Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

Huawei Technologies Tanzania donated ICT Laboratory to DIT

0
0
Huawei Technologies Tanzania has donated ICT Laboratory to DIT as part of Corporate Social Responsibility and ICT Talents cultivation program. The Huawei ICT Laboratory will have advanced equipment and good environment for students to practice in real time. Together with Huawei Tanzania’s Chief Executive Officer Mr Frank Zhou, Hon Elias Kwandikwa Deputy Minister, Ministry of Works, Transport and Communication who represented Hon. Kassim Majaliwa Majaliwa (MP), Prime Minister of Tanzania, opened the Huawei ICT Laboratory at the DIT Campuses.
The year 2015 culminated the existing cooperation between Dar Es Salaam Institute of Technology and Huawei Technology Tanzania. The two were shared a mutual bond centering of Information Communication Technology and together they set out building an ecosystem for improving the ICT Industry in Tanzania.

HUAWEI understands the sheer importance of having to train and research constantly in order to develop better talents and better solutions. This is the reasoning behind donating the first Huawei ICT Laboratory in DIT complete with equipment that will spark the innovative minds of the youth in Tanzania. This will allow students to have first-hand access to practical usage of what they learn about.

HUAWEI has undoubtedly used its resources for a noble cause by partnering and supporting Tanzanian Universities, Colleges and Institutions with various programs and aids which helps in knowledge transfer and ICT skills advancement for the students as well as the teachers. Flagship international programs like the well know ICT competition and Seeds for the future have been soaring in Tanzania pioneered by Huawei.

These efforts help shape the Tanzanian youth talents in today’s ICT Industry not only in Africa but then again in the global stage. We’ve seen this evidently when Tanzania won the 1st prize in the 2018/2019 ICT competition when competing with fellow university students from the sub Saharan region.

These efforts have certainly shown an elaborate attempt by HUAWEI to boost ICT awareness as part of the development of Tanzania. ICT is considered a vital part in any growing economy and it is through technological adoption and innovation that developing countries can take the next step forward.

Tanzania is moving at great speeds and HUAWEI wants to make sure ICT is not left behind when the race to 2025 middle income economy takes off!

Waziri Mwakyembe: Maafisa Michezo lindeni viwanja vya Michezo nchini

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati akifungua kikao kazi cha maafisa hao cha siku mbili (tarehe 12-13, Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akitoa maelezo mafupi kuhusu Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitambulisha washiriki wa Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho cha siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara cha siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Michezo mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara cha siku mbili (tarehe 12-13 Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”

(Picha na Shamimu Nyaki, WHUSM, Dodoma)

……………..

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Michezo kote nchini kulinda viwanja vya michezo na kutoa taarifa ya viwanja vya michezo vinavyobadilishwa matumizi hata kwa siri.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo kinachofanyiki kwa siku mbili chenye lengo la kutathimini, kujadili na kuelekezana namna bora ya kuimarisha michezo na kutumia sekta hiyo kutangaza vivutio vya utalii nchini.

“Wapo baadhi ya Wakuu wa shule na walimu wanaozuia michezo shuleni na mnawajua, mnakaa kimya sasa wajibu wenu ni nini? Tambueni michezo sasa ni ajira ambayo ni mgodi na taifa lina vijana wengi simamieni vyema michezo,” Dkt. Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa kikao kazi hicho Dkt. Mwakyembe amekiagiza Chuo cha Michezo cha Malya kufanya utafiti wa kodi inayotokana na michezo mbalimbali inayofanyika nchini.

Naye Kaimu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo kukakikisha kikao kazi hicho kinakuwa endelevu na kufanyika kila mwaka. Aidha, aandae utaratibu wa kuwa na vikao hivyo kikanda vikiwa na lengo la kuwaandaa vijana waweze kushiriki michezo mbalimbali kitaifa na kimataifa.

“Kikao Kazi hiki kitatoa tathimini ya wapi tulipo, nini kifanyike pamoja na kutoa mwongozo wa kusimamia michezo mbalimbali na kutoa maelekezo kwa kuweka maazimio yatakayosaidia kupeleka michezo kuwanufaisha vijana maana michezo ni ajira,” alisema Dkt. Possi.

Aidha, Dkt. Possi aliwataka maafisa michezo hao kuzingatia mada ya uandishi wa maandiko ya udhamini katika michezo ambayo ni kichocheo cha kufanikisha michezo nchini kwani maandiko mradi hufanyika ni miongoni mwa kazi inayofanyika kila siku katika sekta ya michezo, hivyo ni vyema kuwa na ujuzi huo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo alitoa pongezi na shukrani kwa Makatibu Tawala Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kwa kuwawezesha maafisa michezo hao kushiriki kikao hicho kwa mikoa yote nchini imeshiriki. Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho Afisa Michezo kutoka Wilaya ya Mbarali Bw. Gerald Chiwaya aliishukuru wizara kwa kuandaa kikao hicho ambacho kimefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambacho kina washiriki 265 kutoka mikoa yote Tanzania Bara.

BODI AMBAZO HAZITAWASILISHA GAWIO IFIKAPO JANUARI 23 ZITAKUWA ZIMEVUNJWA

0
0


 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipokea hundi ya kiasi cha Sh. Milioni 200, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Bw. Patrick Ngwediagi, katikati ni Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, wakati wa halfa ya kupokea gawio jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea gawio la kiasi cha sh. Bilioni 12.12, kutoka kwa Taasisi 58 zilizotoa gawio kwa Serikali baada ya agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, alilolitoa  Novemba 24, Ikulu jijini Dodoma.
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, akitoa taarifa ya kiasi cha fedha ambazo zimepokelewa kutoka kwa Taasisi za Serikali ikiwa ni kuitikia agizo lililotolewa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Taasisi ambazo hazikuwasilisha gawio la Serikali Chamwino Ikulu jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiteta jambo na Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbutuka,  wakati wa halfa ya kupokea gawio la kiasi cha Sh. Bilioni 12.12 kutoka kwa Taasisi 58 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, akisoma orodha ya Taasisi za Serikali ambazo zimetoa  gawio la Serikali kwa  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), jijini Dodoma
Sehemu ya Wawakilishi wa Taasisi waliofika kwa ajili ya kutoa gawio la Serikali wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kupokea gawio jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti mbalimbali na Watendaji Wakuu kutoka Taasisi za Serikali baada ya halfa ya kukabidhi gawio la kiasi cha Sh. Bilioni 12.12 kutoka kwa Taasisi 58 jijini Dodoma. kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,  kulia ni Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbutuka
(Picha na Josephine Majura – WFM Dodoma).
………………
Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodaoma
Serikali imesema  Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma ambazo hazitawasilisha gawio na michango yao kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali  ifikapo Januari 23 mwaka 2020, kabla ya saa 6 usiku, Bodi zitakuwa zimevunjwa na watendaji wake kupoteza ajira zao.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati akipokea gawio na michango kutoka Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 11, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa Novemba 24 mwaka huu lililozitaka taasisi hizo kutoa gawio ndani ya siku 60.

Alisema itakapofika saa sita usiku ya tarehe 23 Januari, 2020 kama hawajaleta gawio wala michango ya kuingia kwenye mfuko Mkuu, Bodi hizo zimevunjwa, Watendaji Wakuu wa hizo taasisi husika nao watahusika na akabainisha kuwa hiyo ndiyo amri ya Serikali.

 “Tukio la Novemba 24, 2019 la kupokea gawio, mashirika yalikuwa 79 na Mhe. Rais, alipokea hundi ya jumla ya Sh. trillion 1.05 na aliniagiza ndani ya siku 60, Taasisi, maashirika na kampuni 187 ambazo hazikutoa gawio siku hiyo zitekeleze maagizo yake”, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa baada ya agizo la Rais, katika kipindi cha siku 18, Taasisi, Kampuni na Mashirika 58 yametekeleza agizo ambapo jumla ya fedha zilizopokelewa katika mfuko Mkuu wa Hazina ni Sh. bilioni 12.12.

Dkt. Mpango aliyapongeza mashirika, kampuni na taasisi hizo kwa kuitikia wito huo kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia katika shughuli za maendeleo  ya nchi kwa njia ya ujenzi wa miradi na kuiwezesha nchi kujitegemea.

Alisema kuwa amefurahishwa na gawio na michango lakini amesema wanatakiwa kuongeza kiwango hicho mwakani kwa kuwa Watanzania wanatakiwa kuona kuwa waliopewa  dhamana  ya kusimamia mashirika yao wanatimiza wajibu wao.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbutuka, amesema idadi ndogo ya kampuni, mashirika na taasisi ya umma 71 kati ya 266 yaliyo katika orodha ya Msajili wa Hazina yaliyochangia gawio na michango mingine wakati Mhe. Rais Magufuli akipokea magawio hayo kwa niaba ya  wananchi, haikumfurahisha Kiongozi huyo wa Nchi.

