Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Mkutano wa M4C Operesheni Pamoja Daima,Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe Atua Kibaha na Chopa Nakuhutubia Mamia ya Wananchi wa Mji wa Kibaha

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa mji wa Kibaha, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Kibaha, Pwani jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akimkabidhi kadi ya chama hicho, aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kibaha Mjini, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Kata ya Kongowe, Joseph Baziry, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Kibaha jana.Picha na Chadema

KINANA AZURU NYUMBANI KWA MAREHEMU DK. MGIMWA

$
0
0
 Katibu Mkuuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mama Mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Consolata Mgovano, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa, Kijiji cha Magunga, jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, leo jioni. Wengine ni watoto wa marehemu Mgimwa, Stanisla Mgimwa, na Rozalina Mgimwa.
 Kinana akizungumza na familia huyo ya marehemu Mgimwa. Wapili kushoto ni Johakim Mgimwa
 Kinana akimuaga Mama Mgimwa baada ya mazungumzo
 Kinana akiaga
 Mmoja wa wanafamilia akilia Kinana alipotembelea familia hiyo ya Mgimwa
 Nyumbani kwa marehemu Mgimwa
Kinana akipokea saluti ya Kijana wa CCM, alipowasili Ifunda, Iringa Vijijini kabla ya safari ya kwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msavatavangu: Picha na theNkoromo Blog

tukio la kihistoria, JK apiga picha na ma-bloggers, mpiga picha ni kinana

$
0
0
 Mwenyekiti wa wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na ma-bloggers wakubwa wa Tanzania wakati wa kiadhimisha sherehe za miaka 37 za uhai wa CCM uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana hapo chini...

Article 2

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 37 YA UHAI WA CCM KWENYE UWANJA WA SOKOINE, MBEYA, TAREHE 2 FEBRUARI, 2014

wadau KASUKA NA SALOME WAMEREMETA WILAYANI KILWA

$
0
0
Wadau  John Kasuka na Salome Joseph wameremeta  katika kanisa la KKKT Kilwa Masoko mkoani Lindi na baadaye kusherehekea katika mnuso wa nguvu katika ukumbi wa PEC hotel(kwa sultan) Kilwa

Wadau John Kasuka na Bi salome Joseph  wakiwa na nyuso za furaha
baada ya kumeremeta


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa  Addoh
Mapunda ambae ni mwajiri wa bwana harusi akiwapongeza vijana wake


Maharusi wakielekea beach kupata taswira za kumbukumbu
Ni wakati wa kuvalishana pete za kuemremeta kwao

Kasuka na Salome wakiwa katika Taswira ya kumbukumbu na
wanakamati walioandMnuso huo. Globu ya Jamii inawapongeza na kuwatakia maisha ya heri na ya furaha na yenye watoto kibao. 
Picha na Abdulaziz Video, Lindi.

GADO LEO

WAZIRI MAJI AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA MAJI YA DHARURA KARATU

$
0
0
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe mwishoni mwa wiki alitembelea mradi wa maji wa dharura Karatu Mjini kuona utekelezaji wake. Mradi huo mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na upungufu mkubwa wa maji mjini Karatu unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Arusha (AUWSA).

Pia, Prof. Maghembe alitembelea Halmashauri ya Mji wa Karatu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo katika programu ya vijiji 10 ya BRN.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Karatu Mjini.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Moses Mabula.
Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya akisoma Ripoti ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwa Waziri wa Maji, Prof. Jumannne Maghembe.
Miundombinu ya mradi wa maji wa dharura Karatu Mjini.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akiangalia tanki la maji la mradi wa dharura wa Karatu Mjini, huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya.

