Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 352 | 353 | (Page 354) | 355 | 356 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Kijana wa kitanzania asomae Korea Kusini Bw. Sunday Sokoni ameibuka kidedea kwa kushinda nafasi ya pili katika mashindano ya kukariri na kuongea mashairi ya kikorea kwa hisia. 
  Shindano hilo liliwakutanisha washindani mia moja na therethini (130) wengi wao wakiwa ni Wakorea lakini Sunday Sokoni alifanikiwa kuwabwaga Wakorea hao na kuwa raia pekee wa kigeni aliyeingia kwenye Tatu bora. 
   Ushindi wa Sunday ulikuwa gumzo jijini Seoul-Korea na kupelekea Television za Korea kufanya mahojiano na Sunday Sokoni na pia kutengeneza documentary zinazoelezea maisha yake Korea amabapo ilimfaya kuwa maarufu sana hapo Chuoni (Yonsei). 
   Habari za Sunday pili zilishapishwa katika magazeti kadhaa ya kikorea pia alisikika mpaka katika redio mbalimbali za Korea. Tayari Kijana Sunday ameshafanya mahojiano kwenye television kadhaa; Chosun Tv na KTV na kwa sasa anajiandaa kuenda katika television kubwa maarufu iitwayo KBS (Korean Broadcasting System) kwa mahojiano anatarajia kufanya mwaka huu 2014 March na bado anaendelea kutafutwa na stesheni za television kwa mahojiano, kwa sababu imekua ni historia kutokea mtu wa kigeni kushinda mashindano hayo. 
  Amekua ni kijana pekee ambaye kwa ujasiri wake na kujiamini kwa nafasi hiyo aliweza kupeperusha bendera ya Tanzania na kufanya nchi yetu itambulike zaidi hapa Korea Kusini. Sunday Sokoni ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Yonsei akisomea shahada ya Uchumi.
  Sunday Sokoni akiwa amepozi katika moja ya picha zilizochapishwa kwenye gazeti la kikorea (Yonhap News)
  Sunday Sokoni akipokea medali kutoka kwa mkuu wa chuo cha Yongsei Bw. Kap-Young Jeong baada ya kutangazwa mshindi wa pili wa shindano la kuimba kwa hisia mashairi ya kikorea
  Pichani: Bwana Sunday Sokoni akihojiwa na television ya Korea( Chosun Tv)

  0 0

   Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi katikati akizungungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya mafanikio ya uongozi wake kwa siku mia moja toka waingie madarakani, Kulia ni Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura na kushoto ni Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregenus
   Pichani ni baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika leo ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Kempisk Hyatt Regency Hotel,jijini Dar.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba   jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jioni hii jijini Dar es salaam.
  Wanahabari wakimsikiliza  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhe.  Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba  yakitangazwa jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam. Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 70 (na kuongezewa siku 20 kama hawatoafikiana)  kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana. 
  Kupata orodha kamili ya majina hayo  BOFYA HAPA

  0 0


  Dear All,

  Among 9 names we sent to the President's Office in Dar es Salaam, Mr. Kadari Singo has been selected to represent the Diaspora in the coming Special Parliament Session on Constitutional Review.
  We will let you know on how you can participate in getting our opinions together and have one voice from the Diaspora in regards to the Review of the Constitution.
  With Kind Regards,
  Dr. Ndaga Mwakabuta,
  DICOTA President

