Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120033 articles
Browse latest View live

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kulia) akionge na Mbunge wa Korogwe Mjini Yusuph Abdallah Nassir katika viwanja vya Bunge leo Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kushoto), Mbunge wa Viti Maalumu Margaret Sitta(wa pili kushoto) akifuatiwa na Waziri wa fedha William Mgimwa(mwenye miwani)pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia(kulia) wakibadilisha mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo , baada ya Mbunge James Mbatia kuwaslisha hoja yake binafsi kuhusu Udhaifu ulioko katika sekta ya Elimu nchini.
Mwanasheria Mkuu Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazir wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa akionyesha baadhi ya vitabu vinavyotumika mashuleni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zinazohusu elimu baada ya Mbunge wa kuteuliwa wa NCCR- Mageuzi James Mbatia kuwakilisha hoja yake binafsi ya Udhaifu ulioko katika sekta ya elimu nchini
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari leo Dodoma katika viwanja vya Bunge.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki(katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Ester Bulaya(kushoto)katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

KAMPUNI YA BE FORWARD YAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MTEJA WAO ALIYESHINDA ‘PHOTO CONTEST’

$
0
0
Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya magari ya Be Forward Tanzania, Mashariki na Kati Oliver Philbert akizungumzia kuzinduliwa rasmi kwa Kampuni ya Be Forward hapa Tanzania na pia tukio la kampuni hiyo kukabidhi zawadi kubwa ya gari kwa mmoja wa wateja wake kutoka Uganda aliyeibuka mshindi wa shindano la photo contest..
Amesema Be Forward ni kampuni inayojihusisha na uuzaji magari nchini Japan kwa njia ya mtandao wa Internet, na ili kuongeza ufanisi na Imani kwa wateja wetu tumefungua kampuni Tanzania ambayo inajishughulisha na huduma kwa wateja.
Be forward Tanzania itatengeneza ajira zaidi ya 1,000 kwa watanzania hivyo kuipunguzia mzigo serikali na kuongeza kipato kwa watanzania.
Kampuni hiyo iliendesha ‘Photo Contest’ ambapo wateja wake walitakiwa kutuma picha za magari walionunua kutoka katika kampuni hiyo, na kisha ziliwekwa katika mtandao wa Be Forward na katika ‘Kurasa yao ya Facebook na watu kuzi’like’.

Kinana azindua tawi jipya la ccm na kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii ,wilaya ya kibondo mkoani Kigoma leo.

$
0
0
katibu mkuu wa chama cha CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi jipya la chama hicho ndani ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.
Jiwe la Msingi lililowekwa na Ndugu Kinana.



Ndugu kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM  kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.
Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana alikwenda shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia kushiriki ujenzi wake,pia aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha umeme ofisi za walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili kwa ajili ya shule hiyo.

Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Kumwambu akiwa sambamba na baadhi wa viongozi wa Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.
Ndugu Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni Nyobeye,mara baada ya kuwasili kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo jioni.Picha zaidi Bofya JIACHIE BLOG.

KUWEPO KWA USAFIRI WA TRENI YA RELI YA KATI NI FAIDA KWA WAKAZI WA VIJIJI VYA JIRANI NA STESHENI KUBWA

$
0
0
Hapa ni katika Kijiji cha Saranda,Mkoani Singida ambapo wananchi wa maeneo haya hufaidika sana pindi treni ya reli ya kati inapokuwa inapita katika eneo hilo kwani huwawezesha kuleta biashara zao hapo na kuziuza abiria wanaosafiri na treni hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Makutupora Mkoani Dodoma wakiwa na biarashara zao wakiwauzia wasafiri waliopanda treni ya reli ya kati,ambayo inabeba abiria waendao katika mikoa ya Kigoma,Mwanza na Mpanda.ni dhahiri kwamba Serikali inatakiwa kuonyesha juhudi kubwa kwa usafiri huu ili kuweza kusaidinia kupunguza makali ya ugumu wa maisha kwa wakazi wa maeneo mbali mbali hapa nchini.
Wakazi wengi wa maeneo haya ya vijijini ni Wakulima,hivyo wakati treni ikipita hapo na wao hulazimika kuacha kilimo kwa muda na kuja kuuza bidhaa zao mbali mbali.
Mwanamama na mwanae mgongoni akiwa na bidhaa zake akitafuta wateja wa kununua.
Kuku wa kienyeji ni wengi sana katika vijiji hivi vya njiani (ila utaratibu wa ubebaji ndio hauzingatiwi kabisa).

MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Mtu mzima Lionel Richie aliturusha sana na ngoma yake ya 'All Night Long'
Yaani hapo YMCA ikipigwa ngoma hii ujue disco ndio limeanza...

