Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 351 | 352 | (Page 353) | 354 | 355 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Kampuni ya China Tebian Electrical Apparatus Stocks Company(TBEA) ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kampuni hiyo inashughulika na ujenzi wa miundombinu ya umeme.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Lord Mandelson ikulu jijini Dar es Salaam leo.Lord Mandelson amewahi kushika nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu Tony Blair na Gordon Brown.Lord Mandelson kwa sasa ni mwenyekiti wa taasisi ya Global Counsel(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Balozi wa Tanzania BELUX, Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ACP anayesimamia masuala ya siasa na maendeleo ya jamii Mhe. Michele Dominique Raymond. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kukutana na viongozi mbalimbali wa Sekretarieti ya ACP Brussels kwa lengo la kuelewa vyema changamoto zinazokabili ACP na kubaini masuala kipaumbele wakati wa kipindi chake cha uenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP.

  0 0

  Watu 12 rais wa Iran na Pakistani wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, wakikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na kuingiza nchini kilo 200.5 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya Sh. bilioni 9.022. 
   Washtakiwa hao ni, Kepteni Ayoub Mohamed raia wa Irani, Wavuvi, Buksh Mohamed raia wa Pakistani, wa Irani Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Rahim Baksh wa Pakistani, wa Iran Khalid Ally na Abdul Somad. 
  Wengine ni raia wa Pakistani Abdul Bakashi, wa Iran Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad. 
  Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba wa mahakama hiyo. 
   Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila, ulidai kuwa Februari 4, mwaka huu washtakiwa wote walikutwa ndani ya bahari ya Tanzania wakiingiza dawa za kulevya aina ya heroin nchini. 
   Ilidaiwa kuwa dawa hizo ni kilo 200.5 zenye thamani ya Sh. 9,022,500,000 aina ya heroin. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 
   Hakimu Mwaseba alisema kesi hiyo itatajwa Februari 24, mwaka huu na washtakiwa wapelekwe mahabusu.

  0 0

  Msanii wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu (pichani) anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28), anatarajia kujibu mashitaka yake kwa mara ya kwanza Februari 17, mwaka huu katika Mahakakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
   Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji na bila kukusudia, iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa kanda hiyo, kesi ya Lulu itasikiliza mbele ya Jaji Rose Teemba na mshtakiwa atajibu mashitaka yake kama ni kweli au siyo kweli.
  Aidha ratiba hiyo inaonyesha kwamba mshtakiwa akisomewa mashtaka na kujibu, mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.
  Mnamo Januari 29, mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia.
   Aidha, Lulu alipata dhamana hiyo baada ya Jaji Zainabu Mruke kutoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo baada ya wakili wa utetezi Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).   Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Joseph Maugo na Kishenyi Mutalemwa.
   Wakili Kibatala alidai kuwa hati hiyo imeambatanishwa na hati ya mashtaka yanayomkabili Lulu la kuua bila kukusudia na kwamba kwa mujibu wa shtaka hilo mshtakiwa ana haki ya kupata dhamana.
   Upande wa Jamhuri, ulidai kuwa hauna pingamizi la maombi hayo na kwamba mahakama ijielekeze kwenye kifungu cha 148 kidogo cha (6)ambacho kinamtaka mshtakiwa kufuata masharti yatakayotolewa chini ya kifungu hicho.
   Jaji Mruke alisema kosa linalomkabili mshakiwa lina dhamana kisheria na kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kufuata masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.
  "Tukubaliane wote kwamba hakuna ubishi roho ya mtu imepotea hivyo sheria lazima ifuatwe... pia mshtakiwa awasilishe hati zake za kusafiria, kuripoti kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha msajili huyo" alisema Jaji Mruke.
   Alisema Msajili wa Kanda ya Dar es Salaam ahakiki masharti ya dhamana kabla ya mshtakiwa hajaachiwa kwa dhamana.
   Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba bila kukusudia.

  0 0


   Finally its happening  in London, Mfalmeeeeee,

  The one and only, Mzee Yusuf  akijulikana kama King of Taarabu, anakuja London kwa show moja tu Show yenye hadhi, show ya watu wanaojuwa raha za Pwani na show ambayo hupaswi kukosa kuhudhuria.

