Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 349 | 350 | (Page 351) | 352 | 353 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari 5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.

  Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.

  Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana.

  Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo.

  Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza.

  Rene Meza
  Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania.

  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mohammed Said Mohammed amabe ni Mgeni Rasmin katika siku ya Cancer Duniani iliyo adhimishwa jana 04/2/2014 ofisini kwao Mpendae (kulia) Dkt. Msafiri Marijani ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ja maradhi ya Cancer Zanzibar (ZCA).
  Mwenyeki wa Jumuiya ja maradhi ya Cancer Zanzibar (ZCA). Dkt. Msafiri Marijani akitoa maelezo juu ya ukonjwa hatari wa Cancer katika madhimisho ya siku Cancer Duniani iliyoadhimishwa jana Mpendae Zanzibar.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika madhimisho ya siku ya Cancer Duniani iliyoadhimishwa jana Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0

  Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa utekelezaji wa mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji, Nishati , Uchukuzi na Utafutaji wa Rasilimali).

  Mfumo wa BRN unaweka wazi malengo pamoja na kuainisha uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.

  Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa karibu sana na OR-UUM.

  Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. 

  Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  Mikutano hii inalenga kutatua changamoto Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa.

  BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji.

  Ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha mfumo na taratibu za ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake stahiki katika kutekeleza BRN

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakitia saini makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya Kiislamu ya PBZ Mpirani mjni Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Abrahamani Mwinyi.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili ambapo PBZ itachukua jingo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi na Wizara ya Biashara itachukua Jengo la Makao Makuu ya sasa ya PBZ la Darajani.
  Baadhi ya Maofisa wa PBZ wakiangalia utiaji saini wa makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Benki hiyo na iliyokuwa Ofisi ya Shirika la Biashara ya Magari lililochini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
  Picha ya pamoja ya maafisa wa PBZ na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko baada ya kumalizika hafla ya makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Taasisi hzo mbili iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya kiislamu ya PBZ Mpirani mjini Zanzibar. Picha no.05- Jengo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa ajili ya kujenga Makao Makuu Mapya ya Benki hiyo.
  Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) liliopo Darajani Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyenyoosha mikono) akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam wakati alipokutana na Kamati ya Bunge ya Miundombinu. Kulia kwa Waziri Magufuli ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Eng. Gerson Lwenge na anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba na wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba (mbele mwenye koti la suti) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Segerea Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ujenzi wa barabara ya Mbezi kupitia Malambamawili kuelekea Kifuru hadi Kinyerezi.


  0 0

  Representative of Permanent Secretary of Ministry of Transport Eng Edwin Mujwahuzi (Director of Transport and Infrastructure) presenting a speech on behalf of Permanent Secretary of Minister of Transport during the opening ceremony of GFCS kick off meeting on adaptation programme in Africa- Building resilience on disaster risk management, food security, nutrition and health.
  GFCS Kick off meeting participants from Ministry of Transport, Tanzania Meteorological Agency, World Meteorological Organization, Ministry of Health and Social Welfare, Ministry of Agriculture and Food Security, Disaster Management Department, World Health Organization, World Food Programme, Embassy of Norway, International Research Institute, International Federation of Red Cross and Red Crescent Societies (IFRC), Center for International Climate and Environmental Research-Oslo (CICERO), Climate Change Agriculture and Food Security CCAFS, National Malaria Programme, University of Dar es Salaam (UDSM), Sokoine University of Agriculture (SUA), Climate Consult, Centre for Weather Climate Application and Research (CWCAR), Environmental Protection Management Services (EPMS), and Tanzania Redacross Society TRCS in a group photo.

  0 0

  Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba 
   Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa 
  Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
   Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
   Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.
   Kipa wa Mtibwa Hasani  Sharifu  
   Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo
   Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.
   Simba wakishangilia Goli lao lilofungwa na Khamis Tambwe Bao lililofungwa dakika 50 ya mchezo.

