Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 337 | 338 | (Page 339) | 340 | 341 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Ramadhani Singano 'Mess' (kulia), akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Beki wa Rhino Rangers, Julius Masunga akitafuta mbinu za kumtoka Haruna Chanongo wa Simba.
  Moja ya Jeka heka zilizotokea katika lango la Rhino Rangers.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mlezi wa tawi la Yanga la Green Stone lililoko Mwananyamala , Yusuf Mwandeni akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa tawi hilo, Michael Machellah wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam.
  Mwanachama mpya wa Yanga, Michael Machellah akifurahia kadi yake ya uanachama wa Klabu ya Yanga mara baada ya kukabidhiwa na mlezi wa tawi hilo, Yusuf Mwandeni (wa tatu kushoto) wakati wa hafla fupi ya tawi hilo iliyofanyika katika Ukumi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wanachama wa Yanga,tawi la Green Stone la Mwananyamala wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam.

  Na Michael Machellah

  TAWI la Yanga la Green Stoni lenye makazi yake Mwananyamala CCM Mwinjuma jana limekabidhi kadi tisa kwa wanachama wake wapya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari mlezi wa tawi hilo la Green Stone mara baada ya kukabidhi kadi hizo, Yusuf Mwandeni alisema tawi hilo mpaka sasa lina jumla ya wanachama hai na wenye kadi 45 tangu lianzishe mwaka 20012.

  Mwandeni alisema tawi hilo kwa sasa liko katika harakati ya kuhamasisha wapenzi na mashabiki wa timu ya Yanga wachukue kadi na waichangie Klabu yao kwa kupitia kadi za uanachama na njia nyinginezo.

  Tawi la Green Stone linatarajia kufanya uchaguzi wiki ijayo Februari 2,2014 katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa nafasi ya Mwenyekiti,Katibu,Mwekahazina,Msemaji wa tawi na wajumbe wa kamati kuu ya Tawi.

  Nae Mwenyekiti wa Tawi hilo, Lumole Matovolwa aliushukuru uongozi wa Yanga kwa timu kuipereka Uturuki na juzi imeonyesha mambo mazuri ambayo wameyapata huko baada ya kushinda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ashanti United lakini pia aliitakia timu maandalizi mema na mazuri kwa yote wanayokabiliana nayo hivi karibuni tawi la Green Stone liko nyuma yao kwa sapoti ya namna yoyote.

  0 0

   Marehemu Mhandisi Adam Mayanza Ngaliga


  TAREHE NA MUDA

  TUKIO

  MAHALI

  JANUARI 26, 2014 SAA 10:00 JIONI

  MWILI KUCHUKULIWA KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI NA KUPELEKWA NYUMBANI KWA MAREHEMU BAHARI BEACH

  HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI – KUELEKEA BAHARI BEACH

  JANUARI  27, 2014 SAA 4:00 ASUBUHI

  KUANZA KUWASILI KWA WAOMBOLEZAJI NYUMBANI KWA MAREHEMU

  BAHARI BEACH NYUMBANI KWA MAREHEMU

  SAA 6:00 ADHUHURI – 7:30 MCHANA

  CHAKULA CHA MCHANA

  BAHARI BEACH NYUMBANI KWA MAREHEMU

  SAA 7:40 MCHANA

  MWILI WA MAREHEMU KUONDOKA NYUMBANI KUELEKEA KANISA LA MTAKATIFU ANDREA- BAHARI BEACH

  NYUMBANI KWENDA KANISANI

  SAA 8:00 MCHANA

  IBADA KUANZA

  KANISANI


  BAADA YA IBADA MSAFARA WA MAZISHI KUELEKEA MAKABURINI –BAHARI  BEACH

  MAKABURI YA BAHARI BEACH  0 0

  VICTORIA HOTEL NI HOTEL MPYA MJINI MTWARA  INAYOTEGEMEA KUFUNGULIWA SIKU CHACHE ZIJAZO MAENEO YA SHANGANI WEST MMILIKI WA HOTEL ANAPENDA KUTANGAZA NAFASI HIZI ZA KAZI ZILIZOZOBAKIA ZINAZOHITAJIKA KUJAZWA HARAKA IWEZEKANAVYO.

