Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 345 | 346 | (Page 347) | 348 | 349 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo  mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo.
  Rais Kikwete akiongoza  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto akiwa sambamba na baadhi ya watoto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo. 
   Baadhi ya vijana wakereketwa na chama cha CCM wakiwa na mabango yao. 
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  (pilia kulia) akiwa tayari kuongoza wanachana na Wananchi (hawapo pichani) kushiriki matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Bwa.Phillip Mangula,wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji pamoja na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya wakiwa tayai kuyaanza matembezi hayo.
   Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya watoto waliokuwa miongoni mwa watoto waliojitokeza kushiriki  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
   Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na viongozi wa chama hicho ngazi za juu,pichani akisalimiana na  Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana na anaeshuhudia pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Mh.Phillip Mangula,tayari kwa kuongoza matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
   HAPA 

  0 0


  0 0

   Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa,dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
   Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.

  Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima  pamoja na Beki wa Mbeya City,Yussuf Abdallah wakiwania mpira,wakati wa mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.
   Mbuyu Twite wa Yanga akiangalia nani na kumpatia pasi wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.


  0 0

   "Miaka michache tu wanajigamba, wanapiga kelele, lakini pia kwa kipindi hicho kifupi tayari wameanza mifarakano,Wafanye kazi kubwa kutufikia,"alisema Angellah Kairuki ambaye ni  Mjumbe Baraza la Taifa la Umoja wa Wanawake (UWT), Angellah Kairuki.

  Angellah ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, aliyasema hayo wakati akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 37, ya Chama cha Mapinduzi,  zilizoandaliwa na UWT, kata ya Mabwepande, Kinondoni Dar es Salaam.

  Alisifu kwamba hadi kufika hapo, ni kutokana na mshikamano wa wanaCCM, na kuwataka kushikamana zaidi ili kurudisha majimbo yaliyopotea katika uchaguzi mkuu uliopita. "Wakati ni sasa,m mkono kwa mkono, nyumba kwa nyumba turudishe majimbo uliyopoteza..changamoto za kiamendeleo zipo, lakini haziwezi kutatuliwa kwa siku moja.
  Cheers na Wanachama.

  "Ndio maana Chama kina ilani kwa ajili ya kutekeleza vizuri mikakati ya maendeleo nchini,"aliongeza. Angellah alisema  kwa muda ambao CCM ipo madarakani, imefanya mambo mengi na mfano ni mji huo mpya wa Mabwepande. 

  Alisema kwa muda mfupi mji huo  umepiga hatua kubwa, na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi ambayo mingine imeshaanza, ikiwa ni pamoja na mabweni ya wasichana yanayojengwa kwa kushirikiana na  serikali ya Korea, barabara, madaraja, na mfumo wa maji safi na taka.

  Aliwataka wajivunie mafanikio chini ya serikali ya CCM na kuyatangaza, na kutowapa nafasi wapinzaniaambao wamekuwa wakipiga kelele bila kuona mafanikio hayo. Aidha, aliwahamasisha kushiriki vizuri katika mchakato wa kupata katiba mpya, hususan  wakati wa kura za maoni, kutetea misimamo ya Chama.

