↧
SHORT COURSE ANNOUNCEMENT PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS Dates: 3rd – 7th February 2014
↧
Castle Lite kuwapeleka Watanzania nchini Afrika Kusini kushuhudia onyesho la Timbaland
Meneja Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Promosheni yao mpya kupitia Bia ya Castle Lite ya kupata washindi 12 watakaokwenda nchini Afrika Kusini kushuhudia onyesho kubwa la msanii maarufu duniani,Timothy Zachery Mosley kwa jina Maarufu anafahamika kama TIMBERLAND,Promosheni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo Januari 20 mpaka Machi 30.Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akisisitiza jambo juu ya namna wateja wa bia hiyo watakavyoweza kushiri kwenye Promosheni hiyo,ambapo amesema mteja atatakiwa kununua bia hiyo ya chupa na atakapoifungua ataona namba zilizowekwa ndani ya kizibo na atatakiwa kutuma jina lake na namba hiyo kupitia ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye namba 15499.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akionyesha namba itakayokuwa inatumika kwenye Promosheni hiyo.
↧
↧
TAARIFA YA MSIBA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF, anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw Philemon Minga kilichotokea usiku wa tarehe 19 January 2014 nyumbani kwake Mwenge mjini Dar es salaam.
Mfuko unaendelea na taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia ya marehemu na mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatano tarehe 22 Januari 2014.
Bwana alitoa Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.
Amina
↧
PSPF KWA KUSHIRIKIANA NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE KISARAWE
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kimanzichana iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Kulwa Kijangwa akipokea msaada wa vifaa vya shule kutoka kwa Ofisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Hawa Kikeke uliotolewa kwa kushirikiana na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaoishi katika mazingira magumu humo. Katikati ni mwanzilishi wa taasisi hiyo, Flaviana Matata. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Kisarawe, mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani wakicheza ngojela mbele ya wageni wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya shuleni hapo.
Wapigapicha wakiwa kazini.
Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Chanzige ambao wanaoishi katika mazingira magumu wilayani Kisarawe. Taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na PSPF walikabidhi vifaa mbalimbali vya shule kwa ajili ya watoto hao.(Picha na Francis Dande)

