Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 348 | 349 | (Page 350) | 351 | 352 | .... | 3285 | newer

  0 0


  From left to right: Juliet Kairuki, CEO, Tanzania Investment Centre, Peniel Lyimo, Deputy CEO, Presidential Delivery Bureau, Mrs Sophia Kaduma, Permanent Secretary Ministry of Agriculture; Hon. Chiza, Minister of Agriculture United Republic of Tanzania, Pierre Luigi Sigismund, Board Member and Head of Global Supply Chain Unilever; Dr Ramadhaan Mwinjika, Permanent Secretary Ministry of Transport; Ambassador Modest Mero, Permanent Representative of the Government of Tanzania to the United Nations in Geneva. 
  =========  ========= ===========
  By A Correspondent .

  Tanzania Investment Centre (TIC) has confirmed that 2014 has kicked to a positive start with respect to investment in the agriculture sector in Tanzania.  As signal of their strong confidence in the Tanzanian investment climate and the country's future economic prospects,  Unilever has chosen the SACGOT corridor to expand its tea project.  The planned investment will triple Unilever’s production of tea from smallholders through outgrowers schemes.  This will not only generate significant export revenue (projected at 110 million Euro), it will also position Tanzanian Tea as an original tea of international repute. 

  As a partner of Tanzania’s SAGCOT initiative, Unilever has expressed its full commitment to ensure that it’s investment also addresses social economic and environmental goals.  Smallholders will be accredited according to the rain forest alliance certification.   The investment will catalyze significant socio-economic development in the Iringa and Njombe regions by creating 10,000 more jobs, enhancing the livelihoods of another 2000-3000 tea small holders, and in total, touching the lives of an estimated 50,000 people. 

   At the recent World Economic Forum Annual Meeting in Davos, Switzerland,  Mr Pierre Luigi, Board member of Unilever, met with the Minister of Agriculture, Honourable Chiza and the team that played a key role in supporting Unilever with the  development of the project and reiterated Unilever's commitment to investing in Tanzania. 

  Mrs Sophia Kaduma, Permanent  Secretary in the Ministry of Agriculture, advised that Unilever has signed an MOU with the Ministry, the Tanzania Tea Board and the Tanzania Smallholder Tea Development Agency, to progress the development of the project in line with the social and economic aspirations of the Government of Tanzania.

   TIC,  Executive Director, Mrs. Juliet Kairuki, confirmed that Unilever had applied and was granted National Strategic Investor Status  in December 2013 at a National Investment Steering Committee (NISC) meeting convened by the Honourable Prime Minister, Hon. Mizengo Peter Pinda in Dodoma. 

  Unilever is a leading global supplier of fast moving consumer goods with operations in 100 countries and sales in 190 countries. It directly employs 30,000 people  and has a turnover of 3.5 billion Euros. Africa remains at the heart of their global business strategy.

