Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 346 | 347 | (Page 348) | 349 | 350 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Taswira za University of Dodoma (UDOM) kutoka angani. Ukitaka mengi toka chuo hiki ambacho ni mojawapo ya vyuo vikubwa katika Afrika Mashariki na ya kati BOFYA HAPA


  0 0

  Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akifungua kikao kwa maombi katika baraza la madiwani lilofanyika mwishoni mwa wiki kushoto ni naibu meya Gervas Ndaki na kulia  Mkurugen Theresia  Mahongo kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa. (picha na Denis Mlowe)

  Juu na chini ni Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa katika kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mwishoni mwa wiki. 
  Habari na picha na Denis Mlowe
  MIONGONI mwa watu 6003 mkoani hapa waliopima afya zao kwa hiyari katika kipindi cha Oktoba  hadi Disemba mwaka jana, watu 379 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
  Akizungumza katika kikao cha utekelezaji wa shughuli za ukimwi zilizotekelezwa na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mbele ya baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba na Disemba mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naibu Meya Gervas Ndaki, alisema kati ya waliojitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa 3074 wanawake 2,929.
  Ndaki alisema kati ya watu 379 waliopima kwa hiari na kukutwa na maambukizi,146 ni wanaume na wanawake ni  233.
  Alisema huduma ya kuzuia maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 1,287 walijitokeza na kupata ushauri wa nasaha na kati yao, 84 sawa na asilimia 6.5 walikutwa na maambukizi.

  Ndaki alisema mapambano ya ukimwi yanaambatana  na huduma za tiba sahihi ya magonjwa ya ngono na jumla ya watu 361, wanaume 110 na wanawake 251, walipata tiba sahihi ya magonjwa ya ngono.
  “Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yanaendelea kuwepo na tunajitahidi sana kuwahamasisha wananchi kujitambua na kutumia sana kondom na pia tumefanya sana kampeni kwa wananchi wanaotakiwa kwenda tohara kujitokeza kwenda katika hospitali na vituo vya afya vinavyotambulika kutoa huduma ya tohara” alisema Ndaki
  Aliongoza kuwa huduma ya kitabibu ya tohara kwa wanaume ilitolewa kwa jumla ya wanaume 171 walitahiriwa na kati ya waliopima vvu wanaume 160 na hakuna aliyekutwa na maambukizi.
  Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.
  alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano dhidi ya ukimwi.

  0 0


  0 0

   Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
  .
   Mama Kikwete akimwaga sera za CCM
   Kicheko
   Ngoma ya Tambiko inayochezwa na wananchi wa kabila la wamakonde nayo ilikuwa ni kivutio tosha wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa  kwenye kata ya Kiwalala, Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014.
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ,Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Lindi Dr.Maua Daftari (katikati) huku Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Lindi Vijijini akisikiliza wakati wa uzinduzi rasmi wa kumbukumbu ya kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi zilizofanyika katika Kata ya Kiwalala iliyoko Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014. Picha na John Lukuiwi. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0

  MSHABIKI MBARONI KWA TUHUMA  YA TIKETI FEKIMshabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa  kukutwa na tiketi bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


  Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia. 

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa. 
  Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchini. 
  Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.

  RAIS WA TFF ATEMBELEA RUANGWA
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. 
  Katika ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya Ruangwa.

  RAMBIRAMBI MSIBA WA OMARI CHANGA
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Vijana, Moro United na Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi (Februari 1 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. 
  Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Changa wakati wake uwanjani akichezea timu mbalimbali alitoa mchango mkubwa ambao tutaukumbuka daima. 
  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Changa, klabu ya Moro United na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
   Katika maziko TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kidao Wilfred, na imetoa rambirambi ya sh. 200,000. 
  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari na Mawasiliano

