Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA MARA ASIMAMIA ZOEZI LA KUACHIWA HURU WAFUNGWA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima akiongea na sehemu ya wafungwa 23 walioachiwa katika gereza la Musoma kati ya wafungwa 259 waliofaidika na msamaha wa Rais Mkoani humo.
Mhe Malima, ambae alikuwa ameongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mkoa wa Mara (RAS) Mhe. Carlo Mthaphula,  amewataka wafungwa hao wakamlipe fadhila waliyopewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kwenda kutenda mema na ya maendeleo katika jamii badala ya kuanza uhalifu upya.






Wadau wa Alizeti mkoani Singida watakiwa kupanga mikakati ya pamoja kuongeza uzalishaji

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka amewataka Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa Alizeti ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika alizeti ambavyo vinashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi. 

Rutageruka ametoa wito huo  wakati akiongea na Wasindikaji, wakulima wa alizeti na watendaji wa Serikali wakati wa Mkutano na Wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida uliofanyika leo tarehe 11.12.2019 katika Ukumbi wa VETA. 
Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya  Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.

TCRA yapeleka kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako mkoa Mtwara

$
0
0

 
 
 
Mtwara Jumatano 11 Disemba 2019

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeini ya ‘Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha Usajili mkoani Mtwara huku ikiwahimiza mwananchi wa mkoa kukamilisha usajili wa laini zao za simu kwa alama ya vidole kabla ya mwisho wa mwezi.

Kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha usajili ya laini ni ushirikiano wa makampuni yote ya simu za mkononi hapa nchini huku ikisimamiwa na TCRA kwa udhamini wa FSDT.

Akizungumza Mtwara wakati wa kuzindua kampeini hiyo ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako, Mmwakilishi wa TCRA Kanda ya Mashariki Viollet Essoko amesema changamoto zilizopo zimekuwa zikifanyiwa kazi na kusisitiza kuwa licha ya kuwekwa matangazo ya kuhamasisha umma haachwi mtu nyuma kamilisha usajili bado kuna wananchi wanasua sua kufuatilia michakato ya NIDA ili kupata namba na kusajili line zao za simu.

Amesema idadi kubwa ya vijana wamekuwa wakipuuzia zoezi hilo huku watu wenye umri mkubwa wameonyesha kujitokeza kwa wingi kufuatilia vitambulisho vya nida lakini pia kusajili line zao za simu.

Wakati huo huo, baadhi ya wakazi wa mkoa wa mtwara ambao bado hawajapatiwa vitambulisho vya taifa vya NIDA wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji na vitendea kazi ili kurahisisha zoezi hilo ambalo kwa sasa limekuwa na muamko mkubwa kwa wakazi wake.

Wakazi hao wametoa ombi hilo kutokana na kukaa kwenye foleni ili kupata huduma hiyo kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo ipasavyo.

Hata hivyo wakazi hao wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji sambamba na vitendea kazi ili zoezi hilo liweze kwenda kwa haraka hasa kipindi hiki ambacho idadi ya watu imeongezeka.

Mapema akifungua zoezi hilo ambalo litadumu takribani wiki nzima katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda amewataka wananchi kutopuuzia zoezi hilo ambalo umuhimu wake ni mkubwa.

Amesema huwezi kuitwa Mtanzania kama huna kitambulisho cha NIDA na kuwataka watambue kuwa huduma muhimu zitapatikana tu kwa mtu mwenye kitambulisho cha nida na hivyo kuwasihi kukamilisha zoezi la nida na kupata usajili wa laini zao za simu.

Zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatarajiwa kukamilika disemba 31 mwaka huu.

10TH IPG KICKS OFF, EAC SELECT SIDE LOSE IN SOCCER CURTAIN RAISER, RECOVER IN NETBALL

$
0
0

EAC Select Side featuring legislators from the Partner States’ Parliaments and the management of the East African Water and Sports Cultural Organization (EAWASSCA) in a thrilling encounter at the St Mary’s Kitende Stadium, Kampala.
Ibrahim Jamal intercepts a pass during the match. EALA drew 1-1 with Parliament of Uganda
EALA netball team drew 22-22 with EAWASSCA netball team.
EALA legislators beat the water body managers 22-16


……………


The 10th edition of the EAC Inter-Parliamentary Games (IPG) kicked off yesterday in Kampala, Uganda. To commence the twelve-day extravaganza was a football curtain raiser pitting an EAC Select Side featuring legislators from the Partner States’ Parliaments and the management of the East African Water and Sports Cultural Organization (EAWASSCA) in a thrilling encounter at the St Mary’s Kitende Stadium, Kampala.

The water body pipped the EAC legislators 2-1. In netball, the EALA legislators beat the water body managers 22-16. In the second curtain raiser soccer match involving staff members, EALA drew 1-1 with Parliament of Uganda, while the EALA netball team similarly drew 22-22 with EAWASSCA netball team.

Attention shifts this morning to the MTN arena in Lugogo where netball action kicks off with Parliament of Uganda facing off with Parliament of Burundi in the first match before Parliament of Kenya takes on Parliament of Tanzania in the second match of the day.

In Men’s volleyball, Parliament of Uganda will face stiff opposition from Parliament of Burundi in the first match, before Parliament of Kenya locks horns with Parliament of Tanzania in the second match of the day at the same venue. The Volleyball women matches will take the same script with Parliament of Uganda playing Parliament of Burundi before Parliament of Kenya faces EALA in the next match.

In football, EALA will take on Parliament of Kenya at the KCCA Grounds in a match to be preceded by another thriller involving four-time Champions, Parliament of Uganda, who take on Parliament of Burundi.

