Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

SIMBA WAWILI WAUAWA KIJIJI CHA MATEPWENDE,WILAYANI NAMTUMBO

$
0
0


Na Yeremias Ngerangera….Namtumbo.

Simba wawili kati ya wanne wanaosumbua wananchi wa kijiji cha matepwende kata ya Msisima Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wameuawa kwa kupigwa risasi na mwananchi Omari Mtwalo Shekhe wa kijiji cha Matepwende kwa kushirikiana na askari wasaidizi wa wanyamapori wa kijiji hicho (VGS).

Mtendaji wa kata ya Msisima bwana Onesmo Mbiro alithibitisha kupigwa risasi simba hao muda wa saa nane mchana tarehe 11mwezi huu siku ya jumanne wakiwa wamejificha kwenye msitu uliopo jirani na mashamba ya wakulima.

Bwana mbiro aliongeza kuwa simba mmoja alipigwa na kufa hapo hapo lakini mwingine hakuweza kufia hapo badala yake alikimbia huku akiwa amejeruhiwa na asubuhi ya tarehe 12 alipatikana akiwa amekufa .

Fatuma Saidi mkulima wa mpunga wa kijiji cha Matepwende alidai wananchi wengi hawaendi shambani kwa hofu ya simba hao kwani bado simba wawili kuuwawa kwa kuwa walikuwa wanne katika kundi lao.

Fatuma alidai hofu ya wananchi hao iweze kuondoka ni mpaka pale itakapoonekana simba wawili wengine waliobaki wameuwawa machoni pa wananchi hao.

Tile Bashiru mkazi wa kijiji cha Matepwende alinusurika kuliwa na simba asubuhi na mapema wakati anaelekea shambani miezi mitatu iliyopita katika kijiji hicho na kuokolewa na umati wa wananchi baada ya yeye mwenyewe kupiga kelele kuhitaji msaada huku akiwa juu ya mti na simba wakiwa chini ya mti.

Bashiru alidai ni mungu aliyempa akili ya kuuparamia mti haraka wakati simba wale walipomwona na kutamani kitoweo na ndipo walipoanza kumkimbiza tile aliparamia mti uliokaribu kwa kuwa alifunuliwa na mungu kuwa hawezi kufika kokote na akili ikamtuma aparamie mti kwa haraka na kuwahi umbali mrefu hali iliyowshinda simba wale kufanya chochote baada ya kufika chini ya mti ule.

Wananchi walifurika na kwenda kumwokoa mwenzao na umati mkubwa wa watu ndio uliowafanya simba wale wakimbie katika eneo hilo na kumfanya tile anusurike kuliwa na simba hao.

Hata hivyo maafisa wanyama pori walihamia kijijini hapo na kupiga kambi lakini kwa mwezi zaidi ya mmoja simba hao hawakuonekana na badala yake maafisa wanyamapori waliacha silaha 2 aina ya raifoo katika ofisi ya kijiji na kumtaka shekhe Omari Omari Mtwala wa kijiji hicho kushirikiana na askari wasaidizi wa wanyamapori (VGS) kuendelea na doria kuwasaka simba hao ili wasilete madhara kwa wananchi.

Shekhe Omari Mtwala alisema kuwa alipatiwa taarifa na wananchi walioenda shambani asubuhi kuwa waliziona nyayo za simba katika maeneo ya mashamba yao na kuwafanya warudi shambani kwa hofu ya kuliwa na simba na ndipo yeye na askari wasaidizi wa wanyamapori wa kijiji walienda ofisi ya kijij na kwenda kuchukua silaha na kuelekea mashambani kulikoripotiwa kunekana nyayo za simba na kufanya doria.

Mtwala aliongeza kuwa wakati wapo kwenye doria ya kukagua nyayo za simba hao wakabaini wameingia kwenye msitu uliojirani na mashamba ya watu na wakaingia katika msitu huo kwa tahadhari kubwa na kuwaona simba hao wawili wakiwa wamelala pamoja na kuwamiminia risasi ambapo mmoja alikufa hapo hapo na mwingine alijivuta na kukimbia eneo hilo na leo tarehe 12 amepatikana amekufa.

Kijiji cha matepwende ni moja ya kijiji ambacho wananchi wake waliondolewa katika Hifadhi eneo la Ntanga lililokuwa na wanyama wengi na wananchi kuvamia eneo hilo kufanya eneo la Kilimo cha mpunga na kuondolewa mwaka 2017 na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Binilith Satano Mahenge kuwa eneo hilo ni Hifadhi ya wanyama na sasa wanyama wengi wanafurika katikaeneo hilo na kujitokeza katika makazi ya watu na kuleta hofu kwa watu wakihofia usalama wao.

TANTRADE, SISUPA WAKUTANA KUJADILI TIJA YA UZALISHAJI WA ZAO LA ALIZETI SINGIDA.

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji wa Alizeti mkoa wa Singida (SISUPA), Juma Mene akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha TanTrade na SISUPA kujadili jinsi ya kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti. (Katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Edwin Rutageruka, na Afisa Biashara wa Mkoa wa Singida, Daniel Munyi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAN TRADE), Edwin Rutageruka akiongoza majadiliano ya wadau wa zao la alizeti mkoani Singida jana, kwenye mkutano uliowakutanisha TanTrade na SISUPA kujadili jinsi ya kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti.
Viongozi wa SISUPA, Tantrade na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa zao la alizeti, wakifuatilia mada mbalimbali kwenye mkutano uliowakutanisha TanTrade na SISUPA kujadili jinsi ya kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti mkoani Singida juzi.
Kaimu Meneja wa Masoko ya Ndani kutoka Tantrade, Gertrude Ng’weshemi, akitoa mada mbele ya wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa zao la alizeti mkoani Singida jana. Mkutano huo uliwakutanisha TanTrade na SISUPA kujadili jinsi ya kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti.
Majadiliano yakiendelea.
Farida Muro kutoka Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Mt Meru mkoani Singida akizungumza kwenye mkutano huo.
Rehema Mbula kutoka Ilongelo mkoani Singida akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Simsopa, Singida MC, Timothy Kinara akichangia kwenye majadiliano ya namna ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao la alizeti mkoani Singida.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano huo.

Mmoja wa wajumbe akichangia .


WASINDIKAJI wa viwanda vya kuzalisha mafuta ya alizeti nchini wameomba serikali kufanyia marekebisho msululu wa tozo mbalimbali, ikiwemo VAT zilizopo kwenye mnyororo wa thamani eneo hilo, ili kuongeza tija, kutokana na tozo hizo kuonekana kikwazo kinachopelekea kufifisha ustawi wa viwanda hivyo na kutoa fursa kwa viwanda vya nje kuchukua nafasi kubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE) Edwin Rutageruka, akitoa taarifa fupi ya mambo yaliyojadiliwa kupitia mkutano wa Chama cha Wasindikaji wa Alizeti Singida (SISUPA) na Tantrade mkoani hapa jana, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi kuzungumza, alisema kuna haja ya kuongeza tija na uzalishaji wa zao la alizeti kutokana na ukweli kwamba zao hilo kama malighafi bado halitoshelezi

Akizungumza kwa niaba ya wadau hao, Rutageruka alisema ushuru mkubwa unaotozwa na halmashauri, sanjari na tozo za VAT kwenye bidhaa zitokanazo na zao la alizeti vimekuwa ni miongoni mwa sababu zinazoshusha kiwango cha uzalishaji, kutokana na wasindikaji na wakulima walio wengi kuvunjika moyo na kushindwa kuzalisha kwa tija kukidhi mahitaji ya ndani, sambamba na kukabiliana na ushindani toka nje

Alisema kulingana na majadiliano ya wadau, sababu nyingine zinazopelekea kufifisha ustawi wa zao la alizeti ni uchache wa wataalamu na maafisa ugani, sambamba na zao hilo kutokuwa na bei elekezi, ikilinganishwa na mazao mengine. Pia uhaba wa maghala ya kuhifadhia malighafi hiyo na teknolojia ndogo kuwezesha kuzalisha bidhaa yenye ubora stahiki kwa ushindani wa soko vimetajwa kama sababu