  0 0


  0 0

  IMG_0979 
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke. IMG_1007 
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akizungumza na wakazi wa eneo la mradi wa kisima cha maji cha Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya ya Temeke, kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Barabara ya Mwinyi, Yahya Mnali. IMG_1011 
  Wakazi wa eneo la mradi wa kisima cha maji Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya ya Temeke, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala (hayupo pichani). Mradi wa kisima cha maji Tabata Segerea. IMG_1048 
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke.
  ……………………………………………………………………………….
  Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, leo ameendelea na ziara yake ya jijini Dar es Salaam kwa kukagua miradi ya visima vya maji inayosimamiwa na DAWASA maeneo ya Temeke na Segerea.
  Mhe. Makala aliweza kufika kwenye miradi ya visima vya maji maeneo ya Chang’ombe Unubini, Kichapwi na Segerea na kuona namna miradi hii ilivyosaidia kutatua kwa kiasi kikubwa cha tatizo la maji katika maeneo hayo ya jiji.
  Naibu Waziri aliridhika namna miradi hiyo ya kijamii, ambapo Serikali ikishirikiana na wananchi wameweza kutekeleza mpango wa Serikali kuhakikikisha inaleta ahueni kwa kutoa huduma za kuridhisha za maji kufikia mwaka 2015.
  “Napenda kuwashukuru wananchi na DAWASA kwa kazi nzuri iliyofanyika katika miradi hii, na ni dhahiri kuwa mpango wa kutoa huduma nzuri ya maji jijini Dar es Salaam na nchi nzima inaendelea vizuri. Ningependa kuwaasa wananchi wazidi kushirikiana kwa ukaribu na Serikali ili kuhakikisha miradi hii inatunzwa na kuendelea kupanuka zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wenyewe na nchi nzima kwa ujumla”.
  Vile vile Mhe. Makala aliipongeza Kamati ya Jumuiya ya Watumia Maji ya Mradi wa Kichapwi, Kilakala, wilaya ya Temeke kwa uendeshaji mzuri wa mradi huo na kuweza kukusanya pesa nyingi, kiasi cha sh. Mil 11. Huku wakifanikiwa kufungua akaunti mbili za benki kwa ajili ya makusanyo ya mapato na rasilimali kama walivyoagizwa na DAWASA.
  “Pamoja na uchanga wake, Kamati ya Maji ya Kichapwi imefanya vizuri sana katika kutekeleza majukumu yake na hakika ni mfano wa kuigwa nchini na kwa kweli wanastahili pongezi nyingi”, alisema Naibu Waziri.
  Mhe. Makala atamaliza ziara yake ya siku tano jijini Dar es Salaam kesho, kwa kutembelea maeneo ya Ubungo, na baada hapo kwenda Morogoro kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mkoani humo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Meneja Masoko wa SBL, Allan Chonjo (wa pili kushoto). Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Meneja Masoko wa SBL, Allan Chonjo (wa pili kushoto).Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru (wa pili kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam  Shamrashamra ya Uzinduzi wa promosheni ya Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia bia ya SerengetiShamrashamra ya Uzinduzi wa promosheni ya Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti Shamrashamra ya Uzinduzi wa promosheni ya Shinda safari kwenda nchini BrazilBaadhi ya mabalozi wa Bia ya Serengeti wakionesha shoo kwa wananchi baada ya uzinduzi wa Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti Baadhi ya mabalozi wa Bia ya Serengeti wakionesha shoo kwa wananchi baada ya uzinduzi wa Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia bia ya SerengetiUzinduzi wa promosheni ya shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti uliofanyika leo. Uzinduzi wa promosheni ya shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia bia ya Serengeti uliofanyika leo.

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo  Pinda akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Jukwaa la Ardhi Tanzania,Kauli mbiu  yake ni Ardhi yetu ,Watu wetu na Urithi wetu.
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizindua Jukwaaa la Ardhi Tanzania katika ukumbi wa PSPF .kutoka kushoto ni Muhashamu Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ,Alex Malasusa na kulia na Shekhe Ally kutoka Mkoa wa Tanga .
       Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askof Alex Malasusa akimkaribisha Waziri Mkuu  Mizengo  Pinda katika ukumbi wa PSPF kwa ajili ya Uzinduzi wa Jukwaa la Ardhi Tanzania .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza mhifadhi wa Sokwe wa kimataifa Dkt.Jane Goodall wakati mhifadhi huyo alipomtembelea Rais Ikulu na kumwelezea kazi zake mbalimbali za uhifadhi nchini.Dkt.Goodall anajihusisha na uhifadhi wa Sokwe katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma na kazi yake imeipatia Tanzania umaarufu mkubwa Duniani.Dkt. Goodall ni mwanzilishi wa taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na uhifadhi wa Sokwe. Picha na Freddy Maro

  0 0


  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika usiku wa tarehe 2 Februari kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya.
   Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akizungumza na waandishi wa habari na wasanii wa muziki na sanaa za filamu Tanzania kwenye siku ya Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya, katika usiku huo Komba alisisitiza wasanii kuangalia maisha yao ya mbele na sio sasa kwani wasipojiandaa wataaibika hapa ulimwenguni pia alisisitiza juu ya maslahi ya wasanii kuongezwa kutokana na kazi kubwa wanazofanya na thamani ya kazi wayofanya.
   Wasanii wakimpongeza Kapteni John Komba kwa wosia mzuri aliotoa juu yao .
   Msanii Maarufu nchini Hafsa Kizinja akitumbuiza siku ya usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari,Februari 2 mjini Mbeya ,siku ambayo CCM ilisheherekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake na kitaifa sherehe hizo zilifanyika mjini hapo.
   Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakijumuika kumshangilia Mwenyekiti wao wa Kikosi cha Ziara mkongwe Richard Mwaikenda akijimwaga wakati wa sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika tarehe 2 Februari siku ambayo CCM ilisheherekea ktutimiza miaka 37 ya kuzaliwa kwake na sherehe kufanyika kitaifa mkoani Mbeya.
   Wasanii wa tasnia ya Filamu wakiwa wamepozi kwenye sherehe za usiku wa Wasanii na Waandishi
   Msanii wa Siku Nyingi nchini Dokii akisalimiana na  Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri Wizara ya Fedha (Sera) wakati wa sherehe za usiku wa Wasanii na waandishi wa Habari.
   Baadhi ya waandishi kutoka Jjiji la Mbeya wakipata vinywaji na maongezi kidogo wakati wa sherehe fupi za kukutana pamoja na waandishi na wasanii wa muziki na filamu zilizofanyika tarehe 2 Februari mjini Mbeya.
   Waandishi wa Umoja wa Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa sherehe fupi za kupongezana kwa kazi nzuri wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM lakini pia usiku huo ulipewa jina la Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari.
   Wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu Tanzania nao walikuwepo kutoka kushoto ni Baba Haji, JB na Rich.
   Kila mtu maarufu alikuwepo kwenye tasnia ya sanaa za maigizo na filamu.
   Malkia wa Taarab nchini Hadija Kopa akitoa vionjo vya nyimbo yake mpya ambacho kinasema hata Obama anamjua.
  Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi wa CCM Nape Nnauye akiimba sambamba na band ya TOT wakati wa usiku uliopewa jina la usiku wa Wasanii na Waandishi wa habari.