Earlier on yesterday, the Speaker of the Parliament of Uganda, Rt Hon Rebecca Kadaga, officiated at the Pre-Tournament Conference calling on legislators to use the opportunity to nurture networking and bonding among the legislators.

In her remarks, Rt Hon Kadaga underscored the need for ensuring parliamentary diplomacy, saying various activities were necessary to ensure the people of East Africa move together in integration process. “We are here to learn from each other, appreciate each other in order to strengthen the integration process. I thank you for the honour of giving Parliament of Uganda to host the 10th Inter-Parliamentary Games”, Rt. Hon Kadaga said.

“When we established the Community in 1999, we declared it people-centred. I am happy that the people are moving together in that direction”, Rt Hon Kadaga said.Hon Mary Mugyenyi representing the EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin, called for the spirit of collegiality to prevail as the games take place.

“Through a networking event of this nature, the spirit of harmony, friendship and camaraderie must be extended at all times and all differences resolved amicably”, she said.

As we mark the decade of sporting activities, we should not just reflect on the past achievements, but rather herald on what the future portends. Integration is progressive and therefore, we should chart the path as defined in our integration agenda”, Hon Mugyenyi added.

The legislator reiterated the importance of making the integration pillars work. She said the tenets of the Common Market Protocol were yet to be fully harnessed and exploited.


“Free movement and a free market should just not be a mirage – but a reality”, she said.

“We should exploit the opportunities offered by sports and culture as anchored under Article 119 of the Treaty for the Establishment of the EAC if we are to continue to drive the agenda and to find solutions to the myriad of challenges that sometimes/often come in the way of integration”, she added.

EALA Member, Hon Rose Akol presented a paper on the milestones of the EAC themed: EAC@20: Deepening Integration, Widening Co-operation while former EALA Member, Hon Bernard Mulengani presented a paper on Discipline and Etiquette.

The IPG which was mooted 10 years ago has over the years realized several successes. Fundamentally, Parliamentary games are a key aspect of building relations between the EALA and the National Legislatures in the EAC region. The games play a fundamental part in enabling EALA’s interaction with Members of the National Legislatures in the Partner States as envisaged in Article 49 (2a) of the Treaty for the Establishment of EAC.

The tournament disciplines include football (St Mary’s Kitende and KCCA Grounds), walk-race, netball (MTN Arena Lugogo), golf (Kigo Serena Golf Course), athletics (Namboole Stadium), tug-of-war (Namboole) and volleyball (MTN Arena Lugogo). Athletics will feature races in 100 meters, 200 meters, 400 metres, 800 and 1500 metres respectively for men and women. The 4x 400m relay and the 4x 100m races are also on the cards.


The Games themed: “The EAC: One Spirit; One Destiny: Strengthening Integration through 10 Years of Inter-Parliamentary Games” brings together EALA and the National Legislatures

JAJI KIONGOZI ARIDHISHWA NA MAHAKAMA MTANDAO TANGA

$
0
0
Afisa Tehama wa Mahakama Kuu Tanga, Bi. Amina Ahmad akielezea utekelezaji na usimikaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Maktaba ya Mahakama Kuu Tanga (E- Library).
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Francis Kabwe akisoma taarifa ya Kanda hiyo.
Mhe. Jaji Kiongozi akizungumza na wananchi waliofika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
Mhe. Jaji Kiongozi (wa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama Kuu Kanda ya Tanga. Kushoto kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda Tanga Mhe. Amiri Mruma akifuatiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Francis Kabwe. Kulia kwake ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Edson Mkasimongwa akifuatiwa na Mtendaji wa Mahakama Bw. Ahmed Selemani Ng’eni.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ameupongeza uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ya utekelezaji wa Mahakama Mtandao (E- Judiciary ) licha ya kupata bajeti ndogo.

Aidha, Jaji Kiongozi huyo amempongeza Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Bi. Amina Ahmad kutokana na jitihada zake za kutumia vyema taaluma yake kubuni na kuanzisha mifumo ya kielektroniki ya ndani kwa ajili ya kusaidia utunzaji na uhifadhi salama wa majalada ya mashauri na nyaraka mbalimbali za kiutendaji.

Afisa Tehama huyo alibuni mifumo hiyo kwa kupitia mifumo ya “Tanga Record Centre”, E- Office, E-Library na Receive & Return File Database (Double R).

Vile vile alimpongeza Afisa huyo kwa kuwezesha kusimikwa (Installation) kwa mifumo ya matangazo kwa umma (Public Announcement system) na uoneshaji wa orodha ya mashauri kwenye Televisheni (Case Broadcasting system).

Alipongeza utendaji wa pamoja (Team work) uliojengwa na watumishi wa Kanda ya Tanga chini ya uongozi na usimamizi wa Jaji Mfawidhi, Mhe. Amiri Mruma.

Mhe. Jaji Kiongozi aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya Kanda iliyosomwa kwake na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanga, Mhe. Francis Kabwe, na baadae kujionea shughuli na utendaji wa mifumo ya kielekroniki kupitia ratiba ya ziara yake ya siku moja aliyoifanya tarehe 10 Desemba mwaka huu.

Katika ziara hiyo alionyesha kuridhishwa na utendaji wa kanda hiyo na kusema kuwa, inastahili kuwa ya kimkakati kwa mafunzo ya vitendo kwa viongozi wapya hasa kwa kuzingatia kwamba iko jirani na Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA).

Dkt Feleshi aliutaka uongozi huo kuwatambua, watumishi wanaothubutu kuonesha ubunifu kutokana na vipaji vyao waeleweke na kuenziwa ili waendelee kuwa hazina ya Mhimili wa Mahakama badala ya kukatishwa tamaa.