  Ni kwa kiingilio cha Twenty Pound Only ndani ya The Ville 640 Ripple Road BARKING.
  Njoo upandishwe Jahazini, Njoo Tulambe na Njoo unukie marashi huku tukionja raha za Mpenzi Chocolate,
  Yaaaani itakuwa Hatari Bin Dangerrrr

  0 0

  Na Bin Zubeiry
  Ferroviario wakiwa mbele ya basi la Azam FC liliwapokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Azam inacheza kwa mara ya pili mwaka huu michuano hiyo ya Shirikisho, baada ya mwaka jana kutolewa hatua ya 16 Bora na AS FAR Rabat ya Morocco, ikiwa chini ya kocha Muingereza, Stewart John Hall, aliyejiuzulu Novemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog. 
   Azam imekuwa kambini katika hosteli zake za kisasa zilizopo Azam Complex kwa muda wote wiki hii tangu baada ya mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar Jumapili, ambayo walishinda mabao 4-0 Chamazi. Viingilio katika mchezo huo vinatarajiwa kuwa Sh. 7, 000 kwa jukwaa la VIP A, Sh. 5,000 VIP B na mzunguko Sh. 2,000. 
  Mwenendo wa timu ya Azam chini ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon ‘Simba Wasiofungika’ kwa ujumla ni mzuri, hadi sasa ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu kati ya tisa tangu aanze kazi mwezi uliopita. 
   Azam inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, ni timu pekee inayoendeshwa kisasa nchini ambayo matarajio ni kufuata nyayo za klabu nyingine bora Afrika kama TP Mazembe ya DRC. Omog alisaini mkataba ma Azam Desemba mwaka jana akitokea klabu ya A.C Leopards ya Kongo Brazavville ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013) na kumaliza ukame wa mataji wa miaka 30. 
   Aliiachia timu hiyo ubingwa wa Kongo akiwazidi wapinzani wao, Diables Noirs kwa pointi 10 kutokana na kukusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18. Mwaka juzi (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia. 
   Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38. Kadhalika mwaka jana, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini. 
  Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.

  0 0

  21
  Na Edwin Moshi, Makete
  Kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria barabarani miongoni mwa madereva bodaboda wilayani Makete mkoani Njombe kunakopelekea madereva hao kukamatwa na askari wa usalama barabarani mara kwa mara, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amefanya kikao na waendesha bodaboda hao
  Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete, waendesha bodaboda hao walipata fursa ya kutoa kero zao na kuuliza maswali ambayo yalikuwa yakijibiwa papo kwa papo na Muu wa polisi wilaya ya Makete, askari wa usalama barabarani na Meneja msaidizi wa TRA Makete
  Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) Alfred Kasonde amekanusha vikali tuhuma zinazoelekezwa kwa askari wake kuwa wanakula fedha wanazotoza kama faini kwa vyombo vya usafiri wanavyotoza kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa ni vingumu kwa askari ambaye amekuandikia faini ya kosa lako kwenye kitabu cha serikali kula fedha hiyo
  Bw. Kasonde amesema askari wake hawana vitabu vya risiti na hawaruhusiwi kutembea navyo kwa kuwa jeshi la polisi lina wahasibu wanaokusanya fedha hizo, hivyo kwa wilaya ya Makete dereva akiandikiwa faini na askari, askari haruhusiwi kupokea fedha na badala yake atakuandikia karatasi maalum maarufu kama notification na baada ya hapo dereva huyo atakwenda kulipa faini hiyo kituoni
  Amewataka madereva hao kuacha kuwapa fedha ya faini askari hao na badala yake wahakikishe askari aliyewakamata anaandika kosa hilo kwenye kitabu cha faini, huku akionesha rundo la risiti za madereva bodaboda ambao wamelipia faini lakini hawajafika kuchukua risiti zao kwa madai kuwa fedha walizotoa zililiwa na askari
  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro amewataka madereva hao kuhakikisha wanajikamilisha kwa vitu vyote vinavyohitajika kama sheria za usalama barabarani zinavyolelekeza ili kuepukana na adha ya kukamatwa mara kwa mara na askari na kutozwa faini.
  Mh Mariro amesema ni kweli madereva wengi hawajui sheria za usalama barabarani lakini sheria hazitambui kuwa hawafahamu sheria, hivyo ili kuepukana na adha hiyo wanatakiwa kuwa na vitu vyote vinavyohitajika kama leseni ya udereva, leseni ya biashara, bima, kadi ya pikipiki, stika ya nenda kwa usalama, kofia ngumu(helment 2) pamoja na pikipiki yenye vyake vifaa vyote.
  Amesema kwa kulitambua hilo mkuu huyo atafanya mazungumzo na chuo cha VETA Makete kifanye mafunzo maalum kwa madereva hao kwa gharama nafuu ili wazifahamu sheria za usalama barabarani pamoja na kupata leseni za udereva.
  Katika kikao hicho madereva hao walikuwa wakiuliza maswali mengi ya ufahamu ambapo walijibiwa maswali yao yote na kuondoka kwa furaha na uelewa wa mambo mbalimbali ya usalama barabarani
   Kikao cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo.
  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akionesha kitabu cha polisi kwa ajili ya kutoza faini za makosa ya usalama barabarani.
  Mkuu wa polisi(OCD) wilaya ya Makete Alfred Kasonde akionesha risiti za faini ambazo zimetelekezwa na baadhi ya madereva ambao wengi wao wamekuwa wakilalamika kuwa fedha hizo zimeliwa na askari.
   Meneja Msaidizi wa TRA Makete Hamis Zumba akifafanua jambo kwa madereva bodaboda Makete.
   Dereva bodaboda aliyejitambulisha kama Alex akiuliza swali kwenye kikao hicho
   Mwalimu wa VETA Makete Bw. Mathew Komba akifafanua jambo kwenye kikao hicho

