Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 332 | 333 | (Page 334) | 335 | 336 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa kipindi cha watoto cha Luninga cha ‘JJ-Ubongo Show’ kitakachodhaminiwa na akauti ya Junior Jumbo na kurushwa katika vituo vya televisheni kwa lengo la kuwafanya watoto wapende masomo ya hisabati, sayansi na fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi wa Masoko, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa akimkaribisha  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa kipindi cha watoto cha Luninga cha ‘JJ-Ubongo Show’ kitakachodhaminiwa na akauti ya Junior Jumbo na kurushwa katika kituo cha televisheni cha TBC kwa lengo la kuwafanya watoto wapende masomo ya hisabati, sayansi na fedha. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(katikati) akitoa taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es as Salaam(kulia) ni Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve(Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo, Bw. Assah Mwambeni.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwa pamoja na Viongozi Wengine Wakuu wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akitoa taarifa rasmi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne(wa pili kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Pius Nyambacha.
  Baadhi ya Wakurugenzi mbalimbali wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Prereira Silima kwa Waandishi wa Habari leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

    Mheshimiwa Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  alipowasili wizarani leo asubuhi na kulakiwa kwa shangwe na wafanyakazi wa wizara hiyo.
   Mheshimiwa Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akipokea kadi ya pongezi kutoka kwa Kamishna wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa na katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome.
  Mheshimiwa Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akikaribishwa ofisini kwake na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome

  0 0

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto tarehe 21.1.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha mkutano.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye hoteli ya Serena tarehe 21.01.2014.


  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Elnest Mangu,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Elnest Mangu,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

  0 0


  0 0
  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini waliohudhuria Kongamano la siku mbili linalohusu Rasilimali za Gesi Asilia, Mafuta na Madini kwa Amani na Maendeleo ya Tanzania linalofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Agnes Hokororo (MB) akitoa rai kwa wananchi wake Wilayani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF ulioenda sambamba na upimaji wa afya bure chini ya uratibu wa NHIF Lindi uliofanyika leo hii kwenye viwanja vya CWT Ruangwa.
  Upimaji wa afya bure ukiendelea,madaktari wa mfuko na hospitali ya wilaya wameendelea kutoa huduma za uwiano wa uzito wa mwili (BMI),shinikizo la damu (BP) na sukari ambapo suala la lishe na shinikizo la damu (BP)ni changamoto iliyoweza kubainika hivyo ushauri ulitolewa,kushoto ni Dr. Rashida Omari wa hospitali ya wilaya akimpima kiwango cha sukari mzee Abdalah Ngawenje.
  Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwaeleza wanahabari (hawapo pichani) namna ya utekelezaji wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF utakavyoendeshwa,sambamba na mafanikio yanayotarajiwa kutokana na mkakati wa pamoja wa Mfuko na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa ulivyokusudiwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Agnes Hokoro (MB) akipima BMI kwenye viwanja vya CWT,anayempima ni afisa wa mfuko ofisi ya mkoa wa Lindi Laurent Hoja.
  Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Agness Hokoro hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo .

  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwl. Julius Nyerere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wapiga picha maarufu toka vyombo mbalImbali vya habari hapa nchini (enzi hizo) wakati alipokuwa akiwaaga ikulu jijini Dar es Salaam mwaka 1985. Toka kushoto waliosimama ni mpiga picha Mkuu wa Gazeti la Mfanyakazi Maxi Madebe, Mpiga picha mkuu wa SHIHATA Sam Mmbando, Mpiga picha mkuu wa gazeti la Daily News Vicent Urio na mpiga picha mkuu wa serikali John Baptist Makwaia. Wengine ni mpiga picha wa sinema wa taasisi ya vielelezo (AVI),Sailen, wapiga picha wa SHIHATA Juma Dihule na Adinan Mihanji. Mwisho ni mpiga picha wa maelezo, Moshy Kiyungi. Waliochuchumaa wa pili toka kushoto ni mpiga picha wa maelezo, Charles Kagonji, mpiga picha Daily News Gervas Msillo na mpiga picha wa maelezo Mwanakombo Jumaa. wengine ni mpiga picha mkuu wa Uhuru na Mzalendo, Khatib Ally na mpiga picha wa maelezo Raphael Hokororo.

