Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) London leo Jumamosi

$
0
0

Assalam alaikhum
 
jumuiya ya Bilal Education inafuraha kukualika katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.Maulid yatafanyika leo Jumamosi terehe 2-02.2013.
 
katika ukumbi wa Etton hall,kuanzia saa nane kamili hadi saa kumi na moja(2pm -5pm)
Anuani.Eton Road Ilford IG1 2UE.Opposite no.81-83.Dinner will be served.
 
Kwa Mawasiliano Zaidi wasiliana na Salim 07766957464 au saleh 07710611449

Wassalam Alaikum

HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI JANUARI 2013

$
0
0
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JANUARY, 2013

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Ngoma ya Gregory Abbott ya 'Shake You Down' ilikuwa moto

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Msanii Dokii na ngoma yake ya 'No One Like OBAMA'

Notice to Public: TANZANIA BUSSINESS SCHOOL

$
0
0
Tanzania Commission for Universities
Notice to Public
TANZANIA BUSSINESS SCHOOL

Tanzania Commission for Universities (TCU) would like to inform the general public that Tanzania Business School has invited applications including for postgraduate degrees at locations in Arusha and Dar-es-Salaam. Kindly note that the School has not been accredited to run any degree level program and those advertised are illegal and award offered will not be recognized.

The Commission has directed Tanzania Business School to immediately cease any degree level training in the country. For the non-degree programmes the Commission is advising the public to check the accreditation status of the school with National Council for Technical Education (NACTE).

Issued by:
Executive Secretary
Tanzania Commission for Universities

kumbukumbu

$
0
0
Ilikuwa usiku wa kuamkia Alhamisi, Februari 2, 2012, wakati ulipomaliza kwa amani siku yako ya mwisho ya kuishi hapa duniani na kuanza siku yako ya kwanza ya kuishi makazi ya kudumu akhera.

 Ilikuwa ni siku iliyojaa simanzi kwa mume wako kipenzi Abdallah, watoto wako Hashim na Lulu, mama yako mzazi Mama Babay, Baba yako mzazi Mzee Abdul, kaka yako Yusuf, wadogo zako, shangazi na baba zako wadogo, ambao bado wanakukumbuka.

Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja, viungo vitaungana tena. 

Mungu ametimiza ahadi na mapenzi yake ya kukuita kwenye makazi yake ya kudumu ukapumzike kwa amani, baada ya kuishi nasi duniani kwa furaha, ukarimu, amani na upendo kwa miaka 42. Kimwili haupo nasi nyumbani, lakini ki roho bado uko nasi popote.

Ni mwaka mmoja kamili umetimia leo, lakini kumbukumbu za upole, ukarimu na tabasamu lako, zinatufanya tuone kama umeondoka jana. Dua njema tunakuombea, Mwenyezi Mungu alijalie kaburi lako liwe miongoni mwa bustani za peponi.

Daima unakumbukwa pia na shemeji zako Dawood, Shigongo, Nasibu, Hassan, Kitenge, wafanyakazi wote wa Global Publishers, wifi zako, majirani na marafiki zako wote. 

Kifo chako kinaendelea kutukumbusha kwamba kila nafsi itaonja mauti na ulipoiaga dunia tulisema:

HAKIKA WEWE NA SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE SOTE TUTAREJEA! UWEZO NA UTUKUFU WAKE UTUKUZWE DAIMA - AMIIN!

TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2013 SASA KUFANYIKA APRIL 27

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Mwanamichezo bora wa TASWA, Haji Manara, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, jana mchana, wakati wakitangaza kuhusu kusogezwa mbele kwa shughuli hiyo ya utaoji tuzo ambapo sasa hafla hiyo itafanyika April 27, 2013, ambapo pia alizungumzia kwa ujumla maandalizi hayo. Katikati ni Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, (kulia) ni Mjumbe wa TASWA, Turo Chambo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo, jana.

*******

TUZO za Wanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2012 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kamati inayoratibu tuzo hiyo ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii, ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya kimsingi kuhakikisha tuzo zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita na pengine ziwe bora zaidi.

Kutokana na hali hiyo vyama vyote vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano vitaandikiwa barua kwa ajili ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka jana upande wa michezo yao na yawasilishwe kabla ya Februari 28, mwaka huu.

Tunaomba ieleweke kuwa vyama vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo inafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya mawasiliano ili kuona namna zitakavyoshirikiana na wadau katika kuchambua majina hayo, ambapo kila chama kimetakiwa kiwasilishe majina matano ya wanamichezo wao kwa kila jinsia kama ni mchezo unaochezwa na jinsia mbili, lakini kama ni mchezo wa jinsia moja watatakiwa kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu.

