientific tests, and ensure that logistical limitations, such as mobility and electricity, do not prevent students from conducting scientific experiments ".
  The mobile laboratories are manufactured in Tanzania, and have the ability to be moved from classroom to classroom. Additionally, the laboratories are equipped with solar panels, which produce power to support students while using the equipment and conducting scientific tests. 
   BG Tanzania has been working closely with the Government of Tanzania to build capacity in the sciences through providing scholarships to Tanzanians studying in UK universities and Tanzania universities. The company has also partnered with Vocational Education Tanzania Authority (VETA) in establishing trainings for youth in the gas and oil related fields.

  0 0

   Katibu mkuu wizaraya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Watatu kushoto), akizungumza jambo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa (Wanne kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kujionea kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Raha Mohammed (Kulia), Richard Ndasa (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Yonah Kilagane.
   Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Wapili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiongozwa na mwenyekiti wake, Victor Mwambalaswa (Wakanza kushoto) kuhusu kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Yonah Kilagane.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Victor Mwambalaswa (Wapili kulia) na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mhe Richard Ndasa, wakiangalia kazi ya upakuaji saruji kutoka kwenye meli bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamati hiyo ilitembelea ili kujionea kazi hiyo na ile ya kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akiwaeleza wajumbe wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini (Hawapo pichani), kuhusu kazi ya upakuaji saruji kutoka kwenye meli, bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Saruji hiyo itakayotumika kujengea mabomba ya kupitishia gesi, iliwasili sambamba na shehena ya mwisho ya mabomba hayo.
   TANZANIA  inatarajia kufaidika na matumizi ya gesi asilia ambayo yataokoa zaidi ya shilingi  Trilioni 1.6trn/- kila mwaka, mara baada ya gesi ya Mtwara kuanza kutumika katika sekta mbalimbali, mara kazi ya ujenzi wa bomba la gesi  toka Mtwara kuja jijini Dar es Salaam itapokamilika. 
   Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Victor Mwambalaswa (mb) wakati wa hafla ya kupokea shehena ya mwisho ya mabomba kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es S.alaam.
  Mhe. Mwambalaswa amesema, kiasi hicho cha fedha ndicho kinachotumika na taifa kuagiza mafuta ya kuendesha mitambo mbalimbali ambapo baada ya gesi kufika Dar es Salaam, fedha hizo sasa zitaelekezwa kwenye maeneo mengine kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
  Mhe. Mwambalaswa amesema utekelezaji wa mradi utaleta manufaa makubwa kwa wananchi hasa maeneo gesi asilia inapopatikana. Huduma mbali mbali za jamii kama vile maji, umeme, afya, elimu na miundombinu zitatolewa au kuboreshwa. Mapato ya kodi za Halmashauri yataongezeka na ajira kwa wazawa zitaongezeka.
  Akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakimu Maswi, alizitaja baadhi  ya faida ambazo wananchi wa Mtwara na Lindi watafaidika nazo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi itakayojengwa Madimba na Songo Songo: Kila mtambo utahitaji kiasi cha wafanyakazi wa moja kwa moja wapatao sitini (60) watakaoendesha mitambo hiyo. Vile vile, kutahitajika watu watakaotoa huduma ya chakula, afya, usafiri pamoja na huduma nyingine za kijamii.

  Bw. Maswi ameelezea kuhusu ujenzi wa kiwanda cha saruji cha kampuni ya Dangote ambacho kitatoa ajira rasmi kwa wananchi takribani 500 na zile zisizo rasmi takribani watu 800 na ujenzi wa kiwanda kingine cha Saruji cha kampuni ya Meis kitakatoa ajira kwa wananchi takribani 1000.

  Bw, Maswi amesema, wizara yake ya Nishati na Madini imetenga fungu maalam ambalo litatumika kuwapatia umeme wananchi wa vijiji vyote vinavyopitiwa na bomba gesi.

  Sambamba na faida hizo za jumla, pia sehemu ya gesi itakayozalishwa katika maeneo ya Mnazi Bay, Ntorya na kina kirefu cha maji itaendelea kutumika kuzalisha umeme kwa matumizi ya mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na mikoa mingine inayopakana nayo, wakati kwenye matoleo ya bomba la kusafirisha gesi limeweka matoleo ya kuchukulia gesi asilia (off take) katika miji ya Mtwara, Lindi, Kilwa na Mkuranga ili kuhakikisha kuwa maeneo haya yanapata gesi asilia ya uhakika kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine.
  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, Bw. Yona Kilaghane, amesema mazungumzo ya ujenzi wa mitambo ya (LNG) yameanza kati ya TPDC, kupitia Wizara ya Nishati na Madini na Makampuni ya Statoil, British Gas (BG), Ophir pamoja na Exxon Mobil ili kuzalisha LNG kwa kutumia mtambo mkubwa utakaojengwa karibu na maeneo ya ugunduzi. 