  0 0
 • 02/07/14--23:59: Article 24


 • 0 0

  JUDICIAL ORGANS, INDEPENDENT & STANDING COMMITTEES TFF
  BOARD OF TRUSTEES; Said Hamad El-Maamry, Stephen Mashishanga, Dr Ramadhan Dau, Joel Bendera, Mohamed Abdul Aziz
  Kamati ya Nidhamu; Tarimba Abbas (Mwenyekiti), Advocate Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma, Kitwana Manara.
  Kamati ya Rufani ya Nidhamu; Profesa Mgongo Fimbo (Mwenyekiti), Advocate Hamidu Mbwezeleni (Makamu Mwenyekiti), Titus Bandawe, Twaha Mtengera, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
  Kamati ya Maadili; William Erio (Mwenyekiti), Advocate Ezekiel Maganja (Makamu Mwenyekiti), Advocate Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Said Mtanda.
  Kamati ya Rufani ya Maadili; Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
  Kamati ya Uchaguzi; Advocate Melchesedeck Lutema (Mwenyekiti), Advocate Walter Chipeta (Makamu Mwenyekiti), Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura, Hassan Dalali.
  Kamati ya Rufani ya Uchaguzi; Advocate Julius Lugaziya (Mwenyekiti), Advocate Mwita Waissaka (Makamu Mwenyekiti), Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga, Masoud Issangu.
  Kamati ya Fedha na Mipango; Wallace Karia (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammad, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy, Cyprian Kuhyava.
  Kamati ya Mashindano; Geofrey Nyange (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald Ambi, Davis Mosha, Said George, Nassoro Idrissa (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
  Kamati ya Ufundi; Kidao Wilfred (Mwenyekiti), Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedastus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo, Dk. Cyprian Maro (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
  Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana; Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti), Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya, Ibrahim Masoud (Mshauri wa Ufundi wa Rais- Pelegrinius Rutayuga).
  Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake; Lina Kessy (Mwenyekiti), Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amina Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o, Ingridy Kimaro.
  Kamati ya Waamuzi; Saloum Umande Chama (Mwenyekiti), Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi, Zahra Mohamed.
  Kamati ya Habari na Masoko; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela, Juma Pinto.
  Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji; Advocate Richard Sinamtwa (Mwenyekiti), Advocate Moses Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko, Imani Madega.
  Kamati ya Ukaguzi wa Fedha; Ramadhan Nassib (Mwenyekiti), Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga, Elias Mwanjala.
  Kamati ya Tiba; Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema, Asha Sadick.
  Kamati ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni; Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti), Shaffih Kajuna Dauda (Makamu Mwenyekiti), Boniface Pawasa, Deo Lucas, Juma Mgunda, John Kanakamfumu, John Mwansasu.
  AD HOC COMMITTEES
  Kamati ya Kutathimini Muundo wa Ligi; Dk. Mshindo Msolla (Mwenyekiti),  Idd Mshangama (Katibu), Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir, Lucas Kisasa.

  Kamati ya Kutathimini Muundo wa Bodi ya Ligi; David Nchimbi (Mwenyekiti), Edwin Kidifu, Jones Paul, Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani, Pelegrinius Rutayuga.

  0 0
 • 02/08/14--02:53: Memorial Service
 • It is now Seven Years since you left us. May the Good Lord Rest Geraldina Mutalemwa’s soul in eternal piece.

  Amen.

  Geraldina is fondly missed by her children, family and friends. What moves through us is a silence, a quiet sadness, a longing for one more day, one more word, one more touch, we may not understand why you left this earth so soon, or why you left before we were ready to say good- bye, but little by little, we begin to remember not just that you died, but that you lived. And that your life gave us memories too beautiful to forget.

  There will be a Memorial Mass Service (all masses) at St Joseph Catholic Cathedral on 09th Sunday and 11th Tuesday February

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abas Kandoro akifungua kongano la Muungano kwa vyuo vya elimu ya juu mjini mbeya leo, kushoto ni Naibu katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Bi Angelina madete,na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya muungano kutoka Ofisi ya makmau wa Rais Baraka Rajab
  Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamo wa Rais Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifafanunua kuhusu masuala ya Muungano katika kongamano lililohusisha vyuo vya elimu ya juu mkoani Mbeya leo.
  Washiriki wa Kongamano la Muungano mkoani Mbeya ambao ni wanafunzi wa vyuo ya elimu ya juu wakifuatilia mjadala katika kongamano hilo mjini Mbeya leo.

  Ni wajibu wa kila Mtanzania kutambua kwamba uandikishwaji wa katiba mpya unalenga kuweka misingi ya kuijenga Tanzania ya sasa naya siku nyingi zijazo.

  Hayo yameelezwa leo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abas Kandoro katika ufunguzi wa kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani humo,lililohusu masuala mbali mbali ya muungano kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar.

  Katika Kongamano hilo Bwana Kandoro aliongeza kwa kusema kuwa jambo hili ni kubwa na linahitaji umakini wa hali ya juu saana katika kila hatua ili kufanikisha mchakato huu, aidha Bwana kandoro aliwakumbusha washiriki wa kongamano hilo kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kuwepo kwa mahusiano ya karibu kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika Nyanja mbali mbali kama vile undugu wa damu, biashara,utamaduni lugha na mahusiano ya karibu ya kisiasa.