Mkurugenzi huyo wa Tantrade, alisema changamoto nyingine zinazokwamisha tija ya zao hilo ni kutopimwa kwa udongo wa ardhi inayozalisha alizeti ndani ya mkoa wa Singida, huku suala la uaminifu baina ya mkulima na mnunuzi wanapotekeleza kilimo cha mkataba limekuwa ni pasua kichwa. Na kwenye eneo hilo mikataba mingi imekuwa ikiandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Akijibu baadhi ya hoja hizo, Dkt. Nchimbi huku akionyesha kufarijika na kufurahishwa na ujio wa Tantrade, na hatimaye mkutano huo uliolenga kuongeza uzalishaji na tija ya zao la alizeti ndani ya Mkoa wa Singida, alisema suala la VAT ni la kitaifa zaidi, lakini kuhusu tozo kwenye halmashauri litashughulikiwa. Hata hivyo alisema ushuru wa mashudu ulishaondolewa lakini anasikia kuna baadhi ya halmashauri bado zinatoza

Kuhusu zao hilo mpaka sasa kukosa bei elekezi, Dkt. Nchimbi alisema kabla ya kupanga bei dira inapaswa kwanza kuundwa chombo cha kuratibu mwenendo mzima wa zao hilo. Aidha kuhusu matumizi ya lugha ya kigeni kwenye mikataba alisema mtu yeyote asilazimishwe kutumia lugha asiyoielewa

“Tantrade tusaidieni kuhakikisha mafuta yetu ya alizeti yanakwenda kuchangia kwenye pato la nchi, kinachounganisha wana-Singida ni alizeti,” alisema Nchimbi.

Aidha, katika hatua nyingine, kupitia mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu ya ‘Badili Gia tumia mbegu bora za alizeti zenye tija’ Nchimbi aliwataka wadau wote wa alizeti ndani ya mkoa wa Singida kufahamu kuwa mkoa huo ulikabidhiwa fedha na SADC Dola elfu 20 kwa ajili ya kuinua zao la alizeti, wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula na Lishe, yaliyofanyika mkoani hapa.

“SADC walitoa fedha hizo, ni jukumu lenu kujua fedha zenu hizo zimekwenda wapi, pia Tantrade fuatilieni,” alisema Nchimbi.

UMEME UMEBADILI MAISHA YA WANA-RUVUMA – RC MNDEME

$
0
0
Veronica Simba – Ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme ameipongeza Serikali kwa kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa mkoani humo, ambao umebadili hali ya maisha ya wananchi husika kutoka kwenye uduni na kuwa bora zaidi.

Alikuwa akieleza hali ya upatikanaji umeme mkoani Ruvuma kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, ambaye alimtembelea ofisini kwake akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 12, 2019.

“Tunamshukuru sana Rais John Pombe Magufuli kwa kutuletea umeme. Sisi tangu nchi inapata Uhuru, tulikuwa hatujawahi kupata umeme wa gridi; Sasa hivi tunafurahia umeme kila uchao.”

Akifafanua mabadiliko chanya yaliyoletwa na umeme kwa wananchi wa Ruvuma, Mkuu huyo wa Mkoa alisema yamejikita hasa katika shughuli za kimaendeleo.

Alisema, mashine za kusaga mahindi zilizokuwa zinatumia mafuta ya dizeli na ambazo zilikuwa nyingi, kwa kiasi kikubwa hazipo tena badala yake mashine nyingi sasa zinatumia umeme.

Alieleza zaidi kuwa, uwepo wa mashine zinazotumia umeme kusaga nafaka, kumepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kusaga nafaka hizo kwa wananchi ambao hutumia unga wa mahindi kupikia ugali, ambacho ni chakula chao kikuu.

Vilevile, alieleza kuwa vijiji vingi sasa vimekuwa na mwanga wa umeme hasa nyakati za usiku, tofauti na ilivyokuwa awali, ambapo vijijini kulikuwa na giza totoro.

Kufuatia suala hilo, aliipongeza serikali kwa kupitisha na kutekeleza azimio la kutobagua aina ya nyumba wakati wa kuunganisha umeme na kusema kuwa wananchi wengi wa maisha ya chini wanafurahia umeme kama wengine wenye kipato cha juu pasipo kujiona wametengwa.

Aidha, alishukuru kwa kazi inayoendelea ya kujenga miundombinu ya umeme ili kupeleka gridi ya Taifa wilayani Tunduru huku akibainisha kuwa ndiyo wilaya pekee mkoani humo ambayo haijafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati alimweleza Mkuu huyo wa Mkoa kwamba kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kupeleka umeme wa gridi Tunduru imekamilika na kwamba katika ziara yake amejiridhisha na hilo.

“Wataalamu wamefanya kazi nzuri sana na kwa sasa wanakamilisha kazi ndogo ndogo tu. Tunatarajia siku yoyote kuanzia hivi sasa, tutazima mitambo ya mafuta Tunduru na kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa.”

Katika hatua nyingine, Waziri aliahidi kuwashawishi wawekezaji waende mkoani humo kufanya tathmini kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza nguzo.

Alitoa ahadi hiyo kufuatia maombi ya Mkuu wa Mkoa ambaye alimweleza kuwa mkoa huo pia umejaaliwa kuwa na miti mingi hivyo ingefaa kukawa na kiwanda hicho ili kuunga mkono juhudi za serikali kutumia vifaa vya kuunganishia umeme ambavyo vinatengenezwa ndani ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme (kushoto), akizungumza na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, kuhusu hali ya upatikanaji umeme mkoani humo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, Desemba 12, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme (Meza Kuu-katikati), akizungumza na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, kuhusu hali ya upatikanaji umeme mkoani humo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, Desemba 12, 2019.

ZAIDI YA HEKARI 200 ZA MAZAO ZAHARIBIWA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MONDULI MKOANI ARUSHA

$
0
0
Na.Vero Ignatus,MONDULI

Zaidi ya hekari 200 za mazao mchanganyiko zimeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika kijiji cha Mbaash kata ya Selela wilaya ya monduli Mkoani Arusha.

Ambapo alisema kuwa katika eneo hilo niwakulima mbalimbali wanalima eneo la zaidi ya hekari 480 zilizoko ktika kijij hicho ambapo kwa sasa sehemu kubwa la eneo hilo limezingirwa na maji hali ambayo imewaweka katika njia panda wakulima wa eneo hilo.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Monduli  ambae ni Mkuu wa Wilaya hiyo IDD Hassan Kimanta mara baada ya kutembelea  baadhi ya maeneo ambayo mvua imeathiri katika kata ya Selela iliyoko wilayan Monduli mkoani Arusha.

Hata hivyo amesema kuwa wametembelea eneo hilo kuangalia na kutathimi hali halisi ya uharibifu wa mazao hayo ya chakula katika eneo hilo na kuweza kuchukua jitihada za dharura ili kuweza kunusuru mazao hayo ya wakulima ili kuepuka kupata hasara zaidi katika eneo liliobaki katika hekari hizo ili pia waakulima wa eneo hilo kutoendelea kupata hasara ili kuweza kutafutia njia ya kuchepusha maji hayo kuepuka hasara kubwa kwa wakulima hao na mvua ambazo zinaenedela kunyesha hasa kipidi hiki.

Amelezea na  kubainisha jitihada zinazoendelea kufanyika ikiwemo za kuweka vifusi katika baadhi ya maeneo ili kuunganisha mawasiliano wakati jitihada nyingine zikifanyika.

Amesema kuwa mvua hizo zinzoendelea kunyesha mkoani hapa zimeleta uharibifu mkubwa sana ikiwemo imeharibu Miundo mbinu ya Barabara, ambayo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano vya Kutoka Loliondo kuja Jijini Arusha.