Maendeleo ya Msiba wa Mama Theonestina Rweyemamu

$
0
0
Familia ya Nestory Mwombeki Rweyamamu ya Mt. Vernon New York imetoa ratiba fupi ya shughuli za msiba wa mama yao mpendwa Theonestina Rweyemamu kama ifuatavyo:
  • Kuaga Mwili wa Marehemu Mama Theonestina Rweyemamu itakuwa Jumatano tarehe 5 Februari 2014 kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili usiku. Mahala: Camelot Funeral Home, 174 Stevens Avenue, Mount Vernon, NY 10550;
  • Misa ya Kumwombea Marehemu itakuwa saa nne asubuhi siku ya Alhamisi tarehe 6 Februari 2014 kwenye kanisa la Moyo Mtakatifu au Sacred Heart Church. Mahala: 115 Sharpe Blvd., South Mount Vernon, NY 10550
  • Taarifa ya lini mwili wa Marehemu utasafirishwa kwenda Bukoba, Tanzania zitafuata baadaye baada ya mipango kukamilika. Mipango hadi sasa ni kumsafirisha Marehemu siku ya Ijumaa kwenda Tanzania.
Watoto wa Marehemu kina Doris, Steven, Emmanuel na Diana pamoja na familia nzima wanapenda kuwashukuru wote kwa kufika kuombeleza nao na kwa rambirambi zenu. 

Pamoja na ratiba iliyotajwa hapo juu, bado mnaweza kutuma rambirambi zenu kwao na kufika nyumbani kuwaona. Address ni: 40 East Sidney Avenue, Apt # 10C , Mount Vernon, NY 10550. Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456.

Familia inahitaji kukusanya kiasi cha Dolla 10,000. Mpaka sasa kiasi cha Dolla 6,000 zimeshapatikana na kuna mapungufu ya dola 4,000. Uongozi unawaomba Wanajumuiya kujitolea ili kufikisha kiasi cha fedha kinachotakiwa. Kwa Wanajumuiya wa Queens na Brooklyn Mweka Hazina Msaidizi Dr. Temba atakusanya michango na kuiwakilisha kwa Familia ya Marehemu (na simu yake ni 646-489-6532) na kwa wanajumuiya wengine tunaomba mwasiliane na familia moja kwa moja au kwa kupitia simu zilizotajwa katika tangazo hili. Familia itashukuru msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama Theonestina Rweyemamu kwa kutoa chochote kwenye Bank of America, account number 483044166145 routing number 021000322 na jina kwenye account ni Doris Rweyemamu.

Kwa maelezo zaidi unaweza piga simu kwa wafuatao:

Emmanuel Rweyemamu 6462342418, Steven Rweyemamu 3028837971, Dr. Abbas Byabusha 9145847502, Doris Rweyemamu 6463799135.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Amen.

Uongozi-Jumuiya ya Watanzania New York.

Mwisho wa Tangazo

Mashindano ya Diwani Cup kata ya Mutuka yazinduliwa huko Mkoani Manyara

$
0
0
Diwani wa Kata ya Mutuka, Wilayani Babati Mkoani Manyara, Mwalimu Yona Wao (wa pili kushoto) akizungumza  na wachezaji wa timu za soka za Mutuka FC na Chem Chem FC wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Diwani huyo.kushoto ni Mwenyekit wa halmashauri ya Mji wa Babati, Mohamed Omary Farah.(picha woinde shizza,Manyara)

Diwani wa Kata ya Mutuka Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Mwalimu Yona Wao amezindua mashindano ya soka kwenye kata yake itakayoshirikisha timu tano za vijiji vilivyopo Mutuka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Mwalimu Wao alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha sh 80,000 mshindi wa pili atajinyakulia sh 50,000 na mshindi wa tatu  atapata sh 30,000.

Mwalimu Wao alisema pia ili kunogesha mashindano hayo kipa bora, mchezaji mwenye nidhamu na mfungaji bora, kila mmoja wao atajinyakulia sh 10,000 na waamuzi wa mashindano hayo watakuwa wanalipwa sh 5,000 kwa kila mchezo.

“Lengo langu la kuzindua mashindano haya kwa timu za Mutuka FC, Chem Chem FC, Sendo Rangers na Endagile FC ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana wa eneo hili,” alisema Mwalimu Mao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati, Mohamed Omary Farah alisema ili kuyapa ladha mashindano hayo atajitolea seti moja ya sare za michezo kwa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo.