  0 0

  The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) has remitted 1.7bn/- to the Treasury collected from calls in October last year.

  This follows completion of installation of the Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS).

  The amount is from revenue that TCRA collected in one month from firms dealing in telecommunications outside Tanzania whose subscribers made calls to telephone subscribers in Tanzania.

  According to TTMS regulations, the government is entitled to at least 28 percent of incoming calls from outside the country.

  Speaking during the handing over of the cheque, TCRA Director General Prof John Nkoma told Finance Minister Saada Mkuya that TTMS was installed in October 2013 and started work immediately.

  According to Prof Nkoma, the TTMS uses the Build Operate and Transfer system (BOT). He said the system has managed to increase government revenues from the former eight percent to the present 28 percent of the money one pays per minute when calling Tanzania.

  As the government gets 28 percent, the TCRA gets at least 25 percent of the money one pays for making a call to Tanzania. Further, the company that collaborated with TCRA to install the system is entitled to at least 20 percent of the revenues.

  TCRA handed over another cheque of 1.6bn/- to the Treasury in line with the Finance Law of 2008 that obliges institutions that collect revenues to submit to the government ten percent of such revenues. Meanwhile, Innocent Mungy – TCRA’s Manager Corporate Communications, said in an email to The Guardian:

  “For the months of November and December last year as well as January this year, we await to be paid by each operator in Tanzania given the number of minutes terminated in their network.

  “The process requires verification and calculations in terms of the agreed formula.”
  Speaking at the function, Finance Minister Saada Mkuya commended TCRA for installing the system successfully and starting to pay dividends.

  She urged the TCRA to ensure that it motivates workers manning the system so that they continue to collect more revenue for the government.

  0 0

  Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge. Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha ongezeko hili.


  Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.

  Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa Waziri alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio kweli bali ni maelezo binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo Serikalini wala Bungeni.

  Aidha, tunapenda kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha Wabunge na Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana ukweli na uthibitisho wowote.

  KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA
  4 FEBRUARI, 2014

  0 0

  Book your place today at the hottest Valentine dinner event in town. Great food, live entertainment and so much more! 
  Call 0717 109 362 or 0784 636 169today

  0 0

  Naibu waziri wa maliasili na utalii,Mhe. Mahamud Mgimwa akizungumza katika uzinduzi wa madarasa mawili ykatika shule ya sekondari ya Nkoarisambu wilayani Arumeru.
  Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya taifa TANAPA, Bw. Allan Kijazi akitoa taarifa ya kukabidhi mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule  ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru.
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mh James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mhe. James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.
  Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mh Joshua Nassar akizungumza jambo na mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira Mhe. James Lembeli, kulia kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Henry Shekif.
  Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mhe. Joshua Nassari akizingumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.

  0 0

  CHUO CHA RUNGEMBA MISSION, IRINGA, KINATOA NAFASI ZA MASOMO KWA MUHURA WA 2014 ,CHUO KINAFUNDISHA UALIMU WA SECONDARY NA WA SHULE YA MSINGI. CHUO KIMESAJILIWA NA NATE RGE/KLF/011T USAJIRI WA NECTA ,NUMBER YA KITUO CHA MITIHANI E643. 