Kwa upande wake kaimu meneja wa Tarura kutoka halmashauri ya Monduli alisema kuwa Mhandisi Janeth Erasto Mhokera amesema kuwa kufatia mvua hizo ambazo zimeleta uharibifu mkubwa kwa kukosekana kwa mawasiliano kama Tarura wamefanya jitihada za makusudi ii kuweza kurejesha mawasiliano ya vijiji hivyo ,pamoja na wakulima hao kuweza kuchepusha maji hayo ili kuweza kunusuru hekari nyingine kuendelea kuharibika na pia wakandrasi wako site kuendelea kumarisha barabara zote katika wilaya ili kuweza kukabiliana na hali ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha karibia maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Nae mtendaji wa kijiji wa kata ya Selela  bwana Emmanueli Nitalani   alisema kuwa kwasasa hali ya uharibifu wa mazao hayo mchanganyiko nikubwa sana  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa hasa kata hiyo karibia eneo kubwa la hekari 200 zimezingirwa na maji mengi haliambayo imewaweka njia panda na sintofahamu ya kujua cha kufanya katika eneo hilo walilolima hasa mahindi hasa kipindi hiki cha msimu wakilimo.

Kwa upande wake Wakulima wa eneo hilo bibie  Elikaa na Moleli laizer kutoka kata ya engaruka wa maeneo haya wanasema mbali na Miundombinu ya barabara pia Mvua iliyonyesha kwa imesababisha hekari za mazao yao shambani kuharibika kutokana na kusombwa na Mafuriko hali mbayo inawarudisha nyuma katika jitihada za kuweza kujikwamua katika lindi la umaskini.

Wakulim hao wameiomba Serikali kuweza kuwaletea mahindi kwa bei nafuu na kuweza kuwasaidia namna bora ya kuweza kunusuru mazao yao waliyolima eneo hilo .

hizo pia wameiomba serikali kuwza kuwapatia mbegu ili waweze kurudia na kuwahi hasa msimu huu wa mvua ili kutoweza kupata cahakula kingi kutokanana hali ambayo imekumba Kijiji cha Mbaash  katika kata ya Selela.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Monduli  ambae ni Mkuu wa Wilaya hiyo Idd Hassan Kimanta

VIJIJI 4 VYAKOSA MAWASILIANO SIKU KADHAA KATA YA ENGARUKA.

$
0
0
Na.Vero Ignatus,MONDULI

Zaidi ya hekari 200 za mazao mchanganyiko zimeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika kijiji cha Mbaash kata ya Selela wilaya ya monduli Mkoani Arusha.

Ambapo alisema kuwa katika eneo hilo niwakulima mbalimbali wanalima eneo la zaidi ya hekari 480 zilizoko ktika kijij hicho ambapo kwa sasa sehemu kubwa la eneo hilo limezingirwa na maji hali ambayo imewaweka katika njia panda wakulima wa eneo hilo.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Monduli  ambae ni Mkuu wa Wilaya hiyo IDD Hassan Kimanta mara baada ya kutembelea  baadhi ya maeneo ambayo mvua imeathiri katika kata ya Selela iliyoko wilayan Monduli mkoani Arusha.

Hata hivyo amesema kuwa wametembelea eneo hilo kuangalia na kutathimi hali halisi ya uharibifu wa mazao hayo ya chakula katika eneo hilo na kuweza kuchukua jitihada za dharura ili kuweza kunusuru mazao hayo ya wakulima ili kuepuka kupata hasara zaidi katika eneo liliobaki katika hekari hizo ili pia waakulima wa eneo hilo kutoendelea kupata hasara ili kuweza kutafutia njia ya kuchepusha maji hayo kuepuka hasara kubwa kwa wakulima hao na mvua ambazo zinaenedela kunyesha hasa kipidi hiki.

Amelezea na  kubainisha jitihada zinazoendelea kufanyika ikiwemo za kuweka vifusi katika baadhi ya maeneo ili kuunganisha mawasiliano wakati jitihada nyingine zikifanyika.

Amesema kuwa mvua hizo zinzoendelea kunyesha mkoani hapa zimeleta uharibifu mkubwa sana ikiwemo imeharibu Miundo mbinu ya Barabara, ambayo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano vya Kutoka Loliondo kuja Jijini Arusha.

Kwa upande wake kaimu meneja wa Tarura kutoka halmashauri ya Monduli alisema kuwa Mhandisi Janeth Erasto Mhokera amesema kuwa kufatia mvua hizo ambazo zimeleta uharibifu mkubwa kwa kukosekana kwa mawasiliano kama Tarura wamefanya jitihada za makusudi ii kuweza kurejesha mawasiliano ya vijiji hivyo ,pamoja na wakulima hao kuweza kuchepusha maji hayo ili kuweza kunusuru hekari nyingine kuendelea kuharibika na pia wakandrasi wako site kuendelea kumarisha barabara zote katika wilaya ili kuweza kukabiliana na hali ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha karibia maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Nae mtendaji wa kijiji wa kata ya Selela  bwana Emmanueli Nitalani   alisema kuwa kwasasa hali ya uharibifu wa mazao hayo mchanganyiko nikubwa sana  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa hasa kata hiyo karibia eneo kubwa la hekari 200 zimezingirwa na maji mengi haliambayo imewaweka njia panda na sintofahamu ya kujua cha kufanya katika eneo hilo walilolima hasa mahindi hasa kipindi hiki cha msimu wakilimo.

Kwa upande wake Wakulima wa eneo hilo bibie  Elikaa na Moleli laizer kutoka kata ya engaruka wa maeneo haya wanasema mbali na Miundombinu ya barabara pia Mvua iliyonyesha kwa imesababisha hekari za mazao yao shambani kuharibika kutokana na kusombwa na Mafuriko hali mbayo inawarudisha nyuma katika jitihada za kuweza kujikwamua katika lindi la umaskini.

Wakulim hao wameiomba Serikali kuweza kuwaletea mahindi kwa bei nafuu na kuweza kuwasaidia namna bora ya kuweza kunusuru mazao yao waliyolima eneo hilo .

hizo pia wameiomba serikali kuwza kuwapatia mbegu ili waweze kurudia na kuwahi hasa msimu huu wa mvua ili kutoweza kupata cahakula kingi kutokanana hali ambayo imekumba Kijiji cha Mbaash  katika kata ya Selela.
 Picha ni Mkuu wa wilaya ya monduli  Idd Kimanta akiwa wajumbe(hawapo pichani) wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya  Monduli mkoa wa Arusha wakikagua moja eneo la daraja katika kata ya Engaruka .

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 12.12.2019

WAKANDARASI NA WAZABUNI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA FEDHA NDANI YA BENKI YA CRDB

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga. Kongamano hilo liliratibiwa na Benki ya CRDB. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mkoa Geita, Injinia Robert Gabriel, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, Meneja wa Kanda ya Magharibi Benki ya CRDB, Saidi Pamui, Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya CRDB, Lusing Sitta

Na Mwandishi wetu.

Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kanda ya Magharibi ikihusisha mikoa ya Shinyanga, Geita, Tabora na Kigoma.

Kongamano hilo ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa miradi ya maendeleo ikiwemo makampuni zaidi ya 350 pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwamo, lilifunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo wakuu wa mikoa wa kanda hiyo.

Akitoa hotuba yake wakati wa kufungua kongamano hilo, Bashungwa, amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni vilivyo, changamkieni fursa hizo ili muweze kukuza biashara zenu na kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na hatimaye kulipa kodi stahiki za serikali.” alisema  Bashungwa.

Bashungwa pia alipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miondombinu mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi. “Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini, hongereni sana,” aliongeza Waziri Bashungwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ziwa, Aggrey Mwanri aliwahamasisha wakandarasi na wazabuni wa miradi ya maendeleo katika mikoa ya kanda hiyo ya magharibi kuchangamia fursa zinazotolewa na Benki yetu ya CRDB, ili kwa kushirikiana na serikali waweze lengo la kuimarisha miundombinu nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alimhakikishia Mheshimiwa Bashungwa kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali kutimiza azma ya ujenzi wa uchumi wa kati unoshamirishwa na viwanda kupitia uwezeshaji wa miradi mbalimbali nchini.

Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi nchini huku akitaja baadhi ya huduma ikawamo huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wazabuni ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama “Bid Guarantee” dhamana za utekelezaji wa miradi “Performance Guarantee” na dhamana za malipo ya awali “Advance Payment Guarantee”.

Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB pia imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo na hivyo kuwasihi Wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, kufungua akaunti, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.

Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Junior Construction Ltd na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi aliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akihutubia wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akihutubia wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi akichangia wakati wa kongamano hilo la wakandarasi na wazabuni wa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo.

BRELA YASHEREKEA MIAKA 20 KIDIGITALI ZAIDI NA MFUMO WA 'ONLINE REGISTRATION SYSTEM'

$
0
0
Mkakati wowote wa kukuza uchumi unawategeme wafanyabiashara, Tukiwa kwenyekilele cha miaka 20 tangu Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni kuanzishwa ni mambo mengi tunajivunia ikiwa ni pamoja na kufankiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa urasimu na rushwa uliokithiri katika taasisi hiyo. Heko nyingi kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kwa kubuni mfumo Madhubuti wa usajili kwa njia ya mtandao( ORS Online Registration System) Tangu mfumo huo wa ORS kuanzishwa yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tu zaidi ya makampuni 7000 yameshasajiliwa katika mfumo huo. Tathmini iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu imeonyesha kwa mwezi BRELA walikuwa wakisajili makampuni 60 tu lakini sasa kwa mwezi wanasajili makampuni 750 mpaka 800. Kwa zaidi ya silimia 50 urasimu na michakato mirefu ya kupata vibali na leseni za biashara pamoja na uwekezaji umepungua kwa kiasi kikubwa. Kujisajili kwa mtandao humwezesha mfanya biashara kutambulika na hivyo kuingia kwenye mfumo wa ushindani kwenye masoko mbali mbali ndani nan je ya nchi.

TPDC YAKABIDHI MILIONI 80 ILI KUBORESHA ELIMU NA AFYA WILAYA YA KILWA NA MKURANGA

$
0
0
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi fedha jumla ya Shilingi Milioni 80 ili kuboresha miundombinu ya elimu na afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.



Hii inafanyika ikiwa ni utaratibu wa TPDC wa kuwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika maeneo yanayopitiwa na miundombinu ya bomba la gesi linaloanzia Madimba Mkoani Mtwara mpaka Kinyerezi Dar es salaam. 


Kiasi cha fedha Jumla ya Shilingi Milioni 30 zimetolewa katika Shule ya Msingi Mtoni na Njianne zote zikiwa Wilaya ya kilwa kwa lengo la kuboresha Miundombinu ya elimu kwa kujenga Darasa na vyoo vya wanafunzi. 
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TPDC (Kulia) Bwn.George Seni, akikabidhi mfano wa Hundi kwa Mhe.Diwani wa Kata ya Tingi Bwn Dayani Mkenda katika Shule ya Msingi Njia nne.

Vilevile, katika kuboresha huduma za afya vijijini, TPDC imekabidhi kiasi cha Shilingi Milioni 50 kwa Halmashauri ya Kijiji cha Mwanambaya- Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Mwanambaya.

Akiongea katika hafla hiyo, Bwn Seni alisema "ili kuwa na Taifa bora lenye wananchi yenye afya na nguvu ni lazima watoto wazaliwe katika mazingira yaliyo na huduma bora za afya, ndio maana TPDC imeona vema kujenga Wodi ya mama na Mtoto ili kuwezesha huduma bora".
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TPDC Bwn.George Seni (Mwenye Suti), akikabidhi mfano wa Hundi kwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bwn.Athmani Manicho (Mhe.Diwani).

Bwn.Manicho aliahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo katika kujenga Wodi hiyo. Alieleza kuwa Wodi hiyo itahudumia jumla ya vitongoji saba (7) vilivyopo katika kijiji cha Mwanambaya vyenye wakazi zaidi ya 5,500.
Zahanati ya Mwanambaya, Mkuranga.Hapa ndipo kutajengwa Wodi ya Mama na Mtoto.

Kwa nyakati tofauti, wanufaika wa fedha hizo walitoa shukrani za dhati kwa *TPDC* kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii hasa katika Afya na elimu.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi fedha za ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Njia nne,Mhe.Diwani wa kata ya Tingi Bwn.Dayani Mkenda alitoa shukrani kwa TPDC kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali za kijamii ikiwemo kuboresha miundombinu ya shule ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira yaliyo rafiki.

"Kwa darasa hili linalojengwa kwa fedha za TPDC litawezesha wanafunzi kukaa vizuri darasani na kujisomea bila usumbufu" alionge Bwn. Dayani.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi fedha hizo .


#TPDCTUNAWEZESHA

TANZANIA, KENYA ZAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKINA KATIKA KUKUZA MAENDELEO

$
0
0

Tanzania na Kenya zimeahidi kuendeleza na kushirikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.  
Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 56 ya Jamhuri ya Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Tanzania na Kenya ni ndugu na nchi hizo zitaendelea kushikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya diplomasia ya uchumi baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.
"Sisi Tanzania na Kenya ni ndugu wa damu, kwa hiyo basi tunawatakia sana kila la kheri katika kuiletea Kenya maendeleo…lakini mjue kuwa maendeleo ya Kenya ni maendeleo ya pia ya Tanzania, maendeleo pia ya Uganda, ni maendeleo pia Burundi, maendeleo pia Rwanda na Maendeleo pia ya Sudani Kusini na ni maendeleo pia ya jumuiya ya Afrika Mashariki" Amesema Prof. Kabudi
Kwa upande wake, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Kenya na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Kenya.
"Napenda kuwafahamisha kuwa umoja na mshikamano wetu umekuwa chachu ya maendeleo baina ya mataifa haya mawili…..tukumbuke kuwa umoja ni nguvu na dhamira yetu ni kushirikiana na mataifa yote duniani. Na dhamira yetu ni kuishi kwa amani umoja na mshikamano ili kukuza uchumi wetu," Alisema Balozi Kazungu
Aidha, Balozi Kazungu amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la Kenya kutokana na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi ya Kenya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
"Itakumbukwa kuwa, mwezi Aprili 2019 Kenya tulipokutana na Tanzania jijini Arusha tuliweza kuondoa vikwazo vya biashara 25 kati ya 37, hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani Kenya na Tanzania na ndugu ambao wanapenda kukuza na kuendeleza maendeleo ya biashara" ameongeza Balozi Kazungu.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akihutubia hadhara iliyojitokeza wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya jana jijini Dar es Salaam 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu.

Baadhi ya wageni waalikwa wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Kenya kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya nchi hiyo. 
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya jana jijini Dar es Salaam 


KTO YAPONGEZWA KATIKA KUSHIRIKI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Karibu Tanzania Organization (KTO) imekuwa ni moja kati ya washiriki bora katika kuisaidia Serikali katika kutatua changamoto za kijamii hasa katika masuala ya elimu, ujinsia na kusaidia watoto wa kike katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mafunzo maalumu ya siku tano kwa walimu na wakufunzi kutoka vyuo maendeleo ya  wana nchini nchini Katibu Mkuu kutoka Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamiii Dkt. John Jingu amesema, KTO ni moja kati ya wadau muhimu ambao wamekuwa waliofanya kazi na Serikali kwa ukaribu zaidi.

"Nianze kwa kutoa pongezi kwa taasisi hii hasa kwa kuendelea kumlinda na kumwendeleza mtoto wa kike Tanzania, mmekua mkishirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na
Programu hii iliyowakutanisha ya kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi ni muhimu na kubwa zaidi mmeangalia masuala ya kijinsia na malezi:  tunahaidi kuendelea kutoa ushirikiano ili tuweze kufikia azma tuliyojiwekea hasa katika kumwezesha mtoto wa kike" ameeleza Dkt. Jingu.