  Bwana kandoro aliendelea kusema kuwa, Muundo wa muungano wetu umeweka mfumo wenye vyombo mbalimbali vyenye mamlaka za utendaji, kutunga sheria na kusimamia shughuli za umma na utoaji haki.

  “Pamoja na hiyo mifumo, na kuwepo sababu nyingi nzuri na za msingi za kuwepo Muungano, bado ndani ya jamii yetu kuna wanaohoji uhalali wake kupitia maoni yaliyotolewa mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba mahakama na mijadala mingine, alisisitiza.”

  Mkuu wa Mkoa alisema kuwa yawezekana kabisa kuwa washiriki wanaweza kuwa na hoja zinazofanana na hizo..na hivyo mada zitakazotolewa zinaweza kusaidia kujibu baadhi ya hoja.

  Katika Kongamano hilo wasomi hao wametoka na kauli mbiu inayosema “MUUNGANO IMARA NI MUSTAKABALI WA TAIFA LETU.”

  Kungamano hili linaondeshwa na Idara ya Muungano ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mikoa ya Mbeya ya Iringa ni moja ya makongamano katika vyuo vikuu nchini kuelekea maadhisho ya miaka hamsini ya Muungano

  0 0

   Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akiwatoka mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 2-0.
   Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akichuana vikali na Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro,Ahmad Houmadi (5) wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 2-0.
   Wachezajiwa timu ya Yanga wakishangilia bao lao la pili lililotiwa kimiani na Mchezaji Nadir Haroub.
   Kiungo Mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akiafanya makeke yake wakati alipotaka kumtoka Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro,Ali Mohamed wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 2-0.
   Mashabikiwa Timu ya Yanga.

  0 0

  Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia. Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake. Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

  0 0

  Kikundi cha wake wa Viongozi (Mellinium Women Group) yatoa msaada wa Chakula, Mavazi na Vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. Milioni 6.8/- kwa “New Hope for Girls Organization’’ kinacholea wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.

  Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda alieleza kuwa, wake wa viongozi waliguswa baada ya kukutana na Bibi. Consoler Eliya mwaka jana katika mkutano wa wanawake wajiwezeshe kiuchumi ambaye ni miongoni mwa wasichana walioishi katika mazingira magumu na kuahidi kumsaidia.  

  Misaada hiyo ilitolewa jana mchana (Ijumaa, Februari 7, 2014) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay, jijini Dar es Salaam

  “Wakina mama wameona jitihada za Bibi. Consoler katika kusaidia wasichana hawa wanaoishi katika mazingira magumu, ambayo watu wengi wamekuwa wakiyapitia na kushindwa kujitolea kama ilivyokuwa kwa Bibi. Consoler’’,alisema.

  Mama Pinda aliongezea kuwa, nia ya Serikali ni kuhakikisha watoto husasani wakike wanaishi kwa amani na kupata haki zao za msingi kwani maisha yao yamekuwa ya huzuni kubwa mno.

  Baada ya makabidhiano hayo, Bibi Consoler Eliya, aliwashukuru sana wake wa viongozi kwa msaada waliotoa: “mhitaji si lazima awe yatima, mhitaji anaweza kuwa na wazazi wote na bado akawa anaishi katika mazingira magumu hivyo sisi tunaishi na watoto walitoka katika makundi tofauti ya mazingira magumu’’ alisema.

  Mbali na kulelewa katika kituo hicho, pia wasichana hao wanabuni na kutengeneza vitu kama batiki, mikufo ambayo inasaidia kuendesha maisha yao, aliongezea Bibi. Consoler.