Miongoni mwa Taasisi zilizotoa mchango ni pamoja na Chuo cha kilimo- SUA, Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini- IRDB, Taasisi ya Taifa ya  Usafirishaji – NIT, Mfuko wa Misitu Tanzania- TFF, Chuo cha Ufundi Stadi- VETA, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Kudhibiti ubora wa Mbegu Tanzania.

TRC YALETA MAGEUZI MAKUBWA MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI

0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu Mafanikio ya Shirika hilo kwenye miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam leo Disemba 12, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akifafanua jambo katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mafanikio ya Shirika hilo kwenye miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam leo Disemba 12, 2019.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
………………

Eric Msuya,MAELEZO

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanya mageuzi makubwa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

Kadogosa alisema kuwa pamoja na mageuzi yanayoendelea katika sekta mbalimbali hapa nchini, Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kufufua miundombinu ya reli katika maeneo mbalimbali ikiwemo njia ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam hadi Kilimanjaro ambayo kwa sasa inasafiri mara tano kwa wiki.

“Kutokana na maombi ya wananchi wengi tumeamua kwamba kuanzia Desemba 16 mwaka huu safari ya treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Kilimanjaro itakuwa ni mara tano kwa wiki” alisema Kadogosa.

Kadogosa alieleza kuwa TRC imefanikiwa kuongeza idadi ya mizigo ambapo zaidi ya tani 1,456,537 zimeweza kusafirishwa katika reli ya kati (Dar es Salaam, Mwanza na Kigoma) na kwa upande wa abiria treni za mikoani wameongezeka kutoka 411,172 mwaka 2014/15 hadi 578,439 mwaka 2018/19.

Sambamba na hilo, TRC imeweza kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 17.4 mwaka 2014/15 hadi bilioni 30 mwaka 2018/19 kwa treni za mizigo, kutoka bilioni 8.3 hadi bilioni 10.7 kwa treni za abiria wa mikoani na kutoka milioni 316.6 hadi bilioni 1.96 kwa treni za mjini.

Aidha TRC inajivunia mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali katika sekta ya reli kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) wenye gharama ya shilingi trilioni 7.5

“Mradi wa SGR katika mindombinu ya reli hapa nchini ni mradi mkubwa sana ambao utamwezesha mfanyabiashara au abiria wa kawaida kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi mwanza kwa saa 9 na treni hii itakuwa na uwezo wa kutembea umbali wa kilomita 160 kwa saa hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi hapa Tanzania” alieleza Kadogosa.

Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa (SGR) yenye mtandao usiopungua kilometa 2,561 umefikia asilimia 70 ambapo reli hiyo itaunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na Katavi pamoja na nchi zisizokuwa na bandari (Rwanda, Burundi na DRC Congo).

Pia Kadogosa aliongeza kuwa TRC inatekeleza mradi wa uboreshaji wa reli ya kati- TIRP wenye lengo la kuongeza ubora na uimara wa njia ya reli kutoka Dar hadi Isaka ili kuweza kubeba mizigo kufikia tani 18.5  na mwendokasi wa kilometa 70 kwa saa.
Mradi huo wa TIRP umezalisha ajira kwa vijana wa kitanzania zaidi ya 1,600 pamoja na kuwanufaisha wafanyabiashara mbalimbali na watoa huduma.

DC CHONGOLO AZINDUA MAONESHO YA BIDHAA ZA NGOZI VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS, AWEKA MKAKATI WA SOKO LA UHAKIKA

0
0





Mjasiriamali akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo wakati akikagua mabanda ya maonesho ya bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa katika kutatua changamoto ya kupata soko la uhakika la bidhaa za ngozi, Wilaya hiyo imejipanga kuwatafutia maeneo wazalishaji wa ndani ambapo wote watakaa sehemu moja kwa ajili ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za ngozi yanayofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers , Mhe. Chongolo amesema kuwa mkakati huo utasaidia kuinua uhakika wa soko kwa wazalishaji.

Amefafanua kuwa maonesho hayo ya bidhaa za ngozi yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Wilaya hiyo na kwamba ni lazima kila mwananchi ajenge utamaduni wa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kuwataka kuondokana na dhana ya kuona bidhaa zinazotoka nje ndio bora zaidi.

“ Ukienda kwenye nchi za wenzetu hasa zilizoendelea, wao wanathamini kwanza cha kwao, cha mwingine badae, nasisi tukifikia hatua hiyo tutafanikiwa sana, lakini tutafikaje hapo ni la zima kuanzia sasa tuamke tuanze kupenda vya kwetu” amesema Mhe. Chongolo.

Mhe. Chongolo ameongeza kuwa uwepo wa maonesho hayo utaongeza tija na mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu sambamba na kuongeza wigo mpana wa kutangaza bidhaa hizo na wananchi kupenda kuzitumia.

“ Uwepo wenu hapa utawezesha wale wananchi ambao wanakuja kununua bidhaa zenu , ndio watakuwa mawakala kwa wananchi wengine ambapo na wao watapenda kuja kununua bidhaa hizi bora na nzuri za kitanzania” ameongeza.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kawe , Mhe. Muta Rwakatare amempongeza Mhe. Chongolo kwa kubuni na kufanikisha kuwepo kwa maonesho hayo. Ameongeza kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao mkuu huyo wa Wilaya wa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, anaamini kuwa sasa ni wakati wa wajasiriamali hao kunufaika kwani changamoto zao pia zimefikia kikomo.

Ameongeza kuwa Rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele kusisitiza uchumi wa viwanda na kwamba hadi sasa tayari adhma hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele amesema kuwa wazo la kuwepo kwa maonesho hayo lilitolewa na Mhe. Chongolo wakati wa maonesho ya nanenane ambapo alihitaji kuandaliwa kwa mpango kazi wa kuwa na maonesho hayo.

Amesema kuwa kabla ya kufanyika kwa maonesho hayo, awali yalifanyika mafunzo ya siku nne ambayo yaliendana sambamba na maonesho ya bidhaa hizo kwa siku moja yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Dk. Henjewele amesema kuwa maonesho hayo ya siku nne yatafikia kilele Disemba 15 ambapo bidhaa zote za ngozi ikiwemo viatu, mikoba, mikanda na mabegi ya shule ya wanafunzi yanapatikana hapo.


Miaka Minne ya JPM Sh. Billioni 300 Zilitolewa kwa TADB Kuboresha Kilimo

0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Japhet Justine akizungumza katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu Mafanikio ya Benki hiyo  katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam leo Disemba 12, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Japhet Justine akifafanua jambo  katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mafanikio ya Benki hiyo katika  miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam leo Disemba 12, 2019.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
………………..

Na Mwandishi Wetu- MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano Chini, Rais Dkt. John Magufuli imejikita katika kuwawezesha wakulima kwani ilitoa zaidi ya Billioni 300 kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake.

Akielezea mafanikio ya Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali,  Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Japhet Justine alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli alitoa pesa hiyo, kwa ajili ya kusaidia sekta hiyo katika shughuli mbalimbali   ikiwemo kutoa mikopo kwa Wakulima.

‘’Katika kipindi cha miaka minne cha utawala wa Rais Dkt. Magufuli alituwezesha kutupa mtaji wa zaidi ya Sh. Billioni 300, ambapo mpaka Novemba mwaka huu, tumefanikiwa kutoa kiasi cha Sh. Billioni 148 kwa ajili ya mikopo kwa wakulima’’, alisema Bw. Justine

Justine alisema wakati wanaanzisha Benki hiyo mwaka 2016 Rais Magufuli aliwapa Billioni 60 kama mtaji, lakini  waliweza kuizungusha pesa hiyo kwa kutoa mikopo katika vyama mbalimbali vya wakulima ambapo walifanikiwa kurudisha Sh. Billioni 68 kwa muda mfupi.

Aidh Mkurugenzi huyo alisema, pesa hiyo ilijikita zaidi katika mpango wa pili wa  Maendeleo ya Kilimo, matumizi bora ya Ardhi na Maji, ambapo mpango huo ulifanikiwa na kutimiza malengo yaliyotarajiwa.

‘’Pesa hiyo ililenga zaidi katika mnyororo wa thamani wa mazao , ambapo Sh. Billioni 10 tulipeleka katika Mifugo, Billioni 1 ilienda ufugaji wa Samaki, Millioni 700 ilienda kwenye Kuku na Billioni 37 zilienda katika Mazao mbali mbali ya biashara’’, alisema Japhet.