Amesema kuwa Asasi za kiraia zifanye kazi kwa ukaribu na Serikali katika kushughulikia matatizo ya wananchi na kueleza kuwa kupitia programu hiyo ya malezi na makuzi kwa watoto ni muhimu sana  kwa kuwa msingi mkuu  wa malezi kwa mtoto ni katika miaka  5 tangu kuzaliwa ambayo ndio muhimu katika misingi ya ukuaji kwa watoto kiakili, kimaono na kihisia.

"Watoto ndio msingi wa taifa, jinsi watoto wanavyolelewa sasa ndio picha ya taifa la kesho litakavyokuwa na tuna mpango wa kuwa na vituo vya malezi nchi nzima kwa malengo ya kuwajenga ili wawe wazalendo, wachapakazi pamoja na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa hata na wanafamilia lakini pia vituo hivyo vitawasaidia watoto kutoa taarifa na watakuwa salama zaidi" Ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu ya mafunzo ya ufundi (TVET) Dkt. Noel Mbonde amesema kuwa KTO ni wadau wakubwa katika sekta ya elimu na programu za taasisi hiyo pia zimeisaidia pia Wizara hiyo katika kuboresha utoaji wa huduma bora zaidi.

" Ninaamini kwamba Wizara imepata mwarobaini wa changamoto za watoto wa kike kuacha shule kwa matataizo mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni, tutawapeleka kwenye vyuo hivi ili wapate elimu  na watoto wapate malezi bora" ameeleza.

Amesema kuwa takribani shilingi bilioni 38 zimetengwa katika kuhakikisha kila Chuo cha maendeleo ya jamii kinakuwa na darasa la chekechea ambapo hadi sasa madarsa 20 yamekamilika, 20 yanajengwa na hadi kufikia Aprili 2020 vyuo vyote vitakuwa na madarasa hayo.


Awali akitoa maelezo kuhusiana na taasisi hiyo Mkurugenzi wa miradi (KTO) Mia Mjengwa amesema kwa siku hizo tano wametoa mafunzo kwa vitendo ambayo wanaamini yataleta tija katika sekta ya elimu na kueleza kuwa ni muhimu sana kuwa na vituo vingi vya chekechea kutokana na misingi ya malezi na makuzi ya watoto huanzia hapo.

Amesema kuwa wakufunzi  kutoka vyuo vya maendeleo  ya wananchi wana nafasi kubwa sana katika kuleta maendeleo kwa kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu zaidi na wanajamii.

"Miaka ya 60 Hadi 70 Sweden ilianza kuwa na elimu ya chekechea naamini ni sawa na hapa Tanzania, na kwa sasa taifa limejiegemeza katika kujenga uchumi, Hapa Kazi Tuu! kadri maendeleo yanavyokua akina mama wanajishughulisha katika shughuli za maendeleo hivyo lazima kuwe na sehemu sahihi na salama za kuwaacha watoto wetu" ameeleza.


Pia mwenyekiti wa Bodi ya KTO Aidan mchawa amesema kuwa
Serikali imeendelea kushirikiana na taasisi hiyo kupitia  Wizara za afya na elimu ambao wamekuwa wakishirikiana katika kufanikisha programu hiyo;

"Wizara ya elimu, kupitia idara ya elimu  imeonesha ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha KTO inasonga mbele zaidi, na tanaamini tutafika mbali na tunaomba Wizara kushirikiana nasi katika kuendesha mafunzo ya namna hii kwa vyuo vyote 54 vilivyopo nchini" ameeleza.

Baadhi ya washiriki ambao ni wakufunzi waliohudhuria kikao kazi hicho wameonesha kufurahishwa kwa namna serikali inavyoshirikiana na asasi za kiraia katika kutatua changamoto za kijamii.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamiii Dkt.John Jingu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya siku tano kwa walimu na wakufunzi kutoka vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini ambapo  amesema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kutatua changamoto za wananchi, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati hafla ya  ufungaji wa mafunzo hayo na kuwataka wawezeshwaji kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta matokeo chanya katika jamii, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa miradi (KTO) Mia Mjengwa akitoa taarifa ya kikao kazi hicho kilichofanyika kwa siku tano na kueleza kuwa malezi wapatayo watoto sasa ni picha ya taifa la baadaye hivyo lazima wapate elimu Bora ya makuzi, uadilifu na kufanya kazi. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa elimu ya mafunzo ya ufundi (TVET) kutoka Wizara ya Elimu Dkt. Noel Mbonde akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo ambapo amesema kuwa vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi lazima viwe na madarasa ya chekechea na mchakato umeanza na utakamilika Aprili 2020 kwa bajeti ya shilingi bilioni 38, leo jijini Dar es Salaam
Mkufunzi wa Chuo Cha maendeleo ya  Wananchi Felister Nanguka akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo ambapo ameishukuru Serikali kupitia Wizara kwa kushirikiana KTO katika kuleta maendeleo kwa jamii, leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

SHANGWE ZATAWALA ZANZIBAR MSHINDI WA TIGO CHEMSHA BONGO APOKEA GARI YAKE RASMI NYUMBANI KWAKE

$
0
0


Tunashukuru jinsi kampuni ya mawasiliano ya TIGO inavyoleta hamasa kwa vijana kupitia miradi mbalimbali ya kuwainua. Leo tunakabidhi gari kwa mshindi wa TIGO Chemsha Bongo toka Zanzibar Bw. Shaban Hamis” Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan
#MshindiTigoChemshaBongo





Msheheshaji akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Bwana Hassan Khatib Hassan katika halfa ya kumkabidhi zawadi ya gari mshindi wa TIGO Chemsha Bongo #MshindiTigoChemshaBongo


“Tunampongeza mshindi wa Tigo Chemsha Bongo Bw. Shaban Hamis aliejishindia gari aina Renault Kwid kutoka Tigo kampuni ambayo tunashirikiana nayo kwenye mambo mengi ya kimaendeleo”Aljazeera - Mwakilishi wa Jimbo Raha Leo #MshindiTigoChemshaBongo


PICHA ADIMU ya mshindi wa TIGO Chemsha Bongo Bw. Shaban Khamis akiwa na “mke mdogo” katika gari yake mpya aina ya Renault KWID yenye thamani ya Tsh 23,000,000 (Zero Km)‬#MshindiTigoChemshaBongo
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan akikabidhi nyaraka za usajili wa gari aina ya Renault KWID yenye 0 Km (yenye thamani ya 23,000,000) kwa mshindi wa TIGO Chemsha Bongo Bw. Shaban Khamis akiwa na “mke mdogo” wake.
#MshindiTigoChemshaBongo


NJOO KWEREKWE USHUHUDIE sasa hivi gari la mshindi wa TIGO Chemsha Bongo akiwepo na Mshindi mwenyewe Bw. Shaban Khamis #MshindiTigoChemshaBongo

GARI IMEFIKA salama nyumbani kwa Bw. Shabani Khamis wakapata na picha ya ukumbusho na familia. Tukumbuke hii ni Renault Kwid yenye thamani ya Tsh 23,000,000 (Zero Km)#MshindiTigoChemshaBongo

MAAZIMIO YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MWANZA

$
0
0



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza. Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.

Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.
Wanachama hao ni;-
  1. Ndg. Januari Makamba (Mb)
  2. Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,
  3. Ndg. William Ngeleja (Mb)
Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.
Wakati uo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-
  1. Abdulrahman Kinana
  2. Mzee Yusuf Makamba na,
  3. Benard Membe
Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.
Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-
  1. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
  1. Ndg. Batilda Salha Buriani
  2. Ndg. Zelothe Stephen Zelothe
  3. Ndg. Bakari Rahibu Msangi
  1. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa
  1. Mafanikio Paulo Kinemelo
  2. Hilary Adelitius Kipingi
  3. Lucas Felix Lwimbo
  1. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara
  1. Petro Mwendo Mwendo
  2. Mustafa Nguyahamba Mohamed
  3. Selemani Manufred Sankwa
  1. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma
  1. Ndg. Damas Mukassa Kasheegu
  2. Baraka Andrea Mkunda
  3. Christopher Thomas Mullemwah
  1. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani
  1. Mary Daniel Joseph
  2. Fredrick Gasper Makachila
  3. Samaha Seif Said
Licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.