Yapo marekebisho kadhaa yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya tuzo kutoka 36 za mwaka jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza kuongezeka ama kupungua kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama vitaleta.

Tunaomba wadau watupe ushirikiano wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya tuzo ziwe bora na kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa kwa kuthamini kile alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo utatangazwa hivi karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.

Idadi ya michezo itakayopewa tuzo pamoja na aina nyingine ya tuzo zitakazotolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima tutaendelea kujulishana kadri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele. Washindi wa kila tuzo ndiyo mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2012.

Dhamira ya kamati yangu ni kutaka kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na tutaleta wanammichezo sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye ataungana na wengine waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.

Wanamichezo ambao wamepata kutwaa Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006),  Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati mwaka 2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi Hassan ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe.

Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo za TASWA

01/02/2013

YALE YALEEE.....

$
0
0
Dear Uncle Michuzi,

niko safarini naelekea Tanga nikitokea Morogoro,Huku njiani najionea uendeshaji ambao ni hatari sana.

Naamini waweza kushawishi ushauri ufuatao kwa mabosi wa Jeshi la Polisi (upande wa Traffic Police).

Please, kama walivyotupatia simu za Viongozi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya "ulinzi shirikishi" basi watupatie email address za makamanda wa mikoa wa traffic, ili tuwatumie hizi picha za ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani.

Nakuhakikishia, hatua hiyo itapunguza makosa hayo na vifo vinavyosababishwa na uzembe wa madereva wetu.

Kila la kheri.

Mdau.

President Kikwete to implement APRM recommendations

$
0
0
By Special Correspondent, Dar es Salaam

 A week after his country submitted its Country Review Report in Addis Ababa, Ethiopia under the auspices of the African Union governance assessment Mechanism-the African Peer Review Mechanism (APRM) President Jakaya Kikwete has promised to work on all the recommendations from his peers.

President Kikwete and Michael Sata of Zambia Country Review Reports’ were reviewed by African Heads of State and Government participating in the APRM process last Saturday the 26 th January, 2013.

Speaking in Dar es Salaam on Friday evening in his scheduled monthly address to the nation, President Kikwete told the nation that Tanzania has finally reached major milestones in the APRM process by submitting its report to the AU Forum.

“While in Ethiopia, we participated in the Ordinary Summit of AU Heads of State and Government and in the APRM Forum where Tanzania and Zambia reports were submitted for discussions,” he said.

 He told the nation that during the peer review, many African Heads of State and Government were pleased with governance reforms in Tanzania and the report was swiftly endorsed.

The President used the address to inform Tanzanians that there are however some areas where the government received recommendations for improvement, which his government will implement them. “In general there were no areas that we were pointed fingers.

 We have been congratulated for a number of reforms and we have been advised on some areas for improvement. I had a chance to elaborate on some of the issues. We promised to work on their recommendations.

Our Review Report was then endorsed,” said the President. APRM process which celebrates 10 years in March, 2013 was incepted in 2003 with the aim of fostering reforms in diverse areas of governance to make African leadership participatory and offer a cross learning resources for Afrca.

 Tanzania signed to the Memorandum of joining with the APRM in 2004, completed formation of its national structures in 2007 and completed its Country Self Assessment Report in 2011. 

 Speaking in Addis Ababa last week the founders of the Mechanism Thabo Mbeki of South Africa and Olessegun Obasanjo of Nigeria said the Mechanism offers unique opportunities for African governments to resolve governance issues from an African perspective and solidarity.

Ubao wa Matangazo usomekavyo leo mjini Kigoma

$
0
0
 Mtoto ambaye jina lake halikupatikana mara moja akisoma maandishi yaliyoandikwa leo kwenye ubao wa matangazo wa tawi la Chama fulani cha cha Siasa Mkoani Kigoma.

PRESS PLAY - DJ Choka ft, Mrap, Gosby, Vanessa Mdee, Mabeste & Deddy

Maandalizi wa Miaka 36 ya CCM kufanyika kesho Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma

$
0
0
Moja ya mabango ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM kitaifa,yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

kinana akamilisha ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya ya kakonko na kibondo mkoani kigoma.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi kuhusiana na bwawa la umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa Kigoma,Elinatha Elisha (haonekani pichani).Kinana amefanya ziara ya kuutembelea mradi huo wa umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma akiwa ameambatana na wajumbe wake wa chama cha CCM. 
Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi ya mitambo ya umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa Kigoma,Elinatha Elisha.Kinana amefanya ziara ya kuutembelea mradi huo wa umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma. 