  Mpira Umemalizika Mtibwa 1 -1 Simba. Goli la Mtibwa Sugar Lilifungwa dakika ya 18 ya Mchezo bao Lililofungwa na Mussa Mgosi .Hadi Mapumziko Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa Goli Hilo Moja.Kipindi cha Pili Mpira ulianza kwa kasi Simba walishambulia Lango la Mtibwa mara kwa mara Na kujipatia bao la Kusawazisha katika dakika ya 50 ya Mchezo.Katika Mchezo Mchezaji wa Mtibwa Shaban Nditi Alionyeshwa kadi Nyekundu Dakika ya 69 baada ya Kutoa maneno Machafu kwa Mwamuzi.Dakika ya 72 Said Ndemla anaingia Kuchukua nafasi ya  Haruna Shamte,Dakika ya 75, Juma Mpakala Aliingia Kuchukua nafasi ya  Jamal Mnyate. Dakika ya 87  wanafanya mabadiliko ya mwisho, aliingia Abdallah Salum Kuchukua nafasi  Mgosi..

  0 0

  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.

  Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki  anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.

  Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi  Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.

  Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi  Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .

  Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.

  Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji   anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.

  Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe  Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi  (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,   Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.  
     
  Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.

  Imetolewa na:
  Advera Senso-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi

  0 0

  Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu (MMHEN) liliyopo Mikocheni, Regent Estate, Dar es Salaam, anapenda kuutangazia umma kuwa tarehe 06/02/2014 kuanzia saa 02:00 asubuhi Shirika, pamoja na Taasisi zake zikijumuisha Kairuki Hospital (KH), Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) na Mikocheni School of Nursing (MSN) wataadhimisha miaka 15 ya kutokwa na muasisi wa MMHEN na Taasisi zake PROF. HUBERT CLEMENCE MWOMBEKI KAIRUKI .

  Katika kuadhimisha siku hiyo, MMHEN na taasisi zake zilizo chini ya zitatoa huduma ya afya bila malipo kwa jamii pamoja na uchangiaji wa damu kwa hiari kwa ushirikiano wa BLOODAT na DAMU SALAMA itakayotolewa katika viwanja vya shule ya msingi Mikocheni kwa muda wa siku mbili (2) kuanzia tarehe 05/01/2014 hadi 06/02/2014. Shughuli hizi zitafuatiwa na mada (public lecture) itakayotolewa na Dr. Kaushik Ramahiya kutoka Hindu Mandal Hospital kuanzia saa 8:30 mchana ukumbi wa mihadhara , ghorofa ya tano hapo HKMU.

  Pamoja na kutoa huduma ya afya bila malipo, Mwenyekiti wa MMHEN pia atakabidhi jengo la madarasa manne (4), ambalo limekarabatiwa na Kairuki Hospitali, vifaa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya shule pamoja na msaada kwa wahanga wa maafa ya mafuriko yaliyotokea Dumila mkoani Morogoro, hivi karibuni.

  Kwa taarifa zaidi, wasiliana na : Gerlad Manongi manongiss@yahoo.co.uk 0715 847 444 or 2700021-4 : Arafa Juba 0715 289 264 arafamody@yahoo.com E-mail : info@kairukihospital.org Website: www.kairukihospital.org

  0 0

  Mkufunzi kutoka  Shirika la Opportunity Education Foundation (OEF), la Marekani, Lisa Beth Walker, akitoa mafunzo kwa walimu wa shule ya sekondari ya Tusiime jijini Dar es salaam kuhusu namna ya kutumia kompyuta za viganjani (tablets) ikiwa ni maandalizi kwa wanafunzi wa shule hiyo kuanza kusoma kwa kielekroniki.


  0 0


  0 0

  As the world marks the International Day for Zero Tolerance to Female Genital Mutilation and Cutting (FGM/C) on 6th has called on government and communities to step up efforts to stop the practice.

  “FGM/C is a harmful traditional practice that results too often in significant health problems for women and girls and violates their human rights, said Ms. Khan.

  “FGM/C is deeply entrenched in the cultural practices of the community and often protected by local leaders, the efforts for its eradication should be directed on and led by the communities to effect change.” Emphasized Ms. Khan.

  Millions of girls around the world are under threat of FGM/C, despite a century of efforts to put an end to it. In the 29 countries in Africa and the Middle East where the practice is concentrated, more than 125 million girls and women have been cut.