Nawashukuru sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WAZIRI WA AFYA AIOMBA NMB KUENDELEA KUCHANGIA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitanda vya wodi ya watoto wanaohitaji uangalizi maalumu (PICU) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, vitanda hivyo vimetolewa na Benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MNH Bi. Zuhura Mawona akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Benki ya NMB Bw. Juma Kamoli akikabidhi rasmi vitanda hivyo kwa Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari na Wauguzi wa wodi ya watoto wenye kuhitaji uangalizi maalumu (PICU),pamoja na wawakilishi wa Benki ya NMB.
………………..
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ameziomba sekta binafsi ikiwamo benki ya NMB kuelendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa vitanda vitano kutoka Benki ya NMB vyenye thamani ya shilingi milioni 35 kwa ajili ya wodi ya watoto wanaohitaji huduma ya uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na vitanda 10 pamoja na magodoro 10 kwa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vyenye thamani ya shilingi milioni 10. 
Amesema sekta ya binafsi ina wajibu mkubwa katika kuchangia shughuli za maendeleo ikiwamo huduma za afya kama ilivyofanya Benki ya NMB.
“Nawapongeza NMB kwa jitihada zake kwani msaada vitanda vya ICU ni msaada mkubwa kwa watoto na pia NMB inafanya vizuri kurejesha fedha zake kwa jamii,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Pia, Waziri Ummy amesema kutokana na juhudi za Serikali ya awamu ya tano, Muhimbili inaendelea kutoa huduma za ubingwa wa juu ikiwamo huduma ya kupandikiza figo, huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia.
Naye mwakilishi wa Benki ya NMB, Bw. Juma Kimori ameipongeza Muhimbili na serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha huduma za afya.
Bw. Kimori amesema NMB imeweka utaratibu kutoa misaada katika sekta ya afya kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH, Bi. Zuhura Mawona ameishukuru NMB kwa msaada huo kwa kuwa umekuja wakati ambapo MNH kwa kushirikiana na wahisani imejenga wodi za uangalizi maalumu kwa watoto wenye umri kati ya siku 1 hadi siku 28 (NICU) na wenye umri wa siku 29 hadi miaka 14 (PICU), hivyo kuwa na uhitaji wa vitendea kazi mbalimbali ikiwemo vitanda.
 “Vitanda hivi vya kisasa vinatumia umeme na vinaweza kurekebishika kwa kupandishwa juu na kushushwa  kulingana na uhitaji, hivyo vinasaidia mgonjwa kulazwa katika mlalo unaofaa na pia kupunguza maumivu ya mgongo kwa wauguzi na madaktari wakati wa kutoa huduma,”amesema Bi. Zuhura.
Bi zuhura amesema kuwa vitanda hivyo pia vimesaidia wauguzi kutoa huduma kwa urahisi na ufanisi zaidi ikiwamo kumwezesha mgonjwa kupumua (Intubation) kwa urahisi.
Pia. Bi. Zuhura ameshukuru NMB kwa kutoa msaada huu na pia ameiomba kuongeza vitanda vingine kwani mahitaji ya vitanda ni makubwa kwa watoto wanaohitaji uangalizi maalumu.

MINADA 6 YA KOROSHO MSIMU WA MWAKA 2019/2020 YAINGIZA BILIONI 406.3 Inbox x

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara kufuatilia hali ya malipo ya wakulima wa korosho leo tarehe 13 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara kufuatilia hali ya malipo ya wakulima wa korosho leo tarehe 13 Disemba 2019.  Wengine pichani ni  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evord Mmanda.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


Zao la korosho katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 limeingiza zaidi ya Bilioni 406.3 kupitia minada sita ambayo imekwishafanyika kwa nyakati tofauti.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe  13 Disemba 2019 wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara kufuatilia hali ya malipo ya wakulima wa korosho.


Waziri Hasunga amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana kabla ya minada itakayofanyika kuanzia tarehe 13 Disemba 2019 na kuendelea.


Amesema kuwa mpaka sasa tayari Tani 163,000 zimekusanywa huku Tani 151,554 zikiwa zimeuzwa kati ya korosho hizo zilizokusanywa.


Mhe Hasunga amesema kuwa muendelezo wa minada ya korosho inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini inatoa taswira chanya kwa wakulima hivyo kuwa na uhakika wa kipato chao kutokana na minada hiyo kuendelea kutoa matokeo chanya hususani kuongezeka kwa bei.


Alisema kuwa Korosho ni zao muhimu na ndilo linaongoza kwa kuiingizia nchi Pato kubwa la kigeni likifuatiwa na zao la Tumbaku.


“Bado hatujamaliza kukusanya korosho, hatujamaliza kuuza korosho na shunguli zingine za serikali kusimamia zao la kilimo ikiwa inaendelea lakini mpaka sasa tumeshakusanya zaidi ya Bilioni 406 hivyo hayo ni maendeleo mazuri kabisa” Alikaririwa Mhe Hasunga


Ili kuboresha zaidi sekta ya kilimo hususani zao la Korosho Waziri huyo wa Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa serikali imekusudia kusimamia vyema vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na kuboresha sheria yake ili kuboresha weledi wa kiutendaji kwa wananchi.


“Tumeamua kuchukua hatua za dhati kabisa kama serikali za kuhakikisha Ushirika unasimamiwa ipasavyo, Ushirika unaonekana kuimarika zaidi Ruvuma, Lindi na Mtwara kuliko maendeo ya Pamba na Kahawa. Hivyo tuna kila sababu ya kutatua changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuboresha ushirika kote nchini” Alisema Mhe Hasunga


Amesema kuwa Vyama vingi vya ushirika havina uwezo wa kuweka kumbukumbu sahihi za makusanyo, madai ya wananchi na mauzo ya korosho, baadhi ya viongozi kutokuwa waaminifu na kuwa wabadhilifu wa mali za wananchi.


Waziri Hasunga amesema kuwa tayari wizara ya kilimo imeanza kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao wamepokonya mali za wananchi.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga leo tarehe 13 Disemba 2019 ameanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara akiwa ametokea mkoani Lindi na Pwani ambapo pamoja na mambo mengine atakagua hali ya uuzaji wa korosho msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na kukagua skimu za umwagiliaji.



WAZIRI UMMY AITAKA BODI MPYA YA WADHAMINI KUSIMAMIA VYEMA TAASISI YA MOI

$
0
0
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa bodi wadhamini wa Taasisi ya MOI Prof. Charles Mkony sheria pamoja mpango mkakati wa Taasisi hiyo kwa ajili utekelezaji.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini wa Taasisi ya MOI mapema leo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya MOI Dkt. Respicious Boniface akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini iliyozinduliwa rasmi mapema leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya MOI Prof. Charles Mkony akiongea jambo wakati wa uzinduzi wa bodi ya mpya ya wadhamini ya Taasisi hiyo ambayo imezinduliwa rasmi leo na Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Bodi mpya ya wadhamini wa Taasisi ya MOI aliyoizindua mapema leo.
……………………Na WAJMW-DSM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu Leo amezindua bodi mpya ya wadhamini  ya taasisi ya mifupa (MOI ) na kuitaka bodi hiyo kusimamia vizuri utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Taasisi hiyo ili kuiwezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa viwango vya juu.

Waziri Ummy amesema mchakato wa upatikanaji wa wajumbe wa bodi mpya ya MOI ulikua mgumu kwani majina yalikua mengi lakini  lengo ikiwa ni kupata wajumbe makini watakaoisimamia vyema Taasisi hiyo.