  0 0

  Washiriki wakimalizia mbio zao kutokea Uwanja wa Taifa mpaka Ukumbi wa taifa wa Burudani wa Dar Live.
  Klabu mwenyeji, Kejo Community wakiwa jukwaani wakicheza kwa furaha katika Bonanza hilo.
  Msanii wa Msondo Music Band, Hassan Moshi (mwenye Mic) akikosha nyoyo za wana Jogging waliohudhuria kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News leo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) , Sharon Mariwa  Meneja wa Mahusiano OXFAM, Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB pamoja na Mkamiti Mgawe Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM, wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa katika Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula leo.
  Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akielezea Mchakato mzima wa kazi ilivyokuwa kabla , wakati wa kuwatafuta washiriki wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula na kutaja rasmi majina ya waliochaguliwa katika usahili huo.


  0 0

   Wafuasi wa CCM Iringa  wakimpongeza kaimu katibu  wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha  chama  hicho kushinda  uchaguzi mdogo kata ya  Nduli.
  Wafuasi wa CCM kata ya Nduli  wakiwa  wamemnyanya  juu  juu  aliyekuwa mgombea  udiwani kata ya Nduli Bw Mtove  baada ya  matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo 
  ...........................
  CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia.
  Wafuasia  wa  CCM  walimpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga na kudai kuwa  kazi  yake  inaonesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini.
  Matokeo katika vituo vyote  tisa  ambavyo  wananchi  wa Nduli  walipata  kuvitumia kupiga kura  ,kituo cha Mawasiliano  CCM (57),Chadema(28),Zahanati  CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli  CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni   CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina  CCM (156 ) Chadema (31)

  Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku  Chadema  wakifuatia kwa kura 487
  Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.

  Katika kata ya  Njombe mjini mgombea  wa  Chadema amembwaga mgombea wa CCM ambapo  matokeo yanaonyesha  mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja pekee   kwa tofauti ya  kura  2  huku  katika vituo vyote  Chadema ikiibuka kidedea.

  0 0

  Joy Kalemera (wapili toka kulia) akiwa College Park Maryland alipowatembelea darasa la kiswahili DMV siku ya Jumamosi Feb 8, 2014. Wengine katika picha ni waratibu wa Miss Tanzania USA akiwemo mkurugenzi Ma Winny Casey (wa kwanza kushoto)
   Wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV wakimsalimia Miss Tanzania USA Pageant na kumwimbia nyimbo mbalimbali za kiswahili ukiwemo wimbo wa Taifa.
   Miss Tanzania USA Pageant akijitambulisha na kuwaambia yeye ni mhandisi anayefanyakazi New Jersey na akawauliza kama wanafahamu maana ya neno uhandisi na wao wakajibu hawafahamu ndipo alipowaelewesha maana yake kwa Kingereza.
   Wanafunzi wa darasa la kiswahili wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant alipowatembelea shuleni kwao College Park, Maryland.
   Mwalimu mpya wa hesabati Cechelela Timo akiwafundisha hesabu kwa kiswahili wanafuzi wa darasa la kiswali DMV.
   Mwalimu Asha Nyang'anyi akiwaelekeza jambo wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV.
   Mmoja ya wanafunzi Briana akiwasomea kitabu cha hadithi wanafunzi wenzake.
   Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akimuelekeza kitu mmoja ya wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV. Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la  Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi msaada wa mabati kwa ajili ya kusaidia uwezekaji wa Jengo la Klabu ya Soka ya Timu ya Kombora iliyopo Kitope, Zanzibar.
  Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kirombero Mwalimu Juma Simai akipokea msaada wa vifaa vya kupikia chai vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kwa skuli zote za jimbo hilo. Hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa michezo wa Kombora Kitope. 
  Picha na Hassan Issa wa OMPR , ZNZ.


  0 0

   Habari na picha 
  na Mahmoud Zubeiry
  AZAM FC imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
  Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche (pichani juu) aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41 baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua shuti kali.
  Mchezo ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
  Kiungo mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umony leo Chamazi.

  0 0

  Mkuu wa wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa amebeba kichwani zawadi ya kibuyu chenye chakula cha asili ya wanyaturu, Mkuu huyo wa Mkoa  alikabidhiwa zawadi hiyo  na umoja wa Wanyaturu waishio mkoani Dodoma wakati wa sherehe yao ya kuukaribbisha mwaka 2014. Wengine wanaoshuhudia ni wanachama wa umoja huo wa Wanyaturu waishio mkoani dodoma.

older | 1 | .... | 353 | 354 | (Page 355) | 356 | 357 | .... | 3286 | newer