  KWA MAWASILIANO ZAIDI :
  MKUU WA CHUO:0763833021
  MENEJA WA CHUO: 0763818244
  KARANI:0677987906

  NAFAZI ZA KAZI YA UALIMU CHUO CHA RUNGEMBA MISSION IRINGA CHUO KINATANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI NA WALIMU WA SECONDARI WALIO NA UZOEFU USIOPUNGUA MIAKA 2 NA KUENDELEA.

  KWA MAWASILIANO ZAIDI :
  MKUU WA CHUO:0763833021
  MENEJA WA CHUO: 0763818244
  KARANI:0677987906

  NAFASI ZA MASOMO YA SECONDARI IGAWA MISSION IRINGA INAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO KWA MUHURA HUU 2014,KWA MAWASILIANO :
  MKUU WA SHULE :0763818244

  0 0

  Jahazi lililokamatwa na madawa ya kulevya.
  ZAIDI ya kilo 200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea nchini Irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na Pakistani.
  Kamanda wa polisi kikosi cha wanamaji Bw. Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala Kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
  Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya, Bw. Godfrey Nzowa amesema jahazi hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
  Chanzo: ITV

  0 0

   Manaodha wa Timu ya Moro Veterani na Tanga Veterani  Wakiwa na Waamuzi wa Mchezo huo Uliofanyika Morogoro. 

  Timu hizo zilicheza Mchezo wa Kirafiki Katika Uwanja wa Mochwari mKoani Morogoro Mara daaba ya Timu ya Tanga Veterani Kufanya ziara ya Kudumisha Urafiki na Undugu walionao dhidi ya Timu ya Morogoro Veterani.Katika Mchezo Huo Wenyeji Timu ya Morogoro Veterani Walishinda kwa Jumla ya Magoli 2 kwa Moja.Magoli ya Moro Veterani Yalifungwa na Mokili Rambo dk 35 na 72 Wakati Goli la kufutia Machozi la Tanga Veterani Lilifungwa Dk 80.
  Kikosi cha  Timu ya Tanga Veterani Kilichoanza katika Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya Morogoro Veteran
  Wenyeji wa Mchezo huo Timu ya Morogoro Veterani wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik (Katikati) akikagua baadhi ya mabwawa ya ufugaji samaki manispaa ya Lindi walipotembelea mradi wa uvuvi katika Ziara ya Mameya wa miji ya Norway waliokubali kujenga urafiki na manispaa za Lindi na Mtwara,Kushoto ni Abdilah Salum mmiliki wa mabwawa hayo na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nasor Hamid.
  Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik akipokea maelezo ya hali ya Uvuvi Ndani ya manispaa ya Lindi toka mkurugenzi wa manispaa Kelvin Makonda huku mmiliki wa mabwawa hayo akielezea mipango yake ya baadae ikiwa pamoja na kuiomba Norway kumsaidia Elimu na utaalamu bora wa ufugaji wa Kisasa.


  0 0

  Rais  Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, (kushoto), alipofika kutoa msaada wa sh. milioni 100 wa benki hiyo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita. Dk. Kimei alifuatana na baadhi ya viongozi wa benki hiyo
  Dk. Kimei akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete.
  Dk. Charles Kimei akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi hundi ya Sh, milioni 100 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea mkoani Morogoro.
  Rais  Jakaya Kikwete akipokea hundi ya sh. milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), kwa ajili ya kusaidia watu waliopatwa na mafuriko Mkoani Morogoro hivi karibuni Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,

        THE STATE HOUSE,

                P.O. BOX 9120,  

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  Jumanne, Februari 4, 2014, amepokea hundi ya Sh. milioni 100 kutoka Benki ya CRDB kusaidia waathirika  wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita.


  Rais Kikwete amekabidhiwa hundi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, na kuhudhuriwa pia na Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia pia masuala ya maafa.


  Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi hiyo kwa Rais Kikwete, Dkt. Kimei amesema kuwa fedha hizo ni sehemu ya Sh. Milioni 850 ambayo ni asilimia moja ya faida ya Benki hiyo ambayo hutengwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za jamii.


  “Sote tumeona madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko haya. Watu wengine wamepata hasara – akinamama, watoto, wajawazito na wazee. Hawa wote wanahitaji misaada ya ziada ili kukabiliana na athari za mafuriko hayo,”amesema Dkt. Kimei.


