Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATETA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII NA NAIBU WAKE IKULU DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu na Naibu wake, Mohamed Mgimwa, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 27, 2014. Picha na OMR

PEACE AND SECURITY KEY FOR REALIZING INTEGRATION–ZZIWA REMARKS

$
0
0
EAC's Peace and Security Expert, Leonard Onyonyi makes his presentation during the Peace and Security.
A section of Members pay attention to the proceedings during the Peace and Security capacity building workshop.

Kampala, Uganda: The East African Legislative Assembly has rallied a call to Partner States to ratify the Protocol on Peace and Security in time to avoid an imminent delay of programmes and projects of the EAC.

The Protocol signed in February last year has been undergoing ratification in the Partner States and the process needs to be completed by mid-February 2014.Addressing a capacity building workshop for EALA Members on the Peace and Security Architecture this morning, EALA Speaker, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa termed the Protocol a key tool in the peace and security agenda of the Community. 

The Protocol touches inter alia on Conflict Prevention Management and Resolution, Prevention of genocide, combating terrorism, combating and suppression of Piracy and Peace and support operations.
So far, two Partner States – Uganda and Rwanda have appended their signatures to ratify the Protocol while the other three, Burundi, Kenya and the United Republic of Tanzania are at various stages in the process of ratification.

The Speaker of EALA, rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa remarked that it was important to have interventions that are dynamic given the fluidity of peace and security operations in the region.“I am of the view that the Peace and Security Sector in the EAC should be dynamic in order to respond to the nature and form of the ever evolving security threats, crime types and trends owing to advancement in technology, information dissemination and globalization”, she said.

“I am hopeful that we shall continue to see enhancement in the security of the citizenry of the region, thus access benefits resulting from the Customs Union, Common Market, Monetary Union and ultimately, the East African Political Federation”, Rt. Hon Zziwa added.

The EAC Peace and Security Expert, Mr. Onyonyi said that the EAC had entered into regional co-operation arrangements with a number of groups including Interpol, International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR), Eastern, Southern Africa Anti-Money Laundering Group (ESAALG) and the Regional Centre on Small Arms (RECSA) to deal with wide ranging matters including theft of motor vehicles, money laundering and small arms among others.

On women, peace and security, the EAC has put in place gender considerations in its interventions.  Mr. Onyonyi remarked that a Peace and Security Organ, which is expected to be established at a later date would require an amendment to the Treaty for the Re-establishment of the Community. 

“The Summit has directed the Secretariat to prepare a paper on how the Organ can be established and its operationalisation”, Mr. Onyonyi remarked. On South Sudan, the Speaker noted that noted that cessation of hostilities was only one step in the peace process.

“I had the privilege of meeting the Speaker of South Sudan last week immediately after the cessation of hostilities was signed in Addis Ababa, Ethiopia. It is comforting to note that apart from sporadic fires reported, peace largely prevailed in South Sudan over the weekend. The cessation of hostilities allows the two sides to begin talking.  It also allows the displaced civilians to have some peace, return home, treat their injured and forge some reconciliation,” she remarked.

In May, the EALA shall hold a Peace and Security Conference in Arusha according to the Chairman of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution.

GERMANY PRO HOLOCAUST EDUCATION

$
0
0
DSC_0083
United Nations Information Centre (UNIC), National Information Officer, Usia Nkhoma-Ledama delivering a message from the UN Secretary General’s to commemorate the victims of the Holocaust of 1933.

By Damas Makangale
THE Federal Republic of Germany is strongly supports the international cooperation in Holocaust education through the European Union, the United Nations and other International bodies in today’s globalized world.

Speaking to invited guests during the International day of commemoration in memory of the victims of the Holocaust today in Dar es Salaam, Embassy of the Federal Republic of Germany, First Secretary, Holger Pfingsten said that teaching about the Holocaust is not limited in educating students about historical facts but to make them understand the consequences of Hitler’s dictatorship.