Wanafunzi 912 Wahitimu Masomo yao TEWW

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 55 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) akimpongeza mhitimu aliyekuwa na mahitaji maalum aliyefanikiwa kuhitimu na kufaulu vizuri licha ya kuwa na ulemavu wa kuona katika mahafali yaliyofanyika 06.12.2019 Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dkt. Leonard Akwilapo ( wa tatu kushoto waliokaa), akifuatiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Naomi Katunzi , Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya watu Wazima (TEWW), Dkt. Michael Ng’umbi (wa tatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakufunzi wa TEWW walioshiriki kwenye Mahafali ya 55 ya TEWW yaliyofanyika Jijini Dar es Salaaam tarehe 6/12/2019
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Michael Ng’umbi akizungumza wa wahitimu (hawapo pichani) wakati wa Mahafali ya 55 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, yaliyofanyika tarehe 06.12.2019 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na TEWW)

**************************************

Wanafunzi 912 wahitimu masomo yao katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Akizungumza wakati wa mhafali ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema kuwa kati ya wanafunzi hao 138 ni wa shahada, 724 ni stashahada na 50 ni wa astashahada.

“ Idadi ya wahitimu kwa mwaka 2018/2019 ni sawa na ongezeko la asilimia 32% ikilinganishwa na 690 kwa mwaka 2017/2018”; Alisisitiza Dkt. AkwilapoAkifafanua amesema wahitimu hao wanatoka Kampasi za Dar es Salaam, WAMO Morogoro na Luchelele Jijini Mwanza wanawake wakiwa 565 na wanaume 397.

Pia Dkt. Akwilapo amewaasa wahitimu hao kuzingatia weledi na taaluma waliyopata katika kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zilizopo kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi hiyo Dkt. Naomi Katunzi amesema kuwa udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 4,598 katika mwaka wa masomo 2018/2019 na kufikia wanafunzi 7,042 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 75.

Aliongeza kuwa ongezeko hilo litachangia kuongeza mapato ya ndani ya Taasisi hiyo yatakayosaidia katika shughuli za uendeshaji na kuongeza tija.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Michael Ng’umbi amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na wadau wa maendeleo kutekeleza programu iliyojikita katika kujenga stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), Pamoja na stadi za maisha ya ujasiriamali ambapo wanufaika 961 wamefikiwa na mradi huo.

Vilevile wasichana 627 wamenufaika na mradi wa elimu ya Sekondari kwa wasichana walio nje ya shule katika mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya juhudi za TEWW kuchangia katika kukuza kiwango cha elimu hapa nchini na kupunguza idadi ya wanaokosa fursa ya elimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni.

Aidha, Dkt. Ng’umbi amesema kuwa TEWW ina jukumu la kushirikiana na wadau binafsi kuwapatia elimu watoto, na vijana takribani milioni 3.5 waliokatisha masomo kwa sababu za utoro na mimba ili waweze kutoa mchango katika kukuza uchumi kupitia shughuli za uzalishaji.


Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imekuwa ikishirikiana na wadau kama UNESCO na KOICA kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kukuza kiwango cha elimu na kuyawezesha makundi maalum kama wasichana walikosa elimu katika mfumo rasmi kwa sababu mbalimbali.

BODI YA BARABARA PWANI YAELEKEZA KUPITIWA UPYA MKATABA BARABARA YA TAMCO-MAPINGA

$
0
0

Mkuu wa mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo




NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

BODI ya Barabara ya Mkoa wa Pwani, imeelekeza, kupitiwa upya kwa mkataba wa mkandarasi wa barabara ya Tamco Kibaha kwenda Mapinga wilayani Bagamoyo ( kampuni ya Skol) ambae anaonekana kusuasua kuanza ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo. 

Wakizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo, baadhi ya wajumbe walisema, wanashangaa kuona mkandarasi huyo tangu apewe kazi hakuna alichokifanya . 

Akizungumza kwenye kikao hicho, mkuu wa mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo alieleza kutokana na wajumbe kutoa malalamiko juu ya kampuni mbili za Skol na Southen Link ni vema wakala wa Barabara Nchi Tanroads kuliangalia kwa kina suala hilo. 

Ndikilo alibainisha, kuna haja sasa ya mkataba wake kuangaliwa ikiwezekana kazi hiyo ipewe kampuni nyingine ili iendelee na ujenzi huo kutokana na kampuni hiyo kutoonyesha uwezo. 

“Nitafanya ziara kutembelea ujenzi wa barabara hiyo ili kujionea hali halisi ya ujenzi huo ambapo ujenzi huo wa kilometa tano zimepewa kampuni hizo lakini kipande walichopewa kampuni hiyo ya Skol bado hakijajengwa kabisa,” alisema Ndikilo. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama alisema,ucheleweshaji wa ujenzi huo itachelewesha utekelezaji wa muda wa ujenzi wa mradi huo ambao unajengwa kwa awamu. 

Naye meneja wa Wakala wa barabara Tanroads mkoa wa Pwani Mhandisi Yudas Msangi alisema kuwa kwa sasa wamewasiliana na makao makuu yao kupitia kitengo cha masuala ya kisheria ili kuangalia mkataba huo ikiwezekana wavunje mkataba huo. 

Msangi alisema kuwa tayari wamemuandikia barua nne kuhusiana na uwezo wake lakini inaonyesha kama kuna tatizo hivyo wanaendelea na hatua mbalimbali ili kumalizana naye. Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alisema kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwani inaunganisha wilaya za Kibaha na Bagamoyo. 