  Akizungumza kabla ya kupokea hundi hiyo, Rais Kikwete ameelezea kwa ufupi mafuriko hayo yaliyotokea alfajiri ya Januari 22, mwaka huu, 2014 na athari ambazo zimetokana na mafuriko hiyo katika maeneo ya Magole, Dakawa na Mateteni huko Dumila, Wilaya ya Mvomero, ambayo aliyatembelea mwishoni mwa mwezi uliopita kujionea madhara.


  “Waswahili husema kuwa ajali haina kinga na ni kweli. Unajua mafuriko yaliyotokea katika eneo la Dumila hayakutokana na wala na mvua ya pale. Mvua ilinyesha kule Kiteto, Mkoa wa Manyara, lakini walioathirika kwa mafuriko ni hawa jamaa zetu wa Dumila. Bahati tu ni kwamba mafuriko hayo yalilikumba eneo hilo alfajiri wakati watu tayari wameamka na ndio maana hakuna mtu aliyepoteza maisha yake katika eneo hilo,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:


  “Watu wamepata hasara kubwa. Baadhi nyumba zao zimesombwa na kuzolewa na maji, nyingine zimebomoka, watu wamepoteza mali zao nyingi kama vile nguo na wengine hata chakula chao kimesombwa na maji. Wanahitaji msaada na kwa kweli sisi katika Serikali tunaishukuru sana CRDB kwa kutoa msaada huu kwa sabababu unachangia katika jitihada za Serikali kukabiliana na tatizo hili.”


  Akizungumza katika shughuli hiyo, Mheshimiwa Lukuvi amesema kuwa tathmini mpya imeonyesha kuwa  watu walioathirika katika mafuriko hayo ni 9,268 na kati ya watu hao kaya 522 hazina makazi kabisa baada ya nyumba zao kubomolewa na maji, nyingi zaidi 466, zikiwa katika Wilaya ya Kilosa.


  Amesema kuwa nyumba 537 zimeharibika hata kama wenye nyumba hizo bado wanaendelea kuishi ndani ya nyumba hizo na nyingine 1,036 ziliingiwa na maji hata kama hazikuharibika.


  Imetolewa na:


  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  04 Februari, 2014
  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam, leo.
  Makamu wa Rais Dkt Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa ofisi hiyo baada ya kufunguliwa rasmi, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR

  0 0

  Balozi Mdogo wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Yunliang akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi Mdogo wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Yunlia aliyefika Ofisini kwake kusalimiana naye. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


  0 0

  Kutoka kushoto ni mratibu mwenza wa Tamasha la Jogging, Mashauri, Mratibu wa Jogging, KP, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mratibu wa Matukio wa Global, Luqman Maloto na Meneja wa Stamina, Said Ramadhani 'Kabwela'.
  Abdallah Mrisho akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
  Mkutano ukiendelea.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
  Mwanamuziki wa Bendi ya Msoondo Ngoma, Said Mabela akizungumzia maandalizi yao katika bonanza hilo.

  Mambo yameiva! Waratibu wa lile tamasha kubwa la mbio za taratibu (jogging) na huduma ya habari mpya zilizotokea punde ya Global Breaking News chini ya Global Publishers wameahidi kufanya makubwa ndani ya Dar Live Jumapili hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza ya Afrika-Sana, Dar leo asubuhi, meneja mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kuwa shughuli itakuwa nzito hivyo watu wafurike kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake.

  “Baada ya jogging, kutakuwa na burudani kubwa ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa, Nay wa Mitego, Stamina, H. Baba na bendi inayopendwa na wengi ya Msondo,” alisema Abby Cool huku akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza Dar Live itaangusha burudani ya nguvu bila kiingilio.

  Kwa upande wake, mratibu wa tamasha hilo la jogging, KP amesema: “Jogging itaanzia pale Uwanja wa Taifa hadi Dar Live. Vikundi zaidi ya 150 vimethibitisha kushiriki. Watu waje kwa wingi kuona mambo matamu bure kabisa kwani hakutakuwa na kiingilio.”

  Naye meneja wa msanii Stamina, Kabwela aliahidi kuwa Stamina amejipanga kufunika vibaya siku hiyo kwani amekuwa kwenye mazoezi ya kufa mtu.

  Mbali na Jogging, Breaking News, pia Global Publishers imetambulisha shindano lake jipya la Global Star Search litakaloanza hivi karibuni kwa lengo la kuibua vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
  PICHA HABARI NA ERICK EVARIST/GPL

older | 1 | .... | 348 | 349 | (Page 350) | 351 | 352 | .... | 3285 | newer