Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

KAMISHNA WA SENSA ATOA SOMO KWA WADADISI NA WAHARIRI WA MADODOSO YA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI 2014 KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI

$
0
0
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akizungumza na Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo ya siku 16 leo mjini Morogoro. Kulia Bw. Mhidini Mtindo, Mtakwimu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya watu wenye uwezo wa kufanya Kazi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara wakiwa kwenye mafunzo ya siku mjini Morogoro.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akiwa katika picha ya pamoja na Wadadisi na Wahariri kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo ya siku 16 leo mjini Morogoro.


TAARIFA YA MSIBA WA BIBI MAGDALENA ONGUKA ALLONGA (MEME)

$
0
0
KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE JOHN ALLONGA WA BUTURI RORYA, NAPENDA KUWAJULISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE KUWA BIBI YETU MPENDWA MAGDALENA ONGUKA(MEME) AMEAGA DUNIA TAREHE 5.2.2014 KATIKA KIJIJI CHA BUTURI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 108 MIPANGO YA MAZISHI YANAFANYIKA KIJIJINI BUTURI, BIBI AMEACHA WATOTO WANNE, WAJUKUU 35 NA VITUKUU 42.

TUTAPEANA TAARIFA YA TARATIBU ZITAKAVYOKUWA

Michael G.Allonga
Mjukuu wa Marehemu

JAJI MSTAAFU RAYMOND MWAIKASU APENDEKEZA VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA WAINGIZWE KWENYE RASIMU YA KATIBA

$
0
0
JAJI mstaafu Raymond Mwaikasu amependekeza Viongozi wa jeshi la magereza waingizwe  katika rasimu ya katiba kwa sababu ni watekelezaji wa sheria za nchi  husika   hivyo viongozi wakuu wa magereza washirikishe katika kamati ya ulinzi na usalama wa taifa kwa sababu ni sehemu ya nchi washirika.
Akizungumza katika warsha iliyofanyika  mjini Iringa yenye lengo la kuwajengea  uelewa wa katiba pamoja na mchakato wa marekebisho ya katiba kwa wananchi waishio wilaya ya Iringa vijijini,  alisema kuwa viongozi wa Magereza waingizwe katika kamati ya ulinzi na usalama wa Taifa ili kuweza kutoa taarifa kwa kamati juu ya yanayotokea gerezani na wanayokabiliana nayo katika magereza.
Kwa upande wake  Mkurugenzi mkuu John Msika alisema kuwa jeshi la magereza halijatajwa kama ni sehemu ya muungano hivyo halimtambui katika kuidhinisha adhabu.
“Mkuu wa jeshi la magereza aidhinishe kama mmoja wa wanakamati na mjumbe katika kamati kuu ya ulinzi na usalama “alisema Msika
Naye mkurugenzi wa mafunzo na utafiti Erick Nyato alisema kuwa Muundo wa serikali tatu utahimiza na kujari maadili na miiko ya viongozi wa umma kupunguza mamlaka ya Rais katika uteuzi wa viongozi mbali mbali.

Suala la serikali tatu sio kuvunja amani hili ni suala la uongozi kama itashindikana ni kubadilisha uongozi kwa sababu ni maamuzi yetu wenyewe wananchi .

NEWS ALERT: WAKULIMA WA MELELA, MOROGORO WAFUNGA BARABARA KUSHINIKISHA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA WAO

$
0
0
Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. 

Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi,Wilayani Mvomero,walilazimika kufunga barabara hiyo ili iwe shinikizo la kufika kwa Mkuu huyo wa Mkoa na kuwasikiliza ikiwezekana kutatua kabisa tatizo lao.

Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kujeruhiwa vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika katika eneo hilo mapema leo na kutaka kuwasikiliza wananchi hao,ambao wakati huo walikuwa wamechoma matairi kukata miti,hali iliyopelekea kuwepo kwa mgongamano mkubwa wa magari yaendayo mikoani,lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza na kumtaka aje Mkuu wa Mkoa. 

Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wakatulize ghasia hizo na kuwataka wakulima kuondoka katika eneo hilo na wale waliokaidi walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.
Askari wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.