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa barabara hiyo ni mbaya kwani imeharibika kwa kiasi kikubwa hivyo ni vema wakandarasi hao wakaongeza nguvu ili kukamilisha ujenzi huo.

MWADUI WAPEWA MWEZI MMOJA KUUZA ALHAMASI SOKO LA NDANI

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua baadhi ya nyaraka za manunuzi ya Madini kwenye moja ya chumba cha kununulia Madini kwenye soko la Maganzo wilaya ya Kishapu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Mwadui Mhandisi Ayubu Mwenda akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini Doto Biteko wakati wa ziara yake mgodini hapo akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao na wafanyakazi wa mgodi wa Mwadui hawapo pichani
Sehemu ya Wananchi wa kijiji cha Maganzo wakimsikiliza . Waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

…………………

Na Issa Mtuwa – Shinyanga

Uongozi wa Mgodi wa Diamond Williamson (Mwadui) unaozalisha madini ya Almasi uliopo mkoani Shinyanga wilayani Kishapu umeagizwa na kupewa muda wa mwezi mmoja hadi kufikia Januari 2020 kuanza kuuza 5% ya Almasi yote inayozalishwa katika mgodi huo kwenye soko la ndani hususani soko la Kishapu huku wazawa wakipewa fursa ya kununua Almasi hiyo.

Waziri wa Madini Doto Biteko, ameyasema hayo tarehe 10/12/2019 kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na uongozi wa mgodi wa Mwadui wakati wa kikao chake alipotembelea mgodini hapo kwa ziara ya kikazi na baadae kuongea na wafaanya biasharaa wa madini wa soko la Kishapu na kisha kuongea na wananchi wa Maganzo wilayani humo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Maganzo.

“Ndugu zangu, nafurahi kuona namna mlivyo kusanyika, bila shaka mnashauku kubwa ya kusikia nikisema jambo. Kabla sijasema naomba niwaambie, Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kuona maisha ya watu yanabadilika kupitia raslimali za madini hasa wale wanaozungukwa na migodi, wakiwemo ninyi”

“Nataka nione maisha yenu yanabadilika kutokana na uwepo wa mgodi huu na uwepo wa Almasi hii hapa Kishapu. Sasa niseme yafuatayo; Moja, kiliochenu cha muda mrefu cha kuomba mabaki ya mchanga uliochenjuliwa (tellings) nimeagiza kuanzia tarehe 22/12/2019 mchanga ule uanze kutolewa na mkaanze kuufanyia kazi. Pili ifikapo Januari 2020, 5% ya Almasi inayozailishwa mgodini hapa wataanza kuuza kwenye soko la hapa Maganzo na watakao nunua Almasi hiyo ni wazawa wanao nunua kwenye soko la Magazo” aliseema Biteko.

Biteko ameongeza kuwa, kila watu mahali walipo wanufaike na walichopewa na Mungu huku akisema wapo waliopata Bahari, Ziwa, Mbuga za wanyama, Vipepeo, Mijusi, Madini na ninyi wa Kishapu mmepewa Almasi kwa hiyo tumieni uwepo wa Almasi kubadilisha maisha yenu, wizara ya madini itaendelea kusimamia na kuhakikisha fursa zinazotokana na uwepo wa mgodi huu zinawanufaisha

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Diamond Williamson Mhandisi Ayubu Mwenda alisema siku zote wanafanya kazi zao kwa taratibu na kwa kuzingatia sheria. Aliongeza kuwa hawana tatizo na uuzaji wa 5% ya Almasi kwenye Soko la ndani hivyo kama uongozi watatekeleza agizo la Waziri na wataanza kuuza mwezi Januari 2020. Kuhusu utoaji wa mchanga wa “makinikia” utaanza kutolewa tarehe 22/12/2019.

Wananchi wa Maganzo walishukuru kwa ujio wa Waziri wa Madini huku wakifurahishwa na agizo la kuanza kwa tarehe ya utoaji wa mchanga wa makinikia. Zainabu Issa mkazi wa Maganzo alisema mchanga huo wataufanyia kazi na watapata kipato kitakacho wasaidia kuendesha maisha yao huku, Katibu wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) Gregory Kibusi alisema wao kama SHIREMA wamefurahishwa na maagizo na maelekezo yaliyotolewa na Waziri na walikuwa wanayasubiri kwa muda mrefu na watafuatilia.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa soko la Maganzo Seif Khatibu alisema, amefurahishwa na kauli ya waziri kuuagiza mgodi wa Mwadui kuuza 5% ya Almasi yao kwenye soko la Maganzo na inunuliwe na wanunuzi wazawa wa soko la Maganzo.

JAMII ISHIRIKIANE NA WAWEKEZAJI ILI KUINUA MAENDELEO NA UCHUMI WA ENEO HUSIKA

$
0
0
 
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ameitaka jamii kushirikiana na wawekezaji katika maeneo yao pamoja na kuwageukia wawekezaji kushiriki kuchangia shughuli za kijamii kwenye maeneo hayo,ili kujiletea maendeleo na kujiinua kiuchumi. 

Aidha ametaja ,changamoto ambazo bado zinakabili baadhi ya maeneo ya uwekezaji ni kutokuwa na umeme wa uhakika ,miundombinu ya maji, umeme ,barabara,malighafi pamoja na ukosefu wa masoko.

Aliyasema hayo ,katika mkutano wa mashauriano kati ya serikali wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa huo ,ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa wizara mbalimbali walifika mji wa Kibaha kutoa ufafanuzi mbalimbali na kuulizwa maswali na wawekezaji na wafanyabiashara hao. 