Mkurugenzi huyo alisema, kutokana na mpango huo watu Millioni 1.6 wamefanikiwa kutokana na huduma zao hivyo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli Benki hiyo pamoja na wadau wake wamepata mafanikio makubwa.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema, mbali na kutoa mikopo kwa wakulima lakini wamekuwa wakiwasaidia kutafuta  masoko hivyo inawarahisishia kuwa na uhakika wa masoko ya mazao yao.

Mkurugenzi huyo alisema katika kuimarisha kilimo na kumpa mkulima nyenzo bora, Benki hiyo imekuwa ikitoa matrekta pamoja na mashine za kuvunia mpunga kwa wakulima.Aidha Mkurugenzi huyo alisema, mbali na pesa hizo, Benki hiyo ilitoa pesa nyingine kiasi  Sh. Billioni 35 mkopo kwa Viwanda 13 vya kuchakata mazao ya Kilimo.

Japhet alitaja baadhi ya viwanda vilijengwa kutokana na mkopo huo ni pamoja na kiwanda cha Alizeti kilichopo Kahama, kiwanda cha kuchakata mafuta kilichopo Manyoni na kiwanda cha kusindika Chikichi kichopo Kigoma.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema TADB baada ya miaka minne ya mafanikio, inatarajia kuweka nguvu zaidi na kuyaongezea thamani mazao ya Pamba na  Mkonge kwani yalikuwa yakiingiza pesa nyingi miaka ya nyuma hapa nchini.

‘’Kwakweli TADB tuna nia ya dhati ya kurudisha thamani ya zao  la Pamba na Mkonge, enzi za Mwalimu Nyerere, mazao haya yalikuwa yakiingiza pesa nyingi hapa nchini, lakini kadiri miaka ilivyosonga na mazao yalikuwa yakishuka’’, alisema.

Mkurugenzi huyo alisema Benki hiyo, inataka kufanya mapinduzi makubwa katika mazao hayo kwani wanatarajia kufufua viwanda vya kutengenezea nguo, kiwanda cha kutengeneza magunia.

Japhet amewataka Watanzania waache kuwaza kilimo cha zamani na badala yake wajiingize kwenye kilimo cha kisasa, kwani sekta hiyo hivi sasa ni biashara kubwa ambayo inawatoa watu wengi.

Mkurugenzi huyo alisema, licha ya kuwa benki hiyo kuwa na  mafaniko hayo katika kipindi cha miaka minne, lakini bado kuna changamoto ya masoko, hivyo wanatarajia kushirikiana na taasisi zilizo katika mnyororo wa thamani ndani ya Afrika Mashariki na  nchi zilizo kusini mwa Afrika (SADC) katika kutafuta masomo hayo.

KITABU CHA MTOTO WA MIAKA 8 “BIBLIA YANGU” CHA ZINDULIWA KWENYE FURSA YA DAR

0
0
 Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake 

MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda kulia akimkabidhi kitabu hicho Samweli mara baada ya kufanya uzinduzi
MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso kushoto akimpatia nakala ya kitabu kilichoandikiwa na Mwanae Mtangazaji wa Kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM Radio Dkt Isaac Maro wakati wa uzinduzi huo 
Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake na mdogo wake Alan Michael Gimeno 

Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) katikati akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa kitabu chake

Jumamosi tarehe 7/12/2019 ilikuwa siku ya pekee wa mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) ambae alibahatika kuzindua kitabu chake cha kwanza ndani ya fursa ya Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Center 

Kitabu cha BIBLIA YANGU kilizinduliwa na Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda 

Samwel amekuwa mtoto wa pekee kwenye familia ambae Mungu Ameweka kipaji cha kuandika na kuchora na Sisi kama wazazi wake tumeamua kumsaidia ili kuiishi ndoto yake maneno hayo yamesema na mama mzazi wa Bi Suzana Senso

Kitabu cha kwanza cha Samwel kitakwenda Kuwa kinatolewa kwa watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya samwel kurudisha kwa watoto wezake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao ni mara chache sana kupata kitabu kinzuri na chenye hadithi za kwenye Biblia kutokana na mazingira wanayoishi maneno hayo yamesemwa na baba wa Samwel Bw Michael Samwel Gimeno 

KAMPENI KALAMU YANGU
Ni maneno yatakayo kwenda kutumika kwenye kampeni samwel ambayo itakuwa nikutembelee vituo vya watoto yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuwagawia vitabu ili nao waweze kusoma sio tu kusoma kitabu tu ila pia kusoma kitabu kilichoandikwa na mtoto mwezao 

Kampuni hii inaanza mwezi huu wa 12 hadi siku ya wapendanao tarehe 14/2/2020 ambapo samwel atakwenda kula na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambacho tutakitaja siku zijazo na pia kuwagaia vitabu ya BIBLIA YANGU 

Gharama ya kitabu itakuwa shilingi elfu 20,000 kuanzia 15/2/2020 baada ya kampuni ya KARAMU YANGU ukisha tarehe 14/2/2020

Mama Samwel alisema Kwa sasa tunatamani kupata watu wa ku support kutoa nakala ya vitabu ambavyo tunatajia kuvigawa kwenye vituo vya watoto yatima Kwani hii kampeni haina mfadhili wa kufanya Ila ni wazazi tu  ndio tunaifanya na tunatamani kuwafikia watoto wengi sana 
Kwa yeyote atakae wiwa kuungana nasi kwenye Hii kampuni anaweza ku wasiliana Kupitia namba 0736 372138 

Tukiwa kama wazazi wa Samwel tunapenda kuwashukuru Joel Kiiya ambae ni mentor wa Samwel, Bi Ezabel Simuyu ambae ndie ame design kitabu, photography wake Muki, Emanuel, Mkurungezi wa Fursa na wale waliotumia muda wao kufanikisha kitabu cha “BIBLIA YANGU” hadi kutoka.


MUNGU AWABARIKI

NAIBU MKURUGENZI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NCHINI KOREA ATEMBELEA MLOGANZILA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kushoto), akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Uchumi nchini Korea, Bw. Hwang Seokchae alipotembelea hospitalini hapa.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila waliompokea Bw. Hwang Seokchae, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi. Njoikiki Mapunda, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed.
Baadhi ya Viongozi wa MNH-Mloganzila wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa mkutano mara baada ya mapokezi ya wageni waliotembelea hospitalini hapa leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama, Bw. Pius Maswaga akiwaelezea wageni waliotembelea kitengo hicho namna chumba cha kuhifadhi data (Server room) kinavyofanya kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH-Mloganzila Sr. Redemptha Matindi akiwaonyesha wageni baadhi ya wodi za wagonjwa binafsi (Private ward) zilizoko hospitalini hapa.
Wageni wakiangalia namna mashine ya CT-Scan inavyofanya kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha Radiolojia.
Prof. Museru na Bw. Seokchae katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila mara baada ya kutembelea hospitalini hapa.

……………….

Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Uchumi nchini Korea leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kufahamu huduma zinazotolewa hospitalini hapa.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amemueleza kuwa hospitali ya Mloganzila inatoa huduma za kibingwa na kibobezi na ina jumla ya vitanda 608 pamoja na wafanyakazi takribani 700.

“Hospitali yetu inatoa huduma za kibingwa na kibobezi na ina jumla ya vitanda 608 ikiwa ni hospitali ya tatu kwa ukubwa nchini na yenye wafanyakazi takribani 700 wanaofanya kazi ya kutoa huduma za afya kwa umma,” amesema Prof. Museru.

Aidha Prof. Museru amefafanua kuwa lengo la hospitali ya Mloganzila ni kufikia uwezo wa kutoa matibabu ya ubingwa wa juu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na badala yake matibabu hayo kutolewa hapa nchini.

Prof. Museru ametaja kuwa hospitali inatarajia kuanza kutoa huduma mbalimbali za kibingwa kama vile upandikizaji uloto (Bone marrow transplant) na hivyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka Korea itaisaidia hospitali kuweza kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa watanzania.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Uchumi nchini Korea, Bw. Hwang Seokchae amefurahishwa na namna hospitali ya Mloganzila inavyohakikisha jamii inayowazunguka inapata huduma bora za afya.

“Nimefurahi sana kuitembelea hospitali hii na natumaini ushirikiano huu utazidi kuwa na manufaa hasa kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kutoa Huduma za Afya la Korea (KOFIH) pamoja na Shirika la Ushirikiano wa Kimaendeleo la Korea (KOICA),” amesema Bw. Seokchae.

Mgeni huyo ametembelea Wodi ya wagonjwa binafsi (Private ward), Kitengo cha Tehama (ICT), Kitengo cha Magonjwa ya Dharura (EMD) pamoja na Radiolojia na kujionea namna wataalam wanavyofanya kazi.