MKUTANO WA CHADEMA MJINI IRINGA LEO

$
0
0
Hii ndio  Helikopta  iliyowakusanya  wana Iringa  leo uwanja wa Mwembetogwa 
Dr Slaa akiwasili katika  kiwanja cha Mwembetogwa leo 
Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwahutubia wana Iringa leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA CHICAGO CUBS TOKA KWA MMILIKI WAKE JOE RICKETTS, PIA APOKEA TABLET 61 KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SHULE YA WAMA NAKAYAMA

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts 
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete,  wakiangalaia matumizi ya moja ya Tableti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 zilizotoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts. PICHA NA IKULU.

MHE. BALOZI BEGUM K. TAJ AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO HISPANIA

$
0
0
 Tarehe 21 Januari, 2014 Mhe. Begum K. Taj, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake Paris Ufaransa aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa  Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania. Hafla hii ilifanyika kwenye kasri ya mfalme (Zarzuela Palace) Madrid Hispania.  Pichani Mhe. Balozi Begum K. Taj akimkabidhi Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania, Hati zake za Utambulisho.

Mhe. Balozi Begum K. Taj pamoja na mabalozi wengine waliowasilisha hati zao wakimsikiliza kwa makini Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania. Jumla ya Mabalozi 14 waliwasilisha hati zao siku hiyo.

balozi wa nigeria nchini amtembelea dkt salim ahmed salim

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Dr Salim Ahmed Salim akiongea na mgeni wake Mheshimiwa Balozi wa Nigeria Bwana Ishaya Majanbu aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe wa mwaliko maalum wa Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kushiriki katika Kongamano la Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali barani Afrika litakalofanika nchini Nigeria kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Muungano wa Shirikisho la Nigeria.

dkt emmanuel nchimbi akabidhi ofisi ya wizara ya mambo ya ndani

$
0
0
Na Hassan Mndeme na Tumaini Julius – Jeshi la Polisi 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Emmanuel Nchimbi ameahidi kushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi katika kuihimiza Serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo kwani anafahamu umuhimu wa wizara hiyo na changamoto zinazoikabili. 
 Alisema hayo kwenye kikao kilichofanyika jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya makabidhiano na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa waziri wa wizara hiyo. 
Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ni wizara muhimu katika mustakabali wa amani ya nchi hivyo ikiwa na bajeti ya kutosha itaweza kuwajengea watendaji mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao na kuongeza ufanisi, uaminifu na uadilifu katika utendaji wao wa kila siku. Aidha, alisisitiza kuwa misingi na wajibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kutoa haki kwa raia, wizara ikikalia haki nchi haitakalika, hivyo raia wanapaswa kupewa haki zao kwa wakati unaostahili kwani ni njia mojawapo ya kujenga ushirikiano na jamii na kuzuia uhalifu kabla haujatokea. Pia, Mhe Nchimbi amewataka wananchi kufuata sheria katika kutafuta haki zao badala ya kujichukulia sheria mkononi na kuwa serikali itawachukulia hatua za kisheria watu wote watakaobainika kushiriki katika vitendo vya kihalifu. 
Awali akimkaribisha aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Mathias Chikawe alihaidi kutoa ushirikiano kwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa raia kwa wakati unaostahili bila upendeleo ili kutoa uduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Amme Silima amewataka watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kufanya shughuli zao kwa kufuata maadili, sheria na kanuni za kazi zao ili wananchi waweze kupata huduma wanazostahili. 
Silima aliongeza kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili Wizara ya mambo ya ndani ni ufinyu wa bajeti, tabia za wananchi kujichulia sheria mkononi, matukio ya kufunga Barabara, mauaji ya kulipiza visasi au kuadhibu watu wanaotuhumiwa kuwa wahalifu na kusema vitendo kama hivyo havipaswi kuvumiliwa kwa vile vinaweza kusababisha machafuko makubwa hivyo wizara inapaswa kuandaa mikakati ya haraka ya kukabiliana na hali hiyo kabla haijasababisha madhara makubwa katika jamii. 
 Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Amme Silima, Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mwamini Juma Malemi, makamanda wa Vyombo vya dola vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani na wakuu wa idara hiyo.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza jana na wakuu wa idara za wizara hiyo baada ya kukabidhi rasmi ofisi kwa Waziri Mathias Chikawe aliyeteuliwa na Rais hivi karibuni kuongoza Wizara ya Mambo ya Ndani. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