Askari wa Polisi wa Kikosi cha kutuliza Ghasia akizima  Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa mapema leo Asubuhi.
 Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wamkitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.Picha na Matukio TZ

MCHUNGAJI MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI, AACHIWA KWA DHAMANA NI KUTOKANA NA KESI YA KUJERIHI

$
0
0
Na Francis Godwin, Iringa 
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alisema Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli, mjini Iringa.
 Alisema Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita kinyume na kifungu kidogo namba 225 cha sheria ya kanuni za adhabu. 
Akiwa amefunguliwa kesi ya jinai namba 28 ya mwaka 2014, Mchungaji Msigwa anayetetewa na wakili Lwezaula Kaijage alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha kesi hiyo itakayotajwa tena Machi 10, mwaka huu kwa kile kilichoelezwa kwamba uchunguzi wake haujakamilika. 
Pamoja na Mchungaji Msigwa, jeshi la Polisi limewapandisha kizimbani Meshack Chonanga (22) na Paulo Mapunda wote wakazi wa kijiji cha Nduli mjini Iringa wakituhumiwa kumjeruhi Alex Mpiluka wakati wa kampeni hizo.
 Watuhumiwa hao walirudisha mahabusu ya mahakama hiyo baada ya wadhamini wao kuchelewa kufika mahakamani hapo. Kama ilivyokuwa kwa Mchungaji Msigwa, nao kila mmoja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana ya ahadi ya Sh Milioni 2.
Akitoka mahabusu ya mahakama hiyo
Akiwasalimu wafuasi wake

Ndani ya mahakama

MKUU WA BIASHARA ENDELEVU WA VODACOM AKAGUA MAENDELEO YA ELIMU YA MAFUNZO YA KOMPYUTA KATIKA SHULE YA SEKONDARI KAMBANGWA

$
0
0
 .Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,wakijisomea kupitia kompyuta darasani
 Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom "Vodacom Foundation"Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimsikiliza  Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni hiyo Suraya Hamdulay,wakati alipotembelea darasa la mafunzo ya kompyuta katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.
 Mwalimu wa somo la kingereza wa shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Editha Mwinuka(wapili kutoka kushoto)akimwelekeza mwanafunzi wa kidato cha tatu Barnaba Siyame jinsi ya kupata matirio ya kujisomea katika kopyuta wakati Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kulia)alipotembelea Shule hiyo kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Theresia Ng'wigulu.
 Mwalimu wa somo la kingereza wa shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Editha Mwinuka(wapili kutoka kushoto)akimwelekeza mwanafunzi wa kidato cha tatu Barnaba Siyame jinsi ya kupata matirio ya kujisomea katika kopyuta wakati Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kulia)alipotembelea Shule hiyo kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Theresia Ng'wigulu.

Shughuli za Msiba wa Mama Theonestina Rweyemamu new york, MAREKANI

$
0
0
Shughuli za Msiba wa Mama Theonestina Rweyemamu zinaendelea vizuri. Leo kutakuwa na misa ya Kumwombea Marehemu saa nne asubuhi kule Mount Vernon, New York na Anwani ya Kanisa ni kama ifuatavyo: The Sacred Heart Church, 115 Sharpe Blvd, South Mount Vernon, NY 10550. Jana heshima za mwisho zilitolewa ambapo Watanzania wengi walifika kuuaga mwili wa Marehemu pale Camelot Funeral Home, 174 Stevens Avenue, Mount Vernon, NY 10550. Chini ni taswira za picha za jana ni kama ifuatavyo:
Sehemu ya Watanzania waliohuzuria kama inavyoonekana kwenye picha. Katika mstari wa kwanza ni watoto wa marehemu na kutoka kushoto ni Diana, Doris na Emmanuel.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania New York, Deogratius Mhella naye aliiwakilisha Jumuiya ya Watanzania. Hapa alipata nafasi ya kusema machache.

Mama Balozi Mwinyi aliyekaa katikati naye alifika kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu na kuifariji familia ya mama Theonestina Rweyemamu. 
 Mama Kiswaga aliyesoma shule moja na Marehemu Theonestina naye akizungumza.