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0


  Na Ramadhan Ali-Maelezo ZANZIBAR 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej (pichani) amesema juhudi za Serikali ya kuwasogezea wananchi maendeleo hazitokuwa na tija iwapo wimbi la vijana wa Zanzibar watatumika kusafirisha dawa za kulevya na wataendelea kuwa wahanga wa matumizi ya dawa hizo. 
   Amesema hatma ya maendeleo ya Taifa itategemea zaidi vijana wenye mwelekeo mzuri wa tabia na waliojiepusha na matumizi ya mihadharati ambayo inahatarisha afya na akili zao. Waziri Fatma Abdulhabib Ferej ameeleza hayo leo Ofisini kwake Migombani alipokuwa akizindua Kamati ya Kitaalamu ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibi wa dawa za kulevya yenye wajumbe kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi. 
   Amesema kumekuwa na mwamko wa vijana katika kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya kupitia huduma za makaazi za Marekebisho ya tabia (Sober House) lakini mwamko huo hautakuwa endelevu iwapo harakati za usafirishaji, uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya hazitoendelea kupigwa vita. 
   “Harakati za uzalishaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya huleta mtikisiko katika mihimili ya dola na zimekuwa zikiandamana na majanga mbali mbali ikiwemo vifo na kutoweka kwa amani, ”alisema waziri Fatma. 
   Amekumbusha kwamba matukio ya miaka ya karibuni ya hapa nchini ya kukamatwa dawa za kulevya katika viwanja vya ndege unatoa changamoto ya kubuni mikakati imara zaidi na endelevu ya kukabiliana kikamilifu na tatizo hilo. 
   Kutokana na hali hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesisitiza Kamati ya Kitaalamu kwamba dhima ya kuratibu na kusimamia mapambano dhidi ya dawa za kulevya kuanzia sasa imo mikoni mwao na ameitaka kutekeleza jukumu hilo kikamilifu ili kufikia kauli mbiu ya “Zanzibar bila ya dawa za kulevya inawezekana”. 
   Waziri Fatma Abdulhabib Ferej ameihakikishia Kamati hiyo kwamba Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais itakuwa pamoja nao kwa kuwapatia msukumo na kila msaada katika kukamilisha jukumu linalowakabili. 
   Mapema akimkaribisha Waziri Fatma kuzindua Kamati hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais Omar Dadi Shajak alimueleza kwamba wajumbe wake wote ni watu mahiri wenye uelewa mzuri wa madawa ya kulvya. 
   Ameeleza matumaini yake kwamba katika kipindi kifupi kijacho kupitia Kamati hiyo Zanzibar inaweza kuona mwanga wa mafanikio. 
   Kuundwa kwa Kamati ya Kitaalamu ya Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya inatokana na mabadiliko ya Sheria ya udhibiti wa wa dawa za kulevya No. 12 ya mwaka 2011 ambapo moja kati ya jukumu lake ni kuishauri Tume katika suala la udhibiti wa matumizi na usafirisha wa dawa za kulveya nchini. 
   Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Kheriyangu Mussa Khamis inawajumbe 11 kutoka Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya cha Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Idara ya Forodha, Mkurugenzi wa Tiba, Sekta binafsi zinazoshughulikia mapambano dhidi ya dawa za kulevya na wajumbe wawili kutoka taasisi za dini.

  0 0


  0 0

  Kufuatia taarifa ya msiba tuliyowatumia jana, tunapenda kuwakumbusha kwamba watoto wa marehemu na ndugu na jamaa watakuwepo nyumbani leo na mnaweza kwenda kuwafariji na kutoa rambi rambi zenu wakati wowote. Address ni: 
  40 East Sidney Avenue, 
  Apt # 10C , Mount Vernon, 
  NY 10550. 
  Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456. 

  Bado harambe ya kutafuta dolla 10,000 za kufanikisha mipango ya mazishi inaendelea.  Tunawaomba mtafute walau muda mchache mweze kujumuika na Watanzania wenzetu walioondokewa na mama yao, ndugu yao na mpendwa wetu sote. Kwa taarifa zaidi, tafadhali soma maelezo hapo chini na mtaletewa taarifa zaidi kwa kadiri tutakapozipata.

  Familia ya Nestor Mwombeki Rweyemamu ya Mt. Vernon New York inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Theonestina Rweyemamu kilichotokea Feb 1st 2014. Valhalla New York.

  Marehemu ni mama yake Doris, Emmanuel , Steven and Diana Rweyemamu. Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika kumpeleka mama yetu nyumbani Bukoba Tanzania. Tunahitaji kukusanya kiasi cha 10000 us dollars katika mipango ya mazishi.