“Ili kumuunga mkono Diwani wenu nitatoa jezi kwa bingwa wa mashindano haya na ninyi ongezeni jitihada kwenye kucheza vizuri kwani hivi sasa michezo ni ajira mojawapo inayowanufaisha vijana wengi hapa nchini,” alisema Farah.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mashindano hayo, Dawi Sumai ambaye ni Ofisa mtendaji wa kata ya Mutuka, michezo hiyo itakuwa inafanyika kwa mtindo wa ligi ikichezwa nyumbani na ugenini.

Combating Wildlife Poaching and Illegal Trafficking in Tanzania

Article 19

BALOZI KALLAGHE AKUTANA NA WAFANYABIASHARA, ABERDEEN - SCOTLAND

$
0
0
Mheshimiwa Balozi alifanya ziara ya kikazi wiki iliyopita huko jijini Aberdeen,Scotland kufuatia mwaliko wa Kampuni ya Afro-invest kwa ushirikiano na Scottish Development International (SDI) na Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce (AGCOC).

Lengo la ziara hii lilikuwa ni kwanza, kukutanishwa na Ujumbe wa kibiashara unaotarajia kuzitembelea nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania mwanzoni mwa mwezi wa Febrauri. Pili, ni kujionea shughuli za SDI na AGCOC katika uratibu na uendeshaji wa shughuli za Makampuni ya kibiashara.

Kwa kuwa mji wa Aberdeen ni mahsusi kwa shughuli za mafuta na gesi, ziara hii ilikuwa muhimu sana kujifunza mengi kuhusiana na uendeshaji wa shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta hii.

Hata hivyo moja ya mapendekezo muhimu aliyayotoa Mheshimiwa Balozi kwa wenyeji wetu, ni kuisaidia Tanzania ijijengee uwezo ili iweze kunufaika na rasilimali zake hasa katika sekta mpya ya mafuta na gesi, ambayo hatuna uzoefu nayo.

Njia za uwezeshaji ni kwa Makampuni ya kigeni hasa yatoayo huduma kwenye sekta hii, kuingia ubia na Makampuni ya Tanzania. Njia ya pili ni kwa Makampuni au Taasisi za Mafunzo za Scotland kuandaa programme mahsusi zinazoendana na hali na mazingira ya nchi yetu ambayo ndio kwanza imegundua raslimali hii ya mafuta na gesi.

Pamoja na hayo, wenyeji nao wameishauri Tanzania kuonyesha nia ya dhati ya ushirikiano na Uongozi wa jiji la Aberdeen kwa kufanya ziara na mawasiliano ya mara kwa mara. Lakini muhimu zaidi katika hili wangependa kuona Ujumbe wa kibiashara kutoka Tanzania ukitembelea Aberdeen.

Katika ziara hii, Balozi Kallaghe alifuatana na Mkuu wa Kituo cha Biashara Ndugu Yusuf Kashangwa
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akiongea na baadhi ya Wafanyabiashara, watakao fanya ziara ya Kibiashara nchini Tanzania baadae mwezi huu.
baadhi ya Wajumbe wa Wafanyabiashara, mjini Aberdeen, Scotland, wakijaliana jambo katika mkutano wao na Mhe. Balozi Peter Kallaghe.
Mheshimiwa Balozi Kallaghe, akimsikiliza mkuu wa Kampuni ya Afro-Invest, Bwana Desire Katihabwa, akitoa maelezo ya Kampuni yake na jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kutangaza fursa za Uwekezaji. Wengine pichani ni Dilip Navapurka (pili kushoto) wa Kampuni ya Safarihub na mama Sheila Ritchie, Mwanasheria kutoka Kampuni ya Grantsmith, wakimsikiliza.
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, kwenye picha ya Pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Aberdeen, Kutoka kulia, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Alec Carstairs (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce - President), Dilip Navapurka (tatu kushoto), Julien Masse (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce) na Bwana Smart Masoni, mwakilishi kutoka Kampuni ya Scotish Development International).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP MANGU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 4, 2014, kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 4, 2014, kwa mazungumzo. Picha na OMR

Are you graduate from University of Dar es Salaam (UDSM) leaving in Mwanza city????