“Ndugu Mwenyekiti, Prof. Mkony pamoja na wajumbe, ni ukweli kwamba wajumbe wa bodi hii wamechelewa kupatikana kutokana na mchujo uliokua unafanyika miongoni mwa majina yaliyokua yamependekezwa, nitumie fursa hii kuwapongeza mliokidhi vigezo na ni matarajio yangu mtaisimamia vyema Taasisi hii ambayo ni tegemeo kubwa hapa nchini”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya MOI jambo ambalo limepelekea huduma za afya kuimarika na kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

“Uboreshwaji wa miundombinu umepelekea kuongezekaa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji hapa MOI, mwaka 2015 idadi ya wagonjwa waliokua wanafanyiwa upasuaji hapa MOI kwa mwezi ilikua kati ya 400 mpaka 500 lakini sasa hivi imeongezeka na kufikia 700 mpaka 900 kwa mwezi.” Waziri Ummy.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali  ya awamu ya Tano katika Taasisi ya MOI, huduma nyingi mpya zimeanzishwa na katika kipindi cha miaka 4 Taasisi imewafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 43,200.

“Mh. Waziri katika kipindi cha Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya Tano, kupitia usimamizi wa Wizara yako tumeweza kuanzisha huduma za upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu, upasuaji wa kunyoosha vibiongo kwa watoto, upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo, upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia puani, upasuaji wa mgongo kwa kufungua eneo dogo, hii ni hatua kubwa sana kwetu.” Amesema Dkt. Boniface.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti mpya wa Bodi mpya ya Wadhamini MOI Prof. Charles Mkony ameshukuru kwa kupewa dhamana ya kusimamia Taasisi hiyo muhimu  na kuahidi kendelea kuisimamia MOI ili iendelee kutoa huduma bora na za viwango vya juu kwa wananchi.

SERIKALI KUANZISHA VITUO VYA MALEZI YA WATOTO NCHI NZIMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw. Maggid Mjengwa akieleza jinsi Shirika lake linavyoshirikiana na Serikali katika kuhakikisha elimu ya mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi wakati wa hitimisho la mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vyuo na wakufunzi mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa wakufunzi hao jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa cheti cha kuhitimu kwa Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Masasi Bi. Felister Nanguka mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa mkufunzi kutoka Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kwa wakufunzi hao jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakuu wa vyuo na wakufunzi kutoka vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi wakifuatilia mafunzo ya malezi, maendeleo na makuzi wakati wa Siku ya Mwisho ya Mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na wakuu wa vyuo na wakufunzi kutoka Vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi wakati akihitimisha mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa wakufunzi hao jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Serikali imeanza mpango wa kuwa na vituo vya malezi kwa watoto nchini nzima ili kuhakikisha wanajamii wanayapa kipaumbele malezi na makuzi kwa watoto ili kuhakikisha kunakuwa na taifa madhubuti.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha Semina ya Mafunzo ya Elimu ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa wakufunzi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Dkt. Jingu amesema kuwa vituo hivyo vitaratibiwa na Serikali ila vitaendeshwa na kusimamiwa na wananchi katika maeneo yao na mpaka sasa kuna zaidi ya vituo 1500 nchi nzima na vingine vinaendelea kuanzishwa.

Ameongeza kuwa malezi ni msingi mkubwa katika kuhakikisha tunapata kizazi chenye maadili, uwajibikaji na uzalendo katika kizazi itakayosaidia kujenga taifa bora. “Mafunzo haya ni muhimu na mmeamua suala sahihi, watoto wanahitaji malezi ya karibu na sio malezi tu bali wapate malezi sahihi” alisema Dkt. Jingu

Dkt. Jingu pia amewataka washiriki wanatumia stadi hiyo kuisaidia jamii na nchi kuweza kuwa na muelekeo mzuri kwa kuwa na vijana wazalendo wawajibikaji kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Noel Mbonde amesema kuwa Wizara ya Elimu itahakikisha inashirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha Elimu ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa watoto inatekelezwa.

Ameongeza kuwa Wizara ya Elimu imehakikisha kila Chuo cha Maendeleo ya wananchi kinakuwa na kituo cha kulea watoto ili kuhakikisha inawasaidia watoto.

Naye Mwakilishi wa washiriki ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mbinga Bw. Lotty Mwang’onda amesema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuleta mabadiliko hasa katika jamii inayowazunguka katika vyuo vyao ili kuhakikisha malezi, maendeleo na makuzi yanazingatiwa katika ukuaji wa mtoto.

Ameongeza kuwa wao kama washiriki wameshukuru kwa uzoefu na kama wataalam wa wanaofanya kazi na jamii watashirikiana na jamii kuhakikisha elimu walioyoipata inawafikia jamii inayowazunguka.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Karibu Tanzania KTO Bw. Aidan Mchawa ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa ushirikiano wao na asasi za kiraia katika kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi na kuhakikisha program ya Malezi, maendeleo na makuzi ya awali ya mtoto inarudisha misingi ya malezi ya mtoto hasa wa kitanzania.

Naye mshiriki Bi. Felister Nanguka ameishukuru Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa elimu ya mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi katika jamii hasa vijijini na kuahidi kufanya kazi hiyo kwa nguvu zao kwa kukaza msuli ili kuhakikisha watoto wanapata malezi stahili.

Shirika la Karibu Tanzania KOT limeandaa mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu malezi, maendeleo na makuzi ya awali ili wakaitoe elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka.

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA CARBON TANZANIA

$
0
0
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Carbobn Tanzania Bw. Mark Barker aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dodoma ambapo wamejadili namna ya kusaidia wananchi kuwa na matumizi bora ya ardhi kupitia mradi wa REDD unaotekelezwa na taasisi hiyo katika wilaya ya Mbulu, Tanganyika na Kiteto. Katika mazungumzo hayo pia Simbachawene aliiomba taasisi hiyo kupeleleka miradi hiyo katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma ili wananchi wa maeneo hayo wapate elimu hiyo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Carbobn Tanzania Bw. Mark Barker mara baada ya kufanya nae mazungumzo ofisini kwa waziri.

UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA KUWAACHILIA HURU WAFUNGWA WANUFAIKA WA MSAMAHA WA RAIS WAKAMILIKA NCHI NZIMA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na Utekelezaji wa zoezi la Msamaha wa Rais.

Na ASP. Lucas Mboje, Dar es Salaam
JUMLA ya Wafungwa 5,533 katika magereza mbalimbali nchini walionufaika na msamaha wa Rais wakati wa  maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wameachiliwa huru magerezani.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike amesema kuwa utekelezaji wa zoezi la kuwaachiliwa huru wafungwa wote walionufaika na msamaha wa Rais umekamilika nchi nzima.

“Ni matarajio yangu kuwa wafungwa walioachiliwa wamejutia makosa yao na wataacha kutenda uhalifu hivyo kujihusisha na shughuli halali kwa maendeleo yao, familia zao, jamii na taifa kwa ujumla”, amesisitiza Jenerali Kasike.

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike ameelezea manufaa mbalimbali ya msamaha huo; mosi kupungua kwa msongamano magerezani, pili, wanufaika wa msamaha kujumuika na familia zao, tatu, kichocheo cha urekebishaji magerezani kwani msamaha huo utasaidia kuimarika kwa nidhamu na kurejesha matumaini kwa wanaobakia magerezani pamoja na wanufaika wa wamsamaha huo kupata fursa ya kujishughulisha na shughuli za maendeleo uraiani.

“Zipo changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa zoezi hili ambapo baadhi ya wafungwa walionesha kuwa hawako tayari kuungana na jamii zao pamoja na waliosamehewa kurejea kutenda makosa mara baada ya kuachiwa huru. Hata hivyo nitoe wito kwa jamii nchini kuwapokea wafungwa hao na kuacha kuwanyanyapaa”, amesema Jenerali Kasike. 

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amemshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha huo ambao ni wa kihistoria hapa nchini. Pia amewapongeza wanahabari wote nchini kwa namna walivyoshiriki kutoa habari za zoezi la msamaha huo katika ngazi ya Mkoa na wilaya.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 45(1) (d) imempa mamlaka Rais kutoa msamaha kwa wafungwa waliopo magerezani. Kwa kutumia Ibara hiyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru ambapo kilele chake kilifanyika Mkoani Mwanza Desemba 9, 2019.