  Aliwaasa kujipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwakuchagua viongozi, wanaokubali kwenye jamii hodari na mchapakazi.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) na akipata maelezo kutoka kwa Bunker Roy(katikati) Mwanzilishi wa Chuo kinachofundisha mambo ya ufundi wa aina mbali mbali ikiwemo vifaa vya umeme wa jua katika kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajistan Nchni India akiwa katika ziara rasmi na ujumbe wake katika kukuza uhusiani na mashirikiano ya Kijamii.
  Wanafunzi wa kike kutoka nchi mbali mbali wakiwa na mashine ya Umeme unaotumia Jua wanafunzi hao wakiwemo na wanafunzi kutoka Zanzibar katika kisiwa cha Pemba tayari wameweza kujipatia elimu ambayo wanatweza kuwapatia na wenzao watakaporudi nyumbani, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliweza kujionea wanafunzi wanavufanya kazi zao akiwa katika ziara rasmi nchini India.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na mwenyeji wake katika Chuo cha ufundi wa Mafunzo ya Amali Bunker Roy(wa pili kulia) Mwanzilishi wa Chuo kinachofundisha mambo ya ufundi wa aina mbali mbali ikiwemo vifaa vya umeme wa jua katika kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajistan Nchni India akiwa katika ziara rasmi na ujumbe wake katika kukuza uhusiani na mashirikiano ya Kijamii.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na alipofika katika chuo cha ufundi wa mafunzo ya Amali akiwaangalia Wanafunzi kutoka Kisiwani Pemba Kazija Gharib Issa na Fatma Ali Vuai,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Kijiji cha TILONIA wialaya ya Ajmer Jimbo la Rajistannchini India katika ziara rasmi ya kukuza uhusiano.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na alipofika katika chuo cha ufundi wa mafunzo ya Amali akiwaangalia Wanafunzi kutoka nchi mbali mbali duniani wanofika kupata mafunzo hayo akiwa na ujumbe wake walipofika Kijiji cha TILONIA wialaya ya Ajmer Jimbo la Rajistannchini India katika ziara rasmi ya kukuza uhusiano.[Picha na Ramadhan Othman India.]

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq akimshukuru mmoja wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akimweleza kwa kina hali ilivyokuwa baada ya kutokea kwa mafuriko Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq. Nyuma katika picha ni sem trela tano zilizokuwa zimepakia vifaa na vyakula.
  Kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova akisalimiana na Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi.
  Mkurugenzi wa Home Shopping Centre Gharib Said Mohammed (GSM) kushoto akitembea na Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiq katika daraja lilosababisha watu wa kutoka Dar kwenda Dodoma kusimama kwa muda.
  Wathilika wa mafuriko wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq.

  0 0

  Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans wameagwa leo Mkoani Dodoma tayari kwa mazishi.

  Akiongea kwa masikitiko Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewashukuru watu waliojitokeza kuungana pamoja kuaga miili ya Askari hao.

  Pia amewataka madereva wote kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza za namna hii.
  Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akizungumza kwa Masikitiko wakati wa kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akiongoza waombolezaji kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari.
  Waombolezaji.
  Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ikiwa imebebwa.


  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi zawadi kwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vizuri katika chuo hicho.
   Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari Zanzibar Bw. Chande Omar akitoa ushauri wake kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mahafali ya tano ya chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, katika Viwanja vya Wizara ya Habari, Mnazi mmoja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, katika Viwanja vya Wizara ya Habari, Mnazi mmoja. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
    Akitangaza matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake. Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho. 
   Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuanzishwa. Kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba. 
   Nae Mgombea wa Chama cha CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. wakati Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1 
   Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.

  0 0

  It is with deep sorrow and grief that the Rweyemamu family from Mount Vernon New York, lost their mother, Mrs. Theonestina Rweyemamu (pictured) from a long battle with aggressive cancer.

  Her last wish was to be buried in Bukoba at our home – and since travel expense is extremely expensive, we are asking for a simple generous donation in order to fulfill her last wishes.

  You can send your contribution to: 
  BANK OF AMERICA 
  – Account # 483044166145, 
  Routing # 021000322. – DORIS RWEYEMAMU

  We thank you in advance for your kindness and generosity.


  For further information, please contact the following:

  Doris Rweyemamu 646 379 9135

  Emmanuel Rweyemamu 646 234 2418

  Steve Rweyemamu 302 883 7971

  Diana Rweyemamu 914 290 8170


  Mrs. Theonestina Rweyemamu


  Feb 1, 1952 – Feb 1, 2014


  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC  Tanzania,Bi.Mizinga Melu akiongea na watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijiini Dar es Salaam, wakati alipofika kituoni  hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na mashine ya kusagia juisi, alipoguswa kama  mzazi  na  maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akifurahia jambo na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi centre jijini Dar es Salaam,alipowatembelea na kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula.
   Baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika  kituo cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam wakipokea  zawadi za biskuti toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu,walipotembelea na mkurugenzi huyo kama mzazi na kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula pamoja na mashine ya kusagia juisi.
   Mkurugenzi Mtendeji wa benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu(kulia)akimuongelesha jambo mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam,alipotembelea kituo hicho kama mzazi aliyeguswa na maisha ya watoto hao na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,Kushoto  ni  Katibu Mhitasi  wa benki hiyo Jolanda Songoro.

  Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea moja ya msaada wa katoni ya pambazi kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka kwa Mkurugenzi  Mtendeji wa Benki ya Biashara ya NBC  Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati) Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni  Katibu Mhitasi wa benki hiyo  Jolanda Songoro.


  0 0

   Hey Michuzi
  Long time. Hamjambo?
  Was wondering if any of your people covered the swimming gala this morning at IST? Mdogo wangu there (in orange) has moved from London to Dar 4 months ago to discover his country and swam in his first competition today and placed 2nd. Not bad!
  Stay well kaka
  Best Wishes
  Jacqueline Kibacha


  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu vya Ubelgiji. Balozi Kamala kakutana na Watanzania hao leo hii Ubelgiji- Brussels kushauriana nao masuala mbalimbali ya kitaifa.

  0 0

  Hey guys!
  At Miss World, contestants usually need as much support as they can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the representative for Tanzania this year; Happiness Watimanywa.

  People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now.
  Please follow:
  @misstanzania2013 on Instagram
  @misstz2013 on twitter
  And Like Miss World-Tanzania on Facebook
  Thanks for the support.

  0 0


  SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,250 
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,750 

  SALOON CARS TO DAR/MOMBASA NOW £700
  4 X 4 CARS TO DAR MOMBASA NOW £780
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477


  0 0  0 0

   Rais Kikwete akihutubia maelfu ya watu waliofika kwenye sherehe hizo.


  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.

  "Najua wapo baadhi ya watanzania, walitaka Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,  ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa", alisema, Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

  Alisema Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo kutolewa kuhusu nini cha kufanya.

  "Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko hatujafika" alisema Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa sababu ndio hasa unaotakiwa.

  Alisema ziara za Kinana zinakijenga Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa wanachama waliopo ngazi za chini.

  "Katibu Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na ujasiri mkubwa kwa kwenda  maeneo ambayo ni magumu kufikika" alisema Rais Kikwete na kuongeza;

  "Katika ziara hizo  wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha, amewahi kutumia meli  ya MV Songea kutoka mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia wanachama wa ngazi za chini kabisa".

  Rais Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na  kula na wananchi katika ngazi za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo  na zaidi kutoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo na manung'uniko yanayowasibu.

  Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.

  "Pale ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM" alisema Rais Kikwete.


  0 0

  Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakareketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.
   Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.
  Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo. 

  Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo.Pichani nyuma kabisa ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.

  Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
  Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete  akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji. 
  PICHA ZAIDI  YA TUKIO HILI INGIA HAPA

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia vifaa mbali mbali katika chuo cha mafunzo ya Amali  kichofundisha wanawake pekee kutoka nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Zanzibar,katika cha  Tilonia,Wilaya ya  Ajmer Jimbo la Rajastan akiwa  katika siku ya pili ya ziara yake Nchni India pamoja na Ujumbe aliofuatana nao
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi mara alipowasili katika Chuo cha Mafunzo ya Amali kiitwacho Tilonia,Wilaya ya  Ajmer  Jimbo la Rajastan akiwa  katika siku ya pili ya ziara yake Nchni India pamoja na Ujumbe aliofuatana nao

   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) kwa niaba ta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini makubaliano  ya Uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw.Bunker Roy alitia saini (kulia) saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi Nchini India na ujumbe wake.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Bw.Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake katika Kijiji cha Tilonia  Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania  Debnath Shaw (kulia) baada ya Saini ya makubaliano ya uannzishwaji wa Chuo kama hicho Zanzibar. 
  Picha ya pamoja baada ya ziara hiyo. Picha zote na Ramadhan Othamn,Ikulu Zanzibar

older | 1 | .... | 345 | 346 | (Page 347) | 348 | 349 | .... | 3283 | newer