Article 12


TFF YAWAKA WACHEZAJI 9 WA KANEMBWA JKT KUWASILISHA UTETEZI

$
0
0
Wachezaji tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).
 Utetezi huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.
 Kamati ilikutana jana Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko dhidi ya wachezaji hao na timu yao kwa tukio hilo lililotokea Novemba 2 mwaka jana kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Stand United FC iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
 Wachezaji hao ni Abdallah Mgonja, Bariki Abdul, Philipo Ndonde, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement, Mrisho Mussa, Nteze Raymond, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu. Mlalamikiwa mwingine ambaye naye anatakiwa kujitetea ni timu ya Kanembwa JKT.
 Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, Kamati hiyo baada ya kusikiliza malalamiko dhidi ya wahusika na kupokea ushahidi wa aina mbalimbali kutoka kwa mlalamikaji imesema ili iweze kutenda haki katika shauri hilo ni lazima walalamikiwa wapate fursa ya kusikilizwa.
 Katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliyokutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa imesema imesikitishwa na vitendo vya fujo ndani ya mpira wa miguu, na kuwataka watu wasijihusishe na aina yoyote ya fujo.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Weekend Special' ya Brenda & The Big Dudes bado moto - Makala hii ni kwa udhamini wa The Legend is Back @ Isumba Lounge, Dar es salaam

TAARIFA YA MKUTANO KWA WANA WERUWERU JUMAMOSI CINE CLUB, MIKOCHENI, DAR ES SALAAM

$
0
0
NOTICE IS HEREBY Given that a General Meeting of the foundation will be held at Cine Club, Mikocheni/Msasani, Dar es Salaam on Saturday, 8th February, 2014 at 10.00hrs. 

 Mkutano wa Weruweru Alumnae Foundation utafanyika Jumamosi tarehe 8 Februari 2014, Cine Club, Mikocheni/Msasani, Dar es Salaam kuanzia saa Nne (4) asubuhi Tafadhali mtaarifu Golden Girl mwingine

TANAPA WAWATIA MBARONI WAUZAJI WA PEMBE FEKI ZA FARU

$
0
0

Mmoja wa watuhumiwa akiwa na 'mzigo' wake ambao ni feki...

Waziri Kabaka azindua Baraza la Wafanyakazi SSRA

$
0
0

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA, Bagamoyo leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, akisoma hotuba yake na kisha kumkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji, Sarah Kibonde Mkataba wa Huduma kwa Wateja, wakati wa uzinduzi huo. Kushoto niMkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA. Kulia anayepiga makofi ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawa wa wizara hiyo, Noah Mwaikuka.
Mwakilishi wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Athuman Juma, akisoma risala ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi, lililozinduliwa naWaziri wa Kazi na Ajira, Gaudetia Kabaka, Hoteli ya Millenium Sea Breeze, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo.Picha zaidi bofya hapa

1 week left to Valentine's Day!

$
0
0
Book your place today at the hottest Valentine dinner event in town. 
Great food, live entertainment and so much more! 
Call 0717 109 362 or 0784 636 169 today

EP Album ya JANB sokoni

$
0
0
Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wanaweza kuinunua ''360 EP Album'' yangu katika vituo vifuatavyo jijini Dar es Salaam na kwa kiasi cha T.SH 5,000 tuu. SamakiSamaki Mlimani city & Posta, Century Cinemax (Movie theater)-Mlimani City, Aziz Barber Shop zamani Prof Jizzle barbershop-Msasani mwisho, Shebby barber shop-Lufungira Sinza, Billionnaires barber shop-Mikocheni kwa Nyerere, Lily's boutique-Mwenge, Ofisi za Bongo5-Msasani, Pia wanaweza kunicheki kwa namba yangu 0756169978 kuinunua kutoka kwangu. 
Asanteni sana kwa sapoti-JANB
Album: 360 EP ALBUM
Artist: JanB
Genre: Swahili Pop & House
Contacts: 0756169978, Instagram@janbizo