Ndikilo alieleza ,jamii na wawekezaji wanategemeana hivyo hakuna budi kujenga ushirikiano ili kujiletea maendeleo. Hata hivyo, alifafanua kati ya changamoto za uwekezaji pia lipo tatizo la ucheleweshaji upatikanaji wa vibali,masharti magumu,vibali vya ujenzi na riba kwa taasisi za fedha. 

“Baadhi ya maeneo kutotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo,kupata leseni ya EPZA kwa wawekezaji na kukosa kibali cha chassis ya gari ili kuunganisha bodi za magari,” alisisitiza Ndikilo. Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Abdala Ndauka alitaja,changamoto mojawapo ni baadhi ya taasisi za zinazohusika na vibali kutumia nguvu badala ya kutoa elimu.

Kwa upande wake mfanyabiashara na mwekezaji wa masuala ya elimu na hotel ya Njuweni,alhaj Yusuph Mfinanga alisema ifikie hatua jamii ikaona thamani ya wawekezaji kwenye maeneo yanayowazunguka na kushirikiana nao pasipo kuwawekea vikwazo. 

Alichukua fursa hiyo, kutoa dukuduku lake kuhusiana na hasara aliyoipata baada ya kununua shule ya Mangiyo iliyopo wilaya ya Mwanga,mkoa wa Kilimanjaro,shule kupitia Jumuiya ya Wazazi kihalali ,lakini lilitokea kundi la watu wa kijiji na kudai shule hiyo haijauzwa. 

“Nimekwama ,licha ya kununua kihalali, shule hiyo iliyo chini ya Jumuiya ya wazazi miaka minne sasa, lakini uwekezaji wangu umepotea kwakuwa sijanufaika nao, ninaumia,nateseka,naomba Waziri husika na Chama kinisaidie kupata haki yangu”alieleza Mfinanga. Mfinanga anakiomba chama cha mapinduzi (CCM) kumsaidia kurudishiwa fedha zake ama kuachiwa shule ambayo kainunua ili kuondokana na hasara anayoipata. 

Angela Kairuki Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) na baadhi ya mawaziri walitoa majibu kutegemeana na wizara ambapo Kairuki ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti mkutano huo alisema kuwa wanakutana na wadau hao ili kujua changamoto zinazowakabili kwani baadaye wataandaa mipango na mikakati kwa ajili ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. 

Waziri wa ardhi ,William Lukuvi alisema ,amebeba baadhi ya changamoto zilizogusa wizara yake kwani nyingine zinashughulikiwa na zipo katika ufuatiliaji. Hata hivyo, alibainisha kati ya vijiji ambavyo vilikuwa sehemu ya hifadhi na mheshimiwa Rais kusema maeneo hayo yatakuwa ya makazi mkoa wa Pwani ni vijiji 86 ambapo kwa sasa wanajiandaa kuyapima maeneo hayo na kuyaweka kimipangomiji. 

Nae waziri Hasunga alifafanua, wanahimiza uwekezaji kwenye uzalishaji chakula na kwenye pembejeo ikiwemo mbolea ambapo mahitaji ni 186,000 lakini uwezo wa ndani haizidi tani 50,000. 

Naye naibu Waziri Mavunde alisema kuwa kwa sasa wanaangalia namna ya kumkopesha kijana mmoja mmoja kwa baadhi ya maeneo kwani baadhi ya maeneo mikopo ya vikundi ni changamoto na utafiti umeonyesha kwa vikundi kuna ugumu.

TBS: VIWANGO 1,587 VIPO TAYARI KULINDA AFYA YA WATANZANIA

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athman Ngenya akifafanua kitu kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Shirika hilo katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam leo Desemba 11, 2019.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
*********************************

Na. Paschal Dotto-MAELEZO 11.12.2019
Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano Shirika la ViwangoTanzania (TBS) limefanikiwa kutekeleza mambo mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa bidhaa safi zenye hadhi kwa matumizi ya wananchi.

Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, MkurugenziMkuu wa Shirika sla Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya amesema kuwa wamefanikiwa kutekeleza azma ya kulinda afya za wananchi kwani mpaka sasa Shirika hilo limeweza kutayarisha viwango 1,587 katika sekta mbalimbali.

“TBS kwa kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali ya Rais John Pombe Magufulitumefanikiwa kutayarisha viwango 1,587 katika sekta za chakula, kemikali,mazingira, sekta mtambuka, ngozi na nguo, uhandisi (umeme, mitambo, ujenzi, na madini), kwa hiyo viwango hivi vimesaidia wazalishaji na wafanyabiasharakuzalisha bidhaa zilizo na ubora”, Dkt. Ngenya.

TBS wamatekeleza majukumu ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata bidhaaambazo ziko safi na zina ubora kwa matumizi ya afya ya binadamu na katikakutimiza azma hiyo jumla ya sampuli 71,863 zilipimwa katika maabara za TBSambayo ni sawa na asilimia 85.6 ya lengo la kupima sampuli 84,000.

Aidha Dkt.Ngenya alisema kuwa katika maabara za shirika hilo jumla ya mitambo 21,726 ilifanyiwa ugezi sawa na asilimia 82.5 ya lengo la kufanya ugezi mashine 34,000 ambapo suala hilo limefanyika katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Dkt. Ngenya alisema kuwa katika miaka minne ya Rais Magufuli, TBS imewezakutoa vyeti vya ubora kwa bidhaa mbalimbali ambazo zimekubalika kulingana naviwango vya shirika hilo, jumla ya vyeti 1, 137 sawa na asilimia 80.6 vilitolewa kwa bidhaa mbalimbali, na pia hii ilichangiwa na ari ya shirika hilo kusogeza huduma kwa wananchi.