  0 0

  Wanafunzi 4 wa Shule ya sekondari ya Sabodo iliyopo mkoani Mtwara,wamefariki huku wengine zaidi ya 35 wakmiwa wamejuruhiwa katika ajali iliyotokea iliyotokea mapema leo asubuhi baada ya wanafunzi hao kugongwa na gari walipokuwa katika mazoezi ya asubuhi (Mchakamchaka) shuleni hapo ambayo ipo Pembezoni mwa barabara kuku ya Mtwara ,Lindi kuelekea Dar es salaam.

  Waliofariki katika ajali hiyo iliyowakuta wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari ya Sabodo ni Ailat,Nasma na Hilda mmoja bado hajafahamika,Wote ni wanafunzi wa kidato cha kwanza na wametambulika kwa jina moja moja kwa kila mmoja..

  Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Ligula,mkoani humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

  Globu ya jamii inaendelea kufatilia na taarifa kamili itawajia baadae kidogo.

  0 0

  Kampala, Uganda: President Yoweri Museveni has today addressed the 4th Meeting of the 2nd Session of the 3rd East African Legislative Assembly in Kampala, Uganda.

  The President maintained that the EAC was on course and its progress irreversible.  The President noted that the Community was on the verge of prosperous economic development and better quality of life for its citizens following the significant progress in a number of socio-economic and political spheres.

  The Head of State remarked that what the region now needed was to strengthen competitiveness, address costs doing business and reduce risks.

  He noted that free movement was a key aspect of strengthening integration and remarked that the Republic of Uganda was committed to ensuring the Identity Cards’ project would soon be computerized to spur free movement.

  “Once this is done, many more people who cannot access passports which are expensive to acquire”, President Museveni remarked.


  0 0

  Kifungu 20 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2013 inamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali Rasimu ya Katiba ndani ya siku thelathini (30) baada ya kukabidhiwa rasimu hiyo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


  Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inaeleza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikabidhiwa Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba, 2013, na ataichapisha kwenye Gazeti la Serikali litakalotolewa Ijumaa, tarehe 24 Januari 2014.

  Aidha, kifungu 22 (1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2013, kinampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuteua wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka miongoni mwa majina yanayopendekezwa kwao na makundi yaliyotajwa ndani ya Sheria hiyo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anakusudia kukamilisha uteuzi wa Wajumbe hao baada ya kushauriana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwanzoni mwa wiki ijayo na majina hayo kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali kama kifungu 22 (3) cha Sheria iliyotajwa inavyomtaka kufanya.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu
  Dar es Salaam.
  22 Januari, 2014

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin kushoto akimkabidhi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamdam Omari Makame nishani ya heshima wakati walipokutana kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo mjini Lyon,Ufaransa.

  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

  SHIRIKISHO la Polisi wa Kimataifa Duniani INTERPOL, limesema litaendelea kuunga mkono juhudi zozote zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha na kudumisha hali ya usalama wa Visiwa vya Zanzibar kwa lengo la kuimarisha utalii kwenye eneo hilo.

  Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean- michel Louboutin, wakati alipokutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani Omari Makame, aliyetembelea Makao Makuu ya Shirikisho hilo mjini Lyon Ufaransa ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kiusalama yanayoigusa Zanzibar kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

  Bw. Jean-michel amesema ipo haja kwa jumuia nyingine za kimataifa kuunga mkono juhudi za Tanzania katika suala zima la kuimarisha usalama wa eneo hilo lenye historia inayovuta watalii kutoka katika Katika ziara hiyo ambayo ililenga kuimarisha usalama wa kikanda, Kamishna Hamdani alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania litaendelea kutoa msukumo na kushirikiana na Interpol ili kusaidia katika mapambano ya uhalifu wa kimataifa.

  Kamishna Handani ameutaja uhalifu ambao ni kero na kikwazocha uchumi kuwa ni pamoja na Ugaidi, Uharamia, Biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine unaovuka mipaka.

