Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 339 | 340 | (Page 341) | 342 | 343 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Mhe. Ramtane Lamamra (hayupo pichani) walipokutana pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea mjini Addis Ababa. Mazungumzo hayo yalihusu ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya gesi na umeme. Wengine katika picha ni Balozi Vincent Kibwana (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Waziri na Bi. Zuleikha Tambwe, Afisa Mambo ya Nje.
  Mhe. Lamamra naye akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yao.
  Mhe. Membe akiagana na Mhe. Lamamra mara baada ya mazungumzo yao.

  Na Mwandishi Wetu, Addis Ababa

  Tanzania na Algeria zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi mbili.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Mhe. Ramtane Lamamra walipokutana pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea mjini Addis Ababa, alisema kuwa Tanzania inayo mengi ya kujifunza kwa Algeria hususan katika sekta ya gesi na umeme kwani nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika sekta hizo.

  “Algeria ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia sekta ya gesi asilia na umeme hivyo tunapenda kupata utaalam huo ili mtufundishe namna ya kukuza uchumi wetu kupitia gesi” alisema Mhe. Membe.

  Mhe. Membe aliongeza kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa gesi asilia hata hivyo bado inakabiliwa na ukosefu wa utaalam wa namna ya upatikanaji na usafirishaji wa  gesi hiyo ili kukuza uchumi wa nchi. Alieleza kuwa Tanzania inayo mengi ya kujifunza kutoka Algeria kwani ni nchi yenye uzoefu katika masuala ya upatikanaji na usafirishaji wa gesi asilia.

  Katika hatua nyingine, Mhe. Membe alimuomba Mhe. Waziri Lamamra kuisaidia Tanzania kuzungumza na Serikali za Iran na Iraq ili ziweze kuifutia Deni Tanzania kama Algeria ilivyofanya mwaka 2012.

  Kwa upande wake, Mhe. Lamamra alisema kuwa,  Algeria ipo tayari kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika Sekta ya Gesi na Umeme na tayari Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Mhe. Sospeter Muhongo alifanya ziara nchini Algeria mwaka 2013. 
  Aidha, aliongeza kuwa, wakati wa ziara hiyo baadhi ya makubaliano katika sekta hiyo yalisainiwa ambapo Mhe. Muhongo pia alipata fursa ya kutembelea Kampuni kubwa ya Sonatrach inayojishighulisha na masuala ya gesi nchini humo.  
  Alisema  kuwa Waziri wa Nishati wa Algeria amefanya ziara nchini Tanzania mapema mwezi Januari, 2014 na kufikia makubaliano na Wizara husika kuhusu suala la gesi na umeme.

  Kuhusu suala la deni la Iran na Iraq kwa Tanzania, Mhe. Lamamra alisema  atalifikisha suala hilo atakapokutana na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo.“Ndugu yangu umefanya vizuri kulileta suala hili kwetu, hivyo nitalifikisha kwa wahusika ili kutafuta namna ya kulishughulikia” alisisitiza Mhe. Lamamra.

  Sekta ya gesi nchini Algeria inachangia Pato la Taifa kwa asilimia 55 huku asilimia 98 ya wananchi wanapata nishati ya umeme kwa matumizi mbalimbali.
  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) anatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015. 
  Kamati hiyo inayoundwa na  Maspika 37 walioteuliwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge Duniani Mjini Geneva. 
  Mkutano wa pili wa Kamati hiyo ya Maandalizi utafanyika mwishoni mwa mwaka huu. 
  Aidha, kabla ya kwenda Geneva, Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika Wellington, New Zealand kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2014. 
  Kwa ujumla, ushiriki wa nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri ya kuitangaza na kuipa heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa jukwaa madhubuti linalotumika kuiweka nchi katika ramani ya dunia na kuonyesha vivutio hususan katika nyanja za uwekezaji, utalii na maliasili pamoja na fursa mbalimbali zilizomo.