nyumba za dar es salaam zaanza kupewa namba

$
0
0
 Taswira hizi ni sehemu ya nyumba za maeneo ya Temeke Wailesi jijini Dar es salaam ambazo zimeshapata namba katika mpango wa kuwa na Post Codes kwa jiji hilo kuu la biashara nchini Tanzania. Inasemekana asilimia 70  wakaazi wa jiji hilo  wanaishi katika maeneo yasiyopimwa. Mpango huu uliozinduliwa Septemba 14, 2012 una lengo la kurahisisha taarifa ya makazi ya watu kwa mitaa kupewa majina rasmi na nyumba kuwekwa namba.




mambo ya gado

bahati ya mtende...

$
0
0
Si mara nyingi  mtuunaweza kuapata bahati ya kukutana na kula taswirazzzz  ya aina hii. Lakini Ankal amepata bahati hiyo ya kuonana ana kwa ana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhan Dau (kulia) na  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango kabambe wa kugawa kompyuta aina ya Tablet kwa wanafunzi wa sekondari uliofanyika Jumatatu katika shule ya sekondari ya wasichana ya WAMA Nakayama kijiini Nyamisati Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani. 
Dkt Dau ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shule hiyo wakati Bw. Erio aliiwakilisha PPF kama mgeni mwalikwa, ambapo PPF ni moja ya wafadhili wa shule hiyo ambayo inasomesha bure mamia ya wasichana walio katika mazingira magumu ya kimaisha ikiwa ni pamoja na yatima na wanaotoka katika koo masikini zisizoweza kosomesha watoto wao. 
Majabali wawili hawa ni moja kati ya watendaji wanaoongoza kwa ufanisi mifuko ya pensheni nchini. Zaidi kuhusu siku hii BOFYA HAPA

MPIGA TUMBA MAHIRI WA TWANGA PEPETA,MCD AFARIKI DUNIA USIKU HUU MJINI MOSHI.

$
0
0
Mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed, ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD, na aliyekuwa bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band, amefariki Dunia usiku huu  katika hospitali ya KCM mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Taarifa hizo zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Hassani Rehani.
Tutazidi kupeana taarifa za msiba huu kwa kadiri  zitakavyokuwa zikitufikia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.

The day WAMA Nakayama girl's Secondary school in Rufiji went digital with Opportunity tablets...

Rais aamuru Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. Picha na Freddy Maro wa Ikulu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.

Rais pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.

Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza kujitegemea tena.

Rais Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.

Katika hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao wanalala, Rais Kikwete amesema   ameagiza Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.

“Kazi yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa   kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”

Kuhusu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha na hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”

Kuhusu malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini na waje kupata vichomi.”

                        Kuhusu maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya maji itakapoanza kupatikana tena.”

Kuhusu huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye makambi.

Rais ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.


                        “Hili ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”   

BALOZI KAMALA AMTEMBELEA MKUU WA ITIFAKI WA LUXEMBOURG

$
0
0
 Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea  zawadi Kutoka  kwa Mkuu wa Itifaki wa Serikali ya Luxembourg Balozi Sandra Thein. Balozi Kamala alimtembelea leo Balozi Sandra ofisini kwake Luxembourg.


Watanzania wahamasishwa kushiriki shindano la awamu ya tatu la ufadhili Kilimo cha biashara