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA MANIPAL HOSPTAL INDIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Manipal Hospital Ltd,alipotembelea katika Hospitali hiyo akiwa na Ujumbe wake jana,akiwa katika ziara ya siku tisa Nchini India.[Picha na Ramadhan Othman,India.]
 Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd ya Chuo cha kufundishia Madakatari Bw.Rajan Padukone,akitoa maelezo wakati wa Mkutano kati ya Uongozi wa Hospitali  na Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipofika kutembelea Hospitalini hapo akiwa katika ziara rasmi nchini India. 
  Baadhi ya Maafisa waliofuatana na Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara rasmi nchini India wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyotolewa katika Mkutano wa pamoja walipofika kutembelea Hospitaliya Manipal Ltd 
 Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muungano wakifuatilia vyema maelezo yaliyotolewa katika Mkutano wa pamoja Uongozi wa  Manipal Hospital Ltd hapo jana wakiwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapainduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ambayo inaendelea kwa siku tisa Nchini India ambayo ina malengo ya kukuza uhusiano na mashirikiano.
 Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   akizungumza na Uongozi wa  Manipal Hospital Ltd,katika mkutano wa pamoja wa ushirikiano katika kuongeza utoaji wa huduma za Afya,akiwa katika ziara   inayoendelea katika miji tofauti nchini India,yenye malengo ya kukuza uhusiano katika nyanja mbali mbali zikiwemo  Kilimo, Afya na Biashara,(kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd Bw.Rajan Padukone
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk,Saleh Mohamed Jidawi,akitiana saini ya makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd, Rajen Padukone katika Mji wa Bungaluru nchini India, makubaliano hayo yatanufaisha Madaktari wa Zanzibar kuja kujifunza kazi    katika Chuo cha Hospitali hiyo,saini hiyo imetiwa wakati Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika ziara Nchini India. Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

TANZANIGHT DAY IN SOUTH KOREA

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa rasimu ya katiba kwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad   wakiongozana na Sehemu ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa,wakitoka katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Picha na Issa Michuzi.
Video ya hotuba nzima ya JK inaandaliwa....itarushwa punde tu.

HOSPITALI ZATAKIWA ZITUMIE VYANZO VINGINE VYA KUNUNUA DAWA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Dkt. Kebwe Kebwe amewataka viongozi wa halmashauri kushirikiana na waganga wakuu kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kupitia Bohara Kuu ya Dawa MSD vinatumika ipasavyo.

Dkt. Kebwe alisema hayo jana wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara ya kwanza toka uteuzi wake kutoka kwa Rais Kikwete wakati akiwa na kamati ya kudumu ya Bunge  huduma za jamii kukagua taratibu za usambazaji dawa vituo na hospitali za Serikali.

Katika ziara hiyo amezitaka Hospitali za Serikali kutumia vyanzo vingine vya mapato ili kuweza kununua dawa na vifaa tiba katika kuongezea matumizi mbalimbali na bajeti ya Serikali.
“ni muhimu kuelewa kuwa hospitali inavyanzo vingi vya mapato wakati umefika sasa kutumia fursa hizo katika kuhakikisha mapato yanayotokana na vyanzo vya hospitali yanatumika pia katika kuongeza ununuaji dawa na vifaa tiba ili kuipa uwezo Serikali na jamii kufikia huduma ipasavyo”alisema

Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii Magreth Sita alisema ni muhimu suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupewa kipaumbele cha hali ya juu kutokana na kuwa ndio msingi wa huduma bora za afya kwa jamii.

Alisema kutokana na ufanisi mkubwa uliopo katika upatikanaji dawa hospitalini na vituo vya afya baada ya mfumo wa ufikishaji dawa moja kwa moja hadi vituoni (DD) unaofanywa na MSD ni vizuri Serikali kutambua kuwa ufanikishaji wa hatua hiyo unahitaji uwezeshi hasa wa fedha za  bajeti kufika kwa wakati.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya wadhamini MSD Dkt Ahmed Hingola alisema endapo Serikali itadhiti na kuhakiki dawa chache zilizopo ili kutekeleza mahitaji ni wazi lawama za wananchi kwa bohari ya dawa zitakwisha.

“MSD kazi yake kubwa ni upelekaji wa dawa huku usimamizi wa matumizi katika kutumika kama ilivyokusudiwa ikiwa bado ni changamoto hasa katika sehemu husika hivyo MSD imeanza harakati za uwekaji wa nembo dawa za Serikali (GoT) ili kudhibiti dawa hizo zisiweze kupita njia za panya”alisema

MCHAKATO WA KATIBA: JK AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA JIJINI DAR ES SALAM

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images