KASI YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU KATIKA BANDARI ZA ZIWA VICTORIA YAMKOSHA WAZIRI ISSACK KAMWELWE

$
0
0
*Asema chini ya Rais Magufuli mambo yanakwenda vuziri
*Awatumia salamu wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kagera

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele amesema amekuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundombinu katika bandari ya Kemondo na bandari ya Bukoba huku akitumia nafasi hiyo kuelezea mikakati inayochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha sekta ya usafiri nchini.

Katika bandari za Kanda ya Ziwa, Waziri Kamwelwe amesema kupitia maelekezo yaliyotolewa na Rais Dk.John Magufuli baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani kuhusu uboreshwaji wa bandari za maziwa makuu kumekuwa na jitihada zinazoendelea.

Huku akieleza kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ule usafiri wa meli ambao ni wa raha mustarehe utarejea kutokana na ujenzi wa meli mpya unaoendelea pamoja na kufanyiwa matengenezo kwa meli za zamani ikiwemo MV.Bukoba. 

Akizungumza na waandishi wa habari walioko kwenye ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) katika bandari za Ziwa Victoria, Waziri Kamwelwe amesema ziara yake inalenga kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Serikali.

Kuhusu bandari ya Bukoba amesema ilianza kujengwa mwaka 1943 na kukamilika mwaka 1945 na wakati huo ilianza kutumia kwa vyombo mbalimbali vya majini lakini baadaye nchi ikawa na meli kama Mv Bukoba, Mv Victoria, Mv Butiama.

"Mv Victoria kwa bahati mbaya ilizama lakini pia tulikuwa na meli nyingine Mv Clarias ambayo nayo iliharibika.Baada ya kuanza Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli ambaye amekuwa na dhamira thabiti ya kusubutu na ametoa maelekezo, ndio mnaona haya maendeleo sasa bandari hii inakarabatiwa ili iwe mpya.

"Kinachofanyika ni pamoja na kukarabati magati kwa ajili ya meli ili ziweze kufika sehemu na kuegesha, pia maghala kwa ajili ya mizigo, chumba cha abiria ambao wanasubiri kusafiri, ofisi za wafanyakazi wa TPA, Kampuni ya Meli Tanzania pamoja na TASAC ambaye ni dhibiti ili sasa Bandari hii ianze kufanyakazi rasmi,"amesema Waziri Kamwelwe.

Amesema kuwa wanashukuru katika ukarabati unaoendelea tayari wamekarabati meli ya Mv Umoja ambayo yenyewe inaingia behewa 19 na tayari meli hiyo imeanza kufanya kazi. Amefafanua kuwa meli hiyo ya Umoja inabeba behewa ya shehena ya mizigo na kuipeleka pia nchini Uganda katika Bandari ya Port Bell Uganda lakini ikiwa huko inachukua mizigo ikiwemo ya kahawa na mabati inaleta nchini Tanzania.

"Kwa sasa tumekarabati bandari hii na sasa hivi pia tunakarabati Bandari ya Kemondo sasa, juhudi ambazo zimefanywa na Rais wetu Dk. John Magufuli, anakarabati meli ya Mv Victoria, Mv Butiama na ukarabati unavyoendelea unakwenda kwa kasi kubwa.Zile meli zinabadilika zinakuwa mpya kwa sababu vifaa vyote vinavyofungwa ikiwamo injini, majenereta vyote mpaka viti ni vipya,"amesema.

Kuhusu matarajio yake, na Serikali kwa ujumla, amesema kuanzia Machi mwaka 2020 ukarabati wa meli mbili utakuwa umekamilika na hivyo kuanzia Aprili mwakani MV.Victoria itaanza kubeba abiria kutoka Mwanza na kuzunguka kwenye magati mengine kama Nyamirembe na kwenda Musoma kuja Kemondo pamoja na Bukoba. Amesisitiza kazi ya maboresho inaendelea vizuri, hivyo wana Bukoba ule usafiri wao wa raha uliosimama kwa muda mrefu karibu utaanza tena.

"Kama ambavyo tumerudisha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam, treni kutoka Tanga ambayo sasa inakwenda Kilimanjaro inaendelea na safari kwa kubeba saruji na sasa wanabeba abiria. Kwa kipindi hiki cha kueleka mwaka mpya na Krismasi hawalanguliwi tena pale Ubungo kwani treni ipo na ipeleka abiria Moshi.

"Hivyo tukifika Aprili mwakani tutakuwa tunatembeza meli za Mv Victoria ili sasa kurudisha na kurahisisha usafiri ndani ya maji usafiri ambao ni wa raha na pia nauli yake ni nafuu zaidi. Nipongeze TPA, wananchi na sekta binafsi walioamua kutoa huduma za boti za kubeba mizigo na abiria.Ndio maana TPA wamejenga gati dogo hapa Bukoba pamoja na jengo dogo la mizigo,"amesema.

Akielezea maboresho yanayofanyika bandari ya Bukoba,Waziri Kamwelwe amesema kuwa mwaka 1945 Bukoba haikuwa na nyumba nyingi lakini leo hii zipo nyingi na watu ni wengi, hivyo shughuli za uchumi zimeongezeka."Ndio maana Serikali ya CCM iliyochaguliwa na wananchi inaendelea kutekeleza yote ambayo iliahidi."

Akizungumzia bandari ambazo zina usafiri wa reli wa ajili ya kubeba mabehewa ya mizigo, Waziri Kamwelwe amesema tayari TPA wameshaagiza injini sita za treni ambazo zitakuwa katika Bandari ya Kemondo, Musoma kwa ajili ya kumvuta behewa za mizigo.

"Baada ya Rais kumuagiza Waziri Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kuzuia uvuvi haramu hivi sasa tunazalisha samaki wengi na wakubwa ikiwamo minofu ya samaki tani za kutosha, ndio maana tuko kwenye hatua za mwisho ili Air Cargo ije Mwanza ibebe minofu ya samaki na kupelekwa moja kwa moja Ulaya pamoja na maeneo mengine yote ambayo wanaohitaji kula samaki.Watanzania nao watakula samaki si kwamba tutasafirisha wote,"amesema.

Hata hivyo amesema kazi inaendelea vizuri ambapo ametumia nafasi hiyo kuipongeza TPA kwa kusimamia vema shughuli zote hizo na kazi ambayo imebaki itakuwa kutoa huduma tu kwa wananchi.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwelwe akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 13 akiwa katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera ambako amefanya ziara ya kukagua uboreshaji wa miundombinu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele akifafanua jambo akiwa katika bandari ya Bukoba mkoani Kagera.
 :Waziri Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano akiwa katika gati ya Bandari ya Kemondo Bay iliyopo mkoani Kagera ambapo amefika kuangalia kasi ya uboreshaji wa gari hiyo ya reli ambayo ni maalum kubeba mahewa ya mizigo.
 Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza akizungumza mbele ya Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwelwe (aliyekaa kushoto)kuhusu hatua mbalimbali za uboreshaji wa miundombinu katika bandari ya Bukoba na Bandari ya Kemondo baada ya Waziri huyo kufanya ziara jana na leo.
 Mwakilishi wa Kiwanda cha Simba Cement (pembeni ya Waziri kushoto) akizungumza kuhusu umuhimu wa bandari ya Kemondo na Bandari ya Bukoba katika usafirishaji wa saraji kwa mkoa wa Kagera.
 Mfanyabiashara mkubwa mkoani Kagera akizungumza na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Issack Kamwelwe(hayupo pichani) kuhusu huduma za usafirishaji wa mizigo katika bandari ya Bukoba na ile ya Kemondo.
 Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza(kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwelwe.
 Gari ya kubeba mizigo ikiwa katika bandari ya Bukoba ikiwa imeegeshwa baada ya mizigo kupakiwa katika meli ya mizigo katika eneo hilo.
 
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images