  Mwenyekiti wa kikundi hicho Mama Lukuvi aliongezea kuwa, kutokana na juhudi zinazooneshwa na wasichana hao  Kikundi kitawawezesha meza katika mkutano wa wajasiriamali utakaofanyika hivi karibu Jijini Dar es Salaam ili waweze kupeleka bidhaa zao za ubunifu wanazozitengeneza.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara akipiga penati  na kumpeleka siko  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa katavi Dtk Rajabu Rutengwe akikagua Shamba darasa la mfano SAGCOT lililopo mkoani katavi katika kijiji cha Mwenge wilaya ya Nsimbo lililopandwa kitaalamu na kuzingatia kanuni bora za kilimo na kutunzwa kwa kutumia mbolea kutoka kampuni ya yara Tanzania, mbegu bora za mahindi aina ya DKC 9089 kutoka kampuni ya mosanto vipimo vya sm 75*60sm na kupandwa kwa punje mbilimbili za megu. kampuni ya Mosanto akiwa anatekeleza mradi wa kilimo(SAGCOT) mkoani katavi.
  Shamba darasa la mfano SAGCOT lililopo mkoani katavi katika kijiji cha Mwenge wilaya ya Nsimbo linaukubwa wa heka mbili lililopandwa kitaalamu na kuzingatia kanuni bora za kilimo na kutunzwa kwa kutumia mbolea kutoka kampuni ya yara Tanzania, mbegu bora za mahindi aina ya DKC 9089 kutoka kampuni ya mosanto vipimo vya sm 75*60sm na kupandwa kwa punje mbilimbili za megu. kampuni ya Mosanto akiwa anatekeleza mradi wa kilimo(SAGCOT) mkoani katavi.
  Shamba darasa la mfano SAGCOT lililopo mkoani katavi katika kijiji cha Mwenge wilaya ya Nsimbo lililopandwa kitaalamu na kuzingatia kanuni bora za kilimo na kutunzwa kwa kutumia mbolea ya kutoka kampuni ya yara Tanzania, mbegu bora za mahindi aina ya DKC 9089 kutoka kampuni ya mosanto vipimo vya sm 75*60 na kupandwa kwa punje mbilimbili za megu.Bi Joanith mchiwa ni bibi shamba wa kampuni ya Mosanto akiwa anatekeleza mradi wa kilimo(SAGCOT) mkoani katavi.

  0 0

  Bondia Habasi Hamisi wa Kigoma akikwepa konde la Mustafa Murinho  wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Championship yaliyofanyika katika  viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Morinho alishinda kwa point mpambano huo na kuingia fainal
  Bondia Finias Genga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Openchampion ship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Swanga alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza na kufanikiwa kuingia fainal ya mashindano hayo Picha Na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Haruna Swanga akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake
  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis akisaidia kufunga mlingoti wa taa katika mashindano hayo

  Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimwelekeza ofisa habari wake Viduka  jinsi ratiba ya mahindano yanavyokwenda kushoto ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
  Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis na  Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare wakifatilia kwa makini Mashindano hayo
  Aisha Vonialis
  Na Mwandishi Wetu Kawe

  Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis amesema wanawake wanatakiwa wawe na msukumo mkubwa katika kuhakikisha wanajitokeza kwenye mchezo wa masumbwi.
  akizungumza wakati wa mashindano ya kumuenzi Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela Open Boxing Championship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam. 

  Mjumbe huyo alitoa wito kuwa wanawake wanaweza hivyo wajitokeze katika kucheza mchezo wa ngumi na kuangalia mchezo huo kama michezo mingine akitolea mfano unaona katika mashindano haya wanawake ndio walio ongoza kuja kwa wingi kwa kuwa wanapenda mchezo siku zote tulizo kuwepo hapa katika viwanja hivi wanawake wanakuja kushangilia sana tu.
  aliongeza kwa kusema kuwa wanaomba mashilika,makampuni tasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuja kusaidia mchezo wa masumbwi upate wadhamini wa kutosha kwani mashindano hayo yamekutanisha mikoa mbalimbali nchini kwa sasa hivyo wadau wote wanaombwa kujitokeza kudhamini mchezo huo.
  katika mashindano hayo ya kuingia fainali bondia Mustafa Morinho alimsambalatisha Abbasi Hamisi uku Jonson Swanga akimpiga Disson Everest na Abuu Said akimdunda Frank Msindo na Haruna Swanga akimwazibu bila huluma bondia Finias Genga kwa TKO ya raundi ya kwanza

  0 0

  Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa kampuni ya ORIGO Bwana Lieven De Koker anayeshiriki Maonyesho ya Utalii ya Brussels. Bwana Lieven anakaa Arusha na kampuni yake inashiriki Maonyesho ya Utalii ya Brussels kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Balozi Kamala ameishukuru Bwana Lieven kwa kazi anayofanya ya kutangaza utalii wa Tanzania.
  Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya Reisspeciliast ya Ubelgiji akimweleza jinsi kampuni hiyo inavyopeleka watalii Tanzania mara mbili kwa mwaka na jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo kuitangaza Tanzania Ubelgiji. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo na ameiomba iendelee kuitangaza Tanzania.