    
  Imetolewa na:

   Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
  Uhusiano wa Kimataifa,

  Ofisi ya Bunge,

  DAR ES SALAAM


  28 Januari 2014


  0 0

  Vijana wakitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya nadharia, badala yake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Maneno hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho ‘Safari Ya Ndoto’ inayobeba kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi.” 
   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema imefika wakati sasa watanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini na kutimiza malengo yao ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia. 
   “Imetosha kusema kesho, kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo. Kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji,” alinukuu Bw. Nguku kutoka kwenye kitabu chake chenye kurasa 108. Akielezea madhumuni ya kuandika kitabu hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam alisema: 
   “Hiki kitabu ni mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbali mbali katika maisha yao lakini hawajui pakuanzia, iwe ndoto ya kuwa mfanyabiashara maarufu, mwanasiasa au daktari bingwa. Hiki kitabu ni ramani maalum kwao.” 
   Aliendelea, “Kitabu hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa katika maisha. Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua ndoto zao na kufanikiwa katika yale waliyoyapanga.” 
   ‘Safari Ya Ndoto’ pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, mfanyabiashara maarufu Bw. Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Bw. Patrick Ngowi. 
   Kitabu hiki kinasambazwa katika maduka mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchi nzima ili watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh 5000 tu. Kwa sasa, mtunzi Nguku pia anaandika vitabu vingine viwili venye vichwa ‘Ndogo lakini muhimu, kesho’ na ‘What is life for!’ (Maisha ni ya nini!).

   Nguku anaelezea kwamba kitabu hicho yenye kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi,”inatoa hamasa kwa watu hasa hasa kundi la vijana waweze kuwa na uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Wanaoshuhudia ni mama yake mkubwa Bi. Anna Kikwa na baba yake mdogo Bw. Emmanuel Mallewo.
     Bi. Kikwa (kushoto) na Bw. Mallewo wakionyesha kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' alichokiandika mwanao Aman (katikati) anayesoma shahada ya uchumi mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Ardhi.
  Mtunzi wa kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' Aman Nguku akihojiwa na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kitabu hicho jana. Wanaoshuhudia ni walezi wake Bi. Kikwa na Bw. Mallewo.

  0 0

   Mhe Sophia M. Simba (Mb),  Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto

  0 0

   Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bw. Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu  akitoa maelezo ya utangulizi ya kufungua mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.

   Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro Mhe. Joel Bendera  akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.

   Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya Mgeni rasmi Mhe. Joel Bendera (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.
   Juu na chini ni Baadhi ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini. Picha zote na Veronica Kazimoto
   Na Veronica Kazimoto – Morogoro
  Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi popote pale duniani ni kigezo muhimu sana kinachotumika katika kupima na kufuatilia mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira ili kuiwezesha Serikali husika kuboresha Sera na Program mbalimbali za  kukuza ajira nchini.
  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera wakati akifungua mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa Bene mjini Morogoro.

  “Utafiti huu mbali na kusaidia kufuatilia mwenendo wa soko la ajira nchini, husaidia pia kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Millennia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Malengo ya MKUKUTA”, amesema Bendera.

  Bendera amefafanua kuwa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utatoa viashiria kama vile hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi, kiwango cha ukosefu wa ajira, kiwango cha ajira isiyo timilifu na ajira mbaya ambayo ni  hatarishi kwa watoto.

  Viashiria vingine ni wigo wa hifadhi ya jamii na hali ya kipato kutokana na ajira, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2013. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifu ya Takwimu, amesema taarifa za hali ya soko la ajira zinazotumika kwa sasa bado ni zile za mwaka 2006.

  “Takwimu za ajira zinazotumika sasa hazioneshi hali halisi ya mabadiliko yaliyotokea katika soko la ajira nchini, kutokana na hali hii Serikali pamoja na wadau wa maendeleo wameamua kufanya utafiti huu mwaka 2014 ili kupata hali halisi ya sasa”, amesisitiza Kwesigabo.

  Jumla ya wadadisi na Wahariri 100 wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kutoka kanda ya Pwani na Kusini inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Mtwara na Lindi wanaendelea kupewa mafunzo juu ya Utafiti huo utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka huu.