$
0
0
 Mkurugenzi  wa Mfuko wa Sekta Binafsi Afrika (Africa Enterprise Challange Fund) AECF, Bw. Hugh Scott kati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu shindano la awamu ya tatu ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara, ambapo watazania wenye mawazo ya biashara katika sekta ya Kilimo wanahamasishwakuomba ushiriki.Kushoto ni Mjumbe  wa Kamati ya Uwekezaji ya mfuko huo, Dkt. Salum Diwani na kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko huo nchini Tanzania, Dkt. Alexandra Mandelbaum.
Watanzania wenye mawazo ya biashara katika sekta ya Kilimo wamehamasishwa kushiriki shindano la awamu ya tatu ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara kwa ajili ya kuendeleza sekta ya Kilimo ambayo inawagusa watu wengi nchini hasa waishio vijijini.
Mkurugenzi wa Africa Enterprise Challenge Fund (AECF), Bw. Hugh Scott aliwambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa mfuko huo umezindua shindano hilo ili kusadia  Kilimo cha biashara kama njia ya kusaidia kukuza sekta hiyo ya Kilimo hapa nchini.
AECF ni mfuko wa sekta binafsi wa dola za Kimarekani milioni 217 unasaidiwa na baadhi ya wafadhili wakubwa katika fedha za maendeleo chini ya Muungano wa Mapinduzi ya kijani ya Kilimo kwa nchi mbalimbali za Afrika (AGRA).
Mkurugenzi huyo alisema shindano hilo la awamu ya tatu ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara  linalenga kupata mawazo ya biashara katika maeneo mawili yakiwemo ya Kilimo cha biashara katika mnyororo wa thamani na katika ufumbuzi unaoongeza huduma za kifedha vijijini katika kusaidia uzalishaji katika kilimo cha kibiashara na sekta zinazohusiana.
Shindano hilo la dirisha la ufadhili Kilimo cha biashara maalum kwa ajili ya Tanzania lilizinduliwa tarehe 20, January mwaka huu na litakuwa wazi hadi hadi Machi 31, 2014.
Bw. Scott alisema awamu hii pia itashirikisha kufadhili waombaji watakaofanikiwa kupitia mchanganyiko wa ruzuku na mikopo itakayorejeshwa ya kati ya dola za Kimarekani 100,000 na dola milioni 1.
Alisema waombaji wa shindano hilo wanatakiwa kuonyesha mawazo ya biashara yenye matokeo ya uhakika kwa watu masikini vijijini nchini Tanzania, kuongeza ajira na mapato, kupunguza gharama na kuongeza uzalishaji.
Akifafanua zaidi alisema kampuni zinazostahili kuomba ni zile zinazohusika na ukulima au uzindikaji, wale wanaoanzisha mipango ya kilimo cha mkataba, watengenezaji na wasambazaji wa pembejeo za Kilimo, wachukuzi na wafanyabiashara na watoa huduma wengine katika sekta binafsi, ikiwemo huduma za taarifa ya soko. 
Alisema alisema fomu za kuomba kushiriki shindano hilo zinapatikana kwenye intaneti kupitia tovuti http//aecfafrica.org/windows/Tanzania-window.
Kwa upande wake, mjumbe wa kamati ya uwekezaji ya AECF, Dkt. Salum Diwani alisema matarajio ya shindano hilo ni kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania ili kusadia sekta hiyo kupiga hatua.
Alisema wenye mawazo yenye ubunifu wachangamkie fursa hiyo   ambayo italeta manufaa kwa maisha ya watanzania na  ukuaji wa uchumi vijijini nchini.
“Hii ni njia muafaka ya kusaidia mabadiliko katika mfumo wa soko nchini,” alisema na kuongeza kusema kuwa  wenye mawazo bora na bunifu ndiyo wanaolengwa katika shindano hilo.
Akifafanua zaidi alisema si rahisi kwa wakulima kupata huduma za kifedha duniani kote, hivyo mfuko huo umeamua kufanya hivyo kukiwezesha Kilimo kukuwa.
Alisistiza kuwa uchumi wa Tanzania na Afrika utakua kwa kasi kubwa kama sekta ya Kilimo itazidi kuboreshwa na kuwa hiyo ndiyo dhamira ya mfuko wao.
Awamu ya kwanza ya shindano hilo ilizinduliwa mwezi Novemba 2011 na kampuni 10 zilipata ufadhili wakati awamu ya pili ilizinduliwa mwezi Juni 2012 na kampuni 12 zilipata ufadhili.

Ujumbe wa Taasisi ya OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION watembelea zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali kutoka Nchni Marekani  (Opportunity Education Foundation) Bw.Joe Ricketts,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake aliofuatana  nao leo. 
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

white vs black party @ isumba lounge this saturday

$
0
0
THIS SATURDAY @ISUMBA LOUNGE(JOLLIES CLUB) W.V.B dress in white v/s black with the LEGENDS karibu sana. 