Pia katika kipindi hiki cha miaka minne ya Rais John Pombe Magufuli TBSimefanikiwa kutoa gawio kulingana na Sheria ya Bajeti ya kuwasilisha Serikaliniasilimia 15 ya mapato ghafi na kuchangia pato la Serikali kuanzia mwaka2016/2017 mpaka Septemba 2019 jumla ya TZS bilioni 34.8 ziliwasilishwaSerikalini. Katika kuimarisha ufanisi wa kazi TBS lina jumla ya Maabara nane ambapo kati ya hizo sita zimehakikiwa na kupewa vyeti vya umahiri na kutambulika kimataifa na hivyo kumuwezesha mfanyabiashara kupata urahisi wa masoko ya kimataifa.

“Kati ya kitu ambacho kwa miaka hii minne ya Serikali ya Awamu ya Tano,maabara sita za TBS zimethibitishwa kimataifa na kuweza kuleta nafuu kubwa kwa wafanyabiashara kimasoko, maabara hizo ni maabara ya ugezi, chakula, kemia, umeme, mitambo na maabara ya ujenzi, hizi ni maabara ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wetu”, Alisema Dkt. Ngenya.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA INNOCENT BASHUNGWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MWATEX MWANZA

$
0
0
Mhe. Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoa Mwanza amekitembelea kwa mara ya pili kiwanda cha Mwatex (2001) LTD kilichobinafisiswa na Serikali kwa mwekezaji Amin Radhanin na chenye wafanyakazi 600.

Kwenye ziara ya kwanza ya tarehe 30/09/2019 alitoa maelekezo kwa kiwanda kuhusu kuandaa mpango mkakati wa biashara wa kuendesha kiwanda lakini mpaka sasa huo mpango mkakati haujafika wizarani.

Waziri baada ya kufika kiwandani hapo aliomba uongozi na menejiment nzima kutoka nje na mkutano ili kusikiliza kero na changamoto pia na maoni yao yatakayofanya kiwanda hicho kinafanye kazi kwa asilimia 100. 

Amabapo kwa sasa kinafanya kazi asilimia 60 tofauti na matalajio ya serikali ya kiwanda kufanya kazi kwa asilimia 100 Waziri baada ya kusikiliza maona na kero za wafanyakazi ameagiza wizara kuunda kamati maalum ambayo itafika kiwandani kufanya uchambuzi wa uendeshaji wa kiwanda kwa kushirikiana na msimazi anaekiendesha kiwanda hicho na amewapa muda mpaka 01/01/2020 kamati hiyo iwe imeshamfikishia ripoti ya uchambuzi wa mwenendo wa kiwanda cha Mwatex Ripoti hiyo itaisaidia serikali kupata mwelekeo wa nini kifanyike ili kupata Mwatex iliyokuwepo enzi za Mwalimu Nyerere.

Pia Waziri amesisitiza kuwa mkakati wa serikali ni kuona viwanda vyote vinafufuliwa na vinafanya kazi ili serikali iweze kutengeneza mnyororo wa thamani ya mazao yote hapa nchini.

       

SERIKALI YAWATAKA WALIMU WAKUU NCHINI KUHIMIZA WANAFUNZI KUSHIRIKI MASHINDANO YA INSHA

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewataka wakuu wa Shule nchini kuwahimiza na kuwajenga wanafunzi kwenye shule zao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano ya Insha yanayoshirikisha wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na ile ya kusini mwa Afrika SADC.

Walimu hao wametakiwa kutilia mkazo ushiriki wa wanafunzi hao kwani unachangia kuwajenga kitaaluma, kuwaongezea uwezo wa kufikiri lakini pia kuwapatia kipato kutokana na zawadi zinazotolewa.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti washindi wa kitaifa wa shindano la uandishi wa insha kwa Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao.

" Ili tupate washindi wengi katika mashindano haya ni lazima wakuu wa shule za Sekondari wahakikishe wanawahamasisha wanafunzi wengi kushiriki katika mashindano haya kwa sababu yanawaongezea fursa washiriki na kuwasaidia kujiamini Sana.

"Mashindano haya yanasaidia kuwajengea wanafunzi wetu uwezo wa uandishi, udadisi na kuwa wepesi kufanya tafiti pia mashindano haya yanasaidia kuwajengea uzalendo pindi wanapokuwa wanawakilisha Taifa" Amesema Ole Nasha.

Amewataka wanafunzi walioshiriki na kushinda kuwa mabalozi wazuri kwa kuhamasisha wenzao nao kuhakikisha wanashiriki mashindano hayo ili kuwa na wawakilishi wengi zaidi katika mashindano hayo na kuwapongeza kwa kushiriki na hatimaye kuibuka washindi wa mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo yalianzishwa ikiwa ni sehemu ya mkakati mkubwa wa Jumuiya ya SADC na EAC kujenga uelewa kwa wanafunzi juu kazi na mipango ya Jumuiya hizo kwa wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo ya kuandika insha yenye maada zinazoshabihiana na Jumuiya hizo.

Kwa upande wake mratibu wa tukio hilo la uandishi wa insha Sylvia Chinguwile, amesema mada zinazoshindaniwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa Nchi na baadaye Nchi wanachama kuwajibika kutangaza na kubainisha vigezo vya washiriki.

Amesema baada ya kupita katika michakato huo huwasilishwa wizarani na kuteuliwa insha bora katika ngazi ya shule na kusahihishwa na jopo la wataalamu na zile za EAC husimamiwa na balaza la mitihani, na insha tatu bora za SADC hupelekwa Botswana ili kuidhinishwa na mataifa Nchi wanachama, wakati insha tano bora huwasilishwa Arusha Makao makuu ya Jumuiya kushindanishwa na Mataifa mengine.