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA IMEKAMILIKA Inbox x

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua risiti za mauzo ya korosho wakayi alipotembelea ghala la kuhifadhia korosho la BUKO akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa umwagiliaji wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa umwagiliaji wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ta Kilimo)
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipumzika kwenye magunia ya korosho yakliyohifadhiwa katika ghala la Mtama lilipo katika Halmashauri ya Mtama wilaya ya Lindi wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Lindi


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa siku 23 pekee kwa wakandarasi wanaojenga Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa kuwa wamekamilisha ujenzi wa mradi huo.


Waziri Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Disemba 2019 la kukamilika kwa mradi huo wakati alipotembelea na kukagua skimu hiyo yenye hekta zipatazo 300 akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi.


Amesema kuwa mradi huo unaohusisha ujenzi wa banio katika mto Lukuredi, mfereji mkuu wenye urefu upatao mita 525, mfereji wa kati wenye urefu upatao mita 2675, mifereji midogo vigawa maji pamoja na vivuko vya miguu ulipaswa kukamilika Julai 2, 2019 lakini mpaka sasa umeshindwa kukamilika kwa wakati jambo ambalo limewakosesha wakulima fursa ya kilimo cha umwagiliaji.


“Mkandarasi aliomba aongezwe muda wa miezi mitano baadaye ameongezwa tena mwezi mmoja lakini mpaka sasa ameshindwa kukamilisha nadhani ameamua kutuchezea akili hatutakubaliana na hilo hata kidogo” Alikaririwa Mhe Hasunga


Akizungumza na wananchi wa Kijiji na kata ya Namanga Mhe Hasunga amesema kuwa miradi mingi ya umwagiliaji nchini haikamiliki kwa wakati kutokana na wakandarasi kutotekeleza majukumu yao ipasavyo.


“Haiewezekani Waziri Mkuu anayechapa kazi, anahangaika nchi nzima kila kona halafu kwake ndio mradi uwe haujakamilika hivi tutakuwa na akili timamu kweli hilo halikubaliki” Alisema


Amemtaka mkandarasi kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ndani ya muda uliokubaliwa vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


Waziri Hasunga amesema kuwa serikali inajipanga na mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa hakutaanzishwa miradi mipya ya umwagiliaji mpaka pale miradi iliyoanzishwa itakapokuwa imekalmilika.


Kuna miradi mingi imeanzishwa lakini haijakamilika ilihali kiasi kikubwa cha fedha kinakuwa kimetumika.


Mradi wa umwagiliaji Nanganga ni kati ya miradi 16 ya SSIDP III (Small Scale Irrigation Development Project) awamu ya tatu iliyojengwa na serikali ya Tanzania chini ya wizara ya Kilimo na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC).


Katika ziara hiyo ya kikazi Waziri Hasunga ametembelea na kukagua skimu ya umwagiliaji Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa umwagiliaji.


Vilevile Waziri Hasunga ametembelea na kukagua ghala la kuhifadhia korosho la BUKO kadhalika ghala la kuhifadhia korosho la Mtama ambapo amepongeza utunzaji wa korosho za wakulima katika maghala hayo.


POLISI WANAWAKE SHINYANGA,CRDB WATOA ZAWADI KWA WATOTO WENYE UALBINO,WAZEE NA WANAWAKE WALIOJIFUNGUA Inbox x

0
0

Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania ‘Tanzania Police Female Network’ wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Benki ya CRDB tawi la Shinyanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha kulelea watoto wenye ualbino Buhangija Jumuishi,Kituo cha Kulelea wazee cha Kolandoto,Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha afya Kambarage.

Miongoni mwa vitu vilivyotolewa leo Desemba 12,2019 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni pamoja na mchele,unga,sukari,mafuta ya kupikia,mafuta ya kujipaka,sabuni,viberiti,miswaki,dawa za meno,viatu,taulo laini ‘pedi’,kalamu na soda.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitu hivyo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga,amesema polisi wanawake wameamua kushirikiana na Benki ya CRDB kutafuta mahitaji muhimu kwa ajili ya watoto wenye ualbino,wazee na wagonjwa ili kuonesha kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanawajali.

“Tumeguswa na maisha ya watoto wenye ualbino lakini pia wazee hawa kwani wanaonekana kama wanatengwa na jamii,mfano watoto hawa wenye ualbino baadhi yao wamebaki hapa Buhangija baada ya shule kufungwa,hivyo tumewapatia mahitaji muhimu ili kuonesha kuwa jamii ipo pamoja nao na inawapenda”,amesema Salia.

Salia ametumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuwapenda watoto na wazee na kuepuka kuwatenga kwani wana haki sawa na watu wengine katika jamii. Polisi wanawake wakiwa wameambatana na maafisa kutoka Benki ya CRDB wametembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiweko kula keki na watoto kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Jumuishi ambacho sasa kina watoto 230 (wenye ualbino 131,wasioona 25 na viziwi 74) na kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto chenye jumla ya wazee 12.

Aidha wametembelea wodi za akina mama,watoto na wazazi na kuwapatia zawadi wazazi na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya Kambarage.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga akizungumza katika kituo cha Kulelea watoto wenye uhitaji cha Buhangija Jumuishi kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Desemba 12,2019 wakati polisi wanawake walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema wameamua kufika Buhangija Jumuishi ili kuwatia moyo watoto wenye ualbino,wasioona na viziwi kwamba jamii ipo pamoja nao.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buhangija,Selemani Kipanya akiwakaribisha polisi wanawake na Benki ya CRDB. Alisema hivi sasa kituo cha Buhangija Jumuishi kina watoto 230 (wenye ualbino 131,wasioona 25 na viziwi 74).
Afisa kutoka Benki ya CRBD,Lewis Temu akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji cha Buhangija Jumuishi ambapo alisema wameguswa na hali ya maisha ya watoto hao na kuamua kushirikiana na polisi wanawake kutafuta zawadi/mahitaji kwa ajili ya watoto hao.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga Victoria Maro akizungumza katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Sehemu ya zawadi zilizotolewa na Polisi wanawake wilaya ya Shinyanga na Benki ya CRDB kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia na maafisa kutoka Benki ya CRDB Lewis Temu na Getrude Ikongo wakikabidhi sukari kwa Mwalimu Selemani Kipanya (kushoto) na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Jumuishi.Vitu vingine vilivyokabidhiwa kwa watoto hao ni pamoja na unga,mchele,sabuni,dawa za meno,miswaki,viatu,mafuta ya kupikia,sabuni,juisi,soda,taulo laini 'pedi',biskuti n.k.

Mtoto akikata keki iliyoandaliwa na polisi wanawake na benki ya CRDB kama ishara ya upendo kwa watoto waliopo katika kituo cha Buhangija Jumuishi.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akimlisha keki mtoto.
Afisa kutoka Benki ya CRDB Lewis Temu akimlisha keki mtoto.

Polisi wanawake,maafisa wa benki ya CRDB na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakipiga picha ya pamoja na watoto.

Askari Polisi wanawake wakiwa katika kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga walipotembelea kituo hicho na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia na Afande Amina wakikabidhi zawadi ya dawa za meno kwa Mwenyekiti wa Wazee Kolandoto,Samora Maganga.Vitu vingine walivyokabidhiwa wazee hao ni pamoja na sabuni,mafuta ya kupikia,mafuta ya kupaka,unga,mchele n.k.

Kaimu msimamizi wa kituo cha Kolandoto,Godbetha Kacharuzi akitoa neno la shukrani kwa msaada uliotolewa na polisi wanawake na benki ya CRDB.
Polisi wanawake wakiwa katika wodi ya akina mama waliojifungua kwenye kituo cha afya Kambarage kwa ajili ya kutoa zawadi ya sabuni na taulo laini 'pedi'.

Afisa kutoka Benki ya CRDB Getrude Ikongo akitoa zawadi ya sabuni na taulo lain kwa mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage.

Askari polisi akiwa amebeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha afya Kambarage.
Polisi wanawake wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na maboksi ya zawadi mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa na akina mama wajawazito na waliojifungua.

Polisi wanawake wakiwa katika wodi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya kawaida.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akitoa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa mama aliyejifungua katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua kwa njia ya kawaida.
Polisi wanawake wakiwa ndani ya wodi ya akina mama.

Polisi wanawake wakitoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga baada ya kugawa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa wagonjwa na akina mama waliojifungua.