CCM YAENDELEA KUMNADI MGOMBEA WAKE KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muhammad Yussuf     akimnadi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muh’d Yussuf (hayupo pichani) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.

 Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akimpa maiki mwanawe Sukainnah Mahmoud Thabit awasalimie wanachama wa (CCM) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.

Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia wananchi waliofika katika kampeni zake katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja leo. 
Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar

BARAZA LA MADIWANI MAKETE LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2014/2015

$
0
0
 Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete likiendelea.
 Diwani wa kata ya Matamba mh. Asheli Mwalyoyo akichangia hoja
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka akiongoza kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoa ufafanuzi kuhusu suala la leseni katika baraza hilo.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete ambaye pia ni katibu wa kikao hicho Bw. Iddi Nganya akisoma taarifa ya rasimu ya bajeti ya halmashauri yake kwa mwaka 2014/2015.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akisikiliza kwa makini hoja za madiwani katika kikao hicho.
Na Edwin Moshi, Makete
Baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoaniNjombe leo Januari 28 limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2014/2015.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete madiwani hao wamejadili hoja mbalimbali zilizopo katika rasimu hiyo ikiwemo uboreshaji wa namna ya kuongeza mapato kutoka kwenye vyanzo vyote vilivyoainishwa na halmashauri hiyo.
Baadhi ya hoja zilizochangiwa na madiwani hao ni pamoja na halmashauri kuwa na vyanzo vya kukusanya mapato lakini kumekuwa na tatizo la mapato hayo kutofika kama yalivyokusanywa wakimaanisha kumekuwepo na kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya watendaji wanaokusanya mapato hayo.
Diwani wa kata ya Matamba (CCM) Mh. Asheri Mwalyoyo ametolea mfano katika kata yake kuwa kumekuwepo na ukusanyaji wa mapato lakini taarifa zinazofika wilayani zinaonesha yamekusanywa mapato kidogo ilihali ana uhakika yamekusanywa mengi.
"Tuchukulie kwenye kata yangu ya Matamba ushuru tu wa pombe kwa vilabu 10 tu ni shilingi 60,000/- kwa mwezi lakini kwenye taarifa huku wilayani inaonesha ushuru wa pombe za kienyeji ni 70,000/- sasa hii inashangaza maana tuna vilabu vingi, hapa ni kukosekana kwa uadilifu wa baadhi ya watendaji wanaokusanya mapato hayo" alisema Mwalyoyo.
Naye diwani wa kata ya Tandala Mh. Egnatio Mtawa ameshangazwa na hatua ya rasimu hiyo kuonesha kutegemea kwa kiasi kikubwa mapato ya pombe na kudai kuwa wahusika wote wakiwemo watendaji na wao kama madiwani walikuwa wavivu wa kufikiri kubuni vyanzo vipya vya kukusanya mapato badala ya kutegemea ushuru wa pombe kwa kiasi kikubwa.
Amesema hii inaashiria wananchi wazidi kunywa pombe kwa wingi ili mapato yapatikane lakini pia njia hiyo itachochea vilabu na baa kufunguliwa mapema tofauti na sheria inavyoruhusu hivyo kupata wingi wa wananchi watakao kuwa wamelewa muda wote hasa muda wa kufanya kazi.
Aidha rasimu hiyo pia imeainisha vyanzo vipya vitakavyosaidia kuongeza mapato ya halmashauri ikiwemo ushuru wa majengo ambapo watu waliokwisha jenga nyumba tayari watakuwa wanalipia ushuru wa jengo kwa mwaka na wale ambao bado wana mpango wa kujenga watalipia kabla ya ujenzi kuanza.
Halmashauri ya wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya ambayo ina vyanzo vichache vya mapato hali inayosababisha upatikanaji wa mapato yake kuwa mdogo, hivyo inaendelea kubuni vyanzo vipya ili mapato yake yaweze kuongezeka zaidi ya sasa


Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images