  Kamishna Hamdani ambaye amekabidhiwa nembo maalum ya Interol, pia alipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Makao makuu ya Interpol na kupatiwa muhtasari wa mafunzo yanayotolewa na Interol katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa na Askari wa kada mbalimbali.

  0 0

  Mheshimiwa akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kuwajali watoto wenye ulemavu kwa wazazi (hawapo pichani) waliofika kupokea msaada wa baiskeli kwa ajili ya watoto wao. Aidha, katika maelezo yake Mhe. Kairuki aliwasihi wazazi kutowaficha ndani watoto walemavu, bali wawapeleke shule na kuwapatia huduma zingine za muhimu ambaza wao kama binadamu wanatakiwa kuzipata. Pia aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto wenye ulemavu kwani ni ndugu zetu na wanastajili kusaidiwa. Mheshimiwa Kairuki alitoa jumla ya baiskeli 35 kwa watoto wenye ulemavu wa Kawe, jijini Dar es Salaam.
  Mheshimiwa Kairuki akimkabidhi baiskeli na vifaa mbalimbali mtoto mmojawapo (jina halikufahamika mara moja) ambaye ni mlemavu wa viungo ili imsaidie wakati wa kwenda shuleni na mahali pengine.
  Mheshimiwa Kairuki akimsikiliza Bi. Blandina Sembu ambaye ni Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) alipokuwa akitoa shukrani zake kwa Mhe. Kairuki baada ya kukabidhiwa baiskeli 35 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa viungo katika Kata ya Kawe.
  Mmojawapo wa wazazi wa Kata ya Kawe akimshukuru Mhe. Kairuki (hayupo pichani) kwa niaba ya wazazi wenzake kwa moyo wake wa utoaji na wa kuwajali watoto wenye ulemavu na kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kufika shuleni na mahali pengine kwa urahisi.
  Baadhi ya watoto wenye ulemavu waliofika kupokea baiskeli hizo kama msaada uliotolewa na Mheshimiwa Kairuki katika harakati zake za kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho. 
  Wajumbe katika kikao hicho.
  Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akisisitiza jambo wakati akiwatangaza washindi wa droo ya wiki ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa jana na kuwapata washindi wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 na kumpata Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa aliyejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akimpigia simu Bw. Edwin Edmund Kajimbo mkazi wa Iringa aliejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford, katika droo ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. Wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa jana, washindi 14 wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 walipatikana. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.


  0 0

  Na Miza Kona – Maelezo

  Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi atakayeweza kuingia katika bunge la katiba na kuyatetea na kuleta maslahi ya Zanzibar.

  Kauli hiyo ameitoa jana huko Kiembesamaki wakati alipokuwa akizindua kampeni na kumtambulisha mgombea uwakilishi kupitia chama hicho.

  Amesema kiongozi bora ni yule atakaeweza kuitetea Zanzibar na kuipatia maendeleo na kupata mamlaka yake kamili pamoja na  kuleta mabadiliko.

  Aidha ameeleza kuwa CUF inataka kuleta mabadiliko katika mambo ya muungano na kuona kuwa haki inafanyika katika nchi zote.  
  Aidha amesema kupita chama cha CUF wananchi watapata kiongozi mzuri atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kuitetea nchi bila ya woga wala kupoteza mwelekeo.

  “Mpeleke mtu atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kutetea maslahi ya Zanzibar”, alifahamisha.

  Hata hivyo amesisitiza kuwa uchaguzi ufuate utaratibu uwe huru na haki bila ya kushirikisha vyombo vyengine.

  Nae mgombea uwakilishi AbdulMalik Haji Jecha amesema pindipo wananchi watamchagua ataitetea Zanzibar kwa moyo wa uzalendo na kuleta maendeleo kwa maslahi ya nchi.

  Uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Kiembesamaki unafanyika kutokana na aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uwanachama kupitia CCM.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho wakirusha mabofu kama ishara ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Professa Ibrahim Haruna Lipumba katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.

older | 1 | .... | 332 | 333 | (Page 334) | 335 | 336 | .... | 3285 | newer