  Familia itashukuru msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama yetu kwa kutoa chochote kwenye 
  Bank of America , 
  account number 483044166145 
  routing number 021000322 
  na jina kwenye account ni Doris Rweyemamu.

  Mtakaoweza kufika kwenye Msiba address ni: 40 East Sidney Avenue, Apt # 10C , Mount Vernon, NY 10550. Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456.

  Kwa maelezo zaid unaweza piga simu:

  Emmanuel Rweyemamu 6462342418, Steven Rweyemamu 3028837971, Dr. Abbas Byabusha 9145847502, Doris Rweyemamu 6463799135.

  Bwana ametoa na Bwana ametwa. Amen.

  Deogratius Mhella
  The Executive Secretary
  New York Tanzanian Community
  c/o Tanzania Mission to the UN
  307 East 53rd Street, 4th Floor
  New York, NY 10022
  Tel: 201-252-7220
  Email: info@nytanzaniancommunity.org 

  0 0

  Waziri wa Elimu na Ufundi, Shukuru Kawambwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna kwa pamoja wamekutana kujadili mwenendo wa elimu Tanzania na kuchambua matokeo ya Kidato cha nne hususani viwango vya kufaulu na kufeli na hatimae kuwasilisha taarifa ya mkutano wao kwenye Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

  Mawaziri hao walikutana jana mjini Zanzibar na kuongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo na mafanikio ya elimu Tanzania baada ya matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka juzi ( 2011/2012) Waziri Shamuhuna alisema kwa upande wa Zanzibar Wizara yake imejizatiti kuhakikisha vitendo vya udanganyifu katika mitihani vinapungua kwa kutafuta kasoro zilizojitokeza mwaka juzi na kuzirekebisha.

  "Tumekuwa tukizungumza na mabaraza ya mitihani katika shule mbalimbali ili kuhakikisha hatutarejea pale tulipofanya makosa." Alisema Shamuhuna.

  Naye Mheshimiwa Kawambwa amesema baada ya kikao hicho watawasilisha taarifa maalumu kwa mabaraza ya mawaziri ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini pia Waziri huyo amesifu ushirikiano uliopo baina ya Wizara hizo mbili.

  " Ushirikiano wetu unazidi kukua siku hadi siku,hili ni jambo zuri kwa maendeleo ya elimu kwa nchi yetu" Alisema Kawambwa.

  Wizara hizo mbili zimekuwa na kawaida ya kukutana kabla na baada ya mitihani ya Taifa ili kufanya tathmini ya mitihani hiyo.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali zanzibar, Ali Juma Shamuhuna (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri wa Elimu na Ufundi wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa, mkutano uliowashirikisha pia maofisa kutoka Wizara hizo mbili, ulifanyika kwenye makao makuu ya Wizara ya Elimu mjini Zanzibar jana. (kushoto) ni Waziri Shukuru Kawambwa.
  Waziri wa Elimu na Ufundi wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa akizungumza kwenye kikao hicho jana. Picha na Martin Kabemba.
  Mawaziri Ali Juma Shamuhuna na Shukuru Kawambwa wakiongoza mkutano ulowashirikisha maofisa kutoka Wizara hizo jana. Picha na Martin Kabemba.

  0 0

  Kipindi hiki hurushwa TBC1 kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi. Mtoto usikose!


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya iliyowaandalia wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. Kushoto ni Juma Abdulrahman.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipongezwa na mke wake mara baada ya kusoma hotuba yake.
   Mwenyekiti wa Yanga Yanga, Yusuf Manji akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Joyce Mwakisyala  (katikati )akipokea maoni ya  Utafiti  kuhusu Tasnia ya Filamu Tanzania kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba wa kwanza kulia, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo 
  Rais wa Shirikikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba wa pili kutoka kulia akionyesha maoni ya  Utafiti  kuhusu Tasnia ya Filamu Tanzania wa Kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bi leah 

  0 0

   
   Wakili  wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Mhe Angaza Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
  Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Mhe Crecensia Makuru akizangumza jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati sherehe za siku ya Sheria zilizofanyika leo.
   Wakili wa kujitegemea Mhe Mary Munissi wa mkoani Dodoma akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo
   Mahakimu, Mawakili na watendaji wengine wa mahakama wakifuatila jambo walipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
   Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mh. Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za maadhimisho ya siku ya sheria leo.
  Na John Banda, Dodoma
  UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na upungufu mkubwa wa majaji.
  Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
  Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.