$
0
0
University of Dar es Salaam Alumni Event will be held on Friday 07 February 2014 in Mwanza from 5-7pm.Venue will be Mwanza Hotel.

Kindly confirm attendance through 0754-623395 or udsmalumni@gmail.com. This event is for all UDSM (DUCE and MUCE included) graduates from 1964 to 2013 who are in Mwanza.

‘Entrance is free’

For updates please follow us on facebook at

Maadhimisho ya Siku ya sheria nchini yalivyofana mjini Moshi

$
0
0
Jaji Aisha Nyerere akiingia katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake katika Siku ya Shera.
Kikosi cha kutuliza fujo,kikiwa tayari kwa ukaguzi .
Jaji Aisha Nyerere akikagua gwaride maalumu katika viwanja vya mahakama kuu mjini Moshi.

Mbunge wa Ruangwa aanzisha vilabu 102 vya michezo ili vijana wasijishughulishe na mambo ya uhalifu

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, aliyekuwa Ruangwa

 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameanzisha  vilabu  102 vya  michezo kwa kuvipatia jezi na mipira ili kuhakikisha vijana wa jimbo hilo lililopo mkoani Lindi hawajishughulishi na matukio ya uhalifu .

Majaliwa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu TAMISEMI  aliyasema hayo hivi karibuni  wakati wa kilele za sherehe za kutimiza miaka 37 ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika katika kata ya  Likunja wilayani humo.

Katika sherehe hizo Mbunge huyo alizipatia timu za mpira wa miguu za Uhuru City na Mbagala City jezi seti  moja kwa kila timu na mpira mmoja ambapo timu hizo zilipanda uwanjani na kuchuana yote hiyo ikiwa ni kusherehekea  CCM kutimiza miaka 37 .

Baada ya kumalizika kwa mashindano hayo timu ya Uhuru City iliibuka  mshindi wa mabao mawili kwa nunge  dhidi ya timu ya Mbagala City. 

Naibu waziri Majaliwa pia  ameviwezesha vikundi mbalimbali vya ngoma  katika wilaya hiyo ambavyo vinajipatia  pesa kwa ajili ya kazi ya sanaa na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Sherehe hizo zilienda sambamba na maandamano ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi na kupambwa na burudani ya  ngoma za asili, kwaya na mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali kikiwemo kikundi cha Wanapakaya kutoka wilayani Kilwa na msanii Dogo Doto.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA RE-ELECTED TO THE AFRICAN UNION PEACE AND SECURITY COUNCIL (AUPSC)

REDIO 5 WAFUNGUA MWAKA KWA TAMASHA LA BURUDANI.

$
0
0
DSCF2600Timu ya AJTC ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kunyakuwa ushindi katika tamasha la fungua mwaka na redio 5 lililoandaliwa na kampuni ya Tan media jijini Arusha katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
DSCF2564Timu ya Highridge ikipokea zawadi ya saa kutoka kwa mtangazaji Semio Sonyo baada ya kushika nafasi ya pili.
DSCF2557Mashabiki wakiangalia burudani kutoka kwa wasanii wa Arusha
DSCF2553Muonekano wa wachezaji wakiwa uwanjani.
DSCF2627

DSCF2629Jambo squard wakiwapa burudani wakazi wa Arusha.Picha zaidi bofya hapa

WATOTO 287 WAFADHILIWA MASOMO NA COMPASSION IRINGA

$
0
0
 Mgeni Rasmi Daniel Kadinde akimkabidhi zawadi mwanafunzi Monalisa Sungwa aliyefanya vizuri katika masomo yake. Monalisa ni mmoja ya wanafunzi anayesomeshwa na Compassion.
Mgeni rasmi Daniel Kadinde akizungumza na watoto wahitaji katika ukumbi wa kanisa la Anglikana Ipogoro katika siku ya shukrani.
 baadhi ya watoto wenye uhitaji wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na kwaya ya watoto wenzao wa Ebeneza.
  Kwaya ya watoto Ebeneza akitumbuiza katika siku ya kutoa shukrani kwa watoto wenye uhitaji iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana Ipogoro.
 Mwanafunzi bora Monalisa Sungwa akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake wanaosomeshwa na Compassion