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Kidum na Lady Jay Dee ni balaa katika ngoma yao ya kolabo

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Ngoma ya 'We are the World' kusaidia maafa yaliyotokea Haiti

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Ngoma ya 'we are the World' ya Amerika kusaidia Afrika

Dkt. Migiro azindua Mashindano ya Mpira wa Pete Mkoani Kigoma

$
0
0
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akisalimiana na mmoja wa wachezaji wa timu ya Mwandiga Queens wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wachezaji wa timu za Mwandiga Queens,Lake Tanganyika na Mwananchi muda mfupi kabla ya kufanyika wakwa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akizungumza na wachezaji wa timu ya Shule ya Sekondari ya Mwananchi  wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akirusha mpira golini ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Mzee Mbonea Kazeni Mshana.

Leo ni miaka 10 tangu ulipochukuliwa kukaa na Baba yetu wa Mbinguni Milele Tarehe 1/02/2003. Tunakumbuka, busara, hekima, kujali, malezi bora ya kwako uliyotupa. Tunakumbuka bidii, juhudi na uchapa kazi wako. Lakini tunaamini kuwa umepumzika na taabu za dunia hii vizuri.

Unakumbukwa na mkeo mpendwa Rahel Mshana, Wanao wapendwa Joyce, Felix, Joseph, Judith na Brian, pia wakwe zako Godlisten, Stephen na Neema na wajukuu zako Innocent, Rachel, Sarah, Daniel, Gideon, Elisha, Reinhard, Rachel na Jonathan.

Pia unakumbukwa na mkweo Naizihijwa Joseph Mritha, na Ndugu Zako na jamaa na marafiki tulioishi nao kwa upendo Mwadui -Shinyanga na Arusha.

Ufunuo 14: 13...."Heri wafu wafao katika Bwana Tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao"

Article 24

community project in Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara awasili Mkoani Kigoma tayari kwa Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Ndg. Mangula yupo Mkoani Kigoma kwa Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh. Issa Machibya wakati alipowasili kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Juimuiya ya Wazazi Taifa,Ndg. Dogo Iddy Mabrouk.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula (kushoto) akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro wakati alipowasili kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Katikati ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Ndg. Nape Nnauye.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma leo.
Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wa Kigoma wakimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Ndg. Phillip Mangula (hayupo pichani).

NSSF YAWAPA SEMINA VIONGOZI WA SACCOS JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crecentius Magori  akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na shirika hilo kwa viongozi wa Mkoa wa DaresSalam. Kulia ni Meneja Utawala wa Kampuni ya Sccuct, Nicholaus  Wambura ambao ndio waratibu wa semina hiyo.
Mwakilishi wa Saccos ya Ukonga, David Marwa akizungumza wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Saccos Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika semina hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

HIVI NDIVYO HAFLA YA KUITATHMINI LIGI KUU YA VODACOM ILIVYOKUWA

$
0
0
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa,akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wa michezo pamoja na wageni waaligwa wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
Katibu wa TFF Angetile Osiah,(kushoto)Afisa Mtendaji Mkuu wa kamati ya ligi kuu Silas Mwakabinga,pamoja na Mjumbe wa TFF Saad Kwemba,wakibadilishana mawazo wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
Wadau wa michezo.
Katibu wa TFF Angetile Osiah(kushoto)akimsikiliza jambo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa, wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Article 19

Balozi akagua Banda la utalii la TANAPA jijini Brussels

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dkt Deodorus Kamala akiongea na ndugu Crispin Mwinuka wa TANAPA akitaka kujua wanavyoendelea na kazi ya kuitangaza Tanzania Ulaya leo jijini Brussels nchini Ubelgiji

kutoka bungeni dodoma leo

$
0
0
Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, aliwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. 

 Katika hoja hiyo, Bw. Mbatia alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari, kunachangia wanafunzi kufanya vibaya. 

 Alisema hali hiyo inachangiwa na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo ambacho kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka rushwa. 

 Hoja hiyo iliibua mvutano mkali kwa wabunge ambao baadhi yao walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.
 Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR- Mageuzi Mhe James Mbatia (kushoto) akiongea na waandishi wa habari  katika Ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma baada ya kuambiwa aondoe hoja yake ambako alikataa.(Mwengine), ni  Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Mhe Tundu Lissu

 Naibu Waziri wa Fedha Mhe Janet Mbene(kushoto) akisalimiana na Mbunge  Khalifa Suleiman Khalifa (Gando) kat[ka viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma
 Wabunge wa Upinzani Mjini Dodoma leo walipokutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya msimamo wao baada ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR – Mageuzi) Joseph Mbatia kuambiwa aondoe hoja yake Bungeni  na kukataa
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Magaeuzi) James Mbatia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MAONGEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA WANAHABARI MJINI DODOMA JUU YA SAKATA LA GESI MTWARA

Viewing all 120033 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>