Polisi wanawake wakitoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga baada ya kugawa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa wagonjwa na akina mama waliojifungua. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Airtel yazindua kampeni ya LIPA ADA kwa kutumia Airtel Money

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza na kuzindua kampeni maalum ambayo inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayotoa  suluhisho kwa  wateja wake kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule ambapo kwa sasa wateja wataweza kulipa karo kwa kutumia akaunti zao za Airtel Money wakiwa popote katika  kipindi hiki cha msimu wa sikukuu na kuendelea.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema kuwa LIPA ADA kwa kutumia Airtel Money itakuwa ni suluhisho kwa wazazi wengi ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi wa kwenda kupanga foleni benki ili kulipia watoto wao karo na vile vile itaendela kutoa hamasa kwa wateja wa Airtel kuendelea kutumia Airtel Money kulipia malipo mbali mbali ya bidhaa na huduma.
‘Kama mnavyojua, hiki ni kipindi cha wazazi na familia kuwa katika mapumziko, lakini pia muda huu wazazi huutumia kulipia karo za shule za watoto wao. Natoa wito kwa Watanzania kuendelea kutumia Airtel Money kwa malipo yao kwani ni njia rahisi, haraka na nafuu kwa malipo wakiwa popote wanaweza kulipa sio lazima kwenda bank na kupanga foleni, Nchunda alisema.
Nchunda alisema kuwa Airtel imeamua kuja na kampeni ya LIPA ADA kwa Airtel Money kama njia mojawapo ya kutoa suluhisho ya kifedha kwa Watanzania. ‘Kama mnavyojua, kulingana na utafiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa hivi karibuni kuonyesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 22.9 wanatumia huduma za kifedha kwa kutumia simu zao huku miamala yenye dhamani ya zaidi ya Trilioni 8 ikifanyika mpaka kufikia Juni 2019. Kwa miaka ya hivi karibuni, huduma za kifedha kwa simu za mkononi imebadilika kutoka huduma ya kawaida kama vile kununua muda wa maongezi mpaka kuwa moja ya huduma muhimu inayowezesha ukuaji sekta na  mzunguko wa fedha kila mahali.
Jinsi ya kulipia Ada Kwa Airtel Money:
  • Piga *150*60# Ili kufikia Kwenye Menyu ya Airtel Money
  • Chagua 5: Lipia Bili
  • Chagua 4: Weka namba ya kampuni (Namba ya Malipo ya Shule)
  • Ingiza Kiasi cha pesa
  • Ingiza Namba ya Kumbukumbu (Jina la mwanafunzi na Kidato / Namba ya kitambulisho cha mwanafunzi )
  • Ingiza Namba ya siri
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa Airtel inajivunia kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo sasa inakuza kwa kasi mtandao wa huduma za kifedha hapa nchini.
“Airtel tumejipanga na kujikita katika mipango yetu ya kuendelea kupanua wingo wa huduma zetu, Airtel kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money branches Zaidi ya 1000 nchi nzima ikiwa ni moaja kati ya mpango yetu ya kuleta suluhisho za kifedha pamoja na kusambaza huduma na bidhaa zetu karibu na wateja. Dhamira yetu ni kuendelea kujenga mtandao imara na unaotegemewa’. Alisema Singano huku akiongeza kuwa huduma na bidhaa za Airtel kama vile kurundisha muamala uliokosewa, kubadilisha PIN, kusajili laini za simu kwa kutumia alama ya vidole zinapatikana kwenye maduka yote ya Airtel Money branches.
 Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda  akizungumza wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayotoa suluhisho  kwa wateja wa Airtel Money kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule  kwa kutumia akaunti zao za Aitel Money wakiwa popote katika kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu na kuendelea Kushoto ni Meneja wa Airtel Jackson Mmbando
 
Meneja wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayowawezesha  kwa wateja Airtel kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule kupitia akaunti zao za Aitel Money wakiwa popote wakati msimu huu wa Sikukuu na kuendelea, hafla ya uzinduzi ilifanyika ofisi kuu ya Airtel  jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha lipa Ada kwa Airtel Money. Emmanuel Mwaisoloka
 

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI YAELEZA UMUHIMU WA BANDARI YA BUKOBA KIUCHUMI

0
0
 Meli ya MV. Nyakibalya ikiwa katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.Meli hiyo ni maalumu kwa ajili ya kubeba mizigo ndani ya Ziwa Victoria.
 Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza akizugumzia hatua mbalimbali za uboreshaji wa miundombinu katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.
 Ofisa wa Bandari ya Bukoba iliyopo mkoani Kagera Bulenga Komagi akizungumza na waandish wa habari kuhusu umuhimu wa bandari hiyo kwa wananchi wa mkoa huo na nchi jirani.
 Jengo la utawala katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera likiwa limefanyiwa maboresho.Jengo hilo lilijengwa mwaka 1945 ambalo lilikuwa linatumiwa tangu enzi za ukoloni.




Na Said Mwishehe, Michuzi Globu -Bukoba

BANDARI ya Bukoba mkoani Kagera imetejwa kuwa miongoni mwa bandari sita kubwa zilizopo katika Ziwa Victoria ambazo zipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA.

Kwa mujibu wa TPA, bandari hiyo ndio chachu ya wafanyabiashara wa Mkoa wote wa Kagera hususani  Bukoba Mjini ambao hudumia bandari kwa ajili ya kusafirisha shehena ya mizigo ya mazao ya  kilimo pamoja na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji ya wananchi.

Akizungumza leo Desemba 12, mwaka 2019, Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza amefafanua  bandari hiyo ilijengwa mwaka 1945 enzi za mkoloni na baada ya uhuru ikawa chini ya Shirika la Reli na Bandari ya Afrika Mashariki mpaka ilipofika mwaka 1977 baada ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunja ikwa chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).

"Ilipofika mwaka 1997 ikawa chini ya Kampuni  ya Huduma za Meli Tanzania( MSCL) ambao kampuni hiyo waliendelea kuihudumia bandari mpaka mwaka 2004 ilipoundwa Sheria ya TPA kwa Sheria namba 17 ikawa chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. 

"Bandari hii ni kongwe na ilikuwa na miundombinu iliyokuwa imechakaa na hivyo TPA tukaamua kuiboresha miundombinu yake.Tunatarajia baada ya kukamilika bandari hii itarejea tena katika shughuli zake hasa kwa kutambua kuanzia mwakani meli ya MV Victoria inatarajiwa kuanza tena safari zake,"amesema.

Ameongeza mradi wa kuboresha bandari hiyo pamoja na maeneo mengine umegusa pia majengo ya  abiria ambapo kulikuwa na uboreshaji wa awamu mbili, ya kwanza ilishakamilika na awamu ya pili imekamilika hivi karibuni.

"Katika maboresho haya tumetumia gharama ya shilingi  milioni 565 kwa kazi hii ya kuhuisha jengo zima la abiria na jengo la utawala, kwa sasa hivi kila kitu kimekamilika na kwa upande wa huu.

"Pia tunaendelea na ukarabati wa majengo ya kuhifadhia mizigo ambao nao huu upo katika mradi mwingine wa uboreshaji a miundombinu ya Bandari kwa eneo la Bukoba, Kemondo, Mwanza Kaskazini na Kusini,"amesema Mchindiuza.

Ameogeza miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na meli za MSCL ambazo zilifanyakazi ikiwamo meli ya Mv. Bukoba iliyoanzia katika bandari hiyo hadi bandari ya  Mwanza, Meli ya Mv. Victoria nayo ilikuwa ikija hapa pamoja na meli ya na Mv Serengeti. 

"Tunatarajia meli ya Mv.Victoria kuanzia mwezi wa mwakani itarudi kwenye safari zake na kubeba shehena.Kwa kipindi hiki tumekuwa tukiendelea kutoka huduma hasa kwa wateja wakubwa wawili ambao ni Kagera Sugar ambaye amekuwa akitumia bandari hii kusafirisha sukari kutoka hapa kwenda Mwanza.

"Mteja mwingine tunayemuhudumia ni mfanyabiashara Omukwano ambaye yeye amekuwa akileta bidhaa za madukani kama mafuta, sabuni kutoka nchini Uganda mpaka hapa Bukoba kwa ajili ya soko la hapa kwetu,"amesema.

Kuhusu uwezo wa bandari hiyo ameeleza imekuwa ikihudumia tani 6000 pamoja upande la jengo la abiria linauwezo wa kuwa na abiria 400 kwa wakati mmoja.

TPA KANDA YA ZIWA YAWASHAURI WAFANYABIASHARA KUTUMIA BANDARI YA KEMONDO KUSAFIRISHA MIZIGO

0
0


Daraja la reli ambalo linatumika kupitisha shehena ya mizigo inayopakiwa katika behewa na kisha moja kwa moja kuingizwa ndani ya meli. Daraja hilo la reli ambalo lipo katika Bandari ya Kemondo Bay ambayo kwa sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari imeamua kuiboresha na siku za karibuni itaanza kutoa huduma.