  RECEPTIONIST/ MAPOKEZI MTU MMOJA
  1. Awe mkarimu mwenye kupenda kuongea na wageni na uwezo wa kujielezea
  kwa lugha fasaha Kiswahili na kiingereza
  2. Awe mwenye huruma, heshima na mvumilivua kwa wageni pia apende
  kujituma na kuipenda kazi yake.
  3. Awe na uzoefu wa kazi hii kuanzia mwaka mmoja na kuendelea katika hotel.
  4. Aweze msafi / Mtanashati kwakila kitu.
  5. Awe anaweza kutumia compyuta vizuri Ms word, Ms Exell, na internet
  6. Aweze kusoma, kuandika na kuongea kiingereza kizuri
  7. Kama anatoka nje ya mtwara atapatiwa malazi bure
  8. Mshahara mzuri sana

  COOK / MPISHI MMOJA
  1. Awe chapa kazi mwenye kujituna na kuipenda kazi yake
  2. Awe msafi na mwenye uwezo wa kusimama mwenyewe baada ya kuelekezwa menu
  3. Awe na ujuzi wa kuchoma nyama vizuri pamoja na huduma ya A la carte
  4. Awe na uzoefu usiopungua miaka 2 kwenye restaurant ya maana au
  hotel yamaana sio mgahawa.
  5. Awe mtu anaejiheshimu na anaheshimu wateja pia anauwezo wa kuelezea
  chakula chake kwa wateja.
  6. Awe mbunifu na mwenye kichwa chepesi cha kujifunza vitu vipya
  7. Aweze kupika chakula chenye ladha
  8. Kama anatoka nje ya mtwara atapatiwa malazi na mshahara mzuri.

  KWA MAHOJIANO  YA SIMU KABLA YA KUTUMA CV PIGA SIMU HII 

  0685 116440
  UKIFANIKIWA UTAPATA EMAIL NA KUTUMA CV YAKO. 

  MMILIKI 
  VICTORIA HOTEL
  MTWARA.

  0 0

  Dear friends,
  we hope you had a good start into the New Year and a great 2014 ahead of you! A warm "welcome back" to our regular visitors and a hearty "karibu" to those who have not yet found us.
  Have a look at our program to see if there is anything of interest for you - great classes for fun, life-work balance, new hobbies....
  We are happy to introduce a new class in our program:
  SALSA CLASSES!
  Inline images 1

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent  Kalogeris Akimnadi Mgombea wa Udiwani Kata ya Tungi manispaa ya Morogoro Kupitia CCM Ndugu Mzeru Paulo

  0 0

  Machi 26, 2010: Ankal na mdau Hassan (wa pili kulia) wakipozi na crew nzima ya kipindi kikali cha TV cha Talk show  cha 'Sporah Show' wakati wa mkutano wa Diaspora jijini London. Wakati huko Uingereza kipindi hicho kilichojizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wa mtangazaji na mmiliki wake Sporah Njau (kushoto kwa Ankal), kinarushwa kupitia Ben TV  SKY Channel 184 hivi sasa kitaanza kurushwa nchini Tanzania kupitia CLOUDS TV kuanzia mwezi ujao. Globu ya Jamii inatoa pongezi sana kwa Sporah na kundi lake zima kwa kuzidi kupaa. Bofya video chini umsikie katika mahojiano na Ankal ambapo alielezea ndoto zake za kulete kipindi hicho nyumbani.Kunradhi kwa background noise.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi  alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi  Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma   baada  ya kuvalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanaCCM waliohuduria katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,mara alipowasili katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo 
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa  CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

     This is a 64 acre land with 25 acres of a beach plot >(facing the sea) in Bagamoyo.
   The following are some of the potential elements that makes this land unique.  
  It less than 2 kilometers from the proposed construction site of the  Bagamoyo port which would be the largest  in East and Central Africa in  the near future, handling numerous tons of cargo.
  I would advice you to come and visit the place 
  Asking price is $4million
  Joint Venture options are welcome.
   Contacts  0 0

  Tawi jipya la NMB Sumbawanga ambalo limehamishwa kutoka jengo la Bima lililopo makutano ya Mpanda-Msakila na linatoa huduma mbali mbali za kibenki na pia lina mashine tatu (3) za ATM.