  Mafunzo kama haya yanafanyika katika kanda ya Ziwa, kanda ya Kati, kanda ya Kasikazini na kanda ya Juu Kusini ambapo ufunguzi rasmi umefanyika jana kwa baadhi ya kanda na leo katika maeneo mengine.


  Mafunzo haya ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yanafanyika mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya Wakufunzi wa utafiti huo takribani wiki tatu zilizopita.


  0 0

  MADAKTARI VPL KUWASILISHA VYETI TFF
  Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.

  Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.

  Pia TFF itatoa kwa madaktari hao fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu imeelekeza. 
  Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji.

  VPL KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR
  Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Januari 29 mwaka huu) kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini. 
  Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.

  Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.

  Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari na Mawasiliano
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anefanyia kazi Zanzibar Dk.Pierre Kahozi,leo alifika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mdogo wa India anefanyika kazi Zanzibar Pawan Kumar,alipo fika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mdogo wa India anefanyika kazi Zanzibar Pawan Kumar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi. Picha na Ramadhan Othman IKulu.

  0 0

  The Netherland-based, Rebel Group, recently won the $1 million advisory contract for managing the day-to-day operations of the proposed Dar es Salaam Rapid Transit (DART).
     Operations are expected to take off at the end of this year.
     “It is our honour to be part of this project in Tanzania, works of the project that is aimed at reducing traffic congestion at Dar es Salaam include constructing a 20.9 kilometre trunk road at the Kimara terminal, Kivukoni, Msimbazi, Fire, Gerezani and a part of Kawawa Road from Magomeni to the Morocco Road junction,” Rebel Group fare collection advisor, Jeroen Kok said after the deal ws sealed.
     Eighteen firms submitted an expressions of interest, but Rebel Group won out of the selected short-list of six names.
     During the signing of the contract, the Dutch company was represented by its financial advisor, Guillaume Remy while DART Agency was represented by its CEO, Asteria Mlambo. 
  The permanent secretary in the Prime Minister’s Office (Regional Administration and Local Government), Jumanne Sagini witnessed the event.
     The project that was launched in 2010 and expected to be completed at the end of this year is anticipated to ease transportation and traffic congestion in Dar es Salaam. It is hoped this will also open up other economic activities. 


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
    Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya jinzi mpango wa Stakabadhi Ghalani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
  Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal akitoa maelzo kwa Rais Kikwete juu ya mafanikio ya benki hiyo katika mpango wa Stakabadhi Ghalani ambao amesema unaendeshwa kwa mafanikio makubwa.

  0 0
 • 01/28/14--13:02: ONE YEAR DEATH ANNIVERSARY
 •  THE LATE MOSES TITO KACHIMA 
  (27.01.1945 – 29.01.2013)

  You are gone but not forgotten, you are a loss that we can’t replace, we loved you but God loved you more and in our hearts you will always live. Your love, your voice and your smile are forever imprinted in our minds. We remember and cherish the happy times together, remembering them today and forever. You have been a blessing in our lives and your memory lives on.


  Eternal rest grant to him O lord,
   and let perpetual light shine upon him. 
  May he rest in peace. 
  Amen


  0 0
 • 01/28/14--13:10: tushampiga everton 4-0


 • 0 0

  Mtoto huyu anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 2. hadi 2.5 kasoro ameokotwa eneo kati ya Jengo la Wazazi ndani ya  Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Tafadhali yeyote anayefahamu wazazi wake, au ndugu zake atufahamishe mara moja. Mtoto huyu kwa sasa tunaye  na ili uweze kumchukua uje na vielelezo vifuatavyo;

  1.    RB ya Polisi
  2.    Cheti cha Kuzaliwa cha mtoto
  3.    Picha ya mtoto mwenyewe
  4.    Kadi ya Kliniki ya Mtoto
  5.    Barua kutoka Serikali ya Mtaa ikikutambulisha
  6.    Kitambulisho cha Mpiga Kura
  7.    Kitambulisho cha Taifa kama tayari umepata

  Wasiliana nami kupitia 0755 648636. Mtoto hawezi kuongea vizuri hivyo tumeshindwa kufahamu vizuri jina lake anavyolitamka.