Muonekano wa reli inayokwenda bandari ya Kemondo Bay ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupitisha shehena ya mizigo inayosafirishwa kwa njia ya reli na kisha kupakiwa katika meli.
Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza(kushoto) akielezea hatua mbalimbali za uboreshaji wa miundombinu katika bandari ya Kemondo Bay iliyoko mkoani Kagera.
Sehemu ya muonekano wa dara la reli katika bandari ya Kemondo Bay.TPA imeamua kuboresha reli hiyo inayoingia katika meli ili kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Kagera wanakuwa na uhakika wa kusafirisha mizigo yao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.



Said Mwishehe-Michuzi TV

WAFANYABISHARA mbalimbali nchini na hasa wa Mkoa wa Kagera wameshauriwa kutumia usafiri wa meli na reli katika kusafrisha shehena za mizigo ikiwemo inayotokea Bandari ya Dar es Salaam kwani gharama za usafiishaji ziko chini ikilinganisha na usafiri wa malori.

Kauli hiyo imetolewa kipindi ambacho Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kuwa na mpango mkakati wa kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari katika maziwa makuu ambapo miradi mbalimbali imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.

Kutokana na uboreshaji huo wa miundombinu ya bandari, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini imetumia nafasi hiyo kutoa ujumbe kwa wafanyabishara kutumia bandari zilizopo nchini ikiwemo ya Bandari ya Kemondo Bay ambayo sasa iko tayari kufanyakazi kwa namna ile ile iliyokuwa iliyokuwapo miaka ya nyuma.

Akizungumza zaidi ,Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza amewaambia waandishi wa habari waliopo kwenye ziara ya kutembelea na kushuhudia utekelezaji wa miradi ya kuboresha miundombinu ya bandari kuwa TPA katika Bandari ya Kemondo ambayo ni maarufu kwa meli za kubeba mizigo kuwa sasa imekamilika na hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara kuitumia kusafirisha shehena za mizigo ya aina mbalimbali.

"Mwito wetu kwa wafanyabishara wa Mkoa wa Kagera na mikoa mingine nchini waendelee kutumia bandari hii ya Kemondo kusafirisha mizigo yao.Ukweli kusafirisha mizigo kwa njia ya meli na reli ni salama na nafuu zaidi ukilinganisha na aina nyingine ya usafiri, ndio maana TPA tumeamua kuboresha miundombinu ya bandazi zetu ili kutoa huduma ya uhakika wakati wote,"amesema Mchindiuza.

Kuhusu bandari hiyo , amesema ilijengwa mwaka 1971 na kukamilika mwaka 1974 na kwamba lengo la bandari hiyo kwa wakati huo lilikuwa zaidi kusafirisha shehena za mizigo mbalimbali na hasa zao kuu lilikuwa kahawa lakini pia ilikuwa inahudumia abiria. Bandari ya Kemondo Bay ilikuwa ni kituo kikubwa cha kubeba mizigo ikiwamo mihogo, ndizi na maparachichi yaliyokuwa yakisafirishwa kwa wingi kutoka katika eneo hilo.

"Pia mizigo yote iliyokuwa ikitolewa mkoani Mwanza kama vifaa vya ujenzi ikiwamo saruji pamoja na nondo Ilikuwa ikifikishwa hapa na baadaye kutawanywa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera pamoja na vitongoji vyake. Kwa takribani miaka 15 iliyopita Bandari ya Kemondo Bay ilikuwa inakwenda kwa kusimama na kusuasua na baadaye tukajikuta hatuna oparesheni zozote zinazofanyika kwenye hili,"amesema.

Ameongeza kuwa bandari hiyo ina sehemu mbili, kuna sehemu ya mwalo ambayo ipo pembeni pamoja na sehemu ya Bandari kuu na kwamba katika eneo hilo zilikuwa zinafunga meli kubwa kabisa lakini baada ya mdororo uliotokea meli kubwa nazo zikawa hazifiki.
 
"Katika eneo hili bado kukawa na mahitaji ya watu wanapokwenda visiwani na hivyo kukawa na boti ndogondogo ambazo zilikuwa pembeni mwa bandari. Mamlaka baada ya kuona uhitaji na pia ya hizi boti ndogondogo tukajenga eneo la uwezeshaji katika eneo hilo la pembeni ambapo tumejenga gati ndogo zinazoweza kuhimili boti ndogo kutia nanga.

"Katika kipindi ambacho huduma imesimama kwenye eneo hili Bandari ya Kemondo kule upande wa mwalo huduma zikawa zinaendelea kwa kuwa kuna boti ambazo zinatoka huduma katika visiwa kwenye eneo hili. Kwa kifupi baada ya TPA kuona hali hii inaendelea tukasema hapana, hivyo tumeamua kuboresha miundombinu ikiwemo ya kufufua njia ya reli inayoingia bandarini pamoja na daraja la reli,"amesema.

Amesema kuwa reli hizo zilikuwa zimefukiwa kabisa na kutoonekana lakini uboreshaji wa miundombinu katika bandari ya Kemondo sasa reli zinapitika vizuri na hivyo mizigo ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo itaweza kupitishwa katika bandari hiyo.

"Shilingi milioni 815 zilitengwa kwa ajili ya kazi hiyo ambayo ilianza wiki tatu zilizopita na sasa iko mwishoni kumalizika na bandari kuanza rasmi kutoa huduma ya kusafirisha mizigo.Tuna imani kubwa bandari hii itakuwa ni kichocheo cha ajira katika eneo letu hili.Pia itamuwezesha mwananchi wa kipato cha chini wakiwemo wakulima kusafirisha ndizi na parachichi zao bila tatizo,"amesema.

Kuhusu matarajio yao, amesema bandari hiyo itaanza kazi kabla ya mwisho wa Desemba mwaka huu na tayari wanaye mteja ambaye wamekuwa wakifanya naye kazi tangu awali.

KANISA LA ABC LA TABATA JIJINI DAR ES SALAAM KUWEKEZA KWENYE MIRADI KUSAIDIA JAMII

0
0
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila (kushoto),akiongoza kumuombea Askofu wa Kanisa hilo, Flaston Ndabila na mke wake Janeth katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jana.
Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo.Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiwapungia mikono waumini wa kanisa hilo wakati wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo.
 Watoto wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Watumishi wa Mungu kutoka nje ya nchi wakionesha mshikamano kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Bishop Mark Mugekenyi (Kenya) na Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi .
 Nyimbo zikiimbwa.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Nyimbo zikiimbwa.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiingia kanisani.
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiingia kanisani.Kutoka kushoto  ni  Rehema, Tabitha na kaka yao Gadi.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiwa na Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani)
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Katibu Mstaafu wa CPCT Taifa, Askofu  Dkt. David Mwasota, akiomba kabla ya kuanza kwa maadhimisho hayo.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, akitoa historia fupi ya kanisa hilo.
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiwa katika maadhimisho hayo.Kutoka kushoto  ni  Gadi, Rehema na Tabitha.
 Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Peter Sifi akitoa taarifa ya kanisa hilo.
 Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), akiomba katika maadhimisho hayo.
 Bibi na Bwana Dickson Malali wakizungumzia kanisa hilo.
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakizungumzia kanisa hilo.
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakikabidhi zawadi.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakipokea zawadi ya mashine ya kufulia.
 Bwana na Bibi, Martin Muhembano wakizungumzia kanisa hilo.
 Pastor Florian Katunzi  na mke wake Rachel wakizungumza.
 Bishop Musa Ngobese kutoka Afrika Kusini, akizungumza
 Bishop Mark Mugekenyi,  akizungumza.
 Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, akikabidhi zawadi.
 Askofu Dkt. Eric Mwabigaja, akikabidhi zawadi.
Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani),akikabidhi zawadi.
 Zawadi ya vitenge ikienda kutolewa.
 Majirani wa kanisa hilo wakitoa zawadi ya jogoo.
 Majirani wa kanisa hilo, wakizungumza.
 Wanafamilia ya Askofu Ndabila katika picha ya pamoja.
 Keki ikikatwa.
 Watoto wakilishwa keki.
Mchungaji, Nathaniel Ndabila akifunga maadhimisho hayo kwa maombi.
Na Dotto Mwaibale
KANISA la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam linatarajia kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuweza kusaidia jamii hasa vijana waweze kujikomboa kiuchumi.
Hayo yalielezwa jana katika hafla ya  maadhimisho ya miaka 25 ya huduma ya kanisa hilo wakati wa utoaji wa taarifa fupi iliyosomwa na Peter Sifi ambaye ni Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila.
"Katika kipindi hiki cha miaka 25 ya huduma ya kanisa letu tumefanya mengi lakini sasa tunataka kujikita katika uwekezaji wa kujenga chuo cha biblia ambacho ndani yake kutakuwa na chuo cha ufundi " alisema Sifi.
Alisema chuo hicho, kitatoa mafunzo ya ufundi washi, umeme, ushonaji, kompyuta, ujenzi, ushauri wa masuala ya ujasiriamali, useremala  na kuwa  tayari kanisa hilo limetenga sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa kisasa  ambao ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni eneo la Kifuru Manispaa ya Ilala.
Alisema lengo la kuanzisha kwa uwekezaji huo ni kutoa fursa kwa wachungaji watakao kuwa wanasoma kwenye chuo hicho kujifunza stadi za kazi mbalimbali badala ya kutegemea uchungaji pekee na baada ya mafunzo hayo nao wapeleke elimu hiyo kwa jamii.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God  (EAGT) Dkt.Asumwisye Mwaisabila ambaye ni miongoni mwa wazee wenye wanaoheshimiwa aliyedumu katika imani kwa muda mrefu akifanya kazi pamoja na Mzee Moses Kulola na Mungu amemjalia neema katika imani na usemi aliwataka wachungaji kufanya kazi ya utumishi kwa nguvu zote ili waje waweke alama ya utumishi wao.
"Kazi ya utumishi inahitaji uvumilivu na kujituma na sio mchezo mchezo mwenzetu Ndabila sasa anaadhimisha miaka 25 tangu aanze huduma hii na amepita katika magumu mengi na leo anamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapa alipo mungu aendelee kumbariki zaidi huduma yake ikue zaidi ya hapo" alisema Mwaisabila.
Askofu Flaston Ndabila akitoa historia fupi ya kanisa hilo alisema yeye na mke wake walipita katika changamoto nyingi ikiwemo ya kulala njaa wakati wakianza huduma hiyo ya kichungaji huku wakiwa na mshirika mmoja tu kwa kipindi cha miaka miwili.
Alisema wanamshukuru mungu kwani hivi sasa wanawachungaji na baadhi ya makanisa yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi alisema Tanzania ni nchi rafiki na nchi ya Burundi kwani ilijihirisha mwaka 2015 wakati lilipotokea jaribio la kutaka kumpindua Rais wa nchi hiyo wakati yupo hapa ambapo Tanzania ilisaidia kumrudisha nyumbani na mapinduzi hayo kushindwa.
Akimzungumzia Askofu Ndabila, Tharcise alisema mafunzo aliyompa yamemsaidia sana katika kanisa lake na yamebadilisha maisha yake ukilinganisha na hapo mwanzo.
Katika maadhimisho hayo maaskofu na wachungaji kutoka ndani na nje ya nchi walihudhuria baadhi yao ni Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, Bishop Mark Mugekenyi (Kenya), Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Katibu Mstaafu wa CPCT Taifa, Askofu  Dkt. David Mwasota, Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), Pastor Florian Katunzi na Askofu Primus Ishobeza na wengine.