  UNFPA projects that a further 86 million young girls worldwide are likely to experience some form of the practice by 2030, if current trends continue. FGM/C is illegal in Tanzania, yet is since 1998 prevalence is stable at 15%. Research shows that women who have been cut are up to 31% more likely to require a caesarean section in delivery, and babies born to women who have been cut are up to 55% February, UNFPA Tanzania Representative a.i, Ms. Mariam Khan UNFPA in the context of delivering as One with partners in Tanzania is working to eliminate FGM/C interventions include:- to educate communities through media and community meetings, raising awareness of the health repercussions for the girls and of the human rights violations resulting in lost potential.

  The organization engages duty bears, decision makers, and community members, including religious leaders, to change attitudes and identify alternative rites of passage.

  Ending the practice depends on how the global and local communities respond. UNFPA and UNICEF are jointly implementing a programme to accelerate the abandonment of FGM/C. Every young girl, regardless of where she lives, or her economic circumstances, has the right to fulfil her human potential, free from coercion, harm or violence. We can ensure that she does, and we must. The sustainable, equitable, inclusive future we all want depends on the actions we take today to ensure the dignity, health and well-being of every girl.

  FGM/C is being practiced variably in Tanzania and it is mostly predominant in Manyara 71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% and Mara 40%. “Nothing justifies the continued practice of FGM/C it is an obstacle to attainment of the health, development and human rights goal not only for girls and women but also for all members of society; In the 21st century, no woman or girl should suffer or die due to FGM/C.

  Addressing the persistent inequalities that negatively affect women's and girl's health and well-being is our unfinished business,” concludes UNFPA Representative a.i Mariam Khan.

  0 0

   Representative of Permanent Secretary of Ministry of Transport Eng Edwin Mujwahuzi (Director of Transport and Infrastructure) presenting a speech on behalf of Permanent Secretary of Minister of Transport during the opening ceremony of GFCS kick off meeting on adaptation programme in Africa- Building resilience on disaster risk management, food security, nutrition and health.
  GFCS Kick off meeting participants from Ministry of Transport, Tanzania Meteorological Agency, World Meteorological Organization, Ministry of Health and Social Welfare, Ministry of Agriculture and Food Security, Disaster Management Department, World Health Organization, World Food Programme, Embassy of Norway, International Research Institute,International Federation of Red Cross and Red Crescent Societies (IFRC), Center for International Climate and Environmental Research-Oslo (CICERO), Climate Change  Agriculture and Food Security CCAFS, National Malaria Programme, University of Dar es Salaam (UDSM), Sokoine  University of Agriculture (SUA), Climate Consult, Centre for Weather  Climate Application and  Research (CWCAR), Environmental Protection Management Services (EPMS),  and Tanzania Redacross Society TRCS  in a group photo.

   Significantly Tanzania will benefit on enhancing availability of wide range of data and climate services by assuring better access to all available information as long as to empower meteorological services to better serve our key customers. Photos by Monica E. Mutoni

  Public Relation Officer-TMA


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyerembe D. Munasa Sabi (kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Usa River.Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Richard Makungwa pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo . Hafla ya uzinduzi wa tawi hili la NMB Usa River umefanyika mwanzoni mwa wiki katika viwanja vya tawi hili mkoani Arusha.

   Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huu wakifurahia ufunguzi wa tawi jipya la NMB Usa River
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyerembe D. Munasa Sabi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tawi la NMB Usa River Bernadetha Mmary mara baada ya kuzindua tawi na kulitembelea ndani.

  0 0

  The one day Nile Basin Imitative meeting kicked off yesterday at Ubungo Maji aimed at forging more relations on implementation of NBI projects among member States.

  Opening the meeting, Deputy Permanent Secretary Ministry of Water, Eng. Mbogo Futakamba insisted the Nile Basin Initiative Coordination meeting to look on the best ways NBI can implement projects more successful He acknowledged the importance of the meeting as it gives opportunity for our country to exchange information, reports on the implementation of the projects among member states.

  “Nile Basin Initiative (NBI) should be our priority because of the challenges facing the program. Challenges like water pollution, climate change, environmental destruction and decrease of water levels in lakes and rivers should be addressed more seriously with all stakeholders” he said.

  The meeting was aimed at disseminating progress report on NBI projects at regional level.