  Afisa wa Mikopo tawi la NMB Sumbawanga, Godwin Nguma akimhudumia mteja wa mkopo katika tawi jipya la NMB Sumbawanga lililohamishwa kutoka jengo la Bima lililopo makutano ya Mpanda-Msakila.

  Wateja wa benki ya NMB Tawi la NMB Sumbawanga wakiendelea kupata huduma za kibenki katika tawi jipya la NMB Sumbawanga. Tawi hili linatoa huduma mbali mbali za kibenki na pia lina mashine tatu (3) za ATM.

  0 0

  Waziri mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wilaya ya Nanyumbu kulia ni waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo na kutoka kushoto ni Meneja Mwandaminzi wa TANESCO, Kanda ya Dar es salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara Mhandisi Mahende Mugaya,mkuu wa wilaya ya Nanyumbu, mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal mstaafu Joseph Simbakalia, Mbuge wa Nanyumbu Dastani Mkapa.
  Waziri mkuu Mizengo Pinda akiangalia moja kati ya magari yaliyo chomwa moto nyumbani kwa Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia Mpira wa Matambara wa kijana Hasani Kasim alipokuwa katika ziara ya kukagua adhari za vurugu mwaka mmoja uliopita katika Wilaya ya Masasi.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Masasi akimwonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda adhari za vurugu ambapo ofisi ya CCM ilichomwa moto mwaka mmoja uliopita.
  Sehemu ya jengo la CCM Wilaya ya Masasi ambalo liliteketezwa na moto mwaka jana.
  Waziri mkuu Mizengo Pinda akikagua nyumba ya Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe ambayo ilichomwa moto wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.Kulia ni Omary Lada mume wa Mbuge.PICHA NA OWM.  

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya,kikao kilichofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo. 
  Mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya mwishoni mwa wiki.
  ========  =======   =======
  WANAFUNZI 1725  WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO

  Na Denis Mlowe,Kilolo

  JUMLA ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.

  Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango  alisema wanafunzi wasioripoti kati ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937 sawa na asilimia 56.1

  Muwango alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni wanafunzi 3101 wavulana 1442, wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na wasichana 10 wamechaguliwa katika shule za bweni.

  Alisema wanafunzi waliopangwa kwenda katika shule za ufundi walikuwa wavulana 6 na hakuna msichana aliyechaguliwa na wanafunzi 3074 walipangwa katika shule za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.

  Aliongeza kuwa wanafunzi walioripoti hadi Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi 1349 wakiwemo wavulana 638 na wasichana 711 sawa na asilimia 43.

  Muwango alizitaja shule ambazo zina asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni shule ya Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi (19.3%),Udekwa (21%) na Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi walioripoti.

  Aliwataka walimu wa wakuu shule za sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 waliojiunga katika shule zao ili halmashauri iweze kujua na kujiridhisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa taarifa kwa wanafunzi wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata takwimu sahihi.

  Alisema kuwa halmashauri imeandaa mikakati kwa wanafunzi wasioripoti kwa kuwaandikia barua waratibu wote kuwafatilia wanafunzi  hao na kuwahimiza kuhudhuria katika shule walizopangiwa.

   Kwa upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita amewataka watendaji wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila kujali suala la ada na sare za shule.

  Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.

  “Haki ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana na tusiache wazazi wanaowaficha watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao kwa kuwaficha kuna kitu nataka kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni kumwongezea thamani mtoto na mzazi mwenye katika maisha yetu ya kila siku hivyo nawsisitiza sana watendaji wabaneni  sana wazazi wote wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule” alisema Guninita

  0 0

  Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza akimkumbatia mama mmoja kati ya wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye pamoja na rafiki zake wakiwemo wengine toka sekta ya uvuvi pamoja na wafanyabiashara walitembelea kituo hicho kwaajili ya kula pamoja na kutoa misaada kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya 2014.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bernard Polycap akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye aliwaasa wazee hao kuunda vikundi  kwa kuzingatia vipaji vyao na kujiorodhesha ili ofisi yake itizame jinsi ya kuwawezesha mitaji midogo midogo itakayo wasaidia kuanzisha miradi ya kujikimu kwa mahitaji binafsi.

  Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza (kulia) akimkabidhi msaada wa nguo Bi.Angelina Jonas katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2014 iliyofanyika katika Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugrnzi wa kituo hicho. 
  Makabidhiano yakiendelea katika kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza, ambapo zawadi za nguo, mafuta, sabuni, mchele, unga na bidhaa nyinenezo gawiwa kwa mabalozi wa wazee hao ambapo kila balozi anakaa na watu wake kisha wana gawana kwa usawa.
  Picha ya pamoja ya kamati ya wadau walio fanikisha sherehe hiyo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara   la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.

  Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

  Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.
   Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
  Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
  Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani,Mhe. Balozi PhillipMarmo (kushoto) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Ujerumani,Mhe. Joachim Gauck wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu ya Ujerumani,tarehe 13 Januari, 2014.
  Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani,Mhe. Balozi PhillipMarmo (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Ujerumani,Mhe. Joachim Gauck wakati wa hafla fupi ya kusilisha Hati za Utambulisho kwa Rais huyo iliyofanyika Ikulu ya Ujerumani,tarehe 13 Januari, 2014.
  Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani,Mhe. Balozi PhillipMarmo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na na Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania Ujerumani na Maafisa wa Idara ya Itifaki ya Ujerumani baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi Mdogo wa India aliyepo hapa Zanzibar Balozi Pawan Kumar aliyefika kwenye Ofisi yake iliyopo Baraza la Wawakilishi Mbweni kumuaga rasmi akikaribia kumaliza muda wake wa utumishi wa Kidiplomasia hapa Zanzibar.
  Balozi Mdogo wa India aliyepo hapa Zanzibar Bwana Pawan Kumar akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo Ofisini kwake kwenye jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Balozi Mdogo wa India hapa Zanzibar Bwana Pawan Kumari anayekaribia kumaliza muda wake wa kazi hapa Zanzibar kama ishara ya kumbu kumbu ya kuwepo kwake katika Visiwa vya Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Gavana wa Klabu za Lions za Tanzania na Uganda, Wilson Ndesanjo (kushoto) akigawa vifaa vya elimu zilizotolewa kama msaada na Klabu ya Lions ya Amani kwa Mwanafunzi wa kidato cha nne,Hawa Kassim kutoka Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, kwenye makabidhiano ya vitu kwa makundi mbalimbali, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Hafla hiyo ilihudhuria na Rais wa klabu hiyo, Ushman Khan (wa pili kulia) na wanachama wengine wa klabu hiyo.
  Gavana wa Klabu za Lions za Tanzania na Uganda, Wilson Ndesanjo (kushoto) akigawa baadhi ya vyerehanai vilivyotolewa kama mmsaada na Klabu ya Lions ya Amani kwa Mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Salma Khamisi, kwenye makabidhiano ya vitu kwa makundi mbalimbali, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Hafla hiyo ilihudhuria na Rais wa klabu hiyo, Ushman Khan (wa pili kushoto)na wanachama wengine wa klabu hiyo.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh, Dk. Seif Seleman Rashid (wa kwanza kulia) na mtoto kutoka familia ya Aga Khan (wa kwanza kushoto) wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dk. Seif Seleman Rashid akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliohudhuriwa na mtoto kutoka familia ya familia ya Aga Khan, Zahra ulifanyika katika ukumbi uliopo hospitalini hapo.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh, Dk. Seif Seleman Rashid (kulia) akibadilishana mawazo na mtoto kutoka familia ya Aga Khan, Zahra, wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh, Dk. Seif Seleman Rashid (wa pili kulia) akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni mtoto kutoka familia ya Aga Khan, Zahra akishuhudia, uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh, Dk. Seif Seleman Rashid akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa matibabu wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. 

  0 0
 • 01/27/14--06:45: SHUKRANI
 • Ndugu Max Edmund Kafipa wa Ununio Bahari Beach jijini Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa, marafiki wote na wakazi wa Ununio walioshirikiana nae katika msiba hadi mazishi ya mke wake mpendwa  Sophia Uledi Kafipa (pichani) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari tarehe 10/01/2014 na kuzikwa tarehe 13/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

  Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Mungu lihimidiwe.

  Amen

older | 1 | .... | 337 | 338 | (Page 339) | 340 | 341 | .... | 3284 | newer