HARAKISHENI MCHAKATO WA KUIGEUZA BODI YA UTALII KUWA MAMLAKA YA UTALII - BALOZI MULAMULA
Na Geofrey Tengeneza
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula ametoa rai kwa vyombo vinavyohusika kuharakisha mchakato wa kuigeuza Bodi ya Utalii (TTB) Tanzania kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania ili kukiwezesha chombo hili kuwa na uhuru zaidi na uwezo mkubwa katika kutangaza vivutio vya utalii na kusimamia sekta ya utalii nchini.
Hayo yalisemwa na Balozi Mulamula hivi karibuni alipomtembelea Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce K. Nzuki ofisini kwake ili pamoja na mambo mengine kuzungumza namna gani Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani utasaidia juhudi za TTB katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la Marekani.“Ni muhimu ifike mahali TTB iwe na nguvu kisheria na uwezo zaidi katika kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa au kuwepo kwa migongano, hivyo ni vema mchakato huo wa mageuzi ukaharakishwa” alisema Balozi Mulamula.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo Dr. Aloyce Nzuki alisema tayari Bodi ya Utalii ilikwishaandaa andiko kuhusu kuigeuza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) na andiko hilo kwa sasa liko Wizarani.
Aidha balozi Mulamula ameipongeza TTB kwa kubuni onesho la utalii liitwalo Swahili International Tourism Expo (S!TE) litakalo kuwa likifanyika kila mwaka mwezi Oktoba ambalo litatumika pia kuonesha utamaduni wa mwambao na kukuza lugha ya Kiswahili.
Ameahidi kuweka kiunganisho (link) cha tovuti ya onesho hilo la S!TE katika tovuti ya Ubalozi. Sambamba na hilo amesema pia kuwa kuanzia mwaka huu ofisi yake ambayo imekuwa ikiandaa na kuratibu safari ya wafanyabiashara mashuhuri wa Marekani kutembelea Tanzania (VIP Safari) sasa itakuwa ikiandaa safari hiyo na kuwaleta wafanyabiashara hao mwezi Oktoba wakati wa onesho hilo la S!TE badala ya utaratibu wa zamani wa kuwaleta wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba.
Ameahidi kuwa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani utafanya kila liwezekanalo kusaidia juhudi za TTB katika kuitangaza Tanzania kama eneo zuri la utalii duniani na akaiomba TTB kuendelea kuwapa taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii kadri iwezekanavyo ili kuwasaidia kutekeleza azma hiyo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce K. Nzuki (kushoto) akimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula (kulia) baada ya balozi huyo kumtembelea ofisini kwake na kuwa na mazungumzo naye.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula akiangalia nakala ya andiko kuhusu mapendekezo ya kuigeuza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) ambalo limekwisha wasilishwa Wizarani.
↧
↧
NEWS ALERT: AJALI MBAYA YAUA WATU 13 HIVI PUNDE MKOANI SINGIDA
Watu 13 wanasemekana wamepoteza maisha baada ya gari ya abiria aina ya Noah walilokuwamo kupata ajali kwa kugongwa na lori mkoani Singida hivi punde. Habari zinasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi na dereva kushindwa kumiliki lori hilo na kujikuta likipinduka na kusababisha maafa hayo. Waliopoteza maisha ni pamoja na dereva na msaidizi wake.
CHANZO http://www. matukiotz.com/
↧
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Betty Mkwasa na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga washerehekea miak 25 ya Ndoa
Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na Januari 18, 2014 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa.
Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dodoma wakiwa na wake zao wakipiga picha na maharusi. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Bahi.
↧
In Loving Memory
↧
January Night Skies and the Year Ahead
↧
↧
Article 15
![]() |
SPECIAL FARE BOOK NOW FOR TRAVEL UNTIL JUNE 2014 WITH EMIRATES |
*Travel Validity: 20th January 2014 - 25th June 201 *Sales Validity: 20th January - 25th January 2014 * Fares Inclusive Taxes and Service Fee - subject to seats availability For More Information Email us : info@skylinktanzania.com or Call us on : +255 754 451111 |
↧
KIJIWE CHA UGHAIBUNI KESHO JUMANNE
Kesho Jumanne Jan 21, 2014a Benja, Yassin na Jabir watakuletea Kijiwe cha Ughaibuni cha kuwaga mwaka 2013 usikose.
↧
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI MTEULE WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi mteule wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponary Mlima, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponary Mlima, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili mazungumzo. Picha na OMR
↧
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO
↧
↧
Komando Hamza Kalala uso kwa Uso na Kamanda Ras Makunja
Juzi Kati ndani ya studio za Sibuka FM,Katika kipindi cha Pepeta Afrika, mgeni rasmi nyota wa wiki alikuwa kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni,aka Anunnaki Alien au "Watoto wa Mbwa".
Kamanda Ras Makunja alifanya maohijiano ya TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa, Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani alitoa wito kwa watanzania waishio ndani na nje ya Tanzania kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania ,pia kufanya tour za kimataifa.
Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa.
Katika studio za Sibuka FM,jijini Dar-es-salaam Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Hamza Kalala ambaye aliutaja muziki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko.
Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga. Usikose kuwasikiliza FFU wa Ngoma Africa band at www.ngoma-africa.com
↧
Dk. Shein apokea Kifimbo cha Malkia wa Uingereza,Pia awaapisha Viongozi katika Serikali ya Mapinduzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitembea na kifimbo cha Malkia wa Uingereza (Queens Baton) baada ya kukabidhiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania,(wa pili kulia) Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Gulam Abdalla Rashid,na katibu wa Mbio za Kifimbo na Mjumbe wa kamati ya Oilimpiki suleiman Jabir,(kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Kifimbo cha Malkia wa Uingereza (Queens Baton) kutoka kwa Katibu wa Michezo wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Zanzibar Hadaa Khatib,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya wanamichezo wa vikundi mbali mbali vya Michezo vya Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhi kifimbo cha Malkia wa Uingereza (Queens Baton) kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kutoka kamati ya Olimpiki Tanzania katika Viwanja vya Ikuli Mjini Zanzibar leo.
Kiongozi wa Kifimbo cha Kifimbo cha Malkia wa Uingereza (Queens Baton) Adam Best,akitoa maelezo kwa wanamichezo wa vikundi mbali mbali vya Michezo vya Zanzibar baada ya kukabidhi KIfimbo hicho kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ahmad Kassim Haji, kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi. Rukia Mohamed Issa,kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)
↧
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA SINGIDA KUFUATIA VIFO VYA WATU 13 KWENYE AJALI ILIYOTOKEA LEO
↧
News Alert: watu 9 wafariki dunia na 30 kujeruhiwa katika ajali mkoani lindi leo
Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi.
Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ambae alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo Taarifa zaidi za majeruhi hao pamoja na maiti zilizotambuliwa tutawajuza
Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwa
BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini |
Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa Maiti 9 za ajali hiyo
Ajali leo zachukua uhai wa watu 3 Same;
9 Manyara; 9 Lindi; 13 Singida
MANYARA: Woinde Shizza kutoka Arusha ameandika kwenye blogu yake kuwa watu 9 wamefariki dunia hivi punde huku mmoja akinurusika baada ya kufukiwa na kifusi wilayani Karatu, Mkoa Manyara wakati wakichimba mchanga katika eneo ambalo lilikuwa limezuiwa na Serikali, lakini watu hao wameanza tena kuchimba hivi karibuni.
KILIMANJARO: Katika taarifa ya habari ya Radio Sauti ya Injili, Moshi jioni hii, imeripotiwa kuwa watu watatu wamepoteza uhai huku wengine 30 wakiachwa na majeraha mbalimbali wakati basi la kampuni ya Hood lenye namba T.497AHD walilokuwa wamepakia kutokea Iringa kuelekea Arusha, lilipopata ajali majira ya saa 11 jioni kwa kuacha njia na kuanguka katika eneo la Nkwini, huko Makanya-Hedaru katika barabara ya Same-Mombo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Majeruhi wawili hali zao zimeelezwa kuwa mbaya hivyo kuwahishwa katika hospital ya rufaa ya KCMC. Majeruhi wengine wawili walitibiwa katika kituo cha afya cha Hedaru wakati miili ya marehemu waliotajwa na Robert Boaz (Kamanda wa
Source: http://www.wavuti.com