  Crecencia alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni wachache kulingana na kesi zilizopo  ambapo hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya mashauri na 1364 na kuna majaji wawili tu.
  Alisema ''idadi ya kesi ni kubwa mno kwa majaji wawili hii inachangia kwa kiwango kikubwa kesi kutosikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati, upo umuhimu wa kuongeza majaji ili kuwe na uwiano wa masharti yaliyopo'',
  Aidha alisema Mahakimu ni wachache huku mahakama nyingi za wilaya zina hakimu mmoja mmoja licha  ya kuwa na mashauri mengi na tatizo linakuwa kubwa pindi mahakimu hao wanapougua, kuuguliwa au kwenda likizo.
  Aliongeza kuwa mahakama nyingi za mwanzo hazina mahakimu wa kudumu, mahakama hizo hutembelewa na mahakimu kutoka vituo vingine hali ambayo husababisha ucheleweshaji wa haki kwani mahakimu hulazimika kusafiri umbali mrefu na wakati mwingine miundombinu huwa ni mibovu..
  Jaji  huyo alibainisha kuwa sasa posho za washauri wa mahakama zimeboreshwa kutoka Sh.1,500 hadi kufikia 5,000 kwa kila shauri litakalohitimishwa.
  Alisema licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama  kuna mikakati ya kutatua changamoto hizo ikiwemo kuondoa mashauri, kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili, kuboresha takwimu za mashauri, kesi zilizopo mahakamani, kuboresha na kusimamia masjala pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.


  0 0


  0 0

   Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
   Majaji wakuu walioteuliwa kwa ajili ya kufanya mchujo wa kuchagua Mama Shujaa wa Chakula 30 na vijana 45 ambao baadae watafanyiwa usahili na kubakiza wanawake 20 pamoja na vijana 30 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

  0 0

      Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiwaongoza Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania katika Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Sheria nchini leo asubuhi katika viwanja vipya vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala karibu na Southern Sun Hotel.

     Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika Sherehe za Siku ya Sheria nchini.

        Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Augustine Ramadhan  akiwa pamoja na Viongozi wengine wastaafu wa Mahakama katika sherehe hizo zilizofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla.

       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman mara alipowasili katika viwanja hivyo kama Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.


   Ukaguzi wa gwaride kuashiria uzinduzi rasmi wa Shughuli za Mahakama kwa mwaka 2014

     Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na Majaji wenzake wakipokea heshima ya gwaride katika sherehe hizo katka viwanja vya Botanical Ocean road jijini Dar es salaam leo asubuhi.

  0 0

  Jumanne ijayo tarehe Nne Februari Mwaka 2014, ni siku ya saratani duniani. Maudhui ya mwaka huu ni vunja fikra potofu kuhusu saratani. Maadhimisho haya yanakuja wakati ripoti mpya kuhusu mwelekeo wa saratani duniani ikisema ugonjwa huo unazidi kuenea nchi maskini ambako tiba ni changamoto,. Halikadhalika mfumo wa maisha unadaiwa kuwa mojawapo ya sababu za kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Assumpta Massoi katika makala hii ameangaziaTanzania, moja ya nchi zinazoendelea. (Assumpta PKG) Kusikiliza bonyeza hapa


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa India Mohamed Hamid Ansari wakati walipokuwatana nchini India.

  Tanzania na India zimeeleza kuridhishwa na uhusiano na ushirikiano uliopo baina yao na kusisitiza dhamira ya kweli ya kuona kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika kwa manufaa ya Serikali na wananchi wa nchi hizo.

  Hayo yamejitokeza leo wakati wa mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa India Mohamed Hamid Ansari.

  Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo ulioanzishwa mwanzoni mwa miaka ya sitini umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka kwa kuongeza maeneo ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.


older | 1 | .... | 346 | 347 | (Page 348) | 349 | 350 | .... | 3284 | newer