Sehemu ya mradi wa Bwawa la umwagiliaji,ambalo Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana alitembelea na kujionea maendeleo yake,kwa mujibu wa Injinia kutoka Ofisi ya Umwagiliaji kanda ya Magharibi mkoani Tabora,Bwa.Bahati Balekele alieleza manufaa ya  Bwawa hilo kwa wakazi wa eneo hilo.alisema kuwa litasaidia katika matumizi ya Kilimo cha Umwagiliaji,Matumizi ya mifugo pamoja na matumizi ya majumbani.
Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya wanakijiji Nyendara,alipokwenda kukagua mradi wa bwawa la Umwagiliaji la Nyendara
Meneja wa kituo cha uzalishaji Umeme Wilaya ya Kibondo,Damson Lupenza akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake waliofika eneo hilo kwa ajili kukagua maendeleo ya mradi huo wa Umeme.
Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa kituo kinachozalisha umeme Wilaya ya Kibondo.
Mmoja wa mafundi wa kituo cha kuzalisha umeme,Omary Mwinyimkuu akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana (pichani kati),alipokwenda kutembelea mradi wa Umeme,kijiji cha Twabangondozi,Wilayani Kibondo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kichama wilayani humo akiwemo mkuu wa Wilaya,Mh Venance Mwamoto.Picha zaidi bofya JIACHIE BLOG.

YANGA NA MTIBWA NGOMA DROOO LEo

$
0
0

 Wachezaji Jamal Mnyate wa Mtibwa Sugar (kushoto) na Haruna Niyonzima wa Yanga wakiwania mpira wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeao yalikuwa 1-1.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia moja ya shambulizi la timu hiyo, langoni kwa Mtibwa.

JK ATUA KIGOMA KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

$
0
0
 Ndege iliyombeba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mkoani Kigoma jioni hii,tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh. Issa Machibwa wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.Wa tatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara,Phillip Mangula.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu kutoka kwa vijana wa Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma,wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo,tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara,Mh. Mwigulu Nchemba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kumlaki.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Kada wa CCM,Mh.Rajab Mwilima.


biashara huria oye!

$
0
0
 Chezea biashara huria weye. Hapo ni katika mgahawa wa wasafiri wa ndani (mikoani) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo hilo andazi la mviringo maarufu kama doughnut linaenda kwa bei hiyo hapo chini. Hicho kikombe cha kahawa ni 1,500/-

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Ni mwaka 1984 ambapo The Temptations waliwasha moto na ngoma yao ya 'Treat Her Like A Lady'

NEWS ALERT: JENGO LA PPF TOWER JIJINI DAR LASHIKA MOTO

$
0
0
HABARI ZIMETUFIKIA CHUMBA CHA HABARI SASA HIVI KWAMBA JENGO LA PPF TOWER MTAA WA OHIO JIJINI DAR ES SALAAM LIMESHIKA MOTO NA JUHUDI ZA KUUZIMA ZINAENDELEA KATIKA GHOROFA YA 11 . TUNAFUATILIA KUJUA CHANZO NA MADHARA YALIYOTOKEA ILA KWA SASA MOTO UMESHATHIBITWA. 

Rais Kikwete aongoza Matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mkoani Kigoma leo

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete leo wameongoza Matembezi ya Mshikamano yaliyoanzia kwenye eneo la Mnarani na kuishia kwenye ofisi za CCM mkoani Kigoma,asubuhi ya leo. Matembezi hayo hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete akionekana kuwapungia wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliokuwa wamejipanga kwa wingi pembezoni kwa barabara Lumumba/Ujiji asubuhi ya leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo.
Maandamano yakiendelea.

Taswira za uwanja wa ndege wa mwanza

$
0
0
 Sehemu ya kuingilia abiria likikarabatiwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza
 Sehemu ya abiria ndani ya jengo hilo lina viyoyozi vinavyomwaga maji na kutoa raha abiria
Vigari vya kubebea mizigo ya abiria
 Mkusanya ushuru wa magari akipitia madereva kuchukua pesa kabla ya kufungua 'geti' kuruhusu magari yatoke nje ya uwanja. 
 Mtindo wa uwanja wa ndege wa Mwanza kwa madereva siku hizi ni kuingia bure, kutoka pesa...
Geti linaendeshwa kwa nguvu ya binadamu, na mvua na jua ni dhahiri mfanyakazi anapambana navyo
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images