Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Maulid Nabihiyi 2014 Siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) - VOA KISWAHILI


mambo ya presidaa joseph kabila kabange

NEWS ALERT Mwanajeshi feki atiwa mbaroni Tanga akimtapeli DC

$
0
0
Na Mashaka Mhando,TANGA 

VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa,vinamshikilia Edwin John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa.

 "Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT).

Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate nafasi.

Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Tanga,Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema baada ya mahojiano ilibainika kuwa Mponji sia askari wa JWTZ ndipo akalazimika kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa alipopekuliwa alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.

Alisema wakati akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la Polisi lakini alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni alifanya njama za kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka ambaye alitoweka nayo.

Mponji alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya jeshi la Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya kueleweka juu ya wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga. 

Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini mtandao wake.
'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.
 'Koplo' feki akijiandaa kupanda  kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi
 'Koplo' feki akiwa na pamoja na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
  Rais  Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 Rais Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha. PICHA NA IKULU.

15 KUUMANA MREMA CUP 2014

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Moshi

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo (TLP), Dk. Augustino Mrema, amezindua mashindano ya soka, Mrema Cup 2014, yatakayoshirikisha jumla ya vilabu 15 kutoka katika kata zote 15 ya jimbo hilo.

Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya uzinduzi huo, Dk. Mrema alisema lengo la mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika jimboni hapo ni kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta mshikamano katika jamii.

Dk. Mrema alisema kwa sasa hakuna sekta inayofanya vizuri katika kutoa ajira kwa vijana kama michezo huku akisistiza umuhimu wa kushiriki michezo kwa lengo la kuhamasisha Amani, mshikamano na umoja katika jamii.

“Tunazindua mashindano haya kwa lengo moja tu, kuhamasisha mshikamano, amani na udugu wetu, dunia nzima hakuna sekta inayochangia kutoa fursa za ajira kama michezo hasa mchezo wa soka, vijana wakishiriki michezo wanapata kazi lakini pia inasaidia kuimarisha Afya,” alisema Dk. Mrema

Naye, Mratibu wa Mashindano hayo, inspecta msaidizi wa polisi kituo cha himo, Laban Sospeter alisema, Vilabu vitakavyoshiriki katika mashindano hayo ni Himo, Njia panda, Kahe, Makomu, Mamba, Kilema, Mandaka, Riata, Makuyuni, Mitsubishi na Kifaru ambayo ni timu mwalikwa.

Laban alisema baada ya uzinduzi huo, wanatarajia kuanza mashindano hayo wiki ijayo ambapo katika mechi ya uzinduzi kati ya Njia panda FC na Himo SC ulishuhudia Njia panda wakiibuka na ushindi wa 1-0.

Zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili ni shilingi laki tatu na mshindi wa tatu akiondoka na laki mbili fedha taslim ambapo jumla ya shilingi milioni moja zita zitashindaniwa.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014, katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikagua wachezaji wa klabu ya Himo na Njia panda katika mechi ya uzinduzi wa Mrema Cup 2014, uliofanyika juzi katika viwanja vya Himo, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014, katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

Kampuni ya Issere Sports yazawadiwa

$
0
0

Aliekuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo,ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri,Mh. Amos Makala  akimkabidhi vyeti vya utendaji bora wa huduma za michezo Mkurugenzi wa Masoko  Kampuni ya Issere Sports, Abbas Ally Issere katika kongamano la Wasanii lililoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Makala kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Issere Sports inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo nchini ni miongoni mwa wanamichezo, wasanii na awaandishi wa habari 1,000 waliotunukiwa vyeti vya utendaji bora katika fani za michezo kwa mwaka 2013 hadi 2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo ambalo kulitolewa mada mbili za kusaidia jamii ya wanamichezo kujiepuka na matumkizi ya dawa za kulevya, ya pili ikiwa ya maadili bora katika jamii, Kampuni ya Issere ni pekee iliyopata nafasi ya kuwakilisha nyingine zinazojihusisha na uuzaji wa vifaaq vya michezo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere aliyepokea vyeti hivyo kwa niaba ya wanamichezo wengine wa Kampuni hiyo alisema zawadi hiyo ni changamoto kwa wanamichezo kushirikiana pamoja badala ya kubaguana ili kurejesha heshima katika michezo kama ilivyokuwa miaka ya zamani na kutoa mfano kuwa katika riadha ilitawaliwa na Selemani Nyambui, Juma Ikangaa na Filbert bayi.

Kampuni ya Issere Sports ambayo imeingia mkataba wa kuuza jezi za Klabu ya Simba, imekuwa ikiuza na kusambaza jezi hizo nchini na Mashirika ya Umma, Wizara, Halmashauri za Wilaya na mashuleni katika ngazi ya shule za msingi, Sekondari na vyuoni.