Amesema kwa upande wa EAC mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza ni Vanessa Lema, kutoka Longido Sekondari kidato Cha sita, wakati wa pili ni Thomas Kalisti, Kibasila Sekondari Dar as saalam kidato Cha Tatu, huku kwa ujumla wake Wakiwa 13.

Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Elimu nchini Augusta Lupokela ameipongeza wizara ya elimu kwa kuweza kuwasimamia mwanzo hadi mwisho wa mashindano hayo amesema kupitia mashindano hayo wameweza kujipambanua kuwa bado elimu yetu ipo katika Hali nzuri ukilinganisha wanavyoiongelea watu wengine.

Nae mwanafunzi ambaye alifanya vizuri katika uandishi wa Insha kwa mada zote Julieth Mpuya, kutoka Kilangalanga Sekondari kidato Cha kwanza, amesema kilichompelekea kufanya vizuri ni ujasiri, kujituma na kufuatilia mada na kuamini kuwa anaweza na hatimaye kufanya vizuri.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mashindano ya Insha kwa Nchi wanachama wa Jumuiya za SADC na EAC leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akizungumza na walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya utoaji tuzo za Insha jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akizungumza na Walimu, Wanafunzi na Wazazi katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mashindano ya Insha kwa Nchi wanachama wa SADC na EAC. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Jumuiya za SADC, EAC na Wizara pamoja na wanafunzi walioshinda kwenye mashindano ya Insha.

SAMPULI 5106ZIMEFANYIWA UCHUNGUZI NA MAABARA YA MKEMIA KANDA YA KATI Inbox x

$
0
0
Na.Catherine Sungura.Dodoma.

Jumla ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati.

Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Kazumila amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani

"Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja umbali na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa wakati".Amesema Kazumila.

Kwa upande wa vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli 36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa mtoto.

Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda ya kati.

Kwa upande wa wajasiriamali wadogo wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.

Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.
Meneja wa kanda ya kati ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali Musa Kazumila wakati akiongea na maofisa habari wa wizara na taasisi zake

MASAI FESTIVAL KURINDIMA TEXAS MWAKANI.

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi TV

KAMPUNI ya Kitanzania inayolenga kukuza utalii wa ndani (Wonderland) Imezinduwa rasmi Tamasha jipya liitwalo Masaai Festival, ambalo linatarajia kufanyika mwanzoni wa mwaka 2020 Texas Marekani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Said Maulid amesema wameandaa tamasha la maasai kwa lengo la kutoa mchango mkubwa kwenye swala la zima la utalii na pia juu ya maendeleo ndani ya sekta hiyo ya utalii.

“Wonderful imeandaa ili tamasha kwa lengo la kukuza utalii na kutangaza utalii nje na ndani ya Tanzania,"Pia Maulid ametambulisha mabalozi ambao wataenda kushiriakiana nao kwa lengo la kulitangaza tamasha pamoja na kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo kupenda vitu vya kinyumbani zaidi.

Ndani ya mabalozi hao wapo wasanii wa mziki kama G nako kutoka kundi la weusi, Mrisho Mpoto (mjomba), mwigizaji batuli, Welu sengo na wengine wengi.Moja kati ya mabalozi waliopata nafasi ya kuzungumza ni Batul ambae ni muigizaji wa filamu.

"Hiki ni kitu kikubwa na tumeungana kama watanzania kutangaza utalii wetu na tunategemea tutapata muitikio mzuri kwani ni ” tamasha la kipekee ambalo litavuka hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza kitalii zaidi,"

Hata hivyo batul ameeleza sababu za kuchaguliwa kwa wa masai Ni kutokana na kabila Hilo kudumu kwenye tamaduni zao kwa muda mrefu kuanzia mavazi,vyakula na rafudhi zao kuwa kama kielelezo tosha.

"Wamasai ni Kama kielelezo tu ila tunategemea kuwepo na Makabila mengi zaidi na kuhamasika kupitia sekta hiyo ya utalii na kupelekea kuongeza pato la taifa,"
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Wonderland Said Maulid akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari huku akiwa na mabalozi Batuli,well sengo,g nako pamoja na Mrisho mpoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wonderland Said Maulid akizungumza na waandishi wahabari kuhusu tamasha la Masai linalotarajiwa kuanza mwakani huku akiwa na balozi wa tamasha Hilo là kitalii Batuli muigizaji wa filamu nchini.
 

WAZIRI HASUNGA AFANYA ZIARA WILAYANI MKURANGA NA KILWA YA KUKAGUA MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia korosho Nangurukuru wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Sehemu ya wakulima na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Pwani na Lindi


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 10 na 11 Disemba 2019 amefanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.


Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amebaini baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao jambo ambalo limemshangaza Kwakuwa serikali ilishatoa fedha zote kwa ajili ya kuwalipa wakulima.


Amesema kuwa baada ya ziara ya kikazi katika mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara kubaini kadhia iliyopelekea kutolipwa fedha hizo serikali itachukua hatua za haraka.


“Sikutegemea hata siku moja kwamba eti itafika mpaka mwezi wa 12 wakulima wakiwa hawajalipwa kwakuwa imetokea niwahakikishie wakulima wote ambao walileta korosho zao na zilipokelewa, wote watalipwa” Alisisitiza Mhe Hasunga


Amesema kuwa wapo baadhi ya wakulima ambao wanasema hawajalipwa jambo ambalo sio kweli kwani wanafanya hivyo ili kukwepa madeni waliyokopa.


