Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 32 | 33 | (Page 34) | 35 | 36 | .... | 3270 | newer

  0 0

   

   Audio za vipindi viwili (jana na leo) vya Amka na PRIDE FM  hosts
   ni Andrew Mturi na Sospeter Magumba


   
  KAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

  0 0


  The late Moses Tito Kachima

  It is with sorrow the family of Moses Tito Kachima announces the death of their loved one Mr. Moses Tito Kachima which occured on the 29th January 2013 at Mama Ngoma Hospital, Mwenge Dar es Salaam.
  Family, relatives and friends are gathering at the deceased residence at Lugalo Street plot no. 314 Upanga for funeral and burial arrangements.
  There will be a mass at the St. Immaculate Church on United Nations road, Upanga on Friday 1st February 2013, thereafter the body will be laid to rest at the Kinondoni Cemetery at 1600 hrs.
           "Blessed are the pure in heart for they shall see the Lord"

  0 0

   Baadhi ya Watoto ambao majina yao hayakufahamika mara moja,wakipita kwenye mto wakati wakielekea nyumbani kwao ambako ni ng'ambo ya mto huo,kama walivyokutwa na kamera man wetu katika moja ya Vijiji vya Mkoani Singida.

  0 0
 • 01/30/13--14:23: Article 2


 • 0 0

   Waziri wa nchi, Ofisi ya ya Rais (mahusiano na Uratibu) na Mbunge wa Bunda Mhe Steven Wasira (kulia) akikumbatiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe Godbless Lema katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma 
  Baadhi wa wabunge wakielekea katika ukumbi wa mkutano Bungeni mjini Dodoma
   Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe  Freeman Mbowe (kulia) , Mhe Godless Lema (katikati- Arusha mjini) pamoja na Mbunge  wa Musoma Mjini, Mhe Vicent Nyerere  wakielekea katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Mbunge  Lema amerudi tena Bungeni  baada ya kushinda kesi yake
   Wabunge wa Iramba  Magharibi Mhe Mwingulu Nchemba- CCM (kulia), Mhe Joseph Selasini( Mbunge wa  Rombo- CHADEMA ), na Mbunge wa NCCR- MAGEUZI, Mhe Moses Machali wakiwa katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma(Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).


  0 0

  Hizi ni baadhi ya Taswirazz za Wilayaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma kama zinavyoonekana hapa.  0 0

  Najua Old Skul wengi mtawakumbuka Chaka Demus & Pliers na ngoma yao ya 'Murder She Wrote'

  0 0

  Ngoma ya 'Safari siyo Kifo' ya Akudo Sound ni kali

  0 0
 • 01/30/13--23:48: Article 22

 • 0 0


  Ndugu zangu,

  Leo ni mwisho wa mwezi wa mwaka mpya. Na mwaka ulivyo ni kama noti ya shilingi elfu kumi ya Bongo. Ukiichenji tu, utashangaa inavyopukutika!

  Ukae sasa ukijua, kuwa kesho ndio Februari Mosi. Hivyo, mwaka mpya wa 2013, kama ilivyo kwa noti elfu kumi, ndio tutakuwa tumeuchenji. Subiri sasa uone siku, wiki na miezi inavyopukitika. Fumba na kufumbua utasikia tumeshaingia Juni tunaelekea Bajeti ya Serikali ya Julai, na ukitoka hapo utafikiri mwaka unateremsha milima ya Kitonga.

  Inatukumbusha nini?

  Umuhimu wa kupanga mambo yetu. Inahusu muda na matumizi ya muda. Na mwanadamu usipokuwa makini na muda, itakuwa sawa na kisa kile cha mzazi aliyeulizwa na wanawe; " Mbona nguo za Krismasi hatujanunuliwa?"

  Mzazi akawajibu wanawe; " Jamani, Krismasi ya mwaka huu imekuja ghafla sana!"
  Kana kwamba hakujua, kuwa kwenye kalenda ya mwaka tarehe ya Krismasi imeshawekwa, Desemba 25!

  Ndio, Afrika mvua hainyeshi ghafla, huwa kuna dalili zake. Na katika maisha, mambo mengi hayaji ghafla, bali hutukuta tukiwa hatujajiandaa. Jiandae na mwaka unaoanza kupukutika kuanzia kesho, kama noti ya shilingi elfu kumi. Kila la kheri.

  0 0


  Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili.


  Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili.

  Bondia wa Klabu Ya Ashanti ya Ilala Abdallah Shamte akipambana na Hamisi Matunda wa Mashine ya maji wakati wa mashindano ya klabu bingwaShamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili. 

  Mashabiki wa ASHANTI BOXING YA ILALA WAKISHANGILIA. Picha na www.Superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

  Katibu wa Taasisi ya The john mashaka Bi, Rabia Bakari akiungumza kwa ajili ya kufungua mkutano wa waandishi wa habari na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu ili kujadili kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa wenye ulemavu na wengine wasiojiweza.

  Baadhi ya watu wanaotafsili lugha za alama wakiendelea na kazi hiyo wakati wa mkutano

  Baadhi ya wawakilishi wakisikiliza kwa makini

  Mwenyekiti wa TUSPO Bw. E LLEZER Mdakima kushoto akizungumza wakati wa mkutano huo wengine kulia ni Mjumbe wa Taasisi ya The John Mashaka Bi, Latifa Masasi na Katibu wa taasisi hiyo Bi, Rabia Bakari. picha na www.burudan.blogspot.com

  0 0

  Na Thehabari.com 
   VYOMBO vya habari nchi vimeombwa kutoa elimu kwa jamii juu ya manufaa ya iwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (National ICT Broadband Backbone-NICTBB) ili wananchi wauelewe na kuulinda kutokana na umuhimu wake. 
   Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Uendeshaji wa NICTBB, Adin Mgendi alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo anuai vya habari juu ya utendaji kazi wa mkongo huo na manufaa yake kwa taifa. 
   Mgendi alisema manufaa ya ujenzi wa Mkongo wa mawasiliano nchini yameanza kujitokeza hivyo Watanzania wana kila sababu ya kuulinda mtandao huo kwani unaumuhi mkubwa kwa jamii na taifa. Alisema kwa sasa jumla ya nchi sita, ambazo ni pamoja na Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya zimeunganishwa na Tanzania hivyo nchi yetu ikibeba dhamana ya kuwahudumia kupitia mtandao wa Mkongo. 
   Mtalamu huyo alivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa waliopo karibu na njia ya mkongo ili wasiuharibu kupitia shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanyika ardhini. 
   Akifafanua zaidi kwa wahariri wao, Ofisa Biashara wa Mkongo, Thomas Lemunge alisema kwa sasa mikoa yote ya Tanzania Bara tayari imeunganishwa na mkongo hivyo kurahisisha miundobinu ya mawasiliano.
   Aidha aliongeza kuwa mtandao wa mkongo ambao ujenzi wake uaendelea umepita maeneo anuai; ikiwemo ardhini pembezoni mwa barabara, mashambani, juu ya nyaya za umeme na kwenye maji huku ukiwa na mizunguko mitatu yaani wa Kaskazini, Magharibi na Kusini. 
   Awali akizungumza na washiriki hao, kabla ya kufungua warsha hiyo, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini (TEHAMA), Mhandisi Zaipuna Yonah alisema mkongo unamanufaa makubwa kwani hadi sasa matumizi ya intaneti yameongezeka tofauti na awali.
   "Ongezeko la matumizi na faida za mkongo zinaongezeka siku hadi siku na hivyo kukidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya TEHAMA kwa wananchi katika maeneo ya mbalimbali ya nchi yetu na hatimaye kukuza uchumi," alisema Yonah. 
  Wahariri hao walipata fursa ya kutembelea kituo kikuu kinachoratibu shughuli za mkongo maeneo mbalimbali ya nchi na kuona namna wataalamu wanavyofanya kazi eneo hilo. 
   Mkongo wa taifa ambao kwa sasa unategemewa na nchi jirani za Tanzania na makampuni binafsi katika usabazaji huduma za mawasiliano unasimamiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) huku wakiwa ndio meneja wa Mkongo huo.
   Wahariri wakiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
   Mhariri Mkuu wa Tanzania Daima Bw Ansbert Ngurumo akiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
   Wahariri wakibadilishana mawazo wakati wa mapunziko ya semina hiyo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo
   Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
   Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
  Meneja mwendeshaji wa mkongo wa Taifa Bw Adin Mgendi akifafanua jambo
  0
  Mhandisi wa Mkongo wa Taifa Bw Nsaji Mwamukonda akionesha kwa wahariri aina ya waya unaobeba mkongo huo. Taarifa kamili  ya semina hii badae kidooogo...