  0 0

  JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imeunga mkono kazi zinazofanywa na sekretarieti ya chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Abdulrahaman Kinana huku ikiwatupia lawama baadhi ya vigogo kutokana na kukwamisha juhudi hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda amesema, vijana wa UVCCM wanatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga chama kwa kusimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake.

  Makunda alisema, inapofika wakati wasimamizi wa chama wanapoanza kupigwa  vita juu ya kusimamia kanuni za chama hii siyo sahihi.

  “Haiwezekani matajiri na watu wenye uchu wa madaraka watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema kutakilinda chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu”Alisema.

  Hata hivyo Makunda alisema, wanaobezwa leo  kuwa wanaharibu chama ndiyo wameweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama , imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.

  Aidha Makunda alisema, mtu anayebeza ziara zilizofanyika na kuwaita viongozi walizozifanya ziara hizo ni waropokaji na wahuni anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

  “Muhuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo, hana maadili, asiyependa chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine” Alisema Makonda.
   Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
    Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitoa tamko la Jumuiya ya Vijana wa CCM kuunga mkono kazi ya sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu, Mh. Abdulrahaman Kinana.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo, akiwa ameongozana na manaibu wake, Mwiguku Nchemba na Adam Malima.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na manaibu wake, Mwigulu Nchemba na Adam Malima, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo. Kushoto ni Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen (wa pili kushoto) Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm (wa pili kulia) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Genevieve Kisanga (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Grace Usara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

  0 0

  'Simplified way' ya kuipata tovuti ya www.kandanda.co.tz , 'download App' yetu ya Kandanda Version 1.0 katika simu yako ya Android. Bofya hapa http://bit.ly/MpMnYV au katika tovuti kuna link kwenda katika google play.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee muda mfupi baada ya kutembelea banda la Mfuko huo.
  Ofisa Matekelezo Desiderius Buhiye akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa katika banda la NHIF kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana.
  Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru wakiendelea kupata huduma ya kupima afya zao.
  Upimaji ukiendelea
  Ofisa Matekelezo wa NHIF akitoa elimu kwa Maofisa wa Maendeleo ya Jamii waliofika bandani hapo kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali.

  SERIKALI imesema itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hususan za kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo pamoja na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ili wanufaike na huduma za matibabu.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana wakati alipotembelea banda la NHIF katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ambayo yamekwenda sambamba na Mkutano Mkuu wa Maofisa Maendeleo ya Jamii nchini.


  0 0

   President Kikwete delivers his keynote speech as he opens  the Agribusiness Congress East Africa at the Serena Inn in Dar es salaam  on Tuesday 28 JANUARY, 2014
   Participants listen attentively
   It's a full house
   "I thank the organisers for choosing Tanzania to play host to this important meeting: the Agribusiness Congress East Africa. I also commend them for organising the Congress so well and for choosing the theme “Driving Innovation for Agricultural Development in East Africa”, says President Kikwete in his keynote address. 

  0 0

  Marehemu Kepteni Sam Chekingo
  Habari zimetufikia punde kwamba rubani wa ndege maarufu nchini Kepteni Sam Chekingo amefariki dunia Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu Balozi Cisco Mtiro, misa ya kumuombea marehemu itaanza saa nne asubuhi nyumbani kwake, kabla ya mwili wake kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni saa tisa alasiri.
  Marehemu Kepteni Chekingo atakumbukwa kama mmoja wa marubani mahiri na wa muda mrefu wa ndege za serikali alikotumikia toka enzi za Rais wa awamu ya kwanza hayati Mwalimu Nyerere. Alistaafu kazi serikalini na kujiunga na Umoja wa Mataifa akifanyia kazi zake Congo Brazaville, kabla ya kurejea nyumbani na kujiunga na ATC alikofanyia kazi hadi mauti yalipomkuta.
  Mola aiweke Roho ya marehemu mahali pema peponi
  AMINA


  0 0


  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.     Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.


    Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

  Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.

    Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.

  Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.


  Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

older | 1 | .... | 339 | 340 | (Page 341) | 342 | 343 | .... | 3285 | newer