ALIYEKUA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA SASA MKOA WA TANGA NDUGU SALUM MOHAMMED CHIMA AAGA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA TAYARI KWENDA KURIPOTI TANGA

$
0
0
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tanga aliyehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima akizungumza katika hafla fupi ya kuagana na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (kulia) leo baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete ambapo ameteua Makatibu Tawala wapya watano na kuhamisha wengine akiwepo Ndugu Salum Chima. Katika salamu zake za kuaga ameomba viongozi wote wa Mkoa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ya Serikali na wahisani mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa salam zake za maagano ambapo alisikitika kwa uhamisho wa kiongozi huyo ambaye kwake alikua kiungo muhimu na msaada mkubwa katika mambo ya kiutendaji. Aidha alisisitiza juu ya kuchapa kazi na ushirikiano baina ya viongozi wa Mkoa na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akitoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa Ndugu Chima kuhamishiwa Mkoa wa Tanga ambao ni Jiji akitokea Mkoa mdogo wa Rukwa ni "promotion" na anastahiki pongezi kwani uwezo wake wa kuchapa kazi ndo umemfikisha hapo alipo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sifa kubwa ya Ndugu Chima ni uwezo wake mkubwa wa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa wakati sifa ambayo ni muhimu kwa viongozi wa sasa katika maendeleo ya taifa letu.
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Ndugu Samson Mashalla (kulia) akiongea kwa niaba ya watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa. Alieleza kushtushwa na uhamisho huo uliokuwa wa ghafla ambapo kwa watumishi umekuwa ni kusikitisha kutokana na ukaribu, upole na upendo aliokuwa nao Ndugu Chima. Ndugu Chima aliwapenda watumishi wote wa ngazi za juu hadi za chini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Baadhi ya viongozi na watumishi walihudhuria katika hafla hiyo fupi ya maagano. WATUMISHI WOTE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA RUKWA WANAMTAKIA NDUGU CHIMA KILA LA HERI KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI AMBACHO NI MKOA WA TANGA. Tunaamini kuwa Tanga imepata kiongozi thabiti mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza katika kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa muda muafaka, "tunaomba apewe ushirikiano atafanya". Kwa upande wake Katibu Tawala Mteule wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa ndugu Symthies E.Pangisa aliyekuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara anakaribishwa kwa dhati Mkoani Rukwa na ameahidiwa ushirikiano katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa.(Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

SALAMU ZA PONGEZI

$
0
0
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF



Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha. 

Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima. 

Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini. 

PSPF - Tulizo la Wastaafu 
Mkurugenzi Mkuu 
Mfuko wa Pensheni - PSPF

Flaviana Matata Foundation kuendelea kushirikiana na PSPF kukuza elimu ya Tanzania

$
0
0
 Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo,wakati akizungumzia mradi wake unaotambulika kama “FMF Stationeries Project”; mradi unaojihusisha na uhamasishaji wa mashirika mbalimbali, taasisi za serikali na watu binafsi kuchangia na kusambaza vifaa mbali mbali vya shule kama vile madaftari ya mazoezi, kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe, vifutio na mabegi ya wanafunzi, kwa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu hapa nchini Tanzania.
Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke (kushoto) akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na jinsi Mfuko huo ulivyoweza kushirikiana na Flaviana Matata Foundation katika kusaidia kuinua elimu hapa nchini,ambapo kwa ushirikiano huo wamefanikiwa kusambaza vifaa vya shule (stationery kits) vinavyojumuisha mabegi ya shule, madaftari ya mazoezi na vitu vingine,Katika awamu ya kwanza ya mradi (Januari 2014) PSPF wamechangia “FMF Stationery kits” 1000 kwa wanafunzi wasiojiweza mkoani Pwani.
Mratibu wa Flaviana Matata Foundation (FMF),Lusajo Mwaisaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Mpango Mkakati wa Flaviana Matata Foundation kuendelea kusaidia wanafunzi wasiojiweza katika maeneo mbali mbali hapa nchini.Kushoto ni  Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata.
 Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata pamoja na Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke  wakifurahia jambo wakati wa kupata picha ya pamoja.

JOHNNIE WALKER YAFANIKISHA IRELAND SOCIETY OF TANZANIA GOLF CHAMPIONSHIP :

$
0
0
 Katka picha ya pamoja Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia
ya Serengeti Steve Gannon(kushoto)pamoja na mwandaaji wa mashindano ya 
Ireland Society of Tanzania Golf Championship(kulia)
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve
Gannon(kulia) akikabidhi Kombe kwa wachezaji wa timu ya Zimbabwe ambao 
waliibuka washindi katika mashindano hayo mwishoni mwa wiki.

Mdau Osman Bairu na malengo ya kiinua mchezo wa Cricket hapa nchini

$
0
0
Kwa Jina naitwa Osman Bairu ni Mwanamichezo na Mwalimu wa Mchezowa Kriketi (Cricket),Nilianza kucheza mchezo huu wa Kriketi nikiwa na umri wa miaka sita(6) nilipokuwa nchini India katika shule ya msingi iitwayo Barnes school.

Nilipokuwa shuleni India nilivutiwa na timu ya Taifa ya WEST INDIES na mchezaji aitwae VIVIAN RICHARDS ambaeni Keptein wa timu ya taifa ya WEST INDIES.

Katika kipindi cha Mwaka 1984 Nilifanikiwa kucheza katika timu ya shule katika nchi ya Panchigan -1996 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka kumi na saba(17) mjini Mombasa,nchini Kenya na baadae mwaka 1998 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania-Uganda nikiwa Mwafrika peke yangu.

Mwaka 1996 nilipata kushinda na kuwa mchezaji bora wa kuchipukia kutoka katika chama cha Kriketi (Cricket) Tanzania nikiwa Mwafrika wa kwanza. -Nina cheti cha ushiriki katika Kriketi kutoka Alayans Kriketi ligi ya Tanzania.

MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIMKA NA BODABODA YA VODACOM AKABIDHIWA KITITA CHAKE

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto)akimkabidhi Mshindi wa promosheni ya Timka na Bodaboda,Bw.Wiston Urio hundi yenye thamani ya shilingi Milioni ishirini(20,000,000) baada ya kuibuka mshindi wa mwezi Disemba. Ili kushiriki mteja promosheni hiyo mteja wa Vodacom hutuma neno Promo kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto)pamoja na Ofisa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo Mathew Mwampambe wakimshuhudia Bw.Wiston Urio ambaye ni mshindi wa wa Disemba wa shilingi Milioni ishirini(20,000,000)katika Promosheni ya Timka na Bodaboda akihakiki hundi yake kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Mshindi wa promosheni ya Timka na Bodaboda,Bw.Wiston Urio aliejishindia shilingi Milioni ishirini(20,000,000) baada ya kuibuka mshindi wa mwezi Disemba. Ili kushiriki mteja promosheni hiyo mteja wa Vodacom hutuma neno Promo kwenda 15544.
Mshindi wa Disemba wa shilingi Milioni ishirini(20,000,000)katika Promosheni ya Timka na Bodaboda inayonedeshwa na Vodacom Bw.Wiston Urio na Mkewe Consolata Urio wakionyeshwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu nyaraka kuthibitisha jinsi fedha za ushindi zilivyoingizwa kwenye akaunti ya benki ya Urio kupitia mfumo wa kielektroniki wa kibenki wa utumaji pesa. Kushiriki promosheni hiyo mteja wa Vodacom hutuma neno Promo kwenda 15544.
Mshindi wa Disemba wa shilingi Milioni ishirini(20,000,000) wa Promosheni ya"Timka na Bodaboda" Bw.Wiston Urio akitaniana na Mkewe Cosolata Urio huku akihakiki sifuri za kwenye hundi kama zimekamilika kwa thamani ya Sh. 20 Milioni alizojishindia. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.

MAALIM SEIF AKUTANA NA IGP MANGU PAMOJA NA MAKAMU WAKE ZANZIBAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Mangu, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alipofika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kujitambulisha. Katikati ni kamishna wa polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Ernest Mangu, ofisini kwake Migombani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Mangu, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alipofika ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Kutoka kushoto ni Kamishna wa polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu na Naibu Mkuu wa Polisi Abrahmani Kaniki.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na wasaidizi wao. (picha na Salmin Said, OMKR).

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


Dk. Shein azungumza na Balozi wa Italia Nchini

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Italia Nchini Tanzania Luigi Scotto,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Italia Nchini Tanzania Luigi Scotto,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais jana.PICHA NA IKULU,ZANZIBAR.

MH. JUMA NKAMIA ALIVYOLAKIWA KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto) akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam leo katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Elisante Olegabriel.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.Picha na Benjamin Sawe.

ISIKILIZE SINGO MPYA YA KIRARU RARU YA MSANII KILI THE CITY

Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani Moody Bawazir apiga jeki vifaa vya michezo timu ya uhuru na mzalendo

$
0
0
Kiongozi mzuri ni yule anayejitoa kwa watu wake. Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani,Moody Bawazir  leo amekabidhi vifaa vya Michezo kwa Uongozi wa Timu ya Uhuru na Mzalendo ambayo inajiandaa na mashindano ya NSSF CUP,Vile vile wiki anatarajia kutekeleza Ilani ya chama chake cha CCM.

JESHI LA POLISI LAZIDI KUIMARISHA DHANA YA POLISI JAMII

$
0
0
Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa, litamchukulia hatua kali mtu ama kikundi chochote katika jamii chenye lengo la kutaka kuvunja, kuhatarisha amani au kuwa sehemu ya uhalifu jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na kamishna wa Polisi Jamii Nchini (CP) Mussa Alli Mussa, wakati wa mkutano wa maofisa wa Polisi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali uliofanyika katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, jijini Dar es salaam.

Kamishna Mussa, alisema kuwa, kutokana na kupungua kwa matukio ya uhalifu na wahalifu, kumechangiwa zaidi na uelewa wa wananchi pamoja na kushiriki kwao katika dhana nzima ya Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi jambo ambalo kwa sasa limeifanya jamii kuishi kwa amani.

Hata hivyo, kamishna Mussa, aliwataka askari kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi ikiwa pamoja na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na kufichua mitandao ya uhalifu.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mambosasa, amewataka askari pamoja na watendaji wa Jeshi la Polisi kutokujitenga katika kueneza dhana ya Polisi jamii/Ulinzi shirikishi na badala yake wajikite zaidi katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuisaidia jamii kuondokana na changamoto za matukio ya uhalifu na wahalifu.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images