Kuhusu vibarua waliofanya kazi katika msimu huo wa korosho wa mwaka 2018/2019 Waziri Hasunga amesema kuwa madeni yote halali yatalipwa kwa wakati.


Hata hivyo ameeleza kuwa katika msimu wa mwaka 2019/2020 serikali haitajiingiza kwenye ununuzi wa zao la korosho badala yake imetoa fursa kwa wafanyabiashara kununua korosho.


Sambamba na hayo pia amesema kuwa serikali inaendelea kujipanga vyema ili katika siku za hivi karibuni serikali isipange bei elekezi badala isalie kuwa msimamizi mkuu kuhakikisha haki inatendeka katika biashara hiyo.


Ziara ya siku moja mkoani Pwani imetoa taswira ya muendelezo wa ziara ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambapo leo tarehe 11 Disemba 2019 amewasili katika mkoa wa Lindi.

Open Editorial by Ursula von der Leyen, President of the European Commission - EU Green Deal

$
0
0


Do we, humans, want to continue living well and safely on this planet? Humanity faces an existential threat the whole world is beginning to see. Forests burn from America to Australia. Deserts are advancing across Africa and Asia. Rising sea levels threaten our European cities as well as Pacific islands. 

Excessive droughts and changing rainfall patterns is making life very difficult for rural communities that are dependent on agriculture for their livelihoods, while recent flooding in Eastern and Southern Africa has caused havoc in urban areas, destroying both lives and infrastructure.
Mankind has seen such phenomena before, but never at this speed.

Science tells us that we can still stop this epidemic, but we are running out of time. The new European Commission is wasting no time. Today, less than two weeks into our mandate, we present our roadmap for a European Green Deal
The European Union, being one of the most industrialised and developed regions, carries the responsibility of leading in the fight against climate change. Our goal is to become the first climate-neutral continent by 2050, slowing down global warming and mitigating its effects. This is a task for our generation and the next, but change must begin right now – and we know we can do it.
The European Green Deal that we present today is Europe's new growth strategy. It will cut emissions while also creating jobs and improving our quality of life.
It is the green thread that will run through all our policies – from transport to taxation, from food to farming, from industry to infrastructure. With our Green Deal we want to invest in clean energy and extend emission trading, but we will also boost the circular economy and preserve Europe’s biodiversity.
The European Green Deal is not just a necessity: it will be a driver of new economic opportunities. Many European firms are already going green. They are cutting their carbon footprint and discovering the clean technologies. They understand that there are planetary boundaries: European companies of all sizes understand that everyone has to take care of our common home. They also know that if they discover the sustainable solutions of tomorrow, this will give them first mover advantage. 
What businesses and change-makers need from us is easy access to financing. To pull this off, we will deliver a Sustainable Europe Investment Plan.  It will support one trillion euros of investment over the next decade. We will work hand in hand with the European Investment Bank, Europe’s climate bank. 
Next March, we will propose the first-ever European Climate Law to chart the way ahead and make it irreversible: investors, innovators and entrepreneurs need clear rules to plan their long-term investments. 
While we will promote transformation in how we produce and consume, live and work, we must also protect and accompany those who risk being hit harder by such change. This transition must work for all or it will not work at all. I will propose to set up a Just Transition Fund – and I want it to mobilise, together with the leverage of the European Investment Bank and private money, one hundred billion euros in investment over the next seven years. We will make sure that we help those European regions who will have to take a bigger step, so that we leave no one behind. 

But our action is not limited to Europe; the European Commission has proposed that in 2021-2027 25% of the EU budget for external cooperation be devoted to climate related actions.

People young and old are not only asking for climate action, they are already changing their lifestyle. In Tanzania, people from all walks of life have been helping to clean up the beaches; and the recent ban on plastic bags is a commendable decision by the Government. At the same time more and more people are recycling what they use, and in rural areas indigenous knowledge is used to adapt to the new environment.

Through the Global Climate Change Alliance Plus (GCCA+), the EU is supporting Tanzania's government in strengthening the capacity of some of the most affected communities against the impact of climate change, particularly in highly vulnerable sectors such as agriculture.

Nine European citizens out of ten ask for decisive climate action. Our children rely on us. Europeans want their Union to act at home and lead abroad. In these very days, the whole world has gathered in Madrid for the United Nations’ conference on climate, to discuss collective action against global warming. 

The European Green Deal is Europe’s response to our people’s call, and a contribution for a better world.

SAMPULI 5106 ZIMEFANYIWA UCHUNGUZI NA MAABARA YA MKEMIA KANDA YA KATI

$
0
0
Na WAJMW-Dodoma.

Jumla ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati.

Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Kazumila amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani

"Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja  umbali na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa wakati".Amesema Kazumila.

Kwa upande wa vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli 36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa mtoto.

Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda ya kati.

Kwa upande wa wajasiriamali wadogo wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.

Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.
Meneja wa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya kati Bw. Musa Kuzumila akizungumza na Maafisa Mahusiano na Mawasilino wa Wizara ya Afya na Taasisi zake wakati walipotembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini chini ya kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli akiwa madarakani.

Watumishi wa Umma fuateni Maadili ya kazi zenu na mkatae Rushwa - Waziri Mkuchika

CELEB AFRIC:Watanzania na waafrika waishio Marekani, washindwa kutumia fursa za elimu bure na misaada ya kijamii

CELEB AFRIC: Bongo Movie inakufa kwa ukosefu wa elimu ya filamu na pia wasambazaji - Producer Timoth Conrad

Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images