  0 0
 • 01/31/13--03:04: SHUKRANI
 • Familia ya Mzee Wallace Hurbert Shundi wa Upanga, Dar es Salaam ina washukuru Ndugu, Jamaa na Marafiki na wote walioshiriki kwa hali na mali katika kuumuguza, katika mazishi na waliotufariji katika kipindi kigumu cha msiba uliotokea tarehe 19 Disemba 2012. Mungu awabariki.

  Shukurani za pekee kwa Madaktari na Wauguzi wa Hospitali za Tumaini, Muhimbili na Apollo, India. Dr. Robert Mhina, Dr. Kimu wa Muhimbili, Prof. Yongolo wa Tumaini Hospital na Dr. Ngota wa Wizara ya Afya. Padre Kanisa la Mt. Albano, Wanajumuia Mt. Adrea, Majirani Plot. 250 Maweni Str., Upanga. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, Bw & Bibi Bakari Mahiza, Col. Sylvester Msindo, Bw. Sandile Khumalo. Menejimenti na Wafanyakazi wa TAKUKURU na EWURA.

  Familia inawakaribisha katika misa ya Shukurani siku ya jumamosi tarehe 2 Februari 2013 Saa 3:00 asubuhi katika Kanisa ja Mt. Albano, Upanga.

  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

  AMEN.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akitiliana saini na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akibadilishana hati na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega akizungumza machache mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo wa miaka mitatu.

  Na Abdulaziz Video,Lindi.

  WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.

  Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya Sh,144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2013.

  Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Addo Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana na saini ya utekelezaji wa mpango huo.

  Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha miaka mitatu,umeanza rasmi mwezi huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo.

  Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni, Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu.

  Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30 wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18).

  “Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawili watakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule zote hizo”Alisema Mapunda.

  Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu wapatao (71).

  Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.

  Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake.

  Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne Devilliers,amesema lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.

  Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao,kutokana na kutoielewa vyema Lugha ya Kingereza.

  Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidia kuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa ujumla.

  Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongozi wa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.

  0 0


  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

  “Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.

  “Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

  Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

  Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

  0 0

   Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyangamba iliopo kwenye Kijiji cha Janda,Wilayani Buhigwe,Kigoma wakati alipoitembelea shule hiyo na kuangalia maendeleo ya Wanafunzi wa shule hiyo,alipokuwa kwenye ziara ya kukutana na wananchi wa Wilaya hiyo jana.
   Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia  wananchi wa Kijiji cha Muhinda kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.Dkt. Asha-Rose Migiro amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na mshikamano ili kuweja kunyanyua maendeleo ya kijiji na wilaya kwa ujumla.
   Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
   Viongozi wa kijiji wakitambulishwa.


  0 0

   Hivi ndivyo mji wa Kigoma unavyoonekana sambamba na Ziwa Tanganyika mchana wa leo.na kile kikwangua anga kinachoonekana ni cha Shirika la Nyumba ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.


  0 0

  Uncle, 

   Huku kwetu Kijitonyama maeneo ya Sayansi na vitongoji vyake umeme unakatwa kama vile mtu kashika remote ya kuwasha na kuzima, yaani ni hatari hata kutumia vifaa vya umeme. Ila TANESCO wamekaa kimya hawatuelezi kitu gani kinaendelea, mtazamo wangu ni kuwa kuna mgao wa kiaina ila hawataki kutangaza. 

  Cha ajabu wakianza kampeni za kukata umeme huwa wanatangaza vyombo vyote vya habari na vitisho juu, kama hilo linawezekana kwa nini ikitokea wao ndio wenye matatizo wanakaa kimya?? 

  sisi wananchi tuna haki ya kujua kama ni mgao angalau tuwe na ratiba ili tujipange na vibatali na kama ni mitambo mibovu pia tujue ili tuokoe vifaa vyetu vya umeme??? wapi wahusika, maana ukipiga simu pale mikocheni wale wenzangu na mimi unaishia kuwashambulia tu hawajui hata wajibu nini? 

   Mdau.

  0 0

  Ankal akiwa na Mwalimu wa lugha Bi Aziza Mohamed Abubakar jijini Paris. Bofya mshale hapo chini umsikilize akiongelea kazi yake

older | 1 | .... | 32 | 33 | (Page 34) | 35 | 36 | .... | 3270 | newer