  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Dr. Asha Rose Migiro, alipofika nyumbani kwake Mbweni kwa ajili ya kutambulisha.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Dr. Asha Rose Migiro, alipofika nyumbani kwake Mbweni kwa ajili ya kutambulisha.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dr. Aziz Mlima, alipofika nyumbani kwake Mbweni kwa ajili ya kutambulisha. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hizo za kuhamasisha jamii na makundi mbalimbali kuchangia na kumjali mtoto aliye katika mazingira hatarishi na yatima zinalenga kuwasaidia watoto zaidi ya 12,000 hadi kufikia mwisho wa kampeni yaani mwaka 2016.  
  Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hizo za kuhamasisha jamii na makundi mbalimbali kuchangia na kumjali mtoto aliye katika mazingira hatarishi na yatima zinalenga kuwasaidia watoto zaidi ya 12,000 hadi kufikia mwisho wa kampeni yaani mwaka 2016.Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitia saini sehemu maalumu kutoa ujumbe wake mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine fedha zitakazopatikana katika kapeni hiyo zitahakikisha zinaongeza idadi ya vituo vya SOS kuwasaidia watoto yatima na waliopo katika mazingira hatarishi. Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitia saini sehemu maalumu kutoa ujumbe wake mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine fedha zitakazopatikana katika kapeni hiyo zitahakikisha zinaongeza idadi ya vituo vya SOS kuwasaidia watoto yatima na waliopo katika mazingira hatarishiKatibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Anna Maembe akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua kampeni.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Anna Maembe akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua kampeni.

  0 0

  Kwa video hii na zingine kibao nenda youtube 
  kisha search 'Club Rahaleo show'

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipokea shada la maua na kusalimiana na Mkurugenzi Mkuu na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kimataifa ya Mahindra& MahindraLtd,Bw.Ruzbeh Irani,wakati alipowasili katika Makamo Makuu ya Kiwanda kinachotengeneza Matrekta cha Mahindra & Mahindra Ltd Mumbai Nchni India 
   Baadhi ya watendaji katika kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd wakiwa katika mkutano uliowajumuisha watendaji wa kampuni hiyo na Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ulipofika katika kiwanda hicho
   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Mali Asili Affani Othman Maalim aliuliza suala wakati wa mkutano wa watendaji wa  Kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd ,inayotengeneza matrekta na Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ulipofika katika kiwanda hicho
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika Trekta jipya kabisa ambalo bado lipo kiwandani baaba ya kukamilika uundwaji wake,alipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd ,inayotengeneza Matrekta Mjini Mumbai Nchini India,ambacho ni maarufu sana Duniani
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kwa Meneja Mkuu wa Uzalishaji na Uuzaji  (RO) Subodh Arora alipokuwa akiangalia Matrekta ya mfano katika uzalishaji katika Kampuni ya Utengenezaji Matrekta Mahindra&Mahindra Ltd alipotembelea akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi Mumbai Nchini India
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Uzalishaji na Uuzaji  (RO) Subodh Arora walipotembelea kuwa akiangalia Matrekta katika kiwanda cha Kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd ,inayotengeneza Matrekta Mjini Mumbai Nchini India, katika ziara rasmi Mumbai Nchini India
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa  Mahindra & Mahindra Ltd baada ya mazungumzo mafupi alipofika kutembelea Kazi mbali mbali Kiwandani hapo jana,akiwa katika ziara ya Kiserikali Mjni Mumbai India. 
  Picha zote na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kutembelea miradi ya mji wa Mvomero na Mlali, Kata ya Mlali, Tarafa ya Mlali mkoani Morogoro.