TAARIFA YA KUONGEZEKA KWA SIKU ZA SAFARI ZA TRENI YA ABIRIA DAR ES SALAAM-KILIMANJARO


ACHA KABISA WEWE! QUEEN DARLING RASMI KWENYE NDOA ...WAAMUA KUWEKA MAMBO HADHARANI, DIAMOND ASHINDWA KUVUMILIA

0
0
Na Khadija Seif -Michuzi TV

QUEEN Darling kaolewa... Na nani?Hilo ndilo lilikuwa swali kwa wanadamu wanaoishi kwenye ardhi ya Mjomba Magu baada ya kuona picha za Queen Darling Darling akiwa na mumewe wa ndoa Isahaka Mtoro.

Hatimaye wawili hao wameamua kuweka mambo hadharani na wala sio siri tena .Queen Darling kaolewa kweli na Isihaka Mtoro baada ya penzi la kificho kwa muda mrefu ambapo leo wameona isiwe tabu acha Umma wa Watanzania ujue.  Ndoa ilishafika Sikh kadhaa zilizopita na leo wamekutana kwa ajili ya sherehe ya kufurahia ndoa yao.

Kwa kukumbusha tu Queen Darling ambaye ni msanii maarufu kutoka Lebo ya WCB na dada wa Msanii mwenye ubora wake kwa sasa Nasseb Abdul a.k.a Diamonda walifunga ndoa katika moja ya msikiti uliopo Temeke jijini Dar es Salaam ambapo watu wachache sana ndio waliopata nafasi ya kushiriki.

Baada ya   ndoa hiyo leo sasa Desemba 12,mwaka huu  2019 wameona usiwe tabu waliodhani ilikiwa Muvi waone kilichofanyika ,hivyo hapo Mbezi Beach bonge la sherehe linaendelea na kuhudhuria na mataa kibao.Hata yule mwanadada machachari Gigy Money naye ameshiriki.Kha!Unashangaa wakati shughuli za mataa lazima wawepo na mstaa wenzao.

Wakati sherehe hiyo ikiendelea Queen Darling ambaye jina lake halisi ni Mwanahawa Abdul pamoja na mumewe Isihaka Mtoro wamepata nafasi ya kuzungumzia ndoa yao na hiyo ni baada ya kufanyika tukio la Queen Darling kuvushwa pete hadharani.

Unajua Mumewe Queen  Darling kasemaje? Ngoja nikupashe upashike,bila wasiwasi Isahaka amesema ameamua kumuoa Mwanahawa baada ya kupata ridhaa na baraka kutoka kwa mkewe wa kwanza,hivyo maneno ya kwamba mkewe wa kwanza hana habari hazina ukweli wowote.

"Kwanza naomba ifahamike sijamuoa Queen Darling bali nimemuoa Mwanahawa Abdul.Muziki ni kazi yake hivyo siwezi kumkataza lakini nje ya.muziki ni mke wangu wa ndoa halali.Hili la kuoa mke wa pili naomba niseme mimi ni Muislamu na sio dhambi kuoa mke zaidi ya mmoja, tunayoruhusu ya kuoa hadi wake wanne maana Mtume alioa wake saba,amesema.

Kuhusu maneno kuwa ameamua Queen Darling kwasababu ya mkewe wa kwanza kutokuwa na mtoto,Isihaka Mtoro amesema kuwa mkewe hana tatizo la kutopata mtoto,na ndoa yake na Queen haina uhusiano wowote kuwa ameoa ili kutafuta mtoto kwani mtoto  ni mapenzi ya.Mwenyezi Mungu.

Ndoa raha bwana asikwambie mtu! Queen Darling alipoulizwa kuhusu kutolewa mke wa pili amejibu kuwa kwanza nakuaminia Isahaka alivyomwambia anataka kufunga naye ndoa lakini hatimaye imekuwa kweli na leo full bata.

Anasema kuwa kuhusu kuwa mke wa pili  hajisikii vibaya na ndoa ni jambo la kheri na kwamba ukiwa kwenye ndoa unakuwa mtu halali wa mtu.Hata hivyo amesema kuwa kwake anajisikia furaha na kwamba hajamlazimisha Isahaka amuoe bali wote wawili wameridhiana law dhati ya mioyo yao.

Alipoulizwa kuhusu mtoto Queen Darling.amejibu kuwa ndoa ndilo jambo la msingi na kupata mtoto ni jambo la majaaliwa ya Allah lakini wakati ukifika wa kupata mtoto watakuwa  naye kwani sio dhambi .

Alipomwambia anataka kumuona ulihisi  mshangaa na hakuwamiani lakini hatimaye ameolewa.mwanzoni alifikiria ukeweza lakini baada naye akaona wenzake ataitwa mke na yeye atakuwa mkewe.

Kuhusu mtoto amesema darling na mumewe wamesema mtoto ni jambo la kheri na Mungu akipenda watapa mtoto.

Wakati sherehe zikiendelea kwa upande wake Diamond ameshindwa kuficha furaha aliyonayo baada ya dada yake Queen Darling kufunga ndoa ambapo amesema kila kaka mwenye dada anatamani kuona dada anaolewa.

Diamond amesema kimsingi wawili hao waishi vuziri kwenye ndoa na kwamba yeye anayependwa na dada yake atampenda. "Dada zangu wakianimbia huyu ndio mwenzangu nami nitakuwa huko huko, hata wakigomba mimi siwezi kuwa na upande wowote kwani ikitokea wakielewana nitakuwa sina cha kufanya zaidi ya kuona aibu,"amesema.

Baba yake Queen Darlin Mzee Abdull Naseeb amesema wamefurahishwa na kitendo cha mtoto wake kufungua ndoa ,na ushauri wake waishi kwenye ndoa kwa maelewano mazuri na kila mmoja kutambua nafasi yake.