  Tanzania as member of NBI has number projects under umbrella of NBI including NEL Power interconnection between Kenya and Tanzania, Iringa-Mbeya transmission line project, Russumo Falls project and Sustainable development of Mara river Basin project. Participants agreed in principle for the need of frequent consultations, sharing of information among member states and comprehensive sustainability strategy for all projects.

  The meeting was attended by members from the Ministry of Agriculture, Ministry of Energy, Ministry of Foreign Affairs, Ministry of Minerals, TANESCO, and the host, Ministry of Water.
  Deputy Permanent Secretary Eng. Mbogo Futakamaba addressing participants ( not in picture) when he officially opened one day NBI forum at the Ministry of water headquarters at Ubungo Maji yesterday. Left is the Director of Water Resources at the Ministry Mr Hamza Sadiki.
  Participants of the NBI forum in the group photo together with the Deputy Permanent Secretary Ministry of Water Eng.Mbogo Futakamaba.

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom "Vodacom Foundation"Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimsikiliza Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni hiyo Suraya Hamdulay,wakati alipotembelea darasa la mafunzo ya kompyuta katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.
  Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Lay Salumu akimuonesha Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay,jinsi wanavyojifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta mpakato wakati alipotembelea darasa hilo la mafunzo ya kompyuta katika Shule hiyo,kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.
  Mwalimu wa somo la kingereza wa shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Editha Mwinuka(wapili kutoka kushoto)akimwelekeza mwanafunzi wa kidato cha tatu Barnaba Siyame jinsi ya kupata matirio ya kujisomea katika kopyuta wakati Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kulia)alipotembelea Shule hiyo kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Theresia Ng'wigulu.
  Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,wakijisomea .

  0 0

  Mhariri muandamizi wa Gazeti la Financia Report lenye Makao Makuu yake London Nchini Uingereza Bwana Rohit Devan akimuarifu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi azma ya Gazeti hilo ya kutaka kuitangaza Zanzibar Kimataifa katika Nyanja ya Utamaduni, Uwezekaji na Utalii.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Afrika { Africa TV } Bwana Muharami Iddiss akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Cheti maalum cha Africa TV cha kuitumia ZBC – TV kurusha Vipindi vyake.
  Makamu wa Pilio wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Africa TV ulioambatana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Dini mara baada ya mazungumzo yao yalioyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Africa TV Bwana Muharami Idriss na Kushoto yake ni Mshauri wa Africa TV HAPA Zanzibar Bwana Kassim Haidar Jabir. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa,TANAPA,Allan Kijazi akiteta jambo na mwenyekiti wa kamati ya ardhi ,maliasili na mazingira Mh James Lembeli kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo na watumishi wa hifadhi ya taifa ya Tarangire.
  Mwenyekiti wa kamati ya ardhi ,maliasili na mazingira ,Mh James Lembeli akizungumza wakati wa kikao cha kamati yake na watumishi wa hifadhi ya taifa ya Tarangire.
  Mkurugenzi mkuu shirika la hifadhi ya taifa,TANAPA,Allan Kijazi akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya ardhi ,maliasili na mazingira na watumishi wa hifadhi ya taifa ya Tarangire.
  Mhifadhi mkuu hifadhi ya taifa ya Tarangire Stephano Qolli akitoa taarifa ya hifadhi hiyo kwa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira.


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Nasoro Hamid akizungumza na ujumbe toka Norway ulipofika ofisini kwake kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya namna nchi hiyo ilivyoweza kunufaika kwa kuwekeza katika sekta ya gesi mnamo miaka ya 1970. Anayesaini kitabu ni Bw. Alaf Jakobson Meya wa mji wa Hammerfest nchini Norway.
  Meya wa mji wa Alstahaug Bw. Bard Anders akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika ofisini kwa Meya wa mji wa Lindi Bw. Frank Magali mwenye miwani.


  0 0

  Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo na Misaada wa Jumuiya ya Ulaya Mhe. Pierre Amilhat ( kushoto), Bi. Camilla Lombard Msaidizi wa Mhe Pierre (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji Mhe. Nyamtara Mukome (wa pili kulia). Mhe Pierre amekutana leo na Balozi Kamala ofisini kwake Brussels kumweleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na inayopangwa kutekelezwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Ulaya na nchi za ACP.

older | 1 | .... | 349 | 350 | (Page 351) | 352 | 353 | .... | 3285 | newer