  0 0

  Wagombea wakiwa katika mapozi kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura halijaanza

  Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakipiga makofi wakati wakisubiri zoezi la upigaji kura lianze
  wageni rasmi
  Msanii wa CCM Ally Bin Ahamed maarufu kwa jina la mpemba asilia akitoa mashairi ya kuipongeza CCM
  wajumbe wengine

  Wagombea nao wakijifariji kwa makofi ya wajumbe

  KAIMU Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amewasihi wajumbe wa mkutano huo kumchangua mgombea anayoonekana kukubalika kwa asilimia 60 kwa wapiga kura.
  "Falsafa ya chama kwanza, mtu baadaye lazima tuipime vizuri, tunahitaji ushindi na ili tupate ushindi lazima tuangalie wananchi wanataka nini," alisema.
  Akifungua mkutano huo, Mtenga aliwataka wagombea ndani ya chama hicho wawe na utamaduni wa kukubali matokeo kwa afya ya chama.
  Alisema wagombea wote tisa waliojitokeza katika kura hizo za maoni wana sifa za kuwa wabunge na akawataka wajumbe kutumia busara zaidi wakati wakifanya uamuzi.
  Alisema mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho umecchukua siku mbili hali itakayosaidia kukinusuru chama na mipasuko.
  “Tulikuwa na kawaida ya kufanya kura za maoni kwa zaidi ya mwezi mmoja; hali hiyo ilikuwa ikiwaacha wagombea  katika majeraha makubwa ya matumizi ya fedha,” alisema.
  Alisema majeraha hayo yamekuwa yakichangia hasira kwa wagombea walioshindwa ambao badala ya kukisaidia chama kipate ushindi, hufurahia kinapopoteza nafasi.
  Alisema kwa mtaji walionao, CCM wana hakika na ushindi wa kishindo katika jimbo hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
  Waliojitokeza kupitia katika chama hicho ni pamoja na Jackson Kiswaga, Hafsa Mtasiwa, Godfrey Mgimwa.  
  Wengine ni Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kisaba, Msafiri Pagamila na Thomas Mwakoka.

  0 0
 • 02/08/14--10:10: cheka unenepe...


 • 0 0

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakiangalia karafuu 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiangalia bidhaa iliyokwisha kuwa tayari kwa matumizi  ikiwa katika matayarisho yaliyo bora katika kiwanda cha cha  Viungo   cha  (Everest Spice Industries Ltd) Mumbai  India akiwa katika ziara ya Kiserikali,(katikati) Balozi wa Tanznaia Nchini India John W.H.Kijazi. 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akioneshwa kitu na Afisa Rajiv Shah, alipotembelea  katika kiwanda cha Viungo (Everest Spice Industries Ltd) akiwa na ujumbe wake , kuona utendaji kazi za kila siku kiwanadani hapo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiangalia bidhaa zilizokwisha kuwa tayari kwa mauzo, walipotembelea  katika kiwanda cha Viungo (Everest Spice Industries Ltd) akiwa na ujumbe wake    nje ya Mji wa Mumbai, India.

  0 0

   Uzinduzi wa ofisi ya Tawi la CCM Ferry Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam leo. Mjumbe wa NEC Phares Magesa alikuwa Mgeni rasmi ambapo alizindua tawi, na kuendesha harambee ya kuimarisha Chama kuichumi na kuingiza wanachama wapya
    Mjumbe wa NEC Phares Magesa akifungua ofisi za tawi hilo
    Mjumbe wa NEC Phares Magesa akitoa kadi kwa mwanachama mpya
   Mjumbe wa NEC Phares Magesa akihutubia baada ya kuzindua tawi hilo

  0 0


older | 1 | .... | 352 | 353 | (Page 354) | 355 | 356 | .... | 3272 | newer