HUKUMU YA JAMAL MALINZI NA WENZIE

MAHAFALI YA KUMI NA TATU (13) YA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM (DIT) YAFANA

0
0

 Wahitimu wa wakimsikiliza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa wakati akiwahutubia kwenye mahafali ya 13 Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwenye mahafali ya 13 katika viwanja  vya  Taasisi hiyo leo.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa  akiwahutubia Wahitimu  wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwenye mahafali ya 13  katika viwanja  vya  Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Prof Preksedis Ndomba,  akiteta jmbo na Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa na mwisho ni Mwenyekiti wa Baraza la DIT, Prof Apollinalia Pereka.

 Mathias Shayo akimpa mwanae Morgan shada la ua alipokuwa akimpongeza kwa kuhitimu shahada ya uhandisi umeme katika chuo cha DIT jijini Dar es Salaam.
 Mary Sambaya ambaye ni mama mdogo wa Morgan Shayo akimpa zawadi mwanae alipokuwa akimpongeza kwa kuhitimu uhandisi umeme katika chuo cha DIT jijini Dar es Slaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

WANANCHI WILAYA YA MAGU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA UJIO WA CHUO CHA MIPANGO

0
0
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Bajeti ya Serikali Bw. Pius Mponzi akizungumza wakati wa makabidhiano ya eneo litakapojengwa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – IRDP lililopo katika kitongoji cha Kitumba, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bw. Goerge Lutengano, akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya, hati ya umiliki wa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 21 kilichopo kitongoji cha Kitumba, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, eneo ambalo Halmashauri hiyo imelitoa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kudumu ya Chuo hicho -Kanda ya Ziwa
Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt. Philemon Sengati, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya eneo kati ya Halamashauri ya Wilaya ya Magu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini iliyofanyika Jijini Mwanza. Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Mgeni Rasmi Bw. Pius Mponzi aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na anayefuatia ni Mkuu wa Chuo cha Mipango, Profesa Hozen Mayaya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa makabidhinao ya eneo lililotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Mipango-Kanda ya Ziwa.
Wananchi wa Kitongoji cha Kitumba kilichopo-Kisesa- Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Jijini Mwanza. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Mwanza)

…………………..

Na Ramadhani Kissimba na Saidina Msangi, WFM, Mwanza

Wakazi wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazotokana na ujenzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini kitakachojengwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Hayo yalisemwa na Kamishina msaidizi wa Idara ya Bajeti ya Serikali -Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Pius Mponzi wakati akipokea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James eneo lenye ukubwa wa ekari 21 lililotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa ajili ujenzi wa chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Tawi la Kanda ya Ziwa.

Bw. Mponzi alisema ujenzi wa chuo hicho utafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo, hivyo kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwekeza katika miradi ambayo itawasaidia kuongeza kipato na kuwaletea maendeleo.

‘’Chuo hiki kwa sasa kinadahiri wanafunzi zaidi ya 3,000 katika Kampasi ya Mwanza, hivyo ni fursa nzuri hasa kwa wajasiriamali wadogo kubuni na kuanzisha biashara zitakazowasaidia kuondokana na umasikini’’ alisema Bw.Mponzi.

Aidha Bw. Mponzi aliitaka Menejimenti ya Chuo hicho kuhakikisha ujenzi wa chuo hicho unaanza maramoja na kuhakikisha malighafi zote zitakazotumika katika ujenzi huo zinatumika ipasavyo pasipo ufujaji wowote.

“Ninawaagiza pia wakandarasi mtakaojenga chuo hiki kuhakikisha mnawatumia vijana wanaozunguka eneo la mradi kufanya kazi za ujenzi ili kuwapatia ajira vijana wa Halmashauri ya Magu.

Awali akizungumza kabla ya makabidhiano ya eneo hilo, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya alisema uongozi wa chuo uliamua kuanzisha kituo cha mafunzo katika Kanda ya Ziwa -Mwanza ili kuongeza kasi ya kutimiza lengo la Serikali la kuwaandaa watalaam wa kupanga na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi mbalimbali hapa nchini na kusogeza huduma za chuo karibu na wananchi na wadau wa maendeleo.

Prof.Mayaya alisema Kituo cha Kanda ya Ziwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 kimekuwa kikiendesha shughuli zake katika majengo ya kupangisha, hivyo kupatikana kwa eneo hilo kutaondoa changamoto hiyo na kituo kujiimarisha zaidi katika kuwapatia elimu vijana wa Kitanzania wenye sifa za kusoma katika Taasisi za elimu ya juu.

Aidha Prof. Mayaya alisema Chuo cha Mipango kimejizatiti kujenga chuo bora zaidi na cha mfano katika Kanda ya Ziwa na kwa kuanzia yatajengwa majengo mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,220.

Akiwashukuru uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Chuo hicho, Mkuu wa Wilaya Magu Dkt. Philemon Sengati, , alisema ujenzi wa chuo hicho utasaidia kufungua fursa mbalimbali za uwekezaji katika Wilaya hiyo na kuwakaribisha wawekezaji wengine kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa kuwa maeneo ya kuwekeza yapo ya kutosha na yenye mandhari nzuri.

Wadau wakutana kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto na vijana mijini

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford akitoa salamu za UNICEF wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtathimini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Mr. Hong Vu akiendesha chemsha bongo wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakifurahia jambo wakati wa chemsha bongo kwenye kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu, Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete pamoja na Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (katikati) akitoa maelezo mafupi kuhusu ESRF kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu (wa pili kulia) alipofika ofisini kwa mkurugenzi huyo kusaini kitabu cha wageni wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete (wa kwanza kulia).
Baadhi ya wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakishiriki kuchangia maoni wakati wa kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu amewataka watafiti wa programu ya Utafiti itakayoangalia huduma na ubunifu kwa watoto na vijana katika miji nchini Tanzania kutoa suluhisho la kudumu kuhusu mahitaji na usalama wa watoto na vijana ili kuwa na taifa lenye watoto wenye kujitambua.

Alisema ingawa anatambua kwamba tafiti zikifika mwisho wataitwa kuelezwa matokeo lakini kutokana na haja ya kutafuta suluhu ya changamoto zilizopo kwa sasa ni vyema watafiti wakapata muda wa kueleza maendeleo ya tafiti zao na hasa matokeo ya awali kabla ya kufika mwisho.

Alisema hayo katika kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana lililofanyika juzi kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji. Programu hiyo inaandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab).

Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau takribani 40 kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi.
Alisema hali hiyo itasaidia Serikali kuchukua hatua mapema zaidi za kukabiliana na changamoto za watoto na hasa suala la malezi.

Alisema kwa sasa kumekuwa na changamoto nyingi za malezi na hivyo kusababisha uwapo wa watoto wengi kwenye mazingira magumu na pia mitaani.

Alisema utafiti unaokusudiwa ni utafiti wenye maana kubwa kwa kuwa unaangalia mazingira ya leo kwa manufaa ya taifa la kesho na kuondoa viashiria vya hatari katika malezi na hatima ya watoto wa Tanzania hasa wale wanaoishi mijini.

Alisema watoto na vijana wanaoishi mijini wanakabiliwa na changamoto nyingi na ni wajibu wa jamii kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinaondolewa kwa kuwepo kwa mbinu bora za kukabiliana na changamoto hizo, mbinu zenye manufaa na zinazowezekana.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu warsha na programu ya tafiti inayoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na UNICEF alisema wanatengeneza programu hiyo kwa ajili ya kutanzua shida zinazowapata watoto na vijana wanaoishi katika miji.

Alisema warsha hiyo iliyojumuisha watafiti na wadau kadha wa masuala ya utafiti imelenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau ili kuweza kutengeneza programu mpya inayogusa masuala ya watoto na vijana katika miji yetu.

Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu kongamano hilo, alisema kwamba utafiti huo utafanywa chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) na kusema  mipango miji ni suala muhimu kwa nchi ya Tanzania hasa wakati huu inapoelekea katika uchumi wa viwanda.

Alisema wakati Tanzania inatarajia kuwa na watu milioni 45 wanaoishi katika miji ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni nchi ya sita kwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu Duniani ifikapo mwaka 2050 na hivyo ipo haja ya kuwa na sera madhubuti inayohusu ulinzi kwa watoto na vijana wanaoishi mijini.

Alisema kutokana na serikali kutilia umuhimu wa masuala ya ukuaji wa miji katika Mpango wa Pili Miaka 5 wa Maendeleo  2016/17 - 2020/21 (FYDP II) kulianzishwa  TULlab mwaka 2017 ambapo sekretarieti yake ni ESRF wakati mwenyekiti ni Wizara ya Fedha na Mipango.

Kazi ya TULab ni kuisaidia serikali  katika masuala ya ukuaji wa miji Tanzania. Kwa kuzingatia  tayari TULab imefanya tafiti na kuandaa Mpango Kazi kuelekea Maendeleo ya Miji.
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images