=========   =======  =========
WATOTO 287 WAFADHILIWA MASOMO NA COMPASSION IRINGA
Na Denis Mlowe,Iringa
JUMLA ya watoto wahitaji 287 wamefaidika na ufadhili wa masomo ya elimu ya shule ya msingi na sekondari unaotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto cha Anglikana Ipogoro kwa ufadhili wa shirika la   Compassion.
Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi wa kituo hicho Kaini Mwakisyala wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi wakati wa siku ya Shukrani kwa Watoto wahitaji uliofanyika katika kanisa la Anglikana tawi la Ipogoro mwanzoni mwa wiki.
Mwakasyala alisema kuwa watoto walionufaika na ufadhili huo ni kutoka mikoa sehemu za Ilula, Ipogoro na maeneo jirani ya wilaya ya Kilolo huku wengi wao wakiwa ni watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kwani moja ya malengo ya Taasisi hiyo ni kuwasaidia watoto wenye mahitaji hasa wa kike ili waweze kupata elimu sawa na watoto wengine walio na wazazi.
“Watoto hawa wako katika shule za Bweni hii ni kuwafanya waweze kupata huduma zote muhimu ambazo ni chakula, malazi na muda wa kujisomea kwani watoto wengi wa kike wakisoma shule za kutwa  wanatumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani na hivyo kukosa muda wa kujisomea na kucheza michezo mbalimbali” alisema Mwakasyala.
Alisema kuna umuhimu wa watoto wa wa jinsia zote kupa elimu itakayomsaidia katika maisha yake ya kila siku na shirika hilo linamsomesha mtoto hadi anapofikia elimu ya chuo na baada ya hapo atakuwa na uwezo wa kujiendeshea maisha yake.
Mwakasyala alisema watoto wa kituo hicho licha ya elimu ya kawaida wanapa elimu ya ufundi wa kushona nguo, kufyatua matofali na ufundi mwingine unaoweza kuwakomboa mara wamalizapo elimu zao na elimu hiyo hutolewa kutokana na vipaji walivyonavyo.
Aidha aliwataka wazazi kuwapa ushirikiano katika kuwaleta watoto waweze kupata elimu stahiki kwa kugharamiwa kila kitu na shirika hilo zikiwemo ada, sare za shule na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
Mwakasyala alibainisha changamoto wanazokumbana nazo mojawapo ni wazazi wengi kushindwa kuwaleta watoto wao kwa misingi ya dini wakidhani kwamba wakiwapeleka katika kituo hicho watabadilishwa dini walizozaliwa nazo kutokana na chuo kumilikiwa na kanisa la Anglikana.
Kwa upande wao watoto wa kituo hicho wakiwakilishwa na Monalisa Sungwa wa kituo hicho alitoa shukrani kwa uongozi wa kituo hicho kwa kusimamia huduma zote kwa watoto hao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuwakomboa katika kupata elimu iliyobora.
Sungwa aliitaka jamii kuwashirikisha katika maswala ya kijamii kwa ngazi ya kiwilaya katika kutoa maoni kutokana na mtoto kuwa na haki katika kutoa maoni kwa jamii inayomzunguka.
“ Tumekuwa hatupewi fursa nyingi za kushiriki katika mafunzo na matamasha pamoja na shughuli zingine  za kijamii hakika hii inasababisha ushiriki mdogo katika masuala ya kijamii naomba sana tushirikishwe katika kutoa maoni” alisema Sungwa
Aidha alisema wanakumbana na changamoto ya wazazi kutokuwa na ushirikiano na kituo hasa pale wanapohitajika kushirikiana katika kuwafatilia watoto maswala ya shuleni na tabia za watoto kwa ujumla.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live


Latest Images