  Mhe. Makalla ameridhishwa na kiwango cha mradi wa maji wa mji wa Mvomero na mpango kazi wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

  “Nakubaliana na mpango kazi wenu na ninaamini kuwa mpaka mwezi wa tano, mtakuwa mmekamilisha mradi huu na kukabidhi kazi kwa Serikali na wananchi wa jiji la Mvomero waanze kupata maji”, alisema Mhe. Makalla.

  “Napenda kusisitiza mkandarasi aachane na siasa na kurudi mahali pa kazi na kuanza kazi mara moja na kama kuna mambo yoyote, tutakaa chini na kuzungumza wakati kazi ikiendelea. Kinachotakiwa ni mradi kukamilika kwa wakati na maji yapatikane”, aliongeza Naibu Waziri.

  Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji, ameweza kuona hali ya utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali katika mkoa wa Morogoro huku akisisitiza atahakikisha lengo la Serikali kuwapa wananchi wake maji linatimia.
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akifungua rasmi mradi wa maji wa Kigugu.
  Mhandisi Mkazi akimsomea ripoti ya mradi wa mji wa Movemero, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
  Mradi wa maji wa mji wa Mvomero.
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa katika kituo cha kusukumia maji cha mradi wa maji Malali.
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, akizungumza na wananchi wa Mlali.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Bwana Joe Ricketts ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Opportunity Education Foundation ya Marekani.Rais Kikwete alimwandalia mgeni wake chakula cha usiku.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa zawadi ya kinyago cha mpingo Bwana Joe Ricketts wakati wa chakula cha usiku alichomwandalia ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.Bwana Ricketts amezifadhili shule kadhaa hapa nchini kwa teknolojia ya teknohama kwa kuzipatia tablets kuboresha mbinu za kisasa za kujifunza(picha na Freddy Maro)

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.Nape alisema kitendo cha wana CCM kushambuliwa ni kitendo cha kinyama na kinatakiwa kikemewe na kila mtu,pia alisisitiza Vijana wa CCM kuwalinda wapigaji kura wao siku ya kupiga kura.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitazama picha ya X-Ray  ya Sebastian Masonga Katibu wa UVCCM kata ya Majengo Wilaya ya Kahama,Masonga amevunjika mkono wa kushoto baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema wakati walipokua wanarejea kwenye mikutano ya  kampeni za Udiwani.
  Katibu wa NEC Itikadi na uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimpa pole Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambaye alipigwa na kutobolewa macho na wafuasi wa Chadema .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoka nje ya jengo la hospitali ya Bugando akiongozana na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza ambapo waliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi walioumizwa na wafuasi wa Chadema mjini Kahama.

  0 0

  Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao ya kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.

  Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.

  Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.

  Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hazihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa. 

  Hata hivyo Mh. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

  Imetolewa na 
  Ofisi ya Mh. Edward Ngoyai Lowassa 
  Mbunge wa Jimbo la Monduli.

  0 0
 • 02/07/14--19:00: ngoma azipdendazo ankal
 • Mzee mzima Lionel Richie na ngoma yake ya 'All night Long' si mchezo - Makala hii ni kwa udhamini wa The Legend is Back @ Isumba Lounge, Dar es salaam

older | 1 | .... | 351 | 352 | (Page 353) | 354 | 355 | .... | 3348 | newer