Polisi mkoani Kilimanjaro), kuwa ni Stephano Kasimba, Fadhili Kasimba na Aziza Mdee, imehifadhiwa katika hospitali ya Same ambako majeruhi wengine 25 wanaendelea na matibabu.
Walionurusika kifo wamesema basi hilo halikuwa katika mwendo ila dereva wake aliyetajwa kwa jina la Baraka Juma, alionekana kuwa mchovu na huenda ajali hiyo imetokana na usingizi uliomkumba dereva huyo ambaye ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea.
LINDI: Taarifa ya TBC Taifa iliyosomwa saa mbili usiku huu inasema kuwa, watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka chana wa leo katika kijiji cha Mambulu huko katika manispaa ya Lindi, wakati likipishana na lori kabla ya kupoteza mwelekezo na kupinduka wakati mvua kali ikinyesha.
SINGIDA: Imeripotiwa katika taarifa ya TBC saa saba mchana na mbili usiku uu kuwa jumla ya abiria 13 wakiwemo watatu wa familia moja, wamefariki dunia mkoani Singida leo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB.
Ajali hiyo ya mbaya iliyoacha miili ikiwa haitamaniki, imetokea leo mwendo wa saa moja asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma kwenye eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi kuelekea Singida Mjini huku lori lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Singida kuelekea Dar es Salaam, wakati likipishana na Noah hiyo, lilihama upande wake na kuifuata Noah upande wa kushoto na kuigonga na kuiburuza: “...baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisinzia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata Noah. Uchuguzi utakapokamilika tutatoa taarifa hiyo,” amesema.
Hadi sasa miili ya marehemu iliyokwishakutambuliwa na ndugu zao ni pamoja na Omari Shaaban (44) na mkewe Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi Mjini. Haji Mohammed (29) (Msisi), Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda), Salehe Hamisi (28) (Sajanranda), Samir Shaban (20) (Puma), Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi), Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).
Miili ambayo haijatambuliwa imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, mjini Singida.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida, Dk. Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya watu 13, wawili kati yao wakiwa ni watoto.
Katika ajali hiyo, abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo.

LIBENEKE LA MZUNGU KICHAA....
↧
MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Amesema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.
Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
↧
KAMPUNI YA CHINA WORLD BUZ YAENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA LEO
Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akizungumza na wafanya biashara wadogo na wakati kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa Semina kwa wafanya biashara hao iliyofanyika leo, kuhusu mfumo utakaosaidia wafanyabiashara wadogo wa Tanzania kutafuta masoko ya bidhaa nchini China na kuwapa taarifa sahihi za masoko kwa msaada wa kampuni hiyo,Mfumo huo hautampa gharama kubwa mfanyabiashara kama vile Usafiri , Chakula, Hoteli.kwani hatalazimika kusafiri kwenda China ili kununua bidhaa badala yake kampuni hiyo itamuagizia na kumfikisha mahali alipo ama kumshauri ni njia gani anaweza kutumia kupata bidhaa kutoka China, kulia ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu kushoto akipokea kipaza sauti kutoka kwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda ili kujitambulishwa kwa wafanya biashara hao.
Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akiwaelezea na wafanyabiashara wadogo malengo kampuni hiyo katika kuwakomboa wafanya biashara. ![5]()

Baadhi ya wafanya biashara wakiwa katika semina hiyo
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia majarida yanayoelezea mifumo ya ufanyaji kazi wa kampuni hiyo.
Uongozi wa kampuni ya China World Buz ukipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara hao baada ya kumalizika kwa semina hiyo.
Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akizungumza na maofisa wa kampuni hiyo kutoka china. ![9]()

Wakuu wa Kampuni hiyo wakipiga